Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WABUNGE KUHUSU BIASHARA YA VIROBA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akifafanua jambo katika semina ya wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara  pamoja na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.
 Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu Mwenyekiti was  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
                               Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa () akifafanua jambo katika semina ya wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara  pamoja na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa na Said Nkumba.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akimkabidhi jezi Idd Azzan kwa ajili ya timu ya Bunge iliyocheza na timu ya Konyagi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma Jumamosi
 Mgwassa akikabidhi jezi ya timu ya Konyagi kwa Idd Azzan tayari kwa mtanange na timu ya Bunge
 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya BNaibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge

saba washikiRIwa na jeshi la polisi Iringa kwa tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.

$
0
0
Watu saba wanashikiriwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za  kufanya fujo katika chaguzi ndogo za udiwani katika wilaya ya kilolo na mufindi huku likimshikilia  mtuu mmoja aitwaye Saadat Daud kwa kosa la uchochezi.
Akizungumza na wandishi wa habari kamanda wa polis mkoa wa Iringa,Ramadhani Mungi, mnamo tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 7 mchana katika kijiji cha ng’ang’ange wilaya ya kilolo Runyiliko Nyaulingo (60) alifika katika eneo la CCM,wakifamya maandalizi ya mkutano wa kampeni na kuwafanyia fujo.
Kamanda amesema kufuatia fujo hizo wafuasi wa ccm walimpiga na kumjeruhi mkono kitendo kilichopelekea wafuasi wa CHADEMA wakiwa na marungu na mapanga walikwenda kumuokoa mwenzao lakini polisi waliwahi kufika kutuliza fujo na wanamshikilia WILHADI NGOGO 40 inasemekana kuwa ni mfuasi wa chadema.

Kamanda pia majira ya saa 5 wafuasi wa chadema walikuwa wakifanya kampeni za nyumba kwa nyumba walifika katika kijiji cha  maguvani kwenye nyumba ya LUSTIKA MHELELE gafla walifika watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa ccm na kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali DANIEL EDSON 45 na katika tukio hilo wanamshikilia YOHANES MCHAFU 45.

Amesema kuwa baada ya kujeruhiwa kwa DANIEL EDSON wafuasi wa chadema walifunga barabara ya mbeya iringa kwa magogo wakiongozwa na kiongozi wao aitwaye SAADAT DAUD na fujo hizo zilitulizwa na jeshi la polis.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa mnamo tarehe 16 majira ya saa 11 jioni waliwakamata watu watatu wafuasi wa chadema wakiwa na mapanga na misumari katika kijiji cha ukemele kata ya mbalamaziwa DAMIANI OMARI 18 amemaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari sangu mkoani mbeya JOSEPH MWAKATO 17 mwanafunzi kidato cha pili sinde sekondari pamoja na GEORGE MYAO 32 mpishi wa tazara ambaye pia ni katibu wa BAVICHA.

NEW ARRIVALS @AK CLASSIC COSMETICS!!

$
0
0
 WALE MABINGWA WA COSMETICS ZA UKWEE KUTOKA USA, AK CLASSIC COSMETICS SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA UHAKIKA KABISA KAMA KAWAIDA YAO  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS,PERFUMES ZA MADESIGNER'S!! NA BIDHAA ZINGINE ZA KILA AINA!!KWA HAKIKA WATU WALIOTUMIA BIDHAA ZAO WAMEJIONEA UTOFAUTI,BADO WEWE!!

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.

IDD AZAN, HALIMA MDEE WAJIANDAA KUWAKABILI WOLPER NA JB

$
0
0
Halima Mdee na Idd Azan wakijifua mkoani Dodoma.
Mazoezi yakiwa yamepamba moto.
Video
Mdee akijiimarisha kwa ajili ya kumkabili Wolper.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, wameanza kujichua kwa ajili ya mapambano yao ya ndondi katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Halima Mdee atazipiga na Jacqueline Wolper wakati Idd Azan akionyeshana ubabe na Jacob Steven 'JB'
(Picha na Luqman Maloto /GPL, DODOMA)

TANA TRADE ANNOUNCEMENT

Makubwa..! anatafuta kiatu chake.

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa jiji wakimuangalia mtu ambaye hakufahamika jina aliyekuwa akitafuta kiatu kilichotumbukia katika mfereji wa majitaka, kama alivyokutwa Ubungo, Dar es Salaam juzi. (Picha na Prona Mumwi)

Mungu akaipumzishe roho yako mahali pema peponi langa

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAJULIA HALI MAJERUHI WA BOMU LA ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Gabriel Kivuyo (52) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, mtoto aliyetambuliwa kwa jina moja la Fahad (7) aliyelazwa katika chumba cha watu mahututi Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo A, Sarah John (45) aliyelazwa Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu 70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Selian, mkoani Arusha baada ya kudaiwa kushambuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Kata ya Makuyuni, Monduli. Awali Nasari alikaririwa akieleza kuwa anamaumivu ya mgongo baada ya kushambuliwa na vitu vigumu na vijana wa Kimasai. Kwa mujibu wa maelezo ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Kweka, anayemtibu Mbunge huyo, alimueleza Makamu wa Rais kuwa mbunge huyo, baada ya kupimwa na kupigwa picha za X-Ray, ameonekana kuwa hana tatizo lolote la kiafya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Geofrey, kuhusu jinsi mtoto, Aboubakar Adam, mkazi wa Sakina jijini Arusha, aliyelazwa katika Hospitali ya ARumeru baada ya kujeruhiwa na bomu wakati akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika Uwanja wa Soweto kwenye Mkutano wa Chadema wiki iliyopita. Makamu wa Rais, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo, waliolazwa katika Hospitali za Arumeru, Selian na Mtakatifu Elizabeth, jana Juni 17, 2013.Picha na OMR


Vodacom yapanua wigo huduma na ajira kwa Watanzania

$
0
0
 Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)akimkabidhi funguo  Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam Minja,ikiwa ni inshara ya uzinduzi rasmi wa duka hilo.Anaeshuhudia ni Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline Kamuhanda.
 Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam Minja,akifungua duka hilo kwa mara ya kwanza tayari kwa kutoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,akishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline Kamuhanda.
 Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza.Tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wake.
Miriam Minja (right) the Manager of Vodacom Shop at Millennium Towers, Dar es Salaam, shows the features of a phone to Lameck Hanold, a customer who visited the shop during its official opening. Looking on on the left is Vodacom Tanzania Head of Key Accounts and Franchise, Upendo Richard.

shughuli mbali mbali zikiendelea kwenye ufukwe wa ziwa nyasa,wilayani Ludewa mkoani Njombe.

$
0
0
 
Shughuli mbalimbali zikiendelea kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa,mkoani Njombe.

TAARIFA YA MSIBA YA MZEE PHILIP NHINGULA.

$
0
0

MAREHEMU MWL. PHILIP NHIGULA
(1927-2013)

FAMILIA YA MAREHEMU MWALIMU. PHILIP NHIGULA WA MALYA MWANZA WANASIKITIKA KUONDOKEWA KWA BABA YAO MPENZI MWALIMU PHILIP NHIGULA (86) ALIYEFARIKI TAREHE 17/06/2013 SAA SABA MCHANA HOSIPITALI YA TAIFA MUHIMBILI AMBAKO MWILI UMEHIFADHIWA.

SHUGHULI ZOTE ZA MIPANGO YA MAZISHI ZINAFANYIKA KIJITONYAMA, DAR ES SALAAM NYUMBANI KWA MTOTO WA MAREHEMU MRS. SAYAYI. MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 22/06/2013 MAKABURI YA KINONDONI.

TAARIFA ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

JIACHIE NA MAC AUTO ACCESSORIES WALIOPO SINZA MORI.

$
0
0

MAC AUTO ACCESSORIES 
TUPO SINZA MORI KARIBU NA PETROL STATION YA GBP 
::::: OUR HOTLINES: 0767 120 111 
OR 0715 000 890

Shirika la PARALEGAL mkoani iringa laombwa kuingilia kati mahusiano ya baadhi ya mashirika

$
0
0
Shirika  la PARALEGAL la mkoani Iringa limeombwa kuangalia mashirika ya kushirikiana nayo katika utendaji wa kazi,hasa kutokana na mashirika mengi kujikuta yakiingia katika matatizo kufuatia kushindwa kuendana na sera za shirika husika.

Hayo yamesemwa leo na wakili wa kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake na watoto(WLAC),Bwa. WISTON MOSHA alipokuwa akizungumza na wanachama wa shirika hilo alipokuja kujua maendeleo na changamoto ya shirika hilo.


Mosha pia amewaomba wanachama hao kuwa wavumilivu katika suala la msilahi kutokana na shirika kuwa change kwa sasa na kuendelea kujitolea. 


Kwa upande wake mratibu wa  PARALEGAL mkoani hapa SIGARIED MAPUNDA amesema kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazolikabili shirika, ikiwemo ya kushindwa kupata ushirikiano kutoka sekta mbalimbali kutokana na  shirika kutotambulika.


Mapunda amesema kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa ofisi,usafili kwa ajiri ya kuwafikia watu walioko mbali kwaajiri ya kutoa elimu pamoja na ukosefu wa watumishi kutokana na shirika kutokuwa na fedha za kutosha.


Aidha kwa upande wa wanachama wameviomba vyombo vya dola kuwa karibu yao ili kuwapa ushirikiano katika utendaji wao wa kazi kwani wao ndio msaada mkubwa kwao huku wakiomba kusaidiwa zaidi katika suala la masilahi.


MRISHO MPOTO NA MJOMBA BAND KUHAMASISHA KAMPENI YA KUNAWA MIKONO NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MIKOA MITANO NCHINI

$
0
0
IMG_1058 
Msanii wa kughani na kuimba nyimbo za asili Mrisho Mpoto ambaye pia ni Mkurugenzi wa ‘Mjomba Band’ akizungumza na Mhariri wa Mo Blog Lemmy Hipolite (kushoto) kuhusiana na kampeni ya kunawa mikono kwa sabuni na ujenzi wa vyoo bora ili kuepukana na maradhi yanayosababishwa na uchafu. Kampeni hiyo itafanyika katika mikoa mitano hapa nchini ikianzia na Dodoma, Mara, Njombe. Rukwa na Tanga.

Mwanamuziki na mghani maarufu wa nyimbo za asili ya nyumbani Mrisho Mpoto amewataka wasanii na wanamuziki wote nchini Tanzania kuwa kitu kimoja kwa kujenga ushirikiano na muungano ili kuweza kuufikisha muziki wa hapa nyumbani katika malengo ya kimataifa.

Akizungumza na Mtandao Maarufu wa Habari jijini Dar es Salaam, Msanii huyo Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’ amesema katika kujulikana kwenye michezo kama inayofanyika kwa sasa, vikundi vya uhamasishaji vinavyotumia sanaa ya asili ni muhimu kutumika ili kuweza kukuza lugha pamoja na utamaduni wa nyumbani.

Amesema ili kufanikisha usafi wa mazingira ikiwemo siku ya kimataifa ya kunawa mikono ni muhimu jamii ya watanzania kuzingatia usafi ili kuepukana na magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu unaoambukiza maradhi yanayotokana na uchafu.

Aidha amesisitiza jamii kujenga utamaduni wa kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo.

Amesema mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira.

Katika kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la Mjomba Band wataanzia mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine ambayo kwa pamoja na watashirikianana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

Watanzaniawa Nurnberg na chama chao cha Pamojae.V.washiriki Tamasha la nne la Afrika

$
0
0
 Bwana Ramadhani Barungi akitoa maelezo kwa mgeni.
 pirikapirika katika Banda la Tanzania.
Wageni wakionja maandazi na chapati. 
Bwana Mukada Kidawa kushoto na Bwana Erick Morro, mwenyekiti wa Watanzania Nurnberg wakipokea msaada wa vifaa vya michezo na muziki kwa ajili ya Taasisi ya Talent Search and Empowerment.
Erick Morro.  
Mwenyekiti Pamoja e.V. in Nurnberg.
====  =======  =====
Watanzaniawa Nurnberg na chama chao cha Pamojae.V.washiriki katikaTamasha la nne la Afrika

Kuanziatarehe 13.-16.Juni 2013,sisiwatanzanianachamachetu cha Pamojae.V.tuishiohapakatikamjiwa Nurnberg, UjerumanitulishirikikwakukamirifukatikaTamasha la nne la Afrikahapa Nurnberg. KatikaTamashahilotuliitangazanchiyetuya Tanzania katika mambo tofautikama vileUtamaduni, Utaliinakijamii. 

KatikaTamashahilovileviletuliitangazaTaasisiya Talent Search and Empowerment ya pale UbungoKibangu, Dar es Salaam. Taasisihiiinahusikanakukuzavipajivyawatotokatika

Mafunzo kwa Wakufunzi kutoka VETA na Taasisi za Teknolojia

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (waliokaa wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava akifungua mafunzo kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma na Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira - Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (Hayupo pichani)mafunzo hayo ni maalum kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Morogoro na Zanzibar. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam yanalenga kukuza uelewa wa kutambua gesi haribifu kwa mazingira

Kila siku Arusha kimewaka. Kunanini? Nani kasema Arusha ni lazima damu zimwagike?

$
0
0

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

INAHITAJI akili ya kiuwendawazimu kupita huku na kule kusifia mwendelezo mbovu wa siasa za Tanzania, hasa baadhi ya vyama vya upinzani kufanya mambo ya kijinga.

Ni pale mwanasiasa anayejiona anakubalika kwa wananchi wake, anaamua kwa makusudi kuvunja sheria za nchi. Huu ni ujinga. Unahitaji kupingwa vikali na kila muhibiri wa amani.

Kwa wiki moja sasa, jiji la Arusha limekuwa likitawaliwa na uvunjifu wa amani, taharuki na kusababisha matatizo makubwa. Tangu siku ya Jumamosi ya Juni 15, wananchi wa Arusha wamekuwa wakiendelea kuishi kwa mashaka na wasiwasi mkubwa.

Watu watatu wamefariki Dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya, ikiwa ni baada ya bomu kurushwa katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huku ukihudhuriwa pia na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

Ikumbukwe kuwa, matokeo ya ghasia jijini Arusha si mara ya kwanza, maana kila siku kunakuwa na mgogoro mkubwa na kuwaacha Watanzania wenzetu wakiwa hawaelewi cha kufanya.

Mara baada ya kutokea mlipuko huo, Mbowe, kama mwenyekiti wa Chadema, alitangaza kuwazuia wabunge wote wa chama hicho kuingia kwenye vikao vya Bunge.

Ni kauli tata sana kwa maendeleo ya Taifa. Taifa ambalo, linahitaji bajeti bora yenye maslahi na Watanzania wote. Lakini kuzuia wabunge kuhudhuria vikao vya Bunge, ni vitendo vya kushangaza mno.

Kwa mujibu wa Mbowe, aliwazuia wabunge kuhudhuria vikao vya Bajeti ili washiriki kwenye misiba ya waliokufa kutokana na mlipuko huo wa Soweto, jijini Arusha.

Mbowe anatangaza hatua hii huku akijua kuwa Chadema haipo Arusha peke yake. Chadema pia inahitaji kura za wananchi wote, kama vile Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Iringa na mikoa mingine kama kweli inahitaji kushika dola.

Lakini Chadema wao wameonekana kuweka nguvu kubwa kwa jiji la Arusha, tena wakifikia hata kuvunja sheria za nchi. Ndio hapo ninapoanza kujiuliza juu ya mwendo huu.

Tunahitaji viongozi wendawazimu. Wale wanaoweza kufanya kazi bila kuogopa sura au mihemko ya viongozi wa vyama vya siasa. Kwa mfano, sheria inajieleza juu ya vyama vya siasa vinavyofanya vitendo vya vurugu na adhabu yake pia.

Tunahitaji sasa serikali kwa kupitia Msajili wa Vyama vya siasa, John Tendwa kuwa makini zaidi. Jeshi la Polisi nalo lihakikishe kuwa linasimamia vyema usalama wa raia.

Usalama ambao mara kadhaa umekuwa hatarini kwasababu ya matakwa ya viongozi wachache wa kisiasa. Huu ndio ukweli. Jeshi la Polisi Tanzania, mkoani Arusha lilizuia mikusanyiko isiyokuwa na sababu.

Ili kuonyesha kuwa Chadema wana lengo lao binafsi, waliamua kufanya mkutano bila hata kupewa kibali cha polisi. Hapa Chadema walitegemea kitu gani?

Wanataka waendelee kuvunja sheria wakijua wanaogopwa, hawawezi kuchukuliwa hatua za aina yoyote? Kila mara wabunge wa Chadema wanafanya vitendo visivyokuwa vya kiungwana.

Mbunge kama vile Godbless Lema, Tundu Lissu, Mbowe, Mchungaji Peter Msigwa wamekuwa wakijifanya wao ndio kila kitu katika Taifa hili, jambo linaloibua maswali kede kede.

Kuheshimika kwao wanakuchukulia vibaya, ndio maana matamshi yao mara kwa mara hayajengi jamii bora zaidi ya kuibomoa kadri wanavyojua wao, lengo lao ni kuichafua serikali iliyopo madarakani, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hii sio njia nzuri kamwe. Tanzania inazidi kuingia kwenye migogoro kama hii kwasababu ya ujinga wa watu wachache, ambao nashawishika kusema kuwa wana uchu wa madaraka.

Mara baada ya mlipuko kutoka Jumamosi, Mbowe hakuonyesha kumfahamu mlipuaji huyo, zaidi ya kuwazuia wabunge kuingia bungeni, akiwamo Zitto Kabwe, ambaye alipaswa kuwasilisha Bajeti ya Wizara Kivuli ya Fedha na Uchumi.

Lakini siku moja baadaye, yani Jumapili, Mbowe huyu huyu anatangaza kuwa anamfahamu vyema mlipuaji wa bomu, akasema ni Polisi. Sasa kama ndio yeye, maana hakuna anayeweza kufanya uharifu akachekewa, isipokuwa anahitaji kuchukuliwa hatua kali.

Kauli ya Mbowe inakwenda sambamba na tamko la serikali Bungeni, kwa kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, aambaye alionyesha kupigwa na butwaa jinsi baadhi ya Watanzania wenzetu wanavyopigania kuiharibia sifa nchi yetu.

Lukuvi akafika mbali zaidi kwa kusema serikali itatoa Milioni 100 kwa mtu atakayetoa ushahidi wa wanaofanya vitendo vya kiharifu, kama hivyo vya kulipua mabomu, huku nikiamini kuwa Mbowe atatoa ushirikiano kwa kumtaja mtu huyo.

Kwa uelewa wangu na siasa za Tanzania, zenye kila aina ya mihemko, kutoka baadhi ya vyama upinzani, sidhani kama Chadema wangeweza kumuacha mhalifu, arushe bomu na kutokomea kusipojulikana.

Chadema wasingefanya ujinga huu. Wangemng’ang’ania. Kama wanaweza kushindana na polisi kwa kuwarushia mawe, wakisema ukombozi unakaribia, kwanini wamuache mtu anayepiga bomu katika mkutano wao wa kampeni?

Hapa nini kinatengenezwa? Kwa bahati mbaya wale wasiokuwa na uelewa mzuri juu ya mambo ya kisiasa, wanajikuta wakipumbazwa na janja za aina hiyo kwenye propaganda za kisiasa.

Angalia ajabu hii, mara baada ya bomu kurushwa kwenye mkutano huo, mtu ambaye anadaiwa kurusha, hakuweza kukamatwa mara moja kwasababu Polisi hawakupewa ushirikiano.

Ni pale walipoanza kurushiwa mawe na wananchi kwenye tukio hilo, ambalo baadhi yao wamepoteza maisha. Siasa za aina hii sio mahali pake. Kila mtu mwenye mapenzi mema na Tanzania ni wakati wake sasa kuwa makini na kuwa mkali zaidi.

Watanzania tunadanganywa na wanasiasa ambao wanatumia nguvu kubwa kuiweka nchi kwenye kisiwa cha umwagaji damu. Wanasiasa wa aina hii wanatafuta kitu gani?


Hata kesho wakifanikiwa kunyakua dola, wanataka waongoze watu wa aina gani? Inauma sana. Katika kuliangalia hili, naona kufanikiwa kwake ni ngumu, maana kwa bahati mbaya wapo wananchi wanaojifanya hawanazo.

Wanajifanya wana uchungu zaidi na nchi hii kuliko Baba wa Taifa, ambaye licha ya kuhangaika kwa mambo mengi, ila leo hii ametangulia mbele za haki.

Wapambanaji wengi waliohakikisha kuwa mimi na wengine wenye umri wangu wanakuja kuishi katika nchi hii. Nchi ambayo kutokana na uongozi bora, kuheshimiana na kupendana, kulisababisha kutapakaa kwa sifa nzuri ya kisiwa cha amani.

Kisiwa cha amani ambacho leo hii watu wanataka kugawanywa kwa dini zao, makabila yao na mikoa wanayotoka. Leo hii jiji la Arusha, lenye sifa kemkem linanuka damu.

Kila siku Arusha kimewaka. Kunanini? Nani kasema Arusha ni lazima damu zimwagike? Huu sio mwendo mzuri hata kidogo. Ni wakati wetu sasa kila mtu kuwa makini na aweke msimamo.

Kwa wale wanaopenda mabadiliko ya kiutawala, yani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuingia upinzani, pia sio sahihi kushinda kwa kurushiana mabomu na risasi za moto.

Wapo watu wanaocheka kwa vitendo hivi. Hao wanajidanganya kuwa muda wa mabadiliko umefika. Sawa, lakini mabadiliko hayo yana manufaa gani kama watu wanapoteza maisha?

Kwanini tusifuate sheria na taratibu za kiungwana? Angalia, wabunge wa Chadema baada ya kususia Bunge, walivamia jiji la Arusha, wakijifanya wao ndio wenye uchungu kuliko wengine.

Hizi ni janja za kisiasa tu. Hakuna jipya linaloweza kufanywa kwa amani kama watu wanapita kwenye migongo ya wananchi, bila huruma na kuangamiza roho za ndugu zetu na wengine kupata majeraha na kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Wapo radhi watu wafe lakini wao waendelee kujulikana katika mitaa na kaya zetu. Wapo radhi wafanye fujo wakiamini kuwa vyombo vya habari vitawaandika pamoja na kupata mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambayo imejaza wanasiasa uchwara.

Ni wale wanaoacha mambo ya maana na kujadili upupu wa mabwana wakubwa hawa ambao wengi wao wanaishi maisha yenye kila raha, wakati wanaowahadaa na kufariki wanalala njaa, wanakufa masikini.

Wanadanganya kila wawezalo. Wanafanya kila hira, lakini siku akitoka hapo anaingia tena bungeni kwa ajili ya kutunisha mfuko wake kwa posho za serikali.

Kulikuwa na haja gani ya viongozi wa Chadema kufanya mkutano bila kupewa kibali? Hizi si janja za kutaka waandikwe? Mwisho wa siku wabunge watatu, akiwamo Tundu Lissu, Joyce Nkya, Mustapha Akoonay wakikamatwa huku mwenyekiti wao, kinara wa yote hayo, Mbowe akifanikiwa kutoroka.

Ametorokea kusipojulikana. Watu wanajua ametoroka, walioandika wanaandika katika media zao. Kesho akikamatwa au kujisalimisha polisi aandikwe tena.

Huku ni kusumbua umma. Huku ni kutumia ujanja kujinufaisha kisiasa kwa mambo ya kijinga kabisa. Watanzania tuyaseme haya ili kuelimishana kwa ajili ya Tanzania yetu.

Taifa linakabiliwa na changamoto nyingi mno. Bajeti ya mwaka 2013/2014 imetangazwa huku ikishindwa kujibu namna gani wananchi wanaweza kuishi maisha bora.

Kodi kubwa itakuwa migongoni mwao. Bei za bidhaa zinazotumiwa na walalahoi zimeongezwa mara dufu. Biadhaa kama vile mafuta ya dizeli, petrol zitawafanywa wananchi waishi mashakani.

Kuongezwa kwa kodi hizo, kutaongezeka mfumko wa bei mara dufu. Nauli zitapanda na vyakula havitakatika. Watu watakufa njaa. Hapa ndipo tunapohitaji vichwa vya wabunge wetu, badala ya kuelemea kwenye mambo ya anasa, kupiga soga na kulinda umaarufu wao usipotee.

Tunayasema haya hata tutaitwa makada wa CCM au wale wanaombiwa wapo kwenye ndoa, yani wananchi wanaounga mkono siasa za Chama Cha Wananchi (CUF).

Nadhani kwa kulijua hili tunapaswa kuwa makini zaidi. Tuambiane ukweli, maana kinachoendelea leo jijini Arusha, kitakuwapo tena katika mikoa yetu, wilaya au vijiji vyetu.

Kama leo wanaokufa ni Wachaga wanaounga mkono Chadema,  basi kesho sumu hiyo itahamia wilayani Handeni, Korogwe, Lushoto, maana nao wanafuatilia masakata haya yanayofanywa kwa makusudi kama njia ya kulisumbua Taifa letu.

Nachukizwa na vitendo vya kihuni. Natamani sheria ichukuwe mkondo wake. Kwa wale wanaofanya uhuni wa aina hii wakibainika wakamatwe na kufunguliwa mashtaka au kuvifuta vyama vya aina hii.

Najua hili ni jambo litakalozusha ghasia na machafuko, maana watakimbilia kwenye huruma za wananchi, lakini akheri ya pengo kuliko jino bovu.

Chadema ni kero na lazima wajirekebishe, maana wanachofanya sasa, akipatikana kiongozi makini, asiyekuwa na woga na anayesimamia vyema sheria zake, wanasiasa wengi kwenye vyama vya aina hii wanastahili kutulizwa mihemko yao.

Mungu ibariki Tanzania.
Mwisho

safari ni hatua kwa mama wa kiafrika

OXFAM KWA KUPITIA KAMPENI YA GROW YATOA WITO KWA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KWA WAKULIMA WADOGO NA WA KATI.

$
0
0
IMG_7191
Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Haki za Ardhi - Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na salama.

Na.Mo Blog Team
Taasisi isiyo ya kiserikali ya OXFAM kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za kilimo zinaweza kufanikiwa.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi. Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya wajasiriamali nchini ni wakulima.
Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.

Aidha kampeni hiyo inakusudia kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.
IMG_7195
Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.
IMG_7224
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW wakati wa hafla hiyo.
IMG_7262
Khadija Mwanamboka – Mbunifu wa Mavazi akipozi na Tuzo yake mara baada ya kutangazwa rasmi.
IMG_7249
Shamim Mwasha Fashion Blogger.
IMG_7257
Dina Marious- Mtangazaji wa Redio.
IMG_7240
Jacob Stephen Muigizaji.
IMG_7244
Masoud Kipanya Mchora Katuni.
IMG_7280
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan (wa pili kushoto).
IMG_7236
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

UMOJA WA WAMILIKI WA MALORI TANZANIA WALALAMIKIA KUPANDISHWA KWA BEI ZA BIMA

$
0
0

 Msemamaji wa Umoja wa wamiliki wa Malori Tanzania, Bwana Elias Lukumay akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko ya kampuni yake kuhusiana na ongezeko la bima. Kulia kwake ni Makamu mwenyekiti wa TATOA, Bi Angellina Ngalula.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Malori Tanzania, Bi Angellina Ngalula akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko ya umoja wao ya kupanda kwa bei za bima kwa asilimia 400. Kushoto kwake ni msemaji wa TATOA, Bwana Elias Lukumay.
=========  ========  =======  =========
UMOJA WA WAMILIKI WA MALORI TANZANIA WALALAMIKIA KUPANDISHWA KWA BEI ZA BIMA


Umoja cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) umelalamikia ongezeko la bei za bima, ukisema hazijazingatia uhalisia wa soko, pamoja na kukosa uhalali kwa kuwa hazijashirikisha wadau wa sekta ya usafiri pamoja na jamii kwa ujumla.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, msemaji wa TATOA Bwana Elias Lukumay, alisema wanasikitishwa na mamlaka ya uthibiti wa bima Tanzania (TIRA) kuongeza malipo ya bima kwa asilimia 400 bila kutoa sababu za msingi lakini pia bila kushirikisha wadau.


‘Majaribio yetu ya kuzungumza na TIRA yameshindika baada ya TIRA kutojibu barua wala mawasiliano rasmi ya kukutana nao, tofauti na makubalino yetu ya kikao cha mwezi wa pili, kati yetu na wao ambapo tulikubaliana kuwa na kikao kabla ya mazungumzo baina ya wadau na umma juu ya swala hili’ alisema Lukumay.


Akielezea zaidi kuhusu malalamiko hayo, Lukumay alisema vigezo maalumu vya kupandisha bei hizo haviko bayana lakini pia ushindani wa biashara haukuzingatiwa. ‘TATOA inaamini kuna njia nyingi za kufata ili kupandisha bei, lakini kubwa zaidi ni kuacha soko lijiendeshe lenyewe, kwani tuko kwenye soko huria’ alisema Lukumay.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa TATOA, Bi Angellina Ngalula, alisema ongezeko hili la bei ni kubwa mno kwa mara moja na litapunguza ushindani wa makampuni ya usafirishaji ya ndani, lakini pia litaongeza bei za usafirishaji kwa kiwango kikubwa sana na hivyo kuumiza uchumi wa nchi na mwananchi wa kawaida ataathirika kwa bei za bidhaa kupanda.


‘Sababu za TIRA kupandisha bei sio za msingi, sababu kama udanganyifu na kuongezeka kwa kesi za bima pamoja na ajali za barabarani, sio sababu tosha za kupandisha bima kwani kufanya hivyo kutaongeza malalamiko zaidi, na pia kuwavunja moyo wateja waaminifu’ alisema Bi Ngalula.


Bi Angellina pia alitoa wito kwa wahusika, yaani TIRA, kuacha tamaa na kutokuendeshwa na genge la makampuni ya bima na kurudi kwenye meza ya majadiliano ili kuweza kupata muafaka kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi kwa maendeleo ya taifa. ‘Bila TIRA kurudi kwenye meza ya majadiliano TATOA itabidi ichukue hatua mbadala kama kwenda mahakamani na kugomea bei hizi mpya, jambo ambalo litasababisha usumbufu kwenye uchumi wetu’ alisitiza Bi Ngalula.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images