Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1047 | 1048 | (Page 1049) | 1050 | 1051 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii

  HATIMAYE uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi ujio wa kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina toka Zambia anayekuja kurithi mikoba ya mholanzi Hans Van De Pluijm anayekuwa mkurugenzi wa benchi la Ufundi.

  Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Redio cha EFM, Makamu  mwenyekiti wa Yanga  Clement Sanga amesema kuwa ni kweli wameingia mkataba na George Lwandamina aliyekuwa akiifundisha Zesco United nchini Zambia na rasmi ataanza kuinoa timu hiyo mzunguko wa pili wa ligi kuu.

  Sanga mbali na kuweka wazi suala hilo ambalo lilikuwa ni gumzo kwa vyombo vya habari nchini, pia ametoa maelezo ya kina kwa mustakabali wa aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van Pluijm na kusema kuwa bado wataendelea kuwa nae kama mkurugenzi wa benchi la ufundi  kwani ni mwalimu mzoefu na anaijua vyema Yanga  hivyo ushauri wake na uzoefu utakuwa chachu ya mafanikio katika benchi letu la ufundi na klabu kiujumla.

  Hans Van Pluijm ameridhia nafasi hiyo baada ya uongozi wa klabu hiyo kukaa nae chini na kumwomba aendelee kubaki klabuni kwa nafasi hiyo adhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo kimbinu na kiufundi na mabadiliko hayo hayana maana kwamba kiwango cha kocha wa awali  kilikuwa kibaya bali uongozi katika hatua ya kuiboresha klabu yake umeamua kuleta changamoto mpya ili kujiweka bora zaidi katika michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo .

  Wakati huo huo makamu mwenyekiti amezungumzia hatima ya kocha msaidizi wa klabu hiyo ndugu Juma Mwambusi bado wanamtambua kama kocha msaidizi wa klabu hiyo mpaka hapo itakapotangazwa tofauti. 

  "mara nyingi kocha mkuu ndio anaamua au kupendekeza msaidizi wake na sio klabu hivyo bado Mwambusi ni kocha wetu mpaka hapo itakapotangazwa tofauti . Klabu kwa sasa imejikita kwa hao wawili wakubwa wa juu", amesema Sanga.

  Hans Van Pluijm sanjari na Juma Mwambusi wameifikisha timu hiyo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ikiwa nyuma ya wahasimu wao wakubwa Simba SC kwa tofauti ya alama 2  Simba  wanaongoza ligi wakiwa na alama 35 na Yanga 33, kwa sasa uongozi wa Yanga unaandaa siku maalumu ya kuwatambulisha George  Lwandamina kama kocha mkuu na Hans Van Pluijm kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu kwa wanachama , wapenzi na wadau wa soka nchini.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Novemba 21, 2016 asubuhi aliamua kutembea kwa mguu  kutoka makazi  yake yaliyopo Kilimani hadi Ofisini kwake   barabara ya Reli mjini Dodoma .  Pichani, Mheshimwa Majaliwa akilekea Ofisini kwake. (Picha na Ofisi ya Waziri MKuu).


  0 0

  Dk Edwin Mrema (kushoto) wa Muhimbili na Dk. James Savundra kutoka Australia wakifanya upasuaji kwa mmoja wa wagonjwa leo. Kulia ni Sister Akiyo akishiriki katika shughuli hiyo. Mgonjwa huyo amefanyiwa upasuaji wa mkono baada ya kupata ajali ya moto.
  Daktari bingwa, John Masago (kushoto) na Raymond Nkya (katikati) wote wa Muhimbili wakifanya upasuaji wa shingo kwa mmoja wa wagonjwa kwa kushirikiana na daktari bingwa kutoka Marekani, Mark Zafereo. Upasuaji huo unaofahamika kama RT MASTOIDECTOMY.
  Dk Mawala Shabani (kulia) kutoka MNH akishirikiana na Dk Richard Wagner (kushoto) kutoka Marekani wakifanya upasuaji wa sikio kwa mmoja wa wagonjwa Leo. Upasuaji huo unafahamika RT MASTOIDECTOMY.


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeanza kambi maalumu ya upasuaji kwa watu wenye matatizo mbalimbali na watu zaidi ya wanane wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

  Upasuaji huo ambao unahusisha watu wazima na watoto unafanywa kwa ushirikiano kati ya Muhimbili, Tanzania Australia Society na Rafiki Surgical Mission.Timu ya madaktari wa MNH wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na watalaam hao ambao waliwasili nchini Novemba 19, 2016 kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo.

  Watalaam hao wanne akiwamo daktari bingwa wa upasuaji, Dk. James Savundra jana walikutana na watalaam wa MNH wakingozwa na Dk Bingwa wa upasuaji Muhimbili, Edwin Mrema wamewafanyia uchunguzi wagonjwa na kuzungumza nao kabla ya shughuli hiyo kuanza.

  Kwa mujibu wa Dk Mrema lengo ni kutoa huduma, kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani.Leo wataalam hao wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa watatu akiwamo mgonjwa aliyeathirika mkono wake baada ya kupata ajali ya moto.Upasuaji huo unahusisha wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ikiwamo walioathirika baada kuungua na moto, ajali na wenye uvimbe.

  0 0

   Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la  ‘The Foundation For Civil Society’ Nasim Losai, akifungua rasmi Mafunzo ya siku tatu ya Biashara kwa Vijana , Fursa za Vijana pamoja na Taratibu na Sheria za kufanya Biashara ndani ya Soko Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Vijana wajasiliamali kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania yanatarajia kumalizika keshokutwa Nov 23, 2016. 

   Sehemu ya Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati wa ufunguzi huo.

  Sehemu ya Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati wa ufunguzi huo.
   Sehemu ya Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati wa ufunguzi huo.
   Mkufunzi, Leons Mtana, akitoa mada yake ya kuendeleza uwezo wa Mjasiliamali.
   Mafunzo yakiendelea.....
   Mkufunzi akiendelea kumwaga nondozzzz
   Meza Kuu wakifuatilia mada....zilizokuwa zikitolewa ukumbuni hapo

  Mkufunzi na mmoja kati ya waratibu wa mafunzo hayo, Mwajuma Hamza, akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza leo Nov 21, 2016 kwenye Hoteli ya BluePearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatarajia kumalizika Nov 23.
   Mwezeshaji Peninnah Rashid Tenga, akiendelea kutoa mada ya somo lake wakati wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.  
   Mwezeshaji Peninnah Rashid Tenga, akiendelea kutoa mada ya somo lake wakati wa mafunzo hayo katika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam. 
   Waratibu wa Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki baada ya ufunguzi rasmi. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
   Mshiriki akichangia mada
    Mshiriki akichangia mada
   Washiriki wakishiriki katika somo la kuendeleza uwezo wa Mjasiliamali wakati wa mafunzo hayo kwa vitendo 
   Washiriki wakishiriki katika somo la kuendeleza uwezo wa Mjasiliamali wakati wa mafunzo hayo kwa vitendo 
   Mshiriki akichangia mada
    Mshiriki akichangia mada
   Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo kwa vitendo.......
    Mshiriki akichangia mada
    Mshiriki akichangia mada
   Mafunzo yakiendelea.....
    Mshiriki akichangia mada
   Washiriki wakiwa bize kurekodi, kunakili kinachofundishwa....
    Mshiriki akichangia mada
   Washiriki wakiwa makini kusikiliza mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo
    Mshiriki akichangia mada
   Mkufunzi, Leons Mtana, akitoa mada yake ya kuendeleza uwezo wa Mjasiliamali.
    Mshiriki akichangia mada
    Washiriki wakiwa bize kurekodi, kunakili kinachofundishwa....
   Mkufunzi akiendelea kushusha nondozzzzz
    Washiriki wakiwa bize kufuatilia kinachofundishwa....
    Washiriki wakiwa bize kurekodi, kunakili kinachofundishwa....
    Washiriki wakiwa bize kurekodi, kunakili kinachofundishwa....
    Washiriki wakiwa bize kurekodi, kunakili kinachofundishwa....
  Washiriki wakijigawa katika makundi kuanza somo kwa vitendo

  0 0  0 0

  SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. DOTTO JAMES amesema kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya kupitia na kujadili mapendekezo ya baadhi ya wastaafu waliofika Makao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha Jijini Da ers salaam mwezi uliopita wakitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuwalipa kila baada ya miezi mitatu mitatu ili waweze kujikimu kimaisha.

  James amesema kuwa Wizara imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wastaafu kutaka kulipwa kila baada ya kipindi hicho huku wengine wakitaka kulipwa kila mwezi hatua ambayo imeifanya Serikali kuamua kulifanyia kazi suala hilo kwa kina na kuahidi kulitolea uamuzi hapo baadae.


  Benny Mwaipaja, Msemaji Wizara ya Fedhana Mipango

  0 0

  Na Anna Nkinda - JKCI

  21/11/2016 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa kiasi cha shilingi milioni 580 fedha ambazo Serikali ingezitumia kwa kuwapeleka wagonjwa wa moyo 20 nchini India kwa ajili ya matibabu ambapo kwa kila mgonjwa angegharamiwa kiasi cha shilingi milioni 29.

  Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi alipokuwa akielezea kuhusu upasuaji kwa wagonjwa wa moyo wanaoufanya hivi sasa kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia .

  Prof. Janabi aliongeza kuwa upasuaji huo wa wagonjwa unaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wataalamu wa ndani wakiwemo madaktari, wauguzi, wagavi na mafundi wanaohusika na utengenezaji wa mashine za kimatibabu.“Idadi ya wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ambao utachukuwa muda wa siku sita ni 20 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni watano”.

  “Tunafanya upasuaji kwa wagonjwa watatu kwa siku hadi sasa jumla ya wagonjwa nane wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri kati ya hao watu wazima watatu na watoto watano”, alisema Prof. Janabi.

  Alizitaja gharama wanazolipa wagonjwa hao ni shilingi laki tano kwa ajili ya vipimo vya maabara hii ni kwa wagonjwa wenye uwezo wa kulipia, kwa wagonjwa wasio na uwezo wanalipiwa na Serikali, Rotary Club Dar es Salaam na Bahari Beach na BAPS Charity na wagonjwa ambao ni wanachama wa Bima ya Afya wanalipiwa na bima zao.

  Prof. Janabi alisema, “Wagonjwa wanaotumia kadi za Bima ya Afya ni wachache, nawashauri wananchi wajiunge na Bima ya Afya kwani gharama za matibabu ni kubwa na tunakoelekea watu hawataweza kulipa na sisi kama Taasisi hatuwezi kufanya upasuaji bure kwani tunahitaji kununua vifaa tiba ili tuweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wetu”.

  Alizitaja changamoto wanazikabiliana nazo katika zoezi hilo la upasuaji kuwa ni pamoja na damu kwani wanatumia damu chupa sita hadi nane kwa mgonjwa mmoja hii inatokana na wagonjwa kutokuwa na damu ya kutosha.

  Tangu mwaka 2015 Taasisi hiyo imekuwa ikifanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa kushirikiana na Taasisi za kimataifa zikiwemo za OHI, Okoa Moyo wa Mtoto (Save Child Heart –SACH) na Mending Kids (MKI) ya nchini Marekani na madaktari kutoka nchi hizo wamekuwa wakija na vifaa tiba na kijigharamia nauli.

  0 0


  Benjamin Sawe-Maelezo.

  Serikali imesema pamoja na umuhimu wa kilimo bado kuna changamoto ya kuwa na data za kuaminika kwa uundaji, ufuatiliaji na utekelezaji wa sera za kilimo.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka leo jijini Dar es salaam alipofungua warsha ya siku tano iliyowashirikisha wawakilishi kutoka nchi 25 Barani Afrika ambao utajadili namna ya kuweka mikakati itakayowawezesha kupata data sahihi za kilimo.
  “Bado tuna tatizo la Data au Takwimu ambazo tunaweza kuwa na uhakika nazo, hivyo wenzetu wameamua kuweka mikakati itakayosaidia  nchi za Afrika kukusanya Data zitakazosaidia kufanya maamuzi katika sekta ya kilimo na maendeleo vijijini” alisema.

  Alisema kilimo kinachangia asilimia 35 ya pato la taifa na asilimia 70 ya ajira na ukuaji wa kila mwaka wa kilimo unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.
  Wakati huohuo, Meneja wa Takwimu za Kilimo Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Titus Mwisomba alisema bila takwimu hizo hawawezi kupima maendeleo waliyofikia hasa kwa upande wa sekta ya kilimo.

  Alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamejipanga kutumia teknolojia ya kisasa zikiwemo simu za mkononi ili kupata takwimu kwa haraka na kwa wakati sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa tafiti mbalimbali nchini.

  Alizitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa wataalam wa ukusanyaji wa takwimu ambapo tayari wameanza kutoa mfunzo kupitia Chuo cha Afrika Mashariki cha Takwimu ili kukabiliana na changamoto hiyo.
  Mbali na kuwashirikisha wataalam mbalimbali, mkutano huo pia uliwashirikisha wataalamu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB).
   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. FlorensTuruka akizindua Warsha ya siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika, Warsha hiyo imeshirikisha jumla ya nchi 25 na imefunguliwa jijini Dar es Salaam leo. 
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na washiriki wa Warsha ya Siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika, Warsha hiyo imeshirikisha jumla ya nchi 25 na imefunguliwa jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kukusanya Takwimu Sahihi zinazotokana na Kilimo Barani Afrika wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. Florens Turuka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
   Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kukusanya Takwimu Sahihi zinazotokana na Kilimo Barani Afrika wakijadiliana jambo baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Sekta ya Kilimo Dkt. Florens Turuka kufungua warsha hiyo jijini Dar es Salaam leo
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tanzania Dkt. Tonia Kandiero akiongea katika uzinduzi wa Warsha ya Siku Tano ya Kukusanya Takwimu Sahihi Zinazotokana na Kilimo Barani Afrika. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo) 

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong wakati wakelekea kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake akiongoza mazungumzo rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong aliyeambatana pia na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake  Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Watu wa China(PLA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ. PICHA NA IKULU  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Waziri wa Ardhi  Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU  0 0

   
   Mnada wa samaki katika Soko la Feri ukiendelea. 

  Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Paul Makonda amepiga marufuku biashara ya samaki kandokando ya barabara inayoelekea kivukoni na soko la samaki la feri baada ya wafanyabishara wa feri kulalamika kwa mkuu wa mkoa huyo kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakwepa kodi.

  Awali Makonda aliambiwa na wafanyabiashara hao kuwa soko hilo linakosa wateja kutokana na kushindwa kufikiwa na wateja ambao hununua samaki au bidhaa nyengine kandokando ya barabara na kusababisha wateja kutofika sokoni humo.

  Wakati huo huo Makonda amesikitishwa na kitendo cha wakuu wa idara mbalimbali kushindwa kukamilisha miradi kwa wakati kwa kisingizo cha kutopata fedha za bajeti ya serikali kuu ikiwa wangeweza kubuni miradi itakayowaingizia fedha.

  RC Makonda alisema kuwa hatakubaliana na watendaji wa namna hiyo kwani hurudisha maendeleo nyuma.

   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo akizungumza macheche katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
   Viongozi na watendaji wa wilaya ya Ilala wakimsikiliza  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ukumbi wa Anatoglo leo jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Feri ambapo pia alisikiliza  kero zao leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Mkonda akikagua madarasa ya mradi wa MEMS 11 Pugu Station Sekondari leo jijini Dar es Salaam.


  0 0
  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  akizungumza na  Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) wakati alipotembelea Studio za Wasafi Classic kujionea utendaji kazi wa studio hiyo Novemba 23,2016.
  wasf2
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Wasafi Classic Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na wasanii harmonize na Rich Mavoko.
  …………………………………………………….

  Kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Wasafi limemuomba Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye   kusaidia wasanii wa muziki huo kujivunia kazi yao kwa kupata maslahi ya kazi hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Akizungumza wakati Waziri huyo alipotembelea Studio za Wasafi na kujionea utendaji kazi wa studio hiyo, Mmiliki wa studio hizo Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) amesema, kumekuwa na changamoto nyingi katika tasnia ya muziki hasa wizi wa kazi zao ambazo zimekuwa zikirudufiwa na kuuzwa kiholela ndani na nje ya nchi bila wao kufaidika na uuzwaji wa kazi hizo.

  Changamoto nyingine alizozitaja  msanii Diamond ni pamoja na kupunjwa mapato yatokanayo na Miito ya Simu (Caller tunes) , kukosekana kwa ukumbi wa kisasa kwa ajj ili ya kufanyia maonesho makubwa ya muziki nchini, kuongezeka kwa uwiano wa nyimbo za kitanzania zinazopigwa redioni dhidi ya nyimbo za kigeni hasa kutoka Afrika ya Magharibi.

  Aidha wamemuomba Waziri Nape Moses Nnauye kuwasaidia kupata Elimu juu ya ulipaji kodi ili tasnia ya Muziki nayo iweze kuwa kati ya tasnia zenye mchango mkubwa kwa pato la taifa kwa maendeleo ya wasanii na taifa kwa ujumla.

  Kwa upande wake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  amehaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki kuwa ajira kubwa kwa vijana wengi kwa kuongeza vipato vyao na pato la taifa kwa ujumla.

  Wasafi Classic ni kundi la Muziki wa kizazi kipya(Bongo Flavour) Tanzania linalomilikiwa na Msanii Naseeb Abdul (Diamond Platinumz) na mpaka sasa lina wasanii wapatao 16 na linaongozwa na mameneja Babu Tale, Said Fella na Sallam SK.

  0 0  0 0

  Baada ya kuachia video/wimbo wake wa kwanza ‘NOMA’ miezi michache iliyopita, msanii Coyo ambaye ni mwenyeji wa jiji la miamba, Mwanza anatambulisha kazi yake mpya NJOO BAADAE, ikiwa ni ya pili kuachiwa akiwa chini ya usimamizi wa Tetemesha Entertainment. 
  Akizungumzia wimbo wake mpya, Coyo anasema, “NJOO BAADAE ni wimbo unaozungumzia maisha ya kila siku ya vijana”.“Ninamzungumzia mtu anayekuchanganyia mafaili kwa stori (umbea) muda ambao unamishe zako ambazo haziendani na stori  zake, hivyo unaamua kumchana habari hizo apeleke kwa zinaowahusu au aje baadae.” Ameongeza. 
  NJOO BAADAE imeandikwa na Coyo ambaye pia amefanya viitikio vya kuimba, na muziki wake umeandaliwa na watayarishaji watatu, Mr T Touch, mtayarishaji mpya aitwaye Daydream pamoja na KidBway chini ya usimamizi wa Tetemesha Ent.
                                                               
  Wimbo wa NJOO BAADAE pamoja na Instrumental vimeambatanishwa hapa, share na wengine kadri uwezavyo.       
  Tazama video yake iliyopita ‘NOMA’ hapa: https://youtu.be/VEPUTJL_Tj8


  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini walipokutana na wanahabri mkoa Kilimanjaro kuzungumzia tukio la uzinduzi litakalo fanyika kesho Ijumaa katika viwanja vya kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini ,Elizabeth Mushi akizungmza walipkkutana na wanahabari mkoani Kilimanjaro.
  Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili kutoka Mtandao wa Jinsia wa jeshi la Polisi (TPF Network) , Grace Lyimo (Kushoto) na Theresia Nyangasa.(Kulia).
  Meneja Programu wa Shirika lisililo la Kiserikali linalojishughulisha na kupinga ukeketaji (NAFGEM) Honorata Nasuwa akizungumza mbele ya wanahabri juu ya uzinduzi rasmi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia .
  Afisa Programu wa Shirika linalotoa msaada wa Kisheria Kilimanjaro-KIWECO,Hilaly Tesha akizungumza wakati wa mkutano wa na wanahabari kuzungumzia tukio hilo .
  Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
  Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ,Elina Maro akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
  Mkutano na Wanhabari mkoa wa Kilimanjaro ukiendelea.
  Baadhi ya Wanahabri mkoa wa Kilimajaro wakiwa katika mkutano huo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Na Evelyn Mkokoi

  Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Ukwemi uliyopo katika wilaya ya Kahama upo hatarini kutoweka kutokana na shughili za kibinadamu zinazofanywa ndani ya hifadhi hiyo zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

  Hayo yameelezwa na Meneja kutoka wakala wa Taifa wa Misitu Bw. Mohamed Dosa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea HIfadhi hiyo iliyopo ndani ya Halmashauri ya Kahama inayopakana na Halmashauri ya Mbongwe Mmkoani geita.

  Katika Ziara yake ya Ukaguzi wa Mazingira katika Hifadhi ya Msitu Huo, Naibu Waziri Mpina alielezwa kuwa shughuli kubwa zinazotegemewa na wakazi wa vijiji vya jirani na msitu huo ni, ukataji miti kwa uchomaji wa mikaa na ukataji wa magogo kwa shunghuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na shughuli na ujenzi na utengenezaji wa samani za majumbani.

  Meneja Dosa Amemuelezea Naiubu Waziri Mpina kuwa (generation) kizazi cha kwanza cha aina na miti ndani ya hifadhi hiyo kilishakwisha na miti inayoota na kuonekana sasa ni ya kizazi cha pili.

  “changamoto kubwa tunayokumbana nayo katika kulinda hifadhi hii ni magari ya doria kuzunguka ndani ya msitu kwani ni mkubwa sana na hakuna skari wa kutosha kufanya doria. “ Alisisitiza Bw. Dosa.

  Akiwa katikati ya Msitu huo Naibu Waziri Mpina alijionea Uharibifu mkubwa wa uchomaji mkaa na kushuhudia mhalifu Bw John Abdalah Sanga makazi wa kijiji cha jirani cha mwendakulima aliyekuwa akimaliza kuchoma mkaa katikati ya msitu huo na kueleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa takribani miaka mitatu sasa hali iliyompelekea Naibu Waziri Mpina na timu yake kutekekeza baadhi ya matanuru ya mkaa ndani yam situ huo.

  Kwa upande wake Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa Bw. Jamal Baruti alieleza kuwa hali ya uharibifu wa misitu nchini bado ni kubwa na suala la mkaa bado ni changamoto, hivyo wanaanchi washiriki katika kuhifadhi misitu na kutafuta mbadala wa mkaa na misitu ni muhimu kwa kutunza baiyonuwai., wakati katibu tawala wa wilaya ya kahama Bw. Thomas Nganya akitoa Rai kwa wananchi waone kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mmoja na siyo kuiachia seriali peke yake. 
  Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Mkwemu iliyoharibiwa vibaya na shughuli za binadamu ikiwa na pamoja na uchomaji wa mkaa, na baadhi ni magogo yanayoonekana pichani yaliyokuwa yamekatwa na wahalifu wa mazingira.
  Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika kuteketeza tanuru la mkaaa katikati ya hifadhi ya m situ ya Mkwemu Wilayani Kahama.
  Aliyeshika kiuno, Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiangalia Tanuru la Mkaa likitekea baada ya kushiriki kuteketeza ndani ya Msitu wa Mkwemu wilayani Kahama. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

  0 0

  Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa chini ya ulinzi baada ya kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akamatwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kughushi nyaraka za serikali. 

  Malalamiko kuhusiana na kutosoma taarifa ya mapato na matumizi na kukusanya mapato kutoka kwa wananchi kinyume ana taratibu za makusanyo ya fedha za umma.

  RC Makonda anaendelea na ziaraa yake ya siku 10 katika jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wanachi ambapo leo amefanya ziara katika Wilaya ya  Ilala.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Mwenyekiti Wa Serekali Ya Mtaa Wa Gongolamboto, Bakari Shingo alipokuwa akitoa hotuba fupi kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi
   Mwenyekiti Wa Serekali Ya Mtaa Wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa  chini ya ulinzi wa Polisi.
    Mwenyekiti Wa Serekali Ya Mtaa Wa Gongolamboto, Bakari Shingo akiwa  chini ya ulinzi wa Polisi akipakizwa kwenye gari kwa hatua zaidi za kisheria


  0 0

  Vodacom Tanzania’s Managing Director, Ian Ferrao is pleased to announce the appointment of Hisham Hendi as the new Director of Consumer Business Unit with effect from November 2016.

   Hisham will be leading both Marketing and Sales functions allowing Vodacom to build on its customer centric approach in the market. 

   “We brought Hisham on board due to his expertise and experience. Having worked in various other Vodacom operations in Africa and beyond, he understands the ins and outs of our commercial operations. With his leadership in the commercial area,  our customers can expect more valuable products and services that will address all their communications needs” said Ferrao.    

   Hisham has previously worked with Vodacom Tanzania supporting Vodacom’s International Business as the Managing Executive – Commercial.

  Prior to this, Hisham spent 11 years working in various roles across Vodafone’s Consumer Business in Egypt including digital services in Consumer Marketing and Prepaid Sales – Consumer Marketing in 2003 and 2005 respectively. Hisham went on to work in Consumer Proposition in Partner Networks in London, UK in 2007 before moving back to Egypt in 2009 to manage Prepaid Segments and later became Head of Consumer Marketing.

  Hisham holds a Bachelor Degree of Commerce from the University of Cairo, Egypt (2001).

  0 0

  Watanzania watakiwa kuchangamkia ‘Black Friday’

  Na Dotto Mwaibale

  TUNAPOELEKEA mwisho wa mwaka wa 2016 huku sikukuu za krisimasi na Mwaka Mpya zikiwa zinakaribia, Watanzania wametakiwa kuchangamkia ofa za ‘Black Friday’ inayolenga kupunguza pakubwa bei ya kukaa kwenye hoteli nchini.

  Rai hiyo imetolewa na kampuni inayotoa huduma za hoteli mtandaoni ya Jumia Travel ambapo inamuwezesha mtu kujionea hoteli mbalimbali, upatikanaji wa huduma, bei, mahali zilipo na pia fursa ya kuweza kulipia kabisa.

  Mtandao huo umeingia makubaliano na hoteli kadhaa za Tanzania bara na visiwani Zanzibar katika kuhakikisha wateja wanaonja utamu wa huduma zao kwa punguzo kubwa ambalo limekuwa likiendelea kwa wiki mbili sasa na litafikia kilele mnamo Ijumaa tarehe 25 Novemba mwaka huu.

  Akifafanua zaidi kuhusu siku hii ya Black Friday, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa hoteli ambazo zimetoa ofa hiyo ni pamoja na Africa House na Jaffreji House & Spa zilizoko katika Kisiwani Zanzibar pamoja na White Sands na Landmark Beach Resort & Conference Center zilizopo Tanzania Bara.

  “Ninafahamu kuwa wengi wetu huwa tunatamani kutumia muda huu wa mapumziko katika sehemu nzuri yenye starehe zote tofauti na mazingira tuliyoyazoea. Hilo linawezakana kwani kupitia ushirikiano na hoteli tunazofanyakazi nazo tunawatangazia ofa ya punguzo kubwa la kwenda kujivinjari katika hoteli za nyota nne ambayo imeanza wiki iliyopita Novemba 14 na itadumu mpaka Novemba 25,” alifafanua.

  “Kupitia ofa hii unaweza kuitumia pamoja na mpendwa wako, familia, ndugu, jamaa au marafiki. Kwa mfano, White Sands wanayo michezo ya kwenye maji, kituo cha kupiga mbizi chini ya maji na safari ya boti kwenda kisiwani. Tunawasihi watanzania kutumia fursa kama hizi ili kuweza kujionea huduma nzuri na hadhi ilizonazo hoteli za hapa nyumbani. Itakuwa ni jambo zuri sisi kwanza kuwa mabalozi wa vitu vyetu wenyewe na sio wageni wanaokuja kutembelea nchini.” Alimalizia Meneja huyo Mkazi wa Jumia Travel Tanzania

  Kutokana na maendeleo ya teknolojia Jumia Travel (travel.jumia.com) inamuwezesha mteja kufanya huduma zote za hoteli kupitia programu inayoweza kupatikana kwenye kompyuta, tabiti na simu. Hivyo basi kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa njia rahisi na uhakika bila ya kumlazimu mtu mpaka kutembelea hoteli anayoitaka moja kwa moja.

  Kuhusu Jumia Travel

  Jumia Travel (travel.jumia.com) ni kampuni nambari moja unaongoza wa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika ambao humruhusu mteja kupata bei nzuri za hoteli zaidi ya 25,000 kwa nchi za Afrika na zaidi ya hoteli 200,000 duniani kote.

  Dhumuni letu ni kuleta kila aina ya huduma za malazi kwenye mfumo wa mtandao na kutengeneza njia rahisi na nafuu zaidi kwa wateja kuzilipia.

  Hapa Jumia Travel, tunao mamia ya wataalamu katika masuala ya utalii ambao huwasiliana na wateja wetu. Ofisi zetu zinapatikana katika miji na nchi zifuatazo Lagos (Naijeria), Accra (Ghana), Dakar (Senegali), Abidjan (Ivory Coast), Algiers (Algeria), Douala (Cameroon), Kampala (Uganda), Dar es Salaam (Tanzania), Nairobi (Kenya), Addis Ababa (Ethiopia), Porto (Ureno) na Paris (Ufaransa).

  Kabla ya mwezi Juni 2016, Jumia Travel ilikuwa ikijulikana kama Jovago. Ilianzishwa mnamo mwaka 2013 na Jumia huku ikiendeshwa kwa ushirikiano wa karibu na makampuni kama vile MTN, Rocket Internet, Millicom, Orange na Axa.


older | 1 | .... | 1047 | 1048 | (Page 1049) | 1050 | 1051 | .... | 1897 | newer