Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1055 | 1056 | (Page 1057) | 1058 | 1059 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Kufuatia Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Jenerali (Mst) George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA tarehe 29 Oktoba, 2016, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Profesa Jumanne A. Maghembe (Mb) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo kwa mujibu wa Sheria ya Uanzishwaji wa TANAPA Sura ya 282 Jedwali la Pili ikisomwa pamoja na kifungu cha 8(1)(b) cha Sheria hiyo.

  1)        Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania.
  2)     Dkt. Lucy Lugwisha, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi  
  wa Mazingira.
  3)        Kamishina Marijan M. Sato, Mkuu wa Operesheni  na Mafunzo,    Makao Makuu  Jeshi la Polisi.
  4)          Profesa Alexander Songorwa, Mkurugenzi wa Wanyamapori     kutoka   Wizara ya Maliasili na Utalii.
  5)          Profesa Wineaster Anderson, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar  es  Salaam, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii Endelevu Afrika (NARESTi Africa).
  6)          Bw. George Fumbuka, Mhasibu aliyethibitishwa ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya CORE Securities.
  7)        Dkt. Chanasa Mpelumbe Ngeleja, Daktari Mkuu wa Mifugo,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  8)     Bw. Allan J. H. Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA      

                    
  Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 29/10/2016 hadi tarehe 28/10/2019.

            IMETOLEWA NA:
                                               

  Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi
  KATIBU MKUU 
  WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII
  30 Novemba, 2016.  0 0

   Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionyesha kwa waandishi wa habari chupa mpya ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi  iliyofanyika jijini Mwanza leo.
   Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionja Chibuku super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi  iliyofanyika jijini Mwanza leo.
  Meneja Masoko wa TBL Group Oscar Shelukindo,akizungumza na waandisi wa kuhusiana na  muonekano mpya wa chupa ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Mwanza leo. kulia ni Meneja Kiwanda cha Chibuku Super Mwanza Herbert Ilembo.

  Mwanza Desemba 1,2016:Kampuni ya TBL Group, leo imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya ml 500, huku ikitoa wito kwa watanzania kutumia vinywaji vinavyozalishwa hapa nchini ili kujenga uchumi wa taifa kwa ujumla.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL Group, Bw. Oscar Shelukindo alisema uzinduzi wa bia hiyo ya Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi inayorudishwa (Returnable) unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko la Bia hapa nchini.

  “Leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu TBL na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani tumeweza kuzindua Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji Ubora wa hali ya juu, ina ujazo wa nusu lita na itauzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu, kwa chupa na 14,000 kwa kreti,’’ alisema.

  Akiizungumzia bia hiyo Shelukindo alisema inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mahindi na mtama bora toka kwenye ardhi ya Tanzania na hivyo kutoa kila sababu kwa watanzania kujivunia kinywaji chenye asili ya taifa lao.

  “Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachomfanya mtumiaji aweze kuitumia kwa muda mrefu akiwa na marafiki, lakini pia inampa lishe nzuri kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii,’’ aliongeza

  Akizungumzia juu ya usambazaji wa Bia hiyo, meneja mauzo wa TBL Bw. Fred Kazindogo alisema baada ya uzinduzi huo itaanza kupatikana Desemba 2 mwaka huu kwa wasambazaji wakubwa na katika baa mbalimbali na sehemu nyinginezo zinazouza vileo.

  Alisema kwa kuanzia Bia hiyo itaanza kupatikana katika mikoa 15 ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita, Tabora, Singida, Kigoma, Simiyu, manyara , Kilimanjaro, Arusha, Katavi, Mbeya na Rukwa.

  “Na kwa wauzaji wa jumla, tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina faida nzuri na inadumu kwa miezi 4 kwenye soko, muda ambao ni mrefu sana kulinganisha na products zetu nyingine,’’alisema

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Azzan Musa Zungu akiwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo ambapo kwa sasa hali yake inaendelea vizuri. Kutoka kulia ni Muuguzi Mwandamizi Sr. Chagui Mgaza na kushoto ni Mwinyi Maulidi ambaye ni dereva wa Mhe. Zungu.Picha na Anna Nkinda - JKCI.

  Na Anna Nkinda – JKCI.

  1/12/2016 Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Azzan Musa Zungu amewashukuru wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa huduma nzuri ya matibabu wanayompatia na kuiomba taasisi hiyo kutoa huduma kama hiyo kwa watanzania wote.

  Mhe. Zungu ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo amezitoa  shukrani hizo leo wakati akiongea na waandishi wa habari waliotaka kufahamu kuhusu maendeleo ya afya yake.

  “Namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri hali yangu siyo kama jana. Nilianza kuumwa majira ya saa nane  8:30 mchana nikiwa nyumbani katika mazingira magumu ambapo mapigo ya moyo yalipanda ghafla nikapelekwa Hospitali ya Amana na baadaye  Muhimbili  kitengo cha Huduma ya dharula majira ya saa 12jioni  kisha  nikaletwa  hapa”. 

  “Kwa namna ya pekee nawashukuru sana wafanyakazi wa Amana, Muhimbili na Taasisi ya Moyo ambao wamenipokea na kunipa  huduma nzuri na kama mnavyoniona afya yangu inaendelea vizuri tofauti na nilivyokuja jana”. alisema Mhe. Zungu.

  Aidha Mhe. Zungu aliwataka watanzania kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ambao hata yeye ni mwanachama  kwa kuwa mwanachama wa mfuko huu kutawasaidia kupata matibabu pindi watakapoumwa bila ya kutoa fedha  mfukoni.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema hali ya Mhe. Zungu  inaendelea vizuri tofauti na walivyompokea jana.  Hivi sasa madaktari wako katika uchunguzi wa matatizo ya Moyo baada ya hapo watajuwa tatizo na kumpatia tiba  na anaamini baada ya siku tatu zijazo anaweza kuruhusiwa.

  “Kipindi cha nyuma viongozi wenye matatizo kama haya walikuwa wanapelekwa  nje ya nchi kwa ajili ya matibabu  hivi  sasa Serikali imeboresha  huduma za matibabu ya Moyo  hivyo basi wagonjwa  wengi wanatibiwa hapa nchini”, alisema Prof. Janabi.

  Aliwashauri wananchi kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka, wakiona dalili za viashiria vya ugonjwa wa Moyo waende haraka  Kituo cha Afya kilichopo jirani kwa ajili ya matibabu. 

  Prof. Janabi alimalizia kwa kuwasisitiza wananchi kufanya  mazoezi na kula vyakula sahihi na kwa upande wa wagonjwa wa Moyo wanatakiwa kumeza  dawa kipindi chote cha maisha yao wasiache kunywa dawa kwani wagonjwa wengi wanaorudi kupata matibabu ni wale walioacha  kumeza dawa.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Azzan Musa Zungu akiwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo ambapo kwa sasa hali yake inaendelea vizuri. Kutoka kulia ni Muuguzi Mwandamizi Sr. Chagui Mgaza na kushoto ni Mwinyi Maulidi ambaye ni dereva wa Mhe. Zungu.Picha na Anna Nkinda - JKCI

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari. Katika mkutano huo Bi. Kasiga aliwaeleza Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Nne wa Mawaziri wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika Mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016. Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Afrika na Korea pamoja na maeneo mapya ya mashirikiano. 
  Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi akifuatilia mkutano kati ya Bi. Kasiga na Waandishi wa Habari. Wengine ni Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo. 
  Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza na kunukuu kwa makini mkutano uliokua ukiendelea 
  Mkutano ukiendelea.
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Afrika na Korea unaotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

  Mkutano huu ambao umeandaliwa na Serikali ya Korea kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika una lenga kukuza ushirikiano pamoja na kuandaa maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Korea na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu ijayo.

  Tanzania ni moja ya nchi nne (4) za Afrika ambazo Korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya kimkakati “strategic partnership” yatakayozifanya nchi hizo kupewa kipaumbele katika kupokea misaada na mikopo nafuu kutoka Korea katika kipindi cha miaka mitano ijayo kati ya 2016 hadi 2020.

  Katika kipindi hicho Tanzania itapokea kiasi cha dola za Kimarekani milioni 300 ikiwa ni asilimia 17.1 ya msaada utakaotolewa Barani Afrika, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza Barani humo kupata msaada wa Jamhuri ya Korea.

  Pamoja na ushiriki kwenye Mkutano huo, imependekezwa ufanyike mkutano baina ya Tanzania na Serikali ya Korea kuzungumzia masuala ya ushirikiano baina ya nchi zetu mbili. Aidha, ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa Afrika na Korea ni fursa muhimu ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu mbili hususan katika Nyanja ya uchumi. Serikali ya Korea ilitoa ahadi ya kuongeza uwekezaji Barani Afrika hususan katikasekta za nishati, miundombinu na viwanda.

  Itakumbukwa kuwa, tayari Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Mradi wa kuendeleza kilimo cha Mwani Zanzibar wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.6 na Awamu ya Pili ya Mradi wa kuboresha Uchunguzi wa Afya ya Uzazi Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni nne (4).

  Miradi mingine ambayo Jamhuri ya Korea inashirikiana na Tanzania ni ujenzi wa Daraja la Selander Jijini Dar es Salaam, Mradi wa Daraja la Kikwete kwenye Mto Malagarasi Mkoani Kigoma na Ujenzi wa Hospitali ya Kimataifa iliyopo eneo la Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

   Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 01Desemba, 2016.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo sekta ya Elimu, Afya na Kilimo. 
  Balozi wa Kenya hapa nchini, Mhe. Chirau Ali Mwakwere akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya 
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohammed (kulia) naye akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC. 
  Balozi Ben Ogutu, Kiongozi wa Ujumbe wa Kenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Kenya 
  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akizungumza wakati wa Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Kenya 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa mshereheshaji akizungumza, Bi. Mindi Kasiga 
  Sehemu ya wajumbe kutoka Kenya wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa JPC 
  Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano

  0 0

  Moja ya eneo la lililotumiwa na kampuni ya Polyphon Film ya nchini Ujerumani ikirekodi Filamu inayozungumzia maisha kwa ujumla eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti mkoa wa Mara na inatarajiwa kukuza utalii . 
  Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha(kushoto)Gabriel na Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouder wakiwa eneo la kutengeneza filamu hiyo itakayooneshwa kwenye kituo maarufu cha Runinga cha ZDF nchini Ujerumani na kutazamwa na zaidi ya watu 10 milioni katika nchi tatu zikiwemo Austria na Uswizi. 
  Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Manuel Shrouderk(kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa)Ndg Ibrahim Mussa(katikati) anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Hatari Lodge ya jijini Arusha,Gabriel. 
  Mratibu wa Uzalishaji wa kampuni ya Polyphon Film,Mona Lessink akizungumza na waandishi wa habari kuhusu filamu hiyo itayoanza kurushwa katika kipindi cha Pasaka mwaka 2017,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal shulutete akifatilia kwa karibu. 
  Sehemu ya magari yaliyobeba vifaa vya kutengeneza filamu hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Euro 1.7 milioni 
  Wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa eneo la kutengeneza filamu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti 


  Askari wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa Serengeti wakiimarisha ulinzi kwa wageni hao 
  Katika kuboresha filamu hiyo upigaji wa picha kwa kutumia ndege ndogo ili kuonyesha madhari ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ulifanyika chini ya usimamizi wa Tanapa.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhan Madabida kufuatia kifo cha Muasisi wa TANU Bibi Hadija Bint Kamba, kilichotokea jana tarehe 30 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

  Bibi Hadija Bint Kamba ni miongoni mwa wanaharakati waliopigania uhuru na ukombozi wa Taifa letu. Ameshiriki kuanzisha Baraza la Wanawake Tanganyika mwaka 1955 na baadae Umoja wa Wanawake wa Tanganyika (UWT) tarehe 02 Novemba 1962 akishirikiana na Bibi Titi Mohamed.

  Bibi Hadija hakuwahi kushika nafasi za uongozi ndani ya Chama na Serikali baada ya uhuru mpaka mwaka 1985 ambapo Mwalimu Nyerere alimtangaza mbele ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Baraza la Wazee wa Dar es salaam Diamond Jubilee, kuwa ni mtu aliyetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama na Nchi, tangu wakati huo Bibi Hadija Bint Kamba alihudhuria Mikutano mikuu ya Chama kama mjumbe mwalikwa mpaka umri ulipomzuia kuweza kushiriki.

  Bibi Hadija Binti Kamba, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa uadilifu, uvumilivu, ujasiri na mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania uhuru na kuleta ukombozi na maendeleo kwa Wanawake wa taifa hili utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.

  Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 

  Imetolewa na:- 


  Christopher Ole Sendeka (MNEC)
  MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
  01.12.2016

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo

  Kuelekea Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Serikali imepongezwa kwa Mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi chote tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wakati wa mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka hamsini na tano ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 9 Desemba mwaka huu.

  “Tumepiga hatua kubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu,Afya,Maji,usafirishaji na miundo mbinu ukilinganisha na wakati tunapata Uhuru” Alisisitiza Chongolo

  Katika Sekta ya elimu Chongolo anabainisha kuwa Serikali katika awamu zote tangu awamu ya kwanza hadi sasa zimekuwa zikiweka kipamaumbele katika Sekta hiyo hali iliyochangia kuongezeka kwa shule za msingi ,Sekondari na Vyuo Vikuu .

  Akifafanua zaidi Chongolo ameongeza kuwa elimu bure ni miongoni mwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuzidi kuendeleza azma ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kupamabana na maudui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasikini. 

  Akizungumzia kuhusu miundo mbinu ya barabara anabainisha Tanzania ya sasa ina tofauti kubwa na wakati Taifa lilipokuwa likipata Uhuru ambapo barabara za lami na madaraja yalikuwa machache lakini hivi sasa Mikoa yote inafikika kwa urahisi.

  Anaongeza kuwa sekta ya maji pia imeimarika ukilinganisha na wakati wa uhuru ambapo moja ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na Serikali ni mradi wa maji wa ziwa Victoria hadi shinyanga na mwingine ni ule wa upanuzi wa mitambo ya Ruvu juu na Ruvu Chini ambayo imeanza kumaliza tatizo la maji katika Jiji la Dar es salaam.

  Aidha Chongolo aliwaaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za Taifa na miundo mbinu iliyopo kwa maslahi ya taifa kwa kuwafichua wale wote wanaokwaamisha au kuhujumu nia njema ya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Sherehe za Uhuru huadhimishwa kila mwaka inapofika tarehe 9 mwezi Desemba ambapo mwaka huu Kitaifa zitafanyika Jijini Dar es salaam na Kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe mwaka mmpja uliopita.

  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa,Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo yetu.”

  0 0

  Mwenyekiti wa kampuni ya Uwekezaji wa Taifa (NICOl) Bw. Gideon Kaunda kulia akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya kupata uongozi mpya wa kampuni hiyo ulioteuliwa rasmi hivi karibuni na bodi ya NICOL kushoto ni Mtendaji Mkuu Bw. Adam Wamunza.


  Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii

  Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICOL) inatarajia kurudi upya mara baada ya kuingia hasara ya sh. Billion 10 pamoja na kukabiliana na kesi Mbalimbali ikiwemo  kupinga maamuzi ya wanahisa kuchagua uongozi pamoja na maamuzi ya kusitishwa kwa mkutano mkuu uliolenga kuzungumzia maswala ya mahesabu na muelekeo wa Kampuni.

  Akizungumza na waandishi wa Habari  Mwenyekiti wa NICOL Dk. Gideon Kaunda amesema kuwa kesi ya mwisho ya 41 iliamuliwa  mahakamani mara baada ya Mlalamika  makamu mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte kutokuhudhuria mahakamani na hoja hizo zilikataliwa na Mahakama kuamua kuwa mkutano huo ulikuwa wa halali na ambapo mnamo Novemba 26 mkutano huo uliendelea.

  “Mkutano ulikwenda vizuri ambapo zaidi ya watu 300 kutoka mikoa mbalimbali walihudhuria pamoja na mashirika mbalimbali ya umma ambayo yalikuwa yamewekeza  wakiwemo PSPF, walifanikiwa kuhudhuria”. Alisema Kaunda 

  Aidha alisema kuwa Kampuni hiyo iliingia hasara kutokana na  uongozi uliopita kuwa na malimbikizo ya sh. Billion 10 kutokana na mahesabu yaliyofanywa, ambayo taarifa ilionesha kuwa kampuni ilikuwa inapata faida kwa wakati huo  sio sahihi,pamoja na kutokufuatwa kwa sheria na utovu wa nidhamu.

  Kwa upande wake Mtendaji  Mkuu wa NICOL  Adam Wanuza amesema kuwa kuwa pamoja na hasara hiyo,ukiwemo uwekezaji mbovu umechangia kutokana na makampuni mbalimbali kuchukua mkopo katika Kampuni ya Nicol.

  Naye Naibu Waziri Mstaafu katika sekta ya Uchukuzi ambaye pia ni Mtaalamu katika Masuala ya Biashara Dk. Athumani Mfutakamba amesema kuwa kufanikiwa kwa Mkutano huu ni ishara tosha ya kuzaliwa upya kwa NICOL katika jitihada za Kampuni ya uwekezaji ya kizalendo na jitihada hizi lazima ziungwe mkono na wazalendo wote wanaotaka maendeleo ya uchumi wa Taifa la Tanzania katika fursa mbalimbali.

  Kampuni ya Nicol itarudi Rasmi kupitia uongozi mpya sambamba na kuanza kutoa elimu Maalumu kwa wawekezaji katika soko la Hisa mnamo mwanzoni mwa mwaka 2017.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi, akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa Muasisi wa TANU, Khadija Kamba, katika makaburi ya Kisutu, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, Desemba 01, 2016, katika makaburi hayo mjini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwaga udogo kaburini wakati wa mazishi ya Muasisi wa TANU, Khadija Kamba, katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, leo Desemba 01, 2016. Nyuma yake ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi. (Picha na Bashir Nkoromo).

  Na Bashir Nkoromo.
   
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameongoza mamia ya wananchi katika maziko ya muasisi wa chama cha Tanganyika African Union (TANU) na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khadija Kamba, aliyefariki juzi na kuzikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

  Kinana ambaye alifuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akitoa salam za zambirambi za Chama, alisema, CCM itamkumbuka na kuuenzi daima mchango mkubwa alioutoa hasa wakati wa harakati za ujenzi wa TANU na harakati za ukombozi wa Tanzania wakati wa uhai wake.

  "Binti Kamba alikuwa ni nguzo na chachu muhimu katika kuasisiwa kwa TANU na mpambanaji aliyekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutafuta Uhuru wa nchi hii, hivyo Chama kitambukumbuka na kumuenzi daima Mama huyu", alisema Kinana, wakati akitoa salam za rambirambi wakati wa maziko.

  Kinana alisema, licha ya kuwa muasisi, lakini Binti Kamba kamtika maisha yake, aliendelea kuwa nwanachama na kada mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi na kuendelea kuwa kisima cha kuchota hekima na maarifa hadi anafariki dunia.

  Alisema, kutokana na kuguswa na msiba huo, kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu wa Chama, ameandaa hitima itakayosomwa keshokutwa katika Msikiti wa Masjid Quba, kumuombea maghfira.

  Binti Kamba, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 94, alifariki juzi asubuhi, nyumbani kwa mwanae wa kulea, Kamba Abdallah, jijini Dar es Salaam.

  Msafara kwenda kwenye maziko Kisutu ulianzia nyumbani kwa marehemu, Ilala Bungoni, Dar es Salaam, baada ya kuswaliwa, ambako miongoni mwa waombolezaji waliokuwepo ni pamoja na Muasisi mwingine wa TANU Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye mwaka jana alihamia Chadema kumfuata aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Edward Lowassa.


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera  na Katibu Tawala wa Mkoa  huo , Eliakim Maswi  (kulia) wakati  aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha, Desemba 2, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Manyara wakati aliposimama kwa muda mjini Babati akitoka Dodoma kwenda Arusha Desemba2, 2016.

  0 0

   
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo baada ya kuwasili jijini Arusha kuanza ziara ya kazi mkoani humo Desemba 1, 2016.Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Iddi Kimanta baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.
   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige  baada ya kuwasili jijiniArusha kuanza ziara ya kazi Desemba 1, 2016.

  0 0

   Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

   Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo hicho.
   Mwonekano wa ukumbi wa mikutano wa kituo hicho.
   Katika hafla ya kufungua kituo hicho nyama choma zilikuwepo ingawa mimi sikubahatika kupata walau finyango moja.
   Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, akisalimiana na 
  wageni waalikwa.
   Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wengine akitoka kukagua vyumba vya kupumzikia vya kituo hicho.
   Wanataalumu ya Uhasibu wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa kituo hicho pamoja na kongamano lao la 2016 la siku tatu.
   Wasanii Mpoto Mrisho na Banana Zoro wakitoa burudani 
  kwenye hafla hiyo.
   Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo, akitoa taarifa fupi.
   Mkutano ukiendelea.
   Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi.
   Picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa bodi ya NBAA na Mfuko wa GEPF
  Picha ya pamoja.


  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imeitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kutoa hadharani majina ya wahasibu wabadhilifu ili jamii iweze kuwatambua.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizindua Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju na  Kongamano la Uhasibu la 2016 la siku tatu Dar es Salaam leo.

  "Ni vizuri mkaanza kutoa hadharani majina ya wahasibu wasio waadilifu ili jamii iweze kuwajua" alisema Mpango.

  Mpango alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaisaidia serikali kuelekeza fedha zilizokuwa zikitumika na bodi hiyo kukodi kumbi kwa kazi zake mbalimbali kupelekwa kufanya kazi zingine za maendeleo.

  "Nawaombeni mkitunze kituo hiki ili kitimize malengo yake ya kuleta manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla" alisema Mpango.

  Aliwataka wahasibu nchini kutumia taaluma yao kuisaidia serikali hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda badala ya wao kushirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuiibia serikali.

  Mpango alisema kuwa serikali itaendelea kuwatumbua watumishi wasio waaminifu na wahasibu bila ya kumuonea muhusika huruma na kuwa atakayebainika atapelekwa mahakama ya mafisadi iliyofunguliwa.

   Mkurugenzi Mkuu wa NBAA Pius Maneno alisema katika kipindi cha maiaka 12 iliyopita walikuwa wakitumia sh. biliobi 1.5 kwa ajili ya gharama za kulipia kumbi hivyo ujenzi wa kituo hicho utaondoa changamoto hiyo na kuwa kitakuwa ni chanzo cha mapato.

  Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA Profesa Isaya Jairo alisema kituo hicho kimejengwa kwa mkopo wa sh.bilioni 15 kutoka Shirika la Hifadhi ya Taifa (NSSF), Mfuko wa GEPF bilioni 10 na Wahasibu na Wakaguzi walichangia Bilioni 8.

  Alisema awali walikadiria ujenzi huo ungekamilika kwa gharama za sh. bilioni 14 lakini kutokana na sababu mbalimbali kukamilika kwake kumefikia sh. bilioni 33 zaidi ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.

  Mwenyekiti wa Bodi wa GEPF Joyce Shaidi aliishukuru serikali kwa ushirikiano na mifuko ya jamii na NBAA  hasa katika suala zima la kusukuma maendeleo ya nchi ikiwa na kuzitaka taasisi zake kwenda kukodi ukumbi wa kituo hicho cha kimataifa ili kusaidia kurejesha fedha zilizokopwa kukijengea.


  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage  akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ongezeko la wawekezaji nchini katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
  JUMLA ya ajira 16,671 zimetengenezwa na viwanda vya uzalishaji nchini ambapo viwanda vya wawekezaji kutoka nje ya nchi vikiongoza kwa utoaji wa ajira hizo.

  Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu ongezeko la wawekezaji nchini kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

  Waziri Mwijage amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanya juhudi za kuwahamasisha wawekezaji ili waweze kushiriki katika kuchochea mageuzi ya kiuchumi hivyo imeanza kupunguza uuzaji wa malighafi nje ya nchi ikiwa ni njia mojawapo ya kuwavutia wawekezaji kuwekeza nchini.

  ”Katika kujenga uchumi wa viwanda, tunalenga kujenga uchumi shirikishi na ulio endelevu ambao utahusisha watu wengi hivyo utaratibu wa aina hiyo utawasaidia kuwainua wananchi kiuchumi pamoja na kukuza pato la taifa,” alisema Mwijage.

  Kwa mujibu wa Mwijage ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, takwimu zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la uwekezaji katika sekta za ujenzi wa majengo, maliasili, rasilimali watu, viwanda vya uchakataji bidhaa, sekta ya nishati, kilimo, huduma, usafiri pamoja na mawasiliano.

  Aidha, amezitaja sekta zingine za uwekezaji ambazo zinaongoza kwa uzalishaji wa ajira kwa wingi kuwa ni majengo ya biashara ambayo yanazalisha ajira 5537, sekta ya utalii ajira 2011 pamoja na sekta ya huduma inayozalisha jumla ya ajira 680.

  Akizungumzia kuhusu ubora wa makaa ya mawe, Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, John Shija amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na makaa ya mawe ya kutosha ya kuweza kuchimbwa na kutumiwa kwa zaidi ya miaka 200.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda, Mhandisi Lugano Wilson amesisitiza kuwa kati ya nchi zinazozalisha makaa ya mawe zikiwemo za India, China na Afrika ya Kusini, nchi ya Tanzania ndiyo inayoongoza kwa kuwa na makaa ya mawe yenye ubora unaokubalika.

  0 0
 • 12/01/16--07:44: New VIDEO | Esaya - Maumivu

 • 0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS). 
  Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
  Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
  Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
  Semina ikiendelea kwa wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela. 
  Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack. 
  Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack.

  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa laini maalumu za simu za mkononi kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo zitakazokuwa na gharama nafuu za matumizi ya mtandao wa intaneti na ofa mbalimali za matumizi ya simu kuwawezesha wanafunzi kutumia mtandao kwa masomo yao. 

  Akizungumzia ofa hiyo maalum iliyotangazwa kwenye semina kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Biashara Mlimani wa mwaka wa kwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela alisema ofa hiyo kwa wanafunzi wa chuo imetolewa baada ya TTCL kusikiliza ombi la wanafunzi juu ya kupunguziwa gharama hasa kwenye intaneti kwa kuwa hutumia mtandao huo kujipatia masomo.

   Bi. Mwajalebela alisema laini hizo kwa wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la 'Boompack', ambapo wanafunzi wa chuo watakuwa na fursa ya kupata huduma za vifurushi vya bei nafuu, ujumbe mfupi wa simu 'SMS' za kutosha na muda wa maongezi ambao kiujumla utarahisisha huduma kwa matumizi yao.

   "leo na Hivyo basi, tunapenda kuwatangazia kuwa TTCL inatoa laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack, wanafunzi wanafursa ya kupata huduma za vifurushi vya bei nafuu, SMS za kutosha na muda wa maongezi. Laini hii ni maalumu kwa wanafunzi na tumeanzisha ili kutoa fursa kwa wanafunzi kutumia intaneti kwa ajili ya kushughuli za kimasomo na kuimarisha mawasiliano miongoni mwa wanafunzi. 

  Pia, tumeongeza radha zaidi wanafunzi waweza kuchagua vifurushi vya Siku, Wiki na Mwezi. Zaidi na zaidi, Kwa wanafunzi watakajiunga na kifurushi chochote watapata fursa ya kuperuzi facebook, Instagram, Whatsapp na E-mail Bure," alisema Bi. Mwajalebela. Aliongeza kuwa TTCL inaamini kuwa wanafunzi watatumia huduma hiyo kikamilifu ili kuimarisha mawasiliano miongonu mwao, kutumia intaneti kwa ajili ya kutafuta taarifa za kimasomo, kupata taarifa za maendeleo na kutumia fursa hiyo kuongeza wigo wa maarifa kwa kushirikiana na vyuo vingine ndani na nje ya Tanzania. 

  Awali ya yote, naomba kuchukua nafasi hii kushukuru sana Uongozi wa DARUSO- University of Dar es salaam Business School (UDBS) kwa kutualika TTCL ili tuweze kushiriki nanyi kwenye tukio la leo la kuwakaribisha wanafunzi ambao wamejiunga Mwaka wa Kwanza. 

  Kwa niaba ya Menejimenti ya TTCL, inapenda kuwapongeza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tunaamini ni fursa yenu pekee ambayo mnapaswa kuitumia kikamilifu ili muweze kujijenga wewe binafsi na kutumia elimu hiyo kujenga Taifa letu. Pia, tunafarijika sana kuona wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kupitia DARUSO-UDBS kutuamini na kutambua mchango wa TTCL katika kuimarisha mawasiliano ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, kukuza uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo nchini. 

  Tunaimani kuwa wanafunzi na uongozi wa Chuo mtakuwa mstari wa mbele katika kutumia huduma za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Alisema Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) ilianzishwa mwaka 1994 ambapo inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100. Kampuni hii inatoa huduma za mawasiliano ya simu ya mezani, simu za mkononi na intaneti kwa wateja wa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Kampuni hii imekuwa mhimili mkuu wa mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

  Na hii inatokana na uwezo wake wa kuunganisha nchi za jirani kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo TTCL ndio Msimamizi kwa niaba ya Serikali. Nchi hizo ambazo zimeunganishwa kwenye Mkongo wa Tafa ni pamoja na Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya, Malawi na Zambia. Aidha, Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inamiliki Kituo cha Mawasiliano cha Intaneti- TTCL IP-Pop ambacho kinatoa huduma ya intaneti kwa wateja kutoka ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania. Kituo hiki kimekua msaada mkubwa, hivi sasa Intaneti inapatikana hapa hapa Tanzania hakuna tena haja ya kwenda kununua intaneti Ulaya au kwingineko. Alisema kuwa TTCL ni kampuni pekee yenye mtandao ambao umeenea nchi nzima, hivyo kutoa fursa kwa taasisi za Umma na Binafsi kutumia miundombinu hiyo kukuza biashara na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi. 

  TTCL imefanikisha kuuganisha Taasisi za Umma na Binafsi katika Mkongo wa TTCL ambao umeunganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; wateja hao ni pamoja Taasisi za fedha-Benki, watoa huduma za Afya, watoa huduma za elimu, watoa huduma za Mawasiliano (service providers), watoa huduma za usafiri, wafanyabishara wadogo na wakati (SMEs). 

  Mwaka 2014, Kampuni ilianza kutekeleza mkakati kabambe wa kuleta mageuzi ndani ya kampuni, kuongeza uwajibikaji, kukuza biashara na kuboresha miundombinu ya mawasiliano. Mkakati huu umekuwa na manufaa kwa Kampuni kutokana na kufanikiwa kuboresha huduma za simu za Mkononi. Hivi sasa Kampuni hii inatoa huduma za simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti. Kwa simu za mkononi ambazo vijana wengi wanatumia zaidi,

   TTCL inatoa huduma hiyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya 4.5G ambayo inatoa intaneti yenye kasi zaidi, bei nafuu na bora zaidi. Pia, wateja wetu wanapata fursa ya kupiga simu kwa bei nafuu zaidi. Huduma hii tumeanza katika jiji la Dar es salaam na tuko kwenye mchakato wa kukamilisha huduma hiyo katika jiji la Mwanza, Arusha Mbeya na Dodoma pamoja na mikoa mingine itafuata.

  0 0


  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu siku ya UKIMWI Duniani, kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dr. Hamis Mwinyimvua.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko akifafanua juu ya takwimu za maambukizi ya UKIMWI wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.

   
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.

  Waziri Mhagama alisema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

  “UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizo mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu”

  Kwa mujibu wa Waziri Mhagama alisema Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani kuhakikisha wanatokomeza janga la ugonjwa huo  ifikapo mwaka 2030.

  Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

  ”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

  0 0

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa katika kituo cha kupima na kutoa Elimu ya ugonjwa wa Ukimwi kilichopo Mdaula, Chalinze akitolewa damu kwa ajili ya kupima virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi jimboni humo ikiwa ni siku ya Ukimwi Duniani.
  Mbunge Ridhiwani akizungumza na wananchi walijitokeza kituoni hapo hawapo pichani katika siku ya Ukimwi Duniani.Katika zoezi hilo watu walijitokeza i kupima wakiongozwa na Mbunge wao, watu watatu waligundulika kuwa na maambukizi virusi vya HIV kati ya watu 81 waliojitokeza kupima..

older | 1 | .... | 1055 | 1056 | (Page 1057) | 1058 | 1059 | .... | 1898 | newer