Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

MFUMO WA JAZIA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI ‘PRIME VENDORS SYSTEM’ WAZINDULIWA SHINYANGA

$
0
0

siiii

Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na shirika serikali ya Uswizi leo Jumanne Desemba 13,2016 umezindua Mpango wa Mzabuni teule “Mfumo wa Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi”.
Mfumo wa Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja ‘Prime Vendor’ ni moja ya mafanikio ya ushirikiano wa sekta binafsi na serikali ukiwa na lengo la kujazia upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya umma vya kutolea huduma za afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,katibu tawala wa mkoa huo Albert Msovela aliyekuwa mgeni rasmi alisema lengo la mfumo huo ni kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya afya kutoka Bohari kuu ya dawa.
Alisema kutokana na bohari ya dawa ya serikali kutokidhi mahitaji kila halmashauri hununua dawa kutoka kwa wazabuni wanaowataka matokeo yake bei ya dawa inakuwa kubwa,mlolongo mrefu wa manunuzi na kukosekana kwa njia rahisi ya usimamizi wa mfumo wa ugavi na usambazaji.
“Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na mradi wa Tuimarishe Afya( HPSS Project) unaofadhiliwa na serikali ya Uswizi kupitia shirika lake la Maendeleo (SDC) umeamua kutafuta njia ya kuziba pengo linalosababishwa na ukosefu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi kutoka bohari kuu ya dawa kwa kutumia mfumo wa manunuzi ya nje ya bohari kuu unaohusisha mzabuni mmojatu kwa mkoa mzima,ambaye sasa Bahari Pharmacy Limited”,alieleza Msovela.
Naye mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo alisema mkoa wa Shinyanga ni wa pili baada ya Mkoa wa Dodoma kuanza kutekeleza Mpango wa Mzabuni teule huku akisisitiza halmashauri kusimamia matumizi bora ya dawa na wazee kuendelea kupewa kipaumbele.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wakuu wa wilaya,Mkurugenzi wa Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS),mkurugenzi wa MSD,Mfamasia mkuu wa serikali,mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa halmashauri na wageni mbalimbali.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 40 kutoka kwenye uzinduzi huo….Tazama Hapa Chini
Kwa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale,katikati ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Desemba 13,2016 wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi ambapo alisema mfumo huo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga .Aliongeza kuwa bohari ya dawa ina uwezo wa kuhudumia wateja kwa asilimia 57 pekee katika mkoa wa Shinyanga.
Wa kwanza kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo
Wadau mbalimbali wa afya mkoani Shinyanga
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System” yaani Mfumo Jazia Dawa,Vifaa Tiba na Vitendanishi una lengo la kujazia dawa kwenye vituo vya serikalivya kutolea huduma za afya.
Kulia ni kaimu mkurugenzi wa idara ya Ununuzi na Ugavi ofisi ya rais TAMISEMI Datus Matuma,katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi.Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Wakuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba,Shinyanga Josephine Matiro na Kahama Fadhili Nkurlu wakiwa ukumbini
Mbele ni makatibu tawala wa wilaya ya Kishapu,Kahama na Shinyanga
Wenyeviti wa halmashauri za wilaya katika mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Kaimu Mkurugenzi Idara ya afya ofisi ya rais TAMISEMI Deogratius Maufi akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Mzabuni Teule “Prime Vendor System
Kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiwa na Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu kutoka jijini Dar es salaam ambaye ndiye mzabuni mteule aliyeshinda kati ya wazabuni 14 walioomba kuwa wasambazaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi katika mkoa wa Shinyanga
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisaini mkataba kati ya mkoa wa Shinyanga na Mzabuni “Bahari Pharmacy Ltd” ambao watakuwa wasambazaji wakuu wa dawa katika vituo vya afya vya serikali mkoani Shinyanga
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisaini mkataba
Zoezi la kusaini mkataba linaendelea
Mwanasheria kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Lightness Tarimo akisaini mkataba huo
Zoezi la kusaini mkataba linaendelea
Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu kutoka jijini Dar es salaam akisaini mkataba
Viongozi wa halmashauri za wilaya wakisaini mktaba huo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga akisaini mkataba huo
Viongozi wa halmashauri mbalimbali wakiendelea kusaini mkataba huo
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela (kushoto) akikabidhiana mkataba na Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje akichangia hoja ukumbini
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Jazia dawa,vifaa tiba na vitendanishi kwa kutumia mzabuni Teule Mmoja ‘Prime Vendor’
Uzinduzi unaendelea
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga akionesha mkataba baada ya uzinduzi
Kushoto ni Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akipongezana na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela baada ya uzinduzi
Uzinduzi umamelizika
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini……
Wadau wa afya wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza baada ya uzinduzi huo
Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale akizungumza ukumbini
Mwakilishi wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Siana Mapunjo akiwa na Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale
Katikati ni Meneja wa mradi wa Tuimarishe Afya mkoa wa Shinyanga Dr. Harun Kasale akisisitiza jambo
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr. Ntuli Kapologwe akiwa ukumbini
Mkuu wa Masoko kutoka Bahari Pharmacy Limited Richard Olotu akielezea namna alivyojipanga kuhakikisha kuwa dawa nyingi zinawafikia walengwa mkoani Shinyanga hivyo kuomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa viongozi wa mkoa ili kufanikisha malengo yao.
Picha ya pamoja viongozi mbalimbali wa kitaifa,mkoa na wilaya za mkoa wa Shinyanga
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Don King, Mayweather wampa ‘ndondo’ meneja wa Cheka za kuandaa mapambano ya ngumi za kulipwa

$
0
0
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota na tajiri duniani, Floyd Mayweather Jr wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na promota nyota dunaini, Don King wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota Wladimir Klitschko wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wa bondia nyota marehemu Mohammed Ali wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota mtaafu, Evander Holyfied wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.



Meneja wa mabondia nyota nchini, Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile amesema amejifunza na anaendelea kujifunza masuala mbalimbali ya kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa duniani kupitia kwa mapromota wakubwa kama Don King.


Ndambile kwa sasa yopo nchini Marekani akihudhuria mkutano wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) ulioanza jana kwenye ukumbi maalrufu wa Hollywood. Akiwa Mtanzania pekee katika mkutano huo, Ndambile alisema kuwa ameweza kujiunganusha na mapromota nyota duniani ili kuleta maendeleo katika mchezo huo hapa nchini.

Alisema kuwa ameweza kujadiliana na mapromota kadhaa ambao wanajua umuhimu wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kupitia kampuni yake ya Advanced Security Limited ataweza kuandaa mapambano ya ngumi ya Kimataifa, yenye ubora wa hali ya juu.

“Ubora huo utatokana na mbinu za kutafuta masoko ya ‘kuuza’ pambano au mapambano ya ngumi, mchezo wa ngumi unapendwa sana, hivyo nikiwa Mtanzania pekee niliyepata fursa hiyo, nitaitumia ipasavyo ili kufikia malengo niliyojiwekea na kwa faida ya Tanzania,” alisema Ndambile kwa njia ya simu.

Alisema kuwa ameweza kupata ‘contact’ za mabondia makubwa, lengo kuu ni kuongeza wigo wa kazi zake na kufikia hatua ya juu kabisa katika ngumi za kulipwa.“Kinchotakiwa hapa ni kuwa makini na ‘serious’ katika kazi, ukichukulia mchezo wa ngumi kimchez mchezo, hautafikia mbali, lakini ukiuchukulia kama kazi na lengo ni kuendeleza vipaji na kujiongezea kipato, utafaidika wewe na mabondia wao,” alisema.

Mbali ya Dong King, Ndambile alikutana uso kwa uso na mabondia nyota kama Floyd Mayweather, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield, Lennox Lewis, Mike Tyson, Amir Khan na wengine wengi.

Alisema kuwa umoja ni selaha pekee ya kuendeleza mchezo wa ngumi hapa nchini. “Tofauti na wenzetu, hapa kwetu ni chuki, unafiki na mizengwe kibao, wenzetu wanashirikiana, lengo ni ‘kuuza’ mchezo na si vinginevyo, mtu akiandaa pambano, wanashirikiana wote,” alisema.

Mkutano huo umeshirikisha wadau wa ngumi za kulipwa zaidi ya 1000, unatarajia kumalizika Desemba 17. Mbali ya kutoa tuzo kwa mabondia na majadiliano kadhaa, mkutano huo pia ulimuenzi bondia nyota, marehemu, Mohamed Ali ambapo wadau wote walipiga picha kwenye sanamu yake.

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAINGIA MKATABA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA

$
0
0

Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya.


Na JamiiMojaBlog

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, leo imeingia mkataba na makandarasi mbalimbali wa ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja katika Kata 14.Mkataba huo, umesainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi huku ukishuhudiwa na baadhi ya madiwani wa Kata husika pamoja na mwanasheria wa halmashauri hiyo Davis Mbembela.

Awali akizungumzia tukio hilo kabla ya kusaini, Meya Mwashilindi amesema, mkatba huo, unalenga kuboresha miundombinu katika baadhi ya kata katika halmashauri hiyo ambapo kazi hiyo inataraji kuanza mapema mwezi huu.Aidha, amesema kuwa mkataba huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 300 na kwamba kazi kubwa itakayofanyika ni uboreshaji wa barabara na matengenezo ya madaraja katika kata 14 kati ya 36 zilizomo ndani ya Jiji la Mbeya.

“Kampuni zilizoingia mkataba leo ni tano na zote ni makandarasi wa ndani na kubwa zaidi ni wazawa,”amesema.Pia, Mwashilindi amewataka makandarasi waliochukua kazi hizo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa muda muafaka huku akiwatoa hofu juu ya fedha, kwani bajeti ya matengenezo hayo tayari imeidhinishwa..

Hata hivyo, katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100, Mwashilindi amewataka watendaji pamoja na madiwani kuhakikisha wanatembelea na kukagua miradi hiyo, wakati ikiendelea kufanyika na kuachana na tabia ya kusubili mradi ukamilike na kukabidhiwa na ndipo kuanza kubaini kasoro.

“Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi na asilimia kubwa inatokana na kodi za wananchi hivyo ninawaombeni madiwani na watumishi hasa wa idara husika kuhakikisha mnatembelea na kuukagua mradi huu wakati wote wa mchakato, sitapenda kusikia changamoto mara baada ya mradi kukamilika,”amesema.
Baadhi ya Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata jijini Mbeya
Baadhi ya Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata jijini Mbeya hafla ambayo imehudhuriwa pia na baadhi ya madiwani na watendaji wa halmashauri ya jiji katika ofisi ya Meya .

Prof Kamuzora atambulishwa kwa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimtambulisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mbele ya menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Utambulisho huo umefanyika leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Menejimenti wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kutambulishwa.

Tanzania yetu maliasili zetu,Msimu wa sikukuu ndio huu

$
0
0
Tanzania yetu maliasili zetu Hakuna jambo zuri kama kusherekea Sikukuu ukiwa kwenye mandhari  tulivu ambayo itakufanya ussosike na chakula kizuri  huku ukifanya vitu vipya au kuona vitu tofauti ambavyo huvioni mara kwa mara katika mzunguko wako wa maisha.

Msimu wa Sikukuu ndiyo huu!!! Fanya sikukuu yako kuwa ya kipekee kwa kutembelea HIFADHI ZA TAIFA. Tuendelee kusapoti Utalii wa Ndani kwa kutembelea #HifadhiZetu. More info piga 0784133217| 0765908073. 

HapaKaziTU

SERIKALI YAZINDUA MPANGO KAZI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO.

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  
 
Na: Eliphace Marwa – MAELEZO.
 
 
SERIKALI imezindua  Mpango Kazi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto unaolenga kushirikisha wadau wengine katika jitihada jumuishi za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na hivyo kusaidia wahanga wa ukatili huo kupata huduma stahiki ili kudhibiti ukatili nchini.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa jamii inajukumu la kuhakikisha ukatili wa wanawake na watoto unapigwa vita kwa vitendo.
 
“Serikali inaikumbusha jamii kupambana na vitendo vya ukatili kwani ukatili unafanyika kuanzia ngazi ya familia hivyo ni jukumu la wananchi kutoa taarifa za ukatili wa wanawake na watoto ili vyombo vya dola viweze kuwachukulia hatua za kisheria”, alisema Waziri Ummy.
 
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa Kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili yanayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umaskini katika familia, mila na desturi potofu zenye athari katika jamii, malezi na makuzi mabovu na sheria kandamizi.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Asasi za Kiraia zinazoshughulika na utetezi wa haki za watoto (TCRF) Bw. Erick Guga amesema kuwa watoto ndiyo wahanga wakubwa wa ukatili huu hivyo ni wakati muafaka kwa mpango kazi kuanza kazi ili kuwanusuru wanawake na watoto katika ukatili.
 
“Mpango Kazi huu wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto nchini Tanzania utakuwa ndiyo dira kwa wadau wote wa masuala ya maendeleo ya wanawake na watoto hapa nchini hivyo ni vema Serikali kushirikiana na wadau kila inapohitajika”, alisema Bw. Guga.
 
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema kuwa, kabla ya kuandaliwa kwa Mpango Kazi huu, Tanzania ilikuwa na mipango kazi minane (8) ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
 
Aidha Bi. Sihaba ameongza kuwa mipango hiyo haikuwa na mfumo wa pamoja wa kufuatilia na kutathmini ufanisi unaopatikana. Vilevile, kutokana na madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maendeleo ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa nchi wanachama waliazimia kwa pamoja kutokomeza ukatili huo kupitia utekelezaji wa lengo Na. 5 na 6 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo 2030.
 
“ Tanzania ni kati ya nchi nne (4) za kwanza duniani na nchi pekee katika Afrika iliyowezeshwa kupitia jukumu lilioanzishwa la kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuandaa mpango wa kuzuia na kuitikia afua za kudhibiti ukatili ili kuwa na mipango thabiti ya upatikanaji wa haki, usawa na maendeleo kwa wote”, alisema Bibi.Sihaba.
 
Akieleza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Sera na Mipango Emmanuela Achayo aliseama kuwa Mpango kazi huo wa aina yake una maeneo makuu manane (8) yatakayotekelezwa na wadau wa maendeleo ya wanawake na watoto.
 
“Maeneo hayo ni kuimarisha uchumi wa kaya, Uzuiaji wa mila na desturi zenye madhara na Uboreshaji wa mazingira salama katika jamii”, alisema Achayo.
 
Maeneo mengine ni Kuendeleza mazingira salama ya mafunzo shuleni na stadi za maisha na kuhuisha mahusiano, malezi na makuzi katika familia, Utekelezaji na usimamizi wa sheria, Utoaji huduma kwa wahanga na Uratibu, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa miaka mitano kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 20121/21022.
 
Mpango huu mahususi unatarajiwa kuwa na matokeo makubwa baada ya miaka mitano ya utekelezaji kwani utawezesha kuondoa ukatili dhidi ya wanawake kwa asilimia 50 kufikia mwaka 2021/2022; na Kuondoa ukatili dhidi ya watoto kwa asilimia 50 kufikia mwaka  2021/2022, na hivyo kuleta mabadiliko makubwa kwa kuwa na familia salama, na jamii yenye utulivu.
 
Kazi zitakazotekelezwa na kila mdau kuanzia familia, jamii, halmashauri, mikoa, wizara, sekta binafsi, asasi za Kiraia na wabia wa maendeleo Mpango umeweka mfumo fungamanishi wa uratibu, ufuatiliaji na tathmini ambao utaratibiwa katika ngazi ya Taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ngazi ya mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, na ngazi ya halmashauri na Wakurugenzi Watendaji.

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA POLISI ZANZIBAR, APIGA MARUFUKU MIRADI BINAFSI ENEO LA JESHI

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kaunda suti) akitoka ndani ya Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo. Naibu Waziri huyo alitoa agizo kwa Kamishna Hamdan Omar Makame (hayupo pichani) kuwaondoa haraka wamiliki wa miradi mbalimbali iliyopo eneo la Kituo hicho pamoja na katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, Zanzibar. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi wa Bomani, Drill Shed, Unguja, Zanzibar. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Omar Makame pamoja na Watendaji wengine wa Jeshi hilo, wahakikishe wanawaondoa wamiliki wote wa miradi binafsi katika eneo la Jeshi kwa kuanzia na Kituo cha Polisi Bububu. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akionyeshwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Abdulhalim Ali Haji, mpaka wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alipiga marufuku miradi binafsi iliyozunguka kituo hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar, Mohamed Talihata, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati kiongozi huyo alipofanya mazungumzo na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Unguja. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar, Mohamed Talihata, akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati kiongozi huyo alipofanya mazungumzo na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Unguja. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani, Zanzibar, Kamishna Msaidizi, Mkadam Khamis alipokuwa anatoa taarifa ya Usalama Barabarani katika kikao kilichowashirikisha Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na Askari wa Usalama Barabarani, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bomani, Drill Shed, Zanzibar. Masauni aliwataka askari hao kuwakamata madereva wote wanaovunja sheria za barabarani na kuwachukulia hatua kali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rais Magufuli amteua Bw. Ngusa Dismas Samike kuwa Mnikulu

$
0
0
Bw. Ngusa Dismas Samike ambaye ameteuliwa kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu.


HAYA NDIYO MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM BAADA YA KIKAO CHAKE CHA SIKU MOJA

$
0
0
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-

1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.

Ili kuwa  na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-

a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama  ifuatavyo:-

Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya Bara           26x1                               =      26
Mikoa ya Zanzibar      6x1                              =          6

Wajumbe wa NEC wa Mikoa
 Mikoa ya Bara                      26x1         =        26
 Mikoa ya Zanzibar                    6x4         =        24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
 Kutoka  Bara                                   =               15
 Kutoka  Zanzibar                           =               15

Nafasi za Mwenyekiti                    =                7

Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
        UVCCM                                                =        5
        UWT                                                     =        5
        WAZAZI                                               =        5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni     =        5

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM      =       1

Wajumbe wa  NEC kutoka BLW                     =       3

Katibu wa Kamati ya Wawakilishi                =       1

Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa CCM                  =       1
- Makamu Mwenyekiti (B)         =       1
-Makamu Mwenyekiti (Z)           =       1
- Makamu wa Rais                        =       1
-  Waziri Mkuu                               =       1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z)   =       1
- Spika wa Bunge                          =       1
- Spika  wa  BLW                           =       1
- Mwenyekiti wa UWT                =       1
- Mwenyekiti wa WAZAZI          =       1
-Mwenyekiti wa UVCCM             =       1
- Katibu Mkuu – WAZAZI            =       1
- Katibu Mkuu – UWT                   =       1
- Katibu Mkuu – UVCCM              =       1
                                              Jumla:      158
#. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM        (Zanzibar)
Makamu wa  Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika  wa BWL
Mwenyekiti  wa WAZAZI
Mwenyekiti  wa UWT
Mwenyekiti  wa UVCCM
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Organaizesheni
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Itikadi na Uenezi
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Uchumi na Fedha
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe  watatu (3)  wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania 

Wajumbe watatu  (3) wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.

#. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada  ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe  watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa         -       1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa        -       2

#. Vikao  vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya    -       1
 Katibu wa Kamati ya Madiwani                   -       1
 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)-  2
                                                                            Jumla:  4

#.Vikao  vya kawaida  vya Kamati ya Siasa ya Wilaya  vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.

Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50  hadi 300.

Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.

Vikao vya kawaida vya  Kamati za Siasa  za  ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi  moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.

#. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.

#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo  ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.

#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM  na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu.   Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu.

#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za CCM  zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na  matakwa ya Katiba ya CCM.

#.Uaendeshaji  wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu  na  Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

#. Wakati tukiendelea kubaki  na Bendera yenye rangi ya kijani na njano  na  alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.

#. Utumishi  katika  Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake.

Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya  za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa.  Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.

#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na  Uchaguzi wa    Zanzibar .
Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.

# Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017.

#. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.

#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya  za Chama.

#. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba.

Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.

Imetolewa na:-

NAPE NNAUYE 
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI 
13/12/2016

Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence melo ashikiliwa na jeshi la polisi, kupanda kizimbani leo

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, 
kampuni inayomiliki mtandao maarufu, Jamii Forums, Maxence Melo.

Maxence Melo ambaye ni mwanzilishi wa Jamii Forums, anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam (Central Police) toka jana na leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyoko Mtaa wa Lumumba kwa madai kuwa amekataa amri ya jeshi la polisi kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao huo, Max amenyimwa dhamana.

“Maxence Melo amekamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari,” umeandika mtandao huo.

YALIYOJIRI USIKU WA EATV AWARDS 2016

Skauti wa Afrika ya Mashariki wakutana jijini Arusha kwa mashindano ya stadi na kongamano

$
0
0
Skauti kutoka nchi za Afrika ya Mashariki, wapo jijini Arusha kwa mashindano ya stadi za kiskauti ambayo yalianza Jumatatu tarehe 12 Desemba 2016 na yatafikia kilele chake tarehe 16 Desemba 2016.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Msaidizi (Mawasiliano na Habari) wa Chama cha Skauri  Tanzania, Bw. Hidan Ricco, Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa shule ya Breburn International iliyopo eneo la Kisongo Arusha. 

Bw. Ricco amesema kwamba sambamba na hayo mashindano Skauti pia wanashiriki katika Jukwaa la Vijana (youth Forum) katika hoteli ya Crown iliyopo katikati ya Jiji la Arusha. sambamba na  Mkutano wa Makamishna Wakuu wa Skauti kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Amesema shughuli zote hizo tatu  zitafikia kilele chake siku ya Ijumaa tarehe 16 Desemba 2016 na zinatarajiwa kutafungwa rasmi na Mkuu wa Majeshi wa Nchi ya Uganda.
 Skauti wa TZ na wengine wa  nchi za    Afrika Mashariki  wakipita mbele ya  mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa    kambi ya mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea  mkoani   Arusha
Skauti wa Tanzania  na wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa     kambi ya mashindano inayoendelea mkoani Arusha.
 Skauti kutoka Kenya   na wengine wa    nchi za Afrika Mashariki  wakipita mbele ya  mgeni rasmi wakati wa   ufunguzi wa kambi ya mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki   inayoendelea mkoani Arusha
 Kamishna Mkuu wa Skauti Kenya bw.  Ray Charles Musau akizungumza na skauti wa nchi za Afrika Mashariki wakati  wa ufunguzi wa kambi ya mashindano inayoendelea mkoani Arusha.

WATUMISHI WA KARAKANA ZA TEMESA WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI.

$
0
0

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akizungumza na watumishi wa karakana za TEMESA wakati akifungua mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya watumishi wa karakana za TEMESA wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam.


Na Theresia Mwami TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu leo amefungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa karakana juu ya mfumo wa utozaji gharama za matengenezo ya magari katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za uzalishaji na matengenezo za kila mwezi.

Dkt. Mgwatu amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuleta uwiano sawa katika gharama za matengenezo ya magari kwa karakana zote za TEMESA bila kujali mikoa zilipo karakana hizo.

Aliongeza kuwa utaratibu utakaoelekezwa katika mafunzo hayo utasaidia kupunguza gharama za matengenezo ya magari ya serikali, suala linalolalamikiwa na wateja wa TEMESA kwa muda mrefu sasa.

“Nataka sasa tuanze kutoza gharama za matengenezo ya magari kulingana na muda unaotumika kutengeneza gari husika (man hour), badala ya kutumia kigezo cha asilimia ya fedha iliyotumika kununulia vipuri kwa ajili ya matengenezo ya magari, kwani baadhi ya vipuri ni ghali sana lakini hutumia muda mchache sana kuvifunga,” alisema Dkt. Mgwatu.

Dkt. Mgwatu alisema kuwa, kumekuwa na changamoto ya uwasilishaji wa taarifa za utendaji kutoka katika mikoa/vituo vya TEMESA, mara nyingi taarifa hizi hazifiki kwa wakati. Huku akisisitiza kuwa ni matumaini yake baada ya mafunzo hayo taarifa hizo zitakuwa zikifika kwa wakati tena zikiwa sahihi.

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Matengenezo, Mhandisi Sylivester Simfukwe alisema idara yake imejipanga kutoa huduma bora zinazokidhi viwango hasa katika matengenezo ya magari ya serikali, ili kuhakikisha kuwa uzalishaji unaongezeka na kero za wateja zinakwisha.

Aliongeza kuwa mafunzo kama hayo yatatolewa kwa wawakilishi wa karakana zote za TEMESA nchi nzima.

Mafunzo hayo elekezi juu ya Mfumo wa utozaji gharama katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za kila mwezi, yanafanyika kwa siku 5 katika ukumbi wa MT. Depot, Dar es salaam na yamehusisha watendaji wa TEMESA kutoka mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara, pamoja na vituo vya MT. Depot na Kikosi cha Umeme.

AIRTEL FURSA YAZIDI KUNUFAISHA VIJANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

$
0
0
 Kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando  na maafisa biashara wa Airtel Mtwara Jerry Issaya  na Moses Bhalalusesa wakiongea na mmoja wa wanufaika wa mradi wa Airtel Fursa mkoani Mtwara bi. Prisca Chilumba (aliyesimama) walipomtembelea mnufaika huyo katika saluni yake mpya mkoani Mtwara. Airtel ilifanya ziara hiyo ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha msaada huo ili aweze kutimiza ndoto zake. 
Kushoto ni Katibu wa Lindi Sauti ya Jamii kundi la wajasiliamali la bw, Salum Muunguja- na mwenyekiti wake Shaban Zuberi wakionyesha mmoja kati ya mbuzi 10 wa kisasa walionunua baada ya kuweshwa na mradi wa kijamii wa Airtel Fursa mara baada ya kutembelewa na Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando na meneja biashara wa mkoa huo bw, Saleh safy. Airtel ilifanya ziara hiyo ili kujionea maendeleo yao pamoja na kuboresha  kuboresha msaada wao ili vijana waweze kukabiliana na changamoto zilizojitokeza. Habari kamili BOFYA HAPA

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LANG’ARA TENA TUZO ZA UBORA DUNIANI.

$
0
0
Makamu wa Rais wa ShirIka la Ndege la Etihad, Kitengo cha Huduma kwa Wateja Linda Celestino na Meneja Masoko na Mawasiliano Abdulrahman Al-Hadhrami, wakipokea tuzo za  ‘World's Leading Airline’ na ‘World's Leading Airline - First Class’ wakati wa sherehe za 23 za utoaji tuzo hizo zilizofanyika Maldives.

Shirika  la Ndege  la Etihad kwa mara nyingine limenyakua tuzo ya watoa huduma bora wa kwanza zilizotolewa kwa mara ya 23 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) katika sherehe zilizofanyika mwaka huu.

Ushindi huo umelifanya Shirika hilo kufikisha tuzo nane kwa mwaka huu ambazo limezipata kutoka kwa taasisi zinazoheshimika ulimwenguni. Sherehe za kukabidhiwa tuzo hizo zilifanyika kwenye ufukwe wa Sun Siyam Iru Fushi katika visiwa vya Maldives.

Shirika hili la ndege la Etihad pia lilipokea tuzo ya  kuwa watoa huduma bora kwa daraja la kwanza na ukarimu unaotolewa kwa kiwango cha hali ya juu ikiwa ni pamoja na kupigiwa kura kutokana na kuwa na machapisho bora, ushauri na huduma bora zaidi kwa wateja. Tuzo za The World Travel zinajumuisha idadi kubwa ya wapiga kura waliopo katika sekta ya usafirishaji pamoja na watu wengine kutoka kwenye jamii wapatoa  wapigakura 1.2 kwenye Grand Tour 2016.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad alisema, “Dhamira yetu ni kuandaa sera na kuleta mabadiliko kwenye sekta ya usafirishaji wa anga ili iendelee kutambuliwa na kupata tuzo kila mwaka. Tunajivunia kwa mara nyingine tena kwa kupata tuzo hizi mbili za heshima kwa kile tunachoamini kuwa watoa huduma bora na wenye uzoefu kwenye sekta ya usafiri wa anga”

Tuzo za Wold Travel ni jambo la msingi ambapo imewezesha kuonyesha mafanikio ya shirika letu la ndege la Etihad  na kuleta mabadiliko Abu Dhab ambako ndio makao makuu ya shirika hili na kuufanya mji huo kuwa kitovu cha kibiashara na utamaduni ulimwenguni kote.

Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa shirika hili la ndege kupokea tuzo mbalimbali za ubora na huduma. Ndani ya mwaka huu tuzo kadhaa zimenyakuliwa zikiwamo ubora wa daraja la kwanza, na nyingine ya hivi karibuni ya utoaji hudma bora Mashariki ya Kati  na huduma bora za mapumziko kwenye uwanja wa ndege katika ukanda huo.

Rais wa Tuzo za Wold Travel, Graham Cooke alisema, “Kwa mara nyingine tena shirika la ndege la etihad limekuwa kinara kwenye sekta ya usafiri wa anga . Wapigakura wa tuzo za Worl Travel hujumuisha wadau waliopo kwenye sekta ya anga pamoja na umma wa watu wengine, ambao ambao wametambua mchango wa shirika hili kwenye usafiri wa anga na kujizolea tuzo. Bila shaka shilika hili lilistahili kupokea heshima hii.”

“Salamu zangu za pongezi nazielekeza kwa timu ya wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Etihad kwa kupata mafanikio haya makubwa na ninatumaini huu ni mwanzo wa kujiandaa na Grand Tour 2017,” Alisema.

Mambo 8 ya kuzingatia pindi unapotaka kusafiri

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Hakuna jambo linalokera kama kugundua kuwa umesahau kitu fulani ambacho kilikuwa kina umuhimu mkubwa sana kwenye safari yako uliyokwishaianza.

Hali kama hii huwa inawatokea watu wengi hivyo kupelekea kuchelewa au wakati mwingine kuachwa kabisa na usafiri.

Kuepukana na usumbufu huu hasa ukizingatia asilimia kubwa ya watu wako kwenye pilikapilika za kusafiri kipindi hiki cha sikukuu na shamrashamra za mwaka mpya, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukutahadharisha kuzingatia yafuatayo ili safari yako iwe ya raha mustarehe.

Tafiti kuhusu mahali unapokwenda.

Ni muhimu kufahamu mahali unapokwenda hasa umbali wake, itakugharimu kiasi gani kufika, hali ya hewa, gharama za maisha pamoja na mila na utamaduni za watu wanaoishi huko. Kama unasafiri mkoa ambao haujawahi kufika hapo awali ni vizuri ukafanya tafiti au ukaulizia kutoka kwa marafiki, ndugu na jamaa ili usiende kupata tabu ukifika.  

Tambua usafiri utakaokufikisha huko
Zipo njia nyingi za usafiri za kuweza kukufikisha mahali unapotaka inategemea chaguo, uharaka au uwezo ulionao. Kama unataka kuwahi mahali unapokwenda kutokana na shuguli nyingi au kuepuka uchovu basi usafiri wa anga (ndege) utakuwa ni sahihi kwako. Na kama hautojali kuwahi au uchovu njia ya barabarani kwa kutumia basi itakufaa kwani utaweza kuwa na muda wa kutosha kujionea vitu vingi njiani vitakavyopelekea kunogesha safari yako.

Kata tiketi mapema siku moja kabla ya safari
Usipendelee kukata tiketi siku ya safari kwani unaweza kukuta usafiri haupatikani, nafasi zimejaa, bei imebadilika au kupata basi ambalo halikuridhisha na hadhi yake. Kata tiketi siku moja kabla ya safari kwani itakuondolea hofu ya kutokuwa na uhakika wa kusafiri na kukupa muda wa kupanga mambo mengine vizuri zaidi.

Panga vitu unavyovihitaji kwa ajili ya safari mapema.

Kutojipanga mapema na safari mara nyingi hupelekea mtu kusafiri huku akiwa ameacha vitu muhimu huko mbele aelekeapo. Na kamwe usijidanganye kwamba utaweza kumudu kukumbuka na kupanga vitu vyako vyote unavyovihitaji siku ya safari kwani unaweza ukachelewa kuamka na ukahamaki mwishowe ukajikuta unasahau kubeba vitu vya msingi. Hivyo tunakushauri weka kila kitu unachokiona ni muhimu kwa safari yako ndani ya begi siku moja kabla ya safari bila ya kusahau kuiweka tiketi yako sehemu ambapo unaiona kwa urahisi.

Fahamu mahali utakapolala pindi utakapowasili.

Siku hizi huhitaji kusumbukaili kufahamu sehemu ya malazi kwa sababu taarifa zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. Kwa mfano, ukitembelea mtandao wa Jumia Travel (www.travel.jumia.com) utaweza kuperuzi orodha ya hoteli na sehemu mbalimbali za malazi nchini, utafahamu mahali ziliko, hadhi zake, gharama, upatikanaji na namna ya kulipia.

Amka mapema na wahi kituoni siku ya kusafiri

Kama una mazoea ya kuchelewa kuamka asubuhi ni vema ukaweka kengele ikuamshe asubuhi kupitia simu au kifaa ulichonacho au kumtaafiru ndugu au rafiki akuamshe mapema. Kuamka mapema kunakuwezesha kujiandaa vya kutosha kwa safari hata kukupa kuda wa kukumbuka vitu ambavyo pengine ulivisahau pamoja na kuwahi kituoni tayari kwa kusafiri.

Kuwa makini na vyakula unavyokula njiani.

Huna budi kuzingatia aina ya vyakula utakavyokuwa unakula njiani kwani vinaweza kukudhuru kiafya. Vyakula vinavyopikwa na kuuzwa njiani huna uhakika vinaandaliwa vipi na kupikwa katika mazingira gani hivyo umakini mkubwa unahitajika. Hata hivyo, kutokana na maboresho ya miundombinu siku hizi safari nyingi hazichukui muda mrefu kwa hiyo unaweza ukala vyakula vikavu kama vile keki au mikate pamoja na vinywaji kama maji, soda au juisi mpaka utakapofika ndipo ule chakula cha kutosha.

Jihadhari usiachwe na basi njiani
Kuna matukio kadhaa ambapo abiria huachwa na usafiri hususani kwenye vituo vifupi vinavyowekwa njiani kuwapa fursa abiria kujisaidia au kununua chakula. Kama unajijua ni mzito kula kituoni ni vema ukanunua, ukabeba chakula na kwenda kulia ndani ya basi vilevile kwa kujisaidia nakushauri jisaidie mahali ambapo utaliona basi au abiria unaosafiri nao ili isiwe rahisi kuachwa.

Tunatumaini kwamba mbinu hizi chache zitakusaidia pakubwa katika safari yako unayoitarajia msimu huu wa sikukuu.

KINANA AZUNGUMZA NA WATENDAJI WA CCM WA MIKOA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa mikoa, alipokutana nao katika kikao maalum kilichofanyika jana, katika ukumbi wa Sekretarieti kwenye Ofisi Ndogo  Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.

Watendaji wakiwa ukumbiniKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa mikoa, alipokutana nao katika kikao maalum kilichofanyika jana, katika ukumbi wa Sekretarieti kwenye Ofisi Ndogo a Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine walioko meza kuu, kutoka kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatibu, Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.

MAKALA: HAYA NI MAMBO MBALIMBALI YALIYOFANYIKA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kuelimisha jamii kuzuia ukatili wa kijinsia. WiLDAF inashirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia (MKUKI), wadau wa maendeleo na mashirika mengine kuadhimisha kampeni hizi kitaifa. 

Yafuatayo ni matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kama yalivyofanyika sehemu mbalimbali nchini Tanzania chini ya kauli mbiu: Funguka! Pinga ukatili wa kijinsia. Elimu salama kwa wote. 

Maandamano ya amani kupinga ukatili wa kijinsia Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa jiji la Dar es salaam ulianza kwa maandamano ya amani ambapo maelfu walishiriki maandamano hayo kutoka Biafra hadi Millenium towers jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalifanyika tarehe 25 Novemba 2016. 
Waziri Ummy Mwalimu mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika tarehe 25 Novemba 2016, jijini Dar es salaam. 

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy alisema serikali ya awamu ya tano imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu salama bila aina yoyote ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu bora bila malipo. "Lengo kuu la elimu bila malipo ni kuhakikisha kuwa watoto wetu hususan wa kike wanapata fursa ya kwenda shule kusoma na kufikia ndoto zao katika maisha." 

Aidha alitoa wito kwa wadau na serikali kwa ujumla kutumia nafasi zao kupinga vitendo vyote vya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vilevile kwa jamii kuwa na malezi bora na kuzingatia maadili kwa watoto na vijana wetu. 

Mama Anne Makinda mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la Haki za Wanawake. Aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kwanza la kitaifa la Haki za wanawake lililofanyika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam tarehe 28 Novemba 2016. 

Kongamano hilo lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la LSF lilikuwa na lengo la kujadili namna mbalimbali za kuwawezesha wanawake kisheria na kiuchumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

Jamii imeaswa kuhusika kikamilifu katika mapambano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na salama. Kongamano hilo lilipambwa na kauli mbiu isemayo; Jitambue! Jiamini, Simamia Haki yako. Wageni mbalimbali wanaharakati wa Haki za binadamu walihudhuria kongamano hilo la aina yake wakiwemo Dr. Helen Kijo Bisimba, Mary Rusimbi, Edda Sanga na Dr. Judith Odunga. 
 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe azindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Challya Julius alizindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika wilaya yake na kuahidi kusimamia katika kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani humo. 

Uzinduzi huo ulifanyika 29 Novemba 2016. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia uliotolewa na wasaidizi wa kisheria (Paralegals) wa wilaya ya Rungwe wakishirikiana na shirika la WiLDAF Tanzania. 
 Jukwaa la Wanafunzi wakati wa maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

Wanafunzi wa kidato cha 1, 3, 5 na 6 kutoka shule za sekondari za Benjamin Mkapa, Jangwani, Tandika, Turiani na Temeke walihudhuria jukwaa lilioandaliwa kwa ajili ya wanafunzi ili wapate fursa ya kutoa maoni juu ya mambo mbalimbali yanayowakabili mashuleni. Jukwaa hilo lilifanyika 30 Novemba 2016 katika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam.  Jukwaa hilo liliandaliwa na shirika la WiLDAF Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia. Elimu Salama kwa wote.  Siku ya UKIMWI Duniani 

Januari mosi kila mwaka hutumika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani. Maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia kubwa yanatokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake vinavyopelekea maambukizi ya VVU kama vile ubakaji, mila mbalimbali ambazo zimepitwa na wakati kwa mfano: - - Ndoa za utotoni ambapo mtoto wa kike hulazimishwa kuolewa na mtu mzima ambaye pengine ana maambukizi ya VVU. 

- Mume kumlazimisha mke kufanya tendo la ndoa iwapo mume ameathirika bila kutumia kinga. - Mjane kulazimishwa kufanya ngono na mzee anayetakasa wajane. - Na wajane kulazimishwa kurithiwa na ndugu wa mume wake bila kujali afya ya wote wawili. Jamii inapaswa kuacha na kukemea mila zilizopitwa na wakati ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI. 

 Mdahalo wa wadau wa maendeleo kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Wadau wa maendeleo kutoka mashirika, serikali na taasisi mbalimbali walikutana pamoja ili kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Mdahalo huo ulifanyika Desemba 1, 2016. 
Hizi ni baadhi ya nukuu kutoka katika mdahalo huo; 

"Ukatili wa kijinsia huanzia nyumbani, shuleni na kwenye jamii. Jamii ipatiwe elimu ya kutokomeza ukatili.""Wazazi wawe na ukaribu na watoto katika malezi na kujua mienendo ya watoto wao.""Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa mtukutu ila inatokana na malezi ya nyumbani na muda mwingine kupeleka hivyo vitu shuleni na hata kuwafanyia watoto wengine vitendo vya kikatili.""Ukatili wa watoto unafanywa na ndugu wa karibu wa nyumbani anaweza akawa mjomba, dada wa nyumbani.""Fimbo sio solution (suluhu) ya kumrekebisha mtoto, itafutwe njia mbadala ya kumuadhibu mtoto." 
Vibanda vya Filamu Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, shirika la TGNP Mtandao liliandaa vibanda vya filamu ili kujenga uelewa kwa jamii na kuibua mjadala juu ya vitendo mbalimbali vya ukatili.
Wawakilishi wa Bodaboda wapata mafunzo ya ukatili wa kijinsia, waandamana kupinga ukatili. Wawakilishi wa madereva wa bodaboda kutoka Wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke mkoa wa Dar es salaam walipata mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Madereva bodaboda wanahusika katika kubeba abiria mbalimbali wakiwemo wanafunzi hivyo ni muhimu kuwapatia elimu hii ili waweze kutambua madhara ya ukatili na kusaidia kuilinda jamii dhidi ya vitendo vya ukatili. 

Aidha madereva hao waliungana na shirika la WiLDAF kuandamana kama ishara ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia. 
Kauli mbiu ya maadhimisho ni FUNGUKA! PINGA UKATILI WA KIJINSIA. ELIMU SALAMA KWA WOTE. Kauli mbiu hii inakusudia kuhamasisha jamii na taifa kwa ujumla kuangalia ni kwa kiasi gani changamoto zilizopo katika miundombinu, mifumo ya kibaguzi na kukosekana kwa usawa wa kijinsia, sio tu kunachochea ukatili wa kijinsia, bali pia kunakwamisha juhudi za serikali, asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika kuboresha elimu na hivyo kusaidia watanzania kujikwamua katika wimbi la ujinga na umaskini. #UkatiliSasaBasi 

Maonyesho ya bidhaa ya vyakula kutoka India yafana Jijini Dar es salaam

$
0
0

Balozi wa India Sandeep Arya akiongea na wadau wa biashara wakati wa uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za vyakula kutoka India katika hafla iliyofanyika Hotel ya Golden Tulip, Dar es Salaam mapema jana.

Balozi wa India Sandeep Arya akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa za vyakula kutoka India uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam jana.

Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa maonesho hayo.

Balozi wa India Sandeep Arya akipata maelezo toka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula toka india mara baada ya hafla ya uzinduzi wa maonesho ya bidhaa vya vyakula kutoka India uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam jana.

Maonesho ya bidhaa za vyakula yakiendelea

Dar Es Salaam, Tuesday, 13th December 2016- India is the 3rd largest producer of food in the world. The country has an outstanding competitive strength in food processing, being blessed with unsurpassed natural advantages, plentiful sunshine, variable soil texture, varied agro-climate tropical zones, sub-temperate and temperate rainfall-all set for the production of a whole range of agricultural products all the year around in different parts of the country. Thus, every economic crop species in the world, ranging from temperate orchard crops like apples to tropical mangoes, thrive and flourish in India.

Tanzania has been among the fastest growing economies in the world in the past decade with an annual average growth of 7%. The country features in the list of top five fastest growing economies in the world in 2011-15. It has been observed that the Tanzanian market has to be sensitized as it has a huge potential and Indian exporters should take advantage of the country, particularly with Tanzania being a member of the East African Community (EAC), enjoying customs tariff and trade preferential agreements.

India’s total Agro Export is USD 32.09 billion out of which The Agricultural and Processed Food Products Export Development Authority’ (APEDA) processed food products export is USD 16.20 billion (50.48% share). Export of agricultural and food products have grown at 20% annually in the last decade. The export of APEDA products to Tanzania during 2015-16 is USD 29.02 million. The main products include Cereal Preparations, Jaggery and Confectionery, Basmati Rice, Alcoholic and Non-Alcoholic Beverages, Non-Basmati Rice, Miscellaneous Preperations, Fruits & Vegetables Seeds, other Processed Fruits & Vegetables etc.

There are prospects to promote trade between India and Tanzania. We bring the spirit of India.

APEDA is participating in Brand Promotion of Indian Foods in Dar Es Salam, Tanzania, where we are displaying Rice, Indian snack food items, Ready to Eat Foods and various processed food products, which are meant to add spice to dietary lifestyle. We invite buyers and agents to visit APEDA pavilion where Shri S. S. Nayyar, General Manager and Mr Harpreet Singh, Executive Officer along with other exporters are available for business related information and negotiations. ndia is the second largest producer of fruits in the world and produces over 83 million tonnes of fruits. India’s tropical fruits such as mango, banana, sapota, pomegranate and guava are quite famous. The royal fruit mango is the king of fruits. Besides consuming in fresh form, Indian mangoes are also processed for preparing pulps, juices, nectars, squashes, jams, pickles, chutneys and many more products. India has also emerged as a major exporter of seedless grapes.

Indian food preparations are becoming popular internationally not only amongst the ethnic population but also with mainstream. Products like vegetables curries, ready to eat, pulses, snacks, sweets, etc. in improved packaging have been introduced for reaching the new markets.

These products are available in cans, retort pouches and other best international standard of packaging for exports. The processed food sector in India is considered to be sunrise industry because of abundance, diversity and technological advancement. A whole range of quality food products are being exported at the most competitive prices. India’s export of processed food products is around USD 10,570.05 million.

India is famous for its aromatics ‘Basmati’ rice, which is one of its major exports. It is much in demand in the International market for its fragrance and good cooking qualities. India’s export of Basmati Rice is around USD 4518.11 million.

Indian alcoholic industry has emerged as dynamic commercial entity. Indian choices quality of Beer, Whiskey, Rum, Gin, Vodka and White Spirit are becoming increasingly popular in the international market. Quality of Indian grapes lends special flavors to the Indian wines. Today the country produces excellent wine, both red and white.

The awareness regarding the importance of organic food has increased globally; this is due to the residue of chemical pesticides in the food chain by conventional farming, resulting in health hazards of consumers. The consumers demand residue free food.

Organic agriculture holds the key to rural transformation and sustainable development in our country. There is an organic revolution brewing throughout the country. The urge to preserve bio-diversity and improve farm production without the use of chemical inputs has encouraged our farmers to become less dependent on unsustainable inputs. This approach is contributing towards rural livelihood opportunities.

It is mandatory, now, for the producers of organic products in the country to adhere to well develop procedures and practices during the entire operations as per the national standards for organic production and it is essential to go through the process of certification.

Considering the effectiveness and credibility of the accreditation and certification system, India has been recognized for the following:




∙ Recognition of NPOP standards by European Commission for equivalence and inclusion in the Article 11 list of EC regulation.
∙ Recognition of the conformity assessment procedures of India (1SO -17011).
∙ Recognition of NPOP standards by Switzerland for equivalence.

To address the concerns about food safety and traceability in food products, grower’s processors and exporters in India have established backward linkages for effective monitoring of the procurement of raw materials. The integrated units have been set up for processing and packaging in most hygienic environment. The food processing industry’s capabilities have increased manifolds in last few years leading to India’s emergence as global player in the food trade with a diversified range of products. Indian Government has focused on infrastructure development to provide a strong backbone to the economy. This sector has the potential to absorb FDI.






India assures its buyers to provide quality products acceptable in the international market, regular supply with improved infrastructure and very competitive prices.






The Indian economy has undergone tremendous transformation and subsequent to liberalization of trade, fiscal and industrial policies in last 20 years, the economic environment in India is very conducive now for investment in food processing. A rising wave of consumerism has taken India by storm. Its raining malls in metros and small towns alike driven by a 500 million strong consumer segment and passionate young demographic, India is on a shopping spree. Several globally recognized names in the food world viz. Nestle, Kellog’s, McDonald’s, Dominos, Cadburys, Seagram, Perfetti Van Melle, Heinz, Coke and Pepsi have established large scale production base in India, serving domestic markets as well as exporting their products to other countries.






The Agricultural and Processed Food Products Export Development Authority (APEDA), an apex organization under the Ministry of Commerce, Government of India, is mandated with the responsibility for Promotion and Development of the export of scheduled products namely Fruits, Vegetables and their Products, Meat and Meat Products, Poultry and Poultry Products, Dairy Products, Confectionery, Biscuits and Bakery Products, Honey, Jaggery and Sugar Products, Cocoa and its products, chocolates of all kinds, Alcoholic and Non Alcoholic Beverages, Cereal Products, Groundnuts, Peanuts and Walnuts, Pickles, Papads and Chutneys, Guar Gum, Floriculture and Floriculture Products, Herbal and Medicinal Plants, Basmati and Non Basmati Rice. More than 30,000 exporters are registered with APEDA.






Agricultural & Processed Food Products Export Development Authority (APEDA)


(Ministry of Commerce & Industry, Govt. of India)


3rd Floor, NCUI Building,


3, Siri Industrial Area,


August Kranti Marg, Opp. Asiad Village


New Delhi – 110016 (INDIA)


Tel: +91 11 26514046(D)/26513219


Fax: +91 11 26534870/26526187


E-mail: headq@apeda.gov.in


Website : www.apeda.gov.in







Naibu Waziri Mavunde apokea tuzo aliyoshinda mjasiriamali Jenifa Shigole.

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana Bi.Venerose Mtenga na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na vyombo vya habari kuhusu Tuzo aliyoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea cheti alichoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole Bi. Jenifer Shigole akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) tuzo aliyoshinda nchini Morocco na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola moja na nusu. Kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images