Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1059 | 1060 | (Page 1061) | 1062 | 1063 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa (kulia), akizungumza na wanawake wafanyabiashara katika masoko ya Ilala na Temeke wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya  Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (kulia), akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo.
  Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa (kushoto), akiteta jambo na Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia .
  Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano huo.
  Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa (kulia), Mwezeshaji sheria masokoni, Consolatha Cleophas na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele wakifuatia kwa karibu mafunzo hayo.
  Mwezeshaji wa sheria katika Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akiandika changamoto na  za uendeshaji na usimamizi wa umoja kwenye masoko.
  Mkutano ukiendelea.

  Mkutano ukiendelea.
  Makofi yakipigwa baada ya hutuba ya mgeni rasmi Emma Kawawa.
  Usikivu katika mkutano huo.
  Mafunzo yakiendelea,
  Mgeni rasmi Emma Kawawa akifunga mafunzo hayo.

  Tabasamu wakati wa mafunzo hayo.
  Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
  Picha  hiyo 
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi.


  Na Dotto Mwaibale

  WANAWAKE Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwa na mshikamano, uthubutu, na upendo ili kusonga mbele katika shughuli zao za kiuchumi.

  Mwito huo ulitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  "Mkitaka kusonga mbele kiuchumi kupitia ujasiriamali wenu kama wanavyo fanya wanawake wenzetu katika nchi mbalimbali duniani mnapaswa kuwa na uthubutu, kupendana, kuacha majungu, kutunza muda  na kushirikiana" alisema Kawawa.

  Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa alisema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha viongozi wa vikundi vya umoja wa wanawake kwenye masoko ya Manispaa  ya Ilala na Temeke ili kuweza kujadili changamoto za uendeshaji na uimarishaji wa umoja masokoni kwa mwaka 2017.

  "Malengo mengine ya mkutano huu ni kutengeneza mpango kazi wa kufufua na kuimarisha umoja masokoni kwa mwaka 2017, kupeana mrejesho wa usajili wa umoja wa kitaifa (Uwawasota) na kupokea taarifa ya kamati ya uhamasishaji wa umoja kwa mwaka 2016" alisema Mlawa.

  Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia alisema mkutano huo uliwahusisha wanawake wajasiriamali kutoka masoko sita ya katika manispaa za Temeke na Ilala ambayo ni Gezaulole, Tabata Muslimu, Ferry, Temeke Sterio na Mchikichini.

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam.
   Mwimbaji Alfonsina Samweli wa kanisa la Assemblies of God la Kinziga Salasala Jijini Dar es Salaam akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kabrasha lenye DVDs zenye nyimbo za Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina akikata Utepe katika CD kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya Nyimbo za Injili za mwimbaji Alfonsina Samweli.
  Sehemu ya waumini wa kanisa la Assemblies of God la Salasala wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga  Mpina Hayupo Pichani wakati wa ibada maalumu ya kuiombea Taifa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
   (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

  Na Evelyn Mkokoi – Salasala DSM.

  NAIBU  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema Serikali ya awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi wake na si vinginevyo.
  Pia amesema  Serikali ya awamu ya Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba katika kutenda yaliyomema kwa maendeleo ya nchi  kwa kuogopa maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa.

  Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu  na Kuabudu na kuliombea Taifa la Kanisa la Tanzania Assemblies  of God lililopo katika eneo la Kinzugi Salasala, alisema  Serikali itaendelea kusimamia misingi yake bila kuogopa maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa kwani Sheria na Katiba za nchi zinatokana na maneno yaliyopo  katika vitabu vya Mungu.

  Alisema watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda kazi zao kwani uongozi waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa nguvu za mtu yeyote.

  " Uongozi unatokana na  Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa Waziri nilimaliza siku mbili sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri kipindi hicho  nilikuwa shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa ,nikasema ni uweza wa Mungu,"alisema na kuongeza kuwa 
  "Utawala wa awamu ya tano tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba muendelee kutuombea tutekeleze majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yetu,"alisema Mpina
  Aidha aliziomba familia za wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani bila kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii.

  "Familia za Kikristo lazima  ziwe mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira, hizi faini tunazowapiga watu kutokana na ukiukwaji wa sheria za mazingira kwa uchafuzi  wa Mazingira, sio kama tunawaonea bali kuwakumbusha wajibu wao "alisema.

  Kwa Upande wake,Mchungaji wa Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni alisema  watahakikisha wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya awamu ya tano na viongozi wake.

  Alisema roho za uadui zilizopo na watu kusema vibaya na kuwakatisha tamaa kusiwavunje mioyo kwa kusikiliza  maneno ya watu katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa ya taifahili na watu wake."Makanisa na Misikiti tupo pamoja nanyi katika kuwaombea na kama serikali hii ikiendelea hivi ndani ya miaka mitatu nchi yetu itabadilika,"alisema Mch.Sabuni.

  Ibada maalum ya Kuliombea Taifa, kusifu pamoja na kuimba, ilienda sambamba na uzinduzi wa Ablum ya nyimbo za injili za mwimbaji Alfonsina Samweli pamoja na mnadawa kuuza DVDs zenye nyimbo za injili.


  0 0  0 0


  Grace Kijo, Mratibu wa Masoko wa Shirika la Ndege la Etihad nchiniTanzania akigawa chokoleti kwa abiria siku ambayo Shirika hilo liliadhimisha mwaka wake wa kwanza wa huduma zake hapa nchini

  Shirika la Ndege la Etihad lenye makao makuu yake nchi za falme za kiarabu, limetimiza mwaka mmoja wa mafanikio tangu lianze kufanya huduma zake nchini Tanzania ikiwamo kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara ya usafiri wa anga kwa wasafiri wa Dar es Salaam na makao makuu ya falme hizo, Abu Dhabi.

  Zaidi ya wasafiri 60,000 wametumia usafiri huo tangu kuzinduliwa kwa huduma zake ambazo zinawaunganisha abiria wengi na miji mikubwa duniani, tangu Desemba Mosi 2015. Wasafiri wengi wamekuwa wakitumia usafiri wa Shirika la ndege la Etihad kutokana na shirika hilo kuwa kitovu cha safari za kwenda Ulaya na Asia.

  Shirika hilo linatoa huduma zake kwa kutumia ndege mbili za Airbus A320 yenye nafasi 16 kwa daraja la kwanza na viti 120 kwa daraja la kawaida. Kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam,ndiyo ndege ya tatu kuondoka kutoka Afrika Mashariki ikipitia Uwanja wa Ndege wa Nairobi Kenya na Entebbe Uganda.

  Meneja Mkuu wa Kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara wa Shirika la Ndege la Etihad, John Friel alisema, " Kwa mwaka mmoja tangu kuanza kwa huduma zetu kumekuwa na mafanikio makubwa, ndiyo sababu tuliamua kuichagua Tanzania kwa ajuili ya kufanya shughuli zetu. Tunafurahia kufanya kazi kwa ufanisi jambo ambalo limewavutia wateja wengi kulingana na mahitaji ya soko la usafiri wa anga hapa nchini."

  "Lengo letu ni kuendelea kushirikiana na wadauwa sekta hii ya anga hapa nchini ili kuhakikisha kwamba abiria wengi zaidi wanatumia usafiri wetu ambao umepata heshima kubwa ulimwenguni kwa kunyakua tuzo mbalimbali za ubora zinazotolewa na Shirika la Ndege la Etihad,” alisema.

  0 0

  Mkuu wa Mauzo wa Zantel Tanzania, Herbert Louis (kulia), akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa mji wa Tanga kupitia simu ya mkononi jinsi mtandao wa kasi  wa 4G wa kampuni hiyo unavyofanya kazi pamoja na baadhi ya bidhaa, hudumana ofa maalumu  kwa ajili ya mji wa Tanga. Hafla hiyo ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja ilifanyika katika Viwanja vya Tangamano mjini humo hivi karibuni.
  Ofisa Masoko wa Zantel, Deus Mtena (kulia), akizungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga jana kuhusu huduma, bidhaa na ofa maalumu kwa mji wa Tanga  ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja.
  Ofisa Masoko  Masoko wa Zantel, Emmiliana Vokolavene (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wakazi wa mji wa Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga jana kuhusu huduma, bidhaa wazitoazo na ofa maalumju kwa ajili ya Tanga  ikiwa ni moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu na wateja.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Bw.Frank Kanyusi akizungumza jambo juu ya maonesho ya viwanda vya Tanzania yatakayoanza Desemba (kesho) 07 hadi Desemba 11 katika uwanja wa maonesho ya Biashara ya kimataifa wa Mwl.J.K Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es salaam yenye lengo la kuitangaza na kuikuza sekta ya viwanda ili iweze kuchangia pakubwa katika uchumi wa nchi. BRELA itatoa huduma zake za urasimishaji wa biashara katika maonesho hayo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha kampuni zinazomilikiwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo hazipewi  zabuni zinazotolewa katika maeneo yao kwa ajiliya  kuepusha migongano ya kimaslahi.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha katika ukumbi bwalo la  Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Karatu akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

  "Hauzuiliwi kufanya biashara ili mradi kampuni yako isifanye kazi katika halmashauri ambayo wewe unaitumikia na una nguvu nayo ili kuepusha migongano ya kimaslahi kwani miradi yote utajilundikia," amesema.
  Pia amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri hiyo walisaidie Baraza la Madiwani katika kubaini vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri yao.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri wa umma  kujitathmini na kujiridhisha kama wanafuata misingi ya utumishi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Amewasisitiza  wawatumikie wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

  "Hatuhitaji kuwa na mtumishi mvivu, asiyewajibika, mwizi, mla rushwa na asiyekuwa muadilifu mahali pa kazi.Na  atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa " watumishi wa umma lazima mbadilike na muwe na nidhamu ya kazi. Muache malalamiko fanyeni kazi na msitafute  sympathy (huruma) kutoka kwa watu kwani Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ," amesema.

  Amesema katika baadhi ya ofisi za Serikali kuna ugonjwa wa watumishi wanapoona wageni wamelifika kwa ajili ya kupatiwa huduma wanawapita bila ya kuwasikiliza. " sasa hatutaki watumishi wa namna hiyo, Jukumu lako ni kumtumikia Mtanzania na tunataka kuona mabadiliko. Hatutaki kuona watu wakizubaa maofisini,".

  Waziri Mkuu amesema Serikali ikikuta wananchi wanalalamika kutokana na kutoridhishwa na  huduma zitolewazo na watumishi wa umma itahakikisha watumishi hao wanachukuliwa hatua. Serikali ni ya Watanzania wote hivyo lazima wahudumiwe vizuri bila ya kujali uwezo wao kifedha wala itikadi zao za kidini na kisiasa.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATATU, DESEMBA 5, 2016.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo akizungumza na Wahasibu kutoka Taasisi za umma na binafsi waliohudhuria katika hafla ya kutoa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akizungumza na Washindani wa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015 kutoka Taasisi za umma na binafsi takribani 56, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Lupama akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo baada ya kukabidhiwa tuzo ya Taarifa nzuri ya Fedha kwa mwaka 2015 kwa upande wa Wizara na Idara zake, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 Bw. Christopher Lupama akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Bw. Pius Maneno baada ya kukabidhiwa tuzo ya Taarifa Bora ya Fedha kwa mwaka 2015, ambayo imevuka asilimia 75 kwa ubora, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Baadhi ya Maafisa walioambatana na Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Lupama, wakipeana mkono na Viongozi wa Serikali na Bodi ya NBAA baada ya kupokea tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Mhasibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 Bw. Christopher Lupama, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa alioambatana nao wakati wa kupokea tuzo ya Taarifa Bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
  Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo wakibadilishana mawazo wakati wa zoezi la kuwakabidhi washindi wa Tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, tukio lililofanyika katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
    Kamishna Msaidizi wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akiwa katika picha ya pamoja na na washindi wa tuzo ya Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

  Wahasibu nchini wametakiwa kuzingatia viwango vya uhasibu vinavyotakiwa na kukubalika kitaifa na kimataifa wakati wa kuandaa taarifa za fedha kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

  Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi Sera, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi, wakati akikabidhi tuzo za Taarifa Bora za Fedha kwa mwaka 2015/2016, kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James tukio lililofanyika katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam

  Katika tukio hilo ambalo liliambatana na kufungwa  kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu unaojumuisha nchi za Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Mipango, kupitia Fungu 50, imepata tuzo ya kuandaa vitabu bora vya mahesabu vinavyokidhi viwango vilivyowekwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).

  Bw. Msangi amesema kuwa taarifa za fedha hutumika katika matumizi mbalimbali katika Sekta ya umma na binafsi, hivyo iwapo taarifa hizo zitakuwa katika viwango vyenye ubora zitaongeza imani ya wananchi kwa Serikali yao. 

  Amesema kuwa taarifa hizo pia hutegemewa na wawekezaji katika kupanga maamuzi yao ya uwekezaji hapa nchini hatua itakayosaidia nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Bw. Pius Maneno, amesema kuwa, kumekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa taarifa za fedha kwa upande wa Taasisi za Umma na Binafsi mwaka huo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

  “Mwaka uliopita Taasisi nyingi za umma zilishindwa kufikia asilimia 75 ambacho ndicho kiwango cha chini kabisa cha Taasisi kuingia katika ushindani wa Tuzo ya taarifa bora ya Fedha ya mwaka, lakini kwa mwaka huo, Taasisi za Serikali zilizokidhi kiwango hicho ni zaidi ya Asilimia 50.” AliongezaBw. Maneno.

  Aidha, amesema kuwa katika kutafuta mshindi wa Tuzo hiyo taasisi mbalimbali zimehusishwa ikiwemo Mamlaka ya Bima Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Utawala wa Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya matokeo kuthibitishwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). 

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Prof. Isaya Jairo amebainisha faida za tuzo ya taarifa bora ya fedha kuwa ni pamoja na kujenga uwazi, uwajibikaji, uadilifu na kuwa na taarifa ya fedha yenye viwango. 

  Amezitaka Taasisi nyingi kushiriki katika ushindani ili kuboresha taarifa za fedha za Mashirika yakiwemo ya umma na binafsi, huku akitoa wito kwa Serikali kuziagiza Taasisi zake kushiriki kikamilifu.

  Miongoni mwa wizara zilizoibuka na ushindi wa Tuzo hiyo ni Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50 ambapo iliwakilishwa na Mhasibu wake Mkuu Bw. Christopher Lupama kupokea Tuzo hiyo, ambaye amebainisha kuwa Tuzo hiyo imewapa nguvu ya kuendelea kufanya vizuri katika utoaji wa Taarifa ya Fedha yenye viwango.


  Taasisi 56 zimeshiriki kuwania tuzo hiyo inayoandaliwa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

  0 0

  Na: Frank Shija –MAELEZO

  WAKAZI wa Pangani waaswa kujitokeza kwa wingi katika wiki moja ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara inatarajia kuanza siku ya Desemba 7 mwaka huu.

  Wiki hiyo inalenga kutoa fursa kwa wananchi kuelezea ,kusikilizwa na kutatuliwa kero zao zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo rushwa na ufisadi.Kauli hiyo imetolewa jana (leo) na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi.Zainab Abdallah alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara. 

  Bi. Zainabu amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru Wilaya yake imeandaa Wiki ya Uhuru ambayo itatumika kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mahakama na Serikali kwa ujumla kusikiliza kero za wananchi hasa zinazohusu masuala ya Rushwa na Ufisadi.

  “Mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakama nimemzungumza na Mahakimu kujitahidi kuharakisha usikilizwaji wa kesi zote zinazohusiana na rushwa kwani mueleke wa Serikali yetu ni kutokomeza rushwa kabisa,” alisema Bi. Zainab.Aliongeza kuwa Wilaya yake imeamua kuandaa wiki hii ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamo ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na adui rushwa na ufisadi kwa vitendo.

  Amesema kuwa kutokana na dhamira ya dhati aliyonayo Mhe. Rais Magufuli katika kukabiliana na rushwa na ufisadi ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkoni jitihada hizo.

  “Ni wahakikishie Watanzania kwamba Serikali yao imedhamiria kwa dhati kubwa kuhakikisha inatokomeza tatizo la rushwa na ufisadi kwani watu wamekuwa wakihujumu uchumi wa taifa katua Awamu hii haitafumbia macho watu wa namna hiyo,” alisisitiza Bi. Zainabu.

  Aidha ameongeza kuwa mbali na kusikiliza kero za wananchi wiki hiyo pia itatumika kuhamasisha wajasiriamari wadogo wadogo kuanzisha viwanda ili kutekeleza azma ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.Desemba 9 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Dar es salaam na kauli ya mwaka huu ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuhimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu.”

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo pamoja na ujumbe wake.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha  picha ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dream liner wakati alipokuwa akisikiliza maelezo yake kutoka kwa Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo. Ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 262 na itakuwa na uwezo wa kuruka kutoka nchini Marekani hadi Tanzania bila kutua mahali popote.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Doto James na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ununuzi wa ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dream liner mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi wa mauzo wa Kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuaga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kuagana na Mhe. Rais Dkt. Magufuli. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.Dkt. Tonia Kandiero ameteuliwakuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini. PICHA NA IKULU  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw. Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.

  Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James.

  Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano imedhamiria kununua ndege nyingine nne zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.

  "Sisi hapa tunazungumza kuwa watalii hawajafika hata milioni 2 kwa mwaka, lakini nchi kama Morocco inapata watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka, hii yote ni kwa sababu hatuna mashirika ya ndege ya kwetu, watalii wakitaka kuja hapa ni lazima waje kwa kuungaunga, wafikie nchi nyingine halafu ndipo wapate moyo wa kuja huku, licha ya kwamba sisi Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 duniani zenye maeneo mazuri yenye utalii

  "Kwa hiyo niwaombe tu Watanzania wapende mali zao, kwa sababu wakati mwingine nikiangalia mitandao na magazeti ni ajabu huwezi kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta wanasifia tu ndege za watu wengine na wanazibeza za kwao" amesisitiza Rais Magufuli.

  Mhe. Rais Magufuli ametaja aina ya ndege mpya ambazo Serikali itazinunua kuwa ni ndege 1 aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kufika nchini Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018 na ndege moja aina ya Boeing 787 Dash 8 Dream Liner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 na inayotarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika.

  Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi za Serikali zenye lengo la kuinua utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.

  "Tumeleta ndege aina ya Bombardier hapa, zimepunguza gharama za safari mfano kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, sasa wanalipa kati ya 160,000/ hadi 200,000/- wakati nauli ilishafika Shilingi laki 8 na kitu, lakini watu wengine utakuta wanazungumzazungumza wee maneno ya hovyo kwa kutumiwa, tumeshaamua na tutafanya hivyo" amesisitiza Rais Magufuli.

  Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika hapa nchini (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye amepandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika ofisi zake zilizopo Afrika Kusini.

  Rais Magufuli amemshukuru Dkt. Tonia Kandiero kwa juhudi kubwa alizozifanya akiwa Mwakilishi Mkazi wa AfDB hapa nchini ambapo miradi mikubwa na muhimu katika maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa.

  Akizungumza baada ya kuagana na Rais Magufuli Dkt. Tonia Kandiero amemshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha miaka 6 aliyokuwa hapa nchini na amesema anaondoka akiwa ameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimahusiano na AfDB ambapo miradi yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni imetekelezwa hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

  Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo anayemaliza muda wake baada ya kuiwakilisha nchi ya Cuba kwa miaka minne.

  Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo kwa uhusiano na ushirikiano mzuri aliouendeleza kati ya Tanzania na Cuba uliojengwa na waasisi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Fidel Castro wa Cuba.

  Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo amemshukuru Rais Magufuli na Serikali kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Cuba na amesema anaondoka akiwa anaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizi utaendelea kuwanufaisha wananchi ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za kijamii.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  05 Desemba, 2016
   

  0 0

  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo asubuhi kabla ya kuanza rasmi mazoezi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaoanza rasmi Desemba 17 mwaka huu, wachezaji na benchi la ufundi walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao, Ismail Khalfan.

  Khalfan alifariki dunia jana wakati akikimbizwa hospitali baada ya kudondoka uwanjani kufuatia kugongana na beki wa Mwadui kwenye mchezo wao wa michuano ya Ligi ya Taifa ya Vijana kituo cha Bukoba mkoani Kagera kinachohusisha timu za Kundi B.

  Kikosi hicho kimerejea tena kwenye mazoezi kufuatia kuwa mapumzikoni kwa muda wa takribani wiki mbili mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza.

  Ni wachezaji watatu tu wa Azam FC waliokosekana kwenye mazoezi hayo wakiwa na ruhusa maalumu, ambao ni beki Erasto Nyoni, washambuliaji wapya kutoka Ghana, Samuel Afful na Yahaya Mohammed, wanaotarajiwa kuanza rasmi kujifua na wenzao kuanzia kesho Jumanne.

  Wachezaji wengine walioshindwa kufanya mazoezi ni winga Khamis Mcha, anayesumbuliwa na maumivu ya nyonga ambaye alipewa programu maalumu ya mazoezi na Mtaalamu wa Viungo wa Azam FC, Sergio Perez Soto, huku beki wa kushoto, Gadiel Michael, akiwa ameteguka mkono alioumia wakati akifanya mazoezi binafsi wakati wa likizo iliyopelekea kufungwa plasta gumu ‘p.o.p’.

  Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuhusu programu yake ya wiki hii, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameelezea kufurahishwa na namna wachezaji wake walivyorejea mazoezini wakiwa na hali nzuri licha ya kutoka mapumzikoni hali ambayo inampa wakati mzuri kukiandaa kikosi chake kuelekea mechi za mzunguko wa pili.

  “Tumeanza mazoezi leo kwa spidi kubwa kwa ajili ya kuingia kwenye mzunguko wa pili wa ligi, tumeanza kwa mazoezi mara moja leo, kesho (Jumanne) tutafanya mara mbili asubuhi na jioni kwa ajili ya kuwa fiti zaidi tayari kuingia kwenye ushindani, kwa sasa tunawasubiria wachezaji wambao hawajafika (Erasto, Yahaya, Afful), ambao watajiunga nasi kesho,” alisema.

  Katika kuimarisha safu yake ya ulinzi, Azam FC imemrejesha kikosini beki wake wa kati, Abdallah Kheri, aliyekuwa akicheza kwa mkopo kwenye timu Ndanda ya Mtwara katika mzunguko wa kwanza wa ligi.

  Azam FC inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 25, inatarajia kufungua dimba la raundi ya pili ya ligi, kwa kukipiga na African Lyon Desemba 18 mwaka huu, mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.  0 0


  Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kwa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakati akiitambulisha program ya ‘ReadtoWork’ ya benki hiyo yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri. Wengine ni baadhi ya washikiri na wawezeshaji katika mkutano huo ambao pia kituo cha televisheni cha EATV kilikuwa kikitambulisha tuzo na wasanii wanaowania tuzo hizo zinazotambuliwa na Baraza la Sanaa la Taifa.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakihudhuria mkutano huo. 
  Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (katikati), akihojiwa na wandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano ambapo benki hiyo iliitambulisha program yake ya ‘ReadtoWork’ yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri.
  Meneja Masoko wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika mkutano ambapo benki hiyo iliitambulisha program yake ya ‘ReadtoWork’ yenye lengo la kuwaandaa wahitimu wa vyuo vikuu na elimu ya juu kujiandaa na ajira au kujiajiri.

  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
  Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo ambayo ni moja ya mdhamini wa mkutano huo.
  Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
  Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger
  Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.

  Mablogger kazini

  Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
  Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence  Mello akitoa mada.
  Meza kuu. Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Kranty Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi pamoja na Katibu wa muda wa TNB, Khadija Kalili.

  Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
  Bloggers wakifuatilia mada.
  Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.
  Mgeni rasmi akihutubia.
  Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
  Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
  Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.  Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
  Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
  Picha ya pamoja.

  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).

  "Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Abbas.

  Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.

  Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine. 

  Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

  Wanamitandao hao  wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa  wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MMILIKI wa maduka ya nguo Jijini Dar es Salaam,Hussein Mkangala (38) maarufu 'Hussein Pamba Kali' amefunguliwa mashtaka ya kesi ya madai baada ya  kushindwa kulipa Sh.Milioni 75 alizokopa kutoka kwa Anna Kiabi.

  Shauri hilo lilitajwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ambapo upande wa mdai ulikuwa unasimamiwa na Wakili Jonas Nkya, wakati ule wa mdaiwa ukiongozwa na Ernest Swai.

  Mbele ya Hakimu Is -Haq Kuppa, Upande wa mdai ulisema kwamba Novemba 20 mwaka jana mfanyabiashara huyo alikopeshwa kiasi cha sh. Miloni 80 kwa makubaliano atamlipa kwa kipindi walichokubaliana kitu ambacho amevunja makubaliano.

  Wakili Nkya alidai Mei 22 mwaka huu mdaiwa Husseni alimtuma mdogo wake aitwaye Hassan Mkangala, apeleke fedha kiasi cha sh. Milioni 5 kwa Anna na kiasi kilichobakia hakulipa tena.

  Kwa upande wa utetezi wao waliomba mahakama hiyo iwape muda wa siku 6 ili waweze kujibu madai hayo.

  Hivyo Hakimu Kuppa aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena lakini Mdaiwa hakufika mahakamani.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  SERIKALI kwa kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Mh Sospeter Muhongo, imesema itaendelea kufanya kazi kwa bidii ya kusambaza umeme ili kufikia malengo ya Duniaya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 Watanzania wote waweze kupata nishati hiyo muhimu.Waziri Muhongo aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Alisema usambazaji wa umeme umefanyika kwa kiasi kikubwa lakini bado wanaendelea na miradi ikiwa na lengo la kuwapatia wananchi nishati kwa uhakika kutokana na vyanzo vya nishati vilivyopo hapa nchini.

  Profesa Muhongo amesema mradi wa usambazaji wa umeme vijijini umerahisisha upatikanaji wa maendeleo ya haraka kwa Watanzania wengi, hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini ambayo serikali imeendelea kuweka mkazo wa kufikisha huduma hiyo.

  Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika duniani kwa nchi masikini kunawafanya wananchi wakose huduma muhimu kama vile elimu afya pamoja na kufifisha maendeleo ya ukuaji wa sekta binafsi, 

  Aidha Rodriguez alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha nchi zinazoendela ikiwemo Afrika kuwezesha kifedha katika upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuweza kufikia lengo la Dunia 2030.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO,Dar es Salaam

  SERIKALI imetoa wito kwa wamiliki na watendaji wa mitandao ya kijamii (Blogs) nchini kufuata Misingi, Sheria na Maadili ya taaluma ya habari.

  Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Idara ya Habari(MAELEZO) Hassan Abbas wakati wa uzunduzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Tanzania Bloggers Nertwork(TBN) na mafunzo kwa wanachama hao kuhusu uendeshaji wa mitandao ya jamii kwa manufaa.

  Mkurugenzi Abbas alisema kuwa Blogger ni mwandishi wa habari, mwanahabari, na mwanataaluma ya habari hivyo anawajibu wa kuhakikisha anaandika na kusambaza taarifa zenye ukweli kwa manufaa ya nchi.“mitandao ya kijamii inalisha sehemu kubwa ya taarifa duniani hivyo wamiliki na watendaji wanapaswa kufuata misingi mikuu mitatu ya uandishi wa habari, ambayo ni ukweli, ukweli, ukweli ili kuweza kuheshimika na kusonga mbele” alifafanua Abbas.

  Aidha Abbas amewataka watendaji wa Blogs kushirikiana na Serikali katika kutoa Elimu kwa umma kuhusu Sheria ya Huduma ya Habari iliyopitishwa hivi karibuni.Akijibu baadhi ya changamoto zinazowakabili wamiliki wa mitandao ya kijamii, Abbas alisema, ametoa rai kwa vyombo vya habari pale watumiapo kazi zao wanapaswa kuwatambua au kuomba idhini kwa mmiliki wa picha au makala husika.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa muda wa TBN Joachim Mushi alisema mkutano huo unalenga kuwafundisha wanachama juu ya uendeshaji mitandao ya kijamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo.Naye Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Jamii Media Maxence Melo akiwakilisha mada kuhusu masuala mbalimbali ya umoja na mikakati ya kujenga chama alisema kuwa ili blogger kuweza kufika walipokusudia wanatakiwa kwenda na wakati.

  Alisema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za ndani na nje ya ya bidhaa ama kampuni kuweza kufa, hivyo wamiliki wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuwa wabunifu na wafuatiliaji ili kuweza kujua mteja anahitaji nini na kwa wakati gani.

  Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mitandao ya kijamii ni ajira, itumike kwa manufaa” ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalamu wa masuala ya habari na mitandao ya kijami.
  Mkurugenzi Idara ya Habari(MAELEZO) Hassan Abbas (wa pili kulia).

  0 0


  Bango liliandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho hayo
  Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akiwasili kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mwembeni, Vngunguti kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Jinsia na watoto kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mwwembeni, wilayani humo mkoani Dar es Salaam, leo. Pamoja naye ni Kamanda wa Polisi Ilala, Salum Hamdani.
  Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alifurahia jambo na Kamanda wa Polisi IlalaSalum Hamdan baada ya kuketi meza kuu
  Watoto wakiselebuka kwa burudani ya muziki wakati wa hafla hiyo
  Maandamano maalum yakipita mitaani, kwenda kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwembeni ambako yalipokelewa na Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
  Maandamano maalum yakipita mitaani, kwenda kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwembeni ambako yalipokelewa na Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
  Maandamano maalum yakipita mitaani, kwenda kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwembeni ambako yalipokelewa na Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo
  Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Kamanda Salum Hamdani na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omari Kumbilamoto, wakiwa wamesimama kupokea maandamano hayo.
  Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Kamanda Salum Hamdani na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omari Kumbilamoto, wakiwa wamesimama kupokea maandamano hayo.
  Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Kamanda Salum Hamdani na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti Omari Kumbilamoto, wakiwa wamesimama kupokea maandamano hayo.
  MC wa shughuli hiyo, Eugen Mwapondele akihamasisha
  Watoto kutoka kikundi cha Kituo cha Mwana cha Vingunguti wakiimba wimbo Maalum
  Watoto kutoka kikundi cha Kituo cha Mwana cha Vingunguti wakiimba wimbo Maalum
  Baadhi ya waliohudhuria wakitoa ujumbe kwa bango
  Sheikh  Mohammed Mtutuma akisoma dua kabla ya shughuli kuendele
  Mratibu wa shughuli hiyo Judith Faustine akiomba dua kabla ya shughuli kuendelea

  Msanii kutoka kikundi cha Buyope Youth Centre Mohammed Thabiti, akifanya vitu vyake kuchangamsha shughuli hiyo.
  Mohammed thabiti na Peter John wa kikundi cha Buyope wakionyesha uhodari wao katika kucheza ngoma
  Sijali Mohammed wa kikundi hicho naye akionyesha umahiri wake katika kucheza ngoma
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto akitoa salamu, baada ya kukaribishwa kuwasalimia wananchi katika hafla hiyo
  Mwakilishi wa Taasisi ya WiLDAF akizungumza
  Baadhi ya Maofisa wa Polilisi waliohudhuria shughuli hiyo
  Baadhi ya maofisa wa Polisi waliohudhuria hafla hiyo
  Mtoto akiwa amepanda na kutulia tuli kwenye uzio ili kuona vizuri kila kilichokuwa kikifanyika kwenye uzinduzi wa maadhimishohayo
  Kamanda wa Polisi Ilala, ACP Salum Hamdani akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo
  Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo akitoa hotoba yake wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo. Kuisoma hotuma hiyo Tafadhali/>>BOFYA HAPA
  Vijana wakifuatilia hotuba ya Mpogolo
  Watoto wakiwa wametulia wakati Mpogolo akihutubia
  kamanda wa Polisi Ilala, ACP Salum Hamdani na Katibu tawala wa Ilala Edward Mpogolo wakiwa wameshika TV tayari kuwakabidhi watoto wa kituo cha Mwana cha Buguruni, ili waweze kuwa wanaangalia taarifa mbalimbali na burudani bila kulazimika kutoka kwenye kituo chao. Wapili Kulia ni Diwani Kumbilamto
  wakikabidhi Tv hiyo iliyotolewa na Kamanda  Hamdani
  Watoto wakimshukuru DAS
  Watoto wakimshukuruKamanda Hamdani
  Mpogolo na Kamanda Hamdani wakienda kukagua shughuli za madawati ya Polisi kuhusu kupinga ukatili wa Jinsia na watoto katika wilaya ya Ilala
  Sajenti Doris Gweba wa Dawati la kupambana na ukatili wa kijinsia na watoto Ilala, akitoa maelezo kwa DAS jinsi wanavyofanyakazi
  DAS Mpogolo akizungumza na waandishi wa habari mwisho wa uzinduzi huo
  Mpogolo akiagana na Makamanda wa Ilala kabla ya kuondoka
  Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akiwa tayari kupanda gari kurudi ofisini baada ya kuzidua maadhimishohayo. Picha zote na Bashir Nkoromo. Tafadhali ukipenda kusoma Hotuba aliyotoa Mpogolo kwenye uzinduzi huo, usipate taabu/>>BOFYA HAPA TU

  0 0


   Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akihojiwa na waandishi wa habari

  Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa wamezisimamisha Daladala kwa kosa la kupakia abira eneo ambalo sio rasmi

   Jinsi magari yanavyogeuza katika eneo la Buhongwa
   Eneo la stendi isiyokuwa rasmi ya Buhongwa ilivyo katika kadhia ya ubovu
   Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akikagua eneo la barabara ya Buhongwa ambayo inatumiwa na madereva Daladala kama stendi
   Gari likigeuza katikati ya barabara kutokana na kukosekana kwa eneo maalumu la stendi


   Wajasiriamali wakiwa katika eneo la biashara huku Daladala zikitumia eneo hilo pia kupakia na kushusha abiria
   Gari inageuza kituoni ambapo ni barabarani huku watu wakiendelea kuvuka barabara
   Dede akikagua barabara iliyoharibika
   Gari ikiwa imepaki katika eneo bovu la barabara ya Buhongwa   Mwandishi wa habari wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akimhoji moja ya madereva katika eneo la Buhongwa

   Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede akisalimia na wakazi wa eneo la Nyashishi mara baada ya kuzuru katika eneo hilo ambalo ndilo amependekeza kuwa stendi ya daladala, kushoto kwake ni Mwandishi wa habari wa www.blogspot.com Ndg Mathias Canal

  Na Mathias Canal, Mwanza

  Uongozi wa Mkoa wa Mwanza umetakiwa kubainisha stendi za Daladala, maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia biashara za mbogamboga na matunda kwa kina mama sambamba na kubainisha maeneo maalumu ambayo daladala haziruhusiwi kusimama kwani kufanya hivyo kutaondoa urasimu uliopo baina ya madereva wa Daladala na askari wa usalama barabarani.

  Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa madereva Kanda ya ziwa Bw Hassan Dede wakati alipozuru kujionea kadhia wanazokumbana nazo madereva wawapo barabarani sambamba na kujionea kandia wanayoipata kutokana na ubovu wa barabara na kutokuwa na stendi ya Daladala katika Mtaa wa Buhongwa nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Nyamagana.

  Dede alisema kuwa ni ajabu kwa nchi yetu kuwa na kituo cha daladala chenye mwanzo lakini hakina mwisho hivyo kuwafanya madereva kugeuza mahala pasipokuwa rasmi ambapo ni hatari kwa uhai na magari na madereva hao.

  Katika eneo la Buhongwa zinapogeuzia daladala kama kituo, barabara yake ni mbovu huku pembeni kukiwa na machinga sambamba na wajasiriamali wanaouza mbogamboga na matunda jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa wafanyabiashara hao endapo kama gari litaharibika kutokana na hitilafu ya breki.

  Hata hivyo alisema kuwa kumekuwa na wimbi la ukamataji na kutozwa faini na askari wa usalama barabarani kwa madereva hao kutokana na kuegesha magari katika eneo la barabara kwa ajili ya kupakia abiria jambo ambalo ni kinyume na utaratibu kwani hakuna kituo katika eneo hilo pamoja na madereva hao kulipia ushuru kila siku.

  Dede alisema kuwa katika njia itokayo Kishiri, Airport, Ilemela na Kisesa kuelekea Buhongwa kuna jumla ya Daladala 1900 ambayo kwa siku moja kila gari inalipia ushuru wa shilingi 1000 ambapo kwa gari zote 1900 kwa siku serikali inakusanya kodi ya jumla ya shilingi 1,900,000/=.

  Katika kipindi cha mwezi mmoja serikali inakusanya jumla ya shilingi 57,000,000/= huku ikiwa inakusanya jumla ya shilingi 693,500,000 kwa mwaka.

  Dede amehoji fedha zote hizo serikali inafanyia nini kama imeshindwa kukarabati barabara itokayo Mwanza Mjini kuelekea Airport sambamba na kukarabati na kubainisha eneo maalumu la stedi kwa ajili ya Daladala.

  Sambamba na hayo pia Dede amependekeza serikali kuhamisha kituo cha daladala kisichokuwa rasmi cha Buhongwa kuhamia katika eneo la Nyashishi lililopo mwanzoni mwa Wilaya ya Misungwi kwani kupitia kuwepo kwa eneo hilo daladala zote zitafanikiwa kuingia katika stendi hiyo na serikali itakusanya mapato mengi kwani itakuwa rahisi kuwabana madereva wote.

  Katika Barabara itokayo Makao makuu ya Mkoa wa Mwanza (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa) kuelekea eneo hilo la Buhongwa kuna vituo rasmi visivyopungua sita huku vituo visivyo rasmi vipo zaidi ya 15 hivyo ni vyema uongozi wa Mkoa wa Mwanza kupitia ofisi ya usalama barabarani kusimamia jambo hilo na kuweka alama mahususi zitakazobainisha vituo hivyo.


  0 0

     Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mbali na jitihada za makusudi za Serikali na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado hali siyo ya kuridhisha ambapo Jiji la Dar es Salaam linashika nafasi ya Sita barani Afrika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
  Dar es Salaam ambalo ni Jiji kubwa kuliko yote Tanzania linakadiriwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo kati yao asilimia 58 ni wanawake, na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa jiji hilo inakadiriwa kuwa Milioni 5.
   Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani kutoka Shirika la Mpango wa UKIMWI la Umoja wa Mataifa - Tanzania (UNAIDS) kwa mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limekuwa kati ya majiji Barani Afrika yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI.

  Afisa wa UNAIDS Tanzania, Fredrick Macha anasema asilimia 16 ya maambukizi yote mapya Tanzania Bara yanatokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo kwa wanawake wenye umri mdogo wa miaka 15-24 kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 7%,sababu kubwa ikiwa ni kujiingiza katika ngono wakiwa na umri mdogo pamoja na biashara ya ukahaba.

  Anafafanua kuwa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Jijini Dar es Salaam ni asilimia sita (6%) licha ya jitihada kubwa za Serikali na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI,kuelimisha na kuhamasisha wajawazito kupima na kufuata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga na VVU.
  Takwimu za Wizara ya afya za mwaka (2011-2012), mtu mmoja kati ya watu watano jijini Dar es Salaamana mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja,na mara nyingi wanafanya ngono zisizo salama hivyo hicho ni kiashiria kikubwa cha ongezeko la maambukizi hasa kwa wana ndoa”alisema Macha.
   Aidha amevitaja baadhi ya vichocheo na viashiria vinavyochangia uwepo wa ongezeko kubwa la maambukizi katika jiji hilo kuwa ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara unaosababisha muingiliano wa watu kutoka Mikoa mbali mbali nchini pamoja na mataifa mengine.
  Dar es Salaam kama yalivyo majiji mengine duniani yenye muingiliano wa tamaduni na desturi mbalimbali limeathirika pia na makundi yanayoelezwa kuchochea maambukizi mapya ya UKIMWI kama vile wafanya biashara ya ngono, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na watumiaji wa madawa ya kulevya na kwa kujidunga.
                                                                                        
  “Kwa mujibu wa takwimu hizo, kati ya wanawake 4 wanaojihusisha na biashara ya ngono, mmoja ni mwaathirika na virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 26).Vile vile kati ya watu watano wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, mtu mmoja ameathirika, sawa na asilimia 22.3) na kati ya watu sita wanaotumia madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano, mmoja ni mwathirika wa virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 15.5),”alisema Macha.
   Aidha Macha alisema pamoja na changamoto mbalimbali, Jiji la Dar es Salaam limependekezwa kuwa moja ya majiji machache ya mfano ulimwenguni katika mkakati wa dunia wa kuimarisha udhibiti wa UKIMWI kwenye majiji (UNAIDS Fast Track Cities Initiative).
   Mkakati huo ni kuyafanya majiji makubwa Afrika kuwajibika zaidi katika kuongeza ufanisi kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI katika maeneo ya mijini kwani kasi ya maambukizi na wingi wa maambukizi yapo mijini.
   Pamoja na majiji kuwa na rasilimali nyingi, mifumo ya utoaji huduma za afya bado inaandamwa na changamoto mbalimbali, hususani katika kuandaa na kutekeleza mipango mizuri yenye kuhakikisha ushirikishwaji wa watu wote hasa makundi maalumu katika jamii, ambayo kiwango cha maambukizi ni kikubwa.
   
  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama anasema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake  nchini wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume,jambo ambalo linahitaji jitihada zaidi kujikinga.

  “Kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.
   
  Waziri Mhagama anasema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.
   
  Aliongeza kuwa UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizi mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu hivyo Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani,pamoja na mashirika ya kupambana na UKIMWI kuhakikisha janga hilo linatokomezwa  ifikapo mwaka 2030.

  Alisema Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao kwa hiari ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU,bila kusubiri hadi kinga zao zipungue.


  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

  ”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema wataalam wa afya wametuambia UKIMWI unapungua nchini Tanzania, suala hilo linatokana na misaada mbalimbali tunayoipata kutoka nchi wahisani  kwahiyo ili kutokomeza kabisa suala la upungufu wa dawa na misaada kwa waathirika wa ugonjwa huo Watanzania wanahitaji kujichangia wenyewe na sio kutegemea fedha za wahisani peke yake.

  Alifafanua kuwa ili kuwezesha suala hilo,Sheria Na. 5 ya mwaka 2015 imeitaka Wizara yenye dhamana kuwa na Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI pamoja na Bodi yake hivyo, kuanzishwa kwa Mfuko huo kutaleta chachu kwa Watanzania kuungana kuzuia maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU) pamoja na kuwahudumia wananchi wanaoishi na virusi hivyo.
   “Kwa kawaida fedha zinazotoka kwa wahisani huwa zina mwisho wake hivyo Tanzania tunazindua Bodi rasmi itakayosimamia Mfuko huo ili na sisi tuongeze nguvu pale wahisani watakapoishia,”alisema Mama Samia.
   Naye muathirika wa UKIMWI, (jina limehifadhiwa) ameishkuru Serikali kwa kuwasaidia kwa hali na mali watu wenye ugonjwa huo kwani sio wote wenye ugonjwa huo wameupata kwa kujitakia.
   “Kitendo hiki kinatufanya tusijione wanyonge wala kukata tamaa kwani Serikali yetu haitutengi inatupa ushirikiano sawa na watu wengine wasio na maambukizi ya ugonjwa huu,”alisema muathirika huyo.
   Tarehe 1 Disemba kila mwaka ni siku maalumu ambayo tunaadhimisha Siku ya UKIMWI duniani, siku ambayo kwa pamoja tunaungana na watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 78 ambao tayari wameshapata mambukizi na watu milioni 35 ambao tayari wamefariki ulimwenguni kote kutokana na athari zitokanazo na maambukizi ya UKIMWI.


older | 1 | .... | 1059 | 1060 | (Page 1061) | 1062 | 1063 | .... | 1897 | newer