Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1030 | 1031 | (Page 1032) | 1033 | 1034 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

  Wanawake mkoani Mwanza wamehimizwa kuhudhuria Kongamano la Sauti ya Mwanamke litakalowakutanisha baadhi ya wanawake waliofanikiwa kiuchumi nchini, ili kujifunza na kuhamasika katika kujikwamua kiuchumi.

  Mwandaaji wa Kongamano hilo, Mboni Masimba ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha runinga cha The Mboni Show, amesema kongamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii na kwa kujiamini zaidi bila kuongopa vikwazo vya kibiashara.

  “Njoo ujifunze nguvu ya mwanamke katika biashara, kushinda vikwazo, kujiamini, kufanya kazi kwa bidii, kutoogopa hatari za kibiashara pamoja na kuwa na malengo ya muda mrefu ambapo wahamasishaji na wafundaji mbalimbali watakuwepo”. Amesema Masimba na kuongeza kwamba pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa Isha Mashauzi na Zarry Edosha pamoja na vichekesho kutoka kwa Katarina Wa Karatu.

  Aidha Masimba amesema tayari tiketi za kongamano hilo litakalofanyika tarehe sita mwezi huu kwenye ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza zimeanza kuuzwa kwa shilingi elfu arobaini katika maeneo mbalimbali ikiwemo Gold Crest Hotel, TSN Super Market Rock City Mall, Flora Salon, Kayvies Beaty Parlour Magnum Hotel Ghana, Idda Garments Ghana, Diamond Bar Kona ya Bwiru pamoja Bladict Classic Wear mtaa wa Uhuru Dampo.

  Bonyeza HAPA Kwa Taarifa Zaidi.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwake wakati wa kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3, 2016.
  ya12
  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiendelea na kiako cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3, 2016.Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO
  ya
  Baadhi ya wabunge na mawaziri wakiwasili katika viwanja vya Bunge kuhudhulia kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3,2016.
  ya1
  ya2
  ya3
  ya4
  ya5
  ya6
  ya7
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akiingia Bungeni kuongoza katika kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3,2016.
  ya8
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akiongoza   kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3,2016.
  ya9
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3, 2016.
  ya10
  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa  (kushoto) pamoja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika kikao cha tatu cha Mkutano wa tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma Novemba 3,2016.


  0 0

  Kaimu Kamishna  Utawala  na  Fedha  wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna Abbas Irovya,  akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara ya Uhamiaji kujadili shughuli zinazofanywa na idara hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na nchi za Afrika Mashariki ikiwemo  suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida)
  uv3
   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza  shughuli mbalimbali zinazofanywa  ikiwemo utoaji wa pasi za kusafiria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ni  Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima. Mkutano huo umefanyika  jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida).
  uv
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania, Makongoro Nyerere(kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza  shughuli zinazofanywa na idara  hiyo . Wengine ni Wabunge  Shyrose Bhanji(kulia) na   Angela Kizigha(kushoto). Mkutano huo umefanyika   jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida)
  uv5
   
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza  shughuli zinazofanywa na idara .Kulia ni Mbunge Makongoro Nyerere  na Kushoto ni  Angela Kizigha.Mkutano huo umefanyika   jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida)
  uv1
  Kaimu Kamishna  Jenerali   wa  Uhamiaji, Victoria Lembeli  akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara  hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza shughuli  mbalimbali zinazofanywa  na idara  hiyo ikiwemo suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.(Picha na Abubakari Akida.
  uv4
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli(wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge  wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania baada ya kutembelea Makao Makuu ya Idara hiyo katika kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na idara .Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Makongoro Nyerere.Ziara hiyo imefanyika   jijini Dar es Salaam.(Picha na Abubakari Akida)

  0 0


  Benjamin Sawe-MAELEZO

  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumefanyika jitahada kubwa za kuhakikisha inafufua mashirika yalifikia hali mbaya na kushindwa kutoa huduma ili hatimaye yaanze upya kutoa mchango wa ujenzi wa uchumi nchi. Mojawapo wa Mashirika hayo ni pamoja na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ambapo kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani lilikuwa na Ndege mmoja tu.

  Hatua hiyo ya Rais Magufuli kuamua kununua Ndege mbili aina ya Bombadier Q400 zimesaidia kuimarisha Kampuni hiyo na kurejesha nembo ya Twiga iliyoanza kupotea. Licha ya juhudi hizo na kazi mkubwa aliyoifanya Rais Magufuli ya kutimiza ahadi yake ya kuanza kuijenga upya Kampuni hiyo, wapo baadhi ya wananchi wachache ambavyo wamewakuwa hawana shukurani na kuanza kubeza jitihada hizo.

  Ni vema wakumbe ule usemi unaotumiwa na baadhi ya watu kuwa “ Hata mbuyu ulianza kama mchicha” .Kauli hii inadhihirisha kuwa kila jambo uwa na mwanzo wake kwani tokana na dhihaka za baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibeza juhudi za Mhe. Rais Magufuli. Ununuzi wa Ndege hizo umesaidia kumeimarisha huduma za usafiri wa anga na kuongeza ushindani katika utoaji wa huduma za anga hapa nchini kati yake na kampuni binafsi za ndege zinazotoa huduma hiyo kwa sasa

  Azma hiyo ya Serikali ya kununua ndege mpya imetimiza ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli wa kulifufua tena Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kulipatia mtaji ili lianze upya kutoa huduma hiyo kwa Watanzania. Akizindua ndege hizo Rais Magufuli alisema kuwa ,ndege hizo zina sifa ya matumizi madogo ya mafuta na ni suluhisho la kupanda kwa bei ya usafiri wa anga nchini na pia zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini.

  “Ndege hizi zinatumia wastani wa mafuta ya shilingi milioni moja kutoka hapa hadi Songea, wakati ndege za Jet zinatumia mafuta ya shilingi milioni 28.1 kwa safari kama hiyo,” anasema Mheshimiwa Rais. Ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege.

  “Tunataka watalii wanaokuja nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine” anasema Rais Magufuli. Mbali na kuleta ndege hizo, yapo mambo mengi makubwa ambayo Rais Magufuli ameanza kuyatekeleza, aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, hatua ambayo imewavutia watu wengi ndani na nje ya nchi.

  Aidha WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo alizindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma ili uweze kupokea ndege kubwa za mizigo, abiria na viongozi wa kitaifa na kimataifa. Uzinduzi huo ni miongoni mwa maandalizi ya kutimiza azma ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Tanzania. Ujenzi huo umegharimu Sh bilioni 11.5 ambazo ni fedha za ndani na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma, ikiwemo ndege ambazo zimenunuliwa na serikali.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anasema, uzinduzi huo hautaathiri mchakato wa kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Msalato. “Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato uko pale pale,” anasema Rugimbana na kuongeza kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeamua kufanya upanuzi wa uwanja huo ili ndege kubwa zitue mkoani humo.

  ‘’Wizara ya Ujenzi imeamua kufanya upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Dodoma ili ndege kubwa ziweze kutua na sisi tunamshukuru Rais kwa kutupa uwanja huo kwani utazidi kufungua fursa katika mkoa wetu,” anaeleza Rugimbana.

  0 0


  0 0

  WAKATI Bunge la Tanzania wiki hii linatarajiwa kujadili na kupitisha muswada wa habari, Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) limehadharisha juu ya uwapo wa sheria zinazotishia uhuru wa vyombo vya habari.

  Akizungumza katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay alisema katika utekelezaji wa maendeleo endelevu sekta ya habari ni muhimu na hivyo watendaji wake wanatakiwa kuwekewa mazingira huru ya kiutendaji.

  Serikali ya Tanzania imepeleka muswada wa habari ambao unalalamikiwa na wadau wa habari kwamba haukupatiwa muda wa kutosha wa kujadiliwa na kuondolewa kwa vipengele ambavyo vinawanyima waandishi wa habari uwezo wa kuandika.
  Mkuu wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Aidha ndani ya muswada huo imeelezwa na Jukwaa la Wahariri kwamba kuna vipengele ambavyo vinakwamisha umahiri wa uandishi na uchunguzi kama kufutiwa kwa leseni na kuuzwa kwa mitambo kutokana na makosa mbalimbali ambayo yamegeuzwa ya jinai.

  Aidha wadau hao wanasema kwamba serikali imejitengenezea nafasi ya kuwa na nguvu kubwa ya kudhibiti habari kupitia Kurugenzi ya Maelezo na Waziri mwenyewe huku Bodi iliyopangwa kuwa huru ikionekana kwamba haina nguvu zakutosha.

  Akizungumza haja ya mazingira rafiki Legay alisisitiza kuwaTaifa linastahili kuhakikisha kwamba kumewekwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa habari na kwamba kila mwananchi anapata haki yake ya kupata, kusambaza habari kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na sheria zinazohusu habari za taifa.
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza akifungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Alisema ingawa haki ya kupata habari imeelezwa waziwazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vifungu 18 na 21 mambo yanayojitokeza sasa katika sheria za habari nchini Tanzania yanatishia haki hiyo, kutokana na sheria hizo kuonekana kubana uchakataji wa habari. Akitolea mfano wa sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.

  Alisema katika mkakati wa utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia kuna mpango mkakati wa kulinda waandishi wa habari na upatikanaji wa habari kama ilivyoelezwa katika lengo namba 16, kifungu kidogo cha 10.Alisema kwa sasa dunia inakabiliwa na tishio kubwa la upatikanaji wa habari kutokana na vitisho vinavyowekwa kwa waandishi wa habari ikiwa na pamoja na kuuawa, kutiwa kizuini au kupotea bila kujulikana.

  Alisema katika muongo mmoja uliopita waandishi 827 waliuawa na kwamba ni asilimia 7 tu ya mauaji hayo yalipatiwa ufumbuzi. Aidha alisema mwaka jana ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari, huku waandishi 16 pekee wakiuawa katika bara la Afrika.Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa akijadili rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Alisema kitendo cha kuwadhibiti waandishi wa habari kunaashiria udhibiti wa upatikanaji wa habari huru ambao ndio msingi wa demokrasia na maendeleo ya jamii.Aliitaka jamii kuhakikisha kwamba inakaa pamoja na kuona haja ya kulinda uhuru wa habari ikiwa na pamoja na kuwalinda wachakataji habari ili kila mtu anayetaka kupata habari aweze kuipata na kuitumia kwa maendeleo yake, jamii na taifa.

  Akimkariri Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova, mkuu huyo wa mawasiliano alisema kwamba ukatili na vitendo vinavyoshabihiana navyo dhidi ya waandishi wa habari ni kinyume na uhuru na haki ya upatikanaji wa habari na wanaofanya mambo hayo wanatishia utawala bora wa kisheria na kusababisha utoaji habari usiokamili kwa hofu ya udhibiti na matokeo yake jamii nzima inapotoka na kuhangaika. Leo hii tunahitaji dhamira mpya ya kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira salama na rafiki kwa waandishi wa habari.

  UNESCO ni mdau mkubwa wa habari nchini Tanzania na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ilikumbushia kazi inayofanya pamoja na wadau wengine wa habari wakiongozwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition kutengeneza mpango kazi wa ushawishi wa namna bora ya kuchakata na kufanyakazi ya uandishi wa habari nchini Tanzania.Mdau wa tasnia ya habari, Kenneth Simbaya akiwasilisha fursa na changamoto walizokumbana nazo wakati wa uandaaji wa rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  Kutokana na mkakati huo mwaka jana kuliundwa kikosi kazi cha kuangalia usalama wa waandishi wa habari na taarifa inatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa namna bora ya kuwawezesha waandishi wa habari kufanyakazi kwa usalama.

  Naye msemaji wa serikali ya Tanzania akizungumza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel katika tukio hilo alitoa wito kwa taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za sheria na vyombo vya habari kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanyia kazi waandishi wa habari ni salama na haki za upatikanaji wa habari haudhibitiwi.

  Alisema ili kuwezesha hali hiyo serikali imepeleka muswada wa waandishi wa habari bungeni na pia ikiwa kama moja ya nchi iliotia saini mikataba ya kimataifa kuhusu upatikanaji wa habari serikali itafanyakazi kwa pamoja na wadau kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanapata mazingira rafiki na salama ya kufanyia kazi.Mmoja wadau wa masuala ya sheria akizungumza jambo katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Mwanasheria kutoka Nola, James Marenga akifafanua jambo wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi (kushoto) akiwa na wadau wa tasnia ya habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Wadau wa tasnia ya habari na masuala ya Sheria walioshiriki kwenye kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.Washiriki wakitazama moja ya video ya shuhuda inayozungumzia usalama wa waandishi wa habari wakati wa uchaguzi wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (kushoto), akisalimiana na mkazi wa Bugururuni, Awadh Selemani, Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko katika kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana kwa zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.
  Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert Louis (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa timu ya mauzo, wakizungumza na baadhi ya wakazi wa Bugururu, Dar es Salaam, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.
  Mkuu wa Masoko wa Zantel, Gasper Mbowa (katikati) na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Zadok Prescott (kulia), wakiwafahamisha wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, Dar es Salaam, Yassin Hassani (kushoto) na Abdallah Issa, baadhi ya huduma za kampuni hiyo katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma zao karibu na wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.

  Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert Louis (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiti njia katika mtaa wa Kongo, Dar es Salaam jana, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania.
  Maofisa wa Zantel wakizungumza na wachuuzi wa matunda karibu ya soko la buguruni, Dar es Salaam, katika moja ya kampeni za masoko kufikisha huduma na bidhaa zao karibu kwa wateja. Zantel imemaliza hivi karibuni ukarabati mkubwa wa mtandao wake wa 3G na 4G wenye lengo la kuboresha ubora wa huduma za intaneti na sauti hivyo kupatikana zaidi za asimilia 85 ya Tanzania. Kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya, Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit Janin na Mkuu wa Mauzo, Herbert Louis.
  Maofisa wa ngazi ya juu wa Zantel wakibadilishana mawazo karibu na soko la Buguruni, Dar es Salaam walipokwenda pamoja na timu ya mauzo kuzungumza na wateja na wakazi wa maeneo hayo kuhusu huduma za Zantel na jjnsi ilivyojipanga upya kuwaletea huduma bora. Kutoka kushoto; Ofisa Mtendaji Mkuu, Benoit Janin, Kaimu CEO, Zadok Prescott, Mkuu wa Masoko, Gasper Mboya na Mkuu wa Mauzo, Herbert Louis.

  0 0

  Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.

  Novemba 5, mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii.

  Katika kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa upande wake umesaidia Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia PSPF kuongezeka kutoka 394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa agizo lake. 

  Hatua hii ya PSPF imelenga kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanufaika na huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma za Bima za afya wakati wa kampeni na baada ya kuingia madarakani.

  Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa na Costantina Martin kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo hii inajumuisha Watanzania walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi nchini. 

  Kundi hili kubwa lilikuwa limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii , lakini baada ya Mhe. Rais Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake hivi sasa mwamko wa kujiunga na hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi kuchangia na kujiunga katika Bima ya Afya.
   
  Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za afya kwa watanzania wengi ambao wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo kujenga jamii yenye afya bora inayochangia katika ujenzi wa nchi.

  Chini ya makubaliano yanawasaidia wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya tiba kupitia NHIF kwa gharama ya shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali mbalimbali ziliingia makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.Mpango huo wa PSPF unaounga mkono juhudi za Rais Magufuli za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanapata huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa gharama nafuu.

  Hivi sasa huduma hiyo ya PSPF kuwadhamini wananchama wake kwa ajili ya kupata matibabu imesaidia watanzania wengi sana kunufaika na huduma hii husasan katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli.Akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Rais Magufuli alisema kuwa dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umaskini linakwenda sambamba na kuwa na wananchi wenye afya bora.

  Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kuhamasisha wananchi wengi wanajiunga na Bima ya Afya.Katika kutekeleza hilo PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) imeshawafikia Watanzania 2,710 walio katika sekta isiyo rasmi kuanza kunufaika na huduma za Afya kupitia PSPF.Mbali na sekta ya afya , katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli PSPF kwa upande wake imesaidia kuhakikisha kuwa Tanznaia inakuwa Nchi ya Viwanda kwa lengo la kutoa ajira kwa Watanzania walio wengi.

  Viwanda hivyo ambavyo PSPF imewekeza ni pamoja na 21st Century cha Morogoro, Saruji Tanga.Martin ameongeza kuwa hivi sasa PSPF imejipanga kuwekeza katika Kituo cha Biashara cha Kurasini (Kurasini Logistic Center) kwa lengo la kuchochea uwekezaji wa viwanda na kutoa ajira kwa wananchi.

  Viwanda vingine ambavyo PSPF imejipanga kuwekeza ni kile cha Nguo cha Urafiki, Morogoro Canvas Mill na Kiwanda cha Viatu Karanga kilichopo Moshi.Hatua hiyo iliyoanza kutekelezwa na PSPF ni sehemu utekelezaji hotuba ya Mhe. Rais Magufuli wakati anafungua rasmi Bunge 11 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka jana ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaweka mkazo katika ujenzi wa viwanda ili mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote hapa nchini.

  PSPF ilianzishwa kwa sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma namba 2 ya mwaka 199 . sura ya 371 na inatoa huduma za Hifadhi ya Jamii katika Mapngo wa lazimana wa hiyari.

  0 0

  Jeshi la Polisi nchini, katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika, limeendelea na operesheni za kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya usalama barabarani katika mikoa yote ili kudhibiti vitendo vya uhalifu na wahalifu. Katika operesheni hizo, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha na katika baadhi ya mikoa, wananchi wameweza kusalimisha silaha kwa hiari katika vituo vya Polisi.

  Operesheni hizi ni endelevu, na ili tuweze kufanikiwa zaidi katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususani katika kipindi hiki tunapoelekea mwisho wa mwaka, wananchi wanatakiwa kuwa makini na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu haraka kwa kutumia namba za bure 111 na 112 pindi wanapowatilia shaka watu wasiowajua katika maeneo yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

  Kwa wamiliki wa maduka makubwa, hoteli na maduka ya kufanyia miamala ya fedha kwa njia ya simu waangalie namna ya kuweka vifaa maalumu vyenye uwezo wa kurekodi mienendo ya watu wanaoingia na kutoka ama kufuata huduma katika maeneo yao ya biashara.

  Pia, wananchi katika makazi yao waimarishe ulinzi kwa kutumia mpango wa ulinzi jirani kwa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kubadilishana taarifa za hali ya usalama ili kuhakikisha mitaa yao inakuwa salama wakati wote.

  Aidha, Jeshi la Polisi nchini linawataka madereva wa vyombo vya moto kuheshimu na kutii sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na kuokoa maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara. Jeshi la polisi nchini, litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, bila woga ama upendeleo katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika.

  Imetolewa na:
  Advera John Bulimba - Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
  Msemaji wa Jeshi la Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0

  Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa amri ya  kukamatwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kufika kusikiliza kesi yake bila ruhusa.

  Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.

  Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa jana kutajwa lakini mshtakiwa wa nne Lissu hakuwepo mahakamani.

  Hata hivyo, alijitokeza mdhamini wake mmoja kati ya wawili Robart Katula kudai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza.

  Hakimu alihoji kwa nini mshtakiwa amesafiri na kuacha kuhudhuria kesi yake bila kuomba kibali cha mahakama yake.

  "Mshtakiwa Lissu anafanya dharau  kila wakati inapopangwa kesi yake mahakamani anashindwa kuhudhuria bila kutoa sababu ama kuomba ruhusa ya mahakama... kama asingekuwa nje kwa dhamana angefanyaje? angetumia busara kuomba ruhusa" alihoji na kuongeza kuwa.

  "Wadhamini wa mshtakiwa wapelekewe wito wa mahakama waje kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kama walivyoahidi kwenye hati ya dhamana ya maneno ya Sh. milioni 10 kila mmoja" alisema Hakimu Simba.

  Hata hivyo, Wakili wa Serikali Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa.

  Hakimu Simba alikubali ombi la Jamhuri na kutoa amri ya kukamatwa mshtakiwa na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba 21, mwaka huu kujieleza kwa nini wasilipe fungu la dhamana dhidi ya mshtakiwa kwa kushindwa kuhudhuria kesi yake.
  Mbali na Lissu, washtakiwa wengine ni, Wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

  Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu,  Dar es Salaam, Lisu na wenzake  walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

  Pia Lissu na wenzake walidaiwa  Januari 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa nia ya kuleta chuki na uchochezi  kati ya wananchi na mamlaka halali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye uchochezi.

  Aidha, Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar   wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

  Washtakiwa walikana mashtaka hayo kwa nyakati tofauti na wako nje kwa dhamana.

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Abdullah Al Maadadi ofisini kwake na kuzungumza kuhusu masuala ya sekta ya afya(Picha na Wizara ya Afya).

  0 0

  Na: Frank Shija & Daud Manongi, MAELEZO.

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufu la kufikisha umeme kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product kilichopo Mwandege mkoani Pwani.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Makao Makuu, Leila Muhaji amesema kuwa agizo hilo limeshaanza kutekelezwa katika hatua mbalimbali na kuahidi kuwa litakamilika kwa wakati.

  Muhaji amaesema kuwa agizo linapotolewa na Mhe. Rais kinachobaki ni utekelezaji tu, hivyokufuatia agizo hilo Tanesco wameanza kufanya utekelezaji kwa kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha wanakamilisha kulinga na wakati kama agizo linavyosema.

  “Utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais unaendelea na hadi kufikia mwezi Desemba tutakuwa tumefikisha umeme katika kiwanda hicho”. Alisema Bi. Muhaja.Aidha alitumia fursa kutoa rai kwa uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji punde umeme utakapofika kiwandani hapo ili kuongeza uzalishaji.

  Kwa upande wake Meneja Ushirikiano wa Jamii wa Kiwanda cha Bakhressa Food Product Hussein Sufian Ally amesema kuwa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuona umuhimu wa kupelekewa umeme kiwandani hapo.

  Aliongeza kuwa utekelezwaji wa agizo hilo utakapo kamilika utasaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama ambazo kwa sasa zinachangiwa na matumizi ya Jenereta katika kuendeshea uzalishaji wa Kiwanda hicho.

  Utekelezaji huu umefutia agizo la Rais alilolitoa tarehe 06/10/2016 wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product ambapo alimuagiza meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani kuhakikisha ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika kiwandani hapo.

  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzazi wa mpango wakati wa kuhitimisha mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group uliofanyika jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa GFF Dkt. Christopher Elias akiongea na wadau pamoja na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu ushiriki wao katika kuchangia maendeleo ya uzazi wa mpango wakati wa  kuhitimisha mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.Picha Na Ally Daud-MAELEZO.


  Na Ally Daud-MAELEZO 

  Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya ya mwaka 2007 inavyosema. 

  Hayo yamesemwa na Waziri Ummy Mwalimu(Mb) hivi karibuni wakati akifungua mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group.

  “Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya yam waka 2007 inavyosema” alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amesema kuwa mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na hususani katika ardhi ya Tanzania hii ni kutokana na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika eneo hili la uzazi wa mpango .

  Waziri Ummy amesema kuwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la bajeti katika eneo la uzazi wa mpango na kupunguza hali utegemezi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wahusani,kuimarisha mìfumo ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba za uzazi wa mpango hapa nchini

  Mbali na hayo Waziri Ummy alieleza kuwa katika mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi mwa nchi kumekuwa na ongezeko la uelewa na utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango kama vile mkoa wa Mara kuna ongezeko la utumiaji kutoka asilimia 10 hadi asilimia 29 kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 na katika mkoa wa kagera kumekuwa na ongezeko kutoka asilimia 24 hadi asilimia 39.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya uzazi wa mpango Dkt.Babatunde alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya nchi yetu katika kuhakikisha huduma hii inaimarika.

  Mkutano huo wa siku tano ulioanza Oktoba 31 hadi Novemba 4 mwaka huu unahudhuriwa na wajumbe na wadau kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwa na lengo la kujadili fursa mbalimbali na changamoto zilizopo katika eneo la afya ya uzazi wa mpango duniani.

  0 0

  Na Eliphace Marwa - Maelezo

  Ni mwaka mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani na kutekeleza kwa vitendo moja ya ahadi alizozitoa Mgombea Urais wakati ule, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Mafisadi.
   
  Mahakama ambayo imeanza miezi michache iliyopita inaleta matumaini kwa watanzania hasa wanaipenda nchi yao wakiwa na uzalendo na fikira za kiutaifa. Katika ahadi za TANU, baadae CCM imetamkwa wazi kuwa Rushwa ni adui wa Haki, Sitapokea wala Kutoa Rushwa.

  Rais John Pombe Magufuli anatekeleza kwa vitendo anachokiahidi. Leo naomba nizungumzie utekelezaji wa ahadi yake ya kuanzishwa kwa mahakama maalum ya kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa nchi yetu.

  Ni dhahiri kuwa Dkt. Magufuli anafuata nyayo za muasisi wa Taifa letu, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alithubutu kukemea na kuwaadhibu viongozi wote wala rushwa.

  Mwalimu Nyerere alichukia sana rushwa na alichukua hatua kali sana kwawala rushwa wote bila kujali nyadhifa zao au uwezo wao wa kifedha kwani nakumbuka kuna waziri wake mmoja alihukumiwa kifungo na viboko baada ya kupatikana na hatia ya kula rushwa .

  Watumishi wa umma, waliohusika na ufisadi walichukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufungwa jela na kufilisiwa mali zao na hiyo ilipunguza sana rushwa na ifisadi serikalini. Mwalimu aliamini kwamba mtu hawezi kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja na alikuwa sahihi kabisa. Kitendo cha kuruhusu wafanyabiashara kuingia kwenye siasa, na viongozi kuruhusiwa kufanya biashara ndio chanzo cha wizi na ufisadi wa mali na fedha za umma.

  Katika hotuba ya kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma Novemba 20,2015, Rais Magufuli jambo moja alilolisitiza na kulisemea kwa nguvu ni juu ya ahadi yake wakati wa kampeni ya mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

  “Sikufanya hivyo kwa sababu nilitaka tu kuwarubuni wananchi ili wanipe kura zao na kunifanya kuwa Rais wao. Nililiongea jambo hili kwa dhati kabisa, na nilichokisema na kuwaahidi wananchi ndicho hasa nilichokikusudia”, alisema Dkt. Magufuli.

  Ni kweli kuwa wananchi wanachukia sana rushwa na ufisadi, na wamechoshwa na vitendo hivyo na hata yeye pia anachukia rushwa na ufisadi na wala hafurahishwi kabisa na vitendo vya rushwa na ufisadi vinavyoendelea hapa nchini kwani vitendo hivyo vinawanyima haki wananchi na kuitia hasara serikali kwa mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kujenga miradi ya maendeleo..

  Rais Magufuli aliongeza kuwa Chama chake, Chama cha Mapinduzi, kimejengwa katika misingi ya kukataa rushwa na ufisadi na ndiyo maana moja ya Imani kuu za CCM ni ile isemayo, “Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa” na hivyo Mtanzania mwaminifu kwa imani yake hatakuwa na kigugumizi katika kuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa na ufisadi.

  Rais Magufuli alimnukuu Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa aliwahi kuifananisha rushwa na ufisadi ‘Kama Adui Mkubwa wa Watu’.

  Akiongea Bungeni Mei 1960, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo kuhusu rushwa, “Rushwa [na ufisadi] havina budi kushughulikiwa bila huruma kwa sababu naamini wakati wa Amani rushwa na ufisadi ni adui mkubwa kwa ustawi wa watu kuliko vita.”

  Haya ni maneno makali ya mtu na kiongozi aliyeichukia na kuikemea rushwa katika maisha yake yote ya uongozi. Ni maneno yanayotukumbusha tu nini kinaweza kikatutokea kama taifa endapo tutaendekeza rushwa na ufisadi. Chuki za wananchi dhidi ya rushwa na ufisadi ni dhahiri. Watanzania wamechoka kabisa, wamechoka sana, hawako tayari kuvumilia serikali inayoonea haya rushwa na kulea mafisadi.

  “Nimewaahidi wananchi, na nataka niirejee ahadi yangu kwao mbele ya Bunge lako tukufu, kwamba nitapambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi na bila haya yoyote na Dawa ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua majipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine, hivyo ninaomba Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote mniombee na mniunge mkono wakati natumbua majipu haya”, aliongeza Rais Magufuli.

  Aidha, katika siku ya kilele cha Wiki ya Mwaka Mpya wa Mahakama Jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu, Rais Magufuli alimtakia Jaji Mkuu, Othman Chande kutosubiri Bunge kupitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi, badala yake mahakama hiyo ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

  Alisema kuchelewesha kuanza kwa mahakama hiyo kunatoa mwanya kwa mafisadi kuendelea kuangamiza nchi na kuifanya kuwa masikini wakati ina rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kuiendesha nchi bila kutegemea fedha za wafadhili.

  Rais Magufuli alisisitiza umuhimu wa uanzishwaji wa mahakama hiyo ambayo alitaka ifanye kazi ndani ya mahakama kuu kama zilivyo Mahakama za Ardhi na Biashara.

  Akifunga maadhimisho hayo, Rais Magufuli alisema azma yake ni kuona nchi inakuwa na uchumi mzuri ambao utamnufaisha kila mtanzania na rasilimali zilizopo badala ya kumilikiwa na watu wachache.

  Tamko la kuanza kazi kwa Mahakama hiyo lilitolewa bungeni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi yake.

  “Kuhusu ahadi ya kuanzisha Mahakama Maalum ya Ufisadi napenda kuliarifu Bunge lako kwamba, Serikali imeanzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi mwezi Julai 2016,” alisema Majaliwa.

  Aidha, Waziri Mkuu alisema pia Serikali itaimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki kwa kesi zitakazofikishwa kwenye mahakama hiyo.

  Akizungumza Bungeni Majaliwa alisema katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya uhaba wa majengo ya mahakama na vitendea kazi katika ngazi zote, Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake aliyoitoa Februari 4, mwaka huu ya kutoa fedha za maendeleo ya mahakama Sh. bilioni 12.3.

  Alisema hatua hiyo imewezesha mahakama kuendelea na ukarabati na ujenzi wa mahakama katika ngazi mbalimbali pamoja na ununuzi wa vitendea kazi kwani Serikali imedhamiria kupunguza kero ya mlundikano wa mashauri mahakamani ili wananchi wapate haki kwa wakati.

  Katika kufanikisha dhamira hiyo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeimarisha utendaji wa mhimili wa mahakama kwa kuongeza rasilimali watu na fedha.

  “Serikali pia imeboresha na kuongeza ufanisi katika upelelezi na uendeshaji wa mashauri kwa kutenganisha jukumu la upelelezi na uendeshaji mashuari kwa majaji na mahakimu kujiwekea utaratibu wa kuwa na malengo ya idadi ya mashauri ambayo wanapaswa kuyasikiliza kila mwaka,” alisema Majaliwa.

  Aidha Tarehe 24 Juni 2016 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho Mbalimbali, ambayo pamoja na mambo mengine, yamempa Jaji Mkuu mamlaka ya kuanzisha Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ya Mahakama Kuu.

  Kwa mujibu wa muswada huo uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, adhabu kwa watakaokutwa na hatia zimeongezwa, huku mahakama hiyo ikiwekewa mazingira wezeshi ili iendeshe kesi hizo kwa haraka.

  Muswada huo wa sheria ambao kwa sasa utakuwa ukisubiri Rais ausaini ili iwe sheria kamili, umekusudia kuanzisha divisheni hiyo ya mahakama, ambayo itakuwa na majaji wake na watumishi wake wanaojitegemea.

  “Divisheni Maalumu ya Mahakama Kuu, itakuwa na majaji pamoja na watumishi wengine, ambao wanahusika moja kwa moja na kesi za rushwa na uhujumu uchumi tu, hatua hii itawezesha kesi za makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kusikilizwa kwa urahisi, ufanisi na kwa haraka,” alisema Masaju wakati alipokuwa akisoma muswada huo kabla ya kupitishwa na Bunge.

  Hatua hiyo ya kuwa na majaji maalumu na wafanyakazi wake, Masaju alisema imelenga kuondoa udhaifu uliojitokeza wakati wa kushughulikia kesi za rushwa na uhujumu uchumi, kwa kuwa majaji waliokuwa wakisikiliza mashauri hayo, walikuwa hao hao wanaosikiliza mashauri mengine ya jinai, madai, katiba na mengine yanayofunguliwa Mahakama Kuu.

  Kwa mujibu wa Masaju, hali hiyo ilisababisha uendeshaji wa kesi za rushwa na uhujumu uchumi, kutokuwa na tofauti na uendeshaji na usikilizwaji wa kesi zingine.

  Aidha Masaju aliongeza kuwaMazingira mengine wezeshi yanayotengenezwa na sheria hiyo kwa divisheni hiyo, ni thamani ya fedha inayohusishwa na makosa hayo, kuwa inaanzia Sh bilioni moja.

  “Inapendekezwa kuwa pale makosa ya rushwa na uhujumu uchumi yanapohusisha thamani ya fedha, basi makosa yatakayofunguliwa katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, yawe ni yale ambayo thamani yake haipungui Sh bilioni moja,” alisema Masaju.

  Lengo la kuweka thamani hiyo ya fedha, limeelezwa kuwa ni kuiwezesha divisheni hiyo kujikita kusikiliza makosa makubwa ya rushwa na uhujumu uchumi, ili makosa madogo yasiyofikia thamani hiyo, yasikilizwe na mahakama za wilaya, mahakama za hakimu mkazi na Mahakama Kuu.

  Hata hivyo, divisheni hiyo pia kwa mujibu wa sheria hiyo itasikiliza makosa mengine ya rushwa na uhujumu uchumi bila kujali thamani ya fedha, kutokana na namna makosa hayo yalivyotendeka, asili yake na ugumu wa kuyawekea thamani ya fedha.

  Pia, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) amepewa mamlaka ya kutoa hati ambayo itataka mashauri mengine yatakayofunguliwa, yasikilizwe katika divisheni hiyo kwa maslahi ya umma.

  Marekebisho mengine yaliyopendekezwa ni pamoja na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi chini ya sheria hii iwe ni kifungo cha gerezani, kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30 au vyote kwa pamoja na hatua nyingine za kijinai, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zilizopatikana kutokana na makosa hayo.

  Kifungo hicho kimeongezwa kutoka katika sheria ya sasa ambayo ndiyo inayorekebishwa, ambayo ilitaka kifungo kisizidi miaka 15. Kwa mujibu wa Masaju, maneno hayo “kifungo kisichozidi miaka 15”, yaliipa Mahakama mamlaka ya kutoa adhabu ndogo zaidi, ilimradi tu adhabu hiyo haizidi miaka 15, jambo lililoonekana kuwa baadhi ya adhabu zilikuwa ndogo kuliko uzito wa makosa.

  Katika kutaifisha mali za waliokutwa na hatia, sheria hiyo imeweka masharti ya kuzuia kutumika kwa sheria zinazohusu ufilisi au uamuzi wa kufilisi kampuni, kwa mali ambayo inachunguzwa chini ya Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi.

  “Marekebisho hayo yanalenga kukabili vitendo vya watu au kampuni kujifilisisha wakati uchunguzi unapoanza dhidi yao na pia kuhakikisha kuwa mali zote zinazohusika na kosa linalochunguzwa, au linaloendelea mahakamani, inaendelea kuwepo hadi uchunguzi au kesi husika itakapohitimishwa,” alisema Masaju.

  Hatua hiyo imetajwa kuwa na nia ya kuiwezesha serikali kutaifisha mali hiyo, wakati kesi husika itakapokamilika na ikathibitika kuwa ina uhusiano na kosa la rushwa na uhujumu uchumi lililothibitishwa mahakamani.

  “Kwa ujumla hatua hii ni njia mojawapo ya kuwafanya watu waogope kutenda makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na pia kuhakikisha kuwa mhalifu, hanufaiki na uhalifu alioutenda kwa kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa, ufisadi na uhujumu uchumi,” alisema Masaju.

  Hata hivyo Masaju aliongeza kuwa Marekebisho mengine yaliyoingia katika sheria hiyo, yanahusu ulinzi wa mashahidi, ambapo Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), kwa kushauriana na Mkurugenzi wa Mashitaka, wanatakiwa kuweka utaratibu wa kuhakikisha usalama wa shahidi pamoja na familia yake ikiwa na lengo ni kusaidia usalama wa mashahidi wa kesi hizo, ili mashahidi wawezeshwe kutoa ushahidi wao bila woga, kwa kuwa kesi hizo zinahusisha watu wenye fedha na makosa yanayofanyika ni ya kupanga.

  Awali Rais Magufuli alipoahidi kuanzisha mahakama hiyo, wengi walichukulia kama ni suala lisilowezekana, lakini kasi yake ya kusimamia suala hilo, imewafanya baadhi ya mafisadi waingiwe na kihoro na kuanza kutafuta njia za kujinusuru ikiwemo kutoroka nchini.

  Mpaka sasa serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha mwaka mmoja imefanikiwa kufungua majalada zaidi ya 300 yanayohusiana na kesi mbalimbali za ufisadi ambayo yako mezani kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ikiwa ni sehemu ya hatua muhimu kabla ya kufikishwa mahakamani.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametimiza siku ya 365 Watanzania wameona, kushuhudia utendaji na mwelekeo wake wa kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio.

  Kauli hiyo imetolewa na leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa kabla ya kuanza kujibu maswali ya papo kwa papo ambayo huulizwa na Wabunge kwa Waziri Mkuu kwa kumwomba Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuridhia kuwakumbusha Watanzania kuhusu muda wa uongozi tangu Rais Dkt. Magufuli aingie madarakani.

  “Jukumu letu, ni kumwombea Mhe. Rais aweze kuendelea vizuri na kazi ya kuiongoza nchi yetu na wananchi wote tuungane pamoja kila moja kwa dhehebu lake kuweza kuiombea Serikali hii ili iweze kupata mafanikio makubwa” amesema Waziri Mkuu.

  Akijibu swali lililoulizwa na Munde Tambwe Abdallah (Mb) juu ya mifumo ya Serikali ya kupeleka fedha za maendeleo katika halmashauri kwa kuzingatia mifumo, sheria, taratibu na miongozo ambayo husababisha halmashauri kuchelewa kupelekewa fedha mara baada ya bajeti kukamilika, Waziri Mkuu amesema kuwa baada ya Bunge la Bajeti kukamilisha kazi yake, Serikali inawajibika kutekeleza maamuzi ya Bunge kwa kupeleka fedha zilizopangwa kulingana na bajeti hiyo.

  Akifafanua suala hilo, Waziri Mkuu amesema kuwa baada ya Bunge kuridhia na kutoa mamlaka ya matumizi ya fedha, Serikali ya Awamu ta Tano ilianza na majukumu muhimu ya kujiridhisha na uwepo wa mifumo sahihi ya makusanyo ya mapato na matumizi yake, kupeleka watumishi watakaosimamia shughuli za usimamizi wa ukusanyaji wa mapato na matumizi yake kwenye halmashauri zote nchini na kuratibu na kutathmini miradi yote iliyokuwa imeanza halafu kutokuendelezwa pamoja na miradi mipya ili kutambua pamoja na thamani zake.

  Baada ya kujiridhisha juu ya mambo hayo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeanza kupeleka kwenye halmashauri zote nchini ambapo kufikia mwezi Oktoba kwa mujibu wa Hazina, jumla ya zaidi ya shilingi Bilioni 177 za miradi ya maendeleo zimepelekwa kwenye halmashauri.

  Kwa kudhihirisha masuala hayo, Waziri Mkuu amesema kuwa hivi karibuni vyombo vya habari ikiwemo magazeti kwa wiki tatu yameanza kutoa matangazo ya zabuni kutoka kwenye halmashauri mbalimbali juu ya miradi iliyokuwepo na ile inayoendelea na miradi mipya imeanza kutengewa fedha na ambayo imeanza kutangaza kwa ajili ya kuetekeleza miradi hiyo.

  Aidha, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kupeleka fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuzisisitiza halmashauri ziendelee kukusanya mapato ya ndani ili kuongezea bajeti fedha za Serikali zinazopelekwa na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo uwe wa mfumo wa kielekroniki ili kudhibiti mapato yanayopatikana.

  Akijibu swali la nyongeza juu halmashauri zote kutumia mashine za kielekroniki, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wote wa Halmashauri wakiwemo Wakurugenzi kuhakikisha kila eneo la makusanyo vifaa vya kielekriniki vinatumika na matumizi ya vifaa hivyo yaendelee ili kuboresha ukusanyaji wa mapato nchini.

  Zaidi ya hayo Waziri Mkuu ameendelea kusisitiza kuwa matumizi sahihi ya fedha ambazo zinapelekwa kwenye halmashauri ni lazima zitumike kulingana na malengo yaliyokusidiwa katika kutekeleza miradi iliyoandaliwa kwenye halmashauri na kuwasihi Wabunge wakiwa wajumbe wa baraza la madiwani katika halmashauri zao waendelee kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha zinazopelekwa ili zitekeleze miradi hiyo kikamilifu.

  Kuhusu swali la Mbunge wa Ukonga Mwita Witara juu ya Mfuko wa Jimbo, Waziri Mkuu Majaliwa amemhakikishia Mbunge huyo kuwa Serikali haijafilisika, na kusisitiza kuwa suala la Mfuko wa Jimbo bado unatambulika na fedha zitapelekwa kwenye majimbo na wabunge wote watajulishwa ni kiasi gani cha fedha kimepelekwa kwenye majimbo yao ili sheria ziendelee kutumika na kutekelezwa na Mbunge akiwa mwenyekiti wa Mfuko huo anatakiwa kuendelee kuratibu fedha hizo.

  Waziri Mkuu amesema kuwa fedha za Mfuko wa Jimbo ni miongoni mwa fedha inayotengwa kwenye Bajeti na kukumbusha kuwa tangu Bunge la bajeti limalize kazi yake miezi mitatu, bado kuna miezi saba ya kutekeleza bajeti hiyo ambapo fedha hizo zitapelekwa kwenye miradi iliyokusudiwa kwenye majimbo mbalimbali nchini.

  Kwa upande wa Wafanyabishara kunyanyaswa na Maafisa wa Kodi nchini swali lililoulizwa na Ritha Kabati Mbunge wa Iringoa, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inaheshimu na kuwathamini wafanyabiashara wote nchini, wawekezaji, wadau na walipa kodi wote wa ndani ya nchi kwa kuzingatia kuwa maendeleo katika nchi yataletwa na sekta ya wafanyabiashara na wawekezaji wakiwa ndio walipa kodi wakubwa nchini.

  Kuhusu suala la nidhamu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA), Waziri Mkuu amewaonya wafanyakazi hao kuwa watumie lugha nzuri na busara wanapokwenda kutimiza majukumu yao kwa kutumia sheria na kanuni na taratibu za kufanya kazi yao.

  Kwa upande wa wafanyabiashara, Wairi Mkuu amewataka wafanyabishara hao kutoa taarifa juu ya jambo linalowakwaza kwenye vyombo vya usalama ikiwemo kitengo cha nidhamu kilichopo TRA ili kutafuta dawa sahihi juu ya wafanyakazi ambao hawaendani na nidhamu ya watumishi wa umma.

  Swali lingine lililoelekezwa kwa Waziri Mkuu liliulizwa na mbunge wa jimbo la Liwale Zuberi Kuchauka ambalo lilihusu uwepo wa Sera ya wafanyakazi kutoka nje ya nchi (TX) kupitia makampuni mbalimbali, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Sera hiyo bado ipo na Serikali inaisimamia kwa kuzingatia msingi wa kuwapa muda mfupi wataalamu hao wenye ufundi maalumu katika sekta ya kazi ili kujenga wigo mpana kwa Watanzania kupata ajira na kuweza kusimamia maeneo yanayohitaji utaalamu.

  “Tumetoa nafasi kwa watumishi wa nchi za nje kuja nchini Tanzania kufanya kazi ambazo hapa ndani sisi tunakosa utaalamu ndio tunafuata msingi huo, tunawapa miaka miwili ya mwanzo, tukiamini Watanzania waambata watakuwa wamejifunza utaalamu ule kwa miaka miwili hadi mitano ambapo baada ya hapo wataalamu wa nje ya nchi wanaweza kuondoka, tunamini Watanzania watakuwa wamepata taaluma hiyo na kusimamia sekta ya kazi” amesisitiza Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kuwa makakati wa Serikali wa kufugua milango ya ajira katika sekta zote ikiwemo utalamu, utaratibu huo utaendelea kusimamiwa wa kupokea utaalamu kutoka nje ambao Tanzania haupo ili kutoa nafasi kwa Wanzania kujifunza.

  Kuhusu swali la ruzuku ya pembejeo kwenye sekta ya kilimo kuwafikia wakulima kwa wakati ambalo liliulizwa na Mbunge wa Mbeya vijijini Oran Njeza, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeweka utaratibu wa kusambaza pembejeo nchini kwa kutumia Kampuni ijulikanayo Tanzania Fertilizer Cooperation ili kupeleka mbolea kwa wakulima wakati taasisi nyingine zimepewa kazi kusambaza pembejeo nyingine.

  Ili kuhakikisha wananchi wanapata mbolea na pembejeo nyingine kwa wakati, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imetoa fedhakwa ajili ya kununua pembejeo kwa kampuni hizo na zitatumia mawakala waliopo hadi ngazi za vijiji na kuhakikisha pembejeo hizo zinzwafikia walengwa zinazohitajika katika musimu wa kilimo unapoanza.

  Maswali ya papo kwa papo ya Wabunge ambayo huelekezwa kwa Waziri Mkuu yapo kwenye utaratibu kulingana na ratiba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kila siku ya Alhamisi ili kutoa majibu ya maswali hayo yanayoelekezwa kwenye sekta mbalimbali nchini kwa musatakabali wa kuboresha maisha ya Watanzania na taifa kwa ujumla ili kuwa na maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2025 kulingana na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

  0 0

  Pichani juu na chini ni Balozi wa Umoja wa nchi za Ulaya EU kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akihutubia wanafunzi wa vyuo mbalimbali katika ukumbi Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ambapo alifanya ziara ya kutembelea Chuo jijini Arusha.(Picha na Ferdinand Shayo).

  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau akifafanua jambo katika ziara ya Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer alipotembelea chuo hicho.
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akisalimiana na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau, wakati wa ziara ya balozi huyo chuoni hapo.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela wakiwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki, Roeland Van De Geer.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya malengo ya dunia ya Umoja wa Mataifa katika Chuo cha Nelson Mandela jijini Arusha.
  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Karoli Njau (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu (wa pili kushoto) na Amon Manyama (kushoto).

  0 0


  Idadi ya Wataalamu wa Sayansi imekuwa ikikua kwa kasi kutokana na sekta hiyo kuwa chanzo cha maendeleo na ugunduzi na kufanya kupata maendeleo.

  Hayo yamesemwa na Mkuu na Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya Kukabidhiwa Madawati yenye thamani ya Sh. milioni 20 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu ya Shule za Al Muntazir, Azim Dewj .

  "Nimeomba sana wazazi kuhamasisha watoto wao kusoma sayansi, ukifanikiwa kwenye hayo masomo sio kwamba tu utaajiriwa lakini utaajiriwa sehemu unayoitaka kutokana na ajira kuwa nyingi ukitofautisha na masomo tuliyosoma sisi,"amesema Makonda.

  Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu ya Shule za Al Muntazir,Azim Dewji amesema ‘’tumeona litakuwa jambo la busara kama tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano tano inayoongozwa na Rais dk. John Pombe Magufuli ambaye pia alikuwa mwalimu.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akikata utepe kwenye hafla ya kukabidhiwa wadawati leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akikabidhiwa madawati na Mwekiti wa Bodi ya Elimu ya Shule za Al Murtazir Azim Dewji ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia alikuawa mwalimu Mh.John Pombe Mgufuli.

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa madawati yenye tahamani ya Sh. Milioni 20 yaliyotolewa na shule za Al Murtazir, ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa huyo kuhakikisha watoto wote wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es Salaam.

  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza machache kwenye hafla ya kukabidhi Madawati yenye jumla ya thamani ya milioni 20 yaliyotolewa na shule za Al Murtazir, ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa huyo kuhakikisha watoto wote wanakaa kwenye madawati leo jijini Dar es Salaam.


  Sehemu ya wazazi na wanafunzi wa Shule ya Al-Mutanzil leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamiii.

  0 0

   Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge  wa Nkansi Kaskazini, Ally Kessy wa Nkansi  (katikati) na Livingstone Lusinde wa Mtera kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Bovemba 2, 2016.
   aziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa, Dkt. Charles Tizeba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea, nyumbani kwake mjini Dodoma Novemba 2, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
   Wazirii Mkuu Kassim Majaliwa akijibu Maswali  bungeni mjini Dodoma Novemba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Wazirii Mkuu Kassim Majaliwa akijibu Maswali  bungeni mjini Dodoma Novemba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wapiga kura wake kutoka jimbo la Ruangwa waliomtembelea bungeni mjini Dodoma Novemba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wapiga kura wake kutoka jimbo la Ruangwa waliomtembelea bungeni mjini Dodoma Novemba 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wapiga kura wake kutoka jimbo la Ruangwa  waliotembelea bunge mjini Dodoma Novemba  3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali Bungeni leo mjini Dodoma. 


  Na Jacquiline Mrisho, Dodoma.

  Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 13.17 katika Bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa lengo la kutekeleza miradi ya maji katika vijiji vya mkoa wa Ruvuma ili kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata maji safi na salama.

  Kiasi hicho cha fedha kimetajwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge alipokuwa akijibu swali la Mhe. Jacqueline Ngonyani (Viti Maalum) lililohoji juu ya muda ambao Serikali itapeleka majisafi na salama katika Mkoa huo.

  Waziri amesema kuwa Mpango wa Utekelezaji wa Maji Vijijini ulioanza mwaka 2006/ 2007, mkoa wa Ruvuma ulipangiwa vijiji 80 na kati ya vijiji hivyo jumla ya vijiji 76 vilipata maji safi na salama. 

  “Asilimia kubwa ya vijiji vilivyokuwa katika miradi hiyo vimepata maji safi na miradi iliyobakia ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji hivyo kwa mwaka huu wa fedha Ruvuma imetengewa kiasi cha fedha cha bilioni 13.17 ili changamoto ya maji safi na salama katika mkoa huo iishe kabisa”, alisema Lwenge.

  Ameongeza kuwa Serikali imeendelea na mipango ya kuboresha huduma hizo katika miji ya Songea, Mbinga, Namtumbo na Tunduru iliyopo katika mkoa huo ambapo kwa mji wa Songea, mradi wa ukarabati wa chanzo cha maji cha mto Ruhila Darajani umekamilika kwa gharama ya shilingi bilioni 2.6.

  Amefafanua kuwa kukamilika kwa chanzo hicho mnamo mwezi Februari mwaka huu kumeongeza kiasi cha upatikanaji wa maji wa jumla ya lita milioni 6 kwa siku ambapo wakazi 164,162 wamenufaika katika Manispaa hiyo.Aidha, Mhandisi Lwenge amebainisha kuwa kwa sasa Serikali imekamilisha usanifu wa kina na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya uboreshaji wa huduma hizo katika miji iliyopo katika mkoa huo.

  “Serikali inaendelea na jitihada ya kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo kwa mji wa Tunduru mradi utagharimu Dola za Kimarekani milioni 7.3, mji wa Namtumbo ni Dola za Kimarekani 12.08, na Dola za Kimarekani 11.86 kwa ajili ya mji wa Mbinga”, alisema Mhandisi Lwenge.

older | 1 | .... | 1030 | 1031 | (Page 1032) | 1033 | 1034 | .... | 1897 | newer