Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1037 | 1038 | (Page 1039) | 1040 | 1041 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Uharibu wa vyanzo vya maji.
   
  Na Rhoda Ezekiel  Globu ya Jamii-Kigoma,

  MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe,Elisha Bagwenya amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe kushirikiana na watendaji wake kuunda sheria ndogo ndogo zitakazo toa adhabu kwa baadhi ya wananchi wanao haribu vyanzo vya Maji kwa kufanya shughuli za kibinadam katika vyanzo hivyo hali inayo pelekea Halmashauri kukosa maji.

  Rai hiyo aliitoa Jana katika kikao cha Baraza La madiwani wa Halmashauri hiyo Bagwenya alisema kumekuwa na Uhalibifu mkubwa katika vyanzo vya Maji unao sababishwa na wananchi wanaofanya shughuli zao katika vyanzo hivyo na kusababisha uchafuzi wa Maji na kupelekea wananchi kupata magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na kipindu pindu.

  Alisema Mkurugenzi kwa kushirikiana na wataaramu kuunda sheria ndogo ndogo za uhifadhi wa misitu na mazingira ziletwe kwenye kikao zijadiliwe na  zipitidhwe na Halmashauri ilizianze kutumika na kusaidia vyanzo vya Maji kutunzwa na kuisaidia wananchi kupata Maji safi na Salama.

  Hata hivyo Bagwenya alimuomba Muhandisi wa Maji Wilaya kuhakikisha wananweka dawa katika vyanzo vya Maji ilikuhakikisha wananchi na ambapo ya Maji yaliyo safi na Salama na kuweza kuepuka Magonjwa ya mlipuko yaliyo kuwa yakijitokeza kwa kipindi cha nyuma.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kanali Marko Gaguti alisema Serikali ya wilaya imeandaa Mpango wa kupitankatika kila kijiji kutoa maelekezo kuw Wananchi wote kufanya shughuli zao nje ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji ilkuweza kulinda vyanzo hivyo na wananchi waweze kupata Maji ya kutosha.

  Gaguti alisema anaunga mkono wazomlq Halmashauri LA kuunda sheria ndogo ndogo za kutunza vyanzo vya Maji ilikulinda vyanzo vya Maji,alise mpaka sasa kijiji kinamiundombinu chini ya 68% ambapo Wananchi wengi wana kosa Maji upayikanaji wa Maji ni mdogo.

  "Vyanzo vya Maji vinatakiwa kuachwa wananchi hawarusiwi kulima,kupanda miti au kufanya shughuli zozote katika mita sitini kuanzia kwenye vyanzo, Mkurugenzi anatakiwa kuwapa taarifa viongozi wa vijiji kulinda vyanzo hivyo na kuwachukulia hatua wrote watakao Keuka kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo", alisema Gaguti.

  Sambqmba na hayo Gaguti alisema Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa hutuma za Afya Wilaya ni humo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Hospital ya wilaya ya Buhigwe , Halmashauri imeamua kuanza ujenzi wa Hospital I ya wilaya kwa kuchukua lamani ya Hospital ya Monduli na kupitia mapato ya ndani na michango kutoka kwa wadau watajenga hospital I hiyo iliwananchi waweze kupata Huduma Katibu.

  Nae Kaimu muhandisi wa Maji Wilaya ya Buhigwe Muhanfisi Mwafrika Charse alisema Sheria namba 11 ya mwaka 2009 inasema watu hawa ruhusiwi kufanya shughuli zozote za kijamii mita60 kuanzia kwenye chanzo cha Maji ilikuhakikisha vyanzo vinalinda.

  Alisema mikakati iliyopo ni idara ya Maji wilaya humo kuzungukia vijiji vyote vyenye vyanzo,  kutoka Elimu kwa Wananchi iliwaweze kupata Elimu ya kutunza vyanzo hivyo na kupata Maji ya kutosha na safi kwa kuepuka uhalibifu wa vyanzo hivyo.

  0 0

  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akikata utepe kuzindua rasmi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) wakishuhudia tukio hilo.
  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kulia) kwa pamoja wakiwa wameshika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imezindua MPANGO Mkakati wa miaka mitano 2016 – 2020 ambao umeainisha vipaumbele saba kwa kufanyia Utafiti katika masuala mbalimbali ya Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

  Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shabani kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James.

  Mpango Mkakati huo 2016 – 2020 ambao ni wa sita tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo,umeainisha maeneo makuu saba ambayo ndani ya maeneo hayo kuna maeneo mengine madogo madogo ishirini na sita ambayo kwa pamoja yatatiliwa mkazo katika kipindi hicho cha miaka mitano.

  Maeneo hayo makuu ni; Kukuza Uchumi, Ajira na Viwanda; Utawala na Uwajibikaji; Utandawazi na Ushirikiano wa kikanda; Utoaji wa huduma na ulinzi wa kijamii; Mali asili na Usimamizi wa Mazingira; Usimamizi wa Maarifa na Ubunifu pamoja na Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (wa pili kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za ESRF kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF kuzindua Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020. Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili (kushoto) pamoja na Mshehereshaji wa uzinduzi wa mpango mkakati huo, Prof. Samuel Wangwe (wa pili kushoto).(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Bi. Amina alisema kwamba serikali imefurahishwa sana na juhudi kubwa zinazofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)

  kusaidia serikali kusukuma mbele huduma zake kwa jamii na kupanua uwezo wa kutengeneza Taifa linalotekeleza sera za ukuaji wa uchumi.

  Aliwapongeza waandaaji wa Mpango Mkakati huo na kusema Wizara yaFedha na Mipango inafurahishwa sana na namna Taasisi hiyo kama chombo cha Utafiti kinavyosaidia kuonyesha njia na kutoa mwelekeo kwa masuala mbalimbali ya kisera na utekelezaji.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) akiongozana na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

  Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kutokana na Mpango Mkakati huo, serikali imefurahishwa kuona kuwa taasisi hiyo pia imejikita katika kusaidia kuona serikali inafanikisha utekelezaji wa maendeleo endelevu nchini.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida akizungumza kabla ya kumkarisbisha mgeni rasmi Bi. Amina kuzindua Mpango Mkakati huo pamoja na mambo mengine alisema kwamba Taasisi yake imejikita katika kufanya tafiti maeneo saba ambayo yamo katika mpango wa pili wa maendeleo.

  Wadau katika kujadili Mkakati huo wameiomba Serikali kufanikisha Tafiti zote zilizokusudiwa kufanywa zinatekelezwa kwa kuisaidia Taasisi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida akizungumza machache na kutoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Doto M James kwenye uzinduzi wa Mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika hafla ya uzinduzi huo.
  Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Oswald Mashindano akielezea wadau mbalimbali mambo muhimu yaliyomo katika mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 wakipitia mpango mkakati huo uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

  Sehemu ya wadau, wageni waalikwa na wafanyakazi wa ESRF katika hafla hiyo ya uzinduzi.


  Pichani juu na chini ni wageni waalikwa walioshiriki kwenye uzinduzi huo wakitoa maoni juu ya mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

  Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ESRF, Charles Singili akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.
  MC ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya ufundi inayotoa ushauri kwa menejimenti ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF, jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa sita wa miaka mitano wa ESRF 2016-2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaban katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki kwenye uzinduzi wa mpango mkatiti huo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.
   is wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ  Mhe,Shamata Shaame Khamis katika  hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja..
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimuapisha Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Shadia Mohamed Suleiman, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akiwa na Viongozi mbali mbali baada ya kuwaapisha Naibu Mawaziri katika Wizara mbali mbali hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.
   aibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ  Mhe,Shamata Shaame Khamis akiikariri hati ya kiapo kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,(kulia)Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawakena Watoto Mhe,Shadia Mohamed Suleiman
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga,akiikariri hati ya kiapo kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,(kushoto)Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Shadia Mohamed Suleimani
   Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Saidi Hassan Said (kulia) akiwa na Washauri wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Ikulu Mjini Zanzibar.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- uungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba akiongea na Wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya shindano la kutafuta mbadala wa mkaa,   lilioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.  KUHUSU SHINDANO LA KUTAFUTA MBADALA WA MKAA 

  Nchi yetu iko njia panda. Tuna nchi nzuri yenye bioanuai za wanyama na mimea ambazo haziwezi kufananishwa na nchi nyingine yeyote. Takriban asilimia 40 ya eneo lote la nchi limehifadhiwa kwa ajili ya misitu na wanyamapori. Hata hivyo, uharibifu wa misitu unafanyika kwa kasi ya kutisha. Takriban ekari milioni moja za misitu zinateketezwa kwa mwaka. Karibu mabonde na mifumo yote ya mito mikuu hapa nchini inaanzia kwenye misitu ambayo sasa tunaiharibu kwa kasi ya kutisha.

   Kuna mambo kadhaa yanayochangia kasi hii kubwa ya uteketezaji wa misitu hapa nchini, ikiwemo ufyekaji wa maeneo kwa ajili ya kilimo, mifugo, uchomaji wa mkaa na biashara ya kuni. Hakuna shaka kwamba mahitaji ya mkaa na kuni yanazidi uwezo wa misitu yetu ya asili kukukidhi mahitaji hayo. Mahitaji haya yataendelea kuongezeka kwa kasi kwa miaka inayokuja kutokana na ukuaji wa miji na ongezeko la idadi ya watu, kwani inaaminika kwamba ongezeko la asilimia moja ya ukuaji wa miji linasababisha ongezeko la asilimia 14 la matumizi ya mkaa.

  Ikizingatia kwamba, Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa kasi ya ukuaji wa miji, kiasi kwamba ifikapo mwaka 2027 zaidi ya nusu ya Watanzania watakuwa wanaishi mijini, mahitaji na matumizi ya mkaa yatakuwa maradufu kuliko ilivyo sasa. Hivyo, ni muhimu sana hatua za haraka ni muhimu zichukuliewe sasa ili mahitaji haya ya makubwa ya mkaa yasipelekee kuangamizwa kwa misitu yetu. 

  Kuwa na uzalishaji endelevu wa  mkaa, au kuifanya biashara ya mkaa isiwe na tija, au mbadala wa mkaa kuwa na faida zaidi kibiashara, ni jambo la msingi kwa usalama wa nishati kitaifa, kwa kupunguza ukataji misitu na kulinda huduma zitokanazo na mifumo-ikolojia nchini, ikiwemo ulinzi wa vyanzo vya maji, utiririkaji wa maji katika mito na hivyo upatikanaji wa maji nchini.

  Naamini kuwa moja ya njia za kuokoa mazingira yetu, kulinda urithi adhimu uliomo katika Hifadhi zetu, na kurejesha thamani ya maliasili yetu ni kwa kupunguza ukataji wa misitu kwa ajili ya mkaa. Njia bora ya kufanya hivyo ni kwa kupunguza matumizi ya mkaa kupitia  ubunifu wa teknolojia za nishati nafuu na zenye ufanisi zaidi na endelevu; na vyanzo nafuu vya nishati mbadala katika ngazi ya kaya. 

  Lakini leo tunaweza kuanza safari ya kuondokana kabisa na matumizi ya mkaa kupitia ubunifu katika ujasiriamali wa nishati za kupikia - hasa ubunifu kwa upande wa uzalishaji na usambazaji wa nishati mbadala wa mkaa, na katika kuufanya mkaa kupata ushindani mkubwa katika soko la nishati za kupikia au ubunifu katika kufanya uzalishaji na matumizi ya mkaa kuwa endelevu (kutoharibu mazingira). Naamini kwamba inawezekana kabisa kuanzisha na kuendeleza mifumo mipya ya uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa nishati ya kupikia ambayo itapunguza kasi ya ukataji miti na kupunguza athari kwa mazingira nchini.

  Ninazindua kwa mara ya kwanza Shindano la Kitaifa la Kutafuta Mbadala wa Mkaa. Madhumuni ya msingi ya Shindano hili ni kuwatambua, kuwatuza, kuwawezesha na kuwaendeleza wabunifu na wajasiriamali wanaojihusisha na mbinu na jitihada za uzalishaji, usambazaji na matumizi ya nishati endelevu za kupikia. Natoa wito kwa wadau wote: watu binafsi, wabunifu, makampuni binafsi, wajasiriamali, asasi za kiraia na kijamii, taasisi zisizokuwa za Kiserikali, Taasisi za Elimu ya Juu, na Taasisi za Utafiti, kushiriki katika changamoto hii.

  Moja ya madhumuni ya ziada ya shindano hili ni kuwaleta pamoja wadau na wabunifu wanaojishughulisha na harakati za kutafuta na kutumia nishati mbadala wa mkaa. Kama sehemu ya mchakato huu, na hasa baada ya shindano, kutakuwa na warsha, semina, mafunzo ambazo zitawaleta pamoja wadau wote kuendelea kutafakari jitihada za ziada za kupata nishati mbadala wa mkaa. 
  Aidha, mafanikio mengine tunayoyatarajia ni kama  yafuatayo:-
  §  Kuinua uelewa juu ya suala la ukataji miti na umaskini wa nishati kwa mapana zaidi miongoni mwa watu wa kawaida;
  §  Kuvutia na kuhamasisha ujasiriamali na uwekezaji miongoni mwa wananchi katika sekta ya nishati ya kupikia; 
  §  Kuwezesha kuonekana kwa mawazo na fikra mpya za watu wengi wanaojishughulisha na kupunguza matumizi ya mkaa;
  §  Kuweza kubaini makundi yanayojihusisha na ubunifu/ufumbuzi wa nishati endelevu ya kupikia na iwapo yanaweza kuunganishwa, kuwezeshwa au kuwekwa pamoja mnyororo wa thamani ya uzalishaji, usambazaji, uuzaji wa rejareja / jumla wa nishati ya kupikia.

  Mshindi wa kwanza atapokea tuzo ya fedha ya shilingi Milioni Mia Tatu (300,000,000), mshindi wa pili atapokea Shilingi Milioni Mia Mbili (200,000,000) na mshindi wa tatu atapokea Shilingi Milioni Mia Moja (100,000,000). Zawadi hizo za fedha zitatumika tu kwa ajili ya kukuza na kuendeleza mtaji wa miradi/ufumbuzi iliyoshinda. Vilevile, washindi hawa watatu wa kwanza watapatiwa mafunzo ya biashara na uwekezaji kulingana na uvumbuzi wao na watatambulishwa kwa wawekezaji na/au kupelekwa zilipo fursa zaidi za uwekezaji au ubia, ndani na nje ya nchi, kwa ajili ya kupanua  na kuupeleka sokoni ubunifu wao. Mategemeo ni kwamba njia moja au njia zote zilizoshinda zitakuwa zimetoa ufumbuzi wa nishati mbadala ya kupikia nchini.

  Tuzo zitatolewa kupitia mchakato wa wazi kwa tathmini mahiri ya jopo la wadau wa nishati, mazingira na wataalamu wa biashara kwa kipindi cha miezi sita. 
  Kuhusu ubunifu unaohusisha matumizi endelevu ya mkaa, masuala yafuatayo yanaweza kuangaliwa, katika kuamua mshindi:
  §  Usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na upandaji miti;
  §  Teknolojia bora za uzalishaji wa mkaa;
  §  Vyanzo mbadala vya mkaa kama vile briketi,  au mkaa wa taka, nk.
  §  Ubunifu katika mnyororo wa thamani ya mkaa, na
  §  Utengenezaji na usambazaji wa majiko banifu na biashara ya mkaa.
  Ubunifu/ufumbuzi utakaopokelewa kwa ajili ya kushindanishwa ni ule ambao tayari unatekelezwa au ambao upo kwenye majaribio kwa muda usiopungua miezi sita kuanzia tarehe ya kuwasilisha maombi ya kuingia kwenye shindano. Andiko/pendekezo, wazo au dhana ambayo bado iko kwenye makaratasi (paper proposal) haitafikiriwa kuingizwa kwenye shindano.
  Wakati wa mchakato wa tathmini, jopo la thathmini linaweza kutembelea maeneo ubunifu unapotumika, kuomba vifaa vinavyotumika, kuhitaji kufanyika majaribio mara kadhaa, na kuhitaji maelezo mengine yoyote ya ziada kwa ajili ya kufanya tathmini kamili na sahihi na ya haki. 
  Jinsi ya kushiriki: Waombaji watatakiwa kujaza fomu zitakazopatikana katika Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyopo Mtaa wa Luthuli, jijini Dar es Salaam, au kupakuliwa kutoka tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (www.vpo.go.tz) kuanzia tarehe 15 Disemba 2016. Vilevile, watatakiwa kuwasilisha andiko la ubunifu/ufumbuzi wao lenye kujibu maswali yafuatayo:-

   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu unaweza kupanuliwa (scalability) na kutekelezwa, kuzalishwa na kuigwa katika maeneo mengi nchini? 
   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu utaweza kuwa  endelevu na kutekelezwa kwa muda mrefu bila ukomo (sustainability)?
   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu utaweza kutekelezwa/kupatikana nchi nzima, hasa kwa watu wa kipato cha chini?
   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu utatoa unafuu wa gharama ya nishati ya kupikia kuliko mkaa? 
   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu ni kwa namna gani unaweza kuwa biashara yenye faida (commercially viable) kwa mbunifu na mwekezaji?
   • Je, ubunifu/ufumbuzi huu utaweza kuwa na faida gani na kwa kiasi gani kwa mazingira na kijamii?
   Imani yangu ni kwamba shindano hili litaendana na hatua nyingine za kisera za kudhibiti ukataji wa misitu, kulinda vyanzo vya maji, kuondoa umaskini wa nishati, na kuifanya bei ya mkaa itokane na thamani halisi ya miti iliyotumika kutengeneza mkaa huo.
   Uchukuaji na urudishaji fomu za kushirikiki kwenye shindano, pamoja na mawasilisho ya maandiko, yatapokelewa kuanzia tarehe 15 Desemba 2016 hadi tarehe 31 Januari 2017. Tuzo kwa washindi zitatolewa mwezi Juni 2017. Mawasilisho yanaweza kuwa kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili na hakutatozwa ada kwa ajili ya fomu na mawasilisho.
   Maelezo ya ziada ya shindano hili nitayatoa tarehe 29 Novemba 2016, katika kikao cha wadau wa mkaa nilichokiitisha siku hiyo. Katika kikao hicho pia nitatangaza Mshirika wa Sekta Binafsi katika shindano hili. 
   Kwa ufanunuzi wa ziada, unaweza kuwasiliana nami kupitia:

   Facebook: Ofisi ya Makamu wa Rais
   Instagram: VPOTanzania
   Twitter: VPOTanzania
   Simu: 0685 333 444

   January Makamba (MB.)
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira
   10 Novemba 2016

   0 0

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

   Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesitisha kuweka dhahabu kama hazina ya rasilimali za kigeni kwa sababu ya kuyumba kwa bei ya madini hayo katika soko la dunia na kusababisha uwezekano wa kupunguza thamani ya hazina ya rasilimali ya nchi.

   Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Kafumu aliyehitaji kufahamu sababu za Serikali kukataa kutunza dhahabu safi katika Benki Kuu wakati Tanzania ni nchi mojawapo inayozalisha dhahabu safi.

   Mhe. Kijaji amesema kuwa jukumu la msingi la Benki Kuu ni kuandaa na kutekeleza Sera ya Fedha inayolenga kuwa na utulivu wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa hivyo ili kufanikisha azma hiyo Benki Kuu inadhibiti ongezeko la ujazi wa fedha kwa kutumia nyenzo mbalimbali zikiwemo za kuuza dhamana na hati fungani za Serikali pamoja na kushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni kati ya mabenki.

   “Katika kutekeleza jukumu lake la msingi, Benki Kuu hutunza hazina ya rasilimali za kigeni zinazotosha kuagiza bidhaa nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne lakini kwa muda mrefu sasa Benki Kuu ya Tanzania haiweki dhahabu kama sehemu ya rasilimali hizo kutokana na kuyumba kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia”, alisema Mhe. Kijaji.

   Naibu Waziri huyo ametoa mfano wa kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia ambapo dhahabu ilishuka kutoka dola 1,745 za kimarekani katika mwezi Septemba 2012 hadi dola za kimarekani 1,068 kufikia mwezi Desemba 2015.

   Mhe. Kijaji amefafanua kuwa hazina ya rasilimali za kigeni zinaweza kuwa dhahabu – fedha (monetary gold) au fedha za kigeni ambapo uamuzi kuhusu hazina itunzwe vipi unazingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vile vya kudumisha thamani, wepesi wa kubadilisha pamoja na faida inayopatikana kwa kuwekeza hazina hiyo.

   Aidha, Mhe. Kijazi amesema kuwa ununuzi na uuzaji wa madini ya dhahabu unahitaji ujuzi maalum ambapo kwa kuzingatia jukumu la msingi la Benki Kuu inaonyesha dhahiri kuwa Benki hiyo haijajijengea uwezo katika eneo la biashara ya madini hayo.

   0 0

   Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid, akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.

   Na BMG


   Maulid amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.

   Pamoja na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha.
   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na hakimili za wasanii wa filamu nchini.
   Wasanii wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, wakati wa warsha kwa wasanii hao hii leo.
   Afisa Uendeshaji na Maso kokutoka Mfuko wa Pensheni PPF akielezea umuhimu wa wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na mafao kutokana na kazi zao za sanaa. 

   PPF ni miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha warsha ya mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
   Kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid pamoja na afisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF.
   Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (katikati) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa bodi hiyo pamoja na wasanii wa Filamu mkoani Mwanza.
   Zaidi ya wasanii 300 wa Filamu mkoani Mwanza wakifuatilia warsha ya mafunzo ya filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
   Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amesema mkoani Mwanza kuna fursa nyingi kwenye soko la filamu ikiwemo mandhari nzuri hiyo wasanii wa filamu mkoani Mwanza watumie fursa hiyo kuboresha soko lao la filamu.
   Mjumbe wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu, amesema mafunzo hayo yatawasaidia wasanii wa Filamu mkoani Mwanza katika kuboresha filamu zao na hivyo kuinua soko la Filamu mkoani Mwanza badala ya kutegemea soko hilo Jijini Dar es salam pekee.
   Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
   Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (katikati), kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba.
   Mmoja wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo
   Viongozi mbalimbali, akiwemo Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (wa kwanza kushoto), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (wa pili kushoto) pamoja na Innocent Mungy kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA (wa kwanza kulia).
   Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
   Picha ya pamoja

   0 0   0 0


   wadau mbalimbali wakiwa katika banda la data Vision International . Picha zote na Emmanuele Massaka wa Globu ya Jamii
   Meneja mahusiano wa Data Vision International,Teddy Qirtu ,akizungumza na waandishi wa habari katiika maonesho hayo.

   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

   WITO umetolewa kwa makundi ya Vicoba ,Saccos na Tasisi za kifedha kujiunga katika mfumo wa Smart kadi unaondeshwa na tasisi y Data Vision International hili kuepuka madhara yatakayotokea wakati wa kutembea na fedha nyingi kwa wakati mmoja.

   Wito huo umetolewa na Meneja mahusinao wa kampuni hiyo ,Teddy Qirtu alipokuwa akiongea na waandish wa habari wakati wa mkutano na maonyesho ya tasisi za kifedha katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

   “Data vision International ni moa makampuni yanayotuia mfumo wa kisasa wa kuhifadhi fedha katika smart kadi ambayo utaweza kufanya manunuzi sehemu yoyote hilena kutoa pesa popote pale walipo mabenki washirika kwa kutumia kadi ya Pap, kdi mbayo ina uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja”amesema Qirtu. Amemaliza kwa kusema kuwa ufike wakati wa vikundi vya watu kuanzia 30 kujiingiza katika mfumo huu ambao utasidia mambo mengi katika Maisha yao ya kila siku

   0 0


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea mjane wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta, Mama Margaret Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Jeneza lenye mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta likiwa limebebwa na askari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaongoza viongozi mbali mbali wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa UWT Mhe. Amina Makilagi (kushoto) wakimfariji akimfariji Mama Margaret Sitta (katikati) wakati wa mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mwandamizi Mstafu Marehemu Samuel Sitta kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   ...............................................


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi na wananchi katika mapokezi ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ukitokea nchini Ujerumani alipofariki wakati anapatiwa matibabu.

   Akizungumzia jinsi anavyomfahamu Samuel Sitta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa limeondokewa kiongozi mwadilifu,mzalendo, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge hivyo taifa litaendelea kuumuenzi utendaji wake.

   Viongozi mbalimbali waliojumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mapokezi ya mwili wa Spika Mstaafu Samweli Sitta kweye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere ni pamoja na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Seif Ali Iddi, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

   Baada ya Mwili wa Spika Mstaafu Samuel Sitta kuwasili nchini leo mchana amepelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam ambapo hapo kesho asubuhi viongozi na wananchi watatoa heshima zao ya mwisho za kuuaga mwili wa marehemu katika viwanja wa Karimjee jijini

   0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Nchini Norway Bw.Eivind  Hansen,Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Haukeland akiwa na ujumbe aliofutana nao walipofika Ikulu Mjini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Dk.Hallvard Reigstad, Mkuu wa Idara ya Watoto kutoka Hospitali ya Haukeland Nchini Norway akiwa ni miongoni mwa Ujumbe kutoka Nchini Norway uliofika Ikulu Mjini Unguja leo ,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe kutoka Nchini Norway ukiongozwa na Bw.Eivind Hansen, Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Haukeland (wa pili kulia) walipofika Ikulu Mjini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Nchini Norway Bw.Eivind Hansen,Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Chuo Kikuu cha Haukeland akiwa na ujumbe aliofutana nao walipofika Ikulu Mjini Unguja leo

   0 0

    Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016
    Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
    : Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
     Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi alipokuwa akitoka  Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu.leo Novemba 10, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo leo Novemba 10, 2016.Picha na IKULU


   0 0


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 10, 2016

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Novemba, 2016 amewaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa Waziri na mbunge Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Joseph James Mungai katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.


   Pamoja na Rais Magufuli Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali na Siasa.


   Mhe. Joseph James Mungai alifariki dunia tarehe 08 Novemba, 2016 katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua ghafla na mwili wake utasafirishwa kesho Ijumaa kwenda Mafinga Mkoani Iringa kwa Mazishi.


   Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewatembelea na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam wakiwemo Waziri na Balozi Mstaafu wa Tanzania Mhe. Omar Ramadhan Mapuri na Mkewe Mama Janeth Magufuli.


   Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo wamemshukuru Rais Magufuli kwa hatua zilizochukuliwa na Serikali kuboresha hospitali ya Taifa Muhimbili na wamebainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali pia wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi.


   Mapema leo asubuhi, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na mfadhili wa Taasisi ya Gatsby Tanzania Lord Sir David Sansburg na kumuhakikishia kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za kuendeleza kilimo, wajasiriamali na viwanda ambazo zinafanywa na Taasisi hiyo.


   Dkt. Magufuli amesema atafurahi kuona Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikiwasaidia wakulima wa pamba na chai kupata mbegu bora na kusindika mazao yao, inapiga hatua zaidi kwa kuanzisha viwanda vya nguo na kwamba Serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi hizo.


   Gerson Msigwa

   Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

   Dar es Salaam

   10 Novemba, 2016


   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole mjane wa Marehemu Mzee Joseph Mungai.
   Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mungai, aliewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne, ulioagwa leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Joseph Mungai, aliewahi kuwa Waziri katika Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne, ulioagwa leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa nne kushoto), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa (wa tatu kushoto), Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kulia), Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto), Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete (kulia) pamoja na viongozi wengine wakifatilia wasifu wa Marehemu Mzee Mungai, uliokuwa ukisomwa na Mtoto wake Mkubwa, Jimmy Mungai.
    Sehemu ya familia ya aliyekuwa Waziri wa Zamani na Mbunge Mzee Joseph Mungai katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemy katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam  leo Novemba 10, 2016


   0 0
  1. 11/10/16--23:07: AJALI YA LORI
  2. Gari aina ya  SCANIA likiwa limeacha njia na kuingia kwenye mtaro maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam.Hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha

   0 0


   0 0


   0 0

   Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

   Mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samuel Sitta unatarajiwa kuagwa leo mchana na wabunge wa Bunge hilo katika viwanja vya Bunge vya mjini Dodoma.

   Kauli hiyo imetolewa mjini hapo na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai alipokuwa akitoa ratiba ya kuuaga mwili wa spika mstaafu itakayoanza mara baada ya kumalizika kwa shughuli za Bunge za kipindi cha asubuhi.

   Mhe. Ndugai amesema kuwa Bunge linatarajia kuupokea mwili wa mpendwa huyo leo mnamo majira ya saa 8 mchana kutoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupelekwa moja kwa moja ndani ya Bunge hilo kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho na wabunge.

   “Baada ya mwili wa mpendwa wetu kuwasili katika viwanja hivi, tutakuwa na kikao maalum cha Bunge kitakachofanyika mida ya saa 8:30 mchana ambapo wabunge watapata nafasi ya kutoa salamu za rambirambi na baadaye utaratibu wa kutoa heshima za mwisho utafuata”, alisema Mhe. Ndugai.

   Spika Ndugai ameongeza kuwa baada ya utoaji wa heshima za mwisho utakaoongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe, kwa mwili wa marehemu Samuel Sitta utasafirishwa kwa ndege mnamo majira ya saa 10 jioni kwenda wilaya ya Urambo, mkoani Tabora kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Novemba 12 mwaka huu.

   Aidha, Mhe. Ndugai amefafanua kuwa katika msiba huo Bunge litawakilishwa na wabunge 10 watakaochaguliwa na Tume ya Huduma za Bunge kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama ukiongozwa na yeye Spika Mhe. Ndugai kwenda mkoani Tabora kwa ajili ya mazishi.

   Kutokana na msiba huo, Mhe. Ndugai amesema kuwa Bunge litajenga misingi ya kuwaheshimu viongozi wa kitaifa wanaopatwa na jambo la namna hiyo kwa kupewa heshima hizo za kuletwa Bungeni kwa ajili ya kuagwa kwa msingi wa Bunge kuwa ndio nyumba ya uwakilishi wa Watanzania wote.

   0 0   Wapancras ni kundi la Muziki kutoka Kanda ya Ziwa linaloundwa na wasanii Mecrass na Payus. Ni kundi linalofanya vizuri na nyimbo kadhaa ikiwemo Chausiku pamoja na Nitunzie Siri ambayo wamefanya na msanii Abuu Mkali.

   Wamezungumza na BMG Habari na kuelezea furaha yao kwa hatua kubwa waliyofikia kwenye muziki na kuwapongeza mashabiki zao.
   TAZAMA VIDEO HAPO CHINI

   0 0
  3. 11/10/16--23:42: TANZIA

  4. 0 0


   Hospitali ya kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa hususani wale wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
   Kitengo hicho kipya (OPD 3) kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala na kitengo cha magonjwa ya viungo ( Physiotherapy Unit).
    
    kina sehemu kubwa ya mapokezi, vyumba mbalimbali vikiwemo vyumba 10 via madaktari, maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk .
   Kitengo hicho kipya kitaiwezesha hospital hiyo kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwa wagonjwa wasiopungua 120000 kwa mwaka hivyo kupunguza Kero ya foleni na msongamano iliokuwepo siku za nyuma.
   Aidha kitengo hicho (OPD3) kitazinduliwa rasmi hivi karibuni pamoja na vitengo vipya vya kusafishia figo ( Dialysis Unit) na kile cha huduma za dharula ( Emergency Unit)
   Pichani ni Majengo mapya ya kisasa yatakayokuwa yakitumika kutoa huduma.
   Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa.
   Pichani wagonjwa wakisubiri kupata huduma Muda mfupi Mara baada ya majengo hayo kufunguliwa. Na Afisa Mahusiano;Arafa Mohamed

   0 0


   Wanafunzi wa CBE, Adam Luhalala (kushoto) na Petro Nchimbi wakifanya ukaguzi wa Mashine ya kutengeneza vipuri mbalimbali vinavyotumika kwenye mashine za viwandani na Magari ndani ya Karakana ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.
   ahitimu wa chuo CBE mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano la 3 la chuo hicho jijini Dar es salaam.
   Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 katika fani ya Vipimo Mathew Kaizilege akitoa ufafanuzi kuhusu mashine ya kuchonga vipuri kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Jangwani walioitembelea Karakana ya Vipimo ya CBE jijini Dar es salaam.


   Mwanafunzi wa mwaka wa Pili katika Fani ya Utawala katika Biashara Vaileth Monyo akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali kuhusu fani hiyo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Emanuel Mjema walipotembelea mabanda ya maonesho ya wanafunzi hao.

   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda (kushoto) akizungumza na Viongozi na watendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) mara baada ya kuwasili chuoni hapo kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la 3 lililowakutanisha wahitimu wa chuo hicho mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam.
    
    Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu kote nchini wametakiwa kutumia muda mwingi kujisomea na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu , migomo na maandamano yasiyo na tija kwa taifa ambayo yamekuwa yakiwapunguzia ufanisi katika masomo yao.

   Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda wakati akizungumza na Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwenye kongamano la 3 lililowakutanisha wahitimu wa chuo hicho mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam.

   Akiwa mgeni rasmi katika kongamano hilo na mmoja wa wahitimu wa siku nyingi wa chuo hicho Kamanda Suzan Kaganda amesema wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu wanapaswa kutambua kuwa elimu wanayoipata katika vyuo hivyo sio kwa ajili ya manufaa yao binafsi bali ni kwa manufaa ya taifa zima hivyo wanatakiwa kuwa makini na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

   “Naomba nisisitize kuwa elimu mliyoipata na mnayoendelea kuipata chuoni hapa sio kwa ajili ya manufaa yenu binafsi bali ni kwa ajili ya manufaa ya taifa, wakati mwingine mnapoteza muda mwingi pindi mnapojiingiza kwenye migomo na maandamano barabarani kushindana na Serikali, muda ambao mgeutumia kujisomea ninyi wenyewe” Amesisitiza Kamanda Suzan.

   Amewataka wahitimu na wanafunzi wa chuo hicho kutumia elimu na ujuzi walioupata kusaidia katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ya awamu ya tano kwa kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa za ajira zilizopo kujiajiri na kuajiri wengine.

   “Taifa letu linazo fursa nyingi, kinachotakiwa ni wazawa kuazisha makampuni yatakayoweza kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo zitauzwa duniani na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu” Amesisitiza.

   Aidha, amekipongeza chuo cha CBE kwa kupiga hatua na kupata mafanikio makubwa katika utoaji wa elimu tangu kuanzishwa kwake miaka 51 iliyopita kwa kuwa maendeleo makubwa kwa taifa lolote hayawezi kupatikana bila kuwaelimisha wake katika biashara na Ujasiriamali elimu inayotafsiri uchumi wa viwanda pia.

   “Nachukua fursa hii kuupongeza uongozi wa CBE kwa kuongeza matawi ya chuo katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Mbeya pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka pamoja na fani katika ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada, Shahada za Uzamili na Uzamivu” Amesema Suzan Kaganda.

   Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CBE, Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa kongamano hilo amesema kuwa chuo anachokiongoza kimeendedelea kupata sifa ya kuwa chuo bora ndani na nje ya nchi kwa kuwa kimewatoa viongozi mahiri ambao waliotoa mchango katika maendeleo ya taifa.

   Ameeleza kuwa CBE kilianzishwa mwaka 1965 kikiwa na wanafunzi 20 tu ili hali sasa kina wanafunzi zaidi ya 11,000 huku fani za elimu zikiongezeka kutoka ngazi ya cheti hadi shahada za Uzamili na masomo ya Uzamivu ambayo yanatolewa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mashariki cha Finland.

   “ Chuo chetu kimepiga hatua kubwa kimaendeleo toka kilipoanzishwa mwaka 1965, kimepata mabadiliko makubwa tumekuwa kitaaluma, kimachapisho na pia kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo fursa za biashara wakati huu ambao Serikali inahamia mkoani Dodoma” Amesisitiza.

   Ameongeza kuwa chuo hicho kitaendelea kusimamia weledi katika utoaji wa elimu hapa nchini ili kiendelee kutoa vijana wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu mbalimbali kulingana na fani walizosomea.

   “Chuo chetu tunasisitiza ubora wa elimu, tunafanya mchujo kwa kila mwaka ili kudhibiti ubora wa elimu yetu wale wasiofikia viwango kwa kila mwaka tunawaacha warudishwe nyuma sio kila anayeingia hapa lazima ahitimu masomo yake wale wasiokidhi viwango na kuendana na kasi ya masomo chuoni hapa wanajiondoa wenyewe” Amesisitiza Prof. Mjema.

   Katika hatua nyingine Prof. Mjema amebainisha kuwa Novemba 12 Chuo hicho kitaadhimisha mahafali ya 51 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965.

  older | 1 | .... | 1037 | 1038 | (Page 1039) | 1040 | 1041 | .... | 1897 | newer