Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1035 | 1036 | (Page 1037) | 1038 | 1039 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kupitia vyombo mbalimbali vya redio, kesho jumatano Novemba 09, 2016 mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago", ataachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha Hadmad.

  Kabago anatambulika kama mmoja wa watu waliowezesha hiphop nchini kusonga mbele tangu akiwa mkoani Arusha na hata alipohamia Mwanza, akiwa kama msanii na mtangazaji wa redio (kwa sasa Passion Fm Mwanza).

  Atakumbukwa namna alivyosaidia kwenye harakati za kimaendeleo Jijini Mwanza kupitia kazi zake za muziki na hata namna wimbo wa tatizo la umeme ulivyoleta nafuu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.

  Kama hiyo haitoshi, mchango wake redioni ni mkubwa kwa wasanii mbalimbali hususani wanaochipukia ambapo wengi wao ambao sasa ni wanavuma akiwemo Baraka Da Prince na Young Killer, wamepitia mikononi mwake. 

  Kaa tayari kuusubiri wimbo wa Kabago uitwao Tanzania ambao umetengenezwa kwenye studio yake iitwayo K-Records chini ya produza Sam Music.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akielekea kupanda gari ya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
  Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gari ya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
  mke wa mbunge  wa jimbo la Arusha mjini Neema Lema akiwa anaondoka mahakamani  kumsindikiza mme wake mara baada ya mahakama kuisha na lema kuamriwa kwenda mahabusu ya magereza hadi ijumaa ambapo kesi yake itatajwa tena

  Na  Woinde Shizza,Arusha
  Vilio na majonzi vimetawala katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mara baada ya Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana.


  Hatua hiyo imekuja kufuatia mabishano ya kisheria kuhusiana na dhamana ambapo mawakili wa serikali wakiongozwa na wakili Matenus Marandu pamoja na  Paulo Kadushi kupinga dhamana ya Mbunge huyo  kutoka na kile mawakili wa serikali walichodai kuwa iwapo atapewa dhamana ataenda kuendelea kufanya mikutano  ya adhara ya uchochezi.


  Aidha hoja zingine zikizotajwa na mawakili hao  walieleza mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi Desderi Kamugisha  kuwa uchunguzi wa kesi zingine  za uchochezi zinazomkabili Mbunge huyo zinaonyesha  alipewa dhamana ili ajirekebishe  lakini ajirekebishi na amekuwa akirudia rudia makosa yanayofanana kila Mara.


   Kwa upande wake jopo la mawakili wasomi wa upande wa mshitakiwa wakiongozwa na John Malya ,Sheck  Mfinanga ,Ahmed  Hamis  na Charles Adiel Mshitakiwa ana Haki ya kupata dhamani ukizingatia kesi inayomkabili bado uchunguzi wake haujakamilika  hivyo anahaki ya kupewa dhamana kulingana na sheria na katiba inavyo dai aidha waliongeza kuwa mtuhumiwa ni Mbunge wa bunge la Tanzania hivyo mahakama inawajibu wa kumpatia dhamana kwaajili ya kuendelea na majukumu ya wananachi ambao wamemchagua.


  Waliongeza kuwa pamoja na Mbunge huyo kukabiliwa na kesi mbili ambapo alitaja kesi ya kwanza inayomkabili ni namba 440 na ya Pili ninamba  441 za mwaka 2016 ya kutoa lugha  ya  uchochezi dhidi ya muheshiwa Rais ambapo alisema maneno  kuwa nchi hii aita tawalika na  itaingia kwenye machafuko iwapo Rais atafuata katiba na  sheria  hivyo bado anaamini makosa hayo yanastaili kupata dhamana kama sheria ya makosa ya mwenendo ya jinai .


  Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili hakimu kamugisha alihairisha  shauri hilo adi November 11 itakapo kuja kutajwa tena na kutolewa uwamuzi mdogo iwapo mshtakiwa Lema atapata dhamana au Ataendelea kukaa kizuizini .
  Wakati Mbunge huyo akiondoshwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi  Lema alionekana kujiamini huku akiwa ameshika biblia takatifu  ndipo wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo  Chadema waliangua vilio na mayowe huku wakilia Mbunge huyo.


  Akitoa tamko Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha  Amani Golugwa aliwaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wavumilivu katika kipindi hichi kigumu cha Mbunge wao kushikiliwa na kuwataka kujitokeza kwa wingi  mahakamani kufatilia mwenendo wa kesi ya Mbunge wao.

  Awali kabla  ya kuanza kusikiliza kesi hiyo jaji Salma  Majimbi alimuamuru mwanasheria wa serikali  kumleta mshitakiwa Lema  ndani ya nusu saa mahakamani hapo ,baada ya kukaa mahabusu ya polisi ndani ya masaa 175  kinyume cha she ria ya makosa ya jinai.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  SERIKALI imezitaka taasisi zinazosimamia mtandao wa haki za binadamu katika nchi za Afrika Mashariki kupanua wigo wa utoaji elimu kwa umma, hatua inayolenga kutatua migogoro ya mara kwa mara inayojitokeza katika jamii.

  Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome, wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa taasisi zinazosimamia Haki za Binadamu katika nchi za Afrika Mashariki.

  Prof. Mchome alisema jukumu la ulinzi na usimamizi wa haki za binadamu katika eneo la jumuiya hiyo ni la kila nchi mwanachama, kwa kuwa msingi wa maendeleo wa nchi yoyote duniani hupatikana katika sehemu yenye hali ya utulivu na maeleweno.

  Kwa mujibu wa Prof. Mchome alisema kuanzia mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu, nchi zote za Afika Mashariki ziliwasilisha taarifa zao kuhusu hali ya haki ya kibinadamu katika mataifa yao, mjini Gevena Uswisi, ambapo ripoti hizo zitatumika katika kujadili changamoto zilizojitokeza na hatua za kuchuliwa katika kuboresha.

  Aidha Prof. Mchome alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kubwa katika kuimarisha haki za kibinadamu duniani ingawa yapo maeneo kadhaa yenye migogoro ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji, ingawa Serikali imechukua hatua za makusudi za kukabiliana na hali hiyo.

  “Serikali imekuwa ikipeleka taarifa Bungeni kuhusu migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, na maamuzi ya kisera yanayofanywa na Serikali, pamoja na kuendelea kuelimisha umma kuhusu masuala ya sheria mkononi.” Alisema Prof. Mchome.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAG), Mary Massay alisema suala la haki za binadamu ni dhana mtambuka kwa kuwa inagusa sekta muhimu za maisha ya binadamu ikiwemo elimu, maji, ardhi, maliasili na kadhalika.

  Alisema mkutano huo umeandaliwa makhususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya ripoti za utafiti kuhusu hali ya haki za binadamu katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.

  Alisema utafiti huo umejikita zaidi katika kubaini viashiriia vya uvunjifu wa haki za baindamu katika nchi hizo na hatua zinazopaswa kuchuliwa na Serikali za nchi wanachama ili kuzuia machafuko katika siku za usoni kutokana uzoefu uliojitokeza katika nchi za Rwanda na Burundi.

  Kwa mujibu wa Massay alisema migogoro mingi inayotokeza katika nchi nyingi za Afrika hususani zilizopo katika ukanda wa Afrika mashariki husababishwa na kauli na matamko ya viongozi kuagiza jambo ambalo linakwenda kinyume na matakwa ya wananchi walio wengi.

  Naye Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya nchini Kenya, George Morara alisema hali ya haki za kibinadamu ya nchi hiyo ni ya kurithisha ingawa mamlaka za dola katika nchi hiyo zimekuwa zikikuwa zikitumia nguvu kubwa kuthibiti raia kwa kutumia sheria zilizopo.

  Alisema miongoni mwa sheria ni sheria ya kimataifa inayohusu haki za kiraia na kisiasa ambapo, baadhi ya maafisa usalama nchini humo wamekuwa wakitumia nguvu kuzuia mikusanyiko ya kisiasa kwa kigezo cha kudhibiti matukio ya kigaidi nchini humo.

  0 0

  NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kuweka kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda nchini.

  Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa tukiwa tunaelekea katika nchi ya viwanda serikali inajukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji nchini.

  Dkt. Adelhelm amesema kuwa viongozi hao hawana budi kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano wanaoutoa kwa wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika mkoa huo.

  “Dhumuni la serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunaifikia nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda,na hili tutalitekeleza pia kwa kushirikiana na sekta binafsi na ni jukumu la viongozi ikiwemo wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nchini kote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda”. Alisema Dkt. Adelhelm

  Dkt. Adelhelm aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2020 Serikali imepanga kuhakikisha sekta ya viwanda nchini inachangia asilimia 15 kwenye pato la taifa kutoka asilimia 7.3 iliyopo hivi sasa.

  Pia Dkt. Adelhelm alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya ajira za viwandani na ajira zitokanazo na sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia 40 ifikapo mwaka 2020.

  Naye Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza katika viwanda ikiwemo kupitia maandiko ya miradi yao na kuwasimamia ili kuhakikisha kwa pamoja wanatimiza lengo la serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  Bw. Mkucha aliongeza kuwa katika wilaya ya Kibaha kuna hekari 330 zilizotengwa kwa ajili ya viwanda vya aina mbalimbali ikiwamo viwanda vya kuunganisha magari, vuwanda vya madawa na viwanda vya nguo hivyo kama kuna muwekezaji mwenye nia ya kuwekeza katika sekta hizo aende katika ofisi za Shirika hilo ili kuweza kujadili namna ya kutekeleza suala hilo.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho katika mkoa wa pwani ni mwendelezo wa jitihada za kumuunga mkono Rais Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Bw. Joseph Wasonga alishukuru jitihada za serikali na taasisi zake kwa ushirikiano wanaoupata tangu wakiwa na wazo la kuanzisha kiwanda hicho hadi kufikia hatua hiyo ya uzinduzi.

  Bw. Wasonga aliongeza kuwa dhumuni la kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio milioni 16 hadi milioni 20 kwa mwaka na kuongeza zaidi idadi ya ajira kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka kiwanda hicho na maeneo ya jirani.

  Kiwanda cha hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) na kampuni ya Wande Printing and Packaging inayomilikiwa na mzawa.

  0 0  Waombolezaji na viongozi mbalimbali wameendelea kujitokeza kutoa salam za pole kwa familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samweli Sitta aliyefariki ujerumani juzi kwa Maradhi ya Tezi Dume.


  Viongozi walio wasili nyumbani kwa Marehemu mtaa wa Rufiji Masaki jijini Dar es salaam leo ni pamoja na Mzee Waziri wa Afya wa Zamani Profesa Philemon Sarungi, Mbunge wa zamani wa Kahama Mhe. James Lembeli, Mbunge wa zamani wa Mafia Mhe Abdul Karim Shah, Mbunge wa zamani wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi pamoja na Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Mwantumu Mahiza .  Msemaji wa familia, Bw. Gerlad Mongella amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Dar es salaam siku ya Alhamisi majira ya saa nane na kupelekwa nyumbani. Siku ya ujumaa mwili wa marehemu utaagwa kuanzia majira ya saa tatu hadi saa sita katika viwanja vya Karimjee, kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili kuagwa rasmi na waheshimiwa wabunge.

  Bw. Mongella amesema kuwa ratiba ikienda kama wanavyotarajia, mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika siku ya Jumamosi huko nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

  Amesema wanafamilia wanashukuru ndugu jamaa na marafiki  kwa kuendelea kwao kufika hapo nyumbani na kuwafariji katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

   mmoja wa waombolezaji akiwa ameinama kwa uchungu baada ya kusaini  katika daftari la maombolezo nyumbani kwa Marehemu mtaa wa Rufiji Masaki jijini Dar es salaam leo


  Waziri wa zamani Profesa Philemon Sarungi akitoa mpole kwa mtoto wa Marehemu,Agnes Sitta katika msiba wa aliykuwa spika wa zamani Samuel Sitta.

   Dkt Emmanuel Nchimbi akisaini kitabu cha Maombolezo 
   Wabunge wastaafu wakiwa kwenye maombolezo ya Marehemu Samwel Sitta
  Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Banji,akimpa pole Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. paul Makonda. Picha zote na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

  Mkutano wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeishauri Serikali kutosaini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi Kati ya Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) – (EPA) kwa kuwa hauna manufaa kwa nchi ya Tanzania.

  Ushauri huo umetolewa leo mjini Dodoma na wabunge wa Bunge hilo baada ya kuujadili mkataba huo kwa kina kwa kutoa maoni yao ambapo wengi wameunga mkono kutosainiwa kwa mkataba huo.

  Baadhi ya wabunge waliopata nafasi ya kutoa maoni yao katika mjadala huo ni Mbunge wa Mtwara Vijijini(CCM) Mhe. Hawa Ghasia amemshauri Mhe. Rais Dkt .John Pombe Magufuli kutosaini mkataba huo kwa kuwa mkataba huo una hasara nyingi kwa taifa kuliko faida.

  ”Kwa kuzingatia mkataba umeruhusu uingizaji na utoaji wa bidhaa huru na ukizingatia hakuna nchi hata moja ya Ulaya ambayo Tanzania inapeleka bidhaa zake hivyo mkataba huu hauna maslahi kwa watanzania”, alisema Mhe. Ghasia.

  Ameongeza kuwa Tanzania sio nchi ya kwanza kutosaini mkataba huo kwani kuna nchi kama Angola, Nigeria, na Gambia hazijasaini,ameongeza kuwa kama Tanzania itakubaliana na mkataba huo utaua viwanda pamoja na biashara za Tanzania.

  Kwa upande wake Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amesema kuwa tatizo lililopo katika mkataba huo ni kutoitambua nchi kama nchi na badala yake kuangalia nchi zote kwa pamoja hivyo amewashauri wabunge kuhoji kuanzia kwenye kiini cha tatizo.

  “Kwa kuwa kifungu cha 143 cha mkataba huo kinaruhusu kupeleka marekebisho, naishauri Serikali yetu ipeleke marekebisho ya kupendekeza kila nchi iingie mkataba kivyake kulingana na maslahi ya nchi yake”, alisema Bashe.

  Aidha, Mbunge wa Mwibara (CCM) Mhe.Kangi Lugola amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kukataa kusaini mkataba huo kwani ni miongoni mwa mikataba mibovu kati ya mikataba iliyowahi kuletwa nchini kutoka katika nchi za Ulaya.

  “Kama tukikubali kusaini mkataba huu nchi hii itakuwa dampo la bidhaa mbalimbali za ajabu kutoka nje na hivyo kupelekea kushindwa kutimiza dhamira ya nchi ya kuimarisha viwanda vyetu”, alisema Mhe. Lugola.

  Naye, Mbunge wa Mchinga (CUF) Mhe. Hamidu Bobali amesema kuwa mkataba huo haufai kwa maslahi mapana ya taifa hili kwani unataka kuondoa ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini wakati nchi ya Tanzania inaingiza bidhaa nyingi kutoka nje kuliko kupeleka bidhaa nje ya nchi.

  “Kama tukikubali tukaondoa ushuru wa kuingiza bidhaa kutoka nje basi tutapoteza mapato mengi yanayotokana na kuwepo kwa bandari pia tunatakiwa tujiulize kama mkataba umeruhusu uingizaji na utoaji wa bidhaa huru je nchi yetu ina bidhaa zinazokidhi vigezo vya kuingia katika nchi za Ulaya?” , alihoji Mhe. Bobali.

  Mhe. Bobali ametoa rai kwa Serikali kuileta Bungeni mikataba mikubwa kama ya gesi na madini kwa ajili ya kujadiliwa kwa kina ili kuepuka kusaini mikataba isiyo na tija kwa Taifa.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watu Wenye Ulemavu kutoka Dar es salaam kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba  8, 2016. Watu hao Wenye Ulemavu ni miongoni mwa wengi waliotembelea bunge.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  wale2

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hoyo Bw. Amon Mpanju akizungumza na kikosi kazi maalum kinachofanya kazi ya kujadili mapendekezo ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuifanyia marekebisho na iendane na mahitaji ya wakati uliopo  washiriki wa kikosi kazi cha kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ndoa ya 1971 ilikuweza kumlinda mtoto, wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hoyo Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuzungumza nao juu ya utekelezaji wa jukumu lililo mbele yao


  washiriki wa kikosi kazi cha kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ndoa ya 1971 ilikuweza kumlinda mtoto, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof Sifuni Mchome alipokuwa akizungumza nao juu ya utekelezaji wa jukumu lililo mbele yao  Picha ya pamoja

  ……………………………………………………………

  Serikali imeanza mjadala na baadhi ya wadau ili kupata maoni yao juu ya kuifanyia marekebisho Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ili kumlinda mtoto.

  Akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili mapendekezo ya kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya 1971 jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome amesema serikali imedhamiria kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili iende na wakati na kumlinda mtoto wa kike nchini.

  “Tumeamua kuifanyia marekebisho sheria hii kutokana na ukweli kwamba jamii na wanaharakati wameizungumza sana, huku mazingira yakiwa yamebadilika , kuridhia mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo ina lenga kumlinda mtoto na kufanya Utafiti juu ya mapungufu yaliyomo katika Sheria ya Ndoa kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria. Hili ni suala ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu hadi ikafikia jamii kukosa imani na Serikali,na kutokana na hali hiyo tumeamua kuanza kukaa na baadhi ya wadau ili tuweze kupata maoni juu ya kurekebisha sheria hiyo,” alisema Prof Mchome.

  Alisema Serikali imekuwa ikikerwa na suala hilo na kuchukua hatua madhubuti za Kisera na Kisheria kumlinda Mtoto hasa wa Kike kwa kuweka makosa ya kujamiiana (statutory rape) kwa mtoto chini ya mika 18 na kufanya elimu hadi ya Sekondari kuwa ya lazima na kuweka marufuku ya kumuoa/kumuoza mtoto wa kike ambaye bado yuko shuleni, iwe ya Msingi au Sekondari ili aweze kumaliza shule angalau ya Sekondari na kufikia malengo yake ya kimaisha.

  “Serikali imechukua hatua madhubuti za Kisera na Kisheria ili kumlinda Mtoto wa Kike dhidi ya ndoa za utotoni kwa kuweka makosa ya kujamiiana (statutory rape) kwa mtoto chini ya mika 18, kKufanya elimu hadi ya Sekondari kuwa ya lazima; na kuweka marufuku ya kumuoa/kumuoza mtoto wa kike ambaye bado yuko shuleni, iwe ya Msingi au Sekondari, nia hapaikiwa ni kumlinda mtoto hususan wa kike ili aweze kumaliza shule angalau Sekondari na kufikia malengo yake ya kimaisha,” alisema

  Alisema Serikali ilichelewa kuifanyia marekebisho sheria hiyo kutokana na ukweli kuwa suala la ndoa haligusi sheria pekee, linagusa pia mila, desturi na imani za dini na kuongeza kuwa kwa hali hiyo, haitakuwa busara kwa serikali ambayo inaheshimu imani za kidini na inatambua uwepo wa mila na desturi zinazofuatwa na makabila mbalimbali na kujichukulia jukumu la kuamua bila ya kupata maoni na ridhaa ya wananchi na kuongeza kuwa sasa serikali inaona ni wakati muafaka kuingia katika mjadala na wadau ili kukamilisha hatua zilizoanza kufanyika kupitia Sera na Sheria nyingine.

  Wadau kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Wanawake-UN-Women, Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Watoto- UNICEF, wanasheria kutoka WILDAF, WILAC, TAWLA na Wizara ya Mambo ya Katiba Sheria na taasisi zake na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji  Nd,Mustafa Aboud Jumbe Mwinyi pamoja viongozi wengine alipotembelea Ujenzi wa barabara ya Mgagadu-Kinanzini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kutembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo, [Picha na Ikulu.] 07 Nov 2016.
  sei2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Afisa Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mohamed Baucha alipotembelea Ujenzi wa barabara ya Mgagadu-Kinanzini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kutembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo, [Picha na Ikulu.] 07 Nov 2016.
  sei3
  Mkurugenzi wa Mfuko wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Ali Twahir akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea Ujenzi wa Barabara ya Mgagadu-Kinanzini yenye urefu wa Kilomota 7.6 katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba alipofanya ziara leo ya kutembelea barabara hiyo.
  sei4
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe,Mwanajuma Majid Abdalla akimakaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuwasalimia Wananchi wakati alipotembelea Ujenzi wa Barabara ya Mgagadu-Kinanzini yenye urefu wa Kilomota 7.6 iliyojengwa Serikali kupitia Idara ya Barabara katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara maalum  ya kutembelea barabara hiyo leo.sei5
  Sheha wa Shehia ya Kendwa Wilaya ya Mkoani Bibi Subira Mohamed Ali alipokuwa akizungumza kero za Shehia yake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasalimia Wananchi wakati alipotembelea Ujenzi wa Barabara ya Mgagadu-Kinanzini yenye urefu wa Kilomota 7.6 iliyojengwa Serikali kupitia Idara ya Barabara katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba alipofanya ziara leo ya kutembelea barabara hiyo.
  sei6
  Baadhi ya Wananchi na Viongozi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwasalimia Wananchi wakati alipotembelea Ujenzi wa Barabara ya Mgagadu-Kinanzini yenye urefu wa Kilomota 7.6 iliyojengwa Serikali kupitia Idara ya Barabara katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba alipofanya ziara leo ya kutembelea barabara hiyo, [Picha na Ikulu.] 07 Nov 2016.
  sei7
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipozungumza na kuwasalimia Wananchi wakati alipotembelea Ujenzi wa Barabara ya Mgagadu-Kinanzini yenye urefu wa Kilomota 7.6 iliyojengwa Serikali kupitia Idara ya Barabara katika Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara maalum  ya kutembelea barabara hiyo leo, (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe,Mwanajuma Majid Abdalla na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe,Hamed Suleiman, [Picha na Ikulu.] 07 Nov 2016.
  sei8

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini Maazimio ya Wabunge wa Tanzania yenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu” TB Caucus “,mtandao huo ulianzishwa jijini Barcelona,Hispania Oktoba 2014 na kuitwa Mtandao wa Wabunge duniani “The Global TB Caucus
  Mjumbe wa Mtandao wa wabunge duniani,Mhe. Faustine Ndugulile akisaini maazimio hayo
  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii, Mhe. Peter Serukamba akisaini maazimio hayo ya wabunge wa Tanzania.nchini Tanzania takribani wagonjwa 160,000 huugua kifua kikuu kila mwaka.
  .Picha ya pamoja ya maofisa toka wizara ya afya na wadau wa Tb wakiwa na Waziri wa Afya na mjumbe wa mtandao wa wabunge duniani
  Naibu Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na ukoma Dkt. Liberate Mleoh akijibu maswali yaliyoulizwa na waheshimiwa wabunge wakati wa semina ya wabunge kuhusu kifua kikuu iliyofanyika kwenye ukumbi wa wabunge jijini Dodoma.
  Afisa mpango toka mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma dkt. Deus Kamala akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wabunge.(Picha zote na Catherine Sungura-Dodoma)

  0 0  0 0


  0 0

  Ndege ya Shirika la Etihad ya Boeing 787-9 ikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa O.R Tambo jijini Johnnesburg.

  SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner limeanzisha safari zake mpya katika Jiji la Johnnesburg kuanzia tarehe 01 Novemba 2016 mchana kwa uzinduzi wa ndege hiyo kutoka Abu Dhabi.

  Ndege hiyo iliondoka Abu Dhabi saa 4:15 asubuhi na ilitarajiwa kuwasili saa 10:45 jioni. Pia ilitarajiwa kuondoka Jonhnnesburg 1:50 jioni na kuwasili Abu Dhabi saa 12: 10 asubuhi kesho yake.

  Ndege hiyo ya kisasa ya Etihad inayotoa huduma kwa madaraja ya kwanza na kawaida inatarajiwa kutoa huduma za kila siku katika jiji hilo…Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema, “Uamuzi wa kutumia ndege hiyo ya kisasa zaidi kwa safari za Johnnesburg umelenga kukidhi mahitaji halisi ya wateja kutokana na ongezeko la idadi ya watu wanaohitaji huduma za daraja la kwanza na huduma bora kwa wanaokwenda na kutoka nchini Afrika Kusini.
  Wasafiri wanaokwenda na wakati wanahitaji huduma nzuri, zenye ubunifu na salama, na matarajio yetu ni kutoa huduma zenye kiwango cha juu cha ubora zinazokidhi ukarimu na teknolojia ya hali ya juu ili kuifanya safari yako iwe ya kukumbukwa.”

  Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Etihad nchini Afrika Kusini aliongeza kuwa, “Kuanzishwa kwa ndege ya Boeing 787 kutaongeza maendeleo kwa kuvutia wageni wengi kutumia safari hizo. Ndege hii yenye ubora wa hali ya juu ina kila huduma ndani yake na mandhari ya kuvutia.”

  Ndege hiyo ya kisasa imeundwa ikiwa na vitu mbalimbali ndani yake vitakavyokufanya uburudike na kusafiri kwa uhuru zaidi. Kuna vituo takriban 28 kwa daraja la kwanza na kuna vituo vyenye ubora 271 kwa ajili ya daraja la kawaida.
  Kwa daraja la kwanza kuna huduma ya vitanda vyenye ukubwa wa kutosha na nafasi ya kutosha ya mtu kuburudika. Kuna vitambaa laini na vyenye kuvutia ambavyo vimezungushiwa kwenye kila kiti. Huku kukiwa na mfumo wa kielektroniki unaomwezesha mteja kusogeza kiti kwa kiwango anachotaka jambo linalompa uhuru zaidi akiwa safarini.

  Kila chumba kwenye daraja la kwanza kuna runinga kubwa ya flat screen unayoweza kutumia kwa njia ya kugusa huku ukipata huduma ya vifaa vya kudhibiti kiwango cha kelele,

  Vilevle hata kwenye daraja la kawaida kila kiti kina runinga ndogo pamoja na vifaa vya kusikilizia redio kwa wateja wanapokuwa safarini. Pia kuna viti vikubwa ambavyo vinamfanya mteja kuwa huru kuweka miguu kwa kadri anavyotaka.
  Aidha kuna mfumo unaowawezesha wateja kutumia intaneti bure huku kukiwa na mahali ambapo abiria anaweza kuchomeka USB yake ili kuchaji simu na huduma zingine za kimawasiliano. Muda wote unapokuwa kwenye ndege hiyo utaburudika kwa kupata chaneli mbalimbali ambazo zinaonekana katika ubora wa hali ya juu huku wahudumu wakitoa huduma zilizotukuka kwa wateja.

  Wahudumu wa ndege waliopo ni wabobezi kutoka vyuo vikubwa vinavyotambulika ulimwenguni kama vile Flying Nannies waliopata mafunzo Norland College nchini Uingereza kuhusuna na malezi ya watoto wanapokuwa kwenye ndege.

  Pia kuna wasimamizi wa vyakula waliobobea ambao wamefanya kazi katika hoteli kubwa na maarufu duniani huku wakiwa na mafunzo ya kuhudumia daraja la kwanza ikiwa ni pamoja na kuwa na ujuzi wa kuandaa vinywaji laini.

  Wateja wanaotumia ndege hiyo watapata fursa ya kufurahia kuona mandhari ya nje kupitia madirisha makubwa na uwapo wa hali ya hewa tulivu.

  Shirika la ndege la Etihad limekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wasafiri wake wanaotoka Afrika wanapofika kwenye mamlaka ya forodha nchini Marekani na Uwanja wa Ndege wa Abu Dhabi kukamilisha utaratibu wa wahamiaji kwa haraka.

  Utaratibu huu ukiacha Shirika la Ndege la Etihad ukanda wa ghuba, inawapa fursa wateja kukamilisha taratibu zote muhimu za uhamiaji, ushuru na forodha pamoja na kushughulikia vibali vya usalama kwa wasafiri wanapofanya safari kati ya Abu Dhabi na Marekani jambo linalowawezesha kupunguza mlolongo mrefu wanapowasili katika uwanja wa ndege wa Marekani.

  Jiji la Johnnesburg ni mji wa tisa kuhudumiwa na ndege aina ya B757-9 Dreamliner. Ndege hiyo pia inatoa huduma katika miji ya Brisbane, Düsseldorf, Perth, Riyadh, Shanghai, Singapore, Washington DC and Zurich.

  Ratiba ya ndege ya Dreamliner kutoka Abu Dhabi – Johannesburg:
  Ndege No.
  eneo
  Kuondoka
  Eneo
  Kuwasili
  Kipindi
  EY604
  Abu Dhabi
  10:15am
  Johannesburg
  4:45pm
  Daily
  EY603
  Johannesburg
  7:50pm
  Abu Dhabi
  6:10am (+1)
  Daily

  Muda wa kuondoka umeorodheshwa kulingana na muda wa eneo husika.

  0 0

   Kulia ni Mtangazaji wa luninga wa Azam Tv Charles Hillary akifanya mahojiano na Iddi Ligongo (kushoto) na Mzee Boas siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika studio ya Kilimanjaro Beltsville, Maryland,
  Kutoka kushoto ni Nambai mkazi wa DMV akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea na maswala ya utangazaji  DMV Mubelwa Bandio.

  Mtagazaji wa BBC Swahili Zuhra Yunus (kushoto) akifanya mahojiano na mkazi wa DMV Asha Hariz Siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika mgahawa wa Swahili Village.

  kushoto ni Nambai mkazi wa DMV Alawi akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea na maswala ya utangazaji  DMV Mubelwa Bandio.
   kushoto ni Nambai mkazi wa DMV Dotto akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea na maswala ya utangazaji DMV Mubelwa Bandio.
   Kushoto ni Mashaka akipata picha naa John Mbele
   kushoto ni Dotto Haruba mkazi wa DMV Alawi akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea ya maswala ua utangazaji DMV Mubelwa Bandio.
   kushoto ni Mashaka mkazi wa DMV Alawi akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea ya maswala ua utangazaji  DMV Mubelwa Bandio.
    kushoto ni Pius  mkazi wa DMV Alawi akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa siku nyingi ambaye kwa sasa yupo Azam TV Charles Hillary (kulia) siku ya Jumanne Novemba 8, 2016 ya uchaguzi wa rais wa Marekani katika Studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland, Kati ni Mtagazaji aliyobobea ya maswala ua utangazaji DMV Mubelwa Bandio.
  Kulia ni mtangazaji wa BBC Swahili akimwandaa Seif Msabaha kwa mahojiano
  Dedi Luba na Asha Hariz wakipata menyu Swahili Villege

  0 0


  H.E. PRESIDENT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
  PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  BARACK OBAMA ROAD,
  11400 DAR ES SALAAM,
  TANZANIA

  Your Excellency

  RE: CONDOLENCE MESSAGE ON THE SAD AND UNTIMELY DEMISE OF HON. SAMUEL SITTA

  It is with great shock that I have received the news of the sad and untimely demise of Hon. Samuel Sitta, who was at one time the Minister of East African Cooperation in the Government of the United Republic of Tanzania, on 7th November 2016 in the Federal Republic of Germany where he was undergoing treatment.

  On behalf of the East African Community and on my own behalf, I convey my heartfelt condolences to Your Excellency, and, through you, to: the entire bereaved family, relatives, friends and colleagues of the late Hon. Sitta; the Government, the Parliament, and; the people of the United Republic of Tanzania.

  We mourn the passing on of a distinguished son of Tanzania and East Africa who has left an indelible imprint on the history of the Community.

  Indeed, Your Excellency, the late Hon. Sitta played a critical role in the transformation of the EAC Customs Union Protocol into a Single Customs Territory, the implementation of the Common Market Protocol, and negotiations for the East African Monetary Union Protocol, which is now under implementation.

  The entire Community and I share with Your Excellency, the bereaved family and the government and people of Tanzania, the feelings of great loss at this moment of deep sorrow.

  MAY THE ALMIGHTY GOD REST HIS SOUL IN ETERNAL PEACE


  Amb. Libérat Mfumukeko
  SECRETARY GENERAL 


  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Amsons-Camel Bw. Salim A.Salim baada ya kukabidhi msaada wa Mifuko 1000 ya Seruji kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko la Ardhi la Kagera Novemba 09, 2016 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.
   Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim (kushoto) akitoa maelezo ya msaada wa mifuko 1000 ya Seruji kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) walipofika katika Ofisi yake Dar es Salaam Novemba 09, 2016.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (katikati) akipeana mkono wa shukrani na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Camel Bw. Salim A. Salim wakati wa kuwasilisha msaada wao wa mifuko 1000 ya Seruji kwa waathirika wa maafa Kagera, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Amsons-Camal Bw. Ghalib H. Ghalib.
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika zoezi la makabidhiano ya mifuko 1000 ya seruji kwa ajili ya waathirika wa maafa mkoani Kagera kutoka Kampuni ya CAMEL katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na: Geofrey Tengeneza

  Tanzania jana iliwaongoza wananchi kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wageni na washiriki wa maonesho ya utalii ya World Travel Market (WTM) yanayofanyika jijini London nchini Uingereza kutoka mataifa kadhaa duniani kusheherekea siku ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika banda hilo huku watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakikaribishwa kuja kuzitembelea nchi za jumuiya hiyo na kujionea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda huu wa Afrika.

  Sherehe hiyo iliyohudhuriwa pia na mawaziri, mabalozi, maafisa na waoneshaji kutoka nchi wanachama wa Jumuia hiyo ya Afrika Mashariki ilifanyika katika banda la Tanzania ambayo ndiyo nchi Mwenyekiti wa jumuia hiyo kwa sasa.

  Akizungumza kwa niaba ya Jumuia hiyo, Waziri wa utalii wa Uganda Prof Epharaim Kamuntu amesema nchi zinazounda Jumuia hiyo zina vivutio vya utalii vya pekee na kuwataka watalii kuzitembelea nchi hizo huku akiwahakikishia kuwa eneo hilo la Afrika ni salama kabisa kwa watalii.

  Mapema akiwakaribisha Mawaziri wa utalii na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk. Asha Rose Migiro amesema umoja na mshikamano wa nchi wanachama wa Jumuia hiyo umezidi kuimarika na kwamba miundo mbinu ya utalii katika nchi zote wanachma imeboreshwa sana na hivyo kuwafanya watalii kufurahia safari zao katika eneo hili la Afrika.

  Maonesho ya WTM ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani baada ya yale ya ITB ya Ujerumani hufanyika kila mwaka mwezi Novemba nchini Uingereza ambapo mwaka huu yameanza Novemba 7 na yanatarajia kumalizika leo tarehe Novemba 9, 2016.

  Katika maonesho ya mwaka huu makampuni 42 kutoka sekta binafsi na taasisi nne (4) za Serikali yanashiriki maonesho hayo chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania. Taasisi hizo za Serikali ni Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Bonde la Ngorngoro (NCAA) Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) na Bodi ya Utalii Tanzani (TTB).
  Balozi wa Tz nchini Uingereza Dk.Asha Rose Migiro akiwakaribisha mawaziri na mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki kwenye banda la Tanzania wakati wa sherehe ya Jumuiya hiyo iliyofanyika jana katika banda la Tanzania.
  Waziri wa utalii wa Uganda Prof Epharaim Kamuntu akitoa tamko (press statement) kwa niaba ya nchi zote za jumuiya Africa ili kuvutia watalii waweze kutembelea nchi za Afrika mashariki.
  Washiriki toka sekta binafsi wakiwa kwenye maonesho ya utalii ya World Travel Market (WTM) katika banda la Tanzania chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania -TTB.

  0 0

  NA DAUDI MANONGI, MAELEZO.

  Novemba 5 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli ametimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani akiwa na dhamira mpya ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Mara kadhaa Rais Magufuli amekuwa akisisitiza umuhimu wa viwanda ambapo anasema vinaweza kutengeneza ajira kwa watanzania waliojiajiri wakiwemo vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.Katika kutimiza azma iyo aliagiza mifuko ya Hifadhi ya Jamii ijikite zaidi kwenye uwekezaji wa viwanda ili kuunga mkono lengo la Serikali.

  Katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi.Makubaliano haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es Salaam.

  Aidha katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na kufunguliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Pamoja na kiwanda cha sasa PPF itajenga kiwanda kipya cha kisasa ambacho kitakuwa kikisindika ngozi na kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi kwa kutumia mashine za kisasa na teknolojia ya hali ya juu na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ya viatu nchini na kuongeza pato la Taifa.

  Akizungumza wakati wa kutiwa saini mkataba wa makubaliano Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ni utekelezaji wa lengo la Serikali la kuwa na uchumi wa viwanda na faida kubwa kwa nchi kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini kwa ajili ya soko la ndani na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika kununua malighafi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

  Vile vile kiwanda hicho kipya kitatoa ajira kwa watanzania lakini pia PPF itanufaika kwa faida itokanayo na uwekezaji pamoja na kupata wananchama wapya watakaojiunga na mfuko huo.

  Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uzalishaji katika kiwanda kipya cha uchakataji ngozi unatarajiwa kuanza mwaka 2018 na kwamba katika kipindi ambacho ujenzi wa kiwanda kipya utakuwa unaendelea kile cha zamani kitaboreshwa ili kuongeza zaidi ufanisi wa uzalishaji.

  Katika hatua nyingine mfuko wa PPF umeanza hatua za awali za kuwekeza katika kiwanda cha Sukari eneo la Mkulazi lililopo kilometa 195 kutoka Manispaa ya Morogoro na km 75 kutoka Ubena-Zomozi barabara kuu ya Dar es Salaam na Morogoro ambapo uwekezaji huo utafanyika kwa ubia kati ya PPF na NSSF kwenye eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 63000 ambapo tayari kampuni ya pamoja imeshaanzishwa azma hiyo.

  Kiuchumi eneo la Mkulazi liko karibu na Reli ya kati kwenye kituo cha Ngerengere na lipo karibu na Reli ya TAZARA kupitia kituo cha kidunda hivyo uwekezaji katika eneo hilo utafanya usafirishaji wa malighai na bidhaa kuwa rahisi.

  Kiwanda hicho kitazalisha zaidi ya tani 200,000 za Sukari kwa mwaka lakini pia kitatoa ajira za moja kwa moja na ajira shirikishi kwa watanzania zaidi ya 100000 na hivyo kutimiza lengo la Rais na Serikali yake katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na kuongeza pato la Taifa.

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uwekezaji huu utafanyika katika awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha uzalishaji wa Miwa na ujenzi wa kiwanda cha Sukari na awamu ya pili utahusisha kilimo cha nafaka kama vile Mahindi,Mpunga na Mtama.

  PPF itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kufanikisha azma yake ya Tanzania ya viwanda kwa kuwekeza katika maeneo yenye tija kwa mfuko ili kukuza uwekezaji na tija kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

  Katika kuzidi kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano na falsafa yake ya “Hapa kazi tu” PPF itafanya uwekezaji wa ujenzi wa jengo la kiwanda kwenye kiwanda cha nguo cha Touku kilichopo eneo la Mabibo katika ukanda maalumu wa kiuchumi wa Benjamin Mkapa ambapo kiwanda hiki huzalisha nguo zenye ubora kwa ajiri ya soko la Marekani kupitia mpango wa ukuzaji fursa za kiuchumi Afrika AGOA(African Growth and Opportunity Act uku uwekezaji wa Jengo la kiwanda utapanua wigo wa ajira kwa watanzania kutoka 1600 waliopo sasa mpaka kufikia ajira 7000.

  Mfuko wa PPF unaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwafikia watanzania wajasiriamali ili kuboresha biashara na maisha yao.

  Sanjari na hilo tayari PPF imeanzisha mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama Wote Scheme ambao unawalenga wanachama waliojiajiri wenyewe katika sekta isiyo rasmi ambao kwa mujibu wa takwimu za kitaifa sekta hiyo inachukua zaidi ya asilimia 90 ya nguvu kazi ya Taifa.

  Mfuko huu unawalenga watu waliojiajiri katika makundi ama mtu mmoja wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, madereva wa daladala, bodaboda ,mabasi,Teksi,Mama lishe,Wajasiriamali mbalimbali wenye maduka na biashara nyingine pamoja na vikundi vya Vikoba.

  Kwa kupitia mfumo wa wote Scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata bima ya afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni ya uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.

  Kupitia mfumo wa wote scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata bima ya afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni ya uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.

  Kupitia mfumo wa wote scheme mwanachama anaweza kuchangia kiwango kisichopungua elfu ishirini kwa mwezi au zaidi na mfumo huu ni rahisi sana ambapo wanachama wanaweza kulipa michango yao kwa simu ya mkononi kupitia mifumo kama vile M-pesa,Airtel Money,Tigo Pesa popote pale walipo eneo lao la kazi bila hata kufika ofisi za PPF.

  Pamoja na hayo tunayaomba makundi mbalimbali ya wajasiriamali walioko katika sekta isiyo rasmi kujiunga na mfumo huu kwa faida ya maisha yao ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa katika mfumo huu.

  Pamoja na Mfuko wa PPF kusajili wanachama kukusanya michango kuwekeza na kulipa mafao imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za kijamii kama vile afya,elimu na kuchangia kwenye maendeleo ya jamii katika kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwenye sekta ya elimu mfuko wa PPF umekuwa mstari wa mbele kuchangia changamoto ya upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari kitaifa.

  PPF imeendelea kuunga mkono mpango wa serikali katika kutatua changamoto ya madawati kwenye shule mbalimbali ambapo mfuko umechangia shilingi milioni 200 katika kufanikisha mpango huo uku lengo kuu la mfuko wa PPF likiwa ni kuhakikisha wanafunzi hawasomi wakiwa wamekaa chini kwani ndio nguvu kazi ya Taifa la Kesho na ni wanachama watarajiwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo PPF.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akipokea vifaa vya michezo toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Star Times Tanzania Bw. Leo 9 November, 2016 katika ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (aliyekaa katikati mbele) akiongea na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya michezo toka kwa Kampuni ya Star Times Tanzania leo 9 November, 2016 katika ukumbi wa Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Leo.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

  0 0


   Msajili wa VVyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) na Chama cha Jahazi Asilia. Kulia ni Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Monica Mnanka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habariwakati akimkaribisha msajili wa vyama kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Msaji Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Msajili wa Vyama, Jaji Francis Mutungi.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992, amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kuanzia leo hii.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi Jaji Mutungi alivitaja Vyama alivyovifuta kuwa ni Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), kilichopata usajili wake Novemba 15, 2001 kilichokuwa kikiongozwa na James Mapalala kama Mwenyekiti wa Taifa na Mwaka Lameck Mgimwa kama Katibu Mkuu.

  Chama kingine alichokifutia usajili wa kudumu ni Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo)  kilichopata usajili Machi 4, 2003 kilichokuwa kikiongozwa na Peter Kuga Mziray kama Rais Mtendaji Taifa na Nziamwe Samwel kama Katibu Mkuu.

  Jaji Mutungi alikita chama kingine alichokifuta kuwa ni  Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kikiongozwa Kasimu Bakari Ally kama Mwenyekiti wa Taifa na Mtumweni Jabir Seif kama Katibu Mkuu ambacho kilipata usajili wa kudumu Novemba 17, 2004.

  Mutungi alisema vyama hivyo vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ambapo kila chama klipewa taarifa ya nia ya Msajili wa Vyama vya siasa kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kueleza kwanini kisifutwe ambapo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa havikukiuka sheria na bado vinavyo sifa za usajili wa kudumu.

older | 1 | .... | 1035 | 1036 | (Page 1037) | 1038 | 1039 | .... | 1897 | newer