Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1039 | 1040 | (Page 1041) | 1042 | 1043 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Saimon Mwakifwamba akiwaeleza wadau wa filamu wa Jijini Mwanza(hawapo katika picha) umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii katika warsha ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uwezo wanatasnia hao.
  Meneja wa Mawasiliano kutoka Taasisi ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw.Innocent Mungy akijibu maswali yaliyoulizwa na wadau wa tasnia ya filamu baada ya kuwasilisha mada kuhusu matumizi ya mtandao kwa wadau haoleo Jijini Mwanza katika Warsha ya kuwajengea uwezo wadau hao iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Kanda ya Ziwa kutumia.

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini Bibi.Joyce Fissoo akimuelekeza jambo Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wanatasnia wa filamu Leo Jijini Mwanza.
  Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Kanda ya Ziwa Bw. Mohamed Nyenge (katikati) akimpa mkono wa shukrani aliyekuwa Mkufunzi wa Idara ya Fasihi kwa Kiingereza na Sanaa kutoka Chuo cha Ualimu Butimba Bw.Fumbuki Lubasa (kushoto)baada ya kujitolea kiwanja chake kilichopo maeneo ya Nyegezi Jijini Mwanza kwa ya ujenzi wa jengo la studio kwa wanatasnia hao,kushoto kwake ni Afisa Uendeshaji na Masoko wa PPF Bw.Khatibu Musa na kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini Bibi.Joyce Fissoo
  Wadau wa Filamu wa Jijini Mwanza wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wawezeshaji mada katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu Nchini kwa

  Mkufunzi kutoka chuo Kikuu cha Dodoma Bibi.Deogratius Ndunguru akiwasilisha mada kuhusu uhusiano kati ya mtunzi,mwongozaji na mwigizaji katika warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wanatasnia wa filamu Jijini Mwanza.

  ……………………………………………………….

  Na. Lorietha Laurence-Mwanza

  Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw.Saimon Mwakifwamba ameiomba Serikali kupitia Bodi ya Filamu nchini kuendeleza ushirikiano wa kutoa warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa tasnia hiyo kwa ngazi zote za Mkoa na Wilaya ili kuwafikia wadau wengi zaidi.

  Bw.Mwakifwamba aliyasema hayo Jijini Mwanza katika warsha ya kuwajengea uwezo wanatasnia wa filamu iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF kanda ya Ziwa yenye lengo la kuboresha sekta hiyo na kuwa chanzo kikuu cha uchumi binafsi na wa nchi.

  Aidha anaongeza kuwa, kupitia mafunzo hayo wanatasnia wameweza kujifunza fursa mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuboresha maisha yao ya kazi na familia na jinsi ya kujipatia masoko kupitia mitandao ya kijamii.

  “Tunaishukukuru Serikali kupitia bodi ya filamu nchini kwa fursa hii ambayo imetufungua macho ya kuona mbali zaidi ikiwemo uwekezaji kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii na umuhumi wa taaluma na weledi katika kuandaa filamu bora” alisema Mwakifwamba.

  Aliongeza kuwa filamu ni biashara na ajira iliyo na manufaa kwa nchi na wananchi wake hivyo ni wajibu wa wanastnia hao kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa ili kuweza kufika mbali zaidi na kuteka soko la

  0 0

  UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.

  Agosti mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.

  Agyei anasaini mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.
  Tunaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni, hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa kipindi chote atakachokuwa akiipigania jezi ya Azam FC.

  Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.

  Lengo kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata matokeo bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi tulilokuwa nalo, wachezaji wazuri walioko kikosini na wengine watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza kutuvusha kuelekea safari ya mafanikio msimu huu.
  Hivyo, tunawaomba mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu kwani tunaamini ya kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika kuwapa hamasa wachezaji ya kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu kiujumla.

  Wakati huo huo, leo tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),

  Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.

  0 0  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – MARA

  Mradi wa bustani za mbogamboga katika shule ya Msingi Mazoezi Bunda iliyoko kata ya Nyasura, wilaya ya Bunda Mkoani Mara unaingizia shule hiyo kiasi cha shilingi 50,000 hadi 100,000 kwa kila mwezi.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Vicent Ndunguru aliyasema hayo Wilayani Bunda wakati wa mahojiano na timu ya wilaya inayosimamia mpango wa kuinua ubora wa elimu wilayani humo.

  “Shule imeweza kujitunzia akiba ya fedha ambapo kabla ya mradi wa bustani za mbogamboga shule haikuwa na akiba yoyote lakini baada ya kuanzisha mradi huo, shule haikosi kuwa na akiba ya kiasi cha shilingi 50,000 mpaka 100,000 kwa mwezi,” alifafanua Mwalimu Ndunguru.

  Mwalimu Ndunguru aliendelea kwa kusema kuwa, kutokana na mradi huo shule imeweza kujinunulia vifaa vya kufundishia kama vile chaki.

  Pia fedha nyingine imekuwa ikitumika kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo pamoja na kutoa huduma ya kwanza kwa mwanafunzi au mwalimu anayepata tatizo na kuhitaji matibabu ya haraka.

  Aidha mradi huo umewajengea uwezo wa kujitegemea wanafunzi wa shule hiyo na kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la sita kuanzisha bustani za mbogamboga majumbani kwao na kutumika kama chanzo cha mapato cha familia.

  Mwalimu Ndunguru amewashauri walimu, kamati za shule na wazazi nchini kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mbalimbali kama vyanzo vya mapato ambavyo vitasaidia kuendesha shughuli za elimu katika shule zao.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba 12,2016 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. 

  Mhe.Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

  Na BMG

  Na George Binagi-GB Pazzo

  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, amemtaka Afisa Utamaduni mkoani mkoani hapa, kuhakikisha maadhimio yaliyoafikiwa na wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza yanaanza hatua za utekelezaji ndani ya siku saba.

  Nje ya hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Tesha amesema Afisa Utamaduni mkoa wa Mwanza, James Willium, kwa kushirikiana na maafisa utamaduni wa halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye mafunzo hayo ili utekelezaji huo uanze mara moja.

  Miongoni mwa maadhimio saba ya wasanii walioshiriki mafunzo hayo ambayo yamewasilishwa na Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela, ni pamoja na uongozi (Serikali) wa mkoa wa Mwanza kusaidia upatikanaji wa kituo cha sanaa (studio ya kisasa) kwa ajili ya kurekodia filamu na vipindi vya runinga pamoja na kushirikishwa kwenye dhifa mbalimbali za kimkoa na kitaifa ili kuonesha kazi sanaa zao.

  Katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa, ametoa bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza ili wasanii wa filamu mkoani Mwanza wajengewe studio kwa ajili ya kurekodia kazi zao ambapo Mfuko wa Pensheni wa PPF umeonesha nia ya dhati ya kufadhiri ujenzi wake.

  Zaidi ya washiriki 300 wamepata mafunzo hayo ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema yamelenga kuwajengea weledi wadau wa filamu wakiwemo waigizaji, waongozaji na wahariri, kutengeneza kazi zenye ubora, kutambua majukumu ya bodi hiyo, hakimili na hakishirikishi ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
  Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Mwanza, Ramadhan Mustapha (kushoto), akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
  Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela (kushoto), akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
  Mshauri wa sanaa ya Filamu mkoani Mwanza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.

  Mzee Lubasa ametoa bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza kwa ajili ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujengewa studio ya kisasa kwa ajili ya kurekodia kazi zao.
  Kushoto ni mmoja wa washiriki wa mafunzo ya sfilamu yaliyoandaliwa na bodi ya filamu nchini, akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, akifunga Mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fessoo, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza hii leo. Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea weledi wasanii wa filamu ili kutengeneza kazi bora.
  Mshauri wa Utamaduni mkoani Mwanza, James Willium, akizungumza wakati wa zoezi la ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo
  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akitoa mchango wake kuhusu uendelezaji wa soko la filamu mkoani Mwanza.
  Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela , akifuatilia mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
  Msanii wa nyimbo za asili, Chifu Mwananzengo (wa pili kulia) pamoja na wachezaji wake, akitoa burudani kuhusu mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo
  Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza wakifuatilia burudani kutoka kwa msanii wa nyimbo za asili, Chifu Mwananzengo kutoka wilayani Kwimba hii leo
  Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo hii leo kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
  Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso.
  Picha ya pamoja

  Bonyeza HAPA Kwa Habari Zaidi

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Ilala, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (katikati) na Wataalam alifuatana nao katika ziara hiyo, wakati alipotembeleaMradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme katikati ya Jiji la Dar es Salaam. 
  Baadhi ya mitambo iliyofungwa katika kituo cha Dar es Salaam City Center.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Kituo cha Kuboresha Miundombinu ya Umeme cha Ilala, jijini Dar es Saalam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtaalam kutoka TANESCO, Gibson Abdallah (wa kwanza kulia) alipokuwa akieleza namna mifumo ya umeme katika Kituo cha Ilala inavyofanya kazi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa(TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo. Wengine wanaofuatilia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO.
  Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa miundombinu ya umeme Kusambza umeme katika Kituo cha Ilala jijini Dar Dar es Salaam. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe aliofuatana nao, wakisikiliza maelezo ya kuhusu namna kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kinavyofanya kazi.
  Kaimu Meneja wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Katikati ya Jiji la Dare s Salaam, Mhandisi Iddy Rashid (katikati) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) na ujumbe aliofuatana nao namna mifumo katika Kituo cha Dar es Salaam City Center inavyofanya kazi.


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa leo amefanya ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Kuboresha Miundombinu ya Usambazaji umeme jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Usambazaji Umeme Ilala kinachojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam katika Kituo cha Dar es Salaam City Centre na Mradi wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji umeme, kilichopo eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

  Mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, kukamilika kwake kutaimarisha miundombinu ya usambazaji umeme Jijini Dar es Saalam na hivyo kuwezesha Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.

  Akizungumzia kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kilichojengwa na Serikali ya Finland na Tanzania ameeleza kuwa, kituo hicho kimefungwa mashine za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu kama zinazotumiwa katika nchi zilizoendelea na hivyo, kukamilika kwake kutawezesha kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme jijini Dar es Salaam ikiwemo kubaini kwa haraka na moja kwa moja eneo lolote lenye hitilafu kupitia mitambo hiyo na hivyo kuwezesha tatizo kushughulikiwa kwa haraka.

  “ Kwa ujumla nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha miundombinu ya umeme inayotekelezwa jijini Dar es Salaam. Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam, unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 Novemba,2016 na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli. Kukamilika kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa upatikanaji umeme jijini Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Ntalikwa.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Wananchi wa Kata ya Engutoto jijini Arusha wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.

  Wakitioa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hawajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji

  Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Kamete alisema kuwa wameomba sana hati za maeneo ambayo wanaishi lakini wamekuwa awapewi na wanazungushwa zungushwa kitu ambacho kinawatia mashaka makubwa.

  “Mkuu wa mkoa kinachotuuma zaidi sisi tumekaa hapa tangu kipindi cha mikonge lakini tukiomba hati hatupewi lakini akija muwekezaji anapatiwa hati kwa wakati sasa tunajiuliza inamaana sisi atuna haki ya kukaa katika viwanja hivi watuambie tu ili na sisi tujue sio wanafanya kazi ya kutuzungusha zungusha kwakweli tumekuwa tunaishi kama ndege katika maeneo yetu na atuna amani kabisa maana kama wanatunyima hati wanania gani kweli tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwa hili “alisema Zaituni Marunda

  Aidha wananchi hao pia wanasumbuliwa na kero za maji na umeme kwa kipindi kirefu hivyo wameiomba serikali iwasaidie kutatua kero hiyo inayowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alifika katika kata hiyo katika shughuli ya uzinduzi wa daraja  lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine

  Alisema kuwa wao kama serikali wapo tayari kushirikiana na wawekezaji ambao wanalipa kodi kama ipasavyo na wale ambao wanajishuhulisha katika kusaidia jamii inayowazunguka.Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuzindua daraja ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 67.
   Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua daraja katika Kata ya Engutoto ambalo limejengwa na wawekezaji daraja hilo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 65 za kitanzania
  Mkuu wamkoa wa Arusha akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Engutoto ilipo ndani ya jiji la Arusha
  Wa kwanza kulia ni muwekezaji Hans Paul katikati ni mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja

  0 0

  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimpa maelezo ya ufafanuzi ya vazi la asili, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akisalimia na Ayubu Tewele, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayesoma soko la lugha ya kichina wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao akibadilishana mawazo na Maofisa Waandamizi wa Ubalozi wa China nchini, akiwemo Balozi Dkt. Lu Youqing (kulia) wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.


  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Mathew ya Jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho mbalimbali ya vitabu vilivyoandikwa na Waandishi wa zamani akiwemo Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza ikiwa ni sehemu wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi hao wa vitabu vya zamani yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Mathew ya Jijini Dar es Salaam, James Edward (kushoto) na mwenzake Abdulaziz Ahmed wakibadilishana mawazo na Mkufunzi wa somo la lugha ya kichina, Zhu Yajing wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu na William Shakespeare. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Utamduni katika Ubalozi wa China nchini, Gao Wei akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing.
  (PICHA NA MAELEZO).

  ……………………………………………………………..

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam.

  NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nuru Millao ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kutumia fursa ya ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China katika taaluma za masomo ikiwemo kusoma na kujifunza lugha ya kichina ili kuharakisha shughuli za maendeleo nchini.

  Aliyasema hay oleo Jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya utamaduni wa china yaliyolenga kuenzi mchango wa waandisi wa vitabu wa zamani William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.

  Bibi Nuru alisema kuwa kwa sasa Nchi ya China ipo mbali kimaendeleo hivyo wanafunzi wa wakitanzania hawana budi kutumia fursa hiyo katika kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo lugha ya kichina. mbalimbali.

  Aidha, Bibi Nuru aliwaasa watanzania kuiga tamaduni zinazofanywa na watu wa wachina katika kuenzi kazi za waandishi mbalimbali wa mashairi, vitabu, tamthilia na maigizo ili kuweza kufaidika katika nyanya tofauti za maendeleo nchini.

  “Tanzania itafaidika vizuri zaidi wa kuiga mifano chanya ya wenzetu kwa kuenzi kazi za waandishi wa vitabu mbalimbali nchini, kwa mfano Mwalimu Nyerere aliandika vitabu vilivyochochea maendeleo ya Taifa” alifafanua Bibi Nuru.

  Kwa upande wake Balozi wa China Nchini, Dkt. Lu Youqing alisema China itaendeleza ushirikiano uliopo baina yao na Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuweza kuleta manufaa baina ya wananchi wa pande zote mbili.

  Balozi Youqing alisema, kumekuwa na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na China hasa katika sekta ya utamaduni ambapo kwa sasa takribani vyuo vikuu Vinne nchini China vinafundisha lugha ya Kiswahili.

  Aidha Dkt. Youqing alisema shule sita za Sekondari nchini Tanzania zina programu ya kufundisha lugha ya kichina ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tawi la Mlimani na pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Aidha Balozi Youqing alisema kuwa, nchi ya nchina imekuwa ikitafsiri vitabu vya lugha Kiswahili kwenda kwenye lugha ya kichina ambapo wameweza kutafsiri vitabu vya Mwalimu Nyerere vinavyowasaidia katika ujenzi wa Taifa lao.

  Maonyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 400 ya waandishi wa vitabu vya riwaya, tamthilia na filamu wakiwemo William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.

  0 0

  Wimbo: Inuka- Dudu baya Mamba ft Tid
  Producer: Mgwabati Classic & Nice P
  Studio: Tawanyika Studios

  0 0  Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora.
  Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipokuwa ukiteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora.
  Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini
  Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa marehemu Spika Mstaafu Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mwanane katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora
  Mama Margareth Sitta ambaye ni Mjane wa marehemu Spika mstaafu, Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mumewe katika kazishi yaliyofanyika Urambo
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakitupa udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo
  Viongozi wa Vyama vya siasa na serikali pamoja na wanafamilia wakiweka udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
  Maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta wakiweka shada la maua kwenye kaburi katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
  Mama Margareth Sitta ambaye ni mjane wa Spika Mstafu, marehemu Samuel Sitta akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimpa pole Mama wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta, Hajjat Zuwena Fundikira.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimfariji Mjane wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta Mama Magreth Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu. Anayefuatia ni Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa salama za rambirambi wakati wa mazishi wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akieleke Urambo khudhuria mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta, Novemba 12, 2016.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Viongozi wa Serikali wa mkoa wa Tabora, Viongozi wa Vyama vya siasa na dini baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akiwa njiani kwenda Urambo kwenye mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora. Wote walikuwa wakienda Urambo kushiriki mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Spika Mstaafu Samuel Sitta, Urambo mkoani Tabora ambako alishiriki mazishi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Urambo Tabora kwa mazishi
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wanafamilia na ndugu wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Urambo mkoani Tabora kwa mazishi
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wanafamilia na ndugu wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Urambo mkoani Tabora kwa mazishi
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Busega na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya Spika Mstaafu Samuel Sitta yaliyofanyika Urambo Tabora, Novemba 12, 2016. Kulia kwake ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba katika mazishi ya Spika Mstafu, Marehemu Samuel Sitta, Urambo mkoani Tabora
  Maaskofu na wachungaji wakiuombea mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yaliyofanyia Urambo Tabora.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Urambo mkoani Tabora
  Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa Spika Mstafu , marehemu Samuel Sitta akiongozwa na Mgalula Fundikira kwenda kwenye kaburi la mwanae katika mazishi yaliyofanyika Urambo.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa mwananchi kama zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa Unzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akizungumza na wananchi wa Kata ya Engutoto na Moshono wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge
  Mkuu wa wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) na Bw. Bw. Jagjit Aggarwal
   Daraja walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge Hili ndilo Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na uwezo wa kudumu kwa miaka 50. 

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Ndg. David Mwakiposa akimkaribisha Vongozi wa Serikali na wananchi wa Kata ya Engutoto kwenye uzinduzi wa daraja la Mto Kijenge lililojengwa kwa ufadhili wa Dharam Singh Hanspaul
  Kijenge
  Wakazi wa Kata za Engutoto na Moshono wakitoa shukrani zao kwa kukabidhi Mbuzi na kumvika mavazi ya kimaasai Mfadhili aliwajengea Daraja la Mto Kijenge Bw. Hans Paul 

  Diwani wa Kata ya Engutoto kwa kupita Tiket ya Chadema Mhe.Aman Reward alishirki katika uzinduzi wa Daraja na kupongeza Viongozi wa Mkoa na Jiji kwa namna wanavyowatumika wananchi
  Diwani wa Kata ya jirani ya Themi kupitia Tiketi ya Chadema Mhe. Melance Kinabo pia alishirki katika uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge.

  Nteghenjwa Hosseah - Arusha


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.

  Hii ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze katika hili.

  Katika uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za ijamii.

  Akiwasilisha kero zake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Zaituni Marunda amesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji.

  Aidha Neema John aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo wamekuwa wakisumbuliwa na kero za maji, umeme na Zahanati hivyo wameiomba Serikali iwasaidie kutatua kero hizo znazowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji pamoja na kupata taabu wakati wa kujifungua.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero na pia aliweza kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata kwa kuchangia Bati 100 na kuungwa mkono na Bw. Hans Paul aliyetoa matofali 5000 huku Bw. Jagjit Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200 na Mkurugenzi wa Jiji Bw. Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

  Daraja la Mto kijenge lilioanza kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani tatu(3), urefu kwenda juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza kudumu kwa miaka 50; Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .

  0 0

  Leo Siku ya Jumapili November 13,2016 timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itashuka dimbani kucheza na wenyeji Zimbabwe mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Harare mjini Harare.

  Mchezo huo utachezwa majira ya saa tisa alasiri kwa saa za Zimbabwe wakati Tanzania itakuwa saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utakaoneshwa na kituo cha Televisioni ya Taifa ya Zimbabwe (ZBC) na hapa nyumbani wataungana na kituo cha Televisioni cha Azam TV.

  Wakiwa chini ya kocha Mkuu Boniface Mkwasa kikosi chote kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Harare na tayari kwa vita hiyo ya Kesho na ushindi wa kesho utakuwa na faida ya kuipandisha Tanzania katika viwango vya FIFA.

  Mchezaji wa timu ya Tanzania Mbwana Samatta ambaye pia anachezea timu ya Genk ya Ubelgiji akiwa na mchezaji mwenzake Thomas Ulimwengu wakijiandaa kwa mazoezi mjini Harare nchini Zimbabwe tayari kwa mchezo wao na timu ya Taifa ya Zimbabwe jumapili.
  wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars wakijiandaa kwa mazoezi.
  Mchezaji Thomas Ulimwengu akibeba majiya kunywa kwenye toroli kwa ajili kunywa wakati wa mazoezi ya timu hiyo.
  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa taifa Stars Boniface Mkwasa akijadiliana jambo na makocha wenzake.
  Mazoezi yakiendelea.

  0 0


  0 0

   Mwakilishi wa kampuni ya Bureu Veritas inayosimamia uhakiki wa viwango vya kimataifa (Certfying board)  Bw Boniface Githae (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha ubora wa kimataifa kutoka Shirika la Viwango Duniani (ISO) yaani ISO 9001:2008 Certification kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (wa pili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba (wa kwanza kushoto)ambae  kampuni yake ndio ilitoa muongozo kwa kampuni ya ZH Poppe kupata cheti hicho na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Hassan Atako.
  Wanawake wanaweza! Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na dereva pekee wa kike kwenye kampuni hiyo.
  Ikawa ni kujipongeza ni kujipongeza tu!


  Familia nayo haikuwa nyuma… Hongera Babu!
  Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba (wa kwanza kulia)ambae  kampuni yake ndio ilitoa muongozo kwa kampuni ya ZH Poppe kupata cheti hicho akitoa nasaha zake wakati wa hafla hiyo.

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe akitoa nasaha zake kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.
  Timu ya Ushindi! Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwemo madereva mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho, 

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa kampuni hiyo mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho.
  Wadau wakijipongeza!

  KUELEKEA uchumi wa viwanda na biashara hapa nchini, mashirika ya umma, taasisi binafsi na makampuni mbalimbali yameombwa kuwekeza katika utoaji wa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kwenda sambamba na matakwa ya kiushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

  Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba wakati wa hafla fupi ya kukabidhi cheti cha wa  ubora kimataifa kutoka Shirika la Viwango Duniani (ISO) yaani ISO 9001:2008 Certification hicho kwa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd ya jijini Dar es Salaam.

  “Ustawi wa uchumi wa viwanda na biashara hapa nchini utakwenda sambamba na ongezeko la ushindani wa kibiashara pia hivyo suluhisho la msingi katika kuishi kwenye soko hilo ni kutafuta masoko nje hatua ambayo ili kufanikiwa muhusika anatakiwa akidhi  viwango vya ubora wa kimataifa na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuwa na cheti hiki,’’ alibainisha.

  Kwa mujibu wa Dk Sirimba ambae  kampuni yake kwa kushirikiana  na Consumer Pride Africa inatoa mwongozo na mafunzo kwa makampuni binafsi na mashirika ya umma hapa nchini ili yaweze kupata vyeti vya ubora yaani cha ISO, utolewaji wa cheti  hicho kwa kampuni ya ZH Poppe Ltd, ulifuatia kampuni hiyo kukidhi vigezo vyote vinavyohitajika baada ya kufanya vizuri na kufuzu katika mafunzo ya miezi sita yaliyotolewa kwa watendaji wa kampuni hiyo katika nyanja mbambali za kimfumo na kiutendaji.

  Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe alisema si tu kwamba kinaonyesha ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika usafirishaji wa mizigo ya aina mbalimbali ndani na nje ya nchi bali pia kitaongeza chachu katika kuhakikisha kwamba kampuni hiyo inafikia malengo yake ya kutoa huduma zaidi nje ya mipaka ya nchi.

  “Kwa kuwa cheti  hiki kilitanguliwa na mafunzo kwa watumishi wa idara zote wakiwemo madereva wetu tafsiri yake ni kwamba tofauti itaonekana hata huko barabarani kwa maana kwamba tunatarajia ajali zitokanazo na uzembe zitapungua kama sio kwisha kabisa,’’ alisema Bw Poppe huku akiwasihi madereva wa kampuni hiyo kuzingatia mafunzo waliyoyapata katika mchakato wa kupata cheti hicho.

  Akizungumzia cheti hicho Mwakilishi wa kampuni ya Bureu Veritas inayosimamia uhakiki wa viwango vya kimataifa (Certfying board)  Bw Boniface Githae alisema cheti hicho kinatolewa kwa mashirika, taasisi na makampuni baada ya kithitibishwa kuwa  yamekidhi vigezo vya kimataifa katika kutoa huduma zao, uthibitisho unaotanguliwa na mafunzo mbalimbali kwa watumishi na viongozi na mashirika husika.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WAZIRI wa Viwanda, Biashara na  Uwekezaji, Charles Mwijage amesema Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji wa biashara kupitia Kituo cha Uwekezaji  Nchini (TIC).

  Akizungumza katika Mkutano kati wa Wafanyabiashara wa Tanzania na  Ubelgiji, Mwijage amesema kuwa mazingira yaliyowekwa ni rafiki kwa uwekezaji katika mbalimbali ikiwemo ya Kilimo  cha biashara.

  Mwijage amesema kuwa Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi duniani hivyo wawekezaji wana nafasi ya kufanya uwekezaji kutokana na kuwa nchi ya amani ambapo wawekezaji wanaweza kuwekeza na kuzalisha bila kuwepo kwa vikwazo.

  Amesema kuwa serikal ya awamu ya tano inapambana na rushwa ili kuweza wananchi waweze kuishi bila rushwa.

  Mwijage amesema maeneo ya kufanya uwekezaji yamepanagwa katika maeneo ya biashara, kilimo, Miundombinu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Madini,  Gesi , Utalii pamoja Uvuvi.

  Amesema kuna ushirikiano wa muda mrefu kati Tanzania na Belgium hivyo milango ya uwekezaji iko wazi na nchi nyingine zimeweka mikakati ya uwekezaji.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyabiashara wa nchi ya Ubelgiji juu ya serikali ya Tanzania kuweka wazi milango ya uwekezaji leo jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Kundi la Wafanyabiashara wa Umoja wa Ulaya, Rose Blackie akizungumza katika mkutano wa wafanyabishara uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC, Clifford Tandari akizungumza na wafanyabiashara wa nchi ya Ubelgiji juu ya serikali ya Tanzania kuweka wazi milango ya uwekezaji leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Wafanyabiashara wakiwa katika Mkutano wa kuangalia juu ya uwekezaji leo jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Mwenyekiti  wa UWT  wilaya ya  Mufindi Marcelina Mkini (kushoto)  akimpongeza  mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jecsa Msambatavangu kwa  kazi nzuri na kubwa anayoendelea  kufanya mkoani hapa
  Mbunge wa  viti maalum Mary  Chatanda  akisalimia katika kikao cha baraza  kuu la UWT mkoa wa Iringa
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akifungua  baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa
  Marcelina Mkini mwenyekiti wa UWT  Mufindi  akitoa pongezi kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia  katikati ni mwenyekiti wa UWT mkoa  Zainab Mwamwindi na  kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Hafsa Mtasiwa
  Wajumbe wa baraza kuu ya UWT  mkoa wa Iringa
  Msambatavangu  akiagana na wajumbe wa baraza   kuu la UWT mkoa  wa Iringa kutoka  kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini , mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Rose Tweve
  Wajumbe wa baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa  wakimpokea mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  wa tatu kushoto  akilakiwa na mbunge Rose Tweve  kushoto ni mwenyekiti wa UWT mkoa na mbunge wa  viti maalum Zainab Mwamwindi  na wa  pili  kulia ni mbunge Ritta kabati  akisalimiana na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina mkini  huku kulia ni katibu wa UWT mkoa
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa tatu  kushoto akiwa na viongozi  mbali mbali wa mkoa
  Mwenyekiti wa UWT  mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akitoa salam za utangulizi

  Na matukiodaimaBlog
  BARAZA  kuu  la  umoja  wa wanawake  mkoa  wa Iringa limempongeza mwenyekiti wa chama  cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa  kuwa  kiongozi  wa mfano ndani ya  mkoa na nje ya  mkoa wa Iringa na  hivyo  kumwomba  kugombea  tena nafasi  hiyo ya  uenyekiti mwakani 2017 .

  Akitoa pongezi  hizo  leo  wakati  akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa baraza kuu la UWT  mkoa  lililokutana  kwenye  ukumbi wa CCM wilaya ya  Iringa mjini ,mwenyekiti wa  UWT wilaya ya  Mufindi Marcelina  Mkini ambae  pia ni mjumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa (NEC)  alisema  kuwa  ushindi mkubwa ambao CCM iliupata katika  uchaguzi mkuu mwaka jana  uchaguzi  uliomwezesha Rais  Dkt  John Magufuli  kushinda kwa  kishindo dhidi ya  wapinzani  wake ni pamoja na kazi  nzuri  iliyofanywa na Msambatavangu katika  kampeni  za uchaguzi mkuu .

  Mkini  alisema  mkoa  wa Iringa kwenye  uchaguzi huo  uliweza  kufanya  vizuri kwa kushinda  majimbo 6 kata ya 7  yaliyopo ndani ya  mkoa  wa Iringa na kuwa  pamoja na kila  mmoja  kushiriki katika  kupigania ushindi  huo wa chama  ila  wao kama  wanawake  hawanabudi  kumpongeza mwanamke mwenzao ambae ndie mwenyekiti wa chama  mkoa kwa  kuonyesha Taifa  kuwa  wanawake  wanauwezo wa  kuongoza .

  '' Naomba  kuchukua nafasi hii kwa niaba ya  wanawake  wenzangu  kukupongeza  sana mwenyekiti  wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu  umeonyesha  mfano  mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka  wakati wa kampeni  wewe  ulisimama  kidete   kuhakikisha  chama kinashinda  kwa  kishindo  mbali ya figisu figisu zilizokuwa zikielekezwa kwao  ila hukuteteleka ''

  Mbali ya mwenyekiti  kufanya  vema katika  kampeni  za 2015  ila  hajaacha  kuitumikia vema  jamii ya  mkoa wa Iringa ikumbukwe mkoa  umepata  misiba miwili mikubwa  ukiwemo wa  aliyekuwa mwenyekiti  mstaafu wa CCM  mkoa Tasili Mgoda na mwasisi wa maendeleo ya   wilaya ya  Mufindi Joseph  Mungai shughuli  zote  zimeratibiwa  vema na Msambatavangu tena  pasipo  ubaguzi  wowote .

  '' Mwenyekiti   wetu  anafanya kazi  vizuri  ndani ya  mkoa  wetu  tena  pasipo ubaguzi wowote  na ni mtetezi  mzuri  sana kwa  wanawake  ndani ya  mkoa na hanaga unafiki kabisa  kwani  yeye  siku  zote  husema  kweli  tupu ''

  Mkini  alisema   kuwa   kutokana na  utendaji  kazi wake mzuri  ndani ya  chama  wao  wanaona  bado  mwenyekiti huyo anauwezo  wa  kuwavusha wana CCM kwa miaka  mingine mitano ijayo  hivyo  kumshawishi  kuingia tena ulingoni  mwakani 2017 katika  uchaguzi  mkuu wa  viongozi ngazi mbali mbali za  chama .

  Mwenyekiti  wa UWT  mkoa  wa  Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la  UWT  mkoa  wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt  Magufuli  alisema  kuwa   wao kama  wanawake wa CCM  wameendelea   kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli na  kuwa  kubwa  zaidi  ni jinsi  Rais alivyoweza  kujibu maswali ya  watanzania  kupitia   mkutano wake  wahariri  wa  vyombo   mbali mbali  vya habari  hapa nchini.

  .Kwa  upande wake  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa ,Msambatavangu  pamoja na  kupongeza  pongezi za baraza  hilo  dhidi yake  na  zile za Rais alisema atahakikisha pongezi za  wanawake hao zinamfikia Rais Dkt Magufuli  huku  akisisitiza  wanawake  kuendelea  kuongoza  nafasi zao kwa kujiamini  zaidi badala ya  kutanguliza  uoga usio  wa lazima .

  Alisema  wakati  chama kinajiandaa kwa  chaguzi zake mwakani ni vizuri  wanawake  kuanza  kujipima ama  kuwapima  wale ambao wanaingia kuwania nafasi mbali mbali ili  kupata  viongozi wenye  uwezo wa kuwatumikia  wananchi hasa katika  kipindi   hichi  cha kujenga chama  chenye  nguvu na  uongozi wenye  uwezo wa kuendana na kauli  mbiu ya  Rais ya hapa Kazi  tu.


  Kwani  alisema  wapo baadhi ya  watu  ndani ya  CCM kazi yao ni  kusubiri uchaguzi hadi  uchaguzi  kufanya kazi  za chama na kuwa  wanachama hao hawapo kwa  ajili ya  kuwatumikia  wananchi bali  wapo kwa ajili ya  kutumikia matumbo yao jambo ambalo halikubaliki  kwa uhai na  nguvu ya CCM .

  Mwenyekiti   huyo  alisema   hivi  sasa  wananchi  wanauelewa mkubwa  juu ya siasa   na uongozi  hivyo ni lazima  wanaopewa nafasi za  kugombea  ni lazima  wawe wanakubalika katika  jamii  inayowazunguka   vinginevyo  chama  kinaweza  kuyumba iwapo  watu  wasio na sifa  watapewa nafasi za  kugombea hivyo  ni  vizuri  kuanza  kuwatafuta  watu  wanaofaa ambao hawapo  ndani ya  CCM kujiunga na CCM ili mbeleni  waje kugombea kupitia  CCM.

  Kwani  alisema  hivi  sasa kote  duniani ni  vema  viwili  pekee  ndivyo vimebaki kuitwa  vyama tawala na  vyama  hivyo ni  nchini China na Tanzania pekee ila maeneo  mengine  yote  vyama  tawala  imeondolewa madarakani    kwa  kuwa CCM lengo lake ni  kuendelea  kuongoza ni  vizuri kila mwanachama na kila kiongozi  kuhakikisha anawajibika   vema kwa  wananchi kama ambavyo mwenyekiti wa chama Taifa Rais Dkt Magufuli anavyoliongoza Taifa kwa  faida ya  watanzania na  vizazi vijavyo.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  tabo10

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa tiketi ya kusafiria ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, kutoka kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa, kabla ya kusafiri na Ndege hiyo kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, leo Novemba 14, 2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na marubani na wahudumu wa ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 baada ya kukabidhiwa ticket ya kusafiria na Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa kulia leo Novemba 14, 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Makamu wa Rais alisafiri na ndege hiyo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wakati akiindia ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Abiria waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza na kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambapo ndege hiyo pia ilibeba abiria wa kawaida katika safari hiyo.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

  Amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.

  “Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika”

  Makamu wa Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika ufanyaji wake wa kazi kwa viwango bora zaidi.

  Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

  Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika  wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana, Misungwi,Kwimba na Magu.

older | 1 | .... | 1039 | 1040 | (Page 1041) | 1042 | 1043 | .... | 1897 | newer