Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1066 | 1067 | (Page 1068) | 1069 | 1070 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika leo mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
   Mweyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiwa tayari kuongoza kikao hicho
   Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi kabla ya kikaokuanza. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kushoto, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
   Mwenyekiti wa CCM, Dk John Magufuli akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk Shein, alipowasili ukumbini
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Vuai Ali Vuai, akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein walipokutana ukumbini kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa, alipowasili ukumbini kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM, kilichofanyika mjini Dar es Salaam, leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Salimu Ahmed Salim alipowasili kwa ajili ya kushiriki kikao cha kamati kuu ya CCM, kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye kikao cha Kamati kuu ya CCM, kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipowasili kuendesha Kikao Cha Kamati cha Kamati Kuu ya CCM, leo mjini Dar es Salaam. PICHA: BASHIRI NKOROMO  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameitaka jamii kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujiajiri na kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

  Dkt. Mpango ametoa rai hiyo wakati alipotembelea banda la mlemavu asiyeona, Bw. Abdalah Nyangalilo, ambaye amewakusanya watu kadhaa wenye ulemavu na kuwapatia mafunzo ya ushonaji nguo katika maonesho ya kwanza ya viwanda vya ndani, yanayofanyika katika Uwanja wa maonesho ya biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.

  Waziri huyo wa Fedha na Mipango, ambaye ametoa msaada wa vyerehani viwili ili kuwaongezea nguvu, amesema kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kufanya mambo makubwa ya kijasiliamali yatakayo wasaidia kujikimu kimaisha, endapo jamii itajitolea kuwasaidia kwa hali na mali

  Kwa upande wake, mlemavu asiye ona, Abdalah Nyangalilo, ameiomba serikali kuanzisha mitaala ya ufundi ikiwemo ushonaji kwenye vyuo vya ufundi hapa nchini ili kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu waweze kujitegemea kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali badala ya kuwaacha wawe ombaomba

  Akizungumzia maonesho hayo ya kwanza ya viwanda vya Tanzania , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. Amesema kuwa maonesho hayo, pamoja na mambo mengine yamelenga kuonesha bidhaa zinazotengenezwa na viwanda pamoja na wajasiliamali hapa nchini

  Maonesho hayo yanayotarajiwa kufungwa leo katika uwanja wa maonesho ya biashara wa mwalimu J.K Nyerere, barabra ya Kilwa, Dar es salaam, zaidi ya waoneshaji bidhaa za viwanda vikubwa na vidogo hapa nchini, yamewashirikisha zaidi ya kampuni 400.

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, MSOGA 
  .
  KATIKA kukuza sekta ya michezo hapa nchini hususan soka la vijana wadogo wa shule Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na serikali ya chini watarajia kujenga kiwanja cha michezo cha kisasa katika Kijiji Cha msoga kilichopo halmashauri ya mji mdogo Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

  Akizungumza katika halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kwenda kutembelea eneo ambalo litajengwa uwanja huo Kikwete amesema kwamba uwanja huo wa wa mpira wa miguu utajengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa chini na kuongeza utakuwa ni mkombozi mkubwa katika kukuza na kuinua vipaji kwa vijana wadogo.

  Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania katika siku za usoni inakuwa ni wachezaji wengi wenye vipaji ambao wataweza kuunda timu nzuri ya Taifa ambayo itaweza kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya Kimataifa.
  “uwanja huu wa mpira wa miguu pindi utakapokamilika utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa vijana wadogo hususan wale wa shule, hivyo nimeshazungumza na rafiki zetu wa serikali ya china na wamekubali kutujengea kwa hivyo ni jambo la msingi sana katika kuendeleza sekta ya michezo kwa watoto wetu hawa mbao wataweza kuleta mafanikio makubwa katika siku zijazoa,”allisema Kikwete.

  Katika hatua nyingine Kikweke ametoa pongeza kwa serikali ya china kwa kuona umuhimu wa kuweza kusaidia kujenga kiwanja hicho, na kuongeza kuwa pindi kitakapokamilika kitakuwa ni michezo mingine ambayo itakuwa ikifanyika mbali na mchezo huo wa soka lengo ikiwa ni kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji walivyonavyo.
  Naye Mwakilishi wa balozi wa china nchini Tanzania Yang Tong ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kukuza sekta ya mchezo hususan kwa vijana wadogo ikiwa samba na kujenga viwanja ili watoto wasiweze kucheza katika viwanja vya vumbi.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhione Kikwete alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anakuza michezo wa vijana wadogo katika jimbo lake hivyo kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo kutaweza kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyoa.

  Nao baadhi ya wadau wa mcheo wa soka katika kiji hicho cha msogo akiwemo i Michael James pamoja na Mohamed Halfan wamempongeza Rais mstaafu Jkaya Kikwete kwa ubunifu wa ujenzi huo wa uwanja kwa ajili ya vijana wadogo kwani kutaweza kusaidia kwa kisi kikubwa katima kuleta mabadiliko chanya katika mchezo huo.

  KUKAMILIKA kwa ujenzi huo wa kiwanja cha kisasa cha mpira wa miguu katika kijiji cha soga ambacho alizaliwa rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kutaweza kutoa fursa kwa vijana wadogo kuweza kukuza na kuonyesha vipaji walivyonavyo katika medani ya mchezo wa mpira wa miguu.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimksikiliza Mkurungenzi wa Kituo cha Ujasiriamali Kutengeneza Nafasi za Kibiashara kwa Vijana Zanzibar Ndg, Ameir Sheha akitowa maelezo kwa Naibu Waziri alipowasili katika viwanja vya Kituo hicho huko Mbweni Zanzibar wakati wa ziara yake Zanzibar. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mtaalamu Ufundi wa Kituo hicho Dr. Rajeev Aggrwal akitowa maelezo ya mafunzo kwa Vijana wanaojiunga na Kituo hicho kupata Elimu ya Ujasiriamali na baadae kujiajiri mwenyewe baada ya kupata ujenzi kupitia kituo hicho, kilioko katika majengo ya Chuo cha Karume Mbweni Zanzibar.
  Naibu Waziri Ofisi wa Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipitia ripoti ya Kituo hicho baada ya kupata maelezo kutoka kwa Wataalamu wa Kituo hicho wakati wa ziara yake Zanzibar kutembelea Taasisi mbalimbali. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mpina akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kukuza Ujasiriamali Kutengeneza Nafasi za Kibiashara kwa Vijana Ndg. Ameir Sheha, akimtembeza katika Kituo hicho kujionea shughuli zinazofanywa kutowa mafunzo kwa Vijana wanaojiunga kupata mafunzo ya ujasiriamali. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza mwanafunzi wa Kituo hicho Maryam Omar akitowa maelezo ya utengenezaji wa sabuni na mafuta mafunzo wanayoyapata kupitia Kituo hicho kwa sasa kina Vijana 700 wanapata mafunzo ya Ujasiriamali Zanzibar.
  Mwanafunzi wa Kituo cha Ujasiriamali Mbweni Maryam Omar akitowa maelezo ya jinsi ya utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na maziwa, Samli. Siagi na Chizi ni moja ya mafunzo yanayotolea Kituoni Hapo. 
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana katika Kituo hicho.

  W


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitembelea Kituo cha Ujasiriamali Mbweni Zanzibar akiwa na Mkurugenzi wa Kituo hicho Ndg Ameir Sheha.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akipata maelezo kutoka kwa Kijana anayepata mafunzo kituo hicho jinsi ya kutengeneza mishumaa 
  Baadhi ya Bidhaa zainazozalishwa katika Kituo hicho cha Kukuza Ujasiriamali Kutengeneza Nafasi za Kibiashara kwa Vijana Mbweni Zanzibar, hizo bidha za mishumaa.

  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog.
  Zanzinews.com 
  othmanmaulid@gmail.com
  0777424152 or 0715424152.

  0 0

  Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

  KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana mjini Dar es Salaam na kujadili ajenda moja ya kupokea tathmini ya Chama baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kilijadili tathmini hiyo kabla ya kupelekekwa mbele kulingana utaratibu wa Chama.

  Nape Mbaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alisema tathmini hiyo ilitokana na maagizo ya Chama kwenye ngazi zote kufanya tathmini hususan baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu huo.Kwa mujibu wa Nape, huo ni utamaduni wa kawaida wa CCM kufanya tathmini kila baada ya uchaguzi ambayo imekuwa ikifanyika kwa maagizo ya Chama kuanzia ngazi ya tawi, kata, wilaya, mkoa na kuendelea.

  Alisema Kamati Kuu itaipitia tathmini hiyo kisha itawasilisha mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM ambako itajadiliwa na kuelekeza hatua zinazofuata."Hii ndio siri ya uimara na ushindi wa CCM. Tumekuwa tukijitathmini na kuchukua hatua stahili kwa ajili ya kuhakikisha Chama kinaendelea kuwa imara na bora siku zote,"alisema.

  Aidha, alisma awali kikao hicho kilipangwa kufanyika kwa siku mbili lakini kilifanyika kwa siku moja na kwamba kilitarajiwa kukamilika jana.Nape alisema kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kilichopangwa kufanyika kesho kitafanyika kama kilivyopangwa ambapo alitumia fursa hiyo kuwatakia safari njema wajumbe wote wanaotoka sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya kuhudhuria hicho.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Desemba 11, 2016 na kesho anatarajiwa kwenda Singida kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Maulid. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Benedict Liwenga-WHUSM.

  Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye leo ametembelea Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ili kukagua shughuli za marekebisho ya miundombinu inayoendelea uwanjani hapo ikiwemo kukagua ufanisi wa Kamera za kufuatilia matukio Uwanjani pamoja na marekebisho ya viti vya kwenye majukwaa.

  Katika ziara yake Waziri Nape amekagua namna Kamera za CCTV zinavyokuwa na uwezo wa kubaini matukio mbalimbali yanayoendelea uwanjani ambapo ameridhika na utendaji kazi wa kamera hizo na kusisitiza zitumike ipasavyo ili kuwabaini wahusika wanaoharibu miundombinu ya uwanja.

  Amesema kwamba kazi ya kubaini waharibifu wa miundombinu kwa sura katika uwanja huu kwa kutumia hizi kamera yataongeza hali ya usalama kwenye uwanja na pia kusaidia kufuatilia matukio ya kihalifu Uwanjani kama vile kuvunja viti”, alisema Mhe. Nape.

  Aidha, amesema kwamba ukarabati wa uwanja unaoendelea sasa pinid utakapokamilika utaufanya uwanja huo kuwa salama zaidi na ndiyo maana kamera nyingi zimeweka ili kuendelea kubaini matukio yanayoendelea ndani na nje ya mipaka ya uwanja ikiwemo milangoni.

  “Kwa sasa uwanja wetu utaweza kushughulika na mtu mmoja mmoja anayehujumu miundombinu yetu, kwasababu kamera zetu zina uwezo mkubwa wa kumtambua mtu kwa sura pindi awapo uwanjani kuanzia magetini”,alisema Mhe. Nape.

  Ameagiza ukarabati wa miundombinu uendelee ikiwemo mageti na viti uendelee kufanyika kwani yeye anachosubiria ni kukabidhiwa uwanja huo siku ya tarehe 13 Desemba mwaka huu na siku hiyo ndiyo itafahamika thamani ya ukarabati uliofanyika kwa ujumla.

  Aidha, amegusia suala la Mkataba ulioingiwa kati ya Serikali na Klabu ya Yanga African ambapo amesema kwamba, Serikali iliingia Mkataba na Klabu ya Yanga African ya kutumia uwanja wake wa Taifa pamoja na uwanja wa Uhuru tarehe 1 Desemba, 2016 kwa muda wa mwaka mmoja yaani mpaka tarehe 30 Novemba,2017.

  Amesema kwamba, kutokana masharti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF), vilabu vyote vinavyoshiriki michezo ya Kimataifa vinatakiwa kuonyesha uthibitisho wa umiliki wa uwanja au viwanja vitakavyotumika katika mechi zao au kuonyesha mkataba walioingia ambapo mechi hizo zitachezwa.

  “Kwa kuwa klabu ya Yanga haina Uwanja wake, walileta ombi Wizarani, la kuingia Mkataba na Mmiliki wa Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru yaani Serikali. Serikali iliona ni busara kuingia mkataba na Klabu ya Yanga African ili pale ambapo watahitajika kutaja uwanja watakaotumia waweze kutaja Uwanja wa Uhuru au Uwanja wa Taifa”, alisema Mhe. Nape.

  Kwa muktadha huo, Klabu ya Yanga itaendelea kutumia uwanja wa Uhuru ambao haukujumuishwa katika maamuzi ya kufungiwa na hauna tatizo la kukarabatiwa.

  Amesisitiza kuwa, Serikali ina nia njema kwa vilabu vyake na wadau wote wa Michezo na Serikali inafanya shughuli zake kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni, hivyo amevitaka Vilabu vyote viwe na utamaduni wa kufuata sheria, taratibu na Kanuni katika kutekelea majukumu yao.
   Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye jinsi Kamera za CCTV zinavyoweza kumnasa mtu akifanya jambo lolote baya ndani ya Uwanja wa Taifa wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye, Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya pamoja na Waandishi wa habari wakiangalia hatua iliyofikiwa ya urekebishaji wa viti na miundombinu mingine ya uwanjani hapo wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya pamoja na Waandishi wa habari wakielekea kuangalia hatua iliyofikiwa ya urekebishaji wa viti na miundombinu mingine ya uwanjani hapo wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia namna Kamera za CCTV zinavyofanya kazi ya kubaini matukio yanayoendelea ndani ya Uwanja wa Taifa wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Na Adili Mhina, Lindi.
  Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango upande wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri amefanya ziara katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia lililopo katika mtaa wa Likong’o Manispaa ya Lindi na kushauri uongozi wa Manispaa hiyo kuongeza  juhudi za kuhakikisha wananchi waliopisha mradi huo wanalipwa fidia kwa wakati.
  Mwanri alieleza kuwa ni vyema uongozi ukatilia mkazo umuhimu wa kuwalipa fidia wananchi ili waweze  kujiletea maendeleo yao kwa kuwa hawawezi tena kuendelea kutumia eneo hilo.
  Alieleza kuwa dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda inaenda sambamba na kuwajali wananchi wake kwa kutoa fidia kwa mujibu  kanuni na sheria pale wanapolazimika kuachia  maeneo yao ili kupisha miradi ya maendeleo.
  Mwanri aliongeza kuwa pamoja na kuwa mradi huo utakapojengwa na kukamilika utakuwa na faida kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla utasaidia pia kuinua kipato kwa wanachi wa Lindi kutokana na fursa mbalimbali za ajira zitakazojitokeza kwa wakazi hao.
   Nae Mtendaji wa Mtaa wa Ling’oko ambapo ndipo mradi huo unapotekelezwa, Bw. Jacob Anton alieleza kuwa wananchi wa eneo hilo wana matarajio makubwa na wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali kwa kuwa wanaamini ujio wa kiwanda hicho utasaidia kuboresha maisha yao.
  Timu ya Ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji huyo, kwa sasa inaendelea na zoezi la ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara ambapo itatembelea miradi ya Serikali na ile ya sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) yanatekelezwa kwa ufasaha.
   Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango upande wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua nyaraka mbalimbali ikiwemo ramani ya eneo litakalojengwa kujengwa kiwanda cha kuchakata gesi asilia katika eneo la Likong’o Mkoani Lindi. 
   Afisa Ardhi wa Manispaa ya Lindi, Bw. Munisi Andrew (aliyeshika nyaraka) akisikiliza maelekeza kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango - Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri. Wengine ni maafisa wa manispaa hiyo pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Mipango.
   Afisa Mipango Miji Manispaa ya Lindi, Bw. Ismaelo Chepa (mwenye t-shirt) akitoa maelezo juu ya ramani ya eneo la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi. Pembeni ya Kaimu Katibu Mtendaji ni Mchumi Kuu kutoka Tume ya Mipango, Bibi Salome Kingdom.

   Mtendaji wa mtaa wa Likong’o , Bw. Jacob Anton akimwelezea Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri utayari wa wananchi wa eneo hilo katika ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata Gesi asilia. Kushoto (mwenye Tai) ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi mjini Bw. Joel Kianza, Pembeni ya Kaimu Katibu Mtendaji ni Bw. Senya Tuni na Bibi Salome Kingdom wote wachumi kutoka Tume ya Mipango. 
   Kaimu Katibu Mtendaji, Wizara ya Fedha na Mipango - Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiangalia eneo (hauonekani Pichani) lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia. 
  Sehemu ya Eneo la ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata  gesi asilia. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

  0 0

  Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza kupata magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya maisha. Mbwa ni kama binadamu yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa basi anaweza kuwa dhaifu na kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia ni wanyama kama binadamu tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya magonjwa basi wanaweza kustahimili na kupona kabisa.

  Basi leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata viumbe hivi vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu. Kama ilivyo kwa wanyama wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili flani ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa. Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa kuwa ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo hivyo kwa wanyama kama Mbwa.

  Tuanze na Huu leo

  1:Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
  Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa mbwa huyo.

  Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka sana.

  Hizi ndio dalili kubwa sana za ugonjwa huu wa Parvo ni Kuharisha damu, Kutapika, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito ghafla. Mara umuonapo mbwa wako ana dalili hizi basi unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wako wa wanyama kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi ijapokuwa kama mbwa huyo hakuwahi kupatiwa chanjo ya Ugonjwa huo tokea utotoni basi asilimia ya kupona ni ndogo sana kwa maana unapoona dalili za ugonjwa huu basi ni dhahiri unakuwa ushamshambulia sana mbwa huyo.

  Nini husababisha ugonjwa huu wa Parvo?

  Mara nyingi ugonjwa huu usababishwa na mbwa aliyehathirika moja kwa moja na ugonjwa huu japokuwa kuna sababu nyingine kama endapo mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu anapojisaidia haja kubwa na mbwa mwingine akapita kunusa basi mbwa huyo anakuwa anaambukizwa moja kwa moja. Inasemekana virus vya ugonjwa huu vinauwezo wa kuishi kwenye udongo kwa takribani mwaka mmoja na ugonjwa huu unaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa mbwa mmoja kwenda kwa mbwa mwingine.

  Vilevile Ugonjwa huu unaweza kuletwa na viatu endapo mtu amekanyanga kinyesi cha mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu basi anapoingia nyumbani au kwenye mazingira ya mbwa ni rahisi sana kuacha virusi hivyo na ikumbukwe kuwa virusi hivi huishi kwa takribani mwaka mzima kwenye udongo.

  Unapohisi umekanyaga kinyesi au kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na virusi vya parvo basi unashauriwa kusafisha eneo hilo kwa kutumia madawa ya kuua virusi kwaajili ya kujirinda na ugonjwa huo hatari.

  Vilevile Kutompa chanjo sahihi mbwa wako na kwa wakati kunaweza kupelekea kusababisha mbwa wako kupata ugonjwa huo, Kama unavyofahamu kuwa mbwa wanatabia ya kunusa kila sehemu endapo bahati mbaya kanusa sehemu ambayo tayari kuna virusi vya ugonjwa huo na hana chanjo basi ni rahisi kushambuliwa na virusi hivyo.

  Tiba ni Ipi kwa Ugonjwa Huu?

  Inavyosemekana mpaka sasa hakuna tiba sahihi ya ugonjwa huu lakini Mbwa anapozaliwa tu na kufikisha muda wa wiki moja hadi mwezi unashauriwa kumpatia chanjo mbalimbali kwaajili ya kumkinga na magonjwa kama haya na chanjo hio sio ya mara moja tu anapochomwa mwanzoni basi unatakiwa kufata ushauri wa mtaalamu wa wanyama kwa ratiba tena ya kurudia kumchoma chanjo katika kipindi kijacho.
  Aina hizi za mbwa ndio aina rahisi sana kushambuliwa sana na ugonjwa huu RottweilersDoberman Pinschers, Pit Bulls, Labrador RetrieversGerman Shepherds.

  Tukutane tena siku ijayo.
  Je umeipenda makala hii?Basi unaweza kushare na Wenzako 
  Tu follow instagram kwa jina la @lukazablog @lukazablog @lukazablog

  0 0

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  WAFANYABIASHARA katika Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamejenga kisima cha maji salama chenye thamani ya sh.milioni 5.6 kwa kutumia nguvu zao na fedha za  ushuru wanaolipa.

  Akizungumza na mtandao wa  www. habari za jamii.com Katibu Mkuu wa Soko hilo Shaban Malonji 'maarufu kama Wailala' alisema umoja walionao wafanyabiashara katika soko hilo ndio uliofikia maazimio ya kujenga kisima hicho chini ya viongozi wao.

  " Binafsi napenda kuwapongeza wafanyabiashara wa soko letu kwa kuwa na umoja ambao umefanikisha kukamilisha ujenzi wa kisima hiki ambao utakamilika rasmi mapema wiki hii" alisema Malonji.

  Malonji alisema kwa muda mrefu changamoto yao ilikuwa ni kukosa maji sokoni hapo ndipo walipokaa na wafanyabiashara wa soko hilo na kufikia maazimio ya kujenga kisima hicho ambacho kitakuwa kikitoa huduma ya maji sokoni hapo.

  Alisema fedha za ujenzi wa kisima hicho zimetokana na ushuru wanaotoa wafanyabiashara hao na fedha zinazopatikana baada ya kulipa huduma ya choo cha kulipia pamoja na fedha za ushuru asilimia 10 wanazopewa na Manispaa.
   Fundi Martin Justine akitengeneza paa la kisima cha maji safi kinacho jengwa Soko la Madenge Temeke jijini Dar es Salaam kwa nguvu za wafanyabiashara. Ujenzi wa kisima hicho umegharimu sh.milioni 5.6.
   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
   Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala'  akinawa maji yanayotoka katika kisima hicho ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia kubwa.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Tawi la AccessBank Iringa, Frederick Masungwa wakati wa uzinduzi wa tawi hilo hivikaribuni. Kushoto ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Andrea Ottina.

  Kutoka kushoto, Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa AccessBank Andrea Ottina, Meneja wa Tawi la AccessBank Iringa Frederick Masungwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakikata keki wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo mjini hivikaribuni.


  Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa AccessBank Andrea Ottina (kushoto) akilishwa keki Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo mjini Iringa hivikaribuni. Katikati ni Meneja wa Tawi la AccessBank Iringa Frederick Masungwa.


  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (mwenye kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa AccessBank, baada ya kuzindua tawi la benki hiyo mjini Iringa hivikaribuni.

  MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amezindua tawi jipya la ACCESSBANK mjini Iringa, linaloifanya benki hiyo iwe na matawi 13 katika maeneo mbalimbali nchini.

  Mkuu wa maendeleo ya biashara wa benki hiyo, Andrea Ottina alisema ufunguzi wa tawi la benki hiyo mjini Iringa ni ushahidi wa dhamira yao ya dhati ya kutoa huduma bora kwa wateja wao nchini.

  “Pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja wetu, tunataka wapate huduma zetu kwa wakati pamoja na kuimarisha urahisi wa huduma za kibenki,” alisema.

  Ottina alisema Iringa ni miongoni mwa mikoa inayokua kwa kasi nchini kutokana na upatikanaji wa vivutio vingi, uwekezaji na uzalishaji wa chakula cha mazao ya biashara.

  Alisema benki hiyo itaendelea kupanua huduma zake ili kufikia sehemu kubwa ya wateja nchini kote, pamoja na kuanzisha bidhaa na njia mpya za upataji huduma.

  “Njia hizo ni kama vile huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi na wakala wa kibenki ambao wamelengwa zaidi katika maeneo ya vijijini na mijini pia,” alisema.

  Akizundua tawi hilo, Masenza aliipongeza benki hiyo kwa kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma bora za kifedha katika mkoa wa Iringa.

  “Natoa wito kwa wakulima na wajasiriamali, wafanyabishara wakubwa na wadogo kuchukua faida ya huduma zinazotolewa na benki hii kama fursa ya kuendeleza shughuli zenu za kilimo na biashara,” alisema.

  Alisema sekta ya benki ni muhimu katika maendeleo ya Taifa kwani ndiyo inayowezesha uwekezaji unaoweza kuleta mabadiliko kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

  “Matarajio yangu ni kuona mnaendelea kutoa huduma itakayokuwa na mfuto, msiwe sehemu ya wale wanaonyanyasa wananchi katika utoaji wa huduma za kifedha,” alisema.

  Awali Meneja wa tawi la AccessBank mkoani Iringa, Frederick Masungwa alisema benki hiyo ilianza kutoa huduma zake za kifedha mkoani hapa, Julai mwaka huu na hadi Novemba mwaka huu ilikuwa na wateja zaidi ya 3,000.

  Masungwa alisema benki hiyo inatoa huduma za akaunti mbalimbali ikiwemo ya akiba, kikundi, hundi, amana, mikakati, wanafunzi, wafanyabishara wakubwa; na pia inatoa huduma za kutuma fedha ndani na nje ya nchi na huduma ya ATM kupitia Umoja Switch.

  Alisema tangu waanze kutoa huduma hizo,katika kipindi cha miezi sita iliyopita mkoani Iringa wamekwishapata wateja zaidi ya 3,000.

  AccessBank ni taasisi ya kifedha inayolenga kutoa huduma za kibenki kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia wanahisa wake wa kimataifa ambao ni AccessHolding, International Finance Corporation, African Development Bank na MicroVest.

  0 0

   Wananchi wakiangalia daladala lenye namba za usajili T 161 CRP lililoacha njia na kupinduka Mbagala Misheni kwa Bluda Dar es Salaam leo asubuhi na kujeruhi watu watatu.
  Daladala likiwa mtaroni.

  Na Dotto Mwaibale

  WATU watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya daladala walikuwa wamepanda kutoka Temeke kwenda Mbagala Kuu kuacha njia na kupinduka jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com Dar es Salaam leo asubuhi askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa kipolisi wa Temeke ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa polisi alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 na nusu asubuhi.

  Alisema daladala hilo liliacha njia na kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mbagala Misheni kwa Bluda baada ya kuteleza kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.

  Alisema baada ya ajali hiyo wananchi walifika kutoa msaada kwa majeruhi ambao walikimbizwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

  Alitaja daladala hilo kuwa ni lenye namba za usajili T 161 CRP ambapo alitoa mwito kwa madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari yao hasa katika kipindi ambacho mvua zinanyesha.

  Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto ili kuzungumzia ajali hiyo zilishindikana baada ya kupigiwa simu ambayo ilikuwa ikiita pasipo kupokelewa.


  0 0

  Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward akipokea cheti cha ushiriki wa maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji (viwanda) Dkt. Adelhelm Meru wakti wa hafla ya kufunga maonesho hayo jana jijini Dar es Salaam.

  Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward akishiriki hafla kufunga maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania yaliomlizika katika viwanja vya Mwl. Nyerere (sabasaba) jana jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward alipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARDE) Bw. Edwin Rutageruka.  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Kampuni ya Kahama Oil Mills iliyopo katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imeisaidia Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa kuajiri jumla ya watu 639.

  Idadi hiyo imetajwa jana Jijini Dar es Salaam na Meneja Uzalishaji wa kampuni hiyo, Bryason Edward alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii wakati wa kumalizika kwa Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vya Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

  Edward amesema kuwa wameamua kushiriki katika maonesho hayo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na wajasiriamali wengine pamoja na kuwaonyesha Watanzania bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikizalishwa nje ya nchi ambazo kwa sasa zinazalishwa na kupatikana hapa hapa nchini.

  “Mpaka sasa kampuni yetu ina matawi 6 nchi nzima yaliyopo Kahama, Shinyanga, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma ambayo ndio yamewezesha kuajiri jumla ya watu 639, hayo yote yametokana na kuona fursa na kuthubutu kuzitumia fursa hizo,”alisema Edward.

  Ameongeza kuwa ingawa kampuni hiyo bado changa lakini inajitahidi kutoa ajira hasa kwa vijana ili kuwasaidia katika kuendeleza maisha yao pamoja na kuwapatia mafunzo juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujasiriamali ili waweze kupata hamasa ya kuanzisha viwanda vyao vitakavyowasaidia kujiajiri.

  Aidha, Edward ametoa rai kwa vijana kujishughulisha na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii zao ambazo zitawawezesha kujiajiri na kujipatia kipato kwa njia zilizo halali kuliko kujibweteka kusubiri kuajiriwa.

  Ameiomba Serikali kurejea upya tozo za uingizaji wa vifaa kwa ajili ya utengenezaji wa mabati ili ziweze kupunguzwa hivyo kuwasaidia wajasiriamali kupata kipato kinacholingana na biashara hiyo.

  Kampuni hiyo imeanzishwa mnamo mwaka 2005, inajihusisha na uchambuaji wa pamba na uzalishaji wa mafuta ya pamba pia inazalisha mabomba na vyombo vya plastiki pamoja na mabati ya aina zote.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Alhaj Abukary Zubeiry Bin Ally baada ya kuwasili Shelui mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili Shelui mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba. Muungano na Mazingira, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo , Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo , Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi baada ya kuwasili Shelui kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid, Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bibi. Gaudencia Simwanza akiwasilisha mada wakati wa semina maalum kwa wajasiriamali wanawake iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuelekea kilele cha maonesho ya viwanda vya Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bibi. Gaudencia Simwanza akigawa vipeperushi wakati wa semina maalum kwa wajasiriamali wanawake iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuelekea kilele cha maonesho ya viwanda vya Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija – MAELEZO.

  …………………………………………………….

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa wito kwa wazalishaji wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mafunzo kwa urahisi pamoja na kusaidiana kiuchumi.

  Wito huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka hiyo, Gaudencia Simwanza wakati akitoa mafunzo katika semina ya wakina mama wajasiriamali iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kufanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

  Gaudencia amesema kuwa ni lazima kuchunguza kwa makini bidhaa mbalimbali zinazohusisha afya ya binadamu kwa ajili ya kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa hizo ili zisiweze kumdhuru mtumiaji hivyo, mamlaka hiyo haijawekwa kwa bahati mbaya bali ina madhumuni thabiti ya kulinda afya ya watumiaji wa bidhaa hizo.

  “ili kuhakikisha bidhaa hizo ni salama kwa afya ya mtumiaji ni lazima kuhakikisha tunatoa elimu na mafunzo kwa wazalishaji ili waweze kuzalisha kulingana na utaratibu mzuri uliowekwa ndio maana tunawashauri wajiunge kwenye vikundi ili iwe rahisi kupata elimu pamoja na kupata nafasi kubadilishana mawazo yanayohusu uzalishaji wa bidhaa zao,” alisema Bi Gaudencia.

  Afisa Mahusiano huyo ameongeza kuwa, kwa kuwa sifa ya kwanza ya kusajiliwa katika Mamlaka hiyo ni kuwa na jengo la uhakika na salama kwa ajili ya kuzalishia bidhaa hizo, hivyo uundaji wa vikundi vya pamoja utasaidia wazalishaji kutafuta fedha kwa pamoja kwa ajili ya kupata jengo kwani wazalishaji wengi wamekua wakilalamika kukosa fedha kwa ajili ya jengo la kufanyia shughuli hizo.

  Amefafanua kuwa mbali na vikundi hivyo, Mamlaka hiyo imekua ikitoa elimu kwa wajasiliamali mbalimbali kupitia ofisi za za kanda zilizopo katika Mikoa 7 nchini ikiwemo ya Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Mashariki, Magharibi, Kaskazini, Kusini na Kanda ya Kati.

  Amewasisitiza wajasiriamali wote wanaozalisha bidhaa zinazohusisha afya ya binadamu kusajili majengo yao pamoja na kusajili bidhaa zao ili kupata Hati ya Usajili wa Jengo pamoja na kibali cha kutengenezea bidhaa hizo mara baada ya kukamilisha taratibu zote zilizoainishwa kisheria.

  TFDA ni taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyoundwa kwa ajili ya kusimamia na kuhakikisha bidhaa zinazohusika na afya ya mtumiaji zinatengenezwa katika hali ya usafi na usalama.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewashukuru na kuwapongeza madaktari wa Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania ambayo imetoa huduma ya matibabu ya macho kwa zaidi ya wananchi 4,000 wa mkoa wa Dodoma

  Ametoa pongezi hizo jana usiku (Jumapili , Desemba 11, 2016) wakati akizungumza na madaktari waliotoa huduma hiyo walipomtembelea katika makazi ya Waziri Mkuu mkoani Dodoma

  Waziri Mkuu alisema huduma wanayoitoa ni muhimu kwa kuwa imewezesha watu ambao walikata tamaa ya kuona wameona, hivyo aliwaomba waendelee kwenda katika maeneo mengine nchini ili Watanzania wengi zaidi waweze kunufaika.

  “Nawashukuru kwa mchango mkubwa mnaoutoa katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye utoaji wa huduma za matibabu ya macho bure na kuwawezesha hata wale wasiokuwa na uwezo kupata huduma ,” alisema .

  Serikali ya awamu ya Tano ina dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi na kutoa huduma kwa wote , hivyo tuko tayari kushirikiana na taasisi yeyote ambayo inakusudia kuwafikia wananchi.

  Waziri Mkuu alisema “katika utoaji huduma za jamii , Serikali inathamini sana mchango wa taasisi binafsi na za dini ambazo ziko mstari wa mbele kushirikiana na jamii kwa ujumla,”.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwakaribisha madaktari hao kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani Dodoma. “Hapa ndio makao makuu ya Tanzania , hivyo nawakaribisha mje kuwekeza, ardhi ya kutosha ipo . Mnaweza kuja kujenga hospitali kubwa ya macho,” alisema .

  Naye Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa, Anthony Mavunde alisema jumla ya watoto 250 wamefanyiwa upasuaji wa macho na madaktari hao ambao walianza kutoa huduma hiyo Desemba 8, 2016 na wanatarajiwa kumaliza Desemba 12, 2016

  “Nawashukuru kwa moyo wenu wa kujitolea kuja kusaidia watu wenye mahitaji ya matibabu ya macho . Mkoa wa Dodoma una changamoto kubwa ya matatizo ya macho .Nimefarijika sana kuona baadhi ya akinamama waliokuwa wamekata tamaa ya kuona wameweza kuona tena,” alisema.

  Naye Mtaribu wa taasisi hiyo, Noorelain Sharrif alimuahidi Waziri Mkuu kwamba wataendelea kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za matibabu ya macho bure kwa wananchi wenye mahitaji na wako tayari kwenda popote nchini kutoa huduma hiyo

  “Tuko tayari kushirikiana na Serikali katika kutimiza wajibu wetu kwa jamii , tutafanya hivyo wakati wowote na kwa wananchi wote,” alisema.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kodi ili waweze kufahamu aina na madaraja ya kodi pamoja na umuhimu wa ulipaji kodi.

  Mafunzo hayo yametolewa jana na Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, George Haule katika semina ya wakina mama wajasiriamali iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kufanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

  Haule amesema kuwa katika uanzishaji wa biashara ya aina yoyote jambo la kwanza na muhimu ni kujisajili katika mamlaka hiyo na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN – Number) itakayomuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali kuwa na biashara halali ambayo inalipiwa kodi kulingana na mauzo au faida ya biashara husika.

  ”Tanzania ni nchi yetu na sisi Watanzania ndio tuna jukumu la kuitunza nchi hii, njia rahisi ya kuitunza nchi ni kulipa kodi stahiki ili kuinua pato la taifa kwa sababu kodi ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi,”alisema Haule.

  Haule ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inatumia mfumo endelevu wa ulipaji kodi kwa maana ya kila mfanyabiashara mdogo mwenye mauzo yasiyozidi 20,000,000 kulipa kodi ya mwaka kulingana na mauzo yake na mwenye mauzo yatakayozidi kiasi hicho cha fedha kulipa kodi ya mwaka kulingana na faida anayoipata katika biashara husika.

  Amefafanua kuwa wafanyabiashara wadogo wamegawanyika katika makundi matano ambapo wenye mauzo ya kuanzia shilingi 1 hadi 4,000,000 kwa mwaka hawalipi kodi yoyote, wenye mauzo kuanzia 4,000,000 hadi 7,500,000 wanalipa kodi ya shilingi 150,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia 7,500,000 hadi 11,050,000 wanalipa shilingi 318,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia 11,050,000 hadi 16,000,000 wanalipa shilingi 546,000 kwa mwaka na wenye mauzo kuanzia 16,000,000 hadi 20,000,000 wanalipa shilingi 862,000.

  Ameendelea kufafanua kuwa mfanyabiashara mwenye mauzo ya zaidi ya 20,000,000 sheria itamtaka aandae mahesabu ya mauzo yake ili aweze kulipa kodi kulingana na faida anayoipata kwa mwaka mmoja.

  Amewaasa wafanyabiashara kufuata sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya ufanyaji wa biashara nchini ili kwa pamoja tushirikiane katika kuijenga Tanzania yenye maendeleo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurgenzi Mtendaji wa Wakala wa Vyuo vya Nje ya Nchi (GEL) Bw. Abdulmalik Mollel (kulia) alipotembelea banda la Wakala hiyo katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARDE) Bw. Edwin Rutageruka
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bw. James Ndege (watatu kutoka kushoto) alipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania yaliyomalizika jana katika viwanja vya Mwl. Nyerere (sabasaba) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari na Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo Bi. Roberta Ferouz.
  Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika banda la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) walipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Shirika la Kuthibiti Viwango Tanzania (TBS) Bi. Rhoda Mayugu akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akiangalia namna mashine ya kufyatulia matofali inavyofanya kazi alipotembelea mmoja ya banda katika maonseho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.

  Picha zote na: MAELEZO.

older | 1 | .... | 1066 | 1067 | (Page 1068) | 1069 | 1070 | .... | 1897 | newer