Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE,DEC 6

0
0


MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TBN WAFUNGULIWA DAR, SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII

0
0


Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar


SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Blogs) kuwa chombo rasmi cha habari nchini. Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas,  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka na Mafunzo ya Tanzania Bloggers Network (TBN), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana Jumatatu.


"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema  Dkt. Abbas.


Dkt. Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.


Katika hatua nyingine Dkt. Abbas alisema Blogs hazina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weledi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.

Dkt. Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana  asubuhi. 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam jana asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

 Mkurugenzi Mkuu wa mtandao wa Jamii Forums Bw. Maxence Melo akitoa moja ya somo katika mafunzo hayo.


 Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

UTT-AMIS YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI KITAIFA NA HAKI ZA BINADAMU

0
0
Ofisa Masoko Mwandamizi wa UTT-AMIS, Martha Mashiku akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harisson Mwakyembe (kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki.
Ofisa Mafunzo wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhan akishuhudia mwananchi aliyehudhulia Maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa UTT.
Maofisa Mafunzo wa UTT-AMIS, Waziri Ramadhan na Pauline Kasilati wakitoa elimu juu ya Mfuko wa Uwekezaji wa UTT-AMIS wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Uwekezaji wa UTT.

Makomandoo Kupamba Sherehe za Maadhimisho Miaka 55 ya Uhuru.

0
0
 Na: Frank Shija – MAELEZO.

 
MAKOMANDOO wa Jeshi la Ulinzi wanatarajiwa kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo wwatacheza  gwaride  la kimyakimya.
 
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa  leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Jenista amesema kuwa  mbali na maonyesho hayo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya Bendi ya Muziki wa kizazi kipya na Kizazi cha zamani, ngoma za asili za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.

Waziri Mhagama ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha ametoa  wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Uhuru siku hiyo ya tarehe 9 Desemba ili kusjumuika na Watanzania wote katika kuadhimisha sherehe hizo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu” 

Airtel yaungana na Umoja Switch kutoa huduma za kifedha kupitia simu

0
0

Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce akitoa pesa katika mashine za ATM za UMOJA SWITCH mara baada ya kufanya muamala wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi
Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi wakipongezana mara baada ya kuzindua ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa katika kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima.
Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce akitoa pesa kwenye ATM katika mashine za ATM za UMOJA SWITCH mara baada ya kufanya muamala wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi.
 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeshirikiana na UMOJA SWITCH ATMS katika kuwawezesha wateja wake wa Airtel Money kufurahia huduma za kifedha na kutoa pesa kwenye mashine za ATM za UMOJA SWITCH nchi nzima bila kuwa na kadi ya ATM

Ushirikiano huu mpya utasaidia kurahisisha huduma za kifedha kwa watanzania na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa ufanisi zaidi, wateja wa Airtel sasa wanaweza kupata huduma za kifedha wakati wowote masaa 24 siku 7 za wiki kupitia mashine za UMOJA SWITCH ATMs zilizoendea nchi nzima

ushirikiano huu pia utasaidia katika kutanua wigo wa mawakala wa Airtel Money ambapo wateja wa Airtel hawatakuwa na haja ya kufungua akaunti ya benki wala kuwa na ya kadi ya ATM ili kupata huduma hii, kwa kupitia mashine za UMOJA SWITCH ATMs mteja ataweza kufanya muamala kutoka kwenye simu yake ya mkononi na maramoja kutoa pesa zake kwenye mashine ya ATM kwa gharama nafuu. Kiwango kidogo kitatozwa kama tozo kulingana na kiasi cha pesa ambacho mteja atatoa.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce alisema” kupitia huduma yetu ya Airtel money tunaendelea kutumia technologia ya kisasa katika kuhakikisha tunatoa huduma bora zinazotoa suluhusho na kutatua changamoto katika huduma za kifedha kwa wateja wetu. Ushirikiano huu kati ya Airtel na Umoja SWITCH utaleta ufanisi na urahisi katika huduma zakifedha kupitia simu za mkononi”

Kupitia ushirikiano huu pia tunaongeza idadi ya mawakala ambao kwasasa ni zaidi ya mawakala 85,000 nchini nzima,sasa wateja wetu wanauhakika wakupata pesa kupitia mashine za ATM za Umoja SWITCH wakati wowote.

Lengo letu ni kuhakikisha tunaongeza idadi ya mawakala kwa kupitia njia mbalimbali na kuhakikisha huduma za kifedha kupitia simu za mkononi zinapenya na kuwafikia watanzania wengi na hivyo kuleta tija katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa ujumla. Aliongeza Alphonce

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Umojaswitch, Danford Mbillinyi alisema” kuingia kwa makubaliano katika huduma ya Airtel Money kuthihirisha lengo letu la kuchochea ushirikiano wamakapuni katika huduma za kifedha nchini. Tumekuwa ni sehemu ya Airtel katika huduma inayomuwezesha mteja kutoa pesa benki kwenda Airtel Money na Airtel Money kwenda benki na sasa tunafungua milango mingine kwa wateja wa Airtel Money kutoa pesa katika ATM zetu kwa urahisi na uhakika kwa kutembelea katika ATM zetu nchi nzima.

Alisisitiza Umojaswitch iko tayari kuungana na makampuni yanayoamini katika ushirikiano wa kibiashara kwani tunatambua kwa kufanya hivyo kutaleta tija kwa wateja na uchumi wan chi”

Ili kupa huduma hii , mteja atatakiwa kupiga *150*60# kupitia simu yake ya mkononi kisha kuchagua kutoa pesa kupitia ATM, kisha kuchagua UMOJA SWITCH ATM na kupata namba maalumu ya kwaajili ya kutoa pesa. Namba hiyo itatumika katika kutoa pesa kwenye mashine yoyote ya ATM ya UMOJA SWITCH Tanzania. Kila token (namba) itakayotolewa itatumika mara moja na itadumu kwa muda wa dakika tatu (3)

WAZIRI MKUU AWATAKA WANANCHI KUHIFADHI FEDHA ZAO BENKI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki kuepusha kuhatarisha usalama wao. 

Ametoa ushauri huo jana (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akifungua tawi la benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu mkoani Arusha akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama wao, hivyo ni vyema wakatumia benki mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao kwa ajili ya kutunza fedha zao.Akizungumzia kuhusu kufunguliwa kwa tawi la benki ya Uchumi wilayani Karatu, Waziri Mkuu alisema unaashiria ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo kwa kuwa benki ni kichocheo cha maendeleo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliushauri uongozi wa benki ya Uchumi kuangalia uwezekano wa kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha wananchi kukopa na kupata tija.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Bw. Wilson Ndesanjo alisema benki hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mtaji mdogo jambo linalowasababisha washindwe kufungua matawi katika mikoa mingine.

“Changamoto nyingine ni baadhi ya wateja kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, ambapo hatua za kisheria zikichukuliwa wanakimbilia mahakamani. Matukio haya yanadhoofisha kasi ya utoaji wa huduma kwani kesi zinachukua muda mrefu,” alisema.

Bw. Ndesanjo alisema kuna baadhi ya kesi zimechukua miaka sita bila ya kumalizika hivyo kuzuia fedha ambazo kama zingerejeshwa kwa wakati zingezungushwa kwa wananchi wengine.

Benki ya Uchumi ilianzishwa Septemba 22, 2005 ikiwa na mtaji wa sh. milioni 372. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2016 mtaji huo umefikia sh. bilioni 5.4 hivyo umeongezeka mara 14.5 zaidi ya ule wa awali uliokuwepo wakati wa uanzishwaji wake.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, DESEMBA 6, 2016.

DKT KALEMANI AWAAHIDI WAKAZI LYAMKENA KUSHEREHEKEA KRISMAS WAKIWA NA UMEME

0
0
Meneja wa Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Didas Lyamuya (katikati), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga (kushoto), kuhusu maendeleo ya Mradi huo wakati wa ziara ya Naibu Waziri mkoani Njombe hivi karibuni
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lyamkena kilichopo Makambako mkoani Njombe hivi karibuni, wakati akiwa katika ziara kukagua miradi ya umeme.
Wananchi wa Kijiji cha Lyamkena, Wilaya ya Makambako mkoani Njombe, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.
Wananchi wa Kijiji cha Lyamkena, Wilaya ya Makambako mkoani Njombe, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.



Na Veronica Simba - Makambako

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani ametoa ahadi kwa wakazi wa Kijiji cha Lyamkena kilichopo Makambako mkoani Njombe, kuwa watasherehekea sikukuu ya Krismas hapo Desemba 25 mwaka huu wakiwa na umeme. 


Dk Kalemani aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi husika jana kijijini hapo, mbele ya Mbunge wa Makambako Deo Sanga, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.Naibu Waziri alimwagiza Meneja anayesimamia Mradi wa Umeme wa Makambako – Songea, Didas Lyamuya, kuhakikisha kazi ya kutandaza nyaya inafanyika usiku na mchana ili umeme uwake katika eneo hilo kufikia Desemba 25.

“Tumekubaliana na Meneja, amejipanga kuanzia wiki ijayo wataanza kutandaza nyaya na watakamilisha ndani ya siku 10,” alifafanua.Aidha, Dk Kalemani alimwagiza Meneja huyo kuviingiza katika Mradi huo mkubwa wa umeme, vijiji vya Kihumba na Katani ambavyo vilisahaulika, ili vipatiwe umeme sambamba na maeneo mengine yote kama yalivyoainishwa katika Mradi.

Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya Mradi husika kwa Naibu Waziri, Lyamuya aliahidi kukamilisha kazi yote na kukabidhi rasmi Mradi ifikapo mwezi Juni mwakani ambayo ni miezi mitatu kabla ya muda uliopangwa yaani Septemba 2018.Kufuatia ahadi hiyo, Naibu Waziri alimpongeza kwa kufanya kazi kwa bidii na kumtaka aendelee na ari hiyo ili wananchi wa Mikoa ya Njombe na Ruvuma wapate umeme utakaowasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuinua uchumi wao.

Kwa upande wake, Mbunge wa Makambako, Deo Sanga, alimshukuru Naibu Waziri Kalemani kwa niaba ya Serikali kwa jitihada ambazo Wizara yake imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu ya umeme. Aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ili azma ya wananchi wake kupatiwa umeme itimizwe kama ilivyopangwa.

SALAMU ZA RAMBI RAMBI - KIFO CHA PROF. MTULIA

0
0

MIKOA NA HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA TAHADHARI JUU YA KIPINDUPINDU

0
0

Na Ally Daud-Maelezo

MIKOA na halmashauri nchini zimetakiwa kuweka tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia usafi binafsi na usafi wa mazingira hasa wakati wa mvua za vuli na msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ili kuweza kuepuka ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu kwa mwezi Novemba 2016 uliofanyika jijini Dar es salaam.

“Mikoa na Halmashauri zote nchini ziwe katika hali ya tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia usafi binafsi na usafi wa mazingira hasa wakati wa mvua za vuli na msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ili kuweza kuepuka ugonjwa huo” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu ishirikishe sekta mbalimbali za afya nchini bila kusahau jamii husika na kuhakikisha kila Halmashauri inaunda na kuimarisha Kamati ya Afya ya Kata. 

Aidha Waziri Ummy ameiagiza Mikoa na Halmashauri zote nchini kutoa taarifa ya wagonjwa wapya wa Kipindupindu ili jitihada za makusudi za kupambana na ugonjwa huo zifanyike mapema ili kujenga taifa lisilo na magonjwa ya mlipuko.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa takwimu zinaonesha katika mwezi Novemba 2016 jumla ya mikoa sita ikiwemo Morogoro yenye wagonjwa 282, Dodoma 96 na vifo 2, Mara 31, Kigoma 30 na vifo 4, Arusha 11 na Dar Es Salaam 8 kutoka wagonjwa 250 na vifo 4 kwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa wakati huohuo Waziri Ummy amepokea vifaa vya matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi vyenye thamani takribani milioni 100 za kitanzania kutoka Shirika la Kimataifa la Pink Ribbon Red Ribbon ili kupambana na ugonjwa huo nchini.

Akikabidhi msaada huo Mtendaji Mkuu wa Shirikahilo Bi. Celina Schocken amesema kuwa wametoa vifaa hivyo ili kuisaidia nchi kwa juhudi za kimakusudi katika kupambana na ugonjwa wa saratani ili kuokoa maisha ya wanawake wa Tanzania.

“Tumeamua kutoa vifaa hivi ili kuisaidia nchi kwa juhudi za kimakusudi katika kupambana na ugonjwa wa saratani ili kuokoa maisha ya wanawake wa Tanzania ”alisema Bi. Schocken.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akipokea vifaa mbalimbali vya matibabu ya mabadiliko ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi vyenye thamani takribani milioni 100 za kitanzania kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Pink Ribbon Red Ribbon  Bi. Celina Schocken jijini Dar es salaam.

MATUKIO YA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA MKOANI ARUSHA

0
0
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 
Zoezi la kuhakiki wastaafu likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya jiji la Arusha, Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa uhakiki.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akifurahia jambo na baadhi ya wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Hazina, waliojitokeza kuhakikiwa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika Ofisi za halmashauri ya Jiji la Arusha, zoezi litakalo dumu kwa siku tano hadi Ijumaa wiki hii katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akiongea na baadhi ya wastaafu waliofika katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya uhakiki ambapo wastaafu hao wameiomba serikali iwaongezee kiwango cha pensheni wanacholipwa ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, waliofika katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya kuhakikiwa.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa Pensheni yao na Hazina, Livingstone Kisanga (kulia) na Allen Kijazi, wakazi wa Arusha, wakisubiri kuhakikiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha, wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu hao linalofanyika katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara). 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuongea na wastaafu waliofika kwa ajili ya uhakiki, ambopo wastaafu wengi wameridhishwa na zoezi hili la wanashukuru zoezi hili linaenda kwa haraka kwani wengi wao wana nyaraka zote muhimu zinazohitajika.
Wawezeshaji wa zoezi la uhakiki wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika. Kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe na Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bw. Paison Mwamnyasi.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Mohamed Mtonga, akitoa ufafanunuzi kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha kuhusu masuala mbalimbali ya uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Hazina, unaoendelea katika kanda ya Kaskazini, mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.
Mstaafu, Mwanakombo Yusuph, mkazi wa eneo la Kaloleni, Jijini Arusha, akihojiwa na Wanahabari mara baada ya kuhakikiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo ameipongeza Serikali kwa kuendesha uhakiki huo utakaosaidia kuhuisha daftari la wastaafu na kwa uamuzi wake wa kuwalipa wastaafu kila mwezi badala ya miezi mitatu mitatu.
Bi. Amina Msigiti (kulia) ambaye ni mstaafu anayelipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, akijiandaa kutia saini fomu yake ya uhakiki mbele ya Afisa wa Hazina, Winfrida Moshi, kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

SERIKALI YAHIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWA UONGOZI MPYA WA TUCTA.

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akimskiliza Rais wa TUCTA Bw.Tumaini Nyamghokya wakati viongozi wapya wa TUCTA walipomtembelea Ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini(TUCTA) ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.Waziri uyo amehaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi hao ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.


Na Daudi Manongi-MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenister Mhagama amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.
Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Viongozi hao wa TUCTA waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho hilo. 

“Tumefarijika sana kwa TUCTA kupata uongozi mpya ambao tuna uhakika wanachama wamezingatia masuala  muhimu katika uchaguzi wao ikiwemo weledi na kutazama dira ya sekta ya wafanyakazi nchini”.

Aidha aliongeza kuwa Viongozi hao wana jukumu kubwa la kuleta tija na maendeleo chanya katika sekta ya kazi nchini na kuhimiza kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi.
Kwa mujibu wa Mhagama ameahidi Viongozi hao kufanya kikao kazi mapema iwezekanavyo kwani uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kufanya kazi.

Pia amesisitiza ushirikiano wa kudumu kati ya Serikali, Waajiri na wafanyakazi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo.
Kwa upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamghokya alimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kusimamia utu wa mtumishi kwa kuhaidi kuwalinda kutokana na baadhi ya viongozi kutoa lugha zisizosahihi.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu nao kwa muda wote na kuhaidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika kazi.

AFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WAENDELEA KUCHANGIA DAMU SALAMA

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakitoa damu kuchangia  Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, katika ofisi za makao makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni shughuli iliyopangwa na kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani inayoadhiimishwa Desemba Mosi kila mwaka. Wafanyakazi hao walitoa damu lita 50 kuchangia mpango wa damu salama nchini.
Mtaalamu wa Maabara wa mpango wa Damu Salama Taifa Kanda ya Mashariki, Grace Isidori  (aliyesimama) akisaidia wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kutoa damu kuchangia  mpango wa damu salama katika ofisi za makao makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam leo,  ikiwa ni shughuli iliyopangwa na kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani inayoadhiimishwa Desemba Mosi kila mwaka. Wafanyakazi hao walitoa damu lita 50 kuchangia mpango wa damu salama nchini.

WAZIRI MKUU AMALIZA MGOGORO WA SHAMBA LA MANYARA RANCH KWA KUKABIDHI HATI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI,

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi  uliodumu kwa miaka 17 kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei na Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) baada ya kukabidhi hati ya  shamba la Manyara Ranch  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya.

Hati hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 4, 2016) na Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mto wa Mbu kwenye viwanja vya Barafu baada ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji  hivyo vilivyopo kwenye  Kata ya Elesilalei Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Hatua hiyo imekuja baada ya kilio cha muda mrefu cha wananchi hao kudai kuwa Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliagiza shamba hilo ligaiwe kwa wananchi hao lakini jambo hilo halikufanyika na badala yake watu wachache walijimilikisha shamba hilo kinyemela chini ya wenyekiti wa bodi ya TLCT.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kurudisha umiliki wa shamba hilo kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili baada ya Baraza la Madiwani na Uongoziwa Wilaya hiyo ya Monduli kuridhia kwa pamoja umiliki huo kurudi kwa wananchi kama ilivyoamriwa hapo awali.

"Shamba hili lenye ukubwa wa ekari 44,930 sasa si mali tena ya Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) iliyokuwa inafadhiliwa na Shirika la African Wildlife Foundation (AWF) sasa ni mali ya wananchi na halmashauri ya wilaya ya Monduli ndio itapanga matumizi bora ya ardhi ya shamba hili mliloteseka nalo kwa muda mrefu ," alisema.

Alisema nyaraka zinazoonyesha kuwa shamba hilo lililotolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mwaka 1999 kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini jambo hilo  halikufanyika badala yake taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kufuatilia maeneo yote yaliyochukuliwa na watu bila ya kuyaendeleza na kuwapa wananchi. "Ni kwa nini watu wenye fedha wanachukua mashamba mkubwa bila ya kuyaendeleza huku wananchi wakiteseka kwa kukosa maeneo ya kilimo na ufugaji," alisema.

Awali kabla ya kuhutubia mkutano huo wa hadhara Waziri Mkuu alitembelea shule ya msingi ya Laiboni iliyoanzishwa  na mzee maarufu wa kimila wilaya huko Laigwanani Meshuko Ole Mapii ambayo inawanafunzi 102 wakiwemo wajukuu na watoto wa mzee  ambapo alitangaza umiliki wa shamba hilo kurudi kwa wananchi. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa William Ole Nasha alisema wizaraya yake itaendelea kutekeleza Sera za Kilimo nchini pamoja na kusimamia matumizi bora ya ardhi kwenye shamba hilo kutokana na ukosefu mkubwa ardhi kwa ajili ya wafugaji na wakulima.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwa tutaendelea kuhakikisha wananchi wafanya ufugaji wa kisasa wenye kwa tija kwa kutumia shamba hili. Pia nakupongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo na maagizo uliyotupa ya kuhakikisha wananchi wanatumia ardhi hiyo vizuri tutayasimamia,” alisema.

Baada ya shamba hilo kurudishwa kwa wananchi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema ‘’Nashukuru leo umiliki wa shamba hili umebadilishwa na naishukuru Serikali yangu tulivu kwa kutoa hati hii kwa Mkurugenzi  wa wilaya ya Monduli ili wananchi waweze kunufaika na ardhi yao na sio watu wachache wanaolipwa mamilioni ya fedha bila ya sababu za msingi’’.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Jumanne Maghembe aliwasihi wananchi hao kuheshimu njia za mapito ya wanyama (ushoroba) katika eneo hilo ambalo wanyamapori kutoka hifadhi za Tarangire, Manyara na Ngorongoro wanalitumia kwa ajili ya kupita kwenye hifadhi hizo mara kwa mara.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amempa siku mbili Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mazingira wa wilaya ya Monduli , Adil Mwanga kumuondoa muwekezaji, Lekisongo Meijo katika shamba lenye ukubwa wa ekari 2,800 lililoko katika kijiji cha Lemoti tarafa ya Kisongo ambalo alimilikishwa bila ya kufuata taratibu na kulirudisha kwa wananchi.

Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Gambo kufanya uchunguzi wa umiliki wa mashamba mengine makubwa ambayo yana migogoro na  hayajaendelezwa mkoani humo likiwemo la Makuyuni Stein Seed Valley na  kuipatia  ufumbuzi migogoro hiyo.

Serikali yaagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kulinda mazingira

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akifafanua juu ya kuanzisha ujenzi wa mradi wa maji ya uhakika wa kisima ambacho mkondo wake umepita chini sana, lakini pia alitoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutunga sheria ndogo ndogo za matumizi bora ya ardhi na kutojenga au kulima karibu na barabara zinazopita katika maeneo yao.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza (Makao makuu ya kata ya Massa) ambapo asilimia kubwa ya mradi huo ipo katika hatua za mwisho, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mpwapwa Bw. Donald Ng’wenzi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B.Simbachawene (MB) ambaye pia Mbunge wa Kibakwe akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza, mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwakani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B.Simbachawene (MB) ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe akisalimiana na wananchi katika kijiji cha Ikuyu kata ya Ruhundwa wakati wa ziara yake ya kujionea maendeleo katika kata za Ruhundwa na Massa wilayani Mpwapwa. Nyuma yake ni Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri.
 Mkuu wa wilaya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri akikabidhiwa aina ya muhogo unaolimwa katika kijiji cha Ikuyu kata ya Ruhundwa naye pia aliahidi kuwapelekea wananchi mbegu bora ya muhogo inayolimwa na Jeshi la Magereza wilayani humo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ikuyu Bw. Emid Myowera.
 Mojawapo ya barabara inasimamiwa na Halmashauri ya wilaya ikiwa imetengenezwa vizuri na kuwezesha uchukuzi wa mazao, bidhaa na watu kuwa rahisi na kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi. Barabara hiyo inaungansha Kata za Massa, Ruhundwa, Rudi na Kibakwe na ipo wilayani Mpwapwa, pia ipo katika Mpango wa pili wa Taifa 2018/2019 kujengwa kwa kiwango cha lami. Awamu ya kwanza ni kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2017/2018
  Sehemu ya ardhi katika kijiji cha Mkoleko, kata ya Massa iliyopo wilayani Mpwapwa ikiwa imeharibiwa vibaya kutokana na njia mbaya za kilimo, eneo lipo katika muinuko na limezungukwa na makorongo yanayopitisha maji kipindi cha masika hali inayosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na rasilimali misitu na mazingira.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),George Simbachawene ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinatunga sheria ndogo ndogo kwa ajili ya uhifadhi vyanzo vya maji, barabara za mamlaka hizo na njia mbaya za kilimo zinazo athiri mazingira.

 Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe aliyasema hayo  alipotembelea baadhi ya maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa wilayani Mpwapwa ambapo alitembelea kata ya Massa na Ruhundwa katika vijiji vya Mkoleko, Makose, Chogola, Winza, Njia Panda na Ikuyu na alijionea hali halisi ya maendeleo ya wananchi katika vijiji hivyo.

Aidha alibaini kuwapo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na njia mbaya za kilimo katika kijiji cha Mkoleko na kumtaka Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Jabir Shekimweri na timu ya wataalam wa wilaya kuchukua hatua za makusudi kunusuru hali ya mmomonyoko wa udongo unayotishia kutoweka kabisa kwa  kijiji hicho. 

“kamati ya huduma za Jamii ifanye kazi yake, mweke kontua na kuacha kulima na kukata miti katika kingo za makorongo ili kulinda mazingira” alisisitiza Simbachawene. 

Amewaasa wananchi kutumia fursa za ujio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa kulima mazao ya chakula na biashara kwani miundo mbinu ya lami kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe ujenzi wake unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/2018.

“barabara yetu inayotoka Mbande, Kongwa, Mpwapwa, Gulwe, Kibakwe, Rudi hadi Chipogoro itajengwa kwa kiwango cha lami lakini awamu hii Serikali imetangazwa barabara ya lami kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe” alisema Mhe. Simbachawene.

Mhe. Simbachawene Akiwa katika kijiji cha Chogola ameziagiza Mamlaka za Serikali nchini kufuata Sera na Sheria lakini pia kutunga sheria ndogo ndogo zinazozingatia utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwani kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira vijijini.

Aidha, ametoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa nchini kuzingatia ujenzi wa mpangilio katika makazi ya watu vijijini na shughuli za kilimo kando kando ya barabara uzingatie sheria za kuacha umbali unaotakiwa ili kulinda barabara kwa matumizi endelevu.

Kuhusu ombi la wananchi wa kijiji cha Ikuyu kuanzisha kata mpya Mhe. Simbachawene amesema Serikali inapenda kubana matumizi kwa kuepuka uanzishaji wa maeneo mapya ya utawala yasiyo na tija kwa wananchi, hivyo ameshauri kata ya Ikuyu yenye vijiji vya Ikuyu, Kidenge, Mpwanila, Chang’ombe, Muungano na Ruhundwa ibaki kama ilivyo kwa kuwa eneo la kata mpya wanayoomba yenye vijiji vya Ikuyu, Chang’ombe na Muungano litakuwa dogo.

“Sisi kama Serikali ya awamu ya tano hatutaki kufanya vitu visivyo na tija kwa sababu ugawaji wa maeneo ya utawala ya vijiji, kata, halmashauri, wilaya na mikoa, hatudhani kama kufanya hivyo kunaondoa kero au shida ya wananchi, wananchi hawa wanashida za maji, barabara na kupata madawa hospitalini. Mimi nadhani tija ya wananchi sio kuigawa nchi hii katika vipande vidogo vidogo”, Alisema Mhe.Simbachawene.   

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bw. Jabir Shekimweri aliwaagiza wananchi kata za Ruhundwa na Massa kupanda mazao yanayovumilia ukame kwa kuwa mwaka huu kunatarajiwa kuwa na mvua chini ya wastani pia alimwagiza Mtendaji wa Kata ya Massa kufuatilia masuala ya mazingira kwa ukaribu zaidi.

BancABC YAZINDUA OFA YA RIBA ASILIMIA 16 KWA WATEJA WANAOFUNGUA AKAUNTI YA MUDA MAALUM MSIMU HUU WA SIKUKUU

0
0

Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogo wadogo, Joyce Malai, wakionyesha kadi inayoonyesha uzinduzi wa ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, kuzindua ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya muda maalum msimu huu wa sikukuu. Uzinduzi huo ulifanyika Desemba 5, 2016 makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai
 Mkuu wa Masoko na Hazina wa BancABC, Barton Mwasamengo,
 Waandishi wa habari
 Bi.Upendo Nkini(kulia), akiwakaribisha maafisa hao tayari kuzungumza na waandishi wa habari.

Serikali ya Tanzania na Mauritius kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na na Utamaduni.

0
0
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(wa pili kulia) akizungumza na Ujumbe  wa Serikali ya Mauritius pamoja na  baadhi ya viongozi wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam  alipokutana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni Mhe. Santaram Baboo (wa kwanza kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Sanaa na Utamaduni.Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Mauritius kuhusu kuimarisha sekta ya Sanaa na Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo (wa kwanza Kulia) akizumgumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati wa majidiliano ya  kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili  katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(aliyesimama) akiongea jambo wakati wa mazungumzo  kati ya Wizara yake na Serikali ya Mauritius katika  Sekta ya Sanaa na Utamaduni.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Mauritius Mhe.Santaram Baboo baada ya mazungumzo baina yao kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake na viongozi wa Serikali ya Mauritius baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na Utamaduni yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

WATUMISHI WOTE WA SERIKALI ZINGATIENI UHADILIFU KATIKA KAZI

0
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision



Na Woinde Shizza,Arusha.


Watumishi wote wa Serikali wametakiwa kuzingatia uadilifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Jana alipokuwa akiongea na watumishi wa wilaya na halmashauri ya Monduli Mara baada ya kuzindua wodi ya mama wajawazito ya hospital ya wilaya ya Monduli.

Aliwataka watumishi wote wa serikali kuzingatia uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi ili dhana ya hapa kazi tu ichukue sehemu yake.

Majaliwa alisema Serikali ya awamu ya tano niyawawajibikaji,waadilifu katika sekta za umma .Amewataka watumishi wawasikilize,wawahudumie na kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hii itasaidia kuonyesha matokea bora ya kila mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi zaidi serikalini.Aidha amewataka viongozi wa halmashauri kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na zikafanye shughuli ambazo zilipangiwa.

"Kila sekta katika halmashauri ihakikishe inapanga majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa"alisema Majaliwa.Aidha aliwataka wananchi kote nchini iwapo atataka Huduma n a kuhudumiwa vibaya asisite kutoa taarifa katika vyombo husika.

"Mwananchi yeyote ambae atapewa huduma vibaya na mtumishi wa serikali asisite kutoa taarifa sehemu husika ili mtumishi huyo aweze kuchukuliwa hatua Kali"alisema majaliwa.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, KATIBU MKUU PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe  kabla ya kuanza kwa kikao chao cha pamoja na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Makamu wa Rais Samia Suluhu mara baada ya kutoka kwenye kikao cha pamoja kilicho wahusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumaliza kikao chao kilicho wahusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na  Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mussa Iyombe Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza mpaka hapo mamlaka husika itakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.

"Kumeibuka tabia ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwafukuza Wamachinga bila utaratibu wowote wa wapi wanawapeleka na wakati mwingine wanapelekwa maeneo ya mbali ambayo hayafai hata kwa kufanya biashara, hili jambo sio sawa hata kidogo.

"Sipendi Wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara lakini hakuna sheria katika nchi hii inayosema mtu wa biashara ndogondogo au Mmachinga hatakiwi kukaa katikati ya mji, tukianza kwenda kwenye utaratibu wa namna hiyo maana yake tunaanza kutengeneza  madaraja ya Watanzania, kwamba kuna Watanzania fulani wa daraja fulani wanapaswa kukaa katikati ya mji na Watanzania wa daraja fulani hawatakiwi kukaa katikati ya mji, huo sio mwelekeo wetu na wala Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi na wewe (Makamu wa Rais) tulipita kuinadi, haisemi tutengeneze madaraja ya watu wanaostahili kukaa mjini na wengine hawastahili kukaa mjini, sasa nimeona hili nilizungumze na nataka kulirudia kwa mara ya mwisho" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa Wamachinga waliondolewa katika maeneo yao Jijini Mwanza waachwe waendelee na shughuli zao mpaka hapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza itakapokamilisha maandalizi ya mahali watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha Wamachinga wenyewe.

"Narudia na hii ni mara ya mwisho, kawaambieni hata Wamachinga wa Mwanza warudi kwenye maeneo yao mpaka watakapowatengenezea utaratibu mzuri, Kigamboni hapa palikuwa na wamachinga eneo fulani wamehama vizuri kweli, wakatengenezewa miundo mbinu yao katika soko lao na sasa hivi wanafanya kazi vizuri, na waliwashirikisha viongozi wa Wamachinga, lakini Mwanza imekuwa ni amri tu na wengine wanatumia hata msemo wa Hapa Kazi Tu, mimi sikusema msemo wa Hapa Kazi Tu wa namna hiyo, nadhani mmenielewa" amesisitiza Rais Magufuli alipokuwa akiwaekeleza Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza Wizara ya Nishati na Madini kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Nyaligongo kilichopo katika Kata ya Mwakitolyo Mkoani Shinyanga na badala yake wachimbaji hao waachwe waendelee na shughuli zao, na leseni ya mwekezaji anayedai eneo hilo ni lake aondolewe.

"Wale waliofukuzwa Shinyanga wabaki palepale, kama ni leseni ya huyo mwekezaji ifutwe, Mhe. Makamu wa Rais fuatilia hili, mweleze Waziri wa Nishati na Madini, waache kufukuza wananchi hovyohovyo, wale wanapata riziki yao, wanasomesha watoto wao lakini wanafukuzwa tu."Na hizi ndio ajira zenyewe, tulisema tunatengeneza ajira, wewe mwekezaji ni mmoja unakwenda kuwafukuza watu 5,000? haiwezekani na wala haingii akilini" amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli amekemea vitendo vya wawekezaji wakubwa kupewa maeneo ambayo wachimbaji wadogo wanaendesha shughuli zao tena kwa mtindo kwa kutengeneza nyaraka zinaonesha mwekezaji husika alipewa eneo hilo kabla ya wachimbaji wadogo na kusisitiza kuwa mchezo huo hautavumiliwa.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema maagizo yake hayana maana kuwa Wamachinga na Wachimbaji wadogo waendeshe shughuli zao kwa kuvunja sheria bali wazingatie sheria na Mamlaka zisiwanyanyase watu wanyonge

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2016

RAIS MAGUFULI AAGIZA WAMACHINGA WASISUMBULIWE

0
0

NDOTO YA MAMA MMOJA KITANDA KIMOJA INATIMIA –MAKONDA

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ndoto ya mama mmoja kitanda kimoja itatimia endapo ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto inayojengwa Chanika kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini na Mkoa wa Dar es Salaam utakamilika.

Makonda alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni muda mwafaka kwa wanawake na watoto kuwa na uhakika wa kupata huduma ya afya.

Alisema hospitali hiyo inayojengwa itahudumia watu 1000 wa nje huku vitanda katika hospitali hiyo ni 160 kwa ajili ya akina mama na watoto.

Aidha alisema wananchi waendelelee kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli ya ulipaji kodi ili nchi iwe na uwezo hata kusaidia nchi nyingine kama wanavyofanya wa Korea.

Makonda alisema madaktari watakao kwenda katika hospitali hiyo watakuwa na makazi humo ili kuondoa usumbufu wa kusafiri kila siku.

Alisema serikali inawapenda wananchi wake kuhakikisha wanapata huduma ya afya bora hususani wanawake na watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati mwenye miiwani) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto ya Chanika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi ujenzi huo, Bing Hunan leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitembelea ujenzi wa hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images