Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1038 | 1039 | (Page 1040) | 1041 | 1042 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mhe Joseph Mkirikiti akikabidhi lebo za vifungashio kwa Bi Safina Selemani mzalishaji wa mafuta ya alizeti kutoka kata ya Nandagala B kikundi cha CHIUKUTE, lebo hizo zimetengenezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade)
  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Joseph Mkirikiti akipokea lebo za vifungashio kwa wazalishaji wa mafuta ya alizeti katika mkoa wa Ruangwa kata ya Nandagala B kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) Bw Edwin Rutageruka

  MAFUNZO YA UFUNGASHAJI BORA, KUWEKA NEMBO, RAJAMU NA MASOKO (MASASI & RUANGWA) NA KUTOA LEBO KWA WAZALISHAJI WA MAFUTA YA ALIZETI

  Mhe Joseph Mkirikiti Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ahimiza uzalishaji wa mafuta ya Alizeti, Ufuta na Nazi kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa sababu ni kioo na msingi imara ya kuwawezesha ajira iwe ya kudumu na tena ajira bora kwa wananchi. 

  Hayo aliyasema akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa vitendo kwa wakulima ambao ni wazalishaji wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta, nazi na alizeti wa Ruangwa na akipokea lebo za vifungashio vya mafuta ya alizeti kwa wazalishaji wa bidhaa za mafuta ya alizeti zaidi ya 1000 zilizotengezwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade). 

  Mafunzo hayo yameanza tarehe 7 hadi 10 Novemba, 2016 juu ya namna ya ufungashaji bora wa bidhaa za mbegu za mafuta ya ufuta, alizeti na nazi, kuwa na lebo bora kwenye kila bidhaa inayozalishwa, rajamu (branding) kwenye bidhaa hizo, namna ya kuboresha ubora wa bidhaa na mbinu ya kuuza bidhaa hizo kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wazalishaji wapatao 50 wa Ruangwa na 50 wa Masasi.

  “Elimu mtakayopata hapa itawachukueni kwenye hatua nyingine ya kufanya maboresho makubwa ya ajira yenu, hapa nchini mahitaji ya mafuta ya kula kwa mwaka ni lita 350,000 wakati uzalishaji kwa sasa ni asilimia 40 pekee na asilimia 60 huagizwa kutoka nje ya nchi hivyo basi, tuna fursa kubwa ya kunufaika na sekta hii.” 

  Akasisitiza kuwa ni vyema kusikiliza na kutumiamafunzo hayo kwa makini na kwenda kuambukiza elimu hiyo kwa wengine waliokosa kuhudhuria mafunzo haya ili kwa pamoja kama Taifa tufanye biashara yenye faida na kufikia malengo ya Taifa na mtu mmojammoja. 

  Mhe Mkirikiti aliendelea kusema kuwa Ruangwa iwe mstari wa mbele sasa katika kuzalisha bidhaa zenye ubora na kupitia msaada wa lebo kutoka TanTrade na vifungashio bora ili bidhaa zionekane kwenye macho ya mlaji kabla ya kutumia na kuleta ufahari kwa nchi ya Tanzania pindi bidhaa zetu zitakavyoweza kuvuka nje ya nchi hivyo watumie mafunzo hayo kutangaza bidhaa zetu bora zaidi. 

  Alieleza kuwa anaimani kupitia mafunzo haya yataboresha pia maeneo ya kazi ili ubora usipungue na pia wakiendelezwa wajasiliamali wadogo kutapelekea kuanzishwa viwanda vidogo vingi zaidi na kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mafuta na maendeleo kuja kwa haraka sana na kupunguza kwa kiwango kikubwa kuagiza mafuta kutoka nje.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendelo ya Tanzania (TanTrade) alisema moja ya kazi ya taasisi ni kuwajengea uwezo na kuwaendeleza wazalishaji wadogo, hivyo imeandaa mafunzo haya kwa ushirikiano wa wadau wa kimkakati ambao ni SIDO na TBS ilikuimarisha fursa kwa wakulima kuzalisha kitu cha thamani ili kuweza kuleta ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

  “Mwezi Agosti kwenye maadhimisho ya siku ya wakulima (88), TanTrade ilifanya ziara fupi kwenye wilaya za Ruangwa, Masasi na Kilwa na pia kupita kwenye mabanda ya washiriki kubaini fursa zilizopo kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia vikundi mbalimbali vilivyoshiriki maadhimisho hayo ili kuendeleza fursa hizo kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.”

  Akaongeza kwa kusema kuwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania (TanTrade) ilipobaini changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye kilimo biashara (Agribusiness) hivyo ikaona ni vyema kutatua changamoto hizo kwa kuanza kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa hizo kwa kutoa mafunzo kwa vitendoyatakayojikita kwenye mbinu za kutafuta masoko na mikakati ya kuingia sokoni, uzalishaji wa viwango vyenye ubora wa mbegu za mafuta (Alizeti, Ufuta na Nazi) na vifungashio vya mafuta hayo, Nembo ya utambulisho wa bidhaa zao (lebo) na elimu juu ya mfumo wa matumizi ya simbomilia (barcode) na nembo ya ubora katika wilaya ya Ruangwa na Masasi na kuwatengeneza lebo ili bidhaa zao ziweze kutambulika kwenye masoko yao. 

  Akishukuru kwa niaba ya kikundi cha CHIUKUTU kilichopo kata ya Nandagala B wilaya ya Ruangwa Bibi Safina Selemani baada ya kupokea lebo kwaajili ya bidhaa zao kutoka kwa Mkuu wa Wilaya alisema changamoto kubwa ilikuwa ni ukosefu wa elimu ya namna ya uboreshaji wa uzalishaji bora wa bidhaa za mafuta, hivyo ni fursa ya pekee kwao kupatiwa mafunzo na lebo hizo ili kujiendeleza kwenye uzalishaji.

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akihutubia katika hafla ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akizungumza kwenye hafla hiyo.
  Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania Mama Anna Mkapa (kushoto), na Mwenyekiti wa bodi ya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakifurahia jambo katika hafla hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania, Mama Anna Mkapa (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, wakikata keki katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bayport Tanzania yaliyofanyika Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam juzi.
  Ni furaha tupu katika maadhimisho hayo.
  Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Hafla ikiendelea.
  Keki maalumu ya hafla hiyo.
  Keki ikiliwa.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga (kushoto), akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.  Na Dotto Mwaibale

  TAASISI ya Kifedha ya Bayport Tanzania juzi iliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na kuelezea mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi hicho.

  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga alisema ndani ya miaka 10 wameweza kupiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi.

  "Tumepiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamenufaika na huduma zetu" alisema Mbaga.Alisema kupitia taasisi hiyo wananchi wameweza kuanzisha biashara na kujenga nyumba ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto.

  Mgeni rasmi wa hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema Serikali inaipongeza taasisi hiyo kwa huduma za mikopo inayotoa kwa wananchi hivyo kusaidia kuinua pato la taifa na mtu mmoja mmoja.

  "Changamoto kubwa iliyopo ambayo mnapaswa kuiangalia ni riba kubwa katika mikopo yenu jaribuni kuliangalia jambo hilo kwa karibu" alisema Kairuki.

  0 0


  Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya vifurushi vya kimataifa ndani na nje ya nchi, vitakavyomwezesha mteja kupiga simu kwenda nchi zaidi ya 20 kwa gharama nafuu. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na Meneja wa kitengo hicho, Alice Paulsen.

  Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya vifurushi vya kimataifa ndani na nje ya nchi, vitakavyomwezesha mteja kupiga simu kwenda nchi zaidi ya 20 kwa gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo na Meneja wa kitengo hicho, Alice Paulsen.
  · sasa wateja kununua vifurushi vya kupiga simu za kimataifa kwenda nchi zaidi ya 20

  · wateja kujitengenezea vifurushi vya intaneti pindi wanapotembelea nchi ambazo Airtel inazofanya biashara barani Afrika

  Dar es Salaam, Alhamis 10 Novemba 2016, Airtel Tanzania leo imetangaza ofa kabambe itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kununua vifurushi wavipendavyo na kupiga simu kwenda nchi zaidi ya nchi 20 kwa gharama nafuu

  Pamoja na vifurushi vya kupiga simu nje ya nchi , Airtel pia imezindua vifurushi vya intaneti vya roaming mahususi kwa wateja wanaotembelea nje ya nchi vijulikanavyo kama “Safari Internet Roaming” vitakavyowapatia uhuru wateja wake kupanga matumizi yao ya intaneti pindi wanapotembelea nchi ambazo Airtel inafanya biashara zake barani Afrika. Nchi hizo ni pamoja na Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Kenya, Gabon, Ghana, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Uganda na Zambia.


  Akitangaza ofa hiyo Meneja Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo alisema” Tunayofuraha kutangaza ofa nyingine kabambe itakayowapa wateja wetu uhuru katika mahitaji yao ya mawasiliano na kuwawezesha kuwasiliana na familia, marafiki na wafanyabiashara wenzao barani Afrika na kimatifa kwa urahisi zaidi. Ofa yetu ya kupiga simu nje ya nchi inamhakikishia mteja thamani ya pesa yake na urahisi katika huduma za mawasiliano na kupata faida lukuki za kujiunga na timu SIBANDUKI. Vifurushi vyetu vya kupiga simu nje ya nchi zinapatikana kwa siku, wiki au mwezi kwa kupiga *149*13# au kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#. Mteja anaweza kujinunulia kifurushi akipendacho na kupiga simu kwenda zaidi ya nchi 20 kwa gharama nafuu”

  Tembo aliongeza kwa kusema “vifurushi vipya vya intaneti vya roaming yaani wateja wanaotembelea nje ya nchi zinaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za mawasiliano za kibunifu, gharama nafuu na zenye ubora kwa watanzania zinazovuka zaidi ya mipaka ya nchi. Idadi ya watanzania wanaosafiri nje ya nchi kibiashara na safari za kawaida inakuwa kwa kasi, vifurushi vyetu vipya vya nje ya nchi vitawawezesha kupanga matumizi yao na kuwaepusha na ankra kubwa na kuwahakikishia mawasiliano mahali popote waliko”

  Ofa hizi za kupiga simu nje ya nchi na vifurushi vya intaneti nje ya nchi ni kwa wateja wa malipo ya awali yaani ”prepaid” nchi nzima

  Nchi ambazo mteja anaweza kupiga simu nje ya nchi kwa kununua vifurushi vya kimataifa ni pamoja na Zambia, Malawi, DRC, South Africa, India, China, USA, Canada, Uganda, Rwanda, Kenya, Oman, UAE, Saudi Arabia, Yemen, Lebanon, Pakistan, Qatar, Uingereza, Itali na Ujerumani.

  0 0


  Mwalimu wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
  Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiendelea na mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi.

  Mwalimu wa Chuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
  Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,MIKUMI .
   

  Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha watanzania tamaduni ,mila na desturi kuulinda utamaduni wetu , ambao unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku. 

  Akizungumza na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania . 

  Amesema utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
   
  Amesema chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Community College cha nchini Canada kinaandaa kozi hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali. 

  Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
  Aidha mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala. 

  Ayo amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
   
  Ametoa rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda.

  0 0

   Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta Ukiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.

  Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.

   Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya utoaji wa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli(Katikati), Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan(Mwenye shungi) Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa (wa mwisho kushoto) na Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alli Idd (wa mwisho kulia) wakifuatilia idaba ya kuuaga Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee kwa ajili.
   Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ukiwa katika eneo maalum mbele ya waombolezaji kwa ajili ya kufanyiwa idaba na tukio la utoaji heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.

  Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta ukiwa katika eneo maalum mbele ya waombolezaji kwa ajili ya kufanyiwa idaba na tukio la utoaji heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi Mhe. Angela Kairuki akitoa salamu za serikali wakati wa shughuli ya utoaji heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwaeleza jambo Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif alli Idd(katikati) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

   Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta kabla ya kusafirishwa kwenda Bungeni Mjini Dodoma na Hatimaye Mkoani Tabora kwa ajili ya Maziko.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na waombolezaji wakati wa shughuli za utoaji heshima kwa Mwili wa Marehemu Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta.   


  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO

  AZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la tatu la kitaifa la Afya litakalofanyika Novemba 14 mwaka huu Jijini Dar es salaam. 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Rais wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Dkt. Omary Chillo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam wenye lengo la kujadili maendeleo ya sekta afya nchini. 

  Aidha Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo litajadili jitihada ilizofikia Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya kimkakati ya maisha yenye afya njema (SDG-3) yaliyokusudiwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya wachapakazi. 

  Dkt. Chillo aliongeza kuwa kongamano hilo pia linatarajia kujadili mikakati ya kuboresha sheria ya usalama na afya makazini, kanuni na ufanyaji kazi nchini kwa ajili ya maendeleo ya wafanyakazi na usalama wao. 

  Kwa mujibu wa Dkt. Chillo alisema kuwa kongamano hilo pia linatarajiwa kufanyika kuwakutanisha wataalam wa sekta ya afya 700 na kuratibiwa na taasisi tano zikiwemo MoHCDGEC, TMHS,APHFTA,CSSC na BAKWATA. 

  Mkutano huo ambao utakutanisha taasisi 53 za afya, zinatarajia pia kushiriki katika maonesho ya bidhaa zinafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto pamoja na TAMISEMI tangu kuanza kwake 2014.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa kuamkia leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa kwenda Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.

  Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

  Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.

  Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”

  Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.

  Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.
  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.

  0 0

  UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo hivi sasa upo kwenye mchakato wa kukiongezea nguvu kikosi hicho.

  Hatua hiyo imekuja ikiwa ni nia ya dhati kabisa ya Azam FC kutaka kufanya vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na michuano ya Kimataifa inayokuja kuanzia mwezi ujao na mwakani (Kombe la Kagame na lile la Shirikisho Afrika).  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016


   
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel John Sitta aliyefariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.

  Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

  Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi watapata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.

  Wakati huo huo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar Mhe. Hafidh Ali Tahir kilichotokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia muda mfupi alipofikishwa hospitali baada ya kuugua ghafla.

  "Nimeshtushwa sana na kifo cha Mhe. Hafidh Ali Tahir na ninakuomba Mhe. Spika Job Ndugai unifikishie salamu za pole kwa Familia ya Marehemu, Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Dimani, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu.

  "Tutamkumbuka Mhe. Hafidh Ali Tahir kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika utumishi wa umma, katika michezo na akiwa mwakilishi wa wananchi, kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana" amesema Rais Magufuli na kumuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi. Amina.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  11 Novemba, 2016

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.

   Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima  za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
    Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole binti wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimpa pole Mhe. John Sitta, mtoto wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo  Novemba 11, 2016

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Nobemba 11, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia  wa  aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 11, 2016

  0 0
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo tarehe 11 Novemba, 2016 baada ya afya yake kuimarika.

  Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

  "Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.

  "Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth Magufuli. 

  Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  11 Novemba, 2016

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wabunge, viongozi wa kitaifa na watumishi wa Ofisi ya Bunge kuuaga mwili wa Spika Mstaafu, Samwel Sitta.

  Bw. Sitta alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 7 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.Akizungumza  wakati wa kuuaga mwili huo Bungeni mjini Dodoma leo (Ijumaa, Novemba 11, 2016), Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, mke wa marehemu Mheshimiwa Magreth Sitta, mama wa marehemu Hajat Zuena Fundikila na familia ya marehemu na wabunge wote.

  “Nitumie fursa hii pia kukupa pole Mheshimiwa Spika kwa pigo ambalo Bunge lako tukufu imelipata kwa kumpoteza mmoja wa viongozi mahiri wa Bunge hili katika historia ya nchi yetu. Msiba uliotupata wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa (2005-2010) na Mbunge Mstaafu wa jimbo la Urambo mkoani Tabora ni mzito.”

  Amesema Bw. Sitta alikuwa mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.  “Serikali imepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Historia ya Mzee Sitta ni pana sana. Tunatambua utumishi uliotukuka katika nyadhifa mbalimbali alizozitumikia. Tutamkumbuka kwa utumishi wake,” amesema.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa: “Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani yake ili tuweze kufikia japo mema machache aliyoyatenda katika enzi za uhai wake.”

  Enzi za uhai wake Mhe. Sitta alibahatika kufanya kazi na Marais wa awamu nne zilizopita tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, akiwa mbunge kwa miaka 30.

  Nyadhifa nyingine alizowahi kushika ni pamoja na Mkuu wa Mikoa ya Iringa na Kilimanjaro, Waziri wa Ujenzi, Waziri anayesimamia Ustawishaji Makao Makuu, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapili kulia) akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa Spika Mstaafu Mama Margareth Sitta baada ya mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sita kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiusubiri mwili wa Spika mstaafu, Samuel Sitta uteremshwe kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016
  Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta ukiteremshwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Novemba 11, 2016.
  Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mwili wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta ukiingizwa bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao maalum cha bunge cha kumuenzi Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Samuel Malecela akimpa pole mjane wa Spika Mstaafu, Margareth Sitta bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. 
  1A2358 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye jeneza la Spika Mstaafu Samwel Sitta, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta, bungeni mjini Dodoma, Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)​

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norwaya Bw. Victor Mlundo wakati wa kuzindua majengo mapya ya Wodi ya Watoto Kinamama katika Hospitali ya Mnazi mmjoja uliofanyika leo .
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chumba cha kulelea Watoto wachanga wakati alipotembelea majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya uzinduzi rasmi leo,(wa pili kulia) mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia Mcha 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Hauklend Bw.Eivend Hansen wakikata utepe kuzindua jengo la Wodi ya Watoto wakati wa uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto uliofanyika leo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizari ya Afya Nd,Halima Maulid mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Viongozi wengine mara alipowasili katika uzinduzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja leo

  0 0


  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia.

     KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imefunga huduma za mawasiliano ya intaneti bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) itakayowawezesha madaktari, wafanyakazi wengine, wagonjwa pamoja na wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma ya mawasiliano ya intaneti bure yenye kasi ya hali ya juu. 

   Akikabidhi huduma hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba alisema kampuni hiyo imetumia jumla ya shilingi milioni 120 kufunga huduma bure ya intaneti katika kituo hicho na itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.

   Akifafanua zaidi Bw. Kindamba alisema huduma hiyo ambayo itagharimu shilingi milioni 10 kwa kila mwezi ambazo zitakuwa zikilipwa na TTCL ikiwa ni mchango wake kwa jamii na hasa kwa matibabu yanayofanyika katika kituo hicho itakuwa ikitolewa kwa teknolojia ya Wi-Fi bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Novemba 10, 2016 hadi Novemba 10, 2017.

   "Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya na kazi kubwa inayofanywa na Taasisi hii, TTCL tumetoa intaneti yenye kasi hadi kufikia spidi ya 100Mbps, spidi hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma kwa wananchi, kuimarisha mawasiliano miongoni watumishi wa JKCI na nje ya Taasisi, kupashana habari za kitabibu na kubadilishana taarifa za kitabibu miongoni mwa wataalamu kutoka hospitali za ndani na hospital za nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Kindamba. 

   Alisema mbali na huduma hiyo TTCL imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mawasiliano ya uhakika yanatumika katika sekta ya afya ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na tayari imefanikiwa kuunganisha hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es salaam kupitia Mkongo wa TTCL ambao umeunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. 

   Aidha alizitaja hospitali nyingine zinazonufaika na huduma ya mawasiliano hayo ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Hospital ya Amana, Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Bagamoyo, Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro na Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.

   Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akitoa shukrani zake mara baada ya kukabidhiwa huduma hiyo alisema TTCL inapaswa kutambua imetoa mchango mkubwa wa kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali wanaopatiwa huduma katika taasisi hiyo. 

   Alisema kwa maendeleo ya sasa huduma za kitabibu zinatolewa kwa njia ya intaneti kwa wataalamu wa kituo kimoja kufanya mawasiliano na kituo kingine jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma hizo kwa wagonjwa na hata kukabiliana na changamoto ya baadhi ya wataalamu wa afya na vifaa vya matibabu.

   Alisema kwa JKCI huduma za intaneti sio kwa ajili ya starehe bali ni muhimu zaidi kusaidia madaktari katika kutekeleza majukumu yao, jambo ambalo kwa sasa watakuwa wakilipata muda wote wawapo eneo la kazi. Profesa Janabi aliongeza kuwa kiasi cha shilingi milioni 120 ambazo kituo cha JKCI ilipaswa kukilipa kwa gharama ya huduma hiyo sasa watakielekeza kwa wagonjwa zaidi ya 20 watakaofanyiwa upasuaji kwa fedha hizo ikiwa ni kutambua mchango wa TTCL katika kusaidia huduma za afya kwa jamii. 

  "Ndugu Mkurugenzi kwa msaada wenu huu tambueni kuwa mmeokoa maisha ya wagonjwa takribani ishirini ambao hawana uwezo kulipia gharama za matibabu na sasa JKCI itawafanyia huduma za upasuaji kwa gharama mlizozitoa kwetu kutokana na mchango wenu kwa jamii...tutajitahidi kuwapa taarifa juu ya wagonjwa hao na idadi yake. Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano. Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano.

  0 0


  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  YALI Regional Leadership Centre ya Nchini imedhamiria kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana Tanzania Bara na Visiwani kwa kumualika moja ya waandamizi wa masuala ya ujasiriamali kutoka nchini Jordan Laith Al Qassam ili kutoa mafunzo mbalimbali kwa kuhakikisha wanapata nafasi za kujiajiri na kuongeza pato la taifa.

  Akizugumza kabla ya kuanza semina hiyo,Muàndaaji wa Semina hiyo Fabian Shayo amesema kuwa mafunzo hayo yajulikanayo kama Blue Ocean Strategy yatahusisha zaidi masuala ya ujasiriamali hususani kwa vijana na mkufunzi Al Qassama ambaye amebobea katika masuala hayo atatoa elimu kwa vijana waliojitokeza.

  Shayo amesema Blue Ocean Strategy imeweza kusaidia watu wengi hususani vijana katika masuala ya ujasiriamali na hata kuanzisha makampuni duniani kote pia imeweza kutengeneza soko la kibiashafa na kukuza faida.

  Mkufunzi wa mafunzo hayo, Al Qassama ambaye ni mmoja ya waandamizi wa kiwanda cha Jordan ICT na kukiwezesha kuwa moja ya makampuni makubwa duniani amesena kuwa vijana wengi wanaamini kuwa fedha ndiyo kila kitu na kushindwa kuelewa kuwa mawazo yanaweza kuwa msaada kwao.

  Blue Ocean Strategy itaendeshwa katika vipindi vitatu tofauti kwa bara na visiwani kwa ajili ya kuwapatia elimu vijana kwa watakaoleta mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya ujasiriamali kupata fursa za ajira na kukuza kiwango cha maendeleo ya kiuchumi katika taifa.

  Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Vijana waliowahi kushiriki semina hiyo(Alumni) wametumia fursa hii kuwasaidia vijana wenzao ili kuweza kuangalia wanakwamuka vipi kiuchumi kwa kupitia njia ya ujasiriamali.
  Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati yao ya kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutumia sera ya ujasiriamali. Kulia ni Mkufunzi Laith Al Qassam na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha Fortunatus Eklklesiah.
  Mkufunzi Laith Al Qassam akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa vijana na nini wanatakiwa kufanya ili kuondoa dhana ya kuajiriwa au kuamini fedha zinaweza kufanya kila kitu. Kulia ni Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano, Khalila Mbowe na kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uandaaji wa mafunzo hayo, Fabian Shayo.
  Mkufunzi wa Semina hiyo Laith Al Qassam akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliojitokeza yaliyoendeshwa na YALI Regional Leadership Centre kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

  0 0

  Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala amejitosa kusaidia kurejesha heshima ya mkoa wa Tabora katika elimu hasa kwa wasichana ambao ndio nguzo kubwa kwa familia na maendeleo ya taifa.

  Mrembo huyo ameamua kufanya hivyo kwa kutembelea shule mbili za Tabora Girls na Isevya kuongea na wanafunzi, kuwapa moyo na kuangalia matatizo yanayowasumbua katika kujipatia elimu.

  Akizungumza na Moblog amesema kwamba amekuwa na masikitiko makubwa na matokeo ya mitihani ya kitaifa ya sekondari kwa miaka mitatu ilhali simulizi za Tabora miaka iliyopita ni za kufurahisha sana uikionesha kwamba mkoa huo ndio kitovu hasa cha elimu.

  Anasema ukisoma nyaraka mbalimbali unaona jinsi Tabora ilivyokuwa ngome ya elimu huku watanzania wengi wakifika hapo pia kupata elimu ya sekondari.
   Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala akizungumza wa shule ya sekondari Tabora Girls hivi karibuni.

  “Kwa kweli pamoja na masimulizi mazuri kuhusu elimu Tabora miaka ya 80 na 90 ,nilichagua Tabora girls kwa sababu ni shule aliyosoma mama yangu mzazi form 1 mwaka 1977 mpaka 1980 mpaka na aliisifia sana shule yake hiyo na nikapenda niweze kuwa karibu nao kuhakikisha wanafunzi wote wanamaliza,na Isevya ilikua chaguo la pili kwasababu ilikua ni shule ya kutwa (day) na nilipendelea kuongea na wanafunzi hao” alisema Genevieve.

  Mkoa wa Tabora ambao unapatikana kati ya Magharibi ya Tanzania kwenye uwanda wa latitudo 40-70 Kusini na longitudo 310 - 340 mashariki ukipakana na mikoa ya Shinyanga, Katavi, Singida, Kigoma na Dodoma ni mji ulioanzishwa na wafanyabiashara wa Kiarabu kwenye miaka ya 1850 ukijulikana kama Kazeh .

  Kihistoria Kazeh ambayo ilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa, mwaka 1871 robo ya mji ilichomwa moto na kuvurugwa na mtawala wa wanyamwezi Mirambo .

  Ingawa mwaka 1885 hadi 1891 wajerumani walijaribu kutawala, historia zinasema kwamba mji huo ulikuwa na vurugu kubwa lakini baadae ukatawaliwa na wajerumani wakafanya mji wa utawala kabla ya vita kuu ya kwanza kuingia na wao kung’olewa.
  Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na mwalimu wao alipofanya ziara shuleni hapo.

  Pamoja na historia yenye misukosuko ya Mkoa wa Tabora ambao ni moja ya mikoa yenye eneo kubwa unategemea sana kilimo kufanikisha maisha lakini kwa miaka mingi mkoa umekuwa ukididimia kimaendeleo na kijamii.

  Mkoa wa Tabora ambao umekua wa mwisho kwa miaka mitatu mfululizo mwaka 2013,2014 na 2015 unahitaji nguvu kubwa ya kujiondoa katika shida ya kuporomoka katika elimu

  Mrembo Genevieve anasema ziara yake katika shule hizo imemfumbua macho na kuona haja kubwa ya kuendelea na programu za kufufua matumaini.

  Pamoja na kuwashukuru walimu kwa ushirikiano waliompa aliwataka wanafunzi kuweka mkazo katika imani, matumaini na kutekeleza ndoto zao katika uwanda mkubwa zaidi.
  Aidha pamoja na kuzungumza "HAVE FAITH,HOPE FOR MORE AND DREAM EVEN BIGGER", pia aliwaasa kuwa elimu ni msingi mzuri wa maisha na kuwa wasiharakishe na kupotoshwa na mambo ya kidunia kwani haya maisha yapo.

  Akiwa na wasichana wa shule ya Tabora Girls walimweleza changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni pamoja na kutokuwepo na uzio kwenye shule yao hiyo, uhaba wa vitabu, upungufu wa walimu, uhaba wa upatikanaji wa habari mubashara, kwa wanafunzi kwamba hawana king'amuzi,kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wanauhitaji wa msaada wa kofia pamoja na mafuta ya kuwakinga na jua.

  Matatizo hayo yanatokana zaidi na kwamba wengi wao wanatoka kwenye mazingira duni. Changamoto nyingine ni pamoja na kuwa na zahanati ambayo ina uhaba wa vifaa mfano:vyandarua vya kutosha pamoja na vitanda,pia kwa wanafunzi ambao wanaulemavu wa macho ambao ni hafifu na vipofu kabisa hivyo kuna uhaba wa brail paper.

  Ziara fupi ya Mrembo wa Tanzania 2010 Genevieve Mpangala kwa shule mbili za jijini Tabora za Isevya Secondary School na shule ya vipaji maalum ya wanawake Tabora girls.

  Amesema katika mazungumzo yake na wanafunzi hao amebaini pia kwamba kutofanya vyema kwa wanafunzi pia kunasababishwa na wanafunzi hao kutumia madawa ya kulevya, utoro, mimba za shuleni na wazazi kuozesha mabinti katika umri mdogo kabla ya wao kumaliza shule.

  0 0

   Wananchi wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.
   Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.
   Wananchi wakiwa eneo la ajali
   Wananchi wakiwa eneo la ajali.
   Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.
  Prado yenye namba  T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.

  Na  Dotto Mwaibale

  WATU kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye namba  T 177 AHH, pikipiki na lori jingine. 

  Ofisa wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

  "Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa" alisema ofisa huyo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea  hata hivyo alisema alikuwa hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.

  Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.


  0 0
  Watumishi wa TEMESA Njombe wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (Mwenye shati la rangi ya bluu) alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Njombe.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto), akimsikiliza Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga (kulia) wakati alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji wa kazi wa kituo hicho.

  Na Theresia Mwami TEMESA Njombe.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu ameahidi kuwapatia makasha yenye vitendea kazi vya karakana pamoja na mashine ya kucharge betri za magari kwa wafanyakazi wa kituo cha TEMESA Mkoani Njombe.

  Dk Mgwatu amesema kuwa ameamua kuleta mabadiliko katika ufanyaji kazi kwa kuhakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

  “Nitaleta vifaa vinavyohitajika nataka kila mmoja atimize wajibu wake, tufanye kazi kwa kuzingatia uadilifu sababu tunabeba dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya viongozi mbali mbali wa serikali” alisema Dkt Mgwatu.

  ,Mtendani huyo ameongeza kuwa atokuwa na msamaha na mtumishi yeyote atakayeshindwa kuwa muadilifu na kutoimiza wajibu wake ipasavyo. Aidha Dkt Mgwatu aliwaagiza watumishi wa kituo hicho kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi zaidi na kuongeza pato la kituo.

  Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Njombe Mhandisi John Rubaga alimueleza kuwa kituo kinakabiliwa na tatizo la madeni kinayodai wateja wake pamoja na madeni kinayodaiwa na wazabuni mbali mbali.

  Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Musaa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo nyanda za juu Kusini ili kubaini changamoto mbali mbali zilizo kwenye vituo hivyo na kuzitafutia ufumbuzi.

  0 0

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye  Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani  mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016. 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha na IKULU


  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Sewahaji ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo tarehe 11 Novemba, 2016 baada ya afya yake kuimarika.

  Kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.

  "Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.

  "Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth Magufuli. 

  Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini hapo tangu Juzi tarehe 09 Novemba, 2016 baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam


  11 Novemba, 2016


  0 0
older | 1 | .... | 1038 | 1039 | (Page 1040) | 1041 | 1042 | .... | 1897 | newer