Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

Wateja 15,345 wafaidika na Mradi wa Umeme wa KIA

$
0
0
 Naibu Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akikagua Chumba cha kuongozea Mitambo ya Umeme kwenye Kituo cha kupoozea  Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.  Kulia ni Mhandisi Neema Rushema, Mhandisi Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
 Naibu Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akikagua Mitambo ya Umeme kwenye Kituo cha kupoozea Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.  Kushoto Mhandisi Neema Rushema, Mhandisi Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi ya mitambo ya Umeme katika Kituo cha Kupoozea Umeme cha KIA.

Na Teresia Mhagama
Imeelezwa kuwa zaidi ya wateja wa awali 15,345 wameunganishwa na huduma ya umeme baada ya kukamilika kwa mradi wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kituo hicho.

Dkt. Pallangyo alisema kuwa, mradi huo ulihusisha ujenzi wa Transfoma mbili zenye uwezo wa Megawati 20 kila moja (2x20MVA) pamoja na jengo la kuendeshea mitambo ambapo Kituo kinasambaza umeme kwa wateja kupitia njia 6 za msongo wa kilovoti 33.

“Niseme tu kuwa, mradi huu ni muhimu sana kwani kukamilika kwake kumeboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Wilaya ya Hai, migodi ya Mirerani na maeneo mengine ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha,” alisema Dkt. Pallangyo.

Aliongeza kuwa Kukamilika kwa kituo hicho kumeimarisha pia upatikanaji wa umeme katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Alisema kuwa, utekelezaji wa Mradi huo ulianza rasmi tarehe 22 Machi, 2010 na gharama za mradi ni Shilingi bilioni 15.3 sawa na Dola za Marekani milioni 7.08.

Mradi huo wa KIA umetekelezwa kupitia Mradi wa TEDAP ulio chini ya Wizara ya Nishati na Madini ambao unahusika na uboreshaji wa njia za usafirishaji, usambazaji na ujenzi wa vituo vya umeme katika Mikoa ya Dar es salaam, Arusha na Kilimanjaro. 

Mradi wa TEDAP unahusisha Ujenzi wa njia za kusafirishia umeme wa msongo wa kilovolti 132, ujenzi wa vituo vitano vya kupozea umeme jijini Dar es salaam pamoja na Kituo cha kupozea Umeme cha KIA.

Mradi pia unahusisha ujenzi wa vituo vipya 19 vya kusambaza umeme wa msongo wa kilovolti 33 pamoja na njia za usambazaji umeme kwa urefu wa kilomita 102.497 za msongo wa kilovolti 33 na kilomita 34.018 za msongo wa kilovolti 11 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro.

DKT SHEIN AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA TUNGUU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Kumi na nne yaliyofanyika Chuoni hapo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe ya mahafali ya kumi na nne (14) katika Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, (kulia) Prof.Saleh Idriss Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo na (kushoto) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi kutoka wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal wakati wa sherehe ya Mahfali ya kumi na nne iliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya wahitimu katika Mahafali ya kumi na nne (14) ya Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) wakiwa katika sherehe za Kutunukiwa Vyeti,Diploma,Stashahada,na Shahada na nyenginezo zilizofanyika leo katika viwanja vya Chuo hicho Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani).
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof.Suleiman Bin- Nassry Basahal alipokuwa alipokuwa akiwatunuku Stashahad na Shada wahitimu katika fani mbali mbali wa mwaka 2016 wakati wa sherehe ya Mahafali ya kumi na nne yaliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za mahafali ya kumi na nne katika Chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja yaliyofanyika leo, mgeni rasmi akiwa Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, pia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Prof. Suleiman Bin- Nassry Basahal (kulia) baada ya kumalizika kwa sherehe ya Mahafali ya kumi na nne yaliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,wengine (kushoto)Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt. Adissa Muslim Hija na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi mbalimbali na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu ,wakati wa sherehe ya Mahafali ya kumi na nne yaliyofanyika leo katika Chuo hicho huko Tunguu (Zanzibar University) Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo. (Picha na Ikulu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKITAZAMA GARI LILILOJENGEWA BODI LA MBAO

$
0
0
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama gari aina ya Toyota iloyojengewa bodi la mbao wakati alipotembelea kiwanda cha Fibreboars 2000 Limited cha Arusha akiwa katika ziara ya kazi mkoani humo Desemba 5, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WATANZANIA WATAKIWA KUUNGANA ILI KUWEKEZA KATIKA VIWANDA.

$
0
0
Na: Frank Shija – MAELEZO

WATANZANIA watakiwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika Kukuza Uchumi kwa kujiunga pamoja na kuanzisha Viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusu maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania.

Akizungumzia kauli mbiu ya maadhimisho hayo amesema kuwa inasadifu kile ambacho Serikali imedhamiria kukifanya matharani suala zima la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kitu ambacho kimeanza kutekelezwa.

“Watanzania wanapaswa kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutekeleza uanzishwaji wa Viwanda vidogo vidogo na vya kati kwani kufanya hivyo kutapunguza ama kuondoa kabisa tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Bi. Zainab.

Aliongeza watanzania wanapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kuijenga Tanzania ya Viwanda ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani na kuongeza fursa ya ajira kwani viwanda ni eneo linalotoa ajira nyingi kwa wakati mmoja.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amempongeza Rais Magufuli kwa hatua kadha alizokwishachukua katika kuhakikisha anaweka mazingira rafiki kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda akitolea mfano wa hatua ya Kampuni ya Bakhresa kupewa eneo la ekari elfu kumi kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kusindika matunda.

Desemba 9 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Dar es salaam na kauli ya mwaka huu ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuhimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu.”

WABUNIFU WA BIDHAA ZA KILIMO WAKUTANISHWA NA TASISI ZA FEDHA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Jumla ya Vikundi 16 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini vinavyojihusisha na masuala ya kilimo vimekutanishwa na Tasisi za kifedha na mabenki ili kuwezeshwa kama mpango wa taasisi ya Land O Lakes.

Akizungumza na Globu ja Jamii,Mshauri wa biashara bunifu kutoka tasisi hiyo ,Renalda Lema amesema kuwa katika vikundi hivyo 16 wamewakilishwa na watu wawili wawili,ili kuwasilisha ubunifu wao kwa taasisi hizo na kupata fursa ya kupanua biashara yao.

“Kama ambavyo unaweza kuona wabunifu walivyotengeza mashine mbalimbali, ambazo zitaweza kumuondoa mkulima kutoka sehemu moja hadi nyingine, hasa katika serikali hii ambayo inahamasisha uchumi wa viwanda, hivyo sisi tumeona uchumi wa viwanda hauwezi kufanikiwa bila ya kuanza kuwawezesha wakulima katika hatua ya awali kabisa” amesema Renalda.

Ametoa wito kwa wadau na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kuwawezesha wakulima hao kwa namna moja ama nyingine,kuwasiliana na taasisi ya Land O’ Lakes kuwakutanisha na wakulima hao.
Mkurugenzi wa tasisi ya fedha ya Brac, Mahufuzii Ashrafu , akizungumza na baadhi ya wabunifu waliokutanishwa na kampuni hiyo ili waweze kuwezeshwa kama mpango wa tasisi ya Land O Lakes ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
Mbunifu wa mashine ya kukamua matunda kutoka mkoa wa Songwe, Yohana Mwanzyunga(wa kwanza kulia) akiwaonyesha washiriki wengine mtambo wa kukamua matunda.
Baadhi ya washiriki wakiangalia mashine ya kupukucha halizeti

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo tarehe 07 Desemba Ikulu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU

NEWS ALERT:Rais Dkt Magufuli afanya mabadiliko ya Makatibu wakuu, Naibu Katibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;


Dkt. Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.


Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.


Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.


Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. Dkt. Maria Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.


Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.


Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.


Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.Bw. Christopher Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.


Dkt. Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina. 


Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

07 Desemba, 2016

MGODI UNAOTEMBEA; Nina hamu ya kuiona CCM ya Dr Magufuli

$
0
0



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

NAAM! Macho na masikio ya wengi katika nchi yetu kwa sasa ni namna gani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaingia kwenye mabadiliko makubwa kutokana na aina ya utendaji wa Mwenyekiti wake, Dr John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dr John Pombe Magufuli, pichani.

Dr Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anajulikana kama kiongozi asiyependa ujinga na mtumbua majipu, aliyerithi mikoba ya Uenyekiti wa CCM Taifa kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.

Dr Kikwete alikuwa mwenyekiti wa CCM Taifa huku akitawaliwa na huruma, tabasamu kiasi cha watendaji wake kutumia mwanya huo kuwa wala rushwa, wachumia tumbo na ‘majipu’ yanayostahili kutumbuliwa bila ganzi. Ndio ni majipu. Tena majipu makubwa kuliko hata yale ya watendaji wa serikali, ukizingatia kuwa kushamiri kwao wengi wao wamezalishwa na kuchochewa na mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi wa CCM kwa miaka ya hivi karibuni.
Dr Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CCM.
Hakuna asiyefahamu majipu hayo. Hata alipokuwa anahutubia wajumbe mjini Dodoma wakati anakabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa, Dr Magufuli alilizungumzia kwa kina, akionyeshwa kukerwa na aina watendaji na mfumo wa chama chake. Mwenyekiti huyo alifahamu kati ya matatizo mengi ya kupata viongozi wasiokuwa wasafi, wala rushwa, wasiokuwa na uchungu na Taifa lao, baadhi yao wanatokea kwenye chama chake.

Naye ni muathirika mkubwa baada ya kupata wakati mgumu katika mchakato wa kuomba wadhamini alipochukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama cheke kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia CCM, huku baadhi ya makada wake wakituhumiwa kumwaga fedha kama njugu ili kuongeza ushawishi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama katika vijiji, kata, wilaya na mikoa mbalimbali ya nchi yetu.


Licha ya ukongwe wake, CCM ilianza kupoteza sifa na imani kwa wananchi wengi wa mijini huku wa vijijini nao wakianza kuangalia uwezekano wa kuongozwa na wapinzani. Wakaiona CCM ni chama cha mafisadi, wala rushwa na watoa rushwa.


Viongozi wakaanza kupatikana kwa ukwasi wa fedha. Nafasi zote za uongozi ndani ya CCM na zile za ubunge na udiwani ziliuzwa kwa fedha nyingi. Walalahoi wachache walipita. Tena kwa kufanya kazi ya ziada ama kulazimika kuwa kwenye mtandao wa wenye nazo. Kuweka mamilioni ya fedha ili kuongeza ushawishi wa kupata madaraka ndani ya CCM kilikuwa mazoea. Na kila mtu alijua hilo. Mgombea anaulizwa, “Mzee unatuachaje”?

Wakati huu tunapoelekea kwenye matazamio ya kuundwa upya kwa chama cha CCM, nashawishika kusema Dr Magufuli ana kazi kubwa ndani ya chama chake. Wengi wanaomzunguuka hawastahili kuachwa waendelee kuwapo ndani ya nafasi zao, haswa makatibu wa wilaya, mikoa na watendaji wengine ndani ya chama hiki.

Wengi wao waligeuka kuwa madalali wa wataka uongozi ndani ya CCM. Kamwe hawaangalii sifa yoyote isipokuwa fedha, urafiki, undugu na ujirani kama karata ya kupata viongozi wao. Hata wale waliokuwa chaguo halisi la wananchi, hawapewi nafasi na walijikuta wakikanyagwa wakati wote. Hawakuwa na haki yoyote ndani ya chama chao. Viongozi wao wa chama ngazi ya wilaya na mikoa walicheza kamari mchana kweupe.

Mtindo huo na mingineyo iliiweka CCM katika wakati mgumu kwenye chaguzi mbalimbali nchini kwetu. Na utafiti usiokuwa rasmi ulionyesha kati ya wagombea wengi walioangushwa katika majimbo au kata, ni wale waliopitishwa kwa hila bila kuwa chaguo halisi la wengi.


Wagombea wa nafasi za ubunge ama udiwani wakabaki kuwa chaguo la kikundi kidogo cha watu, wanapitishwa bila kuangalia mtaji wao kwa wapiga kura mitaani. Hili linakatisha tamaa. Matokeo yake watu wanapiga kura za chuki dhidi ya chama tawala. CCM kinaonekana ni chama cha wachache. Aliyetaka kugombea nafasi yoyote kwanza angeangaliwa fedha zake. Angeulizwa juu ya mtaji wake kifedha alionao.

Na kama hana fedha, jua angeonekana si lolote katika siasa za chama kwa wakati huu. Ni tofauti na CCM ya wazee wetu, akina Julius Kambarage Nyerere na wenzake. Wao waliijenga CCM ya Watanzania wote, wengine wameifanya ya wachache wenye nazo. CCM kilikuwa chama cha walalahoi. Wote walijivunia nacho bila kujali dini zao, ukabila wao na maeneo watokayo.

Inashangaza kuona umeundwa mfumo mbovu wa nafasi za uongozi ndani ya chama hiki kikongwe. Viongozi hawajui wajibu wao. Si Katibu wa wilaya, mwenyekiti wala MNEC anayefahamu wajibu wa kusimamia sheria, taratibu wala maadili ya uongozi. Kazi yao ikabakia kuwa wapambe wa wabunge katika maeneo yao. Hakuna jingine walilojua zaidi ya hilo. Kama walisema juu ya utendaji mbovu wa Mkurugenzi wa Halmashauri, basi mtendaji huyo atakuwa hayupo kwenye mtandao wa mbunge wake.

Mfumo huu ulichelewesha maendeleo. Wakageuka Bendera, wapambe ama makatibu wa wabunge majimboni mwao. Wataalamu kama walimu, afya na wengineo nao wakalazimika kutii matakwa ya wabunge hao, wakielekezwa kufanya hata yale yasiyokuwa na tija katika nafasi zao kwa mujibu wa sheria.

Wasiofanya hivyo wakanyanyasika na wengineo kujikuta wanahamishwa kwingine bila sababu za msingi. Viongozi wa chama wilaya na mikoa hawajui wajibu wao wala ufahamu wa kusimamia watendaji wa serikali kama chama tawala.


Wakajikuta wao ndio wanasimamiwa na wengine. Hakuna hata anayeweza kuinua mdomo wake kumkemea mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri ama Meya. Watawezaje wakati walinunuliwa katika mchakato wa kura za maoni? Uwezo wa kusema wautoe wapi? Ndio CCM ilivyokuwa kabla ya Dr Magufuli kupewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti Taifa. Sasa ana kazi ya kuitoa CCM katika mikono ya wajanja na kuileta panapostahili. Kuirudisha CCM kutoka kwa walioiendesha kwa mbinu za kimtandao.

Vipi hii ya Magufuli? Ataiweza? Atawaweza wajanja hawa? Katika kuangalia kama ataweza au atashindwa ni budi kwa wanachama wote kuhakikisha kwamba mwenyekiti wao anaweza. Na kwanini ashindwe? Kazi anayoifanya kurudisha nidhamu serikalini ni ishara kuwa uwezo huo anao. Aungwe mkono. Kila mwanachama wa CCM atimize wajibu wake, awe mlinzi kwa mwenzake.

Mwana CCM asikubali kununuliwa wala asinunue mwenzake. Atakayeonekana anahonga ili achaguliwe katu hastahili kuachwa badala yake amulikwe na awajibishwe. Kitendo cha kununua uongozi kinachelewesha maendeleo. Watu hawafanyi kazi kwa moyo badala yake wanawaza kurudisha fedha walizotumia kwenye chaguzi zao.

Watoa rushwa waone sasa mwisho wao umefika. Mwisho wa kuondosha makapi na kuleta watu wanaokubalika kwa sifa zao umewadia. Wana CCM wasioneane haya. Waambiane ukweli na ikiwezekana watumbuane.

Hii itawezekana kama watakubali kubadilika. Isiwe CCM ya wajanja tena ila iwe ya walalahoi na Watanzania kwa ujumla. Mapambano haya yaanzie kwenye uchaguzi wa nafasi za ndani kuanzia shina, tawi, kata, wilaya na Taifa mwaka 2017.


Asitokee wa kupitishwa kwa ghiliba. Ili jambo hili lifanikiwe, Dr Magufuli na safu yake ya juu ya CCM anapaswa kuwahamisha kama sio kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa chama ngazi ya wilaya na mikoa ili aisuke upya kwa kuwa wao ndio tatizo kubwa. Hawa wakiachwa kwenye nafasi zao haswa Makatibu wa Wilaya na Mikoa watamuangusha Mwenyekiti. Hii ni kwa sababu wengi hawajui wajibu wao. Wanalalamikiwa kila kona ya nchi yetu.

Ni wachache waliofanya kazi zao kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa. Ikiwa Dr Magufuli ataanza kuisuka CCM huku akiwabakiza kwenye nafasi zao niliowataja hapo juu ni wazi atachelewa kutimiza malengo ya kuisuka upya. Afanye uchunguzi wa kina. Watendaji mizigo watimuliwe. Wateuliwe wengine watakaokubali kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa na kutoa haki kwa watu wote.

Lazima lifanywe jambo nyeti na lenye tija kwa mustakabali wan chi yetu kama njia ya kukifanya kiendelee kuheshimika kwa miaka 50 ijayo.Sisemi kama wenyeviti waliopita ukiwamo uongozi wa Dr Jakaya Mrisho Kikwete haukufaa. Kikwete alifanya mengi ya msingi, hata hivyo mkazo na mabadiliko zaidi yanahitajika.


Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa mgumu. Isingekuwa juhudi za ziada, huenda mambo yangekuwa mabaya kwa chama hiki. Pia tulishuhudia jinsi Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Abdulrahaman Kinana na timu yake walivyohangaika kufanya mikutano katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kujua kero na kusimamia watendaji wa juu wa serikali, hususan mawaziri.


Ziara za Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi ambaye ni Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni wa serikali ya Awamu ya Tano, Mheshimiwa Nape Nnauye zilizaa matunda. Huu si wakati wa kuchekea ujinga unaokihujumu chama. Utakiangamiza. Kila mtu atimize wajibu wake. Viongozi na watendaji wa chama waifanye kazi yao wakati wote na si kusubiri Uchaguzi Mkuu kama njia za kusaka pesa kutoka kwa wagombea.

Watendaji, Makatibu na Wenyeviti wacheza kamari wakati wa kura za maoni hawahitajiki tena. Waondoshwe. Kwa mfano, wapo Makatibu wa CCM na wana mtandao wenzao wanaomba rushwa kutoka kwa wagombea ili watoe ushindi ama nafasi nzuri ya kura. Nazungumzia nafasi ya kwanza hadi ya tano, ambayo kiuhalisia makada watatu wanaofikishwa Kamati Kuu mmoja wapo anaweza kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM.

Hayo na mengine mengi yaliwafanya makada wafanye kila wawezalo kuhonga wasimamizi wa uchaguzi wa chama katika majimbo, kila mtu akitaka nafasi za juu. Ni jambo la kusikitisha. Na hapo ndipo linapotokea swali la akiba ya fedha kutoka kwa mgombea husika. Mtoto wa mkulima, mlalahoi hata akubalike vipi jimboni kwao ni ngumu kupenya.

Hivyo kuibuka kwa Dr Magufuli na kuapa kuisuka upya CCM, aghalabu matumaini mapya yametokea. Matumaini ambayo wapo wasiyotaka, wakiamini ule ufalme wao unatoweka. Hata hivyo ifikie wakati tuseme imetosha. Chama kisukwe upya na wale wasiostahili washughulikiwe haraka kama walivyoshughulikiwa watendaji wa serikali.

Endapo kwenye CCM hakutakuwa na majipu, hata dhamira ya kuwa na watendaji wenye kujali maslahi ya Watanzania kwenye serikali itafanikiwa kwa vitendo. Hakutakuwa na njia za panya tena. Viongozi wababaishaji, wala rushwa, mafisadi na wasaka tonge watatoweka na kuifanya nchi iwe kwenye mstari mzuri wa kimaendeleo.

Si tu uongozi ndani ya CCM ulinunuliwa na wataka madaraka na kuuzwa na makatibu wa wilaya na mikoa, bali pia watu hao walishindwa kusimamia rasilimali za chama katika maeneo mengi hapa nchini. Kila kona ni ujanja ujanja tu. Mikataba isiyokuwa rafiki na isiyokuwa na tija kwa chama iliingiwa kila siku.


Wakaifanya CCM ya maslahi yao. Wakazichapa kadi feki za CCM ili mabwana wakubwa wao washinde. Kama hiyo haitoshi, wakapeleka mihutasari na ripoti feki ili kuaminisha ushindi huo. Mwisho wa uchafu huo ni kukataa kwa Watanzania juu ya wanaopitishwa katika kata na majimbo husika. Na ndio maana idadi ya viti vya udiwani na ubunge kwa upande wa upinzani inaongezeka maradufu nchini.

Nani wa kusema? Ni dhahiri wamedhamilia kukiangamiza chama hiki kikongwe hapa nchini. Hivyo anapotokea Dr Magufuli na kuamua kwa dhati kurudisha misingi na dira ya chama hiki, kwanini asiungwe mkono?

Ndio maana nasema nina hamu ya kuiona CCM ya Dr Magufuli. Mtu pekee atakayerudisha heshima ya CCM mitaani. Mabadiliko makubwa atakayofanya yataleta imani kwa Watanzania wote, mijini na vijijini.


Kwa bahati nzuri hakuna wakati mzuri wa kuisuka upya CCM kama mwaka ujao wa 2017, ambao chama kitafanya chaguzi zake katika ngazi zote, jumuiya zote. Hata hivyo narudia tena, mabadiliko hayo na dhamira ya kusukwa upya kwa chama hiki yaanzie katika kuwabadilisha ama kuwafukuza kazi watendaji wabovu, waliofanya kazi kwa matakwa yao binafsi haswa makatibu wa wilaya, makatibu wa mikoa na makatibu wa jumuiya za chama ili kuhakikisha kwamba CCM inazaliwa upya na inakuwa katika misingi ya kuongoza nchi kama chama tawala. Chama kikongwe chenye historia murua kwa Taifa letu.


Naamini Dr Magufuli na safu yake uwezo huo wanao. Kilichobaki ni kuombewa na kupewa ushirikiano kwa wanachama wote bila kuangalia vyeo vyao, majina yao, fedha zao na mengineyo.


+255 712053949


JARIDA LA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) - ONLINE EDITION

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete afanya Mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia

$
0
0
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) juzi tarehe 6 Desemba, 2016, amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Haile Mariam Desale alipomtembelea ofisini kwake jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi Waziri Mkuu wa Ethiopia Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanaopata elimu iliyo bora na kwa kiwango kinachofanana dunia nzima.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea.

Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufikida pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo.

Rais Mstaafu ameiomba Ethiopia kujiunga na Mpango huo ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia ameelezea nia ya nchi yake kujiunga na Mpango huo. Ethiopia ni moja kati ya nchi za Afrika ambayo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa fursa ya elimu kwa watoto na vijana wake. Pamoja na mafanikio makubwa bado zipo changamoto zinazohitaji hatua madhubuti ili kufikia lengo la kizazi cha elimu ifikapo 2040.

Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda na Malawi na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkabidhi Ripoti ya Kamisheni ya Elimu Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desale jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia.
Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mheshimiwa Haile Mariam Desale, Waziri Mkuu wa Ethiopia jijini Addis Ababa.

RAIS WA UFARANSA AFUNGUA MKUTANO WA 4 WA OGP,MKURUGENZI TWAWEZA AELEZA MUELEKEO

$
0
0
 Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande akihutubia washiriki katika ufunguzi wa mkutano wa 4 wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP) katika ukumbi wa Salle Pleyel, ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwataka washiriki kuja na matokeo ya hatua zilizochukuliwa katika kushirikisha wananchi kwenye masuala ya maendeleo.
Washiriki wakimsikiliza Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande
 Rais wa Ufaransa Bw. François Hollande akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza Bw.Aidan Eyakuze (kulia) akishiriki katika majadiliano wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 4 wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP) katika ukumbi wa Salle Pleyel,ambapo walijadili masuala mbalimbali ya Serikali kwa uwazi nakueleza mtazamo wake juu muelekeo wa mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi(OGP).

UDART KUENDELEA KUTOA HUDUMA BOARA USAFIRI KWA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
Abiria wakiwa katika Kituo cha mabasi yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Afisa Mawasiliano wa Udart, Deus Buganywa akizungumza na waandishi habari hawapo pichani juu ya utoaji huduma ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam, leo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Kampuni ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam (UDART) imesema kuwa itaendelea kutoa huduma bora ya usafiri kadri ya uwezo wao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mawasiliano wa Udart , Deus Buganywa amesema nia ya kampuni ni kuona wananchi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma usafiri ulio bora.

Deus amesema kampuni imekuwa ikipokea maoni mbalimbali ya wananchi na kuweza kufanyia kazi katika masuala ua utoaji huduma ya usafiri.

Amesema abiria ni kiungo kikubwa kwao katika kuwasafirisha kutoka sehemu moja na kwenda nyingine bila usumbufu huku mifumo mingine ikiendeleaa kuimarishwa ukiwemo wa matumizi ya kadi.

Aidha amesema wanafunzi sasa wamekuwa na usafiri wa uhakika pasipo kupata unyanyasaji wowote ambao unaweza kufanya achukie shule kutokana na adha ya usafiri.

Amesema mabasi yaliyopo na mahitaji ya abiria hayatoshi wataendelea kuongeza ili wananchi kuwa na uhakika wa safari zao na kuweza kuleta maendeleo ya nchi.

Mtanzania achaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari

$
0
0
Mtanzania Felistas Joseph, amechaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari (International Conference on Great Lakes Region –ICGLR).

Bibi Felistas amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo katika uchaguzi uliofanyika mjini Pointre Noire, nchini Congo Desemba Mosi mwaka 2016. Kamati iliyoundwa chini ya Itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari inajumuisha wajumbe 12 kutoka nchi wanachama wa ICGLR  ambapo wajumbe hao huidhinishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR (Regional Inter-Ministerial Council- RIMC).

Bibi Felistas ni Mkurugenzi  Msaidizi  katika Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria na amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari tangu ilipoundwa mwezi Februari mwaka 2012.

Katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanda, Bibi Felistas atasaidiwa na Makamu Mwenyekiti kutoka nchini Burundi, Katibu kutoka DRC ambao kwa pamoja wanatarajiwa kuthibitishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR  katika kikao chao kitakachofanyika wiki mbili  zijazo nchini Kenya.

AIDAN EYAKUZE-TWAWEZA EXECUTIVE DIRECTOR A TANZANIAN OF OGP PARIS 4 SUMMIT DISCUSSIONS

MASAUNI AWAPA HAMASA WACHEZAJI TIMU YA MIEMBENI, YAPAMBANA NA TAIFA JANG’OMBE LIGI KUU ZANZIBAR, ZATOKA SARE UWANJA WA AMANI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wachezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu, Miembeni Club kabla ya timu hiyo kupambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika Uwanja wa Amani, Zanzibar. Masauni aliwaambia wachezaji wa Timu hiyo inayotoka katika Jimbo lake, wajitume na wahakikishe ushinde unapatikana. Hata hivyo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja.Picha na MOHA.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiingia ndani ya Uwanja wa Amani, Zanzibar kwa ajili ya kushuhudia timu hiyo inayotoka katika Jimbo la Masauni, ikipambana na Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu visiwani humo.Picha na MOHA.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwa na Katibu wa Timu ya Miembeni, Simai Mwalimu wakiangalia wachezaji wa Timu ya Miembeni (hawapo pichani) ilipokuwa inafanya mashambulizi dhidi ya Timu ya Taifa Jang’ombe katika mzunguko wa Ligi Kuu ya Zanzibar zinazofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja. Picha na MOHA.
Mchezaji wa Timu ya Miembeni akipiga mpira kichwa akimtoka mpinzani wake wa Timu ya Taifa Jang’ombe katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Amani na Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana goli moja kwa moja. Picha na MOHA
Mashabiki wa Timu ya Miembeni wakishangilia wakati timu yao ilipokuwa imeifunga goli moja, Timu ya Taifa Jang’ombe, katika mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, Zanzibar.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) alihudhuria timu hizo zikipambana katika mzunguko wa Liki Kuu visiwani humo.Picha na MOHA.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu inayocheza Ligi Kuu, Miembeni Club pamoja na viongozi wao kabla ya timu hiyo kuanza kucheza na Timu ya Taifa Jang’ombe. Timu hiyo inatoka katika Jimbo la Masauni, ambapo aliwasili uwanjani hapo kwa lengo la kuwahamasisha wachezaji hao watoke na ushindi. Picha zote na MOHA.

UWEPO ZA SHERIA ZA HABARI NA SHERIA ZA HAKI YA KUPATA TAARIFA HUSAIDIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA- BI. ALINA MUNGIU

$
0
0
Mtafiti katika masuala ya habari Bi. Alina Mungiu (wakwanza kulia)akijibu maswali wakati wa kikao cha Asasi za Kiraia katika mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alieleza jinsi uwepo za sheria za habari na sheria za haki ya kupata taarifa zinavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa.
Mkurugenzi wa Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia Bw. Paul Maasen akiongea na washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alisema serikali kutoa huduma kwa uwazi kutasaidia kuondoa vitendo vya rushwa na uwazi.
Washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia Bw. Paul Maasen
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa wakishiriki katika majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusiana na mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi
Mtafiti katika masuala ya habari Bi. Alina Mungiu akitoa mada kuhusu namna asasi za kiraia na ukuaji wa teknolojia unaweza kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO-PARIS (UFARANSA)

RC Gambo kukabidhi Pikipiki 200 – Jumamosi.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waendesha boda boda 200(hawapo pichani) watakaopatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba wakati wa kikao na vijana hao kukamilisha taratibu na masuala ya usalama kabla ya kukabidhiwa Pikipiki hizo.
Kijana muendesha boda boda(aliyesimama) akichangia kuhusiana na kiasi gani cha Fedha kirejeshwe kwa siku ili kukamilisha mkopo wa Pikipiki watakazopewa. Kwa wakati.
Umoja wa waendesha bodaboda Jiji la Arusha (UBOJA) wakiwa katika Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkubwa akitoa maelezo ya mafunzo ya udereva yatakayotolewa bure kwa vijana hao kuanzia tarehe 08/12/2016 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
 
Nteghenjwa Hosseah, Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.

Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.

Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.

Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.

Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.

Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.

Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:

Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki

Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo

Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.

Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKE WA MWANZILISHI WA TAIFA LA SUDAN KUSINI REBECCA NYANDENG DE MABIOR ILIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

ZINGATIENI MAADILI NA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU: NAPE

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Wizara  katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka akitoa hoja za wafanyakazi katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akipokea hotuba ya wafanyakazi kutoka kwa Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi Magreth Mtaka katika kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Baadhi ya wawakilishi wa watumishi wa  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Taasisi zake wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara yake mara baada ya kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM


Na Raymond Mushumbusi -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.

“Nawataka watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano  tutarudisha maadili ya Utumishi wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe Nnauye.

Mhe. Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.

Alieleza kuwa endapo kuna mtumishi yoyote atakayeshindwa kusimamia suala zima la maadili anapoteza utumishi wake.

“ Wananchi ndiyo tunaowatumikia na ndiyo wanaotufanya tuwepo hapa tulipo wanahitaji huduma bora. Kama hatutazingatia suala la maadili ni hakika hatutaweza kuwatumikia vema” alieleza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo , Prof Elisante Ole Gabriel ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa  kuhakikisha watumishi wanazingatia maadili na suala hili linafanyika kwa vitendo zaidi na sio maneno ili kuendelea kuunga mkono jitihada za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli za kurudisha maadili katika Utumishi wa Umma.

“Mhe. Waziri nakuahidi mimi pamoja na watendaji wenzangu tutalisimamia suala hili na kulitekeleza kwa vitendo ili turudishe heshima ya utumishi wa Umma kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kurudisha uaminifu kwa wananchi”alisema Prof Gabriel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka amesema kuwa ni jambo muhimu kwa watumishi kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao katiKa eneo la kazi.

“Niwashauri watumishi wenzangu tuzingatie maadili ya Utumishi wa Umma ili turudishe heshima ya utumishi wa umma na tutoe huduma iliyo bora kwa wananchi” alisema Bibi Magreth.

PROFESA MBARAWA ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa kawanza kulia), kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini inayotekelezwa na shirika hilo. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa kawanza kulia), walipokutana jjijini Dar es salaam leo. Kushoto kwa Makamu wa Rais wa JICA ni Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania Bw. Toshio Nagase.
Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa walipokutana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Bi Suzuki Noriko (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wao mara baada ya kujadili mikakati ya kuboresha miundombinu nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images