Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 104 | 105 | (Page 106) | 107 | 108 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa mazao wa wizara ya kilimo, chakula na ushirika, Dkt.Mshindo Msolla akisisitiza jambo wakati wa kuzindua huduma ya Z-KILIMO
   Wafabyakazi wa Zantel wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya kilimo
  Mkurugenzi wa mazao wa wizara ya kilimo, chakula na ushirika, Daktari Mshindo Msolla akisisitiza jambo wakati wa kuzindua huduma ya Z-KILIMO.
  Mwakilishi wa Sibesonke akizungumza wakati wa uzinduzi wa Z-Kilimo. Anayemfuatia ni Daktari Mshindo Msolla, Mkurugenzi wa Mazao kutoka wizara ya kilimo, chakula na ushirika akifuatiwa na Mkuu wa kitengo cha rasrimali .
  =======  =======  ========
  Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na kampuni ya Sibesonke leo wamezindua huduma mpya ya kutoa taarifa kuhusu kilimo kupitia simu za mikononi.
  Huduma hiyo mpya inayofahamika kama,Z-KILIMO,itawawezesha wakulima nchini Tanzania kupata taarifa za papo kwa pao na uhakika kuhusu njia za kuendesha kilimo cha kisasa kwenye simu zao za mikononi.

  Kupitia huduma hii ya Z-KILIMO, wakulima nchini, hata wale walio vijijini wataweza kupata taarifa muhimu za namna ya kuendesha kilimo cha kisasa na hivyo kuongeza uzalishaji na kukuza sekta nzima ya kilimo. Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel, Francis Kiaga, amesema kwa kupitia huduma hii wakulima nchini watapata fursa ya kipekee kupata taarifa kuhusu kilimo moja kwa moja kupitia simu zao.

  “Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, na kinachangia sana kwenye kukuza na kuchangia uchumi wa nchi yetu, na huduma hii imekuja wakati muafaka katika kuendeleza juhudi hizo, lakini pia kuwapa wakulima umuhimu wa huduma ya simu katika namna wanayoihitaji zaidi’ alisema Kiaga.

  Akielezea zaidi huduma hiyo Kiaga alisema itawasaidia zaidi wakulima katika kuokoa muda ambao zamani waliupoteza katika kupata taarifa kuhusu kilimo, na pia kuwaongezea uzalishaji wa mazao yao.

  Huduma ya Z-KILIMO pia itawapa wakulima taarifa kuhusu maandilizi ya ardhi, aina za mbolea, aina za mazao, aina za mifugo, aina ya magonjwa yanayoshambulia mazao, upaliliaji, taarifa za usafiri, hali ya hewa pamoja na sehemu ya majadiliano baina ya wakulima.


  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma akisema itasaidia kufungua fursa zaidi kwa wakulima nchini. ‘Kupitia huduma hii, wakulima sasa wataweza kuboresha mbinu zao za kilimo katika hatua zote za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji’ alisema Dkt Msola.

  Nao kampuni ya Sibesonke, ambao wameingia ushirikiano wa kiteknolojia na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na wizara ya maenedeleo ya Mifugo na Uvuvi, ukiwa na lengo la uwafikia watanzania wakulima kuwapa taarifa muhimu za kilimo kwenye simu zao.


  “Sibesonke ina furaha kwa kuwezesha watanzania kufaidika na teknolojia hii kupitia mtandao wa Zantel’ alisema Daktari Uwe Schwarz, Mkurugenzi Mkuu wa Sibesonke. “Kampuni ya Zantel imeonyesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha teknoljia hii inawafaidisha watanzania wote kwa mtandao wake ulioenea nchi nzima’ alisiistiza Daktari Schwarz.


  Wakulima wanaweza kujiunga na huduma hii kwa kubonyeza *149*50#, ambapo wataweza kupata maelekezo ya kutumia huduma hii.  

  0 0

   Baadhi ya wanafunzi Sekondari ya Nduweni wakiwa darasani
   Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Urauri, Wilaya ya Rombo
   Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Nduweni Sekondari, Venance Mramba
  Sehemu ya maktaba ya Sekondari ya Tanya, ikionesha utitiri wa vitabu vya sayansi japokuwa haina walimu wa somo hilo.

  ======= ======= ======
  Wanafunzi kidato cha Sita wabebeshwa mzigo wa ualimu wa Sayansi Rombo

  KITENDO cha upungufu wa walimu wa sayansi nchini hasa katika shule za sekondari zinazomilikiwa na serikali kimezidi kuibua changamoto maeneo mbalimbali nchi. Shule ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa ni sekondari za kata ambazo uwingi wake umechochea zaidi changamoto hiyo.

  Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto hiyo ya uhaba wa walimu wa sayansi kama ilivyo kwa mikoa tofauti ya Tanzania. Hata hivyo walimu wakuu wa shule zenye changamoto wamebuni mbinu mbadala kukabiliana na hali hiyo.

  Zoezi la uhamasishaji ujenzi wa shule za sekondari za kata limekuwa na mafanikio kiasi kikubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kwani hadi sasa wilaya hiyo imefikisha jumla ya sekondari 41 zilizo chini ya serikali ikiwa ni jitihada za wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao.

  Mwandishi wa makala haya amefanikiwa kutembelea shule sita tofauti za sekondari za kata wilayani Rombo na kufanya mazungumzo na walimu wakuu, walimu na wananfuzi ambao wanatoa picha halisi ya uhaba wa walimu wa sayansi. Miongoni mwa shule zilizotembelewa ni pamoja na Sekondari za Nduweni, Tanya, Urauri, Holili na Ngaleku.

  Victus Kiwango ni Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Tanya iliyopo wilayani Rombo. Mwalimu huyu anasema uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni moja ya tatizo zinaloikabili shule hiyo. Kiwango anasema shule yake haina kabisa walimu wa masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia hivyo hulazimika kutumia walimu wa kukodi kwa vipindi tofauti.

  Anasema shule hiyo hutegemea wanafunzi kadhaa waliomaliza kidato cha sita ambao huwakodi na kufundisha masomo hayo pale wanapopatikana ili wanafunzi waweze kupata chochote na hatimaye baadaye kufanya mitihani ya sayansi. "...Hapa shuleni kwetu (Tanya Sekondari) masomo ya sanyansi ndio tatizo, mfano hatuna kabisa walimu wa masomo ya Kemia, Fizikia pamoja na Baiolojia hivyo huwa tunakodisha na shule kuwalipa," anasema Kiwango. 

  Hata hivyo kero na kilio cha uhaba wa walimu kinasikika tena katika sekondari ya duweni wilayani humo. Mwalimu Mkuu Msaidizi wa sekondari hiyo, Venance Mramba anasema tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi linaiathiri shule hiyo kitaaluma. Anasema shule miaka yote shule hiyo imekua ikianzia ufaulu wa daraja la pili.

  Anatolea mfano katika matokeo ya mwisho ya kidato cha nne (juzi), ilifanikiwa kufaulisha mwanafunzi mmoja kwa daraja la pili na wanne kwa daraja la tatu. Anaongeza kuwa katika matokeo hayo wanafunzi 25 walipata daraja la nne na wanafunzi 70 wakiambulia sifuri, kati ya idadi ya wanafunzi 102 waliofanya mtihani huo wa mwisho wa taifa.

  "Tatizo kubwa la kufaulu ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na mengineyo, uhaba wa vifaa vya ufundishaji na kujifunzia pamoja na upungufu wa vitatu vya masomo yote," anasema mwalimu Mramba katika mahojiano na mwandishi wa makala haya.

  Anaongeza ili kukabiliana na upungufu wa walimu wa sayansi shule hiyo huajiri kwa muda wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na kuwasaidia kuwafundisha wanafunzi masomo hayo. Hata hivyo anasema bado kuna changamoto kubwa katika kuwatumia walimu hao wahitimu wa kidato cha sita, kwani hawana mbinu za kufundishia jambo ambalo bado ni kikwazo katika shule hiyo.

  Benson Samizi ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Holili iliyopo katika Wilaya ya Rombo. Mwalimu huyu anasema japokuwa hali ya kitaaluma shuleni hapo si mbaya sana lakini shule inakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi kama ilivyo katika shule nyingine wilayani hapo.

  Mwalimu Samizi anasema shule hiyo haina kabisa walimu wa masomo ya Fizikia na Hesabu na hulazimika kukodi walimu wa muda ili kuwaandaa wanafunzi. Shule hii haina maabara japokuwa ina vitabu vya kutosha vya masomo ya sayansi. Akizungumzia ufaulu wa kidato cha nne kwa mwaka 2011, anasema shule ilipata mwanafunzi mmoja aliyekuwa na daraja la kwanza na wengine wawili waliopata daraja la pili, huku wanafunzi watatu wakipata daraja la tatu.

  Samizi anaendelea kubainisha kuwa katika matokeo hayo jumla ya wanafunzi 55 walipata daraja la nne na 18 kuambulia patupu (sifuri) kati ya watahiniwa 80 waliofanya mtihani wa mwisho wa taifa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2011.  

  Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Urauli, iliyopo Tarakea wilayani Rombo, Sim Silayo anasema mbali na biashara zinazofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya eneo hilo kuathiri taaluma kimaudhurio, upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi ni kero nyingine shuleni hapo.

  Mwalimu Silayo anaeleza kuwa shule hiyo haina kabisa walimu wa masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia; hivyo uongozi wa shule kulazimika kukodi walimu wa muda wa masomo ya sayansi wakiwemo baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita wanaosubiri kuendelea na masomo yao ya juu. Aidha anaongeza kuwa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007, yenye jumla ya wanafunzi 464 haina maabara wala vitabu vya kutosha licha ya kukabiliwa na changamoto zingine mbalimbali.

  Yehova Mashalo ni mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Tanya anasema wapo wanafunzi wengi ambao hukata tamaa kuchukua masomo ya sayansi tangu wakiwa madarasa ya chini kutokana na kukosekana kwa walimu wa masomo hayo. Kwa upande wake Joice Kimaro mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Tanya anaongeza kuwa kutojitosheleza kwa walimu wa sayansi shule za sekondari hasa za kata inakatisha tamaa wanafunzi kupenda masomo hayo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya anasema halmashauri yake inajitahidi kuongeza idadi ya walimu kila mwaka ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu. Anasema kwa uwiano wa kawaida Wilaya ya Rombo haina upungufu mkubwa wa walimu, lakini una upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.

  Anasema kwa sasa wilaya ina jumla ya walimu 800, huku kwa mwaka huu pekee ikiwa imeajiri walimu 134 wakiwemo wa masomo ya sayansi. "...Kwa suala la upungufu wa walimu Wilaya ya Rombo ni tofauti na maeneo mengine, hapa kuna upungufu wa walimu wa masomo; kama Hesabu, Fizikia, Kemia na Baiolojia nitatizo," anasema Mkurugenzi Mboya.

  Hata hivyo anakiri kutokana na suala la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi zipo shule ambazo zimelazimika kutumia walimu wa kukodi na kutumia wanafunzi waliomaliza kidato cha sita ili shule iweze kwenda mbele. Anasema kuwa lengo kubwa la halmashauri hiyo ni kuhakikisha inatatua changamoto hiyo kila inapotokea nafasi.    

  Kwa upande wake Katibu wa CWT Wilaya ya Rombo, Erasmo Mwingira anasema vijana wa kidato cha sita ambao hutumiwa na baadhi ya shule kuokoa jahazi la masomo ya sayansi wamekuwa hawafundishi zaidi ya kuwakaririsha wanafunzi kujibu mitihani jambo ambalo anatahadharisha huenda likawa na madhara makubwa kwa elimu yetu Tanzania. 

  "Kujua kusoma na kuandika si kigezo cha kumfundisha mtu...vijana hawa wa kidato cha sita hawana mbinu za ufundishaji, wanachokifanya ni kuwakaririsha wanafunzi," anasema Mwingira. Pamoja na hayo mdau huyu wa elimu anaishauri serikali kutojitoa katika jukumu la kuendesha shule za kata kwa kuwaachia wazazi kwani shule hizo ziko katika hali mbaya na zinahitaji kuongezewa fedha za uendeshaji.

  *IMEANDALIWA na www.thehabari.com

  0 0


  BREAKING NEWS:  Umoja wa Mataifa wapitisha Azimio la Kihistoria kuhusu Haki za Watu wenye Albinism

   Tarehe 13 Juni, 2013  Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UNHRC) kwa pamoja lilipitisha azimio lililowasilishwa na Kikundi cha Umoja wa Mataifa cha Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza katika ngazi ya kimataifa kutambua na kushughulikia mashambulizi na ubaguzi dhidi ya watu wenye albinism katika nchi nyingi.    

  Azimio hili la kihistoria limefanikiwa baada ya ushirikiano mkubwa baina ya Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Yusuf   Mohamed   Ismail, nchi wanachama zikiongozwa na Kikundi cha Mataifa ya Afrika, Ofisi ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu  (UNOCHRC) na Shirika la Under  The  Same  Sun (UTSS).     

  ·      Tembelea wavuti zifuatazo kutazama video zinazohusiana na azimio hili la kihistoria: http://www.youtube.com/watch?v=EJIFdT8bKM0&feature=youtu.be
  ·      (UTSS  Founder/CEO  Peter  Ash  addresses  the  UN  HRC  Assembly  on  albinism)  

  ·      (The  Ambassador  of  Gabon  (leader  of  The  African  Group  of  Nations)  presents  the  
  resolution  to  the  Council  and  it  is  adopted ) 

  Tafadhali pokea katika kiambatanisho maandishi rasmi ya Azimio L.25 la Baraza la Umoja wa Mataifa yaliyotafsiriwa kwa Kiswahili!


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo aliyokuwa akipewa na Waziri Mkuu Ndugu Mizengo Pinda mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea nchini Uingereza. Rais Kikwete alirejea nchini jana tarehe 18.6.2013 usiku baada ya ziara ya kikazi nchini Uingereza. PICHA NA JOHN LUKUWI

  0 0

     Ufukwe wa ziwa Nyasa katika mwambao wa ziwa hilo kama uonekanavyo  kwa mbaali hivi,kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa mkoani Njombe.Wananchi waishio huko hujishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo  za uvuvi wa dagaa/samaki na kilimo kilimo pia.

  0 0  0 0

   Tunu Kavishe, Communications Manager(centre) and Musa Kitoi Acting Consumer Retail Director in a picture with some of the winners of the Golden Briefcase Campaign during the 2nd Draw today
  Khadija Kashoro and Anorld Shirima posed on a photo with their Golden Brifcase Gift after the 2nd Draw today, right is Tunu Kavishe Communications Manager.

  ========  ========     ========  ==========

  Barclays Bank Tanzaniaruns its second draw on Maisha Bomba with Barclays Golden Briefcase and presents prizes to winners of the first draw.


  Barclays Bank Tanzania has today run it’s second draw on Maisha Bomba with Barclays Golden briefcase campaign to its customers. The draw gives an opportunity for Barclays 13 customers to win Barclays Golden briefcases on a monthly basis for a period of three months.


  Speaking at a press conference today the Acting Consumer Retail Director and Head of Distribution, Mr. Musa Kitoi commented; “Entry is open to Retail customers (both existing and prospective) with Barclays Bank Tanzania deposit accounts. Today we have done the second draw and we have got 13 winners. We are also issuing the prizes for the winners of the first draw that was conducted on 22ndMay 2013, in 13 Golden briefcases. Each winner will randomly pick a briefcase and open to know his/her prize.

  Among the prizes to be won are: i-Pads, A home theatre, Washing Machines and gift vouchers.


  Customers who are eligible in this campaign are Retail Current and Savings Account holders who can earn an entry to the draw upon uplifting and maintaining their balances by at least TZS500,000. This amount is only considered for the respective month for which the deposit was made.


  New customers can get entries to the draw upon opening an account and depositing a minimum of TZS500, 000 and maintaining the balance for the month. Both existing and new customers will get an additional entry for each additional TZS 500,000 deposited in their accounts in the particular month.


  Upon depositing and maintaining this threshold, every customer (new and existing) will enter into a draw where 13 customers will walk away with different prizes in 13 Barclays Golden briefcases and the grand prize winner will walk away with TZS 10,000,000. 


  This campaign was officially launched on 11thApril 2013 and will run until 30th June 2013.The draw for each month will be held on the 1stweek of the proceeding month, based on qualifying entries for the previous month.
  0 0

   Mkurugenzi wa Benchmak Productions na Jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi juu ya uzinduzi wa msimu mpya wa EBSS. Kushoto kwake ni Afsa Biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
   Meneja wa Kampeni wa Push Mobile, Rodney Rugambo akielezea namna usaili kwa njia ya simu utakavyofanyika
   Mshindi wa Epiq BSS 2012, Walter Chillambo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu mpya wa EBSS. Anayemfuatia kulia ni Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, na Ritha Paulsen, Mkurugenzi wa Benchmark Prouductions
  Mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo akipeana mkono na Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa EBSS. Anayetazama ni kulia, ni jaji mkuu wa EBSS, Ritha Paulsen
  ======  =======  ========

  ZANTEL YAZINDUA MSIMU WA SABA WA EPIQ BONGO STAR SEARCH

    
  Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo imezindua msimu mpya wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, mwaka huu ikiwa imejipanga kuwapa vijana wengi zaidi fursa ya kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao.


  Msimu huu mpya,ambao utakuwa msimu wa saba toka shindano hilo lianzishwe mwaka 2006, unatarajiwa kujumuisha wadau wakubwa wa muziki, hivyo kusaidia kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi pamoja na kuwajengea ushirikiano utakaowasidia kuendeleza kazi zao za muziki baada ya mashindano.


  Shindano la mwaka huu litakuwa na kauli mbiu ya ‘KAMUA’ ikimaanisha kutumia uwezo wako wote katika kufanya kile unachopenda, litaenda kufanya usaili kwenye mikoa sita ya Mbeya, Arusha, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.


  Kwa mwaka jana shindano la Epiq BSS lilipata mafanikio makubwa hasa kwa idadi kubwa ya vijana kujitokeza kufanya usaili, na kubwa zaidi ikiwa ni vijana wote walioingia kumi na mbili bora kufanikiwa kutoa nyimbo zao ambazo zimefanya vizuri.


  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production, Rita Paulsen amesema mwaka huu wana mpango wa kuwafikia vijana wengi zaidi lakini pia kutengeneza wasanii nyota wengi zaidi ukiacha mshindi.


  “Sote ni mashahidi wa namna shindano hili lilivyopata mafanikio toka ilipozinduliwa miaka saba iliyopita, na hakika kila mwaka tumekuwa tukisogea mbele zaidi, na mwaka huu mpango wetu ni kuzalisha wanamuziki watakaofanikiwa wengi zaidi’.


  Shindano la mwaka huu pia litakuwa na vitu vingi vipya, ikiwemo ongezeko la jaji mmoja katika usaili wa mikoani, ambapo jaji huyo atakuwa ni mdau wa mziki kutoka mkoa husika.


  ‘Kwenye kila mkoa tutakakoenda kufanya usaili tutakuwa na jaji mwenyeji ambaye tunaamini atasaidia kuongeza ladha ya machaguo ya vipaji na hivyo kuhakikisha tunapata vipaji aina tofaouti’ alisema Paulsen.


  Naye Afsa biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan amesema uzinduzi huu wa leo ni furaha kubwa kwa kampuni ya Zantel kwani unaashiria ufunguzi wa milango ya kuwasaidia vijana wengi wa kitanzania kutimiza ndoto zao.


  ‘Kwa mwaka jana pekee Epiq BSS ilifanikiwa kusaili vijana zaidi ya elfu hamsini, jambo ambalo linaonyesha kitu kimoja, kuna uhitaji wa kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza vijana’ alisema Khan.


  Ikitekeleza ahadi yake ya kuwasaidia vijana baada ya shindano, kampuni ya Zantel iliwarekodia wimbo mmoja mmoja washiriki wote waliongia kumi na mbili bora, ikiwa ni pamoja na kuwapa ziara ya kujitangaza kwenye mikoa mitatu.


   ‘Tumefanikiwa kuwajengea vijana hawa msingi wa kazi yao ya muziki, na tuna furaha kusema wengi wao hadi sasa wanafanya vizuri, na huu ndio aina ya udhamini kampuni ya Zantel inapenda kujihusisha nao’ alisisitiza Khan. Mshindi wa mwaka huu pia atajinyakulia milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.

  Katika kuwapa fursa vijana ambao hawatafikiwa na majaji, Zantel pia itafungua laini za kurekodi kwa simu toka siku ya kwanza ya kuanza usaili mikoani, ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 ili kujirekodi kwa njia ya simu, au kutuma neno KAMUA kwenda 15530 kupata maelezo zaidi.


  Usaili utaanzia Dodoma tarehe 29 and 30 ya mwezi huu katika ukumbi wa Maisha Club, ikifuatiwa na Zanzibar tarehe 5 na 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Bwawani. Mbeya usaili utakuwa tarehe 10 hadi 11mwezi wa saba pale club Vybes, Mwanza tarehe 14hadi15mwezi wa saba Club Fussion, na Arusha itakuwa tarehe 20 hadi 21mwezi wa saba Club Tripple A ikimalizikia na Dar es Salaam tarehe 26  hadi 28pale Uwanja wa Taifa.  0 0

  IMG_1435Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari ambaye amelazwa katika hospitali ya Serian Arusha anakotibiwa  kwa madai ya kushambuliwa na wananchi eneo la Makuyuni. IMG_1416Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole  Mbunge wa Viti Maalum, Namelok Sokoinine  aliyelazwa kwenye hospitali ya Serian Arusha baada ya kuvunjika mguu  akiwa nyumbani kwake. (Picha na Ofisi ya Waziri
  Mkuu)

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne. 
    Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
   Rais wa FIATA, Stanley Lim, akizungumza wakati waka wa ufunguzi wa kutano huo.
   Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua mkutano huo. Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Double Tree, kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne. 

  0 0

   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2013 kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka Kushoto ni Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wateule wa Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi, wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 19, 2013 kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka Kushoto ni Balozi Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva (kulia) ni Balozi Wilson Masilingi, anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda Washington D.C, Marekani. Picha na OMR

  0 0

  Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel ten Bw.Charles Hilila amefariki dunia  saa saba usiku katika Hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya homa ya Malaria iliyokuwa ikimsumbua kwa muda wa siku chache zilizopita...MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU CHARLES HILILA-AMENI.HABARI KWA HISANI YA http://shinyangayetu.blogspot.com

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akiongea machache wakati kamati hiyo ilipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont hoteli jijini Dar es Salaam. Kutoka upande wa mkuu wa Itifaki ni katibu Bosco Majaliwa, Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta wakiwa pamoja muandaaji wa mashindano hayo Dennis Ssebo.
  Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega, akiongea na warembo wanaowania taji la Redds Miss Kinondoni 2013 mara baada ya kuwatembelea kambini kwao na kujua wanaendeleaje. Lundenga aliwaasa washiriki hao kuongeza bidii katika mazoezi yao ili waweze kufanya vyema katika fainali yao.

  Warembo wa Redds Miss Kinondoni wakiwa wamejipanga mara baada ya kumaliza mazoezi.
  ---
  Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.

  Kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Hashimu Lundenga imetembelea kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 wanaotarajiwa  kumenyana leo alhamisi (leo) ya Juni 20 katika shindano Redd’s Miss Kinondoni Talent 2013 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza mratibu wa shindano hilo mara baada ya kuwakaribisha wageni, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.

  Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.

  Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

  0 0

   Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Biashara ya M-pesa Jackson Kiswaga akionesha jinsi M-pesa inavyoweza kuboreshwa kukidhi mahitaji zaidi ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo huitumia huduma hiyo kama njia kuu ya kukusanyia ada ya maombi ya mkopo tangu mewaka 2010. Wanaomuangalia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga. Vodacom ilitembelea makao makuu ya bodi hiyo jana kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo mbili.

   Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Habari na Elimu kwa Umma wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisbwa akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya bodi na kampuni ya Vodacom Tanzania kuangalia namna ya kuimarisha na kubioresha zaidi uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo mbili. Wengine pichani kutoka kulia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga.
  Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Biashara ya M-pesa Jackson Kiswaga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Vodacom ilipotem,ebela makao makuu ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kukuza uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo mbili. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi Juma Chagonja na Naibu wa Tehama wa bodi hiyo Cuthbeth Simalenga. Bodi ya mikopo kwa miaka mitatu sasa imekuwa ikiitumia huduma ya M-pesa kama njia kuu ya kukusanyia ada ya mamombi ya mkopo kutoka kwa waombaji wake.
  Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini - HESLB imesema huduma ya M-pesa inayowawezesha waombaji wa mikopo ya elimu juu kwenye bodi hiyo kulipia ada ya uombaji kwa kiasi kikubwa imesaidia kurahisisha uendeshaji ikwemo usimamizi na ufuatiliaji wa malipo hayo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Bw. Cuthbeth Simalenga wakati wa kikao cha urafiki mwema kati ya uongozi wa Bodi na Kampuni ya Vodacom kilichofanyika makao makuu ya bodi hiyo yaliyopo Msasani Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.

  Bw. Simalenga amesema bodi hiyo ilianza kutumia huduma ya M-pesa kwa malipo ya ada ya maombi miaka mitatu iliyopita na kwamba tangu wakati huo huduma hiyo imekuwa ikiimarika na kutoa tija zaidi kwa upande wa uendeshaji wa shughuli za uombaji wa mikopo.

  "Kwa miaka mitatu sasa tumekuwa tukitumia huduma ya M-pesa kukusanyia ada za malipo ya maombi ya mikopo, kwa sasa waombaji wote wanatumia huduma hii na tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya ndani mara kwa mara kukabiliana na changamoto za hapa na pale zinazojitokeza."Alisema Bw. Simalenga.

  Zaidi ya waombaji 50,000 wakiwemo waombaji wapya na wale wanaaondelea na elimu ya juu hutuma maombi ya mikopo kwenye  bodi hiyo kwa mwaka, na wote kwa sasa wanatumia huduma ya M-pesa kulipia ada ya malipo ya maombi ambayo ni Sh 30,000.

  Bw. Simalenga amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa katika mfumo huo wa malipo kuwa ni uaminifu wa waombaji hasa wanafunzi ambao baadhi yao hulalamika kushindwa kulipia au na kudai kutaka kurejeshewa fedha zao wakati huohuo wakiwa tayari wameshakamilisha mchakato wa uombaji na fedha hizo kupaswa kutumika kama ada ya uombaji.

  "Wamekuwepo baadhi ya waombaji ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu wa hapa na pale kwa kutuma maombi na kufanya malipo baadae wanarudi na kupiga simu Vodacom kudai kurejeshewa fedha zao kwa madai kuwa wamebadili mawazo ya kuomba mkopo wakati sio kweli." Aliongeza Bw. Simalenga.

  "Tunaomba waombaji wote na umma kwa ujumla kutambua kuwa mamlaka ya kurejeshewa fedha Sh 30,000 ya ada ya uombaji yapo nje ya Vodacom, hilo ni la Bodi na kwamba sasa tumeweka utaratibu wa kurudisha fedha hizo mwishoni mwa zoezi la uombaji tukizinagtia taratibu za kiuhasibu za bodi baada ya kujiridhsiha kuwa utambulisho wa muamala (Transaction ID) wa mwombaji haijatumika kuendelea na zoezi la uombaji mkopo."Alifafanua
  Aidha ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uhusiano wa bodi na kampuni ya Vodacom ambao amesema una kila nafasi ya kuwa imara zaidi huku akiishauri Vodacom kuongeza ubunifu zaidi kwenye mfumo wa malipo ya M-pesa ili mfumo huo uweze kuwa na tija zaidi kwa wadau wake hasa wabia wakubwa.

  "Vodacom imekuwa karibu na sisi na bado kuna fusra zaidi ya ubunifu kwenye huduma hii itakayotoa tija zaidi kwetu."Alisema Bw Simalenga na kuongeza "Tunafurahia uhusiano wetu wa kibishara kwa kipindi chote hiki kwani tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Vodacom pekee hivyotumejikuta tukiwa na M-Pesa pekee."

  Kwa upande Mkuu wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya M-pesa wa Vodacom Bw Jackson Kiswaga amesema kiasi cha Sh. Bilioni Moja na Milioni Mia Nne kinapitia katika mfumo wa M-pesa kama ada ya uombaji wa mikopo kila mwaka.

  "Tumekuja kubadilishana uzoefu na wenzetu juu ya uhusiano wetu unaotuunganisha kupitia huduma ya M-pesa, bodi hii imekuwa sehemu muhimu kwetu kibiashara na tunatarajia kuimarisha zaidi huduma hii siku zijazo."Kiswaga aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
  Kiswaga amewakumbusha waombaji wa mikopo wa bodi hiyo ya elimu ya Juu kuendelea kuitumia huduma ya M-pesa katika kulipia ada ya uombaji kwa kuwa ndio njia rahisi na ya kuaminika zaidi kwao inayowapunguzia gharama za usafiri,muda na usumbufu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi hiyo Bw. Juma Chagonja amesema bado zipo fursa nyingi bodi inazoweza kuzitumia kwenye huduma ya M-pesa na kuwataka wananchi kuvuta subira kuona mambo mazuri zaidi siku chache zijazo.

  0 0

  Diamond akilonga na Sauda kuhusu shoo kali atakayotoa Usiku wa Matumaini 2013.
  Sauda na Diamond wakiwa mbele ya kamera.
  Platnumz akijiaandaa kabla ya mahojiano.
  ...Akibadilishana mawazo na Sauda kabla ya kuanza mahojiano.
  Mtu wa kamera akiwa mzigoni.

  Na Wilbert Molandi.

  MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya shoo kali ikiwemo kumfunika msanii wa Uganda, Prezzo katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.  Diamond ametoa majigambo hayo wakati wa mahojiano na Mtangazaji wa kituo cha Star TV, Sauda Mwilima. “Nimeahidi kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha la Matumaini siku hiyo, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi.

  “Ninataka kudhihirisha ubora wangu siku hiyo kwa kumfunika vibaya Prezzo,” alisema Diamond.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi vifa vya michezo kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindao ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika ukumbi wa mikutano wa TFF leo Jumatoano Juni 19, 2013.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando Akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zinazoshiriki mashindao ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.

  =======   =======  ======  ======
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wamekabidhi jezi, vikinga ugoko, mipira na soksi kwa timu za chini ya umri wa miaka 17 zitakazoshiriki kwenye michuano ya Airtel Raising Stars ngazi za mkoa ambayo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbia kuanzia Juni 23, 2013.

  Mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni wataingiza timu za wasichana na wavulana kwenye mashindano hayo huku Mwanza, Morogoro na Mbeya wakileta timu za wavulana pekee wakati mikoa ya Tanga, Ruvuma na Kigoma ikishirikisha timu za wasichana tu.

  Timu zote zimeonyesha mwitikio na hamasa kubwa kwa kuwa na maandalizi ya awali kwa ajili ya kushindana na kushinda katika michuano hiyo. Michuano ya mikoa itafuatiwa na fainali za taifa ambazo zitapigwa kwenye uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

  Akiongea na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya vifaa yailiyofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema Airtel wanajivunia kuwa sehemu ya programu ya kuendeleza vijana katika soka la Tanzania.

   “Tunaamini kuwa ushirikiano wetu na timu ya Manchester United pamoja na TFF utachangia maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Tunaimani vijana wanaweza na ndio maana tunawapa nafasi na kuwasaidia ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye medani ya soka, “ alisema.

  Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema amefurahishwa na mwitikio ulioonyeshwa na vijana waanaoshiriki kwenye michuano ya Airtel Raising Stars. “Michuano ya Airtel mwaka huu imekuwa na msisimko mkubwa, tunawashukuru Airtel kwa kudhamini michuano hii ambayo inatusaidia kubaini zaidi vipaji vilivyojificha“, alisema Kayuni. 

  Programu hii ya Airtel Rising Stars ilimeandaliwa mahsusi kwa vijana wa bara la Afrika, kwa lengo la vijana wanaochipukia katika soka kuonyesha vipaji vyao na kupata nafasi kupata mafanikio katika soka.
  Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita cha programu hii timu ya Manchester United walituma walimu wa mpira kwa ajili ya kliniki kwa wachezaji katika nchi za Tanzania, South Afrika, Gabon na Kenya kwa wachezaji waliofanya vizuri na kuchaguliwa kwenye michuano hiyo walipata nafasi ya kufundishwa kusakata kandanda.

  Ili kuwahamasisha vijana, Airtel imeanzisha mashindano ya kimataifa ambayo mwaka jana yalifanyika kwa mara ya kwanza jijini Nairobi ambapo wavulana na wasichana walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Michuano hiyo ilishirikisha wachezaji nyota wa ARS kutoka nchi 14 ambazo kampuni hiyo inafanya biashara. 

  0 0  0 0

  Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana misuri na Nasibu Ramadhani wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika sikukuu ya Idi pili wengine kushoto ni mratibu Duni Lianjara Promota wa Mpambano huo Side Mkigoma na kocha wa Nasibu Christpher Mzazi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  PROMOTA WA MPAMBANO WA MASUMBWI SIDE MKIGOMA KATIKATI AKIWAINUA MIKONO JUU MABONDIA JUMA FUNDI KUSHOTO NA NASSIBU RAMADHANI
  Mabondia wakisaini mkataba

  0 0


  Habari, naitwa Suzanna, najitokeza kwenye blog yako kutafuta mchumba ambaye yupo serious ili Mungu akitujalia tufike kwenye ndoa. Natafuta mtu aliye serious ambaye anataka kuwa na familia hivi karibuni. Napendelea sana mcha mungu, awe mkristo, awe na elimu ya chuo kikuu. Awe na miaka kuanzia 36 mpaka 43, asiwe mlevi, asiwe malaya, awe na mapenzi ya dhati na ya kweli, asiwe na watoto wala mke. Mimi kwasasa naishi nje ya Tanzania kwenye nchi mojawapo za bara la Africa. Napatikana kwenye email:

older | 1 | .... | 104 | 105 | (Page 106) | 107 | 108 | .... | 1898 | newer