Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

PROF. MAGHEMBE - MOUNT KILIMANJARO CAN ONLY BE CLIMBED FROM ITS HOME, TANZANIA

0
0


MHE. KAIRUKI NA BALOZI WA JAPANI NCHINI WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA JAPANI

0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalam wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini katika sekta mbalimbali.
Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japani hususan suala la wataalamu wa kujitolea wanaokuja kufanya kazi nchini. Kushoto kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Japani nchini, Bi. Yoko Kamiyana.

MKUTANO WA BARAZA KUU LA 24 LA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA WAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza wakati alipokuwa akiufunga mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Fortunatus Kapinga na kushoto ni Kaimu Meneja Biashara wa shirika, Janeth Msofe. Kwa sasa Profesa Kamuzora amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.
Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana. 

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufunga jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Fortunatus Kapinga, kushoto ni Meneja rasilimali wetu wa shirika, William Makumba na wapili kushoto ni Kaimu Meneja Biashara wa shirika, Janeth Msofe. 
Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.  

Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.  
Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.  

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliani (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufunga jijini Dar es Salaam jana. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana. 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufunga jijini Dar es Salaam jana. Katiakti ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Fortunatus Kapinga na kulia ni Meneja Mkuu rasilimali za shirika, James Sando.
Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.  

Juu na chini: Ni baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, walipo kuwa wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana.  

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufunga jijini Dar es Salaam jana. 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufunga jijini Dar es Salaam jana. 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akipongezwa na Meneja rasilimali wetu wa Shirika la Posta, William Makumba mara baada ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo, wakati alipoufunga jijini Dar es Salaam jana. 
Katibu wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Meneja wa Posta Mkoa wa Iringa, Emmanuel Lugomera, akizungumza wakati wa kufungwa kwa mkutano huo wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo, jijini Dar es Salaam jana. 
Mjumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, kutoka Pemba, Zanzibar, Mussa Bilal, akitoa neno la shukurani kwa Katibu Mkuu, Profesa Kamuzora. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano huo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, wakati akizungumza nao, jijini Dar es Salaam jana. 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora (katikati mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya kuufunga jijini Dar es Salaam jana. 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujnzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akiagana na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania mara baada ya kuufunga jijini Dar es Salaam jana. Kwa sasa Profesa Kamuzora amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kufungwa Mkutano wa 24 wa baraza hilo, na Katibu Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora, ambaye sasa amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais.

DKT. MPANGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA

0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumzia umuhimu wa Nishati ya umeme katika kuchochea maendeleo ya viwanda nchini, wakati alipokutana na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Noriko Suzuki (kulia), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo Pichani), alipomtembelea na kufanya mazungumzo naye Ofisini kwake Jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwakilishi Mkuu Mkazi wa JICA nchini Tanzania, Bw. Toshio Nagase na kulia ni Afisa wa Shirika hilo anayeshughulikia masuala ya usafiri na usafirishaji Bi. Lilian Masalu.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akizungumzia namna Serikali ya Tanzania ilivyojipanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo ujenzi wa viwanda mbele ya Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki (hayupo pichani), alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria Bw. Elias Kalist, na kulia kwake ni Mchumi Mkuu, Yosephe Tamamu, wote kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
 Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Yosephe Tamamu (kushoto), akifafanua jambo katika kikao kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki. Aliyekaa kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo Bw. Elias Kalist.
 Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, akizungumza katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Japan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimsindikiza mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, baada ya kufanya mazungumzo namna pande hizo mbili zitakavyoimarisha ushirikiano uliodumu muda mrefu katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Bi. Noriko Suzuki, kabla ya kuondoka baada ya kufanya mazungumzo namna pande hizo mbili zitakavyoimarisha ushirikiano uliodumu muda mrefu  katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kulia ni Mwakilishi Mkuu mkazi wa JICA hapa nchini, Toshio Nagase. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-WFM)

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Noriko Suzuki, amesema kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii ili iweze kufikia malengo yake ya kuondokana na umasikini.

Suzuki ametoa ahadi hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ofisini Kwake Jijini Dar salaam.
Makamu huyo wa Rais wa JICA, amesema kuwa nchi yake inatumia zaidi ya dola za Marekani Milioni mia moja kila mwaka kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini katika sekta za miundombinu ya barabara, maji, nishati, afya na kilimo.

Miongoni mwa miradi mikubwa inayofadhiliwa na serikali hiyo ya Japan ni barabara ya juu ya mzunguko inayojengwa katika makutano ya barabara katika eneo la Tazara, Jijini Dar es salaam.
 “Tuko tayari kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza Mpango wake wa Pili wa Taifa wa Maendeleo kwa kuwekeza fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo mliyoipa kipaumbele kuiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025” alisisitiza Makamu huyo wa Rais wa JICA.

Ameahidi kuwa Shirika lake pia linaagalia uwezekano wa kuishirikisha sekta binafsi nchini Japan kujenga barabara  katika eneo la  Gerezani ili kupunguza msongamano mkubwa wa magari hasa yanayotoka Bandari ya Dar es salaam na Katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa uhusiano kati ya Japan na Tanzania ni wa muda mrefu na kwamba nchi hiyo imekuwa mdau wake mkubwa wa maendeleo.

Amesema katika mazungumzo kati yake na Makamu huyo wa Rais wa JICA, wamekubaliana kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara eneo la Bendera tatu na Gerezani ili kupunguza msongamano wa magari kutoka katikati ya Jiji la Dar es salaam
“Mradi Mwingine ni ujenzi wa barabara kutoka eneo la Moroco hadi Mwenge, Jijini Dar es salaam, ambayo Japan waliahidi  kuijenga muda mrefu uliopita” Aliongeza Dkt. Mpango

Amesema kuwa wamekubaliana pia kwamba Shirika hilo lisaidie kufungua ukanda wa Kati kwa kujenga barabara ya Kigoma-Nyakanazi na Kigoma-Mto Malagarasi, ambazo  hazijapata mfadhili mpaka sasa.

“Halikadhalika nimemwomba atusaidie kuhamasisha sekta binafsi nchini Japan kuja Tanzania kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho serikali inatumia kuagiza dawa nje ya nchi na pia itakuwa chanzo cha ajira kwa vijana” alisisitiza Dkt. Mpango

Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametaja eneo lingine kuwa ni kuiomba Japan iongeze fursa ya mafunzo kwa vijana wa kitanzania katika nyanja za tiba na ujuzi maalumu ambao haufundishwi hapa nchini.

Amesema kuwa ameiomba pia nchi hiyo ya Japan iendelee kusaidia sekta ya kilimo  inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania kwa kusaidia kuongeza uzalishaji na kusindika mazao ya wakulima ili kuyaongezea thamani.

Katika majadiliano hayo, Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Noriko Suzuki, aliiomba Serikali ya Tanzania itoe msamaha wa kodi kwa miradi miwili mikubwa inayotekelezwa na wakandarasi mbalimbali kupitia shirika hilo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Bagamoyo na mradi wa maji mkoani Tabora, maombi ambayo amesema Serikali itayafanyiakazi.

WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NCHINI RWANDA, FRANCOIS KANIMBA ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

0
0
Waziri wa Biashara, Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akizungumza na waandishi habari mara baada ya kutembelea bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtembeza Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba katika bandari ya Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akipata maelezo ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akitembelea bandari ya Dar es Salaam ikiwa sehemu ya mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya biashara kati ya Tanzania na Rwanda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

TAMASHA LA SIFA ZA YERIKO ARUSHA

0
0
Miaka 25 ijayo, Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii inamaanisha nguvukazi kubwa itakuwa mikononi mwao. 

Lakini kama watasalia kuwa idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa kwa ukuaji wa nchi.Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye makusanyiko ya kijamii mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa nguvu. 

Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.

Uwepo wa Tamasha la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto kwenye jamii.Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono Foundation.

Tamasha la Sifa za Yeriko msimu wa kwanza inatarajiwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2016 Jijini Arusha kwenye Kanisa la New Life City Church (Kwa Egon) lililoko Kwa Iddi, na kisha kufuatiwa na Tamasha la pili litakalofanyika tarehe 11 Disemba Kanisa la Tanzania Assemblies of God CCC Upanga Jijini Dar es Salaam ikiwa ni weekend hii. Tamasha hili litahusishwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania, ambapo ugeni kutoka Afrika Kusini utakuwepo. Wageni hawa ni Mercy Manqele, KgotsoMakgalema na Sipokazi Nxumalo.Baadhi ya waimbaji wa ndani ni kama vile, Abednego na The Worshippers, Toddlers International, Yusuphu Nahashon, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,Wengine ni Machalii wa Yesu, The Cahogoz, Voice of Joy, Lilian Kimola, na Bomby Johnson.

LENGO
Lengo la awali nikukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zitatumika
kutafuta eneo la kituo kwa jijini Dar es Salaam na Arusha, pamoja na matengenezo iwapo itanunuliwa nyumba na kuibadilisha kuendana na maono ya jinsi kituo tunavyotaka kiwe kukidhi mambo mbalimbali yatakayokuwa yakipatikana kituoni, kama kujifunza muziki, uimbaji, ushauri nasaha, na utafutaji wa shule za kukuza vipaji ndani na nje ya nchi.ambayo tunatarajia yatawezesha kupatikana kwa kiasi hiki ni kupitia barua za mwaliko kwa watumishi mbalimbali wa dini na taasisi, pamoja na kiingilio kitakachopatikana kupitia matamasha yote mawili.

GHARAMA
Ili lengo la kukusanya milioni 200 kutimia, gharama mbalimbali kutoka kwa waanzilishi na marafiki zimefanikisha katika kuwakaribisha waimbaji hawa kutoka Afrika Kusini, kulipia mahala watakapofikia, matangazo, usafiri wa ndani, chakula, vyombo, muziki na gharama nyinginezo. Hili litasaidia katika ukusanyaji wa kiasi kilichosalia kwa awamu tofauti tofauti. Tunaamini katika ushirikiano katika kutatua matatizo yaliyomo kwenye jamii yetu

Katika Kufanikisha na maono ya kupata fedha katika Tamasha hilo kwa Dar es salaam na Arusha kutakuwa na Kiingilio katika Matamsha hayo,Arusha ni Ijumaa hii Dec 9 pale kwa Egon Wakubwa 5000 VIP 20000 Dar es salaam ni Jumapili hii Dec 11 pale CCC Upanga Opp Chuo cha Mzumbe Watoto 5000 Wakubwa 10000 VIP 30000

Tunategemea support yenu wadau wa vyombo vya habari Bloggers kwa kwa ajili ya kusaidia kutangaza Tamasha hili linalofanyika lengo na maono tuliyo nayo mbele yetu Arusha na Dar es salam kwa wikendi hii.

MFUMUKO WA BEI WAONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 4.5 MWEZI OCTOBA MPAKA ASILIMIA 4.8 MWEZI NOVEMBA

0
0
 kurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epharaim Kwesigabo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu, kulia kwake ni Mtakwimu Bw. Muhidini Mtindo.
Wanahabari wakimsikilizaMkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Epharaim Kwesigabo (hayupo pichani) wakati akielezea hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Novemba mwaka huu. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).

MSD WAASWA KUBORESHA UPATIKANAJI DAWA NCHINI

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kushoto), akihutubia wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na viongozi wao katika mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa kwenye
mkutano huo.



Na Dotto Mwaibale

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya amewaasa watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua Baraza la tatu la Wafanyakazi la Bohari ya Dawa (MSD) ambapo pia amesisitiza kuwa Baraza hilo libuni mbinu na mikakati mbadala za kuboresha utendaji bila kusahau kutii miiko ya utumishi wa umma.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MSD, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amemweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuwa tayari MSD imeanza kununua dawa na vifaa tiba kutoka kwa wazalishaji, ambapo hadi sasa wanawazalishaji 20 ambao wanamikataba, na wazabuni wengine 76 wadawana 79 wa vifaa tiba zabuni zao zinaandaliwa.

Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makao Makuu ya MSD na Kanda zote nane za MSD ambao ni pamoja na Mwenyeviti wa Tughe na matawi pamoja wawakilishi wa wafanyakazi.

SKAUTI WA TANZANIA WAZURU KENYA

0
0
 Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed  Waziri (Kushoto) akisalimiana na Maskauti kutoka Tanzania.

Skauti 27 kutoka shule mbili za msingi za Dar es Salaam wako nchini Kenya kwa ziara ya wiki moja kwa mwaliko wa Chama cha Maskauti cha Kenya.
Watoto hao kutoka shule za msingi za Canossa na Libermann, na maofisa wa Chama cha Maskauti Tanzania waliowasindikiza, Kamishina Anthony Joachim na Kamishina Saidi Debwani, leo wametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na kusalimiana na Kaimu Balozi, Bi.Talha Mohamed Waziri.

Maskauti hao walimwambia Kaimu Balozi kuwa wametembelea maeneo mbalimbali ya Kenya na kujifunza mambo mengi.Kamishina Joachim amesema watoto hao wanatarajiwa kurejea nyumbani kesho.
Maskauti kutoka Tanzania na viongozi wao katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed  Waziri.

BALOZI WA CUBA AMUAGA WAZIRI MWAKYEMBE

0
0
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpatia kadi ya mawasiliano Mgeni wake Balozi wa Cuba Mhe. Jorge Luis Lopez alipofika ofisini kwake leo (8/12/2016) kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
 Balozi wa Cuba Mhe. Jorge Luis Lopez akiandika ujumbe wa kumuaga Waziri  wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwenye kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri huyo alipofika kwa ajili ya kumuaga.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akibadilishana mawazo na Mgeni wake Balozi wa Cuba Mhe. Jorge Luis Lopez  alipofika ofisini kwake leo (8/12/2016) kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

DK MEDARD KALEMANI AFANYA ZIARA MIKOA YA RUVUMA, NJOMBE, IRINGA NA MOROGORO KUKAGUA MIRADI YA UMEME

0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini (REA II na REA III), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.
 Diwani wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Matokeo Kenedi (kushoto), akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme kwa wananchi wa Kata yake, wakati wa ziara ya Naibu Waziri kukagua miradi ya umeme wilayani humo hivi karibuni. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy.
 Nehemia Magendege kutoka Kijiji cha Ng’uruhe, Kata ya Pomerini wilayani Kilolo, akitoa maoni yake kuhusu utekelezwaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA II na REA III) kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto), akiwasilisha taarifa ya Mkoa wake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia-mwenye miwani). Naibu Waziri na Ujumbe wake walifika Ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa hivi karibuni, kabla ya kuanza ziara mkoani humo kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mugoyi Adam (wa pili kutoka kulia), akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya (hawapo pichani), wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Dk Medard Kalemani (kulia) wilayani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.
Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Dk Edmund Mjengwa (kushoto), akimueleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme katika Kituo hicho. Naibu Waziri ameelekeza Kituo hicho kiwe cha kwanza wilayani humo, kuunganishiwa umeme katika Mradi wa REA III.


TGNP YATOA MAFUNZO KWA MAOFISA WA POLISI DAWATI LA JINSIA NA WATOTO KISHAPU

0
0
 Maofisa wa Polisi wanaoshughulikia Dawati Jinsia na Watoto Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakifuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambayo yamefanyika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
 Mwezeshaji wa mafunzo ambaye ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, John Simtowe akitoa mada katika mafunzo hayo kwa maofisa wa Polisi wilayani humo ambayo yameratibiwa na TGNP.
 Mafunzo yanaendelea kwa maofisa wa Polisi wanaoshughulikia Dawati Jinsia na Watoto Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwezeshaji, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, John Simtowe wakati akitoa mada.
Mkaguzi wa Polisi Dawati la Jinsia na Watoto Makao Makuu ambaye pia ni mwalimu wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia, Mohamed Mcheu akichangia katika mafunzo hayo kwa maofisa wa Polisi.

Naibu Waziri wa Ardhi ANGELINA MABULA akagua Mpaka wa TANZANIA na ZAMBIA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua eneo linalotenganisha mpaka (buffer zone) kati ya Tanzania na Zambia katika eneo la Tunduma, Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bw. Juma Said Irando.
Naibu Waziri waArdhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akifuatilia ramani inayoonesha alama za mipaka ya kimataifa kati ya Tanzania na Zambia wakati alipotembelea eneo la Tunduma mwishoni mwa juma, Kushoto ni alama moja wapo ya jiwe lililojengwa na Serikali ya Tanzania baada ya makubaliano baina ya nchi mbili hizo.
Naibu Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akiifuatilia alama moja wapo ya jiwe la mipaka ya kimataifa kati ya Tanzania na Zambia wakati alipotembelea eneo la Tunduma.
Naibu Waziri waArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wakazi wa eneo la mpakani la Tunduma mara baada ya kusikiliza kero zao kuhusu huduma za sekta ya ardhi.

MPANGO WA SAUTI ZA WANANCHI UNASAIDIA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI-AIDAN EYAKUZE

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza Bw.Aidan Eyakuze akishiriki katika kikao alipowasilisha juu ya Mapango wa Sauti za Wananchi unaotekelezwa na Taasisi hiyo, ambapo alisema kwa kiasi kikubwa mpango huo umesaidia kuinua maisha ya watanzania hasa kwenye maeneo ya Sekta ya Afya na Mawasiliano.Wakati wa Vikao vya Mkutano wa Nne wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi(OGP) Nchini Ufaransa, Kushoto ni Mshiriki wa Mkutano huo Bw. Badru Rajabu.
 Wajumbe wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza Bw.Aidan Eyakuze alipokuwa akiwasilisha juu ya Mapango wa Sauti za Wananchi unaotekelezwa na Taasisi hiyo, Wakati wa Vikao vya Mkutano wa Nne wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi(OGP) Nchini Ufaransa
Wajumbe wa Mkutano huo kutoka Mataifa Mbalimbali wakichangia mada mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza Bw.Aidan Eyakuze kuwasilisha taarifa juu ya Mapango wa Sauti za Wananchi ambao alieleza jinsi wanavyowasaidia wananchi kuwa na mchango katika utungaji wa Sera na kutathmini mipango ya serikali zao. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO PARIS

MWAMUZI JONASIA AZAWADIWA GARI

0
0
Wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye hivi karibuni alichezesha vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika nchini Cameroon.
Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini miaka miwili iliyopita, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka, alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.
Umahiri wake, umevutia wengi wakiwamo wadau wa mpira wa miguu ambao hawakupenda kutajwa walioamua kumzawadia gari aina Toyota Vits ikiwa ni zawadi na kumbukumbu yake baada ya kuiwakilisha vema nchi.
Kwa upande wa TFF ilimtuza Mwamuzi Jonesia cheti cha kutambua uwezo na kufikia hatua ya kulitangaza shirikisho  na nchi kwa ujumla. Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ndiye aliyemkabidhi funguo za gari Jonasia.
Rais Malinzi alimsifu Jonesia kwa ujasiri na hatua aliyofikia na kumpa baraka za kumtakia mafanikio zaidi ya hapo ya kusonga mbele baada ya kufanya vema kwenye michuano ya Afrika Mashariki ya wanawake (CECAFA challange) na hiyo ya Wanawake Afrika.
“Ni Mtihani mkubwa to officiate (kuchezesha) mechi kubwa kama hiyo. Maana kila kosa linaweza kukuondoa na mafanikio ya kupata medali ya dhahabu kati ya waamuzi wanne ni hatua kubwa inayopaswa kutuzwa. Siwasemi FIFA, lakini itoshe kusema kuwa Jonasia unaweza kufika hatua ya kuchezesha fainali za kombe la dunia,” alisema Malinzi.
Rais Malinzi alipigia upatu kwa waamuzi wanaume nao kuandaliwa vema na kuchezesha michezo mikubwa ikiwamo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwani kinachohitajika ni mikakati tu na kuitekeleza.
“Kamati ya waamuzi nawaachia kazi hii. Maana kazi kubwa ya uamuzi ni kusoma na mazoezi,” alisema Malinzi mbele ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Waamuzi akiwamo Mwenyekiti wake, Saloum Chama.
Jonesia ambaye wakati wote alikuwa na faraja, alimshukuru Mungu kwa mafanikio aliyofikia pia wadau wote wakiwamo wazazi wake na bibi yake aliyemlea baada ya kufariki mama yake mzazi na viongozi mbalimbali ambao aliwaelezea kumtia moyo.

THE ARRIVAL OF SILVER CLOUD CRUISE SHIP IN DARE ES SALAAM PORT

0
0

 The Marketing Officer of Tanzania Tourist Board, Mr. Hoza Mbura (right) shows a Dar-es-salaam city tourist map to visiting tourists.
The tourist’s cruise ship from USA with more than 100 tourists has arrived and dock in Dar es salaam Port today early in the morning. Upon their arrival the tourists were met officials from Tanzania Tourist Board who among other things supplied them with some tourism information materials including brochures, Dvds Cds, and tourist maps as well as briefing them about destination Tanzania.
 Looking for information on the Tanzania tourist’s travel map
While in Dar, the tourists were expected to have a day city tour to explore Dar es Salaam tourist attractions such as National Museum, Beaches, Kivukoni fish market and Mwenge curio shops.
Tourist standing outside the cruise ship waiting for the bus to take them for the city tour
  A Tourist reads Tanzania tourist map while waiting for the shuttle 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 9, 2016

0
0



































GLOBAL EDUCATION LINK WAISAIDIA SERIKALI KUZALISHA RASILIMALI WATU WENYE UJUZI.

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Taasisi ya Global Education Link imeisaidia Serikali kuzalisha rasilimali watu wenye ujuzi na elimu ya kutosha ili watumike katika kuinua viwanda na uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Abdulmaliki Mollel alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya viwanda Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo jijini humo.

Mollel amesema kuwa Tanzania imeamua kuwa nchi ya viwanda lakini bila kuwa na rasilimali watu wenye ujuzi na elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji na uendelezaji wa viwanda hakutakuwa na maendeleo kwani maendeleo yoyote mzizi wake ni elimu na ujuzi.

“Kuna  baadhi ya masomo ambayo ni muhimu hayapatikani katika vyuo vya Tanzania na kama zinapatikana basi nafasi ni chache hivyo,taasisi hii ni kama daraja la kutengeneza rasilimali watu wenye ubora watakaoleta maendeleo ya nchi kupitia kusoma nchi za nje,”alisema Mollel.

Ameongeza kuwa ili nchi ipate maendeleo kwa haraka ni lazima isaidiwe na taasisi na mashirika binafsi na ndio maana taasisi hiyo imeamua kuisaidia Serikali kwa kuwarahisishia Watanzania kupata elimu nje ya nchi ambayo itasaidia Serikali kupunguza matumizi pamoja na kuzuia wataalamu wa nchi za nje kufanya kazi nchini.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa mpaka sasa chuo hicho kimeshatoa wanafunzi takribani 5400 ambao wengi wao wameshika nyazfa mbalimbali kwenye taasisi za Umma na Binafsi.

Aidha, taasisi hiyo ina mpango wa kuandaa programu za miezi 4 hadi 6 ambazo zitakuwa maalum kwa ajili ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi  kwa kupitia elimu ya vitendo kwenye viwanda mbalimbali vilivyoko nchini India.

Taasisi hiyo imeanzishwa mnamo mwaka 2006 ikiwa na lengo la kurahisisha mchakato na kuwaondolea usumbufu wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi pamoja na kuwasaidia wanafunzi kutimiza ndoto zao.

Wananchi Wilayani Handeni watakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia huduma bora za jamii.

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe, wakisalimia wananchi wa Kata ya Segera
 Mhe. Godwin Gondwe  akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera Iliyopo Halamshauri ya Wilaya ya Handeni kwenye maadhimisho hayo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  BW. William Makufwe akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima akizungumza na wananchi wa Kata ya Segera kwenye maadhimisho.
Mhe Diwani wa kata ya Segera Bw. Yassin Mtamike akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Segera.

 Mkuu wa Wilaya akimpa kipaza sauti moja ya wananchi waliokua wakitoa kero za 
 Baadhi ya Maafisa wa TAKUKURU, Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya. 


 Mkuu wa Wilaya akimuuliza jambo Mkuu wa TAKUKURU wilaya Bi. Esta MUlima juu ya utekelezaji wa maagizo yake

Baadhi ya wananchi wa kata ya Segera .

Mmoja ya wananchi waliokua wakitoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya 





Wananchi Wilayani Handeni wametakiwa kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kujihahakikishia huduma bora za jamii.
  
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akisikiliza kero za wananchi wa Kata ya Segera iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya  siku ya Maadili na Haki za Binanadamu Kiwilaya yaliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU). 

Gondwe alisema “ Maadli ni imani njema, sehemu yoyote yenye maadili haki za binadamu hufuatwa, hakuna ardhi itakayouzwa kiholela, wagonjwa watatibiwa vizuri kwenye vituo vya afya, wageni wataingia kwenye maeneo yetu kwa kufuata taratibu za nchi na shughuli zote zitafanyika kwa misingi ya Haki”.

Aidha aliwataka watumishi wa umma na wananci kwa ujumla kufuata sheria, taratibu na kanuni pasipo kujali wala kubagua rangi au cheo cha mtu yeyote. Alisema kuwa Rushwa ni adui wa haki  na kuwataka kuikataa kwa kauli na vitendo.

Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Handeni alivunja baraza la Ardhi la Kata kwa kulalamikiwa na wananchi kutotekeleza maajukumu yeke na kuwaagiza TAKUKURU Wilaya ya Handeni kulichunguza hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari 2017, na mapungufu yoyote yatakayobainika basi hatua za kisheria  zichukue mkondo wake maramoja.

Vilevile aliwaaagiza  Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa kwenye msitu wa hifadhi ya kijiji

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe aliwataka Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kusimamia miradi yote ya maendeleo kwa  maadili na uadilifu kutokana na dhamana kubwa waliyonayo kwenye maeneo yao ya kiutawala. Vilevile aliwataka  kusoma tarifa za mapato na matumizi na kuwa tayari kujibu hoja za wananchi kuhusu taarifa za mapato na matumizi. “Mtendaji atakayeshindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi atakua amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake” Alisema Makufwe.

Mkuu wa TAKUKURU Wilaya Bi. Esta Mulima, alisema TAKUKURU itaendelea kupambana na Rushwa kikamilifu na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa. Aliwataka wananchi kufichua vitendo vya rushwa vinapotokea au dalili za vitendo hivyo ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu hufanyika kila tarehe 10 Disemba Kitaifa, na Wilayani hapa yalifanyika tarehe 8 Disemba  kutokana na Muingiliano wa Majukumu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.

kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na Mapambano dhidi ya Rushwa”.

Alda  Sadango
Afisa habari 
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
9 Desemba 2016.

Shirika la Ndege la Uturuki laanzisha safari za Zanzibar

0
0
Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani  Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar

Shirika la Ndege la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba 13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.

Shirika hilo maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote, zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.

Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244 ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo. Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.

Safari ya kwanza itazinduliwa Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.

Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST) zitakuwa tatu kwa wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo::
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images