Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

TASWIRA KATIKA MABANDA YA MAONESHO YA VIWANDA VYA NDANI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

$
0
0
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza (kulia) akitoa maelezo kwa wateja wa waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja huduma kwa wateja na Elimu kwa Umma Ndugu Jemes Ndege( kulia)akitoa elimu kwa wananchi waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa Umeme VETA Kipawa, Athuman Ubaya akitoa maelezo kwa wananchi waliofika katika banda la TFDA katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Habari PPR, Paschal Mayara akitoa huduma katika maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata maelezo katika banda la Dar Ropes katika Maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchumi na Biashara wa Nchini, Ukraine, Nataliya Mykolska akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Azam, Omary Kuwe walipotembelea banda la Azam katika Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata huduma katika banda MeTL katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


BUNDI AZIDI KUWIKA ACT WAZALENDO MWINGINE AJITOA

$
0
0
         



      TAARIFA KWA UMMA
------------------------------
--------
YAH:- KUJIVUA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO NA KUTOSHIRIKI SIASA.
------------------------------

Mimi Mchange Habibu Mchange, Leo  Jumaamosi tarehe  10.12.2016,  ninaujuza umma wa Watanzania,  Rafiki zangu,  ndugu na jamaa.

Kwamba kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikijihusisha na harakati za kisiasa,  awali nikiwa mwanachama wa Chadema na baadae ACT WAZALENDO. 

Kwamba katika Chama cha ACT WAZALENDO nimepata heshima ya kuwa kiongozi mwandamizi kama katibu wa Mipango na Mikakati na baadae Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika secretarieti ya Chama hicho.

Na Kwamba tangu kujiunga kwangu na Chama hicho nimekuwa mjumbe wa kamati kuu, mjumbe wa Halimashauri kuu na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Chama.

Kwa moyo mkunjufu kabisa,  na kwa mapenzi mema na taifa langu.

Ninathibitisha Kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma Sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.

Kwa mantiki hiyo basi,  kuanzia Leo hii, nitaiomba jamii katika yote nitakayofanya inione nimefanya kama Mchange huru asiye mwanachama wa Chama chochote cha siasa.

Ninaomba uamuzi wangu huu uheshimiwe na kamwe nisihusishwe na aina yoyote ya siasa bali utanzania wangu.

Ningeweza kufanya uamuzi wangu huu kimya kimya, lakini kwa hatua niliyoifikia na ili kuweka kumbukumbu sawia ni budi niutoe kwa umma.

Ninafahamu kuwa kuwa mwanachama wa Chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba,  lakini nimeamua kuihifadhi haki yangu hiyo kwa sasa Mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.

Ninawatakia kila la heri waliokuwa  wanachama wenzangu wa ACT WAZALENDO katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa Chama hicho.

Kujiondoa kwangu kushiriki katika siasa kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya Chama hicho.

Tafadhali ichukueni hii kama chachu ya kuwafanya mfikie malengo mahsusi kwa wakati muafaka bila kurudi nyuma.

Msivunjike moyo, msirumbane,  pendaneni,heshimianeni  na shikamaneni ili mfikie lengo

Sasa nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na  swahiba. zaidi mtanzania mwenzenu.  Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa.

Kwa wanachama wa vyama vinginevyo kama CHADEMA, CUF, CCM, ADA TADEA na kadharika,  nitaendelea kuwa rafiki mwema kwenu, jirani na ndugu wa kweli kama au pengine zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.

Ninawatakia heri wanasiasa wote wa vyama vyote hapa nchini.

Ninawaomba radhi wote niliowahi kuwakosea, kuwa kwaza ama kuwafanya wajisikie vibaya kutokana na matendo yangu, maandishi yangu Misimamo yangu, matamshi yangu ama na mwenendo wangu wa kisiasa kwa kipindi chote nilichokuwa mwanachama wa vyama vya siasa hapa nchini.

Ninaahidi kuendelea kuwa mtanzania Mtiifu mwenye mapenzi mema kwa taifa langu huku nikiwatakia heri wanachama wapenzi na viongozi wa vyama vyote vya siasa.

Itoshe tu kufahamika Kwamba Mimi Habibu Mchange,  kwa sasa si mwanachama, mpenzi wala mshabiki wa Chama chochote cha siasa.

Zaidi, Ninawaomba radhi watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine nitakuwa nimewakwaza kutokana na uamuzi wangu huu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wasalaam
Habibu Mchange,
0762178678.
Morogoro Tanzania

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na viongozi walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka, Wakwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin pamoja na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo. Picha na IKULU

DK. SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar Nd,Asaa Ahmada Rashid alipowasili katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi Zanzibar Nd,Asaa Ahmada Rashid (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman mara alipowasili katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo.
Kikundi cha Brass Band cha Jeshi la Polisi Zanzibar wakiongoza matembezi ya Taasisi mbali mbali zilizoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

Vijana waliobeba bango linalotoa ujumbe usemao Siku ya Maadili na Haki za Binadamu”Imarisha Utawala Bora kwa Kukuza Uadilifu,Uwajibikaji,Haki za Binadamu na Mapambano Zidi ya Rushwa”wakati wa matembezi ya maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono vijana walioshiki matembezi katika wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja

Vijana walioshiki matembezi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea matembezi hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Ngoma ya Kibati ikichezwa na kikundi cha Vijana Ngoma Group katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

Baadhi ya Viongozi na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
Baadhi ya Vijana waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,wakimsikilizaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)alipokuwa akizungumza katika sherehe hizo.

Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)alipokuwa akizungumza na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]10/12/2016.
Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)alipokuwa akizungumza na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu Duniani zilizofanyika leo katika Viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]10/12/2016.

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM WAMUUNGA MKONO RAIS DK. MAGUFULI KWA KUAHIDI KUENDELEA KUWATUMBUA HADHARANI MAFISADI, SHEREHE ZA UHURU KUFANYIKA DODOMA MWAKANI

$
0
0
theNkoromo Blog, Dar.

SHIRIKISHO la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limemuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, kwa kuamua maadhimisho yajayo ya Uhuru kufanyika Dodoma, likisema uamuzi huo umedhihirisha dahamira yake ya dhati ya kuhakikisha Dodoma inakuwa Makao Makuu ya nchi kwa vitendo.

Limemuunga, Rais Magufuli kwa kuweka wazi katika hotuba yake kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za Watanzania na pia kuendelea kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa na ufisadi, kwa sababu rushwa ni saratani.

Shirikisho hilo, pia limemuunga Rais kwa tamko lake la hivi karibuni la kuamuru machinga, wachimbaji wadogo na wafugaji  kutofukuzwa hovyo hadi mamlaka zinazohusika zitakapotenga maeneo maalumu, likisema pongezi hizo ni kwa sababu Rais amedhihirisha kuwa anajali zaidi masikini na wanyonge.

Salam hizo zimesemwa leo, Desemba 10, 2016, na Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alipozungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake, Makao Makuu ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, jijini Dar es Salaam, akitoa taarifa ya Shirikisho hilo kuingiza wanachama wapya 100 toka Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili.

"Kwa kweli tunayo mengi ya kumuunga mkono na kumpongeza Rais, hata hili la kununua ndege sita. Ndege hizi licha ya kusaidia kurahisisha usafiri wa anga pia zitasaidia sana kukuza utalii ambao  utachangia kuongeza mapato ya nchi, na ni matarajio yetu mapato yakiongezeka uchumi utakua na hata bei za bidhaa zitapungua na hivyo Watanzania walio wengi  kupata nafuu ya maisha".

"Pia sisi kama Watanzania lazima tumuunge mkono na kumpongeza Rais kwa kuendelea kuonyesha dhamira ya serikali ya awamu ya tano kutoa elimu bure kwa kitendo chake cha kutenga kila mwezi sh. bilioni 18.777 kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari na kwa Vyuo Vikuu sh. Bilioni 483 kutoka sh. bilioni 340 za mwaka jana, hali ambayo imewezesha ongezeko la wanafunzi kutoka 98,000 hadi kufikia 125,000 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu", alisema Zenda.

Akizungumzia wanachama hao wapya ambao ni madaktari waatarajiwa, katika hafla iliyofanyika Upanga , Dar es Salaam, Zenda alisema, wakati akiwapokea, aliwaambia wamefanya vizuri kujiunga na CCM kwa kuwa wamejiunga na chama makini chenye serikali sikivu inayowajali wanyonge chini ya Rais Dk. John Magufuli.

Shirikisho linawa taka wanafunzi hao na Watanzania kwa kujumla kubeza propaganda zinazosemwa na baadhi ya wanasiasa, kwamba kwa nini  ndege zinanunuliwa wakati hakuna dawa katika hospitali.

 "Propaganda hii ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kutaka kuwafanya Watanzania hawana akili, maana kila mmoja anajua kwamba katika kipindi hiki kifupi alichoingia madarakani Rais Dk. Magufuli ameboresha sekta ya afya katika maeneo mengi ikiwemo upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vutuo vya afya", Alisema Zenda.

Alisema, miongoni mwa maboresho aliyofanya Rais kwenye sekta ya afya ni pamoja na kuongeza bajeti ya sekta hiyo ya afya kwa ajili ya manunuzi ya dawa kutoka Sh. bilioni 31 hadi kufikia sh. bilioni 250 mwaka huu.
Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akizungumza wakati akiwapokea wanachama wapya 100 wa CCM kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili, katika hafla iliyofanyika jana, Upanga jinini Dar es Salaam.

Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano nas Mazingira Mhe Luhaga Mpina Zanzibar.

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo ya utendaji wa Tume hiyo wakati akiwasilisha Ripoti ya Utafiti iliofanywa na Tume hiyo wakati wa ziara ya Mhe Luhaga, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Tume hiyo maruhubi Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akipitia Ripoti ya Tume ya Sayansi na Teknolijia Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume hiyo ilioko Zanzibar.
Mratibu wa Kituo cha Tume Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina alipofika katika Kituo hicho maruhubi Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizunhgumza na waandishi wa habari Zanzibar baada ya kumalizia mazungumzo yake na kupoata taarifa ya Utendaji wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar katika ofisi zake ziliko maruhubi Zanzibar.  
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muunganio na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwasili katika viwanja vya Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar kutembelea kituo hicho kujionea shughuli zinazofanywa katika kazi za Utafiti wa Zao la Kilimo Zanzibar. 
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar Ndg Khatib Juma akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina alipofika Kituoni hapo kutembelea na kujionea shughuli za utafiti zinazofanya na Kituo hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa katika ziara yake Zanzibar.
Mratibu wa Tume ya Sayansi na Teknolijia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza wakati wa ziara yake na wafanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar kutembelea Miradi inayofadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina akitembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa na Mkuu wa Kituo hicho Ndg.Khatib Juma. 
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar Ndg Khatib Juma akitowa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakiwa katika maabara ya kituo hicho kizimbani Zanzibar wakati wa ziara yake. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiangalia mpunga unaofanyiwa utafiti katika Kituyo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo hicho Ndg Juma Khatib katikati.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitoka katika Jengo la Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani Zanzibar akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ilinayodhaminiwa na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Tanzania katika utafiti wake.

Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.
othmanmaulid@gmail.com
Zanzinews.com 
0715 424152.or 0777424152.
Zanzibar. 

KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUREJESHA FOMU ZA WAGOMBEA UONGOZI WA BARALA LA VYAMA VYA SIASA

Waziri Nape azindua mashindano ya kuogelea ya vijana chini ya umri wa miaka 13 jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kuogelea ya vijana chini ya umri wa miaka 13 yanayoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club yanayofanyika katika bwawa la shule ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea ya Vijana chini ya umri wa miaka 13 wakijaaandaa kuruka ndani ya bwawa la kuogelea kuanza kushindana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Sewimming Club.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea ya Vijana chini ya umri wa miaka 13 wakijaaandaa kuruka ndani ya bwawa la kuogelea kuanza kushindana katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Sewimming Club.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mashindano hayo ya Vijana ya kuogelea yaliyoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club. 
Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwavalisha medani baadhi ya washindi wa kuogelea mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yanayoandaliwa na Dar es Salaam Swimming Club yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.

MAKAMU WA RAIS AITAKA TAKUKURU KUONGEZA KASI KUBAINI WAHALIFU WA VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO,DAR ES SALAAM.
 
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi ya kuwabaini na kuchukua hatua za kisheria bila kuwaonea aibu na uoga wahalifu wa vitendo vya rushwa nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu na uzinduzi wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais alisema mapambano dhidi ya rushwa hayajaelekezwa upande wa watumishi wa Serikali pekee, bali pia kwa wafanyabiashara pamoja na asasi za kiraia.

Samia alisema Serikali itaendelea kutambua mchango wa taasisi za uwajibikaji na utawala Bora katika jitihada zao za kuimarisha misingi ya Utawala bora, uwazi, uadilifu na  uwajibikaji.

Taasisi hizo ni Ofisi ya Rais-(Utumishi na Utawala bora), Takukuru, Sekretarieti ya Maadili, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Tume ya Haki za binadamu, Mamlaka ya Ununuzi wa Umma, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Aidha, Makamu wa Rais alisema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika taasisi hizo ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora za ukaguzi zenye kuleta tija kwa wananchi na hivyo kuimarisha uwajibikaji na thamani ya fedha kwenye makusanyo na matumizi ya rasilimali za umma.

“Serikali imeendelea kuziwezesha kiutendaji taasisi hizi ili kuhakikisha zina uwezo wa kukuza na kusimamia viwango vya maadili kwa kutoa elimu, kufanya uchunguzi, kupokea na kuhakiki matamko ya mali na madeni ya viongozi wa umma kwa lengo la kutekeleza falsafa ya utawala bora” alisema Samia.

Akifafanua zaidi Makamu wa Rais alisema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa baadhi ya watumishi na watendaji wa Serikali wamekuwa  wakiwabambikia kesi wananchi wasio na hatia kwa kupata hukumu zisizostahili, kitendo kinachopelekea kukwamisha maendeleo ya taifa.

Aliongeza kuwa Serikali katika kuhakikisha inalinda rasilimali za umma, inaondoa uonevu na dhuluma, kwa kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ili kukabiliana na tatizo hilo.

“Ni jukumu na wajibu wetu kama Serikali kutoa Ulinzi, Usalama na Huduma Bora kwa jamii, lakini ufanisi wa kutekeleza wajibu huu utawezekana endapo watumishi wote wa Serikali watawajibika ipasavyo kuwaongoza katika utendaji kazi” aliongeza Mama Samia.

Kwa upande wake Mkurugezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola alisema kuwa maadhimisho hayo yamelenga katika kuimarisha nidhamu kwa watumishi wa umma kwa kuzingatia kasi ya maendeleo ya Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa kampeni hii kufanyika nchini kwa lengo la kihimiza ukuzaji wa maadili katika utumishi wa umma na katika jamii kwa ujumla, utetezi na ulinzi wa haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa, wizi, ufusadi na ubadhilifu wa mali za umma.

Kampeni ya siku ya Maadili na Haki za binadamu yenye iliyobeba kauli mbiu “kujenga na kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa” imedumu kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Novema 10 hadi 10 Desemba mwaka huu.

TAASISI YA AGRI-BUSNESS MEDIA INNITIATIVE YASHIRIKI UZINDUZI WA UNGA WA VIAZI LISHE JIJINI MWANZA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe uliofanyika hii leo Jijini Mwanza. Taaisisi hiyo imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.

Unga wa viazi lishe ni muhimu kiafya kwani una wingi wa vitamini A miongoni mwa vitamini mbalimbali ambapo husaidia kuondokana na matatizo ya kuona (upofu). Pia viazi hivyo hutumika kama chakula, na unga wake ni bora kwa ajili ya utengenezaji wa mandazi, chapati, keki, biskuti na vitafunwa vya kila aina.

Taasisi hiyo imeshirikia kama miongoni mwa taasisi hususani za wajasiriamali wanawake zinazojihusisha na kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda. Lengo lake ni kuhakikisha wanawake wanajiinua kiuchumi ili kuondokana na utegemezi na hatimaye kuondoana na adha zinazoweza kuwakumba ikiwemo ukatili kutokana na utegemezi.

Uzinduzi huo umeenda pamoja na Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani, yaliyoanza Novemba 25,2016 hadi leo Disemba 10,2016.
Na BMGHabari
Mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi Koshuma, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe, uliotayarishwa na wanawake wajasiriamali kutoka Shirika la Sauti ya Wanawake lililopo Ukerewe mkoani Mwanza. 

Shirika hilo limefanikiwa kwenye usindikaji wa bidhaa za kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda kwa msaada wa Shirika la Akina Mama Lishe la Tanzania Entrepreneurs Development and Advocacy Organization TEDA.
Akina mama wajasiriamali mkoani Mwanza wakimsikiliza mgeni rasmi, Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mwanza, Kiteto Zawadi Koshuma, wakati akizindua Unga wa Viazi Lishe hii leo Jijini Mwanza.

Koshuma amewahimiza akina mama kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda ikiwemo viazi lishe kwani soko lake ni kubwa ikizingatiwa kwamba viazi hivyo vinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vitafunwa. Amewashauri kuzingatia suala la usindikaji wa mazao yao ili kuvutia zaidi soko la ndani na nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,  Kombe Danty, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe mkoani Mwanza.
Pudentia Ngereza ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika la Sauti ya Mwanamke kutoka Ukerewe (Pia diwani Viti Maalumu Ukerewe), akizungumza wakati wa uzinduzi wa unga wa viazi lishe unaozalishwa na shirika hilo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora nchini ADLG, Jimmy Luhende, akizungumzia ubora wa matumizi ya viazi lishe wakati akinunua unga wa viazi hivyo baada ya kuzinduliwa rasmi hii leo mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi kuhusiana na mbogamboga na matunda zinazozaliwa na taasisi yake.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba,  akonesha bidhaa zinazozalishwa na taasisi hiyo ambapo mteja hujipatia hoho, nyanya, pilipili, chainizi, kabichi, karoti, bamia, mchicha, vitunguu, tangawizi, mchaichai, karanga, kisamvu, sukuma wiki, vitunguu swaumu, nyanya chungu na majani ya kunde ambapo kwa pamoja huuzwa kwa bei nafuu.
Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.
Simon Nkwabe Ng'wanakilala ambaye ni msaidizi katika Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akonesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo ambayo pia imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.
Mgeni Rasmi amepokea zawadi ya vitafunwa zilivyotengezwa na Unga wa Viazi Lishe kutoka Shirika la Sauti ya Wanawake kutoka Ukerewe mkoani Mwanza.
Mgeni rasmi akiwa pamoja na wageni kutoka taasisi na mashirika mbalimbali kwenye picha ya pamoja.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Ama Bonyeza hapo chini.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA ALHAJ ALIKO DANGOTE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO, WAKATA MZIZI WA FITNA WA WAPIGA DILI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Video na IKULU. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda. 

Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.

Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ''amesema Rais Magufuli.

Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.


Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje. 
Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini. 

Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Katika hatua nyingineRais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida. 

Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).


Jaffar Haniu,

Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.

Dar es Salaam.


10 Desemba, 2016.

WAZIRI NAPE APONGEZA TUZO ZA EATV, ALI KIBA ANYAKUA TUZO TATU, DJ BONNY LOVE APEWA TUZO YA HESHIMA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwapongeza Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo,zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,ambapo Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameibuka kinara kwa kujinyakulia tuzo tatu.
 Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo.
1
Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.Tuzo hizo zimeandaliwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es salaam kinachorusha matangazo yake katika nchi za Afrika Mashariki.
2
DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akipongezwa na DJ John Dilinga mara baada ya kupokea tuzo yake ya Heshima katika tuzo zilizoandaliwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.
5
Mwanamuziki Lady Jay Dee akipongezwa na Mme wake baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.
1
Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindi wa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania ,Nandi Mwiyombela  katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 11, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI AWAMU YA TATU

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akikata utepe kama ishara ya kuzindua  Makati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu, kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akishuhudia zoezi hilo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Valentino Mlowola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu akihutubia watumishi na wananchi wakati wa kilele cha  Maadhimisho ya siku ya maadaili na haki za binadamu zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
 Makatibu Wakuu wa Wizara mbali mbali pamoja na viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye Kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.

TUTASHIRIKIANA NA MAKAMPUNI BINAFSI KUPANGA MAKAZI YA WANANCHI- MEYA WA UBUNGO

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe amesema kuwa eneo litalakolokuwa limepimwa na kugundulika ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii kama Manispaa wapo tayari kulipa fidia kwa wananchi ili kupisha.

Hayo ameyasema leo kwenye mkutano na wananchi wa mtaa wa Kunguru, kata ya Goba wakiwa pamoja na taasisi binafsi inayijishughulisha na masuala ya upangaji na upimaji wa maeneo nchini HUSEA.

Jacob amesema, anatoa sifa kubwa sana kwa hatua iliyofikiwa na wananchi wa Kunguru kwa kuamua kupima maeneo yao wenyewe na zaidi kwani Halmashauri ndiyo wenye majukumu ya kufanya hivyo ila kwa hatua hiyo waliyofikia kwa kushirikiana na HUSEA wamefanya jambo kubwa sana na wanawaunga mkono kwa jitihada hizo.

"Kutakapotokea kama kuna eneo ambalo ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii na limejengwa na mkakubaliana kupata eneo lingine kwa ajili ya shughuli hizo basi msisite kutuambia kwani ili sisi kama Halmashauri tuweze kulipa fidia, "amesema Jacob. 

Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa amesema kuwa kwa hatua hii imeweza kusaidia katika kupanga maeneo ya mtaa wa Kunguru na zaidi wananchi wameweza kushirikiana nao kwa hatua nzuri mpaka kufikia kuweka makubaliano ya upangaji wa maeneo na kuna baadhi ya wananchi wamejitolea kuacha maeneo yao kwa ajili ya kuendeleza mipango endelevu.

Katika eneo la Kunguru, kumeweza kupatikana kwa maeneo 1432 na wameweza kuyapima na waliweza kupata ushirukiano mzuri kutoka kwa Wizara ya Ardhi na waliweza kuwapa ramani halisi ya eneo hilo ila kutokana na wanachi tayari wameshajenga wamepata sura ya ramani ambayo ni mpya na itakapokamilikwa kupimwa kuanzia mwezi Januari mwakani watafanya mabadiliko ya ramani hiyo.

Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala amesema kuwa wao kama Wizara wamedhamiria kuhakikisha wanashirikiana na makampuni binafsi kuweza kupima na kupanga maeneo ya makazi ya watu mjini na vijijini na zaidi mpaka kufikia mwaka 2016 ni asilimia 15 tu ya maeneo yamepimwa. 

Mradi huo ulianza mnamo mwezi Mei mwaka huu na uliweza kupata changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwemo watu kusema kuwa ni makampuni ya kitapeli ila baada ya kuwapa elimu waliwez kuelewa na siku ya kwanza ya mkutano huo wananchi zaidi ya 800 walijiandikisha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao.
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe akizungumza  na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo unaoendeshwa na Kampuni ya HUSEA, kulia ni 
Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa  na kushoto ni
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala
Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa 
akizungumza  na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo na kuelezea namna kampuni yake ilivyojikita katika kuhakikisha wanasaidiana na serikali kwenye utatuzi wa migogoro na upangaji wa maeneo. Akiwa amekaa meza moja na Diwani wa kata ya Goba Ibrahim Kenya (wa kwamza kushoto), 
Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala.
Wananchi wakiwa wanaelezewa namna Mtaa wa Kunguru ulivyopimwa na kutakiwa kupangwa.

WATANZANIA WAASWA KUHURUMIANA NA KUPENDANA BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI

$
0
0
Shekhe Hemed Jalala  akizungumza na waandishi wa habari kueleka maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mtume ( S.A.W), kulia ni mlezi wa Hauzat  Imamu Swadiq Mzee Rashidi  Mashtog na  upande wa kushoto ni  Naibu kiongozi Mkuu Mohammad Abdi .


Na Anthon John Globu ya jamii.
IKIWA  imesalia siku moja kufikia maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad Kiongozi wa waislam wa madhebu ya shia Ithnashariya  Tanzania  Shekhe Hemed  Jalala amewataka  watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.

Akizungumza na waandishi wahabari Leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es salaam amesema Mtume Mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza Upendo na amani hivyo ni vyema waTanzania  kuishi kwa Upendo bila kujali utofauti wa dini zao.
  
"Mtu kupenda nchi ni katika amani na pia dini imekuja kutunza upando na amani watanzania tusibaguane kutokana na dini zetu" amesema Jalala.

Hata Hivyo Sheikh Hemed amebainisha kuwa ni vyema jamii kuyaishi maisha aliyoishi Mtume Mohammad ikiwa ni pamoja na sifa kuumbili alizokuwa nazo Mtume ambazo  nikuwa mkweli na mwaminifu.
  
Sambamba na hayo ameongeza kuwa Kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na watanzania hasa kwa kipindi hiki chakukumbukwa kwa kuzaliwa kwa Mtume ni kuishi kwa amani na ushirikiano kwa kuwa vitabu vyote vya dini vimekuja kuunganisha watu.                        

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MAULID KITAIFA SINGIDA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo kitaifa itaadhimishwa mkoani Singida.

 Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau alisema sherehe za Kitaifa za Maulid ya Mtume Mohammad (SAW) kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Mkoani Singida katika Kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, Singida. 

 Wiki iliyopita, akitangaza utaratibu wa sherehe hizo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11 na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12. 

 Mufti wa Tanzania aliwataka Waislamu wote nchini waadhimishe Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu. “Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kwa kufanya matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo,” alisema.

RUTAGERUKA:VIJANA NDIO WENYE KUBEBA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Vijana wametakiwa kubeba uchumi wa viwanda wa Tanzania inayojengwa katika serikali ya awamu ya Tano ya Dk. John Pombe Magufuli.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka wakati wa semina ya vijana iliyofanyika katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.Amesema semina imefika muda mwafaka kutokana na nchi kwenda katika sekta ya viwanda ambapo vijana ndio sehemu yao.

Amesema sekta ya viwanda inategemea vijana ambao ndio waendeshaji wa viwanda katokana na ujuzi wao wa kuendea viwanda hivyo.Nae Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, amesema vijana wanatakiwa kutumia fursa ya viwanda pamoja na ujasirimali na kuachana na kufikiria suala la kuajiriwa.

Amesema Taasisi Doris Mollel Foundation,imeona inawajibu wa kutoa elimu kwa vijana katika kuendea sekta ya viwanda.Amesema kuwa kila mmoja akatumia nafasi yake vizuri Tanzania inaweza kuondoka ilipo sasa na kusogea sehemu nyingine katika uchumi wa viwanda .

Akifunga simina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel amesema hakuna tatizo la ajira kwa vijana kuajiriwa kinachofanya vijana na kukosa mafunzo ya kazi ambayo wanakwenda kufanya.Amesema kutokana na mafunzo hayo kupitia maonesho ya viwanda atafanya mafunzo vijana ambao wanakwenda kutumika katika viwanda wakiwa wanakitu kichwani.

Mollel amesema hakuna mtu anaweza akamuachia kijana kiwanda kwa elimu alioipata anatachotaka mwajiri ni kijana mwenye ujuzi wa kutumikia kiwanda chake.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza katika ufunguzi wa semina ya vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Taasisi Doris Mollel Foundation, Erick Kajwahura akizungumza katika semina vijana kuelekea uchumi wa viwanda iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa I-Learn East Afrika Limited, Noelah Ntukamazina akizungumza katika semina kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel akifunga semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu vijana wakiwa semina ya kuelekea uchumi wa viwanda iiyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

VIJANA WANAWEZA KULETA MAPINDUZI YA VIWANDA VINAVYOJENGWA –WAZIRI MPANGO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema vijana ndiyo wanaweza kuleta mapinduzi ya sekta ya viwanda vinavyojengwa. 

Dk.Mpango ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, ameseama vijana lazima wachangamkie fursa ya viwanda pamoja na ujasiriamali. 

Amesema nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaohitaji hivyo sekta binafsi ndiyo inaajiri sehemu kubwa ikiwemo kujiajiri. Dk. Mpango amesema sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu ambao ni vijana wa kufanya hivyo kwa ujuzi wao. 

Aidha amesema kila mtu anatakiwakulipa kodi ili serikali iweze kutoa huduma kwa wananchi na kodi isipotumika kwa malengo wananchi wanaweza kuhoji kodi i yao.

Dk. Mpango amesema serikali haitaki kuibana sekta binafsi ishindwe kupumua kutokana na kodi kinachofanyika kuangalia uwezo wa ulipaji kodi kwa kilakinachozalishwa. Waziri huyo ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Chakula Dawa (TFDA), kuwatembelea wajasiriamali ili kuweza kupata changamoto zao. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari mara baada ya kutembelea maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL),Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda hilo katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Meneja Uhusiano kwa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la TFDA katika viwanja vya sabasaba leo jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakipata huduma katika banda la majani ya chai katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakipata huduma katika banda la Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji katika maonesho ya viwanda yanayoenelea katika viwanja sabasaba jijini Dar es Salaam 
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NAPE: WADAU JITOKEZENI KUDHAMINI TUZO ZA MUZIKI NA FILAMU NCHINI.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Wadau wa Sanaa nchini wameshauriwa kujitokeza kudhamini tuzo kwa ajili ya wasanii wa muziki na filamu nchini ili kuendelea kuzipa nguvu tasnia hizo kwa maendeleo yake.

Ushauri huo umetolea jana na wazori wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki na Filamu nchini zilizoandaliwa na kituo cha Televisheni cha East Africa (Channel 5).

Ameongeza kuwa wadhamini wengi wajitokeze kwa ili kuongeza idadi ya tuzo zenye kiwango kinachostahili zenye kuzingatia weledi na usawa katika utoaji wake.“Niwaombe wadau wa sanaa nchini jitokezeeni kudhamini tuzo hizi za filamu na Muziki ili tuwe na tuzo nyingi zaidi na zenye viwango vya kimataifa”Alisistiza Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amesema kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa katika kuandaa na kusimamia tuzo mbalimbali ikiwa ni nia ya Serikali kuikuza tasnia ya muziki na filamu ambayo ni moja ya tasnia inayoajiri vijana wengi kwa sasa.

“Nawaalika wadau wa Sanaa na wasanii wote sisi tuko tayari kushirikiana nao katika kulisukuma hili guruduma la maendeleo ya Sanaa nchini na nawasahuri tufate tu utaratibu katiaka kuandaa kazi zenu za sanaa” alisema Bw. Muingereza.

Aidha mwakilishi wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Romanus Tairo amesisitiza wasanii wa filamu nchini kufata sheria na gtaratibu zote kabla ya kuandaa na kusambaza filamu zao.

“Nawaomba wasanii wote wa filamu nchini kufuata Sheria na taratibu zilizopo za kusajili filamu zote zikakaguliwa na kuoewa kibali cha kuoneshwa sehemu mbalimbali”Alisema Bw.Tairo.
Tuzo za Muziki na Filamu za EATV zimeanzishwa kwa dhumuni la kuongeza chachu ya maendeleo ya tasnia ya muziki na filamu nchini na jumla ya tuzo nane zilitolewa kwa wasanii wa muziki na filamu na tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini Bw. Bonny Kilosa (Dj Bonny Love).
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images