Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

RIDHIWANI KIKWETE AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE KUKAGUWA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete Desemba 8, 2016 amafanya ziara katika vijiji vya jimbo lake kukagua Miradi ya kimaendeo na kuona namna utekelezaji wake, Katika kijiji cha Kwakonje Shule ya msingi kulikuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya Madarasa lakini tayari ujenzi umeanza katika shule hiyo pamoja na Shule ya Msingi Kibindu, Mbali na Shule katika vijiji hivi changamoto nyingine kubwa ni Maji pamoja na Barabara lakini kupitia Mbunge wao, tayari wamerekebisha barabara ya kutoka Kwaruhombo kwenda kwa Mduma ambayo ni KM 8 iliyokuwa kero kubwa na wamechimba visima kwa msaada wa waturuki katika kijiji cha Kwamsanje lakini pia kutokana na mvua kutonyesha vizuri mwaka jana katika vijiji hivyo kuna changamoto ya uhaba wa chakula lakini kupitia ofisi ya mbunge ziliombwa tan 1200 katika ofisi ya Waziri Mkuu maafa na zikapatikana tan 200 kwa awamu ya kwanza lakini sasa zimepatikana tan 400 na chakula hicho kitagawiwa,  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanakijiji wa Kibindu katika mkutano baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifungua mani katika kisima kilichojengwa kwa msaada wa watu wa Uturuki kupitia Ofisi ya Mbunge katika kijiji cha Kwamsanje baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.   
Kisima kilichojengwa kwa msaada wa Waturuki kupitia Ofisi ya Mbunge kuondoa adha ya kero ya mani iliyokuwa ikiwakabiri wanakijiji wa Kwamsanje kwa muda mrefu.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na watoto wakijiji cha Kwamsanje baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akishirikiana na mwenyekiti wa kijiji cha Kwamsanje kufungua maji kwatika kisima kilichojengwa na watu wa Uturuki kupitia Ofisi ya Mbunge baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwaunga mono wafanya biashara ya Machungwa katika kijiji cha Kibindu alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwaunga mono wafanya biashara ya Machungwa katika kijiji cha Kibindu alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwetee akiangalia maendeleo ya vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Kwakonje alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete na Diwani wa Kata ya Kibindu Mh Mkufya wakiangalia maendeleo ya vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Kwakonje alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Kwakonje maendeleo alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.     Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akipata maelekezo kuhusu ujenzi wa vyumba vya Madarasa na Vyoo katika Shule ya Msingi Pera alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akipata maelekezo kutoka kwe Diwani wa Kata ya Kibindu Mkufya kuhusu ujenzi wa vyumba vya Madarasa na Vyoo katika Shule ya Msingi Pera alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa katika Madawati ambayo yako nje kutokana na uhaba wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Msingi Pera alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.      Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akipata Kahawa na Wazee wa kijiji cha Kibindu alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiagana na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kibindu baada ya mkutano wa hadhara alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na wanakijiji wa Kwamsanje alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze      Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni katika kijiji cha Kwamsanje alipofanya ziara ya kushitukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake la Chalinze.

WAZIRI MKUU APOKEA RIPOTI YA FARU JOHN NA PEMBE ZAKE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa pembe za faru John na  Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori  (Acting Assistant Director of Antipoaching, Wildlife Division), Bw. Robert Mande, katika kikao klichofanyika kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanninayoelezea e maghembe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Aonyeshwa pia pembe mbili za faru huyo
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana (Ijumaa, Desemba 9, 2016) na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

“Nilipokea taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa yenu,” amesema.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.
“Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Watendaji wa wizara waliohudhuria kikao hicho ni Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Iddi Mfunda; Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bw. Freddy Manongi; Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Bw. Simon Mduma; Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori, Bw. Alexander Songorwa na Mkuu wa Pori la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Bw. Nollasco Ngowe.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, DESEMBA 9, 2016.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE afanya Mazungumzo na Mhe. Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji, Jijini Maputo

0
0
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) Desemba 8, 2016, alikutana na Rais wa Msumbiji,  Mheshimiwa Filipe Nyusi alipomtembelea jijini Maputo, Msumbiji.

Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi  Rais Filipe Nyusi Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja  (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanapata elimu iliyo sawa, na kwa kiwango cha ubora unaolingana dunia nzima.
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mhe. Rais Filipe Nyusi ripoti ya Kamisheni ya UN ya Elimu jijini Maputo, Msumbiji.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea. 

Aidha, ripoti inatahadharisha kuwa takribani ajira bilioni 2 zitakufa ifikapo mwaka 2050 kutokana na maendeleo ya teknolojia, ambapo asilimia 70 ya kazi hizo ziko katika nchi zinazoendelea. Hivyo, nchi zinazoendelea zinapaswa kuangalia upya aina ya elimu na stadi zinazotolewa ili kuendana na wakati ujao.
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimpitisha Mhe. Rais Filipe Nyusi katika ripoti ya Kamisheni ya Elimu kuhusu Mapendekezo Mahsusi kwa nchi ya Msumbiji.

Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufidia pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo. Rais Mstaafu ameiomba Msumbiji kujiunga na Mpango huo.

Kwa upande wake, Rais Nyusi amepokea kwa furaha taarifa hiyo na kuelezea nia na dhamira ya nchi yake ya kujiunga na Mpango wa Kizazi cha Elimu. Kufuatia mazungumzo yao, mapema baadae  Rais Mstaafu alikutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Adriano Maleane, Naibu Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Elimu ya Fundi Mhe. Leda Hugo na Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Armingo Ngunga kujadili mapendekezo mahsusi ya Kamisheni kwa nchi ya Msumbiji.
Rais Mstaafu na Mjumbe wa Kamisheni ya Elimu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji, jijini Maputo.

Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda, Malawi, Ethiopia na Msumbiji.na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.
Mhe. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika mkutano wake na Waziei wa Fedha na Mipango, Naibu Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Elimu ya Juu wa Serikali ya Msumbiji.
Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Naibu Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Elimu ya Juu wa Msumbiji.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5,678 KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA

0
0
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe  9 Disemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

(i)           Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2 (i-xx).

(ii)         Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(iii)       Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(iv)        Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

(v)          Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

2.      Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-

(i)              Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.
(ii)            Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA

0
0

WAAJIRI WATAKIWA KUWAPA WAFANYAKAZI WAO FURSA YA KUJIFUNZA ILI KUWAJENGA KIUWEZO

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa amewataka waajiri kuendelea kuwapa fursa wafanyakazi wao kwa kwenda kupata ujuzi wa aina mbalimbali kwani serikali imeadhimia kutoa mafunzo mahsusi kwa lengo la kuwajenga uwezo waajiriwa.

Majaliwa amesema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka iliyoandaliwa na  Association of Tanzania Employer (ATE) zilizofanyika jana usiku na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.,

Katika utoaji wa tuzo hizo, Majaliwa amesema kuwa waajiri wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa upatikanaji wamitaji, tozo ya kuendeleza ujuzi na utiriri wa tozo mbalimbali ambapo huwa inawapa ugumu kuweza kuwapa stahiki waajiriwa na kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige amesema kuwa bado wanakabiliwa na changamoto nyingi ila wanaimani kuwa kutokana na ushirikiano wanaoupata sasa hivi kutoka kwa serikali ya awamu ya tano wana uhakika wa kuweza kutimiza malengo ya waajiriwa ili kupata haki zao.

Maige amesema kuwa bado wataendelea kuandaa tuzo hizi na zaidi Ubalozi wa Norway umeonesha nia nzuri ya kushirikiana nasi kuweza kuona tunafikia makengo mazuri.

Mkampuni na mashirika mbalimbali waliweza kushiriki na kufanikisha hafla hiyo ikiwemoi NSSF, PPF, NHC, SSRA, Geita Gold Mine, Coca Cola, MeTL, ACACIA na mengine pia.

Mshindi wa kwanza wa tuzo ya mwajiri bora ni Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) wakifuatiwa na Coca cCola Kwanza na mshindi wa tatu ni Geita Gold Mine.
 Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wakati wa utoaji wa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 jhafla iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam, Kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu wake waziri Abdallah Possi.

 Tuzo mbalimbali zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kupatiw amakampuni yaliyoshiriki mwaka 2016.
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employer (ATE).
Mwenyekiti wa Association of Tanzania Employer (ATE), Almas Maige akizungumza wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza ya tuo ya mwajiri bora mwaka 2016 Afisa Mwajiri Mkuu wa Tanzania Breweries Limited (LTD) David Magese jana Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa pili ya Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 Meneja  Mwajiri Coca Cola Kwanza Sigifrid Faustine jana Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akitoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa shindano la mwajiri bora lililoandaliwa na Association of Tanzania Employers (ATE) lililofanyika jana Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu  Kassim M. Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka makampuni mbalimbali na washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka 2016 katika vuipengele tofauti.
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Picha zote na Zainab Nyamka

WAAJIRI WATAKIWA KUWAPA WAFANYAKAZI WAO FURSA YA KUJIFUNZA ILI KUWAJENGA KIUWEZO

0
0
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadhara
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga wakifurahia makubaliano yaliyofikiwa katika ya Serikali na kijiji hicho ya kulipa Tsh 1500 kwa huduma ya maji mwezi mzima kwa wanaotumia mabomba ya Kijiji .

Mkuu Wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexander Mnyeti(kushoto0 wakiwalia katika kijiji cha Nkoasenga kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa maji Makilenga.
Mhandi wa Maji Happy Mrisho (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Maji Makilenga.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makilenga waliohudhuiria kwenye Mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alaxander Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadara.

Nteghenjwa Hosseah – Arumeru


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe . Mrisho Mashaka Gambo amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya miaka mitatu kati ya Bodi ya Maji ya Makilenga na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga, Kata ya Leburuki Wilayani Arumeru. 

Utatuzi wa mgogoro huo ulifikiwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Nkoasenga baada ya Mhe. Gambo kuwashirkisha wananchi wa aneo hilo katika kutatua changamoto hii iliyoathiri wananchi zaidi ya hamsini elfu wa kijiji hiki pamoja na vijiji vingine ishirini na sita vinavyotegemea mradi huo.

Wananchi hawa waliofungiwa maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanya uharibifu wa miundombinu ya Maji pamoja na kuweka kinyesi kwenye mabomba walionyesha kuchoshwa na adha hiyo ya kufuata maji umbali mrefu na kwa gharama kubwa zaidi ilihali maji yanapatikana katika Kijiji chao na walionyesha hali ya kutaka muafaka wa jambo hili ili kuendelea kupata huduma ya maji kama ilivyokuwa hapo awali.

Akiongea katika Mkutano huo baada ya mazungumzo na viongozi wa Kijiji pamoja wananchi Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo alisema katika kutoa huduma ya Maji Vijijini tunaongozwa na Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayotaka kuchangia hudma za maji na sio kununu Maji hivyo kila kaya inawajibu wa kuchangia kiasi kidogo cha Fedha ili kuwezesha huduma hii iendelee kutolewa siku zote.

“Tunafahamu kwamba maji haya yanaanzia kwenye Kijiji hiki na wakazi wa Nkoasenga ndio walinzi wakuu wa mradi huu na wanastahili kupewa upendeleo wapekee katika kutumia maji haya ili wendelee kutunza mradi huu wa Maji, ni wazi kuwa vijiji vya ukanda wa chini haviwezi kupata Maji endapo tu wana Nkoasenga wataharibu mradi huu wa maji mtiririko”, Alisema Mhe. Gambo.

Aliongeza kuwa umuhimu huu wa nyie kuwa Kijiji mama cha mradi huu hauwapi Kinga ya kutokuchangia gharama za maji, hivyo nataka mniambia mnaweza kuchangia kiasi gani kadiri ya uwezo wenu na baada ya makubalino haya mtalipia gharama za maji kwa mwezi na sio kwa mwaka tena kama mlivyokuwa mnafanya hapo awali”.

Awali akizungumza katika Mkutano huo Mhandisi wa Maji Bi. Happy Mrisho alisema “mradi wa maji Makilenga uliibuliwa na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga na baada ya thatmini ya awali ilonekana kuwa mradi ni wa gharama kubwa hivyo usingekidhi vigezo vya kiufadhili kama ungekua mradi wa kijiji kimoja na ili kukidhi vigezo vya kupata fedha toka kwa wafadhili ililazimu kuongeza wanufaika kutoka vijiji 26 na utekelezaji ukaendelea”.

Aliongeza kuwa baada ya mradi kukamilika iliundwa Kamati tendaji ya Makilema ambayo ndiyo inayosimamia mrdai huu na Madiwani na wenyeviti wote wa vijiji waliingia makubaliano ya kuchangia Tsh 10 kwa ndoo lakini baada ya muda mfupi wanakijiji wa Nkoasenga walikiuka makubalino hayo na kudai watalipa Tsh 5000 kwa mwaka na hawewezi kulipa kwa ndoo kwa kuwa maji hayo ni mali ya Kijiji.

Anderson Sikawa ni Diwani wa Kata ya Leburuki kilipo kijiji cha Nkoasenga alisema hawakatai kuchangia huduma za Maji lakini kutokana na hali duni ya wananchi wa eneo hilo hawawezi kulipa kwa ndoo hivyo wanahitaji kufanya mapitio ya gharama za Maji ili kuendana na hali ya wana Nkoasenga ambayo pia itawaongezea ari wakazi hao kulinda mradi huo kwa manufaa ya vijiji vingine pia alitoa tuhuma kwa Bodi ya Makilenga kwa matumizi mabaya ya Fedha za maji.

Katika kutoa mapendekezo ya kiasi stahiki cha kuchangia huduma ya Maji Ndg. Afred Masao ambaye ni mwananchi wa Kijiji cha Nkoasenga aliwakilisha wananchi wote wa Kijiji hicho alisema kuwa wananchi wako tayari kuchangia kwa mwezi lakini uwezo wao ni Tsh 1500 na sio Ths 3000 kama ilivyopendekezwa kwenye vikao vya ndani katika ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Kijiji.

Rc Gambo alihitimisha Mkutano huo kwa kukubaliana na mapendekezo ya wananchi kuwa watalipia Tsh 1500 kwa mwezi kwa wale wanaotumia mabomba ya Kijiji na kwa wale wenye mabomba nyumbani watalipia kadiri ya matumizi yao kwa mwezi na wote watafungiwa Mita za Maji pia aliwaagiza wananchi hao kulipia gharama hizo Halmashauri na sio kwa Kamati ya Maji Makilenga kama awali.

Mradi wa Maji wa Makilenga ulianza mwaka 2011 kwa lengo la kutoa huduma ya Maji na kuhudmia Kata nne na vijiji 27; Ulifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kutoa kiasi cha Tsh Bil 3.7, OIKOS pamoja na nguvu za wananchi. Mradi huu unaendeshwa na Jumuiya ya watumiaji maji ya Makilenga ambayo ina jukumu na mamlaka ya Kisheria kusimamia mradi huu wa maji.

MAJALIWA:TUMETENGA SH. BILIONI 15 ZA MAFUNZO KWA VIJANA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Frederick Msigara wa CCBRT katika hafla ya utoaji tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

……………………….

WAZIRI MKUU Kassim Mjaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 15 kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500 ili kuwajengea uwezo waweze kushiriki kama nguvu kazi kwenye viwanda vinavyotarajiwa kujengwa nchini.

Alitoa kauli hiyo jana usiku (Alhamis, Desemba 8, 2016) kwenye sherehe za utoaji wa tuzo ya muajiri bora wa mwaka 2016, zilizofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Tuzo hizo zimeandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kujielekeza katika kutoa mafunzo kwenye sekta za kipaumbele kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kama kilimo biashara, mafuta, gesi, utalii, usafirishaji, ushonaji na bidhaa za ngozi.

Alisema jitihada zinaendelea kwenye maeneo mengine ili waajiri wawe na wigo mpana wa kuwapata wafanyakazi wenye stadi stahiki kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wao kuwa nguvu kazi yenye ujuzi na umahiri mkubwa kwa lengo la kuongeza tija.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumzia changamoto inayolalamikiwa na waajiri ya uwepo wa tozo mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka tofauti za Serikali kwa huduma ileile kuwa wanaitambua na tayari mchakato wa kuainisha sheria zote zinazoonekana kukwamisha uwekezaji pamoja na mazingira ya biashara nchini.

“Lengo letu ni kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili yaweze kuvutia zaidi na mchakato huu unashughulikiwa na Wizara ya Fedha na Mipango. Tunaomba mvumilie na mshirikiane nasi katika kuendelea kuziainisha sheria zinazokwaza biashara ili tuweze kuzijumuisha kwenye mapitio hayo,” alisema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwashauri waajiri wote nchini waendelee kufanyakazi zao kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima mahala pa kazi. Pia aliwasihi wafanyakazi wote kufanyakazi kwa bidii na uaminifu mkubwa ili waajiri waweze kupata faida, hivyo kuwaboreshea maslahi yao

Alisema “tunaposema Hapa Kazi Tu, tunamaanisha kazi kwenye sekta zote za uzalishaji na utoaji wa huduma bora nchini, iwe sekta ya binafsi au kwenye utumishi wa umma. Nawasihi ndugu zangu Watanzania, wekeni nadhiri kwamba katika mwaka 2017 mtafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuongeza tija na ufanisi mahala pa kazi,”.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama aliwaomba waajiri wawasaidie kuweka msukumo katika juhudi za kutoa mafunzo kwa ajili ya uzoefu na kuongeza ujuzi kwa kutoa nafasi kwa wahitimu kupata uzoefu kwenye maeneo yao ya kazi.

Hata hivyo Mheshimiwa Jenista alisema anatambua umuhimu wa waajiri na wafanyakazi katika utekelezaji wa sera ya maendendeleo ya nchi hasa kwa kuongeza ajira kupitia sekta ya viwanda kwa asilimia 40 kufikia mwaka 2020, mafanikio ya mpango huo yanategemea mchango wa waajiri kutoka sekta binafsi.

Pia aliwapongeza ATE kwa kutambua umuhimu wa kuwekeza katika rasilimali watu hasa kwa kutoa tuzo katika eneo la kuendeleza vipaji, ambapo aliwaomba tuzo ijayo waongeze kigezo cha kumpata mwajiri aliyetumia rasilimali zake kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi wake ambao ndio chanzo cha kuinua tija na ushindani kibiashara.

“Natambua kuwa ATE mnatoa mafunzo katika sheria za kazi na usimamizi wa rasilimali watu ambayo husaidia kupunguza migogoro mahali pa kazi na hivyo kujenga mazingira tulivu maeneo ya kazi. Naomba kutumia wasaa huu kuwakumbusha waajiri kuwawezesha wafanyakazi kwenda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili kuweza kukidhi ushindani katika mazingira ya biashara,” alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka alisema lengo la uaandaji wa tuzo hiyo ni kutambua wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu katika taasisi na makampuni mbalimbali mwanachama hapa nchini.

Alisema kuwa tuzo hizo zinafuata mbinu za Kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali watu katika makampuni ya Kibiashara makubwa na madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi wa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kujituma sehemu za kazi.

Dk. Mlimuka alisema kuwa tuzo hio pia ilijikita zaidi katika kuangalia maeneo muhimu ya rasilimali watu, uongozi, utawala, usimamizi wa Rasilimali watu, kusaidia jamii pamoja na kuwajibika katika jamii, ubora na uzalishaji.

NSSF YASHIRIKI MAONESHO YA VIWANDA VYA TANZANIA

0
0
 Ofisa Mauzo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Fredrick Sawaki (kulia), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Ofisa Mauzo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Fredrick Sawaki (kulia), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sarah Mazengo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sarah Mazengo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu mafao yatolewayo na NSSF kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo wakati wa  maonessho ya Viwanda vya Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika banda la NSSF.
Baadhi ya watu wakipata elimu juu ya NSSF.
Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Sarah Mazengo akitoa elimu juu ya Mafao yatolewayo na NSSF kwa mmoja wa watu waliofika katika banda la NSSF.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo (kushoto), akitoa maelekezo namna ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo.

Zoezi la huduma ya macho lafana mjini Dodoma

0
0
Zoezi la huduma ya macho linaendelea katika Shule ya Darul Muslemeen ambapo mpaka sasa mchana  huu wamejitokeza wananchi 3224. Katika zoezi hili  kila MWananchi Mwenye tatizo  anapatiwa bure miwani,dawa, ushauri. Na mpaka sasa wananchi zaidi ya 100 wameshaanza kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde  amewashukuru sana wananchi wa Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi sana kushiriki katika huduma hii ambayo ni ya bure isiyo na gharama yoyote iliyoratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Taasisi ya Bilal Muslim Mission.  

"Shukran  sana kaka yangu Ridhiwan Kikwete kwa kusaidia kwa nafasi yako jambo hili kufanikiwa...Mungu akubariki sana", amesema  Mhe. Mavunde 
 Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akilaki  wananchi waliofika  kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
 Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia  wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho. Kushoto ni Bw. Ain wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission.
 Wataalamu wa macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission wakihudumia wananchi
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia  wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho. Kushoto ni Bw. Ain wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission.
  Mbune wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akilaki  wananchi waliofika  kupata huduma za bure za macho

SEKTA YA VIWANDA INAHITAJI RASILIMALI WATU – GLOBAL EDUCATION LINK.

0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel ameseama sekta ya viwanda inahitaji rasimali watu hivyo kama wadau wanawajibu wa kuandaa rasilimali ya viwanda yenye tija.

Mollel ameyasema hayo leo katika maonesho ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini, Dar es Salaam, amesema GEL inachokifanya kutafuta fursa ya vyuo vya nje ambavyo vinaandaa wataalam katika sekta ya viwanda.

Amesema sekta ya viwanda haiwezi kusonga mbele kama hakuna rasilimali watu wenye ujuzi wa kuendesha viwanda hivyo. Mollel amesema GEL imeshapeleka wanafunzi katika vyuo vya nje ambao wanasomea uhandisi wa viwanda ambapo ndio rasilimali watu tarajiwa katika sekta ya viwanda nchini.

Aidha amesema kama wadau wanawajibu wakuisaidia nchi katika harakati ya sekta ya viwanda ili nchi iweze kupata uchumi huo. ‘’Hatutakuwa sahihi bila kuonyesha mchango katika taifa hili ya kuandaa rasilimali watu ambao wataleta mageuzi ya viwanda’’ amesema Mollel.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage (wakwanza kushoto) akiwa na Naibu Waziri Uchumi na Biashara wa Ukraine, Nataliya Mykolska (wapili kulia) na Naibu Waziri wa Chakula, Olga Trafimstave (wapili kushoto) akitoa maelezo wa ugeni huo walipotembelea banda la Global Education Link (GEL) katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel. Katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akiwa na Manaibu Waziri wa Ukraine, Nataliya Mykolska wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel wakati walipotembelea banda hilo leo katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akitoa maelezo kwa wanafuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)walipotembelea banda hilo leo katika maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 
 

MAKAMU WA RAIS WA JICA ATEMBELEA KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA ILALA-MCHIKICHINI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto),  akimwelezea jambo Makamu wa Rais wa Shirika la  Serikali ya Japan, linaloshughulikia uratibu wa misada ya maendeleo ya kimataifa, (JICA), Suzuki Noriko,  kuhusu hatua iliyofikiwa na TANESCO katika uboreshaji wa miundombinu ya kupoza na kusambaza umeme alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambapo JICA inashirikana na serikali katika kukiboresha kituo hicho.
Jengo jipya la kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini jijini Dar es Salaam, ambacho JICA imechangia ujenzi wake.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Makamu wa Rais wa Shirika la Serikali ya Japan linaloratibu Misada ya Maendeleo laKimataifa (JICA), Bw. Suzuki Noriko ametembelea kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme cha Ilala-Mchikichini kinachoendeshwa na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Ziara hiyo aliifanya Desemba 9, 2016 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba, alimtembeza kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika uboreshaji miundombinu ya TANESCO ikiwemo jingo na mitambo.
Ziara hiyo inakuja mwezi mmoja tu baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, kuzindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar  es salaam kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo kituo hicho cha Ilala, ni sehemu ya mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye jiji hilo.
JICA na mashirika mengine ya kimataifa yanafadhili mradi huo wa uboreshaji umeme jijini ambapo lengo ni kuwapatia wakazi wa jiji umeme ulio bora na wa uhakika zaidi, ambapo utekelezaji wa mradi huu umehusisha ujenzi wa kituo cha kupoza nguvu za umeme chenye ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV cha City Centre, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmission Line) na kwa kutumia minara (Overhead Line) ya msongo wa wa kilovolti 132 kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha City Centre umbali wa Kilomita 3.4, vile vile ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Line) kutoka kituo cha Makumbusho hadi kituo cha City Centre umbali wa kilomita 6.67.

Mafundi wa TANESCO kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Japan, wakimalizia kazi ya kufunga mitambo kwenye kituo hicho cha Ilala
Mhandisi Mramba akizungumza na mwakilishi wa JICA Tanzania Bi.Toshio Nagase

Mhandisi Mramba, akiongoza ujumbe wa JAICA kutembelea kituo hicho.
 Mhandisi Mramba akimshukuru bi Nagase baada ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
 Wataalamu wa mitambo ya umeme kutoka Japan, wakijadliana




RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukipigwa uwanjani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Vikosi mbalimbali vya Majeshi vikipita mbele ya mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole na Haraka katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Maadhimisho cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikionesha gwaride la kimyakimya mbele ya Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Fatma Karume mara baada ya kumaliza kuhutubia katika uwanja wa Uhuru.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea pamoja na Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya kuwasili. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,BungeKazi,Ajira,Vijana na Wenyeulemavu Jenister Muhagama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwasili  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo


 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
Amiri Jeshi Mkuu  na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati) akitembea kikakamavu  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange baada ya kukagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama  katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa ya tarehe 09 Desemba, 2016 amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara .

Maadhimisho hayo ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa kwa pamoja na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.

Akizungumza na halaiki ya watanzania waliohudhuria sherehe hizo Rais Dkt Magufuli amesema mwaka jana alilazimika kuzuia kufanyika kwa shamrashamra ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara kutimiza miaka 54 kwa kuwa alikuwa na mwezi mmoja tu tangu aingie madarakani na kuitaja sababu ya pili kuwa ni  bajeti kubwa ya shilingi bilioni nne iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya maadhimiso hayo na kuona ni vyema ikaelekezwa katika upanuzi wa barabara ya Alli Hassani Mwinyi yenye urefu wa kilomita 4 ambayo inatumiwa na Watanzania wote badala ya fedha zile kutumiwa na wachache.

"Sherehe za miaka 55 nimeamua zifanyike kwasababu gharama zake ni ndogo sana,kwanza hakuna hata chakula baada ya sherehe hii,hakuna dhifa ya Taifa ,tukimaliza hapa tumemalizana ,lakini pili niliamua sherehe hii niifanye hapa Dar es Salaam kwa kuwa yatakuwa ni maadhimisho ya mwisho kufanyika jijini Dar es salaam na kwamba ni matumaini yake kuwa sherehe za mwaka kesho zitafanyika makao makuu ya nchia mbayo ni Dodoma"

Ameongeza kuwa sherehe za Uhuru ni tukio kubwa sana katika Taifa na hivyo serikali itaendelea kuipa umuhimu siku hiyo na kuiadhimisha.

Rais Dkt Magufuli pia amezitaja changamoto ambazo serikali ya awamu ya tano inazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ufisadi na rushwa ndani ya baadhi ya watendaji na kuongeza kuwa mpaka sasa hivi wafanyakazi hewa wamefikia elfu kumi na tisa huku kaya masikini hewa zinazonufaika na mfuko wa TASAF zikiwa ni elfu 55 na wanafunzi hewa  mpaka sasa hivi wamefikia elfu sitini na tano.

"Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za watanzania na tuataendelea kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa na ufisadi,kwasababu rushwa ni saratani"
Rais Dkt Magufuli amepongeza pia jitihada zilizofanywa na watangulizi wake katika maendeleo ya Tanzania na kuwashukuru kwa niaba ya watanzania huku akiwataka watanzania wote bila ya kujali dini,itikadi za kisiasa  na makabila yao kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili Tanzania iweze kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.

"Hivyo basi tuendelee kuilinda amani yetu na kuwafichua watu wenye nia ovu ya kuhatarisha amani yetu na sambamba na kulinda amani yetu hatuna budi kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ni nguvu na silaha yetu kubwa kama Taifa,lakini pia tuendelee kuulinda muungano wetu ambao ni silaha kubwa ya umoja wetu ili Tanzania tuendelee kwenda mbele"

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhudhuria na kuhutubia katika sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara tangu aingie madarakani.


Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam
09 Desemba, 2016.

 



 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 10, 2016

0
0























WATANZANIA 12 WANASHIKILIWA NCHINI MSUMBIJI

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru JUMA HOMERA akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wakitembea pembezoni mwa mto ruvuma ambao katika kijiji cha wenje  ambapo mto huo unatenganisha Tanzania na Nchi ya Msumbiji.

"Watanzania  ambao wanashikiliwa nchini MSUMBIJI ni wakazi wa kijiji cha Mkapunda na wenje wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ambapo vijiji hivyo vipo mpakani na kijiji cha Luimila cha wilaya ya Niassa nchini Msumbiji, Vijiji hivyo vya Tanzania na Msumbiji vinatenganishwa na Mto Ruvuma. Kwa undani wa habari hii angalia video yake hapo chini ".


Ridhiwani Kikwete aendelea na Ziara Jimboni kwake Chalinze

0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara yake ya kushtukiza katika Jimbo lake kukaguwa miradi ya kimaendeo, Desemba 9 amezunguka katika Zahanati na Shule za Secondary Chalize pamoja na mradi wa ufugaji kuku katika Kata ya Msoga ili kuona utendaji kazi pamoja na miradi ambayo inafanyika pia kuzichukua changamoto zilizopo na kuangalia jinsi ya kuzitatua.
Mh Mbunge Ridhiwani alitembelea katika Hospital ya Msoga ambayo ilijengwa na Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kupitia Ofisi ya Mbunge walitoa vifaa tiba katika Hospital hiyo ikiwamo X-RAY machine, Ado sound Mashine, Vitanda 70,Bed cover, Vitanda zaidi ya 70, mashine za dawa za usingizi zaidi ya tano, mafriji ya kuifadhia damu matatu, kiti kwa ajili ya tiba ya meno na vifaa vingine vingi.

Hospital ya Msoga inatarajiwa kuwa ya wilaya baada ya kukamilisha baadhi ya vitu ikiwemo samani, inaupungufu wa mabenchi ya kukalia wagonjwa 150, viti 150, Meza 40, na Mashelfu ya kuifadhia dawa pamoja na AC katika chumba hicho kwa ajili ya kuifadhia dawa, Ukosefu wa kichomea taka hatarishi pamoja na Mochwari Lakini pia kuna changamoto ya umaliziaji wa chumba cha kuifadhia digital x-ray machine ambayo ni kubwa iliyotolewa na Mh Mbunge
Baadhi ya Dawa kaaika Chumba cha kuifadhia Dawa Hospital ya Msoga
 
Kiti cha matibabu ya meno mbacho kilitilewa na Ofisi ya Mbunge katika Hospital ya Msoga
Mh Mbunge akitoa maelekezo kwa team aliyoongozananayo katika ziara yake ya kushtukiza kukaguwa miradi ya kimaendeo
Mh Mbunge pamoja team yake na madaktari wa hospital ya Msoga wakiangalia shimo la utupaji taka hatarishi katika hospital hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kukaguwa miradi ya kimaendeleo katika Jimbo lake.
Mh Mbunge na madaktari na wafanya kazi wa hospital ya Msoga katika picha ya pamoja badaa ya kukaguwa mirada ya kimaendeleo na utekelezaji wa miradi hiyo katika hospital ya Msoga.
Mh Mbunge akisaini kitabu cha wageni baada ya kuingia katika Shule ya secondary Lugoba akiwa katika ziara ya kushtukiza kukaguwa miradi ya kimaendeo
Mh Mbunge akizungumza jambo na mwalimu mkuu wa Shule ya secondary Lugoba Abdalla Sakasa
 
Mh Mbunge akitoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondary Lugoba Abdallah Sakasa, pamoja na Team yake aliyoongozana nayo alipokuwa akikaguwa nyumba za walimu ambazo zilijengwa chini ya Ofisi ya Mbunge katika ziara yake ya kushtukiza kukaguwa miradi ya kimaendeo
Matank ya Maji kwa matumizi ya Shule pamoja na walimu katika Shule ya Secondary Lugoba.
 
Chumba cha Darasa la Kompyuta katika Shule ya Sekondary Lugoba
 
Mh Mbunge Ridhiwani akiangalia Kiti cha matibabu ya Meno katika Dispensary ya shell ya Secondary Lugoba.
Mh Mbunge akiwa katika eneo ambalo litajengwa tank kubwa la maji litakalo sambaza maji mji mzima wa chalize kutokea Ruvu.
Uchimbaji na Uwekaji maboba ya maji kutokea Ruvu kuja Chalinze ukiendelea.
 
Mh Mbunge akisalimiana na moja ya ijinia alipotembelea eneo la ujenzi wa Kiwanda cha uchakataji matunda
Mh Mbunge akiwa anapewa maelekezo baada kutembelea eneo la ujenzi wa Kiwanda cha uchakataji matunda
   
Nyumba za walimu zikiwa zimemalizika katika Shule ya Secondary Merento
Vyumba vya Madarasa vilivyojengwa chini ya ofisi ya mbunge katika shule ya secondary Morento.
Nyumba za walimu zilivyojengwa chini ya ofisi ya mbunge katikakatika Shule ya Secondary Morento.
Nyumba za walimu zilizopo katika hatua za mwisho za ujenzi katika Shule ya Secondary Morento.
Mh Mbunge akitoa maelekezo kea team yake katika Nyumba za walimu zilizopo kwenye hatua za mwisho za ujenzi katika shule ya Secondary Morento.
Bweni la wasicha lilounguwa kwa moto katika shule ya secondary Morento
Mh Mbunge akipokea taarifa ya mradi wa ufugaji kuku katika Kata ya Msoga
Mh Mbunge akipokea kuku wa kitoweo baada ya kumaliza kukaguwa mradi kuku katika Kata ya Msoga.

MASAUNI AZINDUA MASHINDANO NAGE MAPINDUZI CUP ZANZIBAR, ACHANGIA VICOBA JIMBONI KWAKE

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Unguja. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili ya Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi huyo katika Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiyapokea Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba-Together (hawapo pichani) kabla ya kuzindua kikundi hicho katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kushoto ni Katibu wa Vicoba Together, Mwashum Mohammed Mustafa. Kulia ni Katibu wa Jimbo la Kikwajuni, Kassim Ally Juma.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizikagua timu ya Kikwajuni na Baa kutoka Jimbo la Mtoni kabla ya kuanza Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Mchezaji wa Timu ya Kikwajuni, mjini Unguja, Zanzibar akijaza chupa mchanga wakati wa Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni alizindua Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama  wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba Together. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu. Picha zote na Felix Mwagara

JARIDA LA WIZARA YA HABARI TOLEO LA DESEMBA, 2016.

0
0

JARIDA LA NCHI YETU, MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA

0
0

VIONGOZI WA DUNIA WAPITISHA AZIMIO LA PARIS KATIKA MKUTANO WA OGP

0
0
Na Hassan Silayo-Paris Ufaransa.

Serikali themanini na mamia ya mashirika ya kiraia kutoka duniani kote yamesaini hatua ya pamoja katika Azimio la Paris, ikiwa ni pamoja na mambo kadhaa juu ya kupambana na rushwa.
Hii inakuja mwishoni mwa siku 3 katika mkutano wa nne wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi(OGP) uliofanyika Jijini Paris Nchini Ufaransa ambayo ulishuhudia  uzinduzi wa mageuzi mapya ya uendeshaji wa serikali kwa uwazi kwa wanachama 15 waliokatika mpango wa majaribio  wa OGP ikiwa ni pamoja na Manispaa ya Kigoma kutoka Tanzania.


Azimio la Paris ni pamoja na kumi na tisa vitendo pamoja, ambapo serikali na mashirika ya kiraia kukubaliana kufanya kazi pamoja kufikia matokeo yanayoonekana pato-oriented. Hatua ya pamoja ni pamoja na: Uwazi na mikataba ya wazi katika sekta ya maliasili, Uwazi juu ya ushawishi, kuondoa matumizi mabaya ya makampuni hewa, utekelezaji wa upatikanaji wa sheria ya habari, msisitizo wa Mapinduzi ya takwimu  kwa maendeleo endelevu na mabadiliko ya Hali ya Hewa, utekelezaji wa kanuni za mwongozo kwa ajili ya sera ya takwimu za wazi ;na kuongeza mwitikio wa huduma za umma.

Sanjay Pradhan, Mkurugenzi Mtendaji wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi, kuweka hatua kwa tukio la siku tatu kwa kuwakumbusha washiriki wa mazingira ya sasa kijiografia na kisiasa. "Harakati Open Government haijawahi kuwa chini ya tishio na bado kazi yetu haijawa muhimu sana kwa ajili ya dunia, hivyo tunahitaji wanaharakati wa mashirika ya kiraia, waandishi wa habari, wabunge, sekta binafsi kuongeza nguvu na kuungana il kupata ujasiri wa pamoja wa kupambana na maslahi. "

Akizungumza mwishoni mwa Mkutano huo Mratibu wa mpango wa kuendesha shuguli za serikali kwa uwazi Kigoma Ujiji Mhandisi Sultani Ndoliwa amesema wamejifunza mambo mengi ambayo yatasaidia manispaa kukuza maendeleo kwa raia na kusaidia kukabiliana na changamoto ya na kuzitatua  kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Hussein Ruhava Meya wa Kigoma Ujiji Manispaa ameshauri manispaa nyingine nchini Tanzania kuwa na tabia ya kusikilizag juu ya nini wananchi wanataka kwani itasaidia kujua ni nini wananchi wanataka na mwisho wa siku itasaidia kupunguza malamiko juu ya huduma duni za umma katika Sekta mbalimbali.

Anne Hidalgo, Meya wa Paris, akiwakaribisha viongozi kutoka maeneo yaliyo katika mpango wa majaribio wa OGP  alisema, "kukutana kwa serikali za mitaa,miji Jijini Paris ndiko ni tukio la kihistoria kwamba inaonyesha jinsi lazima ushiriki miji ni katika kukabiliana na changamoto za karne yetu." Serikali na asasi za kiraia viongozi kutoka Austin, Marekani; Bojonegoro, Indonesia; Buenos Aires, Argentina; Elgeyo Marakwet, Kenya; Jalisco, Mexico; Kigoma, Tanzania; La Libertad, Peru; Madrid, Hispania; Ontario, Canada; Paris, Ufaransa; Sao Paulo, Brazil,Scotland, Uingereza; Sekondi-Takoradi, Ghana; Seoul, Korea Kusini na Tbilisi, Georgia walihudhuria tukio.
Mameya kutoka mpango wa majaribio wa OGP  katika picha ya pamoja baada kumalizika kwa kikao hicho.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images