Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

DKT SHEIN AONGOZA SHEREHE YAMAULIDI YA KUZALIWA MTUME (M.A.S) ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali wakiwa katika Sherehe ya kuadhimisha Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na wake wa Viongozi mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) katika Maulid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.


Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur’aan Tukufu ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Wanafunzi wa Madressa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,

[Picha na Ikulu.] 12/12/2016.

DKT. MPANGO ATEMBELEA MAONESHO YA VIWANDA VYA NDANI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kulia) akionesha kwa Watanzania na mahali pengine duniani, nguo iliyoshonwa na mlemavu asiyeona Bw. Abdalah Nyangalilo (aliyevaa miwani), baada ya waziri huyo kutembelea banda lake lililopo kwenye uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, uliopo Barabara ya Kilwa, Jijini Da es salaam, na kumpatia mlemavu huyo msaada wa vyerehani viwili.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. Edwin Rutageruka, (aliyenyoosha kidole), akimtembeza Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, eneo la Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akiangalia kazi ya ubunifu wa Bw. Kaparata, aliyebuni gari na kulipa jina la Kaparata, wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akiangalia kazi ya ubunifu wa mitambo mbalimbali iliyobuniwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo-Sido, wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akiangalia bidhaa zilizotengenezwa na mjasiliamali mmoja, wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (katikati) akiangalia mashine ya kusindika mazao ilibuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (katikati) akiangalia zoezi la uhakiki wa Namba za utambulisho wa Mfanyabiashara (TIN) alipotembelea Banda la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (katikati) akiangalia bidhaa za ngozi kutoka kwa wajasiliamali, wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (katikati) akiongea na maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchi ni (TFDA), wakati alipotembelea maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani yanayofanyika kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam

(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-HAZINA)

LAPF YAWALIPA BILIONI 8.3 ZA FAO LA UZAZI WANACHAMA WAKE WALIOJIFUNGUA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao lazazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.

Mfuko wa LAPF umeweza kulipa fao la uzazi kwa jumla
ya wanchama elfu kumi Tangu mfuko huo uanze kulipa fao hilo kwa
wanchama wake mwaka 2012.

Akiongea katika hafla hiyo Meneja wa LAPF, Kanda ya ziwa, Yessaya Mwakifulefule amesema LAPF imetumia zaidi ya shilingi bilioni 8.3 kulipa fao la uzazi kwa kina
mama wanachama wa Mfuko huo.

Akikabidhi hundi ya malipo hayo kwa mwanachama Nchama Renatus ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Uhuru iliyopo Nansio Ukerewe,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongela ameupongeza mfuko wa LAPF kwa kuwajali wanachama wake na kulipa
mafao kwa wakati.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akiwa amemapaka mtoto wa Mwanachama wa mfuko Nchama Renatus baada ya mama huyo na wenzake kukabidhiwa hundi zao za fao la uzazi. Jumla ya sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo mkoani Mwanza.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akiwa amemapaka mtoto wa Mwanachama wa mfuko Nchama Renatus (katikati) baada ya mama huyo na wenzake kukabidhiwa hundi zao za fao la uzazi. Jumla ya sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo mkoani Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akiwa amepakata mtoto wa mnufaika.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (watatu kulia) akikabidhi hundi kwa mawanachama wa Mfuko wa LAPF, Nchama Renatus (wapili kushoto) ambaye ni mnufaika wa fao la zazi kwa wanawake wanachama wa mfuko huo na kuhuhudiwa na wanufaika wengine wa Mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule ambapo alisema Sh bilioni 8.3 zimetumika kuwalipa fao la uzazi wanawake wanachama wa mfuko huo.

Picha ya pamoja ya wanufaika na mgeni rasmi.

Meneja wa LAPF Kanda ya Ziwa, Yesaya Mwakifulefule akisalimia.

WAHITIMU ZAIDI YA 2000 CHUO KIKUU SAUT JIJINI MWANZA KUTUNUKIWA VYETI MBALIMBALI WIKENDI HII.

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 

Kulia ni Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi.

Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali hayo huku wanafunzi wanafunzi 746 wakishindwa kutunukiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipia ada.

Mahafali hayo yatatanguliwa na Siku ya Jamii itakayofanyika Jumatano Disemba 14 ambapo kutakuwa na Maonesho ya Kitaaluma.
BMGHabari
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustin SAUT, Padri, Dkt.Thadeus Mkamwa (kushoto), akitoa taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 
Bernald James ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho yatakayofanyika kwa siku mbili, Ijumaa Disemba 16 na Jumamosi Disemba 17 mwaka huu chuoni hapo Malimbe Jijini Mwanza. 
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT 
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanabaraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wanahabari na wajumbe wa baraza la Seneti chuo Kikuu SAUT wakifuatilia taarifa kuhusiana na Mahafali ya 18 ya chuo hicho
Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT cha Jijini Mwanza.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Dkt.Thadeus Mkamwa amesema wahitimu hao wakiwemo watatu wa shahada za uzamivu watatunukiwa shahada zao kwenye Mahafali yatakayofanyika ijumaa na jumamosi wiki hii chuoni hapo.

Amesema mahafali hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi yatatanguliwa na Siku ya Maonesho Kitaaluma yatakayohusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka kila kitivo na idara.

Hata hivyo Dkt.Mkamwa amesema wanafunzi 746 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada.

FURAHIA WIMBO MPA WA MSANII CASTLE MC-NIMERUDI.

$
0
0
Castle MC ni msanii chipukizi kutoka Jijini Mwanza. Ameachia wimbo mpa uitwao "Nimerudia" akimshirikisha H.Criss. Wimbo umetengenezwa na producer Day Dream kutoka studio za Over The Classic Music Jijini Mwanza.

Wimbo unavutia kusikiliza na unatoa ujumbe wa watu wengi walio kwene mahusiano ambapo baada ya kutengana, mmoja hurudi na kutaka kufufua upya mahusiano.
Hakika ni HipHop ya maana kusikiliza.
Bonyeza HAPA Au Play Hapo Chini

MAREKANI YARIDHISHWA NA TANZANIA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UENDESHAJI WA SERIKALI KWA UWAZI

Vodacom yawatengea wateja wake Bilioni 5/-

$
0
0
  Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary (kushoto)na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombella (kulia) wakimsikiliza Afisa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Promosheni ya”Nogesha Upendo” leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja  kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa rasmi Promosheni ya Nogesha Upendo leo jijini Dar es Salaam itakayowawesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia muda wa maongezi,Vifurushi vya intaneti pamoja na  fedha taslimu, shilingi Bilioni 5/- zimetengwa kwa ajili ya promosheni hii ambapo wateja 500 watajishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kupitia droo za kila wiki kwa msimu huu wa sikukuu.

Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama”Nogesha Upendo”ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi ya fedha taslimu ,muda wa bure wa maongezi na MB za Interneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu. Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo wateja wapatao 500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.

Akiongea wakati wa uzinduzi ,Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania tunayo furaja kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu.

Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku. ”Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii”.

Aliongeza kusema “Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet,wateja wa Vodacom pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha.Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”.

Kwa ujumla, Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu, muda wa maongezi na bando za intaneti(MB). Promosheni hii itakayodumu kipindi cha miezi 2 kuanzia leo ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni.

“Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote, Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya Maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo”alisisitiza Mworia

MAMLAKA ZA MAJI ZASHAURIWA KUZALISHA MAJI YA KUTOSHA KUHUDUMIA VIWANDA

$
0
0
Kaimu katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango kwa upande wa Tume ya Mipango Bibi Flotrence Mwanri akielekea katika ukaguzi wa mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira mjini Lindi. Kulia (mwenye t-shirt) ni Meneja wa Mamlaka ya Maji Lindi, Mhandisi Idris Sengulo, pembeni yake ni Mhandisi Mshauri wa Mradi huo, Francis Fumbuka na upande wa kushoto ni Mkandarasi wa mradi huo Bw. Rajendra Kumar. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO
Kaimu katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango kwa upande wa Tume ya Mipango Bibi Flotrence Mwanri akiangalia mitambo ya Maji safi Mjini mtwara. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mtwara Mjini, Mhandisi Mashaka Sitta.
Mkandarasi wa mradi mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira mjini Lindi, Bw. Rajendra Kumar akitoa maelezo mbele ya Kaimu Katibu Mtendaji anayeongoza timu ya wataalamu wa Ukagauzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango
Mkandarasi wa mradi mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira mjini Lindi, Bw. Rajendra Kumar akimwonesha Kaimu Katibu Mtendaji mabomba ya kisasa yatakayoweza kubeba maji ya kutosheleza majitaji ya wananchi wa Lindi mjini.
Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mtwara Mjini, Mhandisi Mashaka Sitta akitoa maelezo kwa timu ya wataalamu wa kutoka Tume ya mipango juu ya namna wanavyotibu maji safi kabla ya kuyasambaza kwa wananchi.
Ujenzi unaoendelea wa mitambo ya maji katika mradi mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira mjini Lindi.


Na Adili Mhina.
Mamlaka za maji nchini zimeshauriwa kuwa na mikakati ya kuboresha na kujenga miundombinu ya maji inakayokidhi mahitaji ya viwanda na kuachana na mawazo ya kuzalisha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pekee ili kutekeleza malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaosisitiza uchumi wa viwanda.

Ushauri huo umetolewa kwa nyakati tofauti na Kaimu Katibu Mtendaji Wizara ya Fedha na Mipango kwa upande wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri kwenye ziara yake inayoendelea katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na ile ya sekta binafsi.

Mwanri alionesha kutoridhishwa na hali ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya viwanda baada ya kukagua mradi wa maji wa Kilwa Masoko kwa kutumia chanzo cha mto Mavuji ambao utaanza baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya Serikali Tanzania na Ubelgiji, ujenzi wa mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na usafi wa mazingira mjini Lindi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, Ujermani na umoja wa Ulaya pamoja na mradi wa maji safi mjini Mtwara ambapo alibaini kuwa miradi yote imelenga kukidhi mahitaji ya nyumbani pekee bila kuwepo mkakati madhubuti wa kupata maji ya kuhudumia viwanda.

Alieleza kuwa zoezi la kuhamasisha uwekezaji na ujenzi wa viwanda linaloendelea kutekelezwa na viongozi katika ngazi mbalimbali limekuwa na manufaa makubwa kutokana na kujitokeza kwa wawekezaji wanaojenga viwanda katika maeneo mbalimbali ya nchi. Hivyo halmashauri husika zina wajibu kuhakikisha kuwa kuna mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa maji kwa ajili ya kuhudumia viwanda kwani sio kila muwekezaji atajitafutia maji ya kuhudumia kiwanda chake.

“Mkakati wetu kama taifa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, tunashukuru kuwa hilo mmelipokea na kulifanyia kazi. Changamoto ninayoiona hapa ni kuwa katika suala la kujenga na kuboresha miundombinu ya maji mmelenga kukidhi mahitaji ya nyumbani peke yake na mmesahau kuwa viwanda navyo vinahitaji maji katika kujiendesha”, alisema Mwanri alipokuwa akikagua mradi wa maji mjini Lindi.

Alisisitiza kuwa serikali ya sasa imelenga katika kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima ili kuboresha maisha ya wananchi hivyo katika miradi ambayo inatarajiwa kuanza ni vyema kuwa na mawazo ya kujenga miundo mbinu itakayokidhi mahitaji ya maji majumbani na viwandani kwa wakati mmoja badala ya kusubiri viwanda vijengwe ndipo serikali iingie tena gharama ya kupanua au kujenga miundombinu upya ili kukidhi mahitahi hayo.

“Kuanza upanuzi wa miundombinu ili kukidhi mahitaji ya viwanda ni gharama sana na tungeweza kuepuka gharama hizi kama tuamua kuweka miundo mbinu inayoweza kukidhi mahitaji yote hata kama viwanda bado havijajengwa” Alisisitiza.

Mwanri alieleza kuwa ujenzi wa viwanda ni suala mtambuka kwa kuwa linagusa sekta mbalimbali kutoka maandalizi hadi utekelezwaji wake hivyo ni lazima kila mamlaka inayohusika kuhakikisha inatekeleza wajibu wake kikamilifu ili isiwe kikwazo katika maendeleo ya viwanda nchini.

“Tukizungumzia kujenga viwanda sio kwamba wizara ya viwanda na biashara ndiyo inafanya kila kitu hapana, hili ni suala mtambuka ambalo sekta zingine kama ardhi, mazingira, umeme, maji, barabara na reli, nk, zina nafasi kubwa katika kuhakikisha viwanda vinakuwa katika mazingira salama” alieleza Mwanri.

UN Tanzania yawahamasisha Vijana kujiunga na fursa zilizopo katika malengo endelevu ya dunia

$
0
0
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez amewahamasisha vijana mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zilizopo katika malengo endelevu ya Dunia ilikuwezeshwa kimafunzo na mitaji zaidi.

 Akizungumza katika semina maalum ya FURSA 2016 kwa mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Clouds Media kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) na wadau wengine mbalimbali huku wananchi kutoka maeneo tofauti wamepata kuhudhuria, Bw. Alvaro amesema vijana na wananchi wanayo fursa ya kuchangamkia malengo hayo ya endelevu. 

“Tumeweza kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kuwafundisha vijana kuwa mabalozi wa malengo endelevu ya Dunia. Na zaidi ya vijana 10,000 kwa kufikiwa na elimu ya maendeleo endelevu. Ikiwemo Iringa, Kigoma Mbeya na mikoa mingine” amesema Bw. Alvaro. Aidha kwa upande wa washiriki wengine wakiwemo watoa mada wameweza kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio na namna ya kupata elimu ya kibiashara. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez akitoa elimu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini Dar.
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mh. Richard Kasesela akizungumza kwenye kongamano la Fursa 2016 kwa vijana liliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mtana, Millenium Towers.
  
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo
     
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MaxMalipo, Injinia Juma Rajab akitoa elimu kwa washiriki.
 
Mwanamuziki Nick wa Pili akizungumza na vijana wenzake kwenye Fursa 2016 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga akitoa elimu na maelezo kwa vijana na wakulima kujitokeza kuwezeshwa na benki hiyo.
Injinia Juma Rajab ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MaxMalipo akitoa elimu katika kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Francis Assenga akisisitiza jambo kwenye kongamano hilo.
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce Temu akiwapiga msasa juu ya malengo ya dunia vijana walioshiriki kongamano la Fursa 2016 jijini Dar.
 
Tukio hilo likiendelea.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA KULA CHA MERU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  kiwanda cha kukamua mafuta ya kula cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2017. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akionyeshwa mafuta  ya kula na Mkurugenzi wa Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal  (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2016.  Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na watatu kulia na Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Singida, Martha Mlata. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  kiwanda cha kukamua mafuta ya kula cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2017. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal. 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal kuhusu mafuta ya kula yanayozalishwa na kiwanda cha Meru cha Singida mjini  wakati alipotembelea kiwanda hicho Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya kula cha Meru kilichopo mjini Singida Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha kukamua mafuta ya kula cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2017.  Wanne kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi na kushoto kwake  ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal.

Wafugaji, wakulima wachangamkia fursa shule ya kiingereza Msata

$
0
0
Jamii ya wafugaji na wakulima wa mananasi wilayani Chalinze na Bagamoyo, wamepongezwa kwa kuchangamkia fursa za elimu msingi kwa mchepuo wa Kiingereza kwenye shule ya Mustlead iliyopo kata ya Msata,Wilayani Chalinze,Mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasenyenda Investments, Bw.Benjamin Thompson wakati akikabidhi vyeti vya kumaliza shule ya awali kwa watoto wa shule, hiyo iliyopo kijiji cha Masuguru.

Alisema ni jambo linalotia moyo kuona jamii hizo zilivyoamua kuchukua maamuzi magumu ya kusomesha watoto, huku zikiwa a changamoto nyingi za kimaisha.

“Sehemu nyingi nchini, shule hizi huchukuliwa kwamba ni kwa ajili ya matajiri au watu wa daraja fulani, jambo ambalo ni tofauti na hali niliyoikuta hapa, maana wengi wenu ni wakulima na wafugaji wenye maisha ya kawaida,” alisema.

Amempongeza mwekezaji kwa kuamua kuwekeza shule hiyo vijijini,sambamba na mkakati wa serikali wa kuboresha elimu nchini, kitu kinachochochea maendeleo ya kijiji hicho na vingine vinavyoizunguka shule hiyo vikiwemo Kiwangwa, Fukayosi, Msata, Mandela, Miono, Makurunge Mwavi, Kidomole, Mkenge na Lugoba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bw.Idd Mapiphi alisema yeye ni shahidi wa ubora wa elimu ya shuleni hapo,kwani pamoja na mtoto wake, watoto wanapiga hatua nzuri kielimu kwenye shule hiyo ya Kiingereza haikuwahi kuwepo katika kata zao tangu Tanzania ipate Uhuru.

“Ujio wa shule hii ulitushangaza wengi, kwani tulijua haijengwi kwa ajili yetu.Lakini tuliambiwa kwamba hata sisi tunaruhusiwa kupeleka watoto kwa kulipa ada kidogo kidogo, basi tukasikia faraja sana juu ya hilo,” alisema.

Mwakilishi wa wazazi wa shule hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Bago Bw.Maulid Tamla ameupongeza uongozi wa shule kwa kusimamia utoaji wa elimu bora kwenye mazingira ya kisasa.

Meneja wa shule hiyo Bw. Peter Stewart aliwaasa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuacha kupeleka watoto wao mbali na maeneo ya nyumbani, kwa ajili ya elimu wakati shule yake ipo na ni ya kutwa na pwani ina viwango vya kimataifa.

“Wakati umefika kwa watanzania kuacha kupeleka watoto wetu nchi za nje au mbali sana na nyumbani kwani kwa kufanya hivyo unajikosesha nafasi ya kuwa karibu na watoto kwa kushindwa kumtembelea mara kwa mara.”

Alisema shule mbali na masomo ya kiada, shule ina mpango wakuazisha masomo ya ziada kwa vitendo kwenye fani ya kilimo cha mbogamboga na matunda ili kuwajengea wanafunzi msingi mzuri wa maisha ya kujitegemea.
NB:Kwa kuomba nafasi ya kuleta mtoto shule hii, piga nambari 0764411111/ 0786202202
Mgeni rasmi kwenye mahafali ya elimu ya awali kwenye shule msingi Mustlead ya Msata,Wilayani Chalinze Mkoani Pwani Bw Benjamin Thompson(wa tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu,wazazi pamoja uongozi wa shule hiyo jana
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasenyenda Investments Bw Benjamin Thompson akikabidhi cheti cha uhitimu wa elimu ya wali kwa Mtoto Ibrahim Kimaki kwenye shule ya msingi Mustlead iliyopo Msata,Wilayani Mkoani Pwani.Mama wa Mtoto huyo Adela Kimaki akishuhudia.
 Sehemu ya shule hiyo kwa muonekano wa nje

TTCL yaichapa BOT

$
0
0
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeendelea kutoa dozi kali kwa timu inazokutana nazo katika Mashindano yanayoshirikisha timu kutoka  Taasisi za Umma, baada ya mwisho wa  wiki iliyopita kuifunga Banki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa goli 1-0.
Goli la ushindi la TTCL limefungwa na mshambuliaji hatari Juma Masudi, kwa matokeo hayo, TTCL inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi B ikiwa nyuma mchezo mmoja dhidi ya kinara wa kundi hilo BOT.  
 Kikosi cha timu ya TTCL kilichocheza dhidi ya BOT, Kiwanja cha TPDC mwisho wa wiki iliyopita 
  Kikosi cha timu ya BOT kilichocheza dhidi ya TTCL, Kiwanja cha TPDC mwisho wa wiki iliyopita  
 Wachezaji wa TTCL wakipeana mikono na wachezaji wa BOT kabla ya mechi kuanza, Kiwanja cha TPDC mwisho wa wiki iliyopita 

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA NEC JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza machache kabla ya kumkaribisha  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli,katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Katibu Mkuu  wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC kabla ya kufunguliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam.
Pichani kulia ni  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula pamoja na Makamu Mwenyekiti wa (CCM Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kabla ya kuanza kikao hicho jijini Dar es Salaam. 
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho cha NEC wakifatilia kwa makini Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakimkaribisha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kufungua rasmi Kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.


















WIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA UZAZI KUTOKA ECOBANK

$
0
0
 
UPUNGUFU wa vituo vya afya na watoa huduma wasiokuwa na ujuzi na stadi za kuokoa maisha ni miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kasi ndogo ya kuondokana na vifo vya uzazi na watoto wa umri wa chini ya mwezi mmoja.
           
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Khamis Kigwangalla, alipokuwa akipokea msaada wa vifaa tiba vya uzazi kutoka Eco bank.
 
Vifaa hivyo vilivyotolewa kwa hospitali ya rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati benki hiyo ikiadhimisha siku yao ambayo mwaka huu kauli mbiu ilisema, ‘kuboresha huduma kwa wajawazito barani Afrika.’
 
“Katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi, jawabu lipo katika kuongeza vituo vya afya na watoa huduma wenye ujuzi na stadi za kuokoa maisha pamoja na vifaa tiba vya kutosha,” alisema.
 
Hata hivyo, Dk Kigwangalah alisema hali si nzuri kwa upande wa vifo vya uzazi na watoto wenye umri wa mwezi mmoja kutokana na takwimu zilizopo kuonyesha kuwapo kwa kasi ndogo katika udhibiti wake katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
 
Alisema takwimu za vifo hivyo zinaonesha kuwa mwaka 1996 kulikuwa na vifo 529 vilivyopungua kufikia 432 kwa vizazi hai 100,000 katika kipindi cha mwaka 2012, ikiwa ni sawa na vifo 7,500 kwa mwaka mmoja.
 
Kwa upande mwingine, Dk Kigwangalla alisema vifo vya watoto wachanga wenye umri wa chini ya mwezi mmoja ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili afya ya uzazi kutokana na takwimu kuonesha kuwapo (vifo) 21 kwa kila vizazi hai 1,000
 
Akizungumza katika halfa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Eco Bank, Enoch Osei Safi alisema siku ya benki hiyo inaadhimishwa katika nchi 33 za Afrika na kushirikisha utoaji misaada kulingana na mahitaji na mazingira ya nchi husika.
 
“Tumeazimia kuadhimisha siku yetu kwa kuipatia hospitali hii vifaa tiba vya uzazi ikiwa ni baada ya mashauriano ya pamoja yaliyotuwezesha kuwapo upungufu katika eneo hilo,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Safi, Eco Bank iliichagua hospitali ya rufaa ya Temeke kutokana na namna inavyowahudumia watu wengi kutoka maeneo tofauti ya jijini Dar es Salaam ikilinganishwa na hospitali nyingine.
 
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo, alisema wajawazito kati ya 50 hadi 80 wanajifungua hospitalini hapo kila siku, 10 kati yao wakijifungua kwa njia ya upasuaji.
 
Dk Mwabulambo alisema ipo haja kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali ili kufanikisha mahitaji ya hospitali hiyo katika kuwahudumia wajawazito na watoto.
 
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amani Malima (aliyesimama) akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa ECO Bank, Enock Osei Safi (aliyesimama) akihutubia kwenye hafla hiyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla akihutubia kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wajawazito walioshiriki hafla ya kukabidhi vifaa vya kujifungua vilivyotolewa na benki ya Eco Bank.


  
Mkurugenzi Mtendaji wa Eco Bank, Enock Osei Safi (kushoto) akimkabidhi msaada wa vifaa vya uzazi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Khamis Kigwangalla (wa pili kushoto),
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amani Malimana na
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAFANYA USAILI KUWAPATA WARATIBU NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO KATIKA JIMBO LA DIMANI, ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva (kushoto) akiongoza kikao cha Wajumbe wa Tume na Sekretarieti cha Usaili wa Waratibu na Wasimamizi Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani, Zanzibar utakaofanyika Januari 22, 2017.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume wakati wa kikao cha Usaili wa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva na Kulia ni Mjumbe wa Tume Mhe. Mchanga Mjata.
  Baadhi ya Wajumbe wa Seckretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakifuatilia kwa makini zoezi la Usaili wa kuwapata Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Zanzibar leo.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipitia vyeti na nyaraka mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva wakati wa Usaili wa nafasi ya Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani utakaofanyika Januari, 22, 2017.
 Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Mratibu wa Mkoa katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bw. Salum Juma Mgunya akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini Zanzibar.
 Mmoja wa washiriki wa Usaili katika nafasi ya Msimamizi wa Uchaguzi  katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Bi. Fatma Gharib Haji akijieleza wakati wa Usaili mbele ya Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mjini
Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia Usaili wa Wasimamizi na Waratibu wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar. Picha na Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA SPIKA BUNGE WA BUNGE LA ISRAEL

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Israel (Knesset) Mhe. Yuli Yole Edelsten wakati Mhe. Spika alipomtembelea Bungeni hapo. Mhe Ndugai yupo nchini Israel kwa ibada ya Hija.(Picha na Ofisi ya Bunge).

MASHAUZI KUACHIA KISS ME DESEMBA HII

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwanamuziki wa muziki wa taarabu hapa nchini Aisha Ramadhani (Isha Mashauzi) anataraji kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Kiss Me.

Akizungumza na globu ya jamii Msahauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari.

“hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu hivyo wajue kuwa wimbo huo ambao upo katika viwango vya hali ya juu,imerekodiwa ndani ya studio za Sophia zilizopo kinondoni” amesema Mashauzi

Ameongeza kuwa waliniona kuwa nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hichi kibao ambacho watafurahi wenyewe.

WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 55 YA UHURU WAKABIDHIWA VYETI.

$
0
0

Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwemo Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Waandishi wa Habari wakishuka baada  ya kupanda mlima huo kwa siku sita.Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Witara (Mwenye fimbo mstari wa mbele) na Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ardhini (JWTZ) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipokea Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro walipofika katika lango la Marangu,Kippi akisalimiana na Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu.
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA.
Baadhi ya Washiriki wa changamoto ya upandaji Mlima Kilimanjaro baada ya kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Star Tv ,Ramadhan Mvungi baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. .
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwanadishi wa Habari wa Clouds Media Group ,Kilimanjaro na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini ,Dixon Busagaga baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi ,Arusha ,Zulfa Musa baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari akiwa ni miongoni mwa wasicha wawili waliofika kileleni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mtanzania ,Arusha,Eliya Mbonea baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima,Charles Ndagulla mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Pascal Shelutete mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi makimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi ,Pte,Joyce Kaila baada ya kufanikwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi akimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi,Ally Said baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mwandishi wa Habari ,Idd Uwesso baada  ya kufanikiwa kufika kilele cha Stella.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlia Kilimanjaro,Charles Ngendo mara baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Mstaafu Jenerali George Waitara akiznungumza mara baada ya kushuka Mlima Kilimanjaro ambako timu ya Watu 36 wakiwemo Askari wa jeshi la Wananchi na Waaandishi wa Habari wamepanda mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na askari wa jeshi la ulinzi waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waongoza watalii walioshiriki kufanikisha safari ya Waandishi wa Habari na Askari wa jeshi la Ulinzi  kupanda mlima Kilimanjaro.    Na Dixon Busagaga wa Blogu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


Mwenyekiti wa CCM Dkt. Magufuli afanya uteuzi mpya ndani ya Chama, Polepole achukua nafasi ya Nape

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi.

#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.
Aliyekuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuhusu mambo mbalimbali yaliyoamriwa na chama hicho kupitia vikao vyao vilivyofanyika hivi karibuni.Picha na Michuzi Jr.

Rais Magufuli amteua Dkt. Khatib Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images