Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

TANGA YAWATAKA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI INDIA KUWEKEZA ILI KUWEZA KUNUFAIKA KUTOKANA NA UWEPO WA RASILIMALI NYINGI ZILIZOPO

$
0
0

Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.
Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye
Balozi wa India nchini Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye katikati wakati wa kongamano la wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga uliofanyika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga wakimfuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara juzi kwenye ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort


KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka nchini India kuwekeza mkoani hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo kilimo,utalii,elimu na Afya ili kuweza kunufaika nazo.

Mwilapwa alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na Mkoa wa Tanga.

Kongamano hilo lilikuwa na lengo lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza kuleta tija ya kimaendeleo.

Alisema kuwa India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya ukuaji wa maendeleo.

“India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo “Alisema.

Awali akizungumza Balozi wa India nchini, Sandeep Arya alisema ujio wa Waziri Mkuu wa India Tanzania umeongeza ari kwa Taifa ilo kuona haja ya kuendelea kuwekeza na kusaidia katika masuala mbalimbali ya afya, Elimu Bishara na Kilimo.

Alisema kuwa soko la India linahitaj bidhaa zenye ubora na rahisi hivyo anaamini kutokana na ushirikiano wa nchi hizi mbili kufanana mahitaji kutakuwepo na fursa kubwa ya muingiliano wa kibiashara ambao utaleta tija na faida kwa pande zote mbili.

Hata hivyo alisema licha kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, matibabu ya kansa lakini wanatoa nafasi 350 za mafunzo nchini india kila mwaka ili kuwapatia nafasi watu kujifunza jinsi India inavyofanya kazi katika shughuli zake za uzalishaji.

Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikaribishwa kuzungumza alisema moja kati ya mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ni kuhakikisha inakuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi wa hali ya nchi hivyo hakuna haja ya wananchi kukata tamaa.

Nape alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuzitumia fursa zilizopo hapa nchini ili kuhakikisha zinaleta manufaa kwa wananchi kwa kukuza vipato vyao na hata kuongeza pato la Taifa. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATETA JAMBO NA MCHECHU WA NHC

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kwenye chumba cha watu mashuhuri cha uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dr es salaam Novemba 28, 2016. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu kwenye uwanja wa ndge wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HOJA YA HAJA: MATAMSHI MBALIMBALI YANAYOENDELEA HIVI SASA KATIKA SEKTA YA ELIMU; JE YANALENGA KUDUMISHA ELIMU AU YATABOMOA MISINGI IMARA YA SASA YA ELIMU??

$
0
0
Hivi karibuni kumetokea matamshi mbalimbali kuhusu mfumo mzima wa sasa wa elimu ya Tanzania; Baadhi ya hayo matamshi ni kitendo cha kutaka kubadili mfumo wa elimu kwamba eti kusomea degree ni lazima mwanafunzi awe amepitia kidato cha 6 pekee na si vinginevyo. 

Kwa Mataifa makubwa na yenye nguvu duniani kama Uingereza na mengineyo Mwanafunzi ana uhuru wa kusomea degree endapo kama anayo HND (Higher National Diploma) mfumo ambao ni sawa sawa na moja ya mfumo wa Sasa wa Tanzania ambao Mwanafunzi mwenye Diploma anaweza akasomea Degree.

Kwa mtazamo wangu endapo Mwanafunzi alishindwa kusomea Form 5 and 6 kutokana na Sababu zozote zile then baadae akaweza kujiendeleza kwa kusomea Cheti alafu Diploma ni sawa sawa na kumpatia a Second chance huyu Mwanafunzi aliyeshindwa kipindi cha nyuma; vile vile kumpatia Mwanafunzi huyu hii second chance kuna ongeza ongezeko la raia wenye elimu nchini Tanzania na kudumisha ustawi wa Taifa kwa kuwa na wananchi wengi wenye elimu na kufikia ndoto za kufanikikisha kuwa Taifa lenye Viwanda na human resource wenye competent skills.

Kutaka kuvunja mfumo wa Sasa sio jawabu pekee kwani Form 5 na 6 sio kitu cha ajabu; Cha msingi ni kuhakikikisha vyuo vinavyotoa certificates and diploma hivi sasa viwe na viwango vikubwa vya kutoa elimu iliyo bora ambayo inatakiwa. Kama mataifa makubwa kama Uingereza yenye elimu bora na kubwa duniani yanafuata mfumo wa HND (Higher National Diploma) then Degree; Je ni kwanini Tanzania ione mfumo huu ni mbaya??

Je kuleta haya mabadiliko ya haraka haraka kila kukicha bila ya kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu na kushindwa kuongeza viwango vya elimu kwa kudumisha mfumo uliopo hivi sasa na kuongeza ubora wa elimu ya Tanzania ndio tuseme kutaongeza takwimu na ubora wa elimu nchini Tanzania??

Tukiwa tunabadili badili mifumo kila waziri mpya wa elimu anapobadilishwa au utawala unapobadilika je tunalipeleka wapi Taifa la Tanzania.

Elimu ya Tanzania ni swala muhimu na very sensitive na tukitaka Taifa la Tanzania kuwa kubwa duniani na lenye nguvu swala hili hasiachiwe mtu mmoja pekee kufanya maamuzi bali wadau wote kwenye sekta ya elimu na wananchi kwa ujumla washirikishwe.

Wadau wa elimu msikae kimya na kufumbia macho matamshi yanayoendelea na muweze kutoa maoni yenye kuendeleza elimu ya Tanzania kwa manufaa ya Watanzania na kwa Taifa hapo baadae.

RAIS WA CHAD IDRISS DEBY AONDOKA NCHINI, AAGWA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
 Rais wa Chad, Idriss Deby akipokea heshima kwenye uwnja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati alipoondoka nchini Novemb 28, 2016.  Kushoto kwake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alimsindikiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Chad, Idriss Deby kwenye uwanja wa ndege wa Julius kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo kuondoka nchini Novemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam wakati Rais huyo alipoondoka nchini Novemba 28, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Rais wa Chad, Idriss Deby  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati Rais huyo alpoondoka nchini Novemba 28, 2016. 
 Rais wa Chad, Idriss Deby akiwapungia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam wakati alipoondoka nchini Novemba 28, 2016. Kulia ni  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ambaye alimsindikiza na kushoto ni mke wa Rais wa Chad, Hinda Deby.

UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM

$
0
0

Na Dotto Mwaibale

UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umewasili nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema ziara ya ujumbe huo hapa nchini ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa na kiongozi wa Taifa hilo Hayati Mao  Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Wilaya ya Temeke na Zanzibar umewasili nchini kufuatia ziara ya baadhi ya makada wa CCM walipokwenda nchini China ambapo walijifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho kutoka China ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

" Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi nyingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba,  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa" alisema Chana.

Alisema wenzetu wa China wapo karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao hapa nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyonayo.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,  Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 Mkutano ukiendelea.
 Wajumbe hao wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
 Makada wa CCM wakijumuika na wajumbe wenzao kutoka china.
 Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Pindi Chana (kushoto), akizungumza na wajumbe hao.
 Madabida akiwakaribisha wajumbe hao.
Karibuni wajumbe kutoka China.

RC GAMBO ATOA PIKIPIKI 200 KWA WANDESHA BODA BODA ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.

Nteghenjwa Hosseah

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.

Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki baada ya kukutana na kundi hili la waendesha boda boda kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda boda hizo.

Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa muda umefika kwa kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Katikati) akiwasili kwenye Kikao na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha.

“Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.

Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi hii kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa chombo bila ya riba yeyote wala dhamana.
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Aliendelea kusema utoaji wa Pikipiki hizi utazingatia Kata zote zilizopo katika Jiji la Arusha ili Pikipiki ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili litaendelea kwa vijana wengine kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi kwa wote watakaopata Pikipiki hizi ili waweze kurejesha Fedha kama inavyotakiwa na tuweze kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie vijana wote wenye uhitaji wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.

Serafini Shirima ni dereva wa boda boda Kata ya Levolosi akizungumza katika Kikao hicho alisema kwa mara ya kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi anayetambua na kuthamini kazi ya boda boda na aliyethubutu kuwatafutia Pikipiki za bei nafuu ili kuongeza kipato cha vijana wa Arusha.

Shirima alishauri kuundwa kwa kamati ya mpito itakayosimamia na kuratibu mchakato mzima wa vijana watakaoanza kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha taratibu zote za uanzishaji wa umoja wa wandesha Boda boda utakaofahamika kwa jina la (UBOJA) chini ya Mlezi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akihitimisha kikao chake na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.

RC Gambo alikamilisha Kikao hicho kwa kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito kutoka katika Kila Kata na hatimaye kupatikana viongozi watano watakaoratibu mpango wa awali wa utoaji wa Pikipiki kwa vijana.

Pikipiki zitakazotolewa katika awamu ya kwanza ni 200 zikiwa na thamani ya Tsh Mil 400 na zitatolewa sanjari na Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata itatakiwa kutoa vijana 8.

Vijana wa Arusha watakabidhiwa Pikipiki hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa tarehe 03/12/2016 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau kwenye Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Serafini Shirima(aliyesimama) ni dereva wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa umoja wa wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA).
Viongozi wa mpito waliochanguliwa kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.

VETA yatoa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 200 kata ya Bunju

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAJASIRIAMALI zaidi ya 200 katika Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam wamepata mafunzo ya siku 10 katika ujuzi mbalimbali ili kuwasaidia kukuza ujasiriamali na kuongeza kipato katika familia na jamii kwa ujumla. 

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Dar es Salaam kuanzia tarehe 14 hadi 25,November 2016 chini ya Mpango wa Kukuza Ujasiriamali katika Sekta isiyo Rasmi (INTEP) na yalihusisha stadi za utegenezaji wa Batiki, Mapishi, Mapambo na Ufundi wa Upakaji rangi.

Akizungumza katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo siku ya Ijumaa November 25, 2016 Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike alisema, mafunzo hayo yameongeza fursa ya ajira kwa wananchi wake na kuiomba VETA kuendelea kutoa mafunzo ya namna hiyo zaidi kwani yatawasaidia wananchi wa kawaida kwa kiasi kikubwa.

Alisema, waliopata mafunzo ni watu ambao walikuwa hawana shughuli yeyote ya kuwaingizia kipato hivyo kupata mafunzo yameonyesha njia ya kuweza kuingia katika soko la ajira kwa kuanzisha biashara mbalimbali.

Shumasike aliwaasa wanufaika wa mafunzo kutumia vyema vyeti walivyovipata na kuidhihirishia jamii kuwa ujuzi walioupata ni wa manufaa makubwa kwao na kwa jamii inayowazunguka na sio kurudi katika hali waliyokuwa nayo mwanzo.

Alisema fedha ya ahadi ya Rais iliyotolewa kwa kila mtaa kunufaika na sh. Milioni 50 kwa ajili ya wajasirimali zitatolewa kwa vikundi na sio kwa mtu mmoja mmoja hivyo wajiandae kwa kutengeneza vikundi na kuvisajili ili fedha hizo zitakapowasili waweze kunufaika.

Naye Mkurugenzi wa Kanda ya VETA Dar es Salaam, Habib Bukko alisema anaamini waliopata mafunzo hayo watayatumia ipasavyo katika kubadilisha maisha yao na kwamba VETA inaendelea na juhudi za kuhakikisha mafunzo hayo yanafikia makundi mengi zaidi.

Mmoja ya walionufaika na Mafunzo hayo, Joyce Lweganwa amesema watatumia mafunzo hayo katika kutengeneza kipato na kuitaka VETA kufikia watu wengine kutokana na ukweli kwamba wahitaji wa mafunzo ya aina hiyo ni wengi sana katika jamii.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike akijionea bidhaa mbalimbali za batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo na VETA jijini Dar es Salaam.
.Sehemu ya wajasiriamali waliopata mafunzo ya mapishi wakionesha vyakula mbalimbali walivyoandaa baada ya mafunzo
Wahitimu wa mafunzo ya Upakaji rangi katika picha ya pamoja na Mtendaji wa Kata ya Bunju Shumasike Shumasike wakati wa kufunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.

Moja ya kazi waliyoifanya wahitimu wa mafunzo ya upambaji waliopata mafunzo kutoka VETA kama bwana harusi na Bibi harusi .

Afisa Mtendaji wa Kata ya Bunju katika picha ya pamoja na wajasiriamali waliopata mafunzo ya utengenezaji batiki yaliyotolewa na VETA.

NSSF YAWAONDOA WAPANGAJI WALIOSHINDWA KULIPA KATIKA NYUMBA ZA KIJICHI

$
0
0
 Vyombo vya baadhi ya wakazi wa nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam vikitolewa nje baada ya wamiliki wa nyumba kushindwa kulipia nyumba hizo kwa mujibu mikataba waliyokubaliana na Shirika hilo. (Picha na Francis Dande).

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeendelea na kazi ya kuwaondoa wadaiwa sugu.


Wadaiwa hao ni wale walionunua nyumba na kushindwa kulipa deni lililobaki kwa muda uliopangwa.Akizungumza jjijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Radhia Tambwe, alisema kwamba nyumba hizo ni za Mtoni Kijichi.Radhia alisema kwamba kazi hiyo itafanyika kwa wadaiwa  saba.


“Wakazi wa nyumba zote hizo walitolewa na kampuni ya udalali ya Majembe Action Mart kwa kushirikiana na NSSF,”alisema.Aidha alisema kwamba wadaiwa hao waliondolewa katika nyumba hizo baada ya taratibu za kisheria kufuatwa hivyo nyumba hizo zitauzwa kwa watu wengine.


Aidha alisema kwamba kazi hiyo ni endelevu kwa wale watakaoshindwa kulipa madeni yao kama mikataba inavyosema.Shirika la NSSF limewataka walionunua ama kupanga nyumba kulipa kwa mujibu wa mikataba yao ili kuepuka adha ya kutolewa vyombo vyao nje na kupata hasara.

KINANA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CPC CHINA

$
0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (Wakwanza kushoto),  alipokutana naye na kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. Wapili ni Kaimu Balozi wa China hapa Nchini, Gou hao Domg. Na walioketi kulia, ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Katibu wa NEC, Sisa na Ushorikiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama. (Picha na Bashir Nkoromo)

WAKAZI 800 WA KEREGE WAPATA HUDUMA ZA BURE ZA MATIBABU YALIYOANDALIWA NA KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY

$
0
0
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu bure likiendelea katika mji huo wa Kerege.
Zoezi la Kambi hiyo ya matibabu na upimaji bure likiendelea katika mji huo wa Kerege.
Mmoja wa wananchi wa Kerege (kulia) akipima macho katika kambi hiyo.

Klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na madaktari na wafanyakazi wa kujitolea wametoa huduma za matibabu kwa wakazi wa Kerege wilayani Bagamoyo. Kambi hiyo ya matibabu imeeefanyika Jumapili tarehe 27 Novemba katika shule ya Msingi ya Kerege.

Vipimo na matibabu vilitolewa bure kwa magonjwa kama vile malaria, upungufu wa damu, kisukari na shinikizo la damu, masikio, pua na koo (ENT), magonjwa ya ngozi, macho pamoja na meno. Huduma nyingine zilizotolewa zilikuwa pamoja na ugawaji wa miwani zilizotolewa kwa watu waliokutwa na matatizo ya macho.

Huduma za ushauri kwa wajawazito na vifaa vya kujifungulia vilitolewa bure kwa wajawazito; huduma za ushauri nasaha na upimaji wa UKIMWI pia zilitolewa. Kwa mara ya kwanza, elimu ya usafi na taulo za wanawake zilitolewa kwa wasichana.

Akizungumza katika kambi hiyo, Alfred Woiso, Rais wa Klabu ya Rotary ya Oyster Bay alisema, “Ni furaha yetu kuwa hapa kwa mara nyingine tena na tunafurahi kuona wakazi wa Kerege wamejitokeza kuja kupata huduma hizi. Tumetoa huduma kwa watu waliokuwa na matatizo mbalimbali. Tumeona wagonjwa wengi wenye magonjwa sugu kama kisukari na shinikizo la damu. Inaonekana kuna haja ya kupanua wigo wa huduma zetu kwa vile kuna mahitaji ya huduma za matibabu ya magonjwa mengine.”

Kambi hiyo ya matibabu ilihudhuriwa na wagonjwa wapatao 800 kutoka Kerege na maeneo ya jirani. Kambi hii inayoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay imefanyika Kerege kwa mara ya sita sasa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa Kerege kupata huduma za matibabu, wakazi ambao kwa kawaida hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Kambi hiyo ya matibabu imedhaminiwa na Diamond Trust Bank na kuandaliwa kwa ushirikiano na Shree Hindu Mandal Hospital, Vital Supplies, Whitedent, vClick Concepts Inc, MAK Books and Brains, ABACUS Pharmaceuticals, Fazel Foundation na wanachama wa Klabu ya Rotary na Rotaractor.

WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI NA KUJADILIANA KUHUSU UMUHIMU WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kulia) alipotembelewa na balozi huyo leo Jijini Dar es Salaam ambapo walizungumza kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimueleza jambo  Balozi wa Denmark nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) alipotembelewa na balozi huyo leo ofisini kwake  Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Denmark nchini Bibi. Camilla Christensen (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) wakati wakijadiliana kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen.Picha na Lorietha Laurence

Na Lorietha Laurence-WHSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameeleza kuwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ipo kwa ajili ya manufaa ya kuendeleza sekta ya habari, wanataaluma na Taifa kwa ujumla. 
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa Denmark nchini  Bw. Einar Jensen ambapo aliuliza kuhusu malalamiko ya waandishi wa habari kupoteza ajira kufuatiwa kuwepo kwa sheria hiyo.

 Mhe. Nape alifafanua kuwa sheria hiyo imetoa kipindi cha muda wa miaka mitano kwa wanahabari wasiokuwa na shahada ya kwanza kuweza kujiendeleza kimasomo ili kukidhi sifa za mwandishi wa habari.

“Sheria hii tayari imeshasainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kwa  sasa tupo katika utaratibu wa kuweka kanuni mbalimbali ili kufidia sehemu zenye mapungufu” alisema Mhe. Nape 

Anaongeza kwa kueleza kuwa kuna faida mbalimbali zinazomsaidia mwandishi kunufaika na sheria hii  ikiwemo bima ya Afya na mfuko wa mafunzo kwa wanahabari ambapo watawezeshwa kupata mkopo wa kujiendeleza kielimu.

Naye Balozi wa Denmark Nchini Bw. Einar Jensen ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo nzuri na kuomba ofisi ya Ubalozi wa Denmarm kupatiwa nafasi ya kuweza kukutana na Waziri kwa ajili ya kupata elimu kwa kina kuhusu sheria hiyo. 

Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ilipitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika mkutano wake wa 5 mjini Dodoma na  kusainiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 16 Novemba mwaka juu.

Uongozi bora na matumizi bora ya fedha vimeiletea Tanzania maendeleo

$
0
0
Na. Lilian Lundo – MAELEZO

IMEELEZWA kuwa Uongozi bora na matumizi bora katika usimamizi wa fedha za Serikali ni miongoni mwa sababu zilizoiletea Tanzania maendeleo tangu ilipopata uhuru mwaka 1961.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika Mstaafu, Pius Msekwa wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kuhusiana na hatua ambazo Tanzania imepiga tangu ipate uhuru mwaka 1961.Msekwa alisema kuwa uongozi bora pamoja matumizi bora ya fedha ndizo nguzo kuu zilizoiletea Tanzania maendeleo yanayoonekana leo ambapo takribani sekta zote zimepiga hatua kubwa ukilinganisha na kipindi cha uhuru mwaka 1961. 

“Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 tulirithi vitu vichache kutoka kwa wakoloni ambavyo ni shule hospitali ya Muhimbili iliyokuwa ikijulikana kama Princess Magreth ambayo kwa sasa imepiga hatua na kuweza kufanya upasuaji wa moyo ambao haukuwahi kufanyika kwa miaka ya nyuma,” alifafanua Msekwa.

Alisema kuwa maendeleo yote hayo yametoka na juhudi za marais waliopita na aliyepo, katika uongozi wao ambapo wamekuwa wakipambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni ujinga, maradhi na umasikini.Aidha alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakipambana na maadui hao kulingana na fedha ambazo zimekuwa zikipatikana katika kipindi cha uongozi wao.

Msekwa aliwataka Watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokana na misingi aliyoiacha ambayo imeweza kutumiwa na viongozi wa nchi na kuendelea kuleta maendeleo ambayo Tanzania inajivunia hadi sasa.

MUHIMBILI KUANZA UCHUNGUZI NA KUTOA TIBA YA UGONJWA WA HOMA YA INI

$
0
0

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Homa ya Ini na Matumbo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk John Lwegasha akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuanza kwa uchunguzi na tiba ya homa ya INI (Hepatitis B) katika hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swani na Dk Eva Owisso wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Hedwiga Swai akifafanua jambo kwenye mkutano huo leo.

 Waadishi wa habari wakimsikiliza Dk Lwegasha wakati akifafanua kuhusu madhara ya mtu aliambukizwa homa ya INI.
“Hatua hiyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki katika udhibiti na tiba ya ugonjwa huo”
Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH), Disemba Mosi mwaka huu inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure ya  ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Rwanda katika udhibiti na kutoa tiba ya ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo, John Lwegasha amesema ni wakati muafaka wa watu kujitokeza na kupima afya zao kwa ujumla na kwa wale waliothirika na ugonjwa huo wajitokeze ili kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupata nafasi ya tiba kulingana na miongozo ya tiba inavyoelekeza.
“Utaratibu mwingine wa uchangiaji wa gharama za matibabu katika maeneo mengine ya uchunguzi na tiba ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa gharama za kumuona Daktari utabaki kama ulivyo,” amesema Dk. Lwegasha.
Tatizo la ugonjwa huo Tanzania, kwa mujibu wa Dk . Lwegasha inakadiriwa kuwa watu wanane kati ya watu mia moja wana maambukizi ya ugonjwa huo na kwamba kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kile kinachokadiriwa kwenye maambukizi ya Ukimwi kitaifa ambacho ni asilimia pungufu ya sita.
“Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili asilimia 60 ya wagonjwa wanaokutwa na Saratani ya Ini mara nyingi imetokana na maambukizi ya virusi hivyo,” amesema Dk. Lwegasha.
Kuhusu tiba amesema kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi , ugonjwa huo sugu wa Homa ya Ini hauna tiba ya kuponya isipokua dawa zilizopatikana hadi sasa zinaweza kupunguza kasi ya maambukizi mwilini na kuzuia madhara kwenye Ini.
Ugonjwa wa Homa ya Ini ( Hepatitis) unasababishwa na Virusi viitwavyo Hepatitis B na maambukizi yaugonjwa huo yanashahabiana na njia ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kama vile kufanya ngono zisizo salama , kuchangia sindano au vikatio, kupewa damu isiyopimwa , kupitia uzazi wa mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA KOMPYUTA 205 TOKA KAMPUNI YA BAYPORT TANZANIA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga akikabidhi moja ya kompyuta zilizokabidhiwa na Taasisi yake kwa ajili ya serikali. Anayepokea ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imeipatia serikali msaada wa kompyuta 205 zenye thamani ya Sh Milioni 500 kwa ajili ya matumizi yao ya kiofisi, kwa kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga wa pili kutoka kushoto waliosimama, akipeana mkono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa Angellah Kairuki baada ya kukabidhiwa kompyuta 205 na Taasisi ya Bayport, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Laurean Ndumbaro na Kaimu Katibu Mkuu Bi Susan Mlawi.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam, ambapo kompyuta 125 zitabaki Makao Makuu ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kompyuta 80 zilizosalia zitagawanywa na Wizara yenyewe kwa kuangalia mahitaji ya ofisi zao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia halfa ya makabidhiano ya kompyuta kutoka kwa Taasisi ya Bayport Financial Services.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema msaada wa kompyuta hizo zinatokana na kiu yao kubwa ya kushirikiana na serikali kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa ajili ya kufanikisha huduma bora kwa Watanzania.

Alisema taasisi yao ilipanga wamalize mwaka kwa kukabidhi kompyuta kwa ofisi za serikali, ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea miaka 10 ya huduma zao tangu Bayport ilipoanzishwa mwaka 2006 nchini Tanzania.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki katikati akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa kompyuta kutoka kwa Bayport Financial Services leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Dk Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bayport, John Mbaga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala, Mheshimiwa Angellah Kairuki wa pili waliosimama mstari wa mbele, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi Susan Mlawi pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Laurean Ndumbaro kulia kwa waziri wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Bayport na baadhi ya wakuu wa Idara wa Ofisi ya Rais.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, akizungumza katika halfa ya makabidhiano kompyuta 205 za aina mbalimbali kutoka kwa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services yenye Makao yake Makuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa ofisi za serikali nchini Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Bayport, John Mbaga.

“Tunakabidhi kompyuta hizi 240 kwa serikali huku tukijipa moyo kuwa zitatumiwa ipasavyo na watumishi wetu wa umma wanaotuhudumia katika majukumu yao na kuongeza ufanisi, hivyo Bayport itaendelea kushirikiana na serikali kwa nguvu zote.

“Sisi jukumu letu ni kushirikiana na serikali sambamba na kujitolea kwenye jamii kwa kusaidia mambo mbalimbali kwa ajili ya kuwakwamua wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kwa kupitia sekta ya mikopo,” Alisema.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, aliishukuru Bayport kwa kutekeleza ahadi yao ya msaada wa kompyuta kwenye wizara yao.

Alisema wamevutiwa na kompyuta hizo zilizotolewa kwa wakati muafaka, huku akisema zitarahisisha utoaji wa huduma bora kwa watumishi wa umma katika ofisi watakazopokea baada ya kufikishwa kwao.

“Tulipata taarifa kuwa wenzetu wa Bayport wanatuletea msaada huu ambao kwa hakika ni mkubwa na umekuja wakati muafaka na utawawezesha watumishi wetu kufanya kazi vizuri kwa kupata hivi vitendea kazi,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya fedha kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, huku pia ikitoa huduma za mikopo ya viwanja katika miradi yake ya Bagamoyo, Kigamboni, Kibaha na Kilwa.

WAZAZI HALMASHAURI YA KAKONKO WAFANIKIWA KUTOA CHAKULA S/ MSINGI 59

$
0
0
Judith Mhina - Maelezo

Wazazi Halmashauri ya Kakonko, wafanikiwa kutoa chakula katika shule 59 zilizopo katika Halmashauri hiyo kuamzoa mwaka  2015.

Mkoa wa Kigoma una jumla ya Halmashauri 8 na kati ya hizo ni Kakonko peke yake ndio imefanikiwa kutoa huduma ya uji shuleni. Nikiongea na Waratibu kata kata 5 za Kakonko Bw Jobson Johnston, Scolastica Andrew, Paschal Mlelema, Eliud Kayigwe na Samson Sike kwa wakati mmoja wamesema hatukujua kama Halmashauri nyingine hawana huduma hiyo katika shule zao walidhani ni mpango wa Mkoa 

Hata hivyo, walisema:” Changamoto walizoziainisha waratibu Kata wa Halmashauri nyingine hazina mashiko hivyo ni vema wakajithatiti kuhamasisha  wazazi nina hakika wakielewa umuhimu wa chakula shuleni , watakubali kuchangia na hatimaye watoto watapata Uji na kutoa huduma hiyo.
Watoto wa Shule ya Msingi ButaLe Maalum wakipata Chakula cha Mchana shuleni

Waliongeza kwa kusema utafiti wa Shirika la Kimataifa la Watoto UNICEF uliofanyika 2001-2003,  ulionyesha watoto waliowengi wa shule za msingi Mkoa wa Kigoma wamedumaa kwa kubeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wao na kukosa chakula bora, wakati Mkoa unakila aina ya chakula, na kuongeza mafuta ya mawese matunda mbogamboga za majani yote yanayopatikana Tanzania yapo Kigoma, , hivyo  hakuna sababu ya msingi ya watoto kudumaa. 

Mratibu Kata kiongozi wa Kakonko kwenye Warsha ya Mpango wa Kuinua Kiwango cha Elimu, Bw Jobson Johnston alisema kila mzazi anachangia kilo 5 ya mahindi, hivyo shule kupata mahindi zaidi ya mahitaji ya mwaka , ambapo huuza kiasi kwa ajili ya  kupata fedha ya kununulia maziwa, sukari na mafuta ya mawese. 

Uji unaotolewa mashuleni umekuwa na virutubisho bora kabisa kumfanya mwanafunzi apate usikivu wamasomo darasani, nakuweza kufanya vizuri.Kila mwanafunzi huja shule na kikombe chake kwa ajili ya huduma ya kupata uji. 

Kakonko in jumla ya kata 13 nazo ni Kiziguzigu, vijiji 3 Gwarama, vijiji 6 Kasuga, vijiji 3 Mugunzu, vijiji 4 Muhange, vijiji 4 Kitanga, vijiji 3 Kasanda, vijiji 7 Nyabibuye, vijiji 2 Gwanumpu, vijiji 4 Kakonko, vijiji 4 Kanyonza, vijiji 1 Nyamtukuzavijiji 3 na Rugenge vijiji 4 ambapo kwa ujumla kuna shule 59 za Msingi za Serikali.

Halmashauri ya Kakonko ni kati ya Halmashauri mpya zilizoanzishwa mwaka 2014, ina jumla ya shule za Msingi 59, ambazo kwa sasa zote zimeingia kwenye mpango wa kupata chakula shuleni.

 Aina ya chakula kinachotolewa ni  uji na Baadhi zinztoa Ugali na maharage aidha, chakula kinapata virutubisho kwa kuwekwa mafuta ya mawese na zile shule zenye kufuga ngombe wanaweka maziwa  kwenye uji hii imesaidia kwa  kiasi kikubwa kupandisha mahudhurio kwa watoto   kupenda kwenda shule.

Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula hapa nchini, wenye mazingira mazuri ya kupata mvua bila vikwazo. Ardhi yake ni nzuri yenye rutuba sehemu nyingi wanalima kilimo hai ,yaani bila kutumia mbolea za chumvu cnumvi, lakini kupata mavuno mengi. Hakika Mkoa huu hauna sababu kwa nini usitoe chakula katika shule za Msingi zote Mkoa mzima.

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bi. Malika BARAK akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) alipomtembelea Waziri huyo leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipitia nyaraka zilizowasilishwa na  Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bi. Malika BARAK alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bi. Malika BARAK (kulia) mara baada ya kupokea nyaraka kutoka kwa balozi huyo.

Rais Magufuli na Rais Lungu wakubaliana kufufua TAZARA na TAZAMA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakisaini makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia wakionyesha mikataba ya makubaliano ya kuwa na Mashauriano ya Kidiplomasia iliyotiwa saini leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri wa TanzaniaDkt. John Pombe Joseph Magufuli (aliyekaa) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe. Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Edgar Lungu (nyuma mwenye tai nyekundu) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania Balozi John Kijazi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu (hayupo pichani) leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Lungu (mwenye tai nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Tanzania na Zambia leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu leo tarehe 28 Novemba, 2016 wamekubaliana kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuboresha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA ili miradi hiyo miwili ilete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi Tanzania na Zambia.

Marais hao wametangaza kuchukua hatua hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi baada viongozi hao kufanya mazungumzo rasmi ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku 3 ya Rais Lungu iliyoanza jana hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli.

Katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, tevisheni na mitandao ya kijamii Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa utendaji kazi wa reli ya TAZARA ambao umeshuka kutoka usafirishaji wa tani 5,000,000 za mizigo mwaka 1976 hadi kufikia usafirishaji wa tani 128,000 kwa mwaka hivi sasa, huku utendaji kazi wa bomba la mafuta la TAZAMA nao ukiporomoka kutoka uwezo wake wa kusafirisha tani 1,100,000 za mafuta hadi kufikia tani 600,000 kwa mwaka hivi sasa.

Marais hao wamekubaliana kuwakutanisha wanasheria wakuu wa Serikali za nchi zote mbili haraka iwezekanavyo kwa lengo la kufanya marekebisho ya kisheria kwa maeneo yote yaliyoonesha kuwa kikwazo na pia kupanga upya menejimenti za TAZARA na TAZAMA ili ziweze kuendesha vyombo hivyo kibiashara na kwa manufaa yaliyokusudiwa wakati vilipoanzishwa na Waasisi wa mataifa haya mawili yaani Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Dkt. Kenneth Kaunda wa Zambia.

"Tumekubaliana ni lazima tubadilike na tubadilike kwa haraka, vikwazo vinavyotokana na sheria viondolewe na manejimenti ya TAZARA ipangwe upya, na mimi nataka kusema kwa uwazi, ukiwauliza TAZARA watakwambia tatizo ni mtaji lakini ukweli ni kwamba tatizo ni menejimenti, ingekuwa tatizo ni mtaji, ule uliokuwepo mwaka 1976 umekwenda wapi? maana sasa hivi TAZARA ina vichwa 14 tu vya kuendeshea treni na ina upungufu mkubwa wa mabehewa" amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Lungu amesisitiza kuwa katika kuimarisha TAZARA wamekubaliana kuweka pembeni siasa na kuirejesha TAZARA katika hali yake ya kibiashara kwa kuhakikisha inafanya kazi ya kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo iendayo kusini mwa Tanzania na nchini Zambia.

Mhe. Lungu ameongeza kuwa pamoja na kuimarisha bomba la mafuta la TAZAMA, Zambia inatarajia kunufaika na gesi iliyogunduliwa kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania na pia inajipanga kutumia vizuri fursa ya kufunguka kwa ukanda wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Corridor) na mpango wa ujenzi wa reli ya kati ambapo ukanda wa Kaskazini mwa Zambia una mawasiliano ya karibu na bonde la ziwa Tanganyika.

"Mhe. Rais Magufuli una muda wa kutosha katika uongozi wako na mimi nina muda wa kutosha pia, kwa hiyo kwa pamoja tunaweza kuimarisha maeneo yote ya kuinua biashara na uwekezaji kati ya nchi zetu mbili ikiwemo kuimarisha TAZARA na TAZAMA kwa manufaa ya wananchi wetu" amesisitiza Rais Lungu.

Kuhusu hali ya biashara kati ya Tanzania na Zambia, Rais Magufuli amesema Zambia ni nchi inayoongoza kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam ambapo katika mwaka 2015 mizigo yenye uzito wa tani Milioni 1.9 ilipitishwa na kwamba kumekuwa na ongezeko la biashara kati ya Zambia na Tanzania kutoka Shilingi Bilioni 89.2 mwaka 2010 hadi kufikia Shilingi Bilioni 152.2 mwaka 2015.

Dkt. Magufuli amemhakikishia Rais Lungu kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi bandari ya Dar es Salaam, kupunguza vizuizi vya barabarani kutoka 8 hadi 4, kushughulikia tatizo la vizuizi vya polisi na kujenga Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post)

"Tunataka mambo haya yote yaende haraka, wataalamu wetu ni lazima waharakishe kurekebisha vikwazo vyote vilivyokuwa vinatuchelewa, tufanye kazi pamoja kwa manufaa ya wananchi" amesisitiza Rais Magufuli.

Jioni ya leo Rais Edgar Chagwa Lungu anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam na kesho Rais Lungu anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku 3 hapa nchini.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU


Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu leo tarehe 28 Novemba, 2016 wamekubaliana kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuboresha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA ili miradi hiyo miwili ilete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi Tanzania na Zambia.


Marais hao wametangaza kuchukua hatua hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi baada viongozi hao kufanya mazungumzo rasmi ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku 3 ya Rais Lungu iliyoanza jana hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli.


Katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, tevisheni na mitandao ya kijamii Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa utendaji kazi wa reli ya TAZARA ambao umeshuka kutoka usafirishaji wa tani 5,000,000 za mizigo mwaka 1976 hadi kufikia usafirishaji wa tani 128,000 kwa mwaka hivi sasa, huku utendaji kazi wa bomba la mafuta la TAZAMA nao ukiporomoka kutoka uwezo wake wa kusafirisha tani 1,100,000 za mafuta hadi kufikia tani 600,000 kwa mwaka hivi sasa.


Marais hao wamekubaliana kuwakutanisha wanasheria wakuu wa Serikali za nchi zote mbili haraka iwezekanavyo kwa lengo la kufanya marekebisho ya kisheria kwa maeneo yote yaliyoonesha kuwa kikwazo na pia kupanga upya menejimenti za TAZARA na TAZAMA ili ziweze kuendesha vyombo hivyo kibiashara na kwa manufaa yaliyokusudiwa wakati vilipoanzishwa na Waasisi wa mataifa haya mawili yaani Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Dkt. Kenneth Kaunda wa Zambia.


"Tumekubaliana ni lazima tubadilike na tubadilike kwa haraka, vikwazo vinavyotokana na sheria viondolewe na manejimenti ya TAZARA ipangwe upya, na mimi nataka kusema kwa uwazi, ukiwauliza TAZARA watakwambia tatizo ni mtaji lakini ukweli ni kwamba tatizo ni menejimenti, ingekuwa tatizo ni mtaji, ule uliokuwepo mwaka 1976 umekwenda wapi? maana sasa hivi TAZARA ina vichwa 14 tu vya kuendeshea treni na ina upungufu mkubwa wa mabehewa" amesema Rais Magufuli.


Kwa upande wake Rais Lungu amesisitiza kuwa katika kuimarisha TAZARA wamekubaliana kuweka pembeni siasa na kuirejesha TAZARA katika hali yake ya kibiashara kwa kuhakikisha inafanya kazi ya kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo iendayo kusini mwa Tanzania na nchini Zambia.


Mhe. Lungu ameongeza kuwa pamoja na kuimarisha bomba la mafuta la TAZAMA, Zambia inatarajia kunufaika na gesi iliyogunduliwa kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania na pia inajipanga kutumia vizuri fursa ya kufunguka kwa ukanda wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Corridor) na mpango wa ujenzi wa reli ya kati ambapo ukanda wa Kaskazini mwa Zambia una mawasiliano ya karibu na bonde la ziwa Tanganyika.


"Mhe. Rais Magufuli una muda wa kutosha katika uongozi wako na mimi nina muda wa kutosha pia, kwa hiyo kwa pamoja tunaweza kuimarisha maeneo yote ya kuinua biashara na uwekezaji kati ya nchi zetu mbili ikiwemo kuimarisha TAZARA na TAZAMA kwa manufaa ya wananchi wetu"amesisitiza Rais Lungu.


Kuhusu hali ya biashara kati ya Tanzania na Zambia, Rais Magufuli amesema Zambia ni nchi inayoongoza kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam ambapo katika mwaka 2015 mizigo yenye uzito wa tani Milioni 1.9 ilipitishwa na kwamba kumekuwa na ongezeko la biashara kati ya Zambia na Tanzania kutoka Shilingi Bilioni 89.2 mwaka 2010 hadi kufikia Shilingi Bilioni 152.2 mwaka 2015.


Dkt. Magufuli amemhakikishia Rais Lungu kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi bandari ya Dar es Salaam, kupunguza vizuizi vya barabarani kutoka 8 hadi 4, kushughulikia tatizo la vizuizi vya polisi na kujenga Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post)


"Tunataka mambo haya yote yaende haraka, wataalamu wetu ni lazima waharakishe kurekebisha vikwazo vyote vilivyokuwa vinatuchelewa, tufanye kazi pamoja kwa manufaa ya wananchi" amesisitiza Rais Magufuli.


Jioni ya leo Rais Edgar Chagwa Lungu anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam na kesho Rais Lungu anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku 3 hapa nchini.





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

TANGAZO

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu wakipita katikati ya Gadi ya Mapokezi iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akiangalia kikundi cha ngoma za asili cha Kimasai akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

SERIKALI YA TANZANIA NA CHINA KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA SEKTA YA HABARI

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wajumbe wa Serikali ya China (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana  Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wa Serikali ya China wakati wa mazungumzo ya kuimarisha sekta ya habari  nchini yaliyofanyika  jana Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).



Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Serikali  imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya China katika kuimarisha sekta ya habari  ili kuendana  na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ya utoaji wa habari.

Hayo  yamesemwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  jana Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo  na Naibu  Waziri wa Uenezi  wa China Ndg. Sun Zhijun yaliyolenga kuimarisha sekta ya habari nchini.

“Tunashukuru kwa uhusiano mzuri uliopo baina ya serikali zetu  ikiwemo hii ya  kuendeleza sekta ya habari ambayo ni muhimu  na inamchango mkubwa katika kuleta maendeleo na kutoa ajira kwa watanzania”.Alisema Mhe Nape.
Mhe. Nape anaongeza kuwa ushirikiano huo  utasaidia nchi zote mbili kuwa na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi kupitia vipindi mbalimbali vinatakavyokuwa vikirushwa na vyombo vya habari vya nchi hizo kwa lugha zote mbili.

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri wa Uenezi wa China Mhe.Sun Zhijun ameahidi kufanya mageuzi katika soko la habari kupitia radio na Luninga ambazo  zitatoa fursa ya kuonyesha vipindi mbalimbali vya Kiswahili na hivyo kusaidia katika kukuza na kueneza lugha hiyo.

“Ushirikiano wetu ni wa tangu enzi na enzi hivyo ni budi kuutunza na kuulinda umoja wetu ndo maana tukaona kuna umuhimu  wa kuimarisha  sekta ya habari ambapo Serikali yetu ya China itakuwa ikirusha  vipindi vya radio na luninga kama vile muziki na filamu za kiswahili katika vyombo vyetu vya habari ”.Alisema Mhe.Zhijun.

Vyombo vya Habari vya Tanzania na China vimekuwa vikishirikiana katika kubadilishana Habari na vipindi mbalimbali kupitia Chaneli zao na hivyo kusaidia ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kuendelea  kuimarika na kustawi zaidi.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images