Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1029 | 1030 | (Page 1031) | 1032 | 1033 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma


  Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kukarabati, kupanua na kumalizia ujenzi wa mabweni mapya pamoja na majengo ya utawala katika baadhi ya magereza nchini.
   
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ameyathibitisha hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Hawa Mwaifunga (Mbunge wa Viti Maalumu) lililohoji kuhusu mpango wa Serikali katika kuhakikisha hali za magereza katika Mkoa wa Tabora zinaboreshwa. 

  Mhe. Mwigulu amesema kuwa katika kuhakikisha hali ya magereza nchini inaboreshwa ili kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa, Serikali inaendelea na mpango endelevu wa kufanya upanuzi wa magereza ya zamani na kujenga magereza mapya katika kila Wilaya ambapo utekelezaji huo unafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha. 

  “Katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga bilioni 3 katika Bajeti kupitia Fungu la Maendeleo kwa ajili ya kukarabati magereza ambapo shilingi milioni 185 kati ya bajeti iliyotengwa ni kwa ajili ya kukarabati magereza ya Mkoa wa Tabora, hivyo tunategemea magereza ya mkoa huo yatakuwa katika hali nzuri”, amesema Mwigulu. 

  Ameongeza kuwa Serikali inatambua msongamano wa mahabusu uliopo katika magereza mengi nchini na kuongeza kuwa Jukwaa la Haki Jinai limekuwa likifanya vikao vya kuharakisha kesi ambazo upelelezi wake haujakamilika ili kupunguza msongamano huo. 

  Aidha, Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali inahakikisha Askari Wapelelezi wanapewa mafunzo kulingana na kazi yao ili waweze kufanya ukamataji wa watuhumiwa kwa kuzingatia uzito wa ushahidi wa muhusika na kuepusha malalamiko ya kubambikiwa kesi na kujikuta Serikali inatumia gharama nyingi kuwatunza mahabusu hao. 

  Kuhusu usalama wa askari, Waziri Mwigulu amesema kuwa Serikali itaendelea kuliwezesha Jeshi la Polisi nchini kwa kuwapa vitendea kazi bora na kuwajengea uwezo wa mafunzo askari hao ili waweze kukabiliana na matukio ya uhalifu dhidi ya wanananchi na mali zao pamoja na uvamizi wa vituo vya polisi nchini. 

  “Hadi kufikia Septemba 2016 Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha 19 kati ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa wakitekeleza majukumu yao hatua inayoonesha jeshi la Polisi linavyofanya kazi kwa umakini” alisema Mwigulu. 

  Kwa upande mwingine, Waziri Mwigulu ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyo karibu pindi wanapokuwa na shaka juu ya watu wasiowatambua au kufanya kazi zisizoeleweka ili kuwahakikishia wananchi usalama wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waganga wa Tiba Asili Tanzania waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Makamu Mwenyekiti wao ambaye pia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephene Hillary Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wabunge kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

  KUFUATIA Agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka  Wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ wasibugudhiwe na watafutiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa na mazingira rafiki, Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema  maeneo ya wafanyabiashara hayo tayari yameshatengwa huku yakiwa na mazingira ya kuweza kufanya biashara.

  Mjema ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya  kuzungukia masoko ambayo wanatarajia  kuwahamishia wafanyabiashara walio katika Manispaa ya Ilala, ikiwemo soko la Kivule na Kerezange ambapo kwa sasa yapo tayari huku akiahidi kushughulikiwa kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na stendi ya mabasi.

  Mjema amesema katika kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia biashara ni pamoja kuwa  kituo cha Daladala ambapo abiria wanashuka na kupata mahitaji yao katika masoko.Amesema  soko la Tabata Muslim liko katika hatua za mwisho mpaka mwezi wa 12 masoko yote yatakuwa katika mazingira rafiki ya kufanya wafanyabiashara ndogodogo  waweze kufanya biashara zao. 

  Mjema amesema kutokana na kuondoka kwa wafanyabiashara hao kutakuwepo wa eneo moja la  barabara ambazo wafanyabiashara wataruhusiwa kufanya biashara kando kando ya barabara  kwa siku za Ijumaa, Jumamosi  pamoja na  Jumapili kuanzia majira saa sita mchana kwa wafanyabiashara .

  Mitaa ya Lumumba na Mkunguni itatumika kufanya biashara kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili eneo hilo linauwezo wa kukaa  zaidi ya wafanyabiashara 1800.

  Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesimamia uadikishwaji wa machinga waliokuwa wafanyabiashara  kandokando ya barabara za mabasi yaendayo kasi na kuwataka ambao hawajajiandikisha wajiandikishe  mapema ili wapatiwe maeneo rasmi.
   Wafanyabiashara ndogondogo wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema leo jijini Dar es Salaam.
   Wafanyabiashara Ndogondogo wakijiandikisha majini yao ili wapatiwe maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambayo yatakuwa  na mazingira rafiki, leo jijini Dar es Salam.
   Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule, ikiwa ni ziara yake ya kutembelea masoko ambayo wafanyabiashara ndogondogo watapelekwa kufanya biashara leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo ‘Machinga’  katika soko la kuu la Kelezange lililopo kata ya Kivule leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimkabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015, Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson, wakati kiongozi huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto katikati) akimueleza jambo mgeni wake ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.
  Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (hayupo pichani) wakati alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kulia kwake ni Mtathmini wa Mradi wa Shirika hilo, Consolata Sulley.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimuonesha Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (hayupo pichani) Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ambayo pia alimkabidhi mgeni wake alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi. Giveness Aswile akimueleza jambo Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson wakati alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kaimu Naibu Katibu wa Tume, Idara ya Uendeshaji Uchaguzi, Adam Nyando.
  Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mary Longway (kushoto) akitoa shukrani kwa Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) ambaye ametembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto katikati ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Mst. Damian Lubuva na wa pili kulia ni Mtathmini wa UNDP, Consolata Sulley. Picha na Hussein Makame, NEC

  0 0

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Wa kwanza kushoto ) akizungumza na uongozi wa East Afrika Televisheni na East Afrika Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa vipindi vya EATV Bi Lydia Igarabuza.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji wa EA Radio alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (Kushoto ) akifanya mahojiano na watangazaji wa EATV alipotembelea vituo hivyo Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa vipindi vya East Afrika Televisheni Bi Lydia Igarabuza (wa kwana kulia) akimueleza jambo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho Novemba 2 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

  ………………………………………………………..

  Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo amewashauri  wasanii wa filamu nchini kujiendeleza kielimu ili kuongeza weledi na kutengeneza filamu zenye ubora.

  Akiongea na uongozi wa Kituo cha Radio na Televisheni cha East Afrika leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji huyo amesema kuwa chombo hicho kina nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa wasanii hususani namna ya kuandaa Filamu zenye bora kwa kuwa wako mstari wa mbele katika kuonyesha kazi za tasnia hiyo. 

  “Kituo chenu kina nafasi kubwa zaidi ya kushawishi wasanii kutengeneza filamu bora kwa kuwa mmekuwa mkiwapatia fursa ya kutangaza filamu hizo pamoja na kuzionyesha ndani na nje ya nchi hivyo ni muhimu kuwakumbusha kuzingatia ubora wa filamu .”Alisema Bibi Joyce.

  Aidha ameongeza kuwa vyombo vya Habari ni nguzo muhimu katika kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini hivyo ni budi kwa wasanii kuhakikisha wanatengeneza Filamu bora ambazo zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika vyombo hivyo kwa maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

  Naye Mkuu wa vipindi vya televisheni wa East Afrika Bi Lydia Igarabuza ameipongeza Bodi ya Filamu kwa kufanya maboresho katika tasnia ya Filamu nchini na kuishauri kutoa elimu zaidi kwa wasanii katika kufuata Sheria ya Filamu na michezo ya kuigiza kabla ya kutengeneza filamu zao.

  “Naipongeza Bodi ya Filamu kwa juhudi mnazofanya katika kuboresha tasnia hii na msichoke kutoa elimu hiyo kwani wasanii wetu bado wanahitaji elimu ya filamu na sheria zake kwa ujumla.Alisema Bi Lydia.  Bodi ya Filamu imejidhatiti katika kuhakikisha tasnia ya Filamu inakuwa kwa kutengeneza bidhaa bora ambapo imekuwa ikitoa mafunzo kuwajengea uwezo wanatasnia hao .

  0 0

   Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwajali wanyonge hasa katika mambo yanayohusu elimu.

  Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Shirikisho hilo Zenda Daniel wakati wa mkutano wao na waandishi wahabari kuhusu mambo sintofahamu ya juu ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

  Zenda alisema kuwa wao kama Shirikisho wanampongeza na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kuwakwamu wanyonge

  “Sisi kama Shirikisho tunampongeza na kumuunga mkono mweshimiwa Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuhakikisha wanyonge wanajikwamua kwakupata elimu bora”. Alisema Zenda.

  Pamoja na pongezi hizo Shirikisho hilo limeelezea masikitiko yake kwa kile kinachoendelea kuhusiana na suala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hadi kufikia hatua ya kultilia shaka uwepo wa baadhi ya watendaji wa Serikali kufanya hujuma ili kukwamisha azma ya Serikali kutoka mikopo kwa wate wanaostahili.

  Katika duku duku lao walionyesha miongozo miwili tofauti kuhusiana na vigezo vya wanaostahili kupewa mikopo, mmoja ukitolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku mwingine ukitolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo walisema vigezo vilivyiwekwa kwenye miongozo hiyo vinakinzana.Zenda aliongeza kuwa hata pale wanaposema kigezo cha watoto uyatima kinapopaswa kutumika kumekuwa na changamoto kwani kuna baadhi ya wanachuo ambao wamethibitika kuwa ni yatima lakini hawajapewa mkopo hadi sasa.

  Aidha walitumia nafasi hiyo kutoa ushauri kwa Serikali kupitia Wizara husika kukaa pamoja na Bodi ya Mikopo ili kupitia upya vigezo vinavyotumika kuwapata wanafunzi wanaostahili mikopo hiyo.Kwa upande wake Katibu wa Hamasa wa Shirikisho hilo Nganwa Nzota alitoa angalizo kwa Bodi ya Mikopo kwa hatua yake ya uhakiki ambapo imelenga kuwaondoa wale wote watakao kuwa hawana sifa kulingana na vigezo vya sasa kuwa italeta mkanganyiko mkubwa utakasababisha watu waichukie Serikali yao.

  Alishauri kuwa zoezi la uhakiki liendelee lakini lisihusishe kuwaondolea mikopo wanufaika hao watakaobainika kutokidhi vigezo vya sasa kwani wao tayari wana mikataba nao na badala yake wajikite kuhakikisha wanakuwa makini kwa waombaji wapya.

  Katika Mkutano huo maalum uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bwana Hamid S. Muhina Sherikisho hilo liliiomb Serikali ya Rais Dkt. Jonh Pombe Magufuli kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu hili kuongeza ufanisi wake.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu, Mh. James Kilaba
  Na Mwandishi Maalum, Hammamet, Tunisia.

  PAMOJA na maendeleo na faida mbalimbali za Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), masuala ya Usalama, faragha na imani katika matumizi bado yameendelea kuwa masuala ya kuwekwa maanani katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

  Akihutubia kikao cha Mkutano wa Dunia wa Masuala ya Viwango Katika Mawasiliano (World Telecommunication Standardization Assembly – WTSA-16) mjini Jasmine Hammamet, nchini Tunisia hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Eng. James Kilaba amesema tekinolojia mpya ndani ya TEHAMA zina mchango mkubwa katika usalama (wa mitandao,mifumo, vifaa, data na wa watumiaji); faragha ( katika data na watumiaji) na Imani (kwenye mitandao,mifumo, vifaa, data na kwa watumiaji). 

  “Katika vikao kama hivi vya majadiliano kuhusu TEHAMA, wakati mwingi hatusahau kuzungumzia masuala ya huduma, vifaa na ukuaji wa watumiaji, mtandao na hata mapato. Leo tunazungumzia mchango wa teknolojia mpya katika usalama, faragha na Imani katika matumizi ya TEHAMA”, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA aliuambia mkutano huo.

  Eng. Kilaba ailisema kumekuwepo na mabadiliko ya teknolojia kutoka zilizotawaliwa kwa kiasi kikubwa na kuendeshwa kwenye mfumo wa intaneti kwa kutumia kompyuta binafsi zilizounganishwa kwa mfumo wa waya hadi tekinolojia zinazotumia vifaa ya mkononi vilivyounganishwa bila kutumia waya. Amesema hii imewezesha na kufanikisha mawasiliano zaidi na kwa kupitia mfumo wa intaneti kuifikia dunia iliyounganishwa na mfumo wa kompyuta.

  Eng Kilaba aliongeza kwamba mada kuu ya majadioiano katika mkutano huo ilikuwa ni huduma, vifaa, kukua na kuongezeka kwa watumiaji na kupanuka na kwa mifumo ya mawasiliano ambayo inawafika mbali zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi.

  “Wasimamizi wa mawasiliano duniano kote wanayo changamoto ya kukabiliana na mahitaji ya watumiaji na kubadilika kwa vifaa, bila kujali kuwa vimefungwa wapi au kutumiwa vipi ili mradi vinaimarisha usalama, faragha na Imani ya watumiaji. Kwa hiyo kimsingi ni watu ambao wanaishi kwenye utamaduni tofauti na katika maeneo tofauti ya kijiografia”, amesema Mkurugenzi Mku wa TCRA.

  Ameeleza kwamba Tanzania, kama nchi inayoendelea imefanya mengi katika sekta ya usalama wa mitandao ya kompyuta zinazotumika kwa mawasiliano. Aliongeza kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inao mfumo wa Usalama wa Matumizi ya Usalama Mtandaoni ambao umewekwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

  Amesema Tanzania imeanzisha mfumo wa kitaifa wa kushughilikia dharua zinazohusiana na matumizi ya kompyuta za mawasiliano (TZ- CERT) ambao unatumika kutoa elimu kuhusu masuala ya usalama wa mitandao, taarifa na ujuzi kwa wadau na watumiaji ili kuwawezesha kuwa na kiwango cha kuridhisha cha utaalamu unaohitajika katika kushughulikia masuala makubwa yanayohusiana na matumiai ya mitandao ya inayotumia mifumo ya kompyuta kwa mawasiliano.

  Hali kadhalika, aliongeza kuwa Tanzania ina kituo cha kitaifa kinachohifadhi data. Vilevile aliuambia mkutanio huo kwamba Tanzania imeanzisha utaratibu wa kuzuia matumizi mabaya ya data au taarifa kutoka kwenye simu za mkononi zilizoibwa nchini Tanzania.Eng. Kilaba alisema kwamba vitengo vya kushughulikia dharua za mifumo ya mawasiliano inayotumia kompyuta imeanzishwa katika nchi nne na kwa kiasi kikubwa nchi hizo zinabadilishana na kulinganisha taarifa kuhusu masuala ya usalama wa mitandao.

  Kupitia umoja wa taasisi za Mawasiliano Afrika Mashariki ambao unajulikana kama EACO, nchi wanachama zinakutana na kujadili masuala mbalimbali kuhusu usalama wa mitandao. Aliongeza kwamba changamoto zilizojitokeza kuhusiana na usalama, faragha na Imani katika matumizi ya TEHAMA zinaweza kuainishwa katika maeneo matano ambao ni viwango hafifu, sera, sheria na mikakati.

  “Viwango, Sheria na Mikakati vinahitajika ili kuinua kiwango cha ulinzi wa nchi katika masuala ya ulinzi wa mitandao. Kwa kuwa masuala ya usalama wa mitandao hayaishii ndani ya mipaka ya ncchi moja, viwango vilivyowekwa, sheria zilizowekwa na Kanuni zilizopo znahitajika kuhuishwa ili zitumike katika maeneo ya nchi zaidi ya moja na pia ulimwenguni pote. Inaaminika kwamba kuna wataalamu wachache wa masuala ya usalama wa mitandao wenye hadhi ya kimataifa wanaoweza kushughulikia kikamilifu ulinzi na makosa yanayohusiana na mitandao” alileza Mhandisi Kilaba.

  Alisisitiza kwamba kuna umuhimu wa kuwa na mikakati ya kitaifa kuhusu masuala ya usalama wa mitandaoo ambayo itawezesha kueneza elimu, ufahamu na ujuzi wa watumiaji na wadau wengine na watumiaji wengine ili kuwawezesha kushughulikia kikamilifu matukio ya usalama wa mitandao. Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mfumo wa kuthibiti usalama wa mitandao ndani na nje ya mipaka ya nchi husika.

  “Baadhi ya nchi zinazoendelea hazina mifumo ya kuthibiti usalama wa mitandao ya kompyuta za mawasiliano. Mifumo hii ikiwekwa na kutumika inawezesha uratibu, uchambuzi na uchukuaji wa hatua za kuimarisha mifumo na kubadilishana taarifa kuhusu usalama na tishio kwa mifumo ya kompyuta za mawasiliano’, Eng. Kilaba aliuambia mkutano huo.Mkutano wa WTSA unafanyika kila baada ya miaka minne. Mkutano wa wa mwaka huu ulianza 25 Oktoba hadi Novemba 3. Ulitanguliwa na Mkutano wa Dunia wa masuala ya viwango uliofanyika 25 Oktoba 2016.

  0 0
  0 0


  Kamishna Jenerali wa Mgereza – CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji wa masuala ya Kilimo cha kisasa mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Novemba 2, 2016, Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei(kushoto) ni Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi.

  Na; Lucas Mboje, Jeshi la Magereza – Dar es Salaam

  KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China pamoja na Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION na kumuahidi kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini na Viwanda vinavyoendeshwa na Shirika hilo.

  Akizungumza na Wawekezaji hao leo asbuhi Ofisini kwake (Jumatano, Novemba 2, 2016) alisema kwamba Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali lina fursa nyingi za miradi ya uwekezaji kwenye sekta nyingi kama vile Kilimo, Viwanda na Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa kutosha kwenye uwekezaji wao

  Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na Jeshi la Magereza kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha kisasa katika Gereza Idete lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa Ngo’mbe wa nyama Gereza Ubena, Mkoani Pwani.

  Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza hapa Tanzania.

  Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi ambayo inashughulikia na masuala ya Kilimo cha mazao ya chakula na nyama alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha umwagiliaji na watajenga Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.

  Shirika la Uzalishaji mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla ya Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi zinazosimamiwa na Shirika hilo.

  Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa ubia kwenye miradi yake ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

  0 0

  Na Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar .

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka matarajio makubwa kwa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja katika kufanikisha azma ya kuwa Taasisi yenye mfumo wa kujitegemea baada ya Baraza la Wawakilishi kupitisha Sheria ya kuanzishwa taasisi hiyo.

  Amesema Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti mzoefu wa masuala ya Afya Zanzibar Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil inahitaji mashirikiano ya karibu ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo na wananchi katika Kuleta mabadiliko hayo.

  Waziri Mahmoud ameeleza hayo Ofisini kwake Mnazimmoja alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Mnazi mmoja ambayo lengo lake kuu ni kuifanya Hospitali hiyo kufikia kuwa ya rufaa inayoshughulikia maradhi maalum yaliyoshindikana katika vituo vya afya na Hospitali za kawaida.

  “Tunawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao, vinavyofikia 142, na kuiacha taasisi mpya ya Mnazi mmoja kushughulia magonjwa makubwa,”alisisitiza Waziri wa Afya.

  Ameitaka Bodi kuishauri Serikali njia bora za kuchangia matibabu katika maeneo maalum kwa vile Sera ya Serikali bado ni kuendelea kutoa matibabu bila malipo kwa wananchi.Waziri wa Afya amewaeleza wajumbe wa Bodi hiyo kuwa Hospitali ya Mnazi mmoja inarasilimali kubwa ya kuaminiwa na wananchi wengi wa Zanzibar na linapotokea tatizo lolote huwa ni la nchi nzima hivyo suala la kuongeza ufanisi lina umuhimu mkubwa.

  Amesema hivi karibuni Hospitali hiyo itafunga majengo mengine mawili mapya ambayo yanavifaa vya kisasa hivyo wafanyakazi watapaswa kuwa waangalifu na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.Amewataka viongozi wa sehemu zote za Hospitali ya Mnazimmoja kuwasimamia wafanyakazi walio chini yao na kuiunga mkono Bodi katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo.

  Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil amesema jukumu walilopewa na Serikali ni kubwa lakini kwa kutumia utaalamu wa wajumbe wa Bodi hiyo watajitahidi kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya kuifanya Hospitali ya Mnazimmoja kuwa ya kujitegemea linafikiwa.Hata hivyo amewaomba viongozi wa Wizara na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuwapa ushirikiano na watakuwa tayari kupokea ushauri utakaosaidia kufikia malengo yaliyopangwa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili amewaeleza wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi mmoja kuwa Wizara itaendelea kusimamia sera lakini Bodi ndio yenye jukumu la kushauri maendeleo ya taaisi hiyo.
   Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazimmoja katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Mahmuod Thabit Kombo katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mnazi baada ya kuizindua rasmi Bodi hiyo, wa kwanza (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Jama Malik Akili na (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Abdulwakil Idrissa Abdulwakil.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akiangalia eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya Kivuko cha Lindi Kitundamkoani Lindi.Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Lindi
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akiongea na Meneja wa TEMESA Lindi Mhandisi Grayson Maleko (kushoto) alipotembelea kituoni hapo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (katikati) akiongea na Mafundi wa TEMESA Lindi walioko kwenye mafunzo ya vitendo, alipotembelea kituoni hapo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto w) akiongea na watumishi wa Karakana ya TEMESA Lindi, alipotembelea kituoni hapo mapema.
   


  Na Theresia Mwami TEMESA Lindi

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku.

  “Nawapongeza sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema Dkt. Mgwatu.

  Dkt Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.

  Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri na Idara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.

  Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.

  Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda. Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limemteua Jonesia Rukyaaa – Mwamuzi wa soka kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi wa kati 10 watakaochezesha mechi za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika kwa wiki mbili kuanzia Novemba 19, mwaka huu.

  Kwa uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amempigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za kimataifa.

  Rais Malinzi amesema kwamba Mwamuzi Jonesia ameliletea heshima taifa la Tanzania kwa kujijengea heshima ya kuaminika mbele ya Kamati ya Ufundi ya CAF – Waratibu na Waandaaji wa fainali hizo zitakazofanyika Cemaroon ambako mechi za mechi ya mwisho ya fainali itafanyika Desemba 3, mwaka huu.

  “Namtakia kila la kheri, naamini kwamba Jonesia atafanya vema. Nina uhakika kwamba hii ndiyo njia yake pekee ya kufanikiwa zaidi kwani ipo siku atateuliwa kuchezesha hata fainali za Kombe la Dunia,” yalikuwa ni maneno ya Malinzi akimwelezea Jonesia kwenye simu leo mchana.

  Jonesia anafanya idadi ya waamuzi watakaochezesha mchezo huo kutoka nchi za Afrika Mashariki kuwa watano kwani wengine kwa mujibu wa orodha ya CAF ni Salma Mukansanga (Rwanda), Lydia Tafesse (Ethiopia), Carolyne Wanjala (Kenya) na Suan Ratunga (Burundi).

  Waamuzi wengine ni Maria Packuita wa Mauritius, Gladys Lengwe (Zambia), Akhona Zennith Makalima (Afrika Kusini), Jeanne Ekoumou (Cameroon) na Aissata Amegee (Togo). Katika orodha hiyo pia yumo Mary Njoroge wa Kenya ambaye mwamuzi wa pembeni pekee.

  Katika fainali hizo, timu shiriki ni Cameroon, Afrika Kusini, Misri na Zimbabwe zipo kundi A wakati Nigeria, Ghana, Kenya na Mali zimo kundi B.

  Jonesia ambaye jana Jumanne alirejea kutoka Cameroon kwenye kozi ya uamuzi ngazi ya juu, kesho Alhamisi anatarajiwa kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pale Mtibwa Sugar ya Morogoro itakapokaribishwa na Mwadui kwenye Uwanja wa Mwadui. Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Mbao Fc na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imependa kuwatakia kheri na mafanikio watoto wote wa kidato cha nne walioanza kufanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya Sekondari kuanzia tarehe 01 Novemba, 2016. Wizara yenye dhamana ya maendeleo ya watoto inawaomba watoto wanaotahiniwa kutambua kuwa, muda wa kufanya mtihani ni fursa adhimu kwao, hivyo ni lazima kuutumia kwa umakini mkubwa kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao binafsi, familia na taifa kwa ujumla.

  Wizara inawaasa kuwa waangalifu muda wote wa kutahiniwa, wazingatie kanuni na taratibu stahiki, na pia kuepuka kuandika mambo ambayo yasiyotakiwa katika karatasi za mtihani. Kipindi cha kufanya mtihani ni kifupi ukilinganisha na muda wa miaka minne ambayo watoto hawa wamekaa madarasani wakiwa katika masomo; hivyo watoto wanahimizwa kujiepusha na vishawishi vyovyote ikiwemo vitendo vya udanganyifu katika chumba cha mtihani ambavyo vinaweza kusababisha kubatilishwa kwa matokeo yenu na hivyo kukatisha ndoto zenu. Ni matarajio ya Wizara kuwa wote mtamaliza mitihani yenu vizuri na kwa amani na utulivu.

  Wakati watoto wetu wakiendelea kufanya mitihani yao, Wizara inawakumbusha wazazi na walezi kutambua kuwa mnaowajibu wa kuweka mazingira ya kuwasaidia kukumbuka yote waliyojifunza kipindi chote cha masomo yao na kuwa tayari kujibu mitihani yao wakiwa wameandaliwa kisaikolojia ili kuhitimu vizuri. Aidha Serikali haitarajii kusikia au kuona mzazi au mlezi yeyote akijaribu kutengeneza mazingira ya kuharibu ndoto ya mtoto yeyote hasa watoto wa kike kwa kupanga kuwaozesha mara tu wanapomaliza mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne.

  Wizara inaamini kuwa wazazi na walezi watakuwa makini kuandaa mazingira ya watoto kufikia ndoto zao kielimu, na kuwaepusha watoto wa kike na janga la ndoa za utotoni, hadi watakapofikia umri stahiki. Wizara inasisitiza kwamba atakayethubutu kukatisha ndoto ya mtoto wa kike kwa kumwozesha chini ya umri wa miaka 18, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mzazi na mlezi huyo ili kulinda haki na masilahi ya mtoto kulingana na sheria, taratibu na kanuni zinazomlinda mtoto.

  Wizara inatoa rai kwa wazazi, walezi, makondakta na jamii kwa ujumla, kuwapa ushirikiano madhubuti watoto wetu katika kipindi hiki cha mitihani yao ili waweze kuhitimu vizuri mitihani yao. Watahiniwa ni hawa ni vijana wetu wanaotarajiwa kuendeleza taifa letu, hivyo tuwajengee mazingira murua ya kupata haki ya elimu ili kuwa na vijana mahiri na wenye weledi wakiwa na stadi na maarifa ya kubeba majukumu ya Taifa katika harakati za kuelekea uchumi wa kati,
   
  MARGARET S. MUSSAI 
  KAIMU MKURUGENZI WA MAENDELEO YA WATOTO 
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  MWANDAMIZI wa masuala ya usalama barabarani , Lawrence Kilimwiko amewataka waandishi wa habari  kutumia kalamu zao kuelimisha umma juu ya usalama bora na namna ya kukabiliana nazo.

  Akitolea ufafanuzi juu ya masuala ya usalama barabarani, Kilimwiko amesema kuwa waandishi wengi wa habari wanaripoti habari za ajali kama matukio na kushindwa kufuatilia hasa baada ya kumaliza kuandika hawafanyi ufuatiliaji wa majeruhi.

  Kilimwiko amesema kwa ajali za barabarani zimekuwa janga la afya hasa baada ya takribani watu milioni 50 wanaathirika na ajali hizo na wengine kupoteza maisha  na kundi kubwa linaloathirika ni vijana na inakadiriwa kufika mwaka 2030 ajali za barabarani zitachukua namba 5 katika janga la vifo duniani.

  Kutokana na ajali hizo, zimesababisha kupeleka mzigo mkubwa kwa sekta ya afya na kupelekea kuongeza gharama za serikali na kuchangia umasikini kutokana na nguvumali ya taifa kuangamiakwa ajali za barabarani.

  Uchunguzi uliofanyika kupitia Shirika la Afya Duniani(WHO) kupitai usalam barabarani  wamegundua kuwa asilimia 95 za  ajali zinatokana na matumizi mabya ya barabara na kuhamasisha waandishi wa habari kusaidia na kuchochea mabadiliko ya sera za sheria za Usalama barabarani.

  Kilimwiko amesema nchi kama Afrika Kusini ina sheria ambayo dereva yoyote haruhusiwi kutumia simu wakati anaendesha chombo cha moto na atakapokamatwa basi atapigwa faini na hili linatakiwa kufanyika hata nchini kwetu na hilo litasaidia kupunguza ajali.
   Mwandamizi wa masuala ya Usalama Barabarani, Lawrence Kilimwiko akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala ya Usalama barabarani na jinsi ya kuelimisha jamii kuhusiana na sera za usalama bwa barabara katika semina elekezi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwandamizi wa masuala ya usalama barabarani Lawrence Kilimwiko.Picha na Zainab Nyamka,


  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO. 

  MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imetakiwa kuwa makini na wafanyabiashara wanaoingiza nguo nchini bila ya kulipa kodi kwa kuwa hawalipii biashara zao kwa kila mzigo unaoingia hivyo kuchangia kuleta hasara ukusanyaji wa pato la taifa. 

  Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wakati wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya ujasiriamali kwa wanawake yaliyofanyika jijini Dar es salaam yakiwa na lengo la kukuza na kuwezesha wanawake kujitegemea kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa kupitia viwanda. 

  “Napenda kuwaambia TRA wawe makini wafanyabiashara wanaoingiza nguo nchini bila ya kulipa kodi kwa kuwa hawalipii biashara zao kwa kila mzigo unaoingia hivyo kuchangia kuleta hasara katika pato la taifa kwa kupoteza takribani shilingi bilioni 319 kutokana ukwepaji wa kodi za nguo zinazoingia nchini” alisema Waziri Mwijage. 

  Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa kwa kufanya hivyo TRA itaweza kukusanya mapato mengi zaidi na kukuza uchumi wa nchi kupitia ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara na wanaostahili kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi. 

  Mbali na hayo Waziri Mwijage amesema kuwa wanawake wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu na sio kuiga ubunifu wa mtu mwingine kwa asilimia kubwa ili kuweza kujiletea masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi ili kujipatia soko la kimataifa. 

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa MOWE Bi. Elihaika Mrema amesema kuwa maonyesho hayo yamewalenga wanawake wajasiriamali kuonyesha na kuuza bidhaa zao ambazo zimetokana na ubunifu wao kwa maendeleo ya mwanammke na Tanzania kwa ujumla ili kukuza pato la taifa. 

  “Wanawake wajasiriamali wanatakiwa wawe wabunifu katika kubuni biashara mbalimbali za kujikwamua na uchumi ili kuacha kutegemea wanaume kwa asilimia kubwa na kuendesha jamii kubwa ya Tanzania” alisema Bi. Elihaika.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kulia akisalimiana na Meneja wa huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Gabriel Mwangosi katikati alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam,kushoto ni Meneja wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Bi. Valentina Baltazar.
  Afisa Elimu Mkuu kwa mlipa kodi wa TRA Bi. Rose Mahendeka akiwapa maelekezo wateja waliotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza batiki na unyonyaji wa maji taka Genevive Investment Bi. Jane Mwaituka kulia alipotembelea banda lao wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara na wajasiliamari wanawake jijini Dar es salaam.Picha Na Ally Daud- MAELEZO.

  0 0
 • 11/02/16--09:38: MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
 • Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema akijadiliana jambo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala (kulia) akisalimiana na matabibu wa dawa za asili mjini Dodoma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG

   Wabunge wa Kambi ya Upinzani wakijadiliana jambo bungeni Dodoma
   Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata akiwa makini kusikiliza hoja bungeni
   Mbunge wa jimbo la Pangani, Jumaa Aweso (kushoto) akijadiliana jambo na mbunge mwenzie

   Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo (CCM), akichangia hoja kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/2017 bungeni Dodoma, hasa jinsi ya kuwawezesha vijana nchini
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akijibu maswali ya wabunge

   Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chadema, Sophia Mwakagenda (kulia) akijadliana jambo na mbunge mwenzie
   Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lisu (Chadema), akichangia hoja bungeni, ambapo alihoji watu wasio husika kuwaweka kwenye makumbusho ya mashujaa nchini.
   Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Omary Kitua akichangia hoja wakati wa majadiliano ya mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17

   Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT), akichangia hoja bungeni Dodoma , katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17.
   Wabunge wakiingia bungeni Dodoma jioni hii
   Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga akichangia mpango huo


   Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini,  Charles Msigwa akichangia mpango huo


  0 0


  Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Mussa Kafana akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kuwepo kwa taarifa ambayo inadai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa.


  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii 

  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekanusha taarifa ya kutoa Zabuni kwa Kampuni ambazo hazina vigezo kupata zabuni hizo. 

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Naibu Meya wa Halmashauri hiyo,Mussa Kafana amesema kumekuwepo na taarifa ikidai kuwa Halmashauri hiyo imetoa zabuni kwa Kampuni ambazo hazina sifa. 

  "Tumeona tutoe ufafanuzi kwamba hatujatoa zabuni kwa Kampuni ambayo haina sifa,Mfano Kenya Airport ambayo mpaka leo mkataba wake haujasainiwa,"amesema Kafana 

  Amesema baadhi ya mikataba haijasainiwa kutokana na Kampuni hizo kutotimiza vigezo na masharti vinavyotakiwa kama zabuni inavyoeleza. 

  Kafana ameeleza kuwa Mikataba haijasainiwa kutokana na Kitabu cha Zabuni kinaonyesha kuwa Halmashauri ya Jiji kitu gani inataka ikiwa ni pamoja na kutimiza Masharti hayo ya Halmashauri ya Jiji. Pia amesema Mzabuni anatakiwa kuleta dhamana ya Asilimia 10 ya kile kiwango alichobidi katika kuomba zabuni,hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Kitabu cha Zabuni katika sura ya 41 Kifungu cha kwanza

  0 0


  0 0

   Justice Lenaola (R) taking the oath as a Judge of the Supreme Court of Kenya. Administering the oath is the Chief Registrar of the Judiciary, Ms. Anne Atieno Amadi.
   President Uhuru Kenyatta congratulates His Lordship Justice Lenaola upon his appointment as Supreme Court Judge.

  EACJ congratulates the Deputy Principal Judge, Justice Isaac Lenaola, upon his new appointment as Judge of the Supreme Court Kenya

  East African Court of Justice, Arusha, 31st October, 2016: The Judge President of the East African Court of Justice (EACJ), Hon. Justice Dr. Emmanuel Ugirashebuja, has on behalf of the Court congratulated Hon. Justice Isaac Lenaola upon his new appointment as a judge of the Supreme Court of the Republic of Kenya.

  Justice Lenaola who has been a Judge at the High Court of Kenya has been promoted to the Supreme Court of Kenya after a rigorous recruitment process. His Lordship has replaced retired Justice Philip Tunoi, former Vice President of the EACJ. Until his appointment, Justice Lenaola was the head of the Constitutional and Human Rights Division at the High Court of Kenya.

  The Summit of the EAC Heads of State appointed His Lordship Justice Lenaola as a Judge of the EACJ, First Instance Division, in April 2011 and consequently designated him as the Deputy Principal Judge of the same Division in November 2013, a position he still holds to date. Justice Lenaola replaced retired Hon. Lady Justice Mary Stella Arach Amoko from the Republic of Uganda with effect from 1st December, 2013.   

  The President of the Court, Hon. Justice Dr. Ugirashebuja hailed Justice Lenaola upon his new appointment and wishes him success in his new role as a Supreme Court judge.

  Hon. Justice Dr. Ugirashebuja said that Justice Lenaola’s elevation from the High Court to the Supreme Court demonstrates the judge’s industriousness and commitment to serve, thus his being entrusted with a greater assignment.   

  His Excellency, President Uhuru Kenyatta swore in Justice Lenaola as a Judge of the Supreme Court on 28th October, 2016. Also sworn in at the same ceremony was Justice Philomena Mwilu as the Deputy Chief Justice of the Republic of Kenya.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Troika), Balozi Dkt. Aziz Mlima akifungua rasmi Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Asasi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia agenda mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 03 Novemba, 2016 katika Ukumbi huo. Asasi ya SADC inaundwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania (Mwenyekiti), Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti aliyemaliza). Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax. 
  Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu. Kulia ni Balozi Mlima. 
  Sehemu ya Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa kikao. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi HassanYahya Simba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Job Masima na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Innocent Shiyo. 
  Sehemu ya Ujumbe wa Msumbiji wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo 
  Sehemu ya ujumbe kutoka Angola wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Wakuu 
  Sekretarieti ya SADC .
  Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao hicho cha Makatibu Wakuu

older | 1 | .... | 1029 | 1030 | (Page 1031) | 1032 | 1033 | .... | 1897 | newer