Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1036 | 1037 | (Page 1038) | 1039 | 1040 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah Cooke akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu Elimu Kata ya Msalato Ally Swalehe juu ya mfumo wa taarifa shuleni, ambapo mpango umetoa tablet kwa walimu wakuu na waratibu elimu kata. Kushoto kwake ni afisa elimu Mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo.

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msalato wakiimba wimbo wa kumkaribisha Balozi wa Uingereza Nchini alipotembelea shule hiyo. 

  Wanakijiji wa Chihanga ambao walihamasika na programu ya kuinua ubora wa elimu Nchini na kuanzisha kituo cha utayari kwa watoto wao ambao walikuwa wanashindwa kwenda kwenye shule mama kutokana na umbali, wakicheza ngoma ya kigogo kumkaribisha Balozi.
  Balozi Sarah Cooke akiwa na watoto wa kituo cha utayari cha Chihanga ambapo kabla ya hapo watoto hao walikuwa nyumbani , uwepo wa kituo hicho umewawezesha watoto kufurahia michezo mbali mbali kama vile kuimba na kujifunza maneno ya Kiswahili ili wawe tayari kwa kuanza darasa la kwanza. Kituo kilianzishwa mwaka jana na hii ni awamu ya pili ambayo ina jumla ya watoto 64 

  Balozi akifurahia jambo na Afisa Elimu wa mkoa wa Dodoma, Maria Lyimo

  Baadhi ya zana za kujifunzia watoto katika kituo cha utayari Chihanga

  Balozi akikaribishwa katika kituoa cha utayari Chihanga

  Watoto wa kituo cha utayari wakiwa wamejiandaa kumuimbia balozi baadhi ya nyimbo wanazojifunza kituoni.

  0 0

  TUME ya Jumuiya ya Madola inayosimamia Makaburi ya Vita vya Kwanza vya Dunia (CWGC) inatarajiwa kuzindua hapa makaburi mapya ya askari wa Kihindi waliokufa katika vita hivyo vya kwanza vya dunia. 

  Akizungumza na waandishi habari jijini Tanga jana , Ofisa ufundi wa Jumuiya hiyo, Daniel Achini, alisema uzinduzi huo utafanyika mwezi Novemba 11, 2016.Achini alisema uzinduzi huo utafanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo ya CWGC, Victoria Wallace ukishuhudiwa na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cook na Balozi wa India, Sandeep Arya. 

  Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Balozi wa Ujerumani, Egon Konchake na viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Tanga.Alisema makaburi hayo mapya yapatayo 62 yamezikwa miili ya askari wa Kihindi waliokufa vitani katika eneo la Jasin kati ya Januari na Julai, 1915.Makaburi hayo yamejengwa maeneo ya Usagara na Jasin, karibu na jiji.

  Kumbukumbu ya makaburi ya Wahindi na yale ya Usagara yaliyoko hapa Tanga ni sehemu tu ya makaburi mengi yanayohudumiwa na Tume hiyo ya CWGC.Ofisa huyo alieleza kuwa makumbusho ya Jasin, ulikuwa ni mji wa mbele wa kujihami katika pwani ya kaskazini ya mji wa Tanga na ambao ulichukuliwa na Wajerumani mwezi Januari, 1915. 

  Alisema vikosi vya Jind na Kashmiri ndivyo vilivyoulinda mji, ambao ulitekwa na kuchukuliwa tena na vikosi vya wanajeshi 2,000 wa Kijerumani tarehe 18 Januari, 1915. Makumbusho ya makaburi ya Tanga ambayo yapo katika eneo la Usagara, yanahifadhi kumbukumbu ya vifo 394 vilivyotokea katika vita vikali vilivyopiganwa katika mji wa Tanga kati 1914 na 1916 baina ya mataifa makubwa ya Uingereza na Ujerumani. 

  Achini alifafanua kwamba moja ya kazi muhimu ya Tume hiyo barani Afrika ni pamoja na kutunza makaburi na kumbukumbu za vifo zaidi 190,000 vilivyotokea katika vita vya kwanza na pili vya dunia katika nchi zaidi ya 40 zilizopo Afrika.

  "Nchini Tanzania, tunavikumbuka vifo zaidi ya 55,000 vilivyotokea katika vita vyote katika viwanja 12 vya makaburi", alidokeza Achini.Alitaja baadhi ya maeneo ya makaburi yanayohudumiwa na CWGC yanapatikana Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa na Moshi Zanzibar.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
  Wakazi wa Usagara Tanga, Joseph Kimani, Martin Kiarie na Ali Hamis wakiangalia majina ya askari wa Uingereza na India waliouwawa Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914, jumla ya askari 270 waliuwawa na majina yao kuwekwa na tume ya Jumuiya ya Madola (CWGC).
  Mkazi Usagara Tanga, Joseph Kimani, akiangalia majina
  ya askari wa Uingereza na India waliouwawa wakati wa vita ya
  kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 270 waliuwawa Tanga wakati wa vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1914.Majina hayo yamehifadhiwa na tume ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth War Graves Cammission) (CWGC)

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh Asumta Mshama, akishuhudia uzinduzi wa moja ya madarasa ya kituo cha watoto yatima cha KCVC uliofanywa na mlezi kituo hicho mama Anna Mkapa na mwenyekitiwabodiya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku hafla iliyofanyika kijiji cha Simbani wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani 
  Watoto wanaolelewa katika kituo cha KCVC wakiimba wimbo maalumu.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akiongea na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha KCVC.
  Mlezi kituo hicho mama Anna Mkapa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa 
  Mkuu wa wilaya ya Kibaha mh Asumta Mshama akiongea na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha KCVC. 
  Viongoziwa Bayport wakiongeana Mama Anna Mkapa. 
  Viongozi wa Bayport Tanzania wakiwa katika picha ya pamojana Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mh Asumpta Mshama, Mama Anna Mkapa, mtoto Esther Furaha pamoja na wasimamizi wa kituo cha Kibaha Children’s village centre.

  0 0


  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndg. Jesca Msambatavangu kufuatia kifo cha Mhe Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi kilichotokea jana tarehe 08 Novemba, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Mhe. Mungai, ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.

  Mhe. Mungai, atakumbukwa na wanaCCM, na wananchi wa Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuasisi na kuendeleza shamba kubwa la miti la SAOHILL na kwamba mchango wake huo tutaendelea kuuenzi na kuuthamini.


  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. 
  Imetolewa na:- 

  Christopher Ole Sendeka (MNEC)
  MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

  0 0

  Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) umeitaka serikali ya Tanzania kuimarisha ushirikiano uliopo baina yake ili kuwekeza dola za Marekani bilioni 1.2 (2.6tr/-) katika sekta ya nishati utakaoongeza megawati 1,200 katika gridi ya taifa. 
   
  Tanzania ni mmoja wa wajumbe waliasisi ATI wakala ambao ulianzishwa ili kutoa bima kwa wawekezaji pamoja na kufanya shughuli nyingine za kibiashara miongoni mwa nchi za Afrika ambazo ni wanachama. Chini ya ubia ambao ulisainiwa na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa mwaka 2001, Tanzania na nchi nyingine zilikubaliana kutoa upendeleo wa kupata mkopo katika miradi yote inayoungwea mkono na ATI. 
   
  Ahadi hiyo ambayo inatoa uhakika kwa nchi mwanachama ambao utaiepusha na madai yoyote katika miradi inayoungwa mkono na ATI, kuwapatia wawekezaji, wagavi na na nafasi nyingine muhimu katika kuzindua miradi Tanzania. 
   
  “Lengo letu ni kuisaidia Tanzania kwa kuuleta nchini uwekezaji unaohitajika sana na kupunguza gharama za kukopa. Sisi ni watu wakimya lakini ni sehemu muhimu sana ya fumbo kwa sababu tumesimama nyuma ya uwekezaji na biashara ambayo inakadiriwa kufikia dola bilioni (2tr/-) nchini Tanzania tangu kuanza kwa biashara mwaka 2004”, alibainisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATI George Otieno. Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Bima ya Biashara Afrika (ATI) George Otieno akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es salaam. Tusekile Kibonde ambaye ni Underwriter Responsible for Tanzania Kutoka ATI akieleza maswala mbalimbali mbele ya wanahabari juu ya Mkutano huo ambao unafanyika Jijini Dar es salaam ambapo Jukwaa hilo linawakutanisha pamoja wadau kutoka Nyanja binafasi za umma katika kutafuta masuluhisho ambayo yataondoa hatari zinazoikabili sekta ya nishati ili kuvutia uwekezaji unaohitajika sana.
  Kamishna msaidizi wa Umeme wa wizara, mhandisi Innocent Luoga akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum uliofanyika Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwaeleza wanatazania juu ya kinachojadiliwa katika mkutano wa jukwaa la kimataifa la sekta ya nishati ambalo likiwa na kauli “Kufungua uwekezaji kutawezesha ongezeko kubwa la Nishati Tanzania” ambalo limeitishwa na ATI mkutano ambao unafanyika Jijini Dar es Salaam.
  Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja. Tanzania inaweza kunufaika zaidi kutokana na ubia wake na ATI kirahisi kwa kurudia utekelezaji wa ahadi zake kwa kusaidia miradi inayoungwa mkono na ATI ndani ya Tanzania. Chini ya masharti ya ubia, Tanzania inaweza kuwepo kiwango mbadala wa vipimo vya viwango kwa kipimo cha uwekezaji cha ATI daraja A mara tutakaposaini manunuzi yanayoungwa mkono na ATI.
   
  Chini ya kanuni za Basel, ambazo zinasimamia mabenki mengi ya kimataifa, ynaweza kuikopesha nchi kama Tanzania ikiwa inaungwa mkono katika bima na taasisi kama ATI, ambayo ni taasisi inayoheshimika na inayoaminiwa na masoko ya kimataifa ya fedha. Bima ya ATI inaiwezesha benki kupunguza kiwango cha mwisho cha malipo ya bima, ambacho kwa kiwango kikubwa kinapunguza gharama za kukopa kwa Tanznaia na nchi nyingine za Afrika ambazo ni wanachama. 
   
  Kushindwa kutumia kikamilifu fursa hii, Tanzania inaweza kukosa uwekeza wenye thamani ya mamilioni ya fedha. “ATI inaweza kuisaidia nchi kuwa inavutia kuwekeza kifedha kwa kuvutia uwekezaji zaidi. Hili ni muhimu hususani katika sekta ya nishati ambayo kwa hivi sasa ina ushindani mkubwa,” alisema Mdhamini Mkazi wa ATI nchini Tanzania Tusekile Kibonde.

  0 0

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa AzikiweKaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es SalaamKaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.

    KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL. Kampeni hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W. Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi wa TTCL waliosambaa katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam. "Huu utakuwa ni utamaduni wetu, tutawafuata Wateja popote walipo, tutawapa taarifa za huduma zetu bora na nafuu, tutawasikiliza na kufanyia kazi maoni yao. 

  Tunataka kuwahakikishia Wananchi kuwa, hii ni TTCL Mpya, Shirika lao la kizalendo limerejea katika nafasi ya mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini Tanzania. Watumie huduma zetu, waone tofauti, wapate ubora na viwango vya juu kabisa", amesema Bw Kindamba. Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL Bw Peter Ngota amesema, TTCL inawaletea wateja wake Ofa MPYA kabambe kwa ajili ya Simu ya Mezani inayotoa uhakika wa mawasiliano kati ya Wanafamilia. Kwa Mteja atakayeongeza salio la shilingi 23,000/- atapata ofa ya Simu Bure pamoja na ofa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure.  Afisa Mkuu Masoko na Mauzo wa TTCL, Bw Peter Ngota akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Afisa Mkuu Masoko na Mauzo wa TTCL, Bw Peter Ngota akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan MwinyiKaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es SalaamKaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba akigawa vipeperushi kwa mmoja wa wananchi vinavyoelezea ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba akigawa vipeperushi kwa mmoja wa wananchi vinavyoelezea ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Josephine Nsunaluga, akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Kijitonyama, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Josephine Nsunaluga, akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Kijitonyama, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Blandina Mnyaga akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Moroco, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Blandina Mnyaga akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Moroco, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.Meneja Msaidizi (Support) TTCL Dar es salaam - Kaskazini Bw Michael Nchimbi akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Morocco, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Meneja Msaidizi (Support) TTCL Dar es salaam - Kaskazini Bw Michael Nchimbi akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Morocco, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.Afisa wa TTCL, Bw Aloyce Julius akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Afisa wa TTCL, Bw Aloyce Julius akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (katikati) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri W. Kindamba (katikati) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam.Hapa baadhi ya wafanyakazi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Kindamba na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wakionesha alama ya T mara baada ya kampeni yao. Hapa baadhi ya wafanyakazi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Kindamba na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo wakionesha alama ya T mara baada ya kampeni yao.

  0 0

  MAOFISA wawili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na rushwa ya Sh milioni 25 kwa ajili ya kupanga matokeo.

  Washtakiwa hao Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha (picha ya juu) na Msaidizi wa Rais wa shirikisho hilo, Juma Matandika (picha ya chini), walifikishwa mahakamani hapo jana.

  Walisomewa mashtaka yao na Wakili kutoka Taasaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai pamoja na Wakili wa Serikali Odesa Horombe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

  Wakili Horombe alidai kuwa Februari 4, mwaka huu katika ofisi za Makao Makuu ya TFF, washtakiwa hao waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Salum Kalunge na Ofisa wa Shirikisho la Soka mkoani Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Geita, Constantine Morandi.

  Inadaiwa waliomba fedha hizo kwa ajili ya kuishinikiza na kuishawishi TFF na Idara ya Uhamiaji kupanga uamuzi wa matokeowa mechi ya Klabu ya Mpira wa Miguu ya Tabora ili kuisaidia klabu ya Geita Gold  iweze kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu ya Soka Tanzania, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mwajiri wao.

  Washtakiwa walikana mashtaka na Wakili Horombe alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kumba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, pia hana pingamizi na dhamana.

  Washtakiwa hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye vitambulisho, waliosaini hati ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.
  Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 30, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

  0 0  0 0

   Mratibu wa Mafunzo ya Ujasiriamali, katika  Program ya kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam (YEID) Bw. Dominic Ndunguru akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha ripoti maalumu ya mrejesho wa namna mafunzo ya ujasiriamali yalivyosaidia kukuza ajira kwa vijana, leo Jijini Dar es Salaam.
  b4
  Mratibu wa Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) katika upande wa kujengea uwezo vijana wa kuajirika, Bw. Avitus Mushumba akielezea akifafanua jambo wakati wa mkutano wa tano wa tathmini ya maendeleo ya program hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center leo Jijini Dar es Salaam.
  b5
  Meneja wa Program kutoka Jukwaa la Ushirikiano wa Kimataifa (FIC) la nchini Denmark Bi. Annette Larsen akitoa muelekeo wa namna watakavyo endelea kusaidia uendeshaji wa Program ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar ers Salaam kwa awamu ya pili, program inayotarajiwa kuanza mapema mwezi wan ne mwakani.
  b1
  Afisa Msimamizi wa Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) Bi. Emiliana Muchu akielezea kwa ufupi historia ya program hiyo wakati wa mkutano wa tano wa kutathmini maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar es Salaam.
  b2
  Mratibu wa Ushawishi na Utetezi, katika  Program ya kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) Bw. Elly Ahimidiwe akielezea akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Mikutano ya kutoa taarifa kuhusu mfuko wa Vijana na Baraza la Taifa la vijana, wakati wa mkutano wa tano wa tathmini ya maendeleo ya program hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Centre leo Jijini Dar es Salaam.

  b6
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo katika mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa Program ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam uliofanyka leo katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center Dar es Salaam. Program hiyo ya miaka mitatu kwa awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika mapema mwishoni mwa mwaka huu, huku awamu ya pili ikitarajiwa kuanza mwezi Aprili 2017.
  b7
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha Jijini Dar es Salaam(YEID) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Don Bosco Youth Center leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na: Frank Shija,MAELEZO.

  0 0


  Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakifanyiwa vipimo vya afya na wafanyakazi wa Kitengo cha maradhi yasiyo ambukiza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.
  Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Omar Mwalimu akimpa ushauri Bi. Asha Makame Ali, mfanyakazi wa Wizara ya Elimu, baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa uzito wake hauendani na urefu alionao.
  Muuguzi kutoka kitengo cha maradhi yasiyoambukiza akimfanyia vipimo vya afya Mussa Hassan Zyuma wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali .

  Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Muhammed Abdalla akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ongezeko la maradhi ya kisukari na shindikizo la damu wakati wa kuwapima wafanyakazi wa Wizara hiyo.

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0


  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanzisha mafunzo ya Tiba Shufaa (Palliative Care Services) kwa watumishi wa Sekta ya Afya ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wakati kwa wagonjwa wanaohitaji.

  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla ameyathibitisha haya leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Susan Lyimo aliyehitaji kufahamu juu ya mikakati ya Serikali katika kuhakikisha huduma ya Tiba Shufaa inaboreshwa hapa nchini.

  Dkt. Kigwangalla amesema kuwa katika kuhakikisha huduma za tiba shufaa zinapatikana hapa nchini, hospitali takribani 35 zikiwemo za Rufaa za kanda za Bugando, KCMC na Mbeya , Hospitali za mikoa pamoja na Hospitali za dini zinatoa huduma hizo.

  Ameongeza kuwa huduma hizo pia zimekuwa zikitolewa majumbani kwa wagonjwa wanaokaa karibu na maeneo yenye hospitali zinazotoa huduma hizo ambapo watoa huduma za majumbani husaidia kumfikia mgonjwa moja kwa moja katika maeneo wanayoishi.

  “Sera ya kitaifa ya Tiba Shufaa iliyotolewa Mwezi Juni mwaka huu imeagiza mafunzo yafanyike ili kuwajengea uwezo watumishi waliopo katika vituo vya afya na hospitali nchini ili waweze kutoa huduma hiyo” alisisitiza Mhe. Dkt Kigwangalla.

  Aidha Wizara hiyo imeanza kutoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Chama cha Tiba Shufaa pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na watumishi watano katika kila kituo cha afya ambao wana uwezo wa kutoa tiba hiyo wakijumuisha madaktari, wauguzi, wafamasia pamoja na maafisa ustawi wa jamii.

  Tiba Shufaa ni huduma inayotolewa kwa wagonjwa walio katika hatua za mwisho za maisha yao hasa walio na magonjwa yasiyo na uwezekano wa kupona kwa ajili ya kuwapunguzia maumivu makali wanayoyapata kutokana na magonjwa hayo.

  0 0

  Bi. Sheena Sinare, (katikati) Afisa wa Diamond Trust Bank (DTB), akikabidhi malipo kwa ajili ya ada ya wanafunzi 5 kwa mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Bi. Rachel Mwalukasa. Wanafunzi hao kutoka katika Makao ya Watoto yatima Kurasini ni– Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16). Kushoto ni Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sullivan Provost, Nd. Alex Nicholaus Sibuti. Wanafunzi hao wanajiunga na shule ya bweni ya Sullivan Provost katika kidato cha kwanza mwakani, na tayari wameanza masomo ya awali (Pre-Form one).

  Ilikuwa ni Furaha tele wakati Diamond Trust Bank (DTB), walipotoa udhamini wa kuwasomesha watoto 5 kutoka Makao ya Watoto yatima Kurasini. Wanafunzi hawa watakaojiunga na shule ya Sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani mwakani, tayari wameanza masomo ya awali (pre form one). Benki ya DTB Tanzania kwa kupitia kitengo cha huduma za kijamii, imegharamia mahitaji mengine yote pamoja na ada ya hawa vijana ili waweze kusoma vizuri. katika mstari wa nyuma ni Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16). Walioketi mstari wa mbele kushoto ni Bi. Sheena Sinare, Afisa kutoka DTB Tanzania, Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini, Bi. Rachel Mwalukasa, mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Nd. Alex Nicholaus Sibuti, Mwalimu Mkuu na Bi. Monica Nangale, Afisa toka benki ya DTB Tanzania.(na Mpigapicha Wetu)
  ImmaMatukio
  Afisa wa Benki ya Diamond Trust Bank (DTB) , Bi. Sheena Sinare (katikati) , akiwa pamoja na watoto kutoka Makao ya Watoto yatima Kurasini. Kulia ni Bi. Rachel Mwalukasa, Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya bweni - Sullivan Provost iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani na kushoto ni Bi. Beatrice Mgumiro, Msimamizi wa Makao ya watoto yatima Kurasini. DTB imetoa ada ya mwaka mmoja kwa wanafunzi 5 kutoka katika hicho kituo ambao ni Fadhili Dotto (14), Bakari Majuto (14) , Justin Msafiri (15), Baltadhar Steward (14) na Omary Ramadan (16) ambao wote wapo katika picha. Wanafunzi hao wanajiunga na shule ya bweni ya Sullivan Provost katika kidato cha kwanza mwakani, na tayari wameanza masomo ya awali (Pre-Form one).(na Mpigapicha Wetu)


  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nashi  akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge katika kikao cha saba cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 9, 2016.

   
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 200 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kuongeza mikopo itakayowasaidia wakulima wadogo kuendesha shughuli za kilimo.

  Hayo yamesemwa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Ole Nashi alipokuwa akijibu swali la Mhe. Rose Sekum (Viti Maalum) lililohoji kuhusu mpango wa Serikali kuwafikia wakulima wadogo nchini.

  Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali ilianzisha rasmi Benki hiyo mwezi Agosti 2014 ikiwa na nia thabiti ya kuhakikisha Benki hiyo inapata mtaji wa kutosha ili kutimiza lengo lililokusudiwa la kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo.

  “Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya Benki hiyo ambapo kwa mwaka huu tumetenga Shillingi Bilioni 200, hata hivyo tumejizatiti kuongeza mtaji kupitia Hati Fungani ya mitaji isiyo ya fedha taslimu yenye thamani ya shilingi bilioni 800”, alisema Mhe. Nashi.

  Ameongeza kuwa kufuatia ujio wa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kumekuwa na mazungumzo baina ya benki hizo mbili juu ya kupatiwa mkopo ambao utaiongezea mtaji Benki ya TADB ili iweze kusaidia wakulima wengi zaidi.

  Aidha, ili kuwafikia wakulima wadogo nchini, Mhe. Ole Nashi amefafanua kuwa Benki hiyo imejikita katika kuvijengea uwezo vikundi vya wakulima ili viweze kukopesheka na kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo hiyo.

  Katika utekelezaji wa mpango huo, Benki ilianza kwa kuvijengea uwezo vikundi 89 vya wakulima wadogo vyenye jumla ya wakulima 21,526 na kati ya hivyo, jumla ya vikundi 8 vilitimiza masharti ya msingi ya kuweza kukopa na vilikopeshwa jumla ya shilingi billion1.

  Mpaka sasa TADB inatoa huduma za mikopo kwa wakulima katika mikoa 6 kwa kushirikiana na Sekretarieti za mikoa, Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Mfuko wa Pembejeo na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

  0 0

   Walimu na wanafunzi wa Chuo cha VETA Kipawa wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto) akifafanua juu ya ushirika kati ya Airtel na VETA kwa kuleta mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu yajulikanayo kama Vsomo yaani VETA Somo, katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
   Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi wa chuo hicho juu ya  programu ya Vsomo yaani VETA Somo inayotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ambapo wanafunzi wa Chuo cha VETA watapata fursa ya kusoma  kupitia simu za mkononi, kulia ni Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba. Semina hiyoiliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
   Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Hawa Bayumi (kulia) akielezea faida za programu ya VSOMO kwa walimu na wanafunzi wa chuo cha VETA Kipawa inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. 
   Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba akijibu swali juu ya kozi zipatikanazo kupitia program ya VSomo yaani VETA Somo inayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu, katika semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
   Wanafunzi wa Chuo cha Veta Kipawa wakisikiliza kwa makini katika semina juu ya mpango wa VSomo yaani VETA Somoinayowezesha kupata mafunzo ya ufundi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu, ambapo wanafunzi wa VETA watapata fursa ya kusoma kwa kupitia simu za mkononi wakati wa semina iliyofanyika chuoni hapo Kipawa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita


  0 0  Na Ally Daud-MAELEZO

  WAFANYABIASHARA wa viumbe pori hai wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufungulia biashara ya viumbe hao kutokana na kusitishwa Machi mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Magembe.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai Bw. Salim Mussa amesema kuwa wanamuomba Mh. Rais Magufuli aingilie kati swala hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo ya viumbe kwa maendeleo yao na uchumi wa taifa.

  “Tunakuomba Mh. Rais Magufuli uingilie kati swala hili na kutupatia ufumbuzi wa kudumu ili kuendlea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni za nchi” alisema Bw. Salim.

  Aidha Bw. Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.

  Kwa upande wake Msemaji wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai Bw. Enock Balilemwa amesema kuwa kusitishwa kwa biashara hiyo imepunguza kiwango cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95 wanaishi vijijini.

  “kusitishwa kwa biashara hii ya viumbe pori hai imefanya watanzania takribani milioni moja hasa wakazi wa vijini asilimia 95 kukosa ajira jambo ambalo linapelekea wananchi hao kukosa uwezo wa kujikimu kwa maisha ya kila siku” alisema Bw. Balilemwa.

  Biashara hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha Vyura, wadudu, ndege,mijusi na tumbili, zoo na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika kwa sheria namba 5 ya mwaka 2009.

  0 0

  Rais wa IRMCT, Bw. Theodor Meron akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hapo siku ya jumatano, Ripoti ya utendaji kazi wa Matawi ya Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia zinachokua nafasi ya iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) na Mauaji ya halaiki yaliyotokea katika iliyokuwa Yugoslavia ya zamani ( ICTY. Bw. Meron alitumia pia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa hali na mali katika ujenzi wa majengo yanayochokua nafasi ya ICTR majengo hayo yamejengwa katika eneo la Lakilaki Mkoani Arusha.

  .Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti ya utendaji kazi wa IRMCT ambapo alimshukuru kwa namna ya pekee Msajili wa IRMCT Bw. John Hopkins kwa uongozi wake na ushirikiano ambao ameonyesha katika ujenzi wa majengo mapya huko Lakilaki lakini pia katika kusimamia kipindi cha mpito na makabidhiano kutoka ICTR kwenda IRMCT.

  Na Mwandishi Maalum, New York


  Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena, umeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kusaidia kwa hali na mali ujenzi na hatimaye kuelekea ukamilishwaji wa Majengo mapya ambayo yatatumika kwa shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) ambayo ilihitimisha majukumu yake mwaka jana.

  Shukrani hizo zimetolewa siku ya jumatano na Bw.Theodor Meron, ambaye ni Rais wa Mahakama za Kimataifa za Kesi za Masalia na Utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka zote muhimu za zilizokuwa Mahakama za Kimataifa zilizoshughulikia mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda na Yugoslavia ya zamani ( IRMCT).

  Bw. Theodor Meron alikuwa akiwasilisha Ripoti yake ya Nne kuhusu IRMCT mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa . Ripoti ambayo imeanisha maendeleo ya kipindi cha mpito kutoka ICTR na ICTY kwenda IRMCT kazi ambayo amesema inakwenda vizuri ingawa kumekuwapo na changamoto kadhaa.

  “Wakati ninapowasilisha ripoti hii, nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa mchango mkubwa na ushirikiano ambao tumeupata kutoka serikali ya Tanzania, takribani wiki tatu zijazo majengo hayo yatazinduliwa rasmi baada ya kuwa yamekamilika”. Akasema Bw. Meroe

  Baadhi ya changamoto hizo kwa upande wa iliyokuwa ICTR ni pamoja na kutokamatwa hadi sasa kwa watuhumiwa watatu ambao inaelezwa wapo mafichoni. Ni pili ni mahali pa kuwapeleka watu ambao ama wamekwisha maliza kutumikia vifungo vyao na kuachiwa huru. Watu hao wamekosa nchi ya kuwapokea na hadi sasa bado wanaendelea kuishi nchini Tanzania.

  Na kwa sababu hiyo, Rais wa IRMCT ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano wa kuwachukua watu hao ambao hawana mahali pa kwenda na kwa wale walioko mafichoni nchi ambazo wamejificha watoe ushirikiano kwa kuwafichua na kuwakamata ili hatimaye sheria iweze kuchukua mkondo wake

  Kwa upande wake, Tanzania kupitia Mwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, amesema Tanzania inakaribisha kuhitimishwa kwa ujenzi kwa ujenzi wa makazo mapya ya iliyokuwa ICTR katika eneo la Lakilaki ndani ya wakati na kwa bajeti iliyopangwa.

  “Kwa namna ya pekee tunampongeza Msajili wa Mahakama, Bw. John Hopkins kwa uongozi wake na ushirikiano wake ambao umewezesha kukamilisha hatua hii muhimu sana”. Akasisiza Balozi.

  Aidha kukamilika kwa majengo hayo na ambayo yapo katika ardhi ya Tanzania ni heshima na fahari kubwa na ya kipekee kwa Tanzania na wananchi wake kutokana na jukumu kubwa iliyobeba ya kuwa mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa niaba ya Jumuiya ya Kimataifa. 

  Balozi Manongi pia amepongeza uratibu uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa kupitia Ofisi ya Mshauri wa Sheria, Ofisi ya Msajili na the Hegue ya kuhakikisha kwamba, pamekuwapo na utaratibu mzuri wa kurithishana kutoka ICTR kwenda IRMCT. Na kwamba kazi hiyo haikuwa nyepesi.

  Akizungumzia kuhusu kazi za IRMCT, Balozi amesema, Tanzania ingependa kuona Taasisi za Kitaifa zinawezeshwa ili ziweze kushughulikia kwa ukamilifu, haki na usawa na kwa kuzingatia sheria za kimataifa kesi zinazopelekwa kwenye Taasisi hizo za kitaifa.Aidha akasema uzoefu ambao umepatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na ICTR pamoja na ile ya ICTY ni vema ukatumika kama mfano katika Mahakama nyingine za Kimataifa.

  Kwa upande wa mashahidi, Tanzania imesisita umuhimu wa mashahidi kulindwa na kuhakikishiwa usalama wao dhidi ya vitisho mara baada ya kutoa ushahidi.Kuhusu watu walioachiwa huru baada ya kukamilisha vifungo vyao na bado wapo nchini Tanzania. Tanzania imeungana na wazungumzaji wengine katika mkutano huo wa kutaka pawepo na majadiliano ya kina ya kuangalia namna gani ya kuwasaidia watu hao.

  Vile Tanzania imetoa wito kwa nchi zile ambazo zinahisiwa kwamba zinawahifadhi watuhumiwa watatu ambao wapo mafichoni na wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kutoa ushirikiano ili hatimaye haki itendeke.Watuhumiwa ambao wametajwa kuwa walihusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji ya Kimbari nchini Rwanda na wapo mafichoni hadi sasa ni Augustin Bizimana, Felicien Kabuga na Proitas Mpiranya. 

  Kwa mujibu wa Ripoti iliyowasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, watuhumiwa hao watakapopatikana kesi zao zitafanyika katika Mahakama hiyo mpya nchini Tanzania.Uamuzi kwa kuwa na matawi ya IRMCT huko Arusha na the Hague, Uholanzi unatokana na maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia azimio nambari 1966 la mwaka 2010.

  Kupitia Azimio hilo Baraza la Usalama liliamua kwamba, baada ya kumalizika rasmi kwa ICTR ( 2015) na ICTY ( 2017) Tanzania ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wa ICTR itapewa jukumuu la kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka zote muhimu za iliyokuwa ICTR ikiwa ni pamoja na kumalizia kesi zitakazokuwa zimebaki. Huku the Hague ikiwa na dhamana hiyo hiyo kwa kazi zilizokuwa za iliyokuwa ICTY.

  Mahakama za Kimataifa za Rwanda na Yugoslavia ambazo zimefanya kazi kubwa ya kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa karibu wote waliohusika na matukio ya kutisha ya ukiukwaji wa haki za binadamu ziliazishwa mwaka 1990 na Umoja wa Mataifa.

  0 0  Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar 9-11-2016

  Meneja wa Biashara wa Kiwanda cha sukari Mahonda Bw Pronav Shah amekumbushia ombi lao kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar la kukipatia Kiwanda maeneo zaidi ya ardhi ili kuimarisha uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

  Amesema kiwanda hulazimika kusitisha uzalishaji wa sukari kutokana na upungufu wa miwa na huku ikwalipa mishahara wafanyakazi bila ya kuzalisha na kukipelekea kiwanda kuingia katika hasara.

  Ameeleza hayo Ofisini kwake Mahonda wakati Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ilipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kuangalia mafanikio na changamoto zinazowakabili . 

  Bw Pronav Shah ameieleza Kamati hiyo ya Baraza la Wawakilishi kuwa sehemu kubwa ya mashamba ya kiwanda imevamiwa na wananchi wa kawaida kwa shughuli zao ikiwemo ujenzi wa nyumba huku wakijua kuwa ni sehemu ya kiwanda na kupunguza ukubwa wa shamba hilo. 

  “Sehemu kubwa ya shamba la miwa hivi sasa limevamiwa na watu wa kawaida na inasemekana wanaungwa mkono na baadhi ya viongozi wa shehia,” amelalamika Meneja huyo.

  Katika hatua nyengine Meneja huyo wa Biashara ameiomba serikali kuwapatia bima ili inapotokea ajali waweze kufidiwa gharama za ajali hiyo. 

  Amesema iwapo serikali itawapatia bima itawasaidia hasa kwa vile mara kwa mara mashamba ya miwa hushambuliwa na moto ambao haujulikani chanzo chake licha ya juhudi za uchunguzi zinazofanwa na jeshi la Polisi. 

  Bw. Pronav Shah ameshauri kuruhusiwa kupanua soko la kuuza sukari katika soko la Tanzania Bara ambalo hivi sasa bei ni tafauti na Zanzibar ama kuuza sukari yao Zanzibar kwa bei ya soko la Tanzania Bara.

  Nae mwenyekiti wa Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo Yussuf Hassan ameutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuendeleza uzalishaji wa sukari ili kuwasaidia vijana kupata ajira na kufikia lengo la kujitosheleza kwa bidhaa hiyo.

  Ameuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa ombi lao la kupata ardhi zaidi kwa ajili ya kuongeza mashamba ya miwa watalifikisha katika ngazi za juu ili liweze kupatiwa ufumbuzi.

  Amesema Serikali inafahamu kuwa kufanikiwa kwa Kiwanda cha sukari cha Mahonda itakuwa ni kivutio kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza Zanzibar.

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo(katikati) katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Dini waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Amani.


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akifungua Kikao cha kwanza cha Kamati ya Amani ya viongozi wa dini Mkoa kilichofanyika Ofisini.

  Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Arusha Bi. Jacquline Kapila akielezea kazi za Taasisi yake kwa viongozi wa Dini kwenye kikao cha kamati ya Amani.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo akiongea na viongozi wa Dini wakati wa Kikao cha Kamati ya Amani.

  ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mkoani Arusha, Solomon Masangwa akioelezea mchango wa viongozi wa Dini katika kuhamasisha amani.

  Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma akichangia kwenye Kikao cha Kamati y Amani kwa kawataka wananchi kudumisha amani na kujenga utamaduni wa kuvumiliana.

  Askofu Dr. Leornard Mwizarubi wa Kanisa la SAYUNI EAG (T) akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Amani na kumshkuru RC Gambo kwa kikao hicho na kushauri Kamati hii ikutane mara kwa mara ili kushirikiana kwa karibu na Serikali kutatua kero za wananchi.

  Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Arusha Ndg. Apili Mbaruku akijibu hoja za viongozi wa dini wakati wa Kikao cha Kamati ya Amani.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo(kushoto) katika mazungumzo na ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati (KKKT) Mkoani Arusha, Solomon Masangwa baada ya Kikao cha Kamati ya Amani.

  Nteghenjwa Hosseah – Arusha 

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo amekutana na kamati ya Amani  ya Mkoa ambayo inajumuisha viongozi wa dini mbalimbali zilizoko katoka Mkoa huu kuzungumzia mustakabali wa Amani na namna viongozi hawa wa dini watashirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa wananchi ambao ni waumini wao.

  Akizungumza katika Kikao hicho Mhe. Gambo alisema kazi ya Ulinzi wa Amani itakua rahisi sana kupitia viongozi wa dini ambao wana karama ya kuongea na kubadilisha maisha ya watu bila kutumia nguvu ama kuwashurutisha isipokua kwa chakula cha roho ambacho hujenga misingi imara ya imani na tabia njema.

  Maendeleo ya wananchi hayawezi kupatikana bila Amani kuwepo katika Mkoa wetu ni lazima tusaidiane katika hili dhamira yetu ifanikiwe kwa wepesi zaidi tuna Imani kubwa sana Na viongozi wetu wa dini na ndio maana nikaona ni vyema tukakutana ili tusikie kutoka kwenu ninyi ambao mnawakilisha kundi kubwa la wananchi na pia kufahamu kero mbalimbali zinazowakwaza wananchi katika maeneo yenu alisema Gambo.
   
  Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati KKKT Solomon Masangwa akichangia kuhusu masuala yanayoweza kuhatarisha amani alisema kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tatu na litasaidia sana katika ulinzi wa Amani ni waendesha boda boda pamoja na wanachinga ambao kwa sasa wanaonekana kutopewa kipaumbele au hatuwajali kwa kiasi kinachostahili.

  Tunapaswa kuangalia namna gani watu wanaofanya shughuli hizi wanakua rasmi kwa kupatiwa maeneo maalumu pamoja na utambulisho utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa Amani na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na si kama walivyo sasa wanafanya kazi hizo katika maeneo yasiyo rasmi na kuhama kila siku hali hii ina wafanya wajihisi kama si sehemu ya Taifa hili hivyo wanaweza kutumika kiurahisi kuhatarisha amani ya Nchi yetu alisema Masangwa.

  Akichangia katika viashiria vya uvunjifu wa amani Askofu Dr. Leornard Mwizarubi wa Kanisa la SAYUNI EAG (T) alisema ni vyema Serikali ikajikita katika kutatua changamoto zinazoathiri maisha ya kila siku ya wananchi ili hata sisi viongozi wa dini tunapoongea na waumini tuwe na vielelezo dhabiti vya kuonyesha namna ambavyo Serikali kero zao zimeshughulikiwa.

  Aliendelea kusema “Katika eneo ambalo ninatoa huduma ya Kiroho kwenye Kata za Unga Ltd, Sokoni 1, Daraja II, Sinoni na maeneo ya jirani wakazi wa mitaa hiyo wanapata shida sana ya huduma ya maji Taka na hata katika Kanisa langu inanilazimu kutafuta gari la kunyonya maji taka mara tatu kwa wiki ili kufanya mazingira kuwa safi, sasa kuna maeneo mengine wananchi hao hawana uwezo wa kutafuta gari hilo la kunyonya maji taka hivyo wanaishia kulalamika kwa kuishi katika mazingira machafu”.

  Aidha Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma alishkuru Sekretariet ya Mkoa kwa kikao hiki muhimu kwa ustawi wa jamii ya Arusha na kueleza kuwa katika kipindi hiki cha Mpito Nchi yetu inahitaji maombi ya bila kikomo ili kuweza kuvuka salama na tunategemea kuendelea kuona mabadiliko katika kila eneo; Tunaamini si wote wanafurahia mabadiliko haya hivyo tuna wajibu wa kuwajulisha waumini wetu kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya mifumo katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na faida zitakazo patikana kwa Taifa.
   
  Akiwasilisha changamoto katika upande wake Sheikh Shaaban alisema “Kuna ukuaji wa kasi ya makazi holela katika Jiji la Arusha, Utaratibu wa mipango miji hauzingatiwi na hii inasabisha maeneo mengi kutopitika kwa urahisi hivyo hata itakapotokea dharua sio tahisi kwa wananchi wetu kupata msaada wa haraka, tunaomba wanachi wapimiwe maeneo yao, barabara zifunguliwe ili huduma muhimu ziweze kufika katika maeneo hayo”.

  Mkurugenzi wa Idara ya maji safi na maji Taka (AUWASA) Eng. Ruth Koya alisema Taasisi yake inaanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji safi na Taka ambao matatizo yote yaliyowasilishwa katika kikao hiki yanayohusiana na maji yatashughuliwa kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa mradi huo utahusisha uboreshaji wa mioundombinu ya maji safi, Uhamishaji wa mabwawa ya maji Taka(yaliyokuwa Lemara kwa hivi sasa), ununuzi wa magari ya kunyonyea maji machafu pamoja na magari ya kusambaza na kuuza maji safi.

  Mkuu wa Mkoa Mge. Gambo alitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na kuelezea namna ambavyo Changamoto ya Mipango Miji ilivyopata ufumbuzi kupitia ukamilishaji wa Mpango Mkakati wa Jiji la Arusha (Master Plan) na kuwajulisha wajumbe kuwa mpango umekamilisha na umekwishapitiwa na Halmashauri zote tatu zinazohusika, hivyo kwa hivi sasa utawasilishwa Wizarani na taratibu zote zikikamilika utekelezaji utaanza mara moja.Kuhusu suala la Machinga na waendesha boda boda boda Rc Gambo alisema Serikali imekwisha anza utaratibu wa kutafuta maeneo salama na rafiki kwa ajili ya wafanyabishara ndogondogo maarufu kama machinga na tutaongea nao ili tuwe na makubalino ya pamoja.

  Aidha kuhusu bodabdoa tumeanza kuwatambua kupitia kwenye uongozi wa mitaa na vituo vyao na tutahakikisha tunaboresha mazingira yoa ya kufanyia kazi na zaidi tunawatafutia Pikipiki ambazo watapewa Vijana wanaofanya biashara ya boda boda kwa utaratibu maalumu; Itawapasa kurudisha Fedha za Pikipiki tu na kisha kupata umiliki halali ya Chombo hicho tofauti na sasa hivi ambapo wanapewa pikipiki hizo na kulipa mara mbili ya bei kwa matajiri wao ndipo wapate Umiliki alimalizia Gambo.

  0 0


  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mheshimiwa Hemed Mgaza kushoto, akishuhudia Viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY nchini hapa wakisoma ramani ya Tanzania katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh, ili kuifahamu vizuri Tanzania na maeneo watakayofikia katika msafara wao wa kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma za afya bure kwa siku 10 kwenye Hospitali za Chake Chake na Wete. Picha na Mpiga Picha Wetu, Riyadh.
  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akiwa na viongozi wa Madaktari Bingwa wa Jumuiya ya WAMY ambao walifika Ubalozini mjini Riyadh kujitambulisha na kukamilisha taratibu za safari kuingia Tanzania. Madaktari hao wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba 11.

  0 0
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwa niaba ya Serikali.Shughuli za kuaga zitaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye tayari amekwishawasili ukumbini hapo na kufuatiwa na viongozi wengine waandamizi wa chama na Serikali.

  Marehemu Mungai amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mkuu wa Mkoa, Mbunge kuanzia miaka ya 1970 hadi 2010, na amekuwa Waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzia Awamu ya kwanza mpaka ya nne.

  Viongozi Wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Mh.William Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya Pili Mh.Frederick Sumaye na viongozi wengine waandamizi wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar.

  Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa kuanza kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar.

  Nyimbo mbalimbali za maomboleza zikiendelea

  Ndugu,jamaa na Marafiki wakiendelea kuwasilika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu Joseph Mungai, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mufindi aliyefariki Novemba 08, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam..

older | 1 | .... | 1036 | 1037 | (Page 1038) | 1039 | 1040 | .... | 1898 | newer