Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1069 | 1070 | (Page 1071) | 1072 | 1073 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva  akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani mjini Zanzibar leo  Desemba 14, 2016 . Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan.


  Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Mstaafu Mary Longway akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo Desemba 14, 2016 mjini Zanzibar.


  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid  (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao  cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume mjini Zanzibar leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kulia).


  Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Prof. Amon Chaliga akieleza jambo wakati wa kikao cha Wajumbe na Sekretarieti ya Tume kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar. Kulia  ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Hamid M. Hamid (katikati).


  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumza na Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Zanzibar kwenye kikao cha maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar leo Desemba 14, 2016.  Wajumbe na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damiani Lubuva mjini Zanzibar leo Desemba 14, 2017.Picha/Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amepokea magari hamsini ya kubebea wagonjwa pamoja na magari 8 ya kuratibu shughuli za huduma za afya ya mama na mtoto yenye thamani ya shilingi bilioni 5.9 ambayo yamekabidhiwa kwa Wabunge wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kigoma

  Waziri Ummy amelishukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na UNFPA kwa kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania, ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga. 

  Alizitaja changamoto zilizoonekana katika mikoa hiyo ni huduma hafifu ya rufaa kwa wanawake wajawazito kwa kukosa magari ya kubebea wagonjwa, ukosefu wa damu salama, ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama ikiwemo kutotambua dalili hatari za wakati wa ujauzito pamoja na baadhi ya watumishi wasiokuwa na stadi za kuokoa maisha ambayo yanachangia wingi wa vifo vitokanavyo na uzazi

  Tafiti zilizofanyika mwaka 2010 na tathmini iliyofanyika mwaka 2015 wakati wa kuandaa mpango kazi wa matokeo makubwa sasa, Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kigoma ilionekana kuwa na viashiria hafifu vya afya ya mama na mtoto kwa mfano; utumiaji mdogo wa uzazi wa mpango, wanawake wachache wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya pamoja na vifo vingi vitokanavyo na uzazi.

  Wizara ya Afya imekua ikifanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa awamu hii ya tano tumetengeneza mpango mmoja utakaohusika na masuala ya uzazi wa afya ya mama na watoto na vijana ambapo ndani ya miaka minne hadi kufikia mwaka 2020 tuwe tumepunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 432 hadi 292 kutoka kila kizazi hai laki moja na kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano Tanzania imefanikiwa kufikia lengo namba nne la malengo ya maendeleo ya milenia kwa kupunguza vifo kutoka 50 hadi 40 katika vizazi hai 1,000.

  Aidha Waziri Ummy amewataka Wabunge, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya kuyatumia magari hayo ipasavyo yaani, kwa shughuli iliyokusudiwa, vilevile kuyakatia bima ya ajali pamoja na kuiomba jamii, Taasisi zisizo za kiserikali kuunganisha nguvu kwani vifo vitokananyo na uzazi vinazuilika. 
  IMETOLEWA NA

  Nsachris Mwamwaja
  MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-AFYA
  14/12/2016


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Mh. Balozi Dk. Ramadhan Dau, amekabidhi hati za utambulisho kwa Mfalme wa Malaysia, Tuanku Abdul Halim Muadhwam Shah katika Ikulu ya nchi hiyo ' Istana Negara Taabu National Palace'  Kuala Lumpur.
  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Mh. Dk. Ramadhan Dau akipokelewa katika Ikulu ya nchi hiyo alipokwenda kujitambulisha kwa Mfalme wa nchi hiyo, Tuanku Abdul Halim Muadhwam Shah.
  Balozi wa Tanzania Mh. Dk. Ramadhan Dau akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
   Balozi wa Tanzania Mh. Dk. Ramadhan Dau akisaini kitabu cha wageni.
   Balozi Dk. Ramadhan Dau akiwasili na kupewa gwaride la heshima katika Ikulu ya Malaysia.
   Balozi Dk. Ramadhan Dau akisalimiana na  Mfalme wa Malaysia, Tuanku Abdul Halim Muadhwam Shah.
  Mfalme wa MalaysiaTuanku Abdul Halim Muadhwam Shah (kushoto), akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mh. Dk. Ramadhan Dau.
   Dk. Ramadhan Dau akimshukuru Mfalme wa Malaysia baada ya kukabidhi hati za utambulisho.

  0 0

  Na Bashir Nkoromo.

  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, amesema, anazitambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana na wafanyakazi hao kuzipatia ufumbuzi.

  Mpogolo amekutana na wafanyakazi hao ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  "Mimi nimekuwa katika chama hiki mda mrefu sana, kwa hiyo sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi nazijua hivyo nitatumia juhudi zangu na maarifa kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuisha kabisa".

  "Lakini kubwa zaidi ni mimi na ninyi wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na changamoto hizi na hatimaye tukifikishe chama kunakotarajiwa, na bila shaka mnajua lengo kuu la Chama chochote ni kuwa na nguvu na inayokipa uwezo wa kuongoza kwa kushika dola", alisema Mpogolo.

  Alisema, pamoja na kuwa katika Chama kwa mda wa kutosha kujifunza ana kuelewa mengi, lakini bado atahitaji ushauri kwa baadhi ya wafanyakazi wazoevu, hivyo wafanyakazi wasisite kumpa ushauri wao pale watakapokuwa wanaona kwamba ushauri wao utasaidia kusonga mbele.

  Mpogolo aliwataka wafanyakazi kuongeza bidii ya kazi kila mmoja katika nafasi yake, akisema ni lazima watambue kuwa kila mfanyakazi wa Chama katika eneo aliloko mchango wake unahitajika sana, na aelewe kuwa isingekuwepo haya ya chama kumwajiri kama hakitarajii tija kutoka kwake.

  Mapema, Mpogolo aliwasili ukumbini akifuatana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi.

  Luhwavi aliwaomba wafanyakazi kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu huyo mpya akimwelezea kuwa ni Kada wa Chama ambaye amefanya kazi katika idara nyingi na nyeti hivyo anayo hazina ya mambo mengi anayofahamu katika chama.
   Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Utawala bakari Hamad na wapili ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja.
   Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiwana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo.
   Wafanyakazi wakishangilia ukumbini Mpogolo na Luhwavi walipowasili ukumbini
   Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji,  Makao Makuu ya CCM, Salum Khatib Reja, akitoa utangulizi, baada ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo kuwasili ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo
   Wafanyakazi wakiwa tayari kumsikiliza Mpogolo
   Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, Bakar Hamad (kulia) akishirikiana na viongozi wenzake kunukuu dondoo, Naibu Katibu Mkuu pya wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipozungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, leo Desemba 14, 2016. Kushoto ni Mwangalizi wa Ofisi Rose Francis na Ofisa Mwendeshaji Mwajuma Nyamka.
   Wafanyakazi wakiwa ukumbini
   Wafanyakazi wakiwa ukumbini
   Wafanyakazi wakiwa ukumbini 
   Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodgrick Mpogolo (katikati), kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo, Desemba 14, 2016. Kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Utumishi Makao Makuu ya CCM, Salum Khatib Reja.
    Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Desemba 14, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab 
  Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja. PICHA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande akiongea mbele ya mawakili 258 hawapo pichani wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande katikati akiongoza Majaji wengine kupokea salamu ya utiifu kutoka kwa mawakili 258 waliopishwa hawapo pichani wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Mawakili wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande hayupo pichani baada ya kuapishwa wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Mawakili wakiwa wamesimama kusubiri kula kiapo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othman Chande katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Mawakili waliopishwa wakati wa sherehe ya 55 ya uhapisho huo iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.  Na Lydia Churi-Mahakama 


  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman amewataka Mawakili nchini kuzingatia Maadili na kufuata misingi ya haki katika kutekeleza majukumu yao ili kesi ziendeshwe kwa haki, haraka na kwa wakati ili kuongeza imani ya wananchi kwa Mahakama.

  Akizungumza wakati wa sherehe za kuwapokea na kuwaapisha Mawakili leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu amesema endapo Mawakili watatekeleza wajibu wao kwa kutenda haki watasaidia kupunguza mlundikano wa kesi zilizopo kwenye Mahakama mbalimbali nchini kuanzisha zile za Wilaya mpaka mahakama ya Rufani.

  Aidha, Jaji Mkuu amewataka Mawakili kushirikiana Mahakama pamoja na wadau wengine katika kuutekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ambao pamoja na mambo mengine pia unalenga kupunguza mlundikano wa kesi kwenye mahakama mbalimbali nchini.

  Mhe. Othman pia amewashauri Mawakili walioapishwa leo kujiendeleza kielimu ili waweze kuongeza ujuzi utakaowasaidia kupambana na changamoto mbalimbali za kitaaluma na kwenda na wakati.

  Amewataka Mawakili hao kusambaa na kufanya kazi mikoani ili na raia walioko huko nao wapate haki badala ya wengi wao kung’ang’ania kwenye miji mikubwa pekee kama vile Dar es salaam, Arusha, na Mwanza.

  Naye Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Fednand Wambali amesema suala la ushiriki wa dhati katika utoaji wa haki nchini limesisitizwa kwa Mawakili walioapishwa leo.

  Mhe. Wambali pia amewataka Mawakili hao kuwa waaminifu kwa Mahakama ya Tanzania na kwa wateja wao ambao n iwananchi wanaotafuta haki zao.Aliongeza kuwa bila ya Mawakili hao kuwa na maadili hawataweza kufanya kazi.

  Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amewataka Mawakili hao wapya kufanya kazi zao kwa kufuata maadili ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.Alisema kupitia kamati ya malalamiko, amepokea malalamiko 71 kati ya mwaka 2015 na 2016 yaliyowahusu Mawakili kukiuka taratibu na misingi ya kazi yao.

  Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, baadhi ya malalamiko yalihusu Mawakili kutokuwatetea wateja wao ipasavyo, kufanya kazi ya uwakili bila ya kulipia kibali, na kutoa siri za wateja wao.

  Jaji Mkuu wa Tanzania amewakubali na kuwaapisha Mawakili wapya 285 na kuifanya Tanzania kuwa na Mawakili zaidi ya 6080. Sherehe za kuwakubali na kuwaapisha Mawakili hao zimefanyika kwa mara ya 55 tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo mwaka 1986 hapa nchini.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii .


  MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/= ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika ziara ya Dar mpya.

  Makonda amesema kuwa anatimiza ahadi zake kwa wahusika kama ifuatavyo Sober house kigamboni kwa kuwapa jiko la gesi, mitungi 2,king’amuzi televisheni moja ya nchi 49 na magodoro 50 pia ameweza kutoa zawadii ya pikipiki kwa watendaji wa ofsi yake kwa kuwapa morarli ya kazi pamoja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mivinjeni kata ya buguruni.

  Aidha mkuu wa mkoa ametoa zawadi kwa watumishi wane ambao ni Dr.Grace Magembe,mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mruto kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke,Edward Otieno katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji na Aron Joseph Mkkurugenzi uendeshaji wa DAWASCO.

  Pia ametoa mitaji ya biashara kwa wajasiliamali wawili kwa kwa kukabidhi kiasi cha fedha cha shilingi miioni moja kwa kijana mmoja na shilingi laki mbili kwa mwanamke mjasiliamali kwa ajjili ya kuimarrisha biashara yake.

  Msaada mwingne alitoa mkuu huyo wa mkoa ni pamoja na mabati 2000 kwa ajili ya sekondari ya Jeshi ya jitegemee na shule ya msingi Annex Mbagala mabati 1000 na shule ya msingi ya katoliki kupewasaruji mifuko 1000 .


  Pia ameimarisha kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kutoa Zawadi ya Tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi na kutoa zawadi ya gari kwa ajilli ya kuimarisha huduma katika Zahanati ya kikosi cha kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam Ukonga.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wakazi wa Dar es Salaam vyenye thamani ya 164,272,000/=leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
    Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam, Acp.Stanley Kulyamo akipokea gari la wagonjwa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda leo Jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa kikosi cha kutuliza ghasia kanda maalum ya Dar es Salaam, Acp.Stanley Kulyamo akiwa kwenye gari la wagonjwa alilo kabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akikabidhi zawadi  tumba kwa ajili ya bendi ya jeshi la Wananchi mara baada ya kufanya vizuri katika mahadhimisho ya miaka 55 ya uhuru.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda , akikabidhi  shilingi laki mbili kwa mjasiliamali ,Zuhura Waziri mkazi wa Mwembe Yanga kwa ajili ya kuongeza mtaji wake wa Supu.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi hundi  kwa mchungaji Epafra  Zabron Shinji wa kanisa la AIC Tanzania.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mifuko ya Saruji kwa Mkuu wa shule ya St Joseph Goba , Sister Caroline Kokutekana, kama sehemu ya kutimiza ahadi yake wakat wa mahafali ya shule hiyo.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikabidhi mabati  kwa mkuu wa shule ya sekondari  Jitegemee kama sehemu ya ahadi yake katika kampeni ya Dar es Salaam mpya.

  0 0


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG), anayejenga jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Yuzhang Xiong, wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi huo.
   Meneja Mipago, Ubunifu na Tathimini wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Eng. Mbila Mdemu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu mradi wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.
   Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kinachojengwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG), ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.
   Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salum Msangi akieleza mikakati ya utekelezaji wa upanuzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini. Pembeni yake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
   Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza, Eng. Marwa Rubirya akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa upanuzi wa sehemu ya barabara ya Mwaloni-Furahisha yenye urefu wa Mita 725, wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja la Furahisha na upanuzi wa Barabara ya Makongoro-Uwanja wa Ndege,  mkoani Mwanza.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa Pasiansi wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja la Furahisha na upanuzi wa Barabara ya Makongoro-Uwanja wa Ndege, mkoani Mwanza.
  Muonekano wa Daraja la Furahisha mkoani Mwanza, ambalo linatarajiwa kukamilika mwazoni mwa mwezi Januari mwakani. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80.


  Serikali imeanza ujenzi na upanuzi wa viwanja 11 ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha na kukuza usafiri wa anga hapa nchini.

  Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mwanza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 150 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya upanuzi wa viwanja hivyo.Ameongezeza kuwa miradi itakayotekelezwa katika viwanja hivyo ni pamoja na ujenzi wa majengo ya abiria na upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege.

  "Maboresho ya miundombinu ya viwanja vya ndege yatachochea ongezeko la pato la Taifa, hivyo basi Serikali imeonesha nia ya dhati katika kuhakikisha usafiri huu utakuwa ni wa uhakika na nafuu kwa wananchi”, amesema Profesa Mbarawa.

  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amevitaja baadhi ya viwanja hivyo kuwa ni kiwanja cha ndege cha Shinyanga, Tabora, Sumbawanga, Kigoma, Mtwara, Songea na Iringa.

  Kuhusu ujenzi wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha  Mwanza, Profesa Mbarawa amesema kuwa Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 7.6 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi na msimamiz wa mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Salum Msangi amesema Mamlaka itaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma zilizo bora na kukuza pato la Taifa.

  Ameahidi kuendelea kutatua changamoto ya ndege hai wanaohatarisha uharibufu wa miundombinu za injini za ndege katika uwanja huo ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa anga na watumiaji wake.

  Naye, Mkandarasi wa Kampuni ya Japan Engineering Construction Group (JECP), anayejenga jengo hilo, Yuzhang Xiong, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kwani kwa sasa jengo limefika  katika hatua nzuri.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ametembelea Daraja la Furahisha na barabara ya makongoro  hadi uwanja wa ndege yenye urefu wa kilomita tano na kusema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kupunguza foleni kwa watumiaji wa vyombo vya moto na  ajali kwa watembea kwa miguu.

  Aidha, amefafanua mradi huo kuwa umegawanyika katika sehemu tatu ambapo kwa sasa sehemu ya tatu ya mradi huo iliyoanza inahusisha upanuzi wa barabara ya Mwaloni hadi Furahisha Mita725 na ujenzi wa barabara ya Pasiansi hadi Uwanja wa Ndege (km 5) kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

  Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutunza na kulinda miundombinu hiyo ambapo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.

  Amewaagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza kumsimamia mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Roads anayejenga barabara hiyo kujenga kwa kiwango kilicho bora ili  kuweza kushawishi Serikali kuwapatia tenda za miradi mengine.

  Meneja wa TANROADS, mkoa wa Mwanza, Eng. Marwa Rubirya amesema kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi wa Daraja la Furahisha umefikia asilimia 80 ambapo ujenzi wa daraja na ufungaji wa vyuma umekamilika na unatarajiwa kukamilika mwanzoni  mwa mwezi Januari.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MSANII wa muziki wa kizazi Kipya 'Bongo Fleva' Abbas Bakari  'Abby skills' amewashukuru mashabiki wake kwa kuupokea wimbo wake wa Averina na kusema kuwa wakae tena kwa mkao wa kula kwani kuna nyimbo saba zipo tayari.

  Abbyskills ameachia wimbo wa Averina mwanzoni mwa  Novemba na umeweza kumpatia show kadhaa na tayari ameanza kupata mafanikio kwa kupitia wimbo huo aliowashirikisha wasanii Ali Saleh Kiba 'Ali kiba' na 'Mr Blu'.

  Amesema kuwa, menejiment yake ambayo kwa sasa yupo chini ya lebo ya KING STUDIO amejipanga kuhakikisha anazidi kuwapa burudani mashabiki wake na zaidi nyimbo zipo tayari zinasubiri kupakuliwa tu.

  Abbyskills ameendelea na kusema kuwa , ujio wa wimbo wa Averina umekuwa na manufaa makubwa sana kwake kwani ndani ya mwezi mmoja na nusu ameweza kupata show ikiwemo FIESTA ya mwaka huu iliyofanyika Novemba 05.

  Kwa sasa Abbyskills anajiandaa kuachia nyimbo mpya itakayotarajiwa kutoka Februari 2017 na mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani atakuja na kikubwa zaidi ya Averina.

  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam.

  Kampuni moja ya Ujerumani ya Ferrostaal, inatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, kitakacho gharimu zaidi ya Euro Bilioni 1 nukta 2 (1.2bln) ambacho kinatajwa kuwa kitakuwa moja ya viwanda vikubwa vya mbolea Barani Afrika.
  Hayo yamesemwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, EGON KOCHANKE, wakati alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Dar es salaam, ambapo wawili hao wamezungumzia masuala kadha wa kadha yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Ujerumani uliodumu kwa muda mrefu.
  Balozi Kochanke amesema kuwa kiwanda hicho kitakachojengwa kwa ubia kati ya kampuni hiyo ya Ujerumani na wawekezaji wazawa na wengine kutoka Bara la Asia, inatokana na  hamasa kubwa ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda.
  “Kiwanda hiki kitakuwa kikubwa zaidi ya mara mbili ya kiwanda cha saruji cha Dangote kilichoko Mtwara na kitagharimu Euro Bilioni 1.2, kitasisimua uchumi wa nchi pamoja na kukuza ajira” alisema balozi huyo aliyeambatana  na naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, John Reyels na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa nchi hiyo Julia Hannig.
  “Mbali ya Kampuni hiyo ya Ferrostaal, wawekezaji wengine ni kampuni ya Mbolea ya Minjingu, na kampuni nyingine kutoka Pakistan ambayo kwa pamoja wameingia ubia wa kujenga kiwanda hicho cha mbolea kitakachokuwa uwekezaji mkubwa” Aliongeza Balozi Egon Kochanke.
  Egon Kochanke, ameiomba serikali kutatua changamoto ya gharama za gesi ili kiwanda hicho kiweze kuanza ujenzi wake mapema iwezekanavyo na kuchochea maendeleo ya kilimo hapa nchini.
  Ameyataja maeneo mengine ambayo nchi yake itaelekeza rasilimali zake kuwa ni kuendeleza sekta ya afya, wajasiriamali wadogowadogo, sekta ya ufundi mchundo pamoja na kuhamasisha wawekezaji kutoka nchini mwake kuja kuwekeza viwanda na biashara mbalimbali hapa nchini.
  Aidha, Balozi huyo wa Ujerumani ameahidi kuwa nchi yake iko tayari kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili kuifanyia ukarabati meli ya MV Liemba, inayofanya zafari zake katika ziwa Tanganyika, ambayo ni meli ya kihistoria kwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100, ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa watanzania na nchi jirani za Zambia, Burundi na DRC Kongo.
  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Ujerumani kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na kwamba Tanzania iko tayari kuendeleza ushirikiano huo.
  Amesema kuwa uwekezaji wa kiwanda kikubwa na cha mfano cha mbolea huko mkoani Lindi, utachochea sekta ya kilimo ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watanzania, kwa kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya wakulima na mbolea ya ziada itauzwa nchi za nje.
  Dkt. Mpango, amemshukuru Balozi huyo wa Ujerumani kwa ahadi yake ya kusaidia kukarabati meli ya MV Liemba, na kiomba nchi hiyo kusaidia ununuzi wa meli mpya ili kuimarisha usafiri na usafirisha wa watu na mizigo katika eneo la maziwa makuu.
  Vilevile ameiomba nchi hiyo kuendeleza misaada yake katika sekta ya ufundi kupitia mamlaka ya Ufundi Stadi (Veta) pamoja na kuendelea kutoa ufadhili wa masomo ya juu kwa wanafunzi wa kitanzania kwenda kusoma nchini humo kama ambavyo imekuwa ikifanya miaka mingi iliyopita kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
  Balozi Kochanke amekubali kufanya hivyo na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika mambo hayo na masuala mengine, ikiwemo kuishauri namna bora ya kuhamishia Serikali mkoani Dodoma, wakitumia uzoefu wa nchi hiyo ilipohamisha makao makuu yake kutoka Berlin kwenda Born.
   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (katikati) pamoja na ujumbe wake wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani),  Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.  
   Ujumbe wa Ujerumani ukiongozwa na Balozi wan chi hiyo nchini Tanzania, Egon Kochanke (katikati) ukiwa katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakati wa mazungumzo kuhusu uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, Jijini Dar es salaam. Kulia kwa Balozi  ni Mkurugenzi wa Ushirikiano Bi. Julia Hannig na na kushoto kwake ameketi Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochankewakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.  Kulia kwa Waziri ni Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Melckzedek Mbise na anayefuata ni katibu wa Waziri Bw. Makamba.
   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kushoto) akielezea namna ya ushirikiano wa maendeleo kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani unavyoweza kuwa na tija kwa pande zote, wakati wa kikao kati yake na  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Konchanke, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi wa ushirikiano kutoka ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bi. Julia Hannig, akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiagana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Egon Kochanke (kulia) baada ya kumalizika kwa kikao kati yao, kilichofanyika  Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Ushirikiano kutoka Ujerumani, Bi. Julia Hannig, nje ya Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kumalizika kwa mkutano katika ya ujumbe huo kutoka Ujerumani ukiongozwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke, Jijini Dar es salaam.


  (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Hazina)

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bw. Onorius Njole akitoa mada ya masuala ya baadhi ya Miongozo iliyotolewa na Mamlaka ili kuboresha utendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mkoani Morogoro hivi karibuni.
  Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera, Bw. Ansgar Mushi akifafanua jambo la kitaalamu katika Semina iliyotolewa na SSRA kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, mkoani Morogoro hivi karibuni.
  Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada toka SSRA katika Semina ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  Meneja wa Huduma za Kisheria akitoa maelezo ya mmoja ya mada zilizokuwa zikiendelea katika Semina toka SSRA kwa Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
  Mwanasheria Mwandamizi, Bw. Omar Sururu akieleza na kufafanua jambo la kisheria katika Miongozo iliyotolewa na SSRA, Katika Semina iliyofanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
  Mmoja ya washiriki wa Semina kutoka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii akiuliza swali na kuhitaji ufafanuzi baada ya mada zilizotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
  Picha ya Pamoja ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii wakiwa na Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya Semina iliyofanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoani Morogoro hivi karibuni.
  Picha ya Pamoja ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii wakiwa na Mameneja na Maafisa wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii baada ya Semina iliyofanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoani Morogoro hivi karibuni.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akikata utepe kuashiria upokeaji wa  madawati ya msaada kutoka kwa Wakala wa  Huduma za Misitu nchini leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akizungumza mara baada ya kupokea madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 5.6  kutoka kwa Wakala wa  Huduma za Misitu nchini leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  Meneja wa Wakala wa Huduma za  Misitu Tanzania Wilaya ya Kinondoni, Alexander Mboya akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi madawati kwa mkuu wa Wilaya leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Alli Hapi.

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi na Meneja wa Meneja wa wakala wa huduma za  Misitu Tanzania wilaya ya Kinondoni, Alexander Mboya wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya kukabidhi leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA, leo December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, Kujiridhisha na Kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu 2016.

  Akiongea na Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa Radio5 baada ya kukamilisha ukaguzi wao, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi amesema wao kama Mamlaka Waliamua kuja kufanya ukaguzi wao kwa ajili ya kujiridhisha kurudisha Matangazo ya Kituo hicho hewani December 16 ambapo ndiyo tarehe rasmi ya kuisha kwa Adhabu waliyokuwa wamewapa Kituo hicho.

  Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi wa Studio ya Kurusha Matangazo (On air Studio), Studio ya kuzalisha Vipindi (Production Studio), Chumba cha Habari (News room), Control Room, ofisi zote za Kituo pamoja na Mnara wa Kurushia Matangazo ambapo kote wamekuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama Mamlaka inavyotaka.

  Hata hivyo Bw. Fredrick Ntobi akiwa ameongozana na Viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya Kaskazini, amewakumbusha Watangazaji na Waandishi kufuata Maadili ya uandishi wa habari ili kulinda Vituo vyao na Kulinda taaluma zao kwa ajili ya kuendelea kuhabarisha na kuelimisha Jamii nzima ya Watanzania.

  “Mimi niwasisitize tu kuendelea kufuata maadili ya taaluma yenu ya uandishi wa habari, kufuata sheria na kanuni za uandishi wa habari ambao mmesomea, tumieni lugha Sanifu ambayo inakubalika kwa jamii na tasnia yenu na niwatakie maandalizi mema ya kurudi hewani pamoja na Sikukuu zinazokuja”. Alimaliza kwa Msisitizo Bw. Fredrick Ntobi.

  Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis, Amewataka Wasikilizaji wa Radio5 kukaa mkao wa Kuhabarika, Kupata Burudani na kuelimika zaidi kupitia Radio5 kwani Wamejipanga vyakutosha kurudi hewani kwa Kishindo.

  “Mimi niwaombe tu wasikilizaji wetu ambao najua wametumiss sana, wakae tayari Kuhabarika, kuelimika na kuburudika zaidi sababu mimi na Wafanyakazi wangu tumejipanga vya kutosha haswa ukizingatia kwamba mwaka mpya ndo huu unakuja. Kingine niwape pole tu wasikilizaji wetu wote kwa kutotusikia hewani kwa kipindi cha miezi mitatu, pamoja na Wadau ambao tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika mambo mbali mbali niwaambie tu tunarudi rasmi Ijumaa ya tarehe 16 December 2016”. Alisema Mkurugenzi wa Radio5 Robert Francis.

  Kituo cha Radio5 Kilisimamishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kurusha matangazo yake tarehe 16 September 2016.
  Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Fredrick Ntobi wakizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis,ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA, leo December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, Kujiridhisha na Kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu 2016.

  0 0

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kulia) akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
   Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao na kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba.
   Kaimu Afisa Utamaduni Mkoa wa Mara Bw. Sheikhdadi Said (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao na Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
   Katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Mara Bw. Jonson Bambai (aliyesimama) akichangia mada wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara. 
   Mtoa mada kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Richard Ndunguru akitoa mada ya uandishi wa miswada ya filamu na utafiti kwa wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau hao leo Mkoani Mara. 
  Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu na michezo ya kuigiza kutoa mkoa wa Mara wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Mara


  Na Genofeva Matemu – WHUSM.

  Wanatasnia wa filamu nchini wametakiwa kutumia fursa zilizopo kikamilifu ili kuifanya sekta ya filamu kuwa chachu ya maendeleo ya nchi na kuleta ushindani wa kazi za filamu zinazozingatia  ubobezi na hatimaye kuingia katika soko la ushindani. 

  Rai hiyo imetolewa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza leo Mkoani Mara.

  “Nimatumaini yangu kuwa mafunzo mnayoyapata hapa yakijumuishwa na fursa mlizonazo za mandhari mahususi ya upigaji picha katika Mkoa wetu wa Mara, maeneo mazuri na asilia ya kitalii, utamaduni wetu, maliasili, lugha ya kiswahili na mambo mengine mengi mkiyazingatia katika uandaaji wa filamu zenu hakika ushindani wa filamu zetu utakuwa mkubwa sana” amesema Bibi. Millao.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuhakikisha kuwa wadau wanazalisha kazi bora na hatimaye wanapata mrejesho stahiki kutokana na kazi zao hivyo wadau walioshiriki warsha watumie fursa waliyoipata kwani warsha imezingatia ushirikishwaji wa hali ya juu kwa kuwapa wadau fursa ya kuchagia na kujadiliana.

   “Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuhakikisha Tanzania inakuwa taifa la viwanda hivyo kwa mantiki hiyo, katika warsha hii suala la namna gani tasnia iimarishwe ikiwa ni pamoja na uwepo wa viwanda vya filamu litatiliwa mkazo kutokana na hali ya Sekta ya Filamu kuendelea kuimarika kutokana na jitihada za wadau kwa kushirikiana na Serikali” amesema Bibi. Fissoo.

  Naye Katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Mara Bw. Jonson Bambai amesema kuwa warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya filamu na michezo ya kuigiza ni nembo tosha kwa waigizaji wa mkoa wa Mara kwani itawawezesha kuandaa filamu zitakazowavutia watazamaji kutoka mwanzo hadi mwisho wa filamu kwa kutumia fursa zilizopo katika mkoa wa mara na kutangaza upekee wa kabila la wakurya ndani na nje ya nchi.

  Tasnia ya filamu imeendelea kuwa chombo muhimu sana kinachochangia katika Maendeleo ya Taifa. Sote tutakubaliana kuwa ile dhana ya awali kuwa filamu ni chombo cha kutoa burudani tu imeanza kufutika kufuatia sekta hii kutoa ajira kwa makundi mbalimbali na kuchangia katika uchumi wa nchi.

  0 0


  Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

  "Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji. Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.

  Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM, Mama Anna Abdallah, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM wakati akienda kuzindua jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Meghji
  Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana akienda kukagua ndani ya jengo Kinana akitazama ukumbi wa mikutano katika jengo hilo Kinana akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa mali za CCM wakati akikagua jengo.  Samani ndani ya jengo
  🔻


  jikoni

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya viongozi kabla ya kuondoka baada ya kuzindua rasmi jengo la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Kenya Nchi Mhe. Ali Makwere, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Brazil Nchi Mhe. Carlos Alfonso Puente, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Denmark Nchi Mhe. E. Hebogand Jensen, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Mhe. Maniza Zaman, mara baada ya kumaliza mazungumzo,Ikulu jijini Dar es Salaam. 

                                          ................................................................. 

  Mabalozi wa Nchi Mbili za Brazil na Kenya wameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa mipango na mikakati yake ya madhubuti ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania -ATCL – kwa kununua ndege mpya kama hatua ya kuhakikisha shirika hilo linakuwa bora katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchini.
  Mabalozi hao wamesema hatua hiyo ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania  itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la taifa kwa ujumla.

  Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es salaama.

  Kwa upande wake, Balozi wa Brazil nchini Carlos Alfonso Puente amesema kutokana na nchi hiyo kuwa ni miongoni mwa nchi kadhaa Dunia zenye viwanda wa kutengeneza ndege hivyo serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini Brazil hasa kulingana na mahusiano mazuri na ya muda mrefu yaliyopo kati ya nchi hizo mbili.

  Kufutia wito huo wa Balozi wa Brazil Nchini, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nchi ya Brazil kuja nchini kutangaza bidhaa wanazotengeneza hasa ndege kama hatua ya kuimarisha mahusiano ya biashara kati ya Brazil na Tanzania.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kutokana na nchi ya Brazil kupiga hatua kubwa katika uzalishaji wa sukari na Tanzania ni moja ya nchi yenye  maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji huo hivyo ni muhimu kwa wafanyabiasha wa Brazil kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta hiyo.

  Kuhusu kilimo cha Pamba nchini, Balozi wa Brazil Carlos Alfonso Puente amesema serikali ya nchi hiyo imeanzisha mradi kabambe unaolenga kusaidia uzalishaji bora wa pamba katika mikoa ya kanda ya ziwa mradi ambao utagharimu dola za Kimarekani milioni Sita kwa miaka minne nchini.

  Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mazungumzo yake na Balozi wa Kenya hapa nchini Chirau Ali Makwere amesisitiza kudumishwa na kuendelezwa kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya hasa katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo Mbili.
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito maalum kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya kufanya biashara na nchi ya Kenya kutokana na nchi mbili kuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara.

  Wakati huo huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Hebogand Jensen ambaye amemweleza Makamu wa Rais nia ya nchi hiyo kwa ushirikiano na nchi nyingine ya kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea wilayani Kilwa.

  Balozi huyo wa Denmark nchini amesema anaimani kiwanda hicho kitakachojengwa nchini kitafanya uzalishaji mkubwa na kutoa ajira kwa mamia ya wananchi wa Tanzania.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali katika kuelekea kwenye uchumi wa viwanda imeweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini kama hatua ya kukuza uchumi wa nchi.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati alipotembelea ofisi hizo mkoani Mwanza.
   Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), Bw. Erick Hamis akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya utendaji wa kampuni hiyo katika ukanda wa Ziwa Viktoria, mkoani Mwanza.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati wa ziara ya Waziri huyo katika ofisi hizo mkoani Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, wakati alipotembelea ofisi za Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), mkoani Mwanza.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema atabadilisha uongozi wa menejimenti ya kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), kwa kushindwa kutekeleza uendeshaji na usimamizi wa kampuni hiyo.

  Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo na kuonesha kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na MSCL, Prof. Mbarawa amesema kutokana na kampuni kushindwa kujiendesha kibiashara na kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake amelazimika kuchukua maamuzi hayo ili kuinusuru kampuni hiyo.

  “Sijaridhishwa na taarifa za mahesabu yenu katika uendeshaji wa huduma za meli katika ukanda wa Ziwa Viktoria, Hamuwezi kusafirisha mizigo milioni 3.6 na nyie mkapata faida ya laki 2.. hamuomyeshi umakini kwenye utendaji”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Aidha, katika kuhakikisha huduma za Kampuni hiyo zinaimarika Serikali kupitia Waziri huyo imeahidi  kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukabarati wa meli nne zilizokuwa zimekufa katika ukanda huo ili kuboresha huduma za usafiri wa Ziwa.

  Prof. Mbarawa amezitaja meli zitakazokarabatiwa ni Mv. Clarious, Mv Serengeti, Mv Sangara na Mv. Ukerewe ambazo zinahitaji ukarabati wa injini, mifumo ya umeme na ufundi na gia boksi.

  Amewatahadharisha watumishi wachache wanaofuja fedha katika kampuni hiyo na wale wazembe wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kuacha maramoja kwani Serikali haitamvumilia mtumishi anayefanya vitendo hivyo.

  Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Erick Hamis, amezitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili MSCL, kuwa ni uhaba wa watumishi wenye weledi na ujuzi  hususan wenye taaluma ya uhandisi  na kukosekana kwa mfumo imara na wakisasa wa udhibiti na ukusanyaji mapato.

  “Kampuni inapoteza mapato kutokana na mfumo wa kizamani wa ukusanyaji mapato, fedha nyingi zimekuwa zikipotea na kutumika kusikojulikana, hivyo basi tumeamua kuhakikisha tunaboresha mfumo huu ili kupata mapato zaidi”, amesema Kaimu Meneja Mkuu.

  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella, ameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua ya ukarabati wa meli ya Mv Serengeti ambayo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Bukoba katika usafirishaji wa ndizi na mbao. 
  Amewasihi wafanyakazi kuondoa dhana iliyojengeka ya kufanya kazi kiholela na kwa mazoea na badala kutoa ushirikiano kwa Kaimu Mkuu huyo na Menejimenti itakayoundwa ili kufufua upya kampuni hiyo.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo yao yalijadili masuala mbalimbali ya Wahamiaji pamoja na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo yao yalijadili masuala mbalimbali ya Wahamiaji pamoja na uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na shirika hilo. 

  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

  Kamati ya kuwezesha na kuboresha usafiri wa anga ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imekutana kwa siku tatu mjini Zanzibar  ikiwa ni sehemu ya mikakati ya nchi wanachama kuboresha sekta hii ya uchukuzi katika nchi wanachama.

  Mkutano huo wa 41 umefunguliwa  rasmi na Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Ali Abeid Amani Karume, ambaye amesema  miundombinu katika viwanja vingi vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinahitaji kuboreshwa ili kumudu ushindani wa kibiashara katika sekta hii. 
  Aidha, amezungumzia umuhimu wa nchi wanachama kupunguza tozo kwa kampuni zinazotoa huduma za usafiri wa anga ili kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta.

  Waziri huyo  amesisitiza umuhimu wa   watalaam wa usafiri wa anga katika nchi za Afrika Mashariki kupatiwa mafunzo ya kutosha  kuimarisha ujuzi  na uwezo wa utendaji kumudu majukumu yao. 

  Awali wajumbe zaidi ya 70 wa kamati ya Kuwezesha Usafiri wa Anga katika nchi za Afrika Mashariki walitembelea kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) ili kujionea  miundombinu na huduma zinazotolewa katika kiwanja hicho cha ndege.


  Wajumbe hao wa kamati ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya,  Uganda na Mwenyeji Tanzania hukutana mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kujadili  ubora wa utoaji huduma za usafiri  anga kwa abiria na mizigo .

  Kamati hiyo hujadili changamoto na kupendekeza suluhu za kuboresha sekta hiyo kwa lengo la kuwezesha sekta hii kutoa mchango katika kukuza uchumi wa nchi wanachama.
   Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akizungumza katika  mkutano wa kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki Unaofanyika  Zanzibar.
   Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akifungua  rasmi mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar leo.
  Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akiwapongeza Wajumbe waliostaafu wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki kwa mchango  wao katika Kamati.
   Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki walipotembelea Kikosi cha Zimamoto katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA) 
   Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amani  Karume,(Kulia) akishiriki Mkutano wa 41 wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari


  0 0

  Aliyekuwa Mratibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, na Baadaye Mratibu wa Kampeni wa ACT Wazalendo wakati wa uchaguzi Mkuu ulipita, Nixon Tugara akikabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipoamua kuhamia CCM wakati wa uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
  Nixon Tugara akifurahia kadi yake ya CCM baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo
  Tugara ambaye ni miongozi mwa watu waliosimamia ujenzi wa jengo hilo la Kitegauchumi akizungumza yaliyomsibu hadi kuhamia CCM, kutoka ACT Wazalendo na Chadema.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdultrahman Kinana akimshukuru Tugara kwa kuwa miongoni mwa viongozi waliosaidia katika kufanikisha ujenzi wa jengo la Kitegauchumi la CCM, lililopo Upanga jijini Dar es Salaam, ambalo amelizindua leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji.
  Tugara akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutokea Chadema, wakati wa hafla hiyo.

older | 1 | .... | 1069 | 1070 | (Page 1071) | 1072 | 1073 | .... | 1898 | newer