Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

RATIBA KAMILI YA MKUU WA RC MBEYA MH. AMOS MAKALLA YA MWEZI NOVEMBA HII HAPA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amoss G. Makalla.


KAMPUNI YA MANTRA TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA VYENYE THAMANI YA MILIONI 12 KWA DAWATI LA KIPOLISI LA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akipokea msaada wa Vifaa kutoka kwa Afisa Mahusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania Khadija Pallangyo.

Kampuni hiyo inajihusisha na utafiti wa uchimbaji wa Madini aina ya Uranium katika eneo la Mto mkuju wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma , imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ofisi kwenye Ofisi ya Dawati la kipolisi la Kushughulikia masuala ya ukatili wa Kijinsia na watoto mjini Songea mkoani RUVUMA vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12. 

TAHARUKI YAIBUKA BANDARINI KUFUATIA MOTO MKUBWA KUZUKA.

$
0
0
Tukio la moto Bandarini leo limepelekea kuibua taharuki kubwa miongoni mwa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa eno hilo,kwa mujibu wa taarifa inaelezwa kuwa kuibuka kwa moto huo ilikuwa ni zoezi la jaribio kwa kikosi cha Zimamoto Bandarini hapo walipokuwa wakifanya mazoezi namna ya kukabiliana na janga la moto linapotokea.

Dkt. Bilal aipongeza Serikali kwa kuridhia Makubaliano ya Paris2015

$
0
0
Na: Frank Shija, MAELEZO.
Serikali ya pongezwa kwa hatua ya kuridhia makubaliano ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, Paris 2015 UN Climate Change Conference COP21.CMP11.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhadhiri wa Heshima wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere 2016, Mhe. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akitoa muhadhara katika Tamasha la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Hali ya Hewa leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bilal amesema kuwa kitendo cha Tanzania kuridhia makubaliano haya ya Paris kina maana kubwa sana  katika suala zima la kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia nchi na utunzaji wa mazingira  kwa ujumla.

“Niipongeze Serikali yetu kwa kuridhia kuingia katika makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 hii itakuwa hatua muhimu sana katika jitihada za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi”. Alisema Dkt. Bilal.

Aidha Dkt. Bilal aliongeza kuwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa ni makubwa sana hivyo ni vyema tukachukua tahadhari kubwa katikakuhakikisha tunakabiliana nayo.

Tuweke utamaduni wa kuhifadhi na kuyatunza mazingira yetu ili vizazi vijavyo visije kupata taabu itokanayo na uharibifu wa mazingira unaoweza kuepukika.

Hakikisheni mnatunza mazingira kwani kufanya uharibifu kunapoteza uhakika wa maisha kwa viumbe hai, pamoja na kupoteza vyanzo vya mapato,hivyo ni vyema tukajiepusha na matumizi ya baruti, uvuvi haramu, ukataji miti na mikoko.

Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini Balozi Hanne – Marie Kaarstad, amesema kuwa Tamasha la Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi limekuja wakati muafaka ambapo dunia imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema kuwa Tanzania inaeneo kubwa la mwambao ambalo lina ulinzi wa asili hivyo ni vyema kuvilinda kwa kufanya usafi ilikuendeleza uhai wa viumbe hai vilivyopo majini na nchi kavu.

Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi Profesa. Pius S. Yanda alisema kuwa Tamasha hilo limewakutanisha wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki kwa lengo la kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia nchi.

Profesa Yanda aliongeza kuwa wataendelea kushirikiana baina ya nchi za Afrika kama na huu ndiyo mwanzo mzuri tulioanza nao, pia alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Norway kwa shirikiano wao katika Nyanja ya mazingira ambapo alisema Norway inafadhili takribani PhD 11 katika eneo la mazingira.

KWA MARA YA KWANZA RAIS DKT MAGUFULI ATAFANYA MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA NAIROBI SOUTHERN BYPASS KATIKA ENEO LA KAREN NCHINI KENYA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, wakiweka jiwa la msingi kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Rutto pamoja na viongozi wengine, wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Karen nchini Kenya mara baada ya kufungua barabara ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.


Sehemu ya barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Bi. Lucy Karuga kuhusu usindikaji wa mazao ya chakula katika kiwanda cha Maziwa cha Eldoville katika eneo la Karen nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia usindikaji wa Samli katika kiwanda hicho cha maziwa cha Eldoville nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakicheza wimbo pamoja na kikundi cha kwaya katika eneo la Karen mara baada ya kufungua barabara hiyo ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais Uhuru Kenyatta pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea mama huyo nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Ngina Kenyatta mama mzazi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipomtembelea nyumbani kwake Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mama yake Rais Uhuru Kenyatta Mama Ngina Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya. PICHA NA IKULU 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika eneo ka Karen jijini Nairobi kwa ajili ya kufungua rasmi barabara ya kupunguza msongamano ya Nairobi Southern Bypass nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa mara baada ya kuwasili katika eneo la Karen jijini Nairobi.

Serikali yatenga bilioni 48 kujenga Mahakama 40 kwa mwaka wa fedha 2016/17

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 48.3 kwa ajili ya kujenga Mahakama 40 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuongeza ufanisi na kuharakisha hukumu za kesi katika ngazi mbalimbali nchini.

Kutokana na fedha itakayotumika kujenga mahakama, shilingi bilioni 36 zinatokana na Bajeti ya mwaka huu wa fedha wakati shilingi bilioni 12.3 zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Hayo yamebainishwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Iramba Mashariki Mhe. Allan Kiula aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama za Wilaya na uteuzi wa Mahakimu katika ngazi hiyo.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha Mahakama zinakuwepo kila wilaya ili kuwaondolea usumbufu wananchi, kurahisisha usikilizwaji wa kesi pamoja na kupunguza gharama kwa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kufuata Mahakama zilipo.“Kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Sheria na Kanuni inaeleza kuwa kila Mahakama ina mipaka yake hivyo hatuwezi kubadilisha mahakama ya mwanzo kutumika kama ya wilaya” amesema Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa mpaka sasa bado kuna wilaya zinapata huduma ya Mahakama kupitia wilaya nyingine ambapo amewahakikishia Wabunge na wananchi kuwa Serikali itajenga mahakama 40 kwa mwaka huu wa fedha.

Akifafanua mgawanyiko wa Mahakama 40 zinazotarajiwa kujengwa nchini, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Serikali itajenga Mahakama Kuu nne, Mahakama za mikoa sita, Mahakama za Wilaya 14 na Mahakama za Mwanzo 16 katika wilaya mbalimbali nchini.

Aidha, Mhe. Mwakyembe ametaja baadhi ya vigezo vinavyotumika kuanzisha Mahakama katika eneo lolote kuwa pamoja na uwepo wa hati ya kisheria ya kuwepo kwa wilaya, mkoa, kata na kijiji, umbali wa upatikanaji wa huduma za Mahakama, idadi ya wakazi wa eneo husika pamoja na uwepo wa huduma zingine za kipolisi na magereza.

Ameongeza kuwa kutokana na changamoto hizo za kukosekana kwa mahakama katika maeneo ambayo yamekidhi vigezo ndiyo yaliyopelekea Serikali kujipanga kujenga Mahakama hizo ambapo ametoa rai kwa wananchi kuwa na subira wakati wakikusubiri kujengwa kwa Mahakama hizo.

MAJALIWA AKUTANA NA MAMA MONGELLA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa Beijing, Getrude Mongella, Ofisini kwake, bungeni mjini Dodoma Novemba 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sababu tano za kuunga mkono Muswada wa Huduma za Habari 2016

$
0
0

Fatma Salum- MAELEZO

Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambao unatazamiwa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni katika kikao kilichoanza Novemba 1 mwaka huu umezua mjadala mkubwa na mpana miongoni mwa wadau wa sekta ya habari.

Mjadala wa muswada huu umekuwa ni mkubwa ukilinganisha na miswada mingine kwa sababu ukweli ni kwamba kila mtanzania ni mdau wa sekta hii ambayo wote tunaitegemea kwa kupata taarifa zinazoaminika ili kutusaidia kufanya maamuzi mbalimbali katika maisha yetu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Usahihi wa maamuzi yote makubwa tunayoyafanya mmoja mmoja au kwa pamoja kama jamii – iwe kuchagua vongozi, kuchagua kozi ya kusoma na mengineyo yanategemea sana taarifa tulizonazo.

Ili tuweze kupata taarifa sahihi ni muhimu vyombo vya habari na waandishi watengenezewe mazingira mazuri ya kufanyia kazi, jambo ambalo ndiyo malengo ya sheria hii tarajiwa.

Licha ya ukosoaji mkubwa unaofanyika, ukweli ni kwamba Muswada wa Vyombo vya Habari 2016, kama utapitishwa, utajenga mazingira mazuri ya tasnia hii na kuirudishia heshima inayostahili.

Katika kupitia muswada huu nimeona faida nyingi za muswada, lakini kwenye makala hii nitataja faida tano kubwa.

Heshima ya tasnia

Kwanza, muswada huu unairejeshea tasnia hii heshima yake iliyoipoteza siku nyingi kwa kuifanya fani hii iwe miongoni mwa fani za uweledi, kama zilivyo nyingine zikiwemo udaktari na uanasheria.

Heshima ya tasnia hii inastahili kuwa juu na ndiyo maana vyombo vya habari vimeitwa mhimili wa nne, ukifanya kazi sambamba na mihimili mingine yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

Tasnia hii ilianza kupoteza heshima kuanzia miaka ya 1990 kufuatia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na baadae kisiasa (vyama vingi 1992) yaliyochochea kuibuka kwa vyombo vingi vya binafsi, hususan magazeti.

Tangu enzi hizo, changamoto kubwa ya fani hii imekuwa ni ukosefu wa udhibiti kiasi kwamba kila anayejisikia, bila kujali kasoma au la, anaingia. Matokeo yake waandishi wasiosoma (makanjanja) wamekuwa wakifanya madudu na lawama zimeelekezwa kwa wanahabari wote. Akioza samaki mmoja ndiyo wote.

Kwa sasa waandishi wanatazamwa kwa kejeli, wanatukanwa, wanabezwa na yote haya ni kwa sababu ya kundi la waandishi wasio na maadili na ambao hawana ukomo wala miiko katika kutafuta habari na wanachokiandika ni tofauti na walivyopokea kutoka katika chanzo chao cha habari.

Mara nyingi tunasikia mwandishi anavamia stara za watu katika majumba yao au katika maeneo yao ya starehe kwa jina la kutafuta habari. Kwa hali hii, ni vigumu kulaumu vyanzo (source) wanapokataa kuzungumza na vyombo vya habari. Yote haya ni kwa sababu ya waandishi waliokosa taaluma na weledi (makanjanja).

Uholela wa kuingia katika fani hii ulitokana na sababu mbili kubwa, kwanza kisingizio cha kipengele cha katiba kinachomhakikishia kila mtu haki ya kukusanya na kusambaza habari (Ibara ya 18.1) kwani baadhi ya watu wametafsiri kipengele hiki kuwa kila mtu anaweza kuwa mwandishi wa habari!

Sababu ya pili ni maendeleo makubwa ya teknolojia ambapo kila aliyeweza kujitengenezea blogu yake alifanya hivyo na kuanza kutafuta na kuchapisha habari.

Lakini ukweli ni kwamba tasnia hii si ya mchezo mchezo na kufanyia majaribio. Zipo nchi zilizosambaratika au kuingia katika vurugu kutokana na vyombo vya habari ambavyo havikuwajibika, vikashindwa kutanguliza uzalendo, weledi na kuzingatia maadili.

Muswada huu katika sehemu ya tatu, Ibara ya 10, unaondoa shida hiyo kwa kuweka Bodi ya Ithibati ya Wanahabari itakayowajibika kutoa vitambulisho (press card) kwa wanahabari kwa kuzingatia sifa na viwango vya elimu vinavyotakiwa. Bodi pia itasimamia kanuni za maadili ya wanahabari zilizoidhinishwa na kutunza orodha ya waandishi waliothibitishwa.

Ibara ya 18.1–2 inapiga marufuku wasio na vitambulisho (press card) kufanya kazi ya uandishi wa habari na ibara ya 47.2 inaweka adhabu ya faini isiyopungua Milioni 5 au kifungo cha hadi miaka mitano kwa wanaovamia tasnia ya habari na kutumia huduma ya habari kueneza habari za uongo kwa lengo la kuhatarisha ulinzi, amani na usalama wa nchi. Bila ya shaka sheria hii ikitekelezwa, heshima ya tasnia ya habari itarejea.

Msisitizo wa elimu

Ukiangalia hali halisi ya uandishi wa sasa, utagundua kuwa kiini cha tatizo ni watu kupita njia za mkato kuingia katika fani hii, yaani kutokuwa tayari kwenda shule kusoma.

Lakini hata wale waliosoma bado wanahitaji kuendelea kupigwa msasa juu ya namna bora ya kufanya kazi zao maana tasnia ya habari inabadilika kila uchao hususan upande wa teknolojia.

Miaka 20 iliyopita hatukuwa na blogu wala hakukuwa na Twitter, Facebook, Instagram na Whatsapp kama ilivyo sasa, lakini hizi ni silaha za mwandishi na anaweza kuzitumia kuboresha kazi zake.

Ukiangalia muswada huu utaona kuwa umeweka msisitizo mkubwa katika elimu ya waandishi wa habari kiasi kwamba bodi itakayoundwa ina jukumu la kuishauri serikali kuhusiana na mafunzo ya waandishi, kushauriana na taasisi za elimu ya mambo ya habari juu ya viwango vya elimu vinavyotakiwa kwa waandishi na muhimu zaidi bodi hii ina jukumu la kuandaa mafunzo ya waandishi wa habari.

Katika Ibara ya 21, muswada huu unazungumzia mfuko wa mafunzo ya habari wenye malengo matatu ikiwemo kuwezesha mafunzo kwa wanataaluma ya habari, kukuza program za uendelezaji wa maudhui ya ndani ya nchi na pia kuchochea na kuchangia utafiti na maendeleo katika nyanja za habari na mawasiliano ya umma.

Kwa mujibu wa Ibara ya 22, mfuko huo utapata fedha kutoka bungeni, misaada na zawadi na michango ya vyombo vya habari. Kwa hiyo ukisoma vifungu hivi unaona kuna faida nyingi ambazo iwapo muswada huu utapita na kutekelezwa ipasavyo, utasaidia kuhuisha tasnia ya habari.


Umuhimu wa Baraza Huru la Habari
Pia muswada huu umeainisha kuwa kutakuwa na Baraza Huru la Habari ambalo kazi na mamlaka yake yatatambulika kisheria. Kila mwanahabari aliyethibitishwa atakuwa mwanachama wa baraza hili.

Ibara ya 25 (1) inaeleza kazi za baraza hili kwa kushirikiana na Bodi ya Ithibati zitakuwa ni kuandaa na kuidhinisha kanuni za maadili ya taaluma ya habari pamoja na kukuza maadili na viwango vya taaluma baina ya wanahabari na kampuni za habari.

Uwepo wa baraza hili utapelekea tasnia ya habari kuwa taaluma rasmi inayotambulika kisheria kama taaluma nyingine, tofauti na baraza lililopo sasa ambalo halitambuliki kisheria hivyo mamlaka yake hayana nguvu.

Kulinda Maslahi ya Waandishi wa Habari
Sababu nyingine ya kuunga mkono muswada huu ni maslahi ya moja kwa moja kwa wanahabari. Sheria hii itasaidia sana kulinda maslahi ya waandishi wa habari pale wanapopata majanga wakiwa kazini, maradhi, kustaafu au kuachishwa kazi. 

Kila mwajiri atatakiwa kuweka bima na hifadhi ya jamii kwa kila mtu aliyeajiriwa katika chombo cha habari husika na wanahabari wa kujitegemea watapaswa kujiwekea kinga kwa mujibu wa sheria hii.
Jambo hili ni la kupongeza sana kwani sheria hii itasaidia kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwenye tasnia ya habari.

Wengi wetu ni mashahidi kwamba kuna baadhi ya waandishi wa habari wamewahi kupata matatizo wakiwa kazini lakini wameishia kusubiri kuchangiwa na wasamaria wema ili wapate matibabu kwa vile hakuna kinga ya kuwabana waajiri au vyombo vya habari viweze kuwasaidia.
Mwelekeo kwa Vyombo vya Habari.

Sababu ya tano ya kuafiki muswada huu ni kwamba, pamoja na mambo yote sheria hii inatoa mwelekeo wa vyombo vya habari kuhusu jinsi ya kufanya kazi kwa ufanisi, kuzingatia maadili na weledi. Katika hili, sheria imeeleza majukumu ya vyombo vya habari vya umma na binafsi ili kuhakikisha majukumu hayo yanaleta tija kwa taifa.

Kwa kuzingatia hayo muswada huu una manufaa makubwa sio tu kwa wanahabari bali watu wote watanufaika kwa kupata taarifa sahihi zenye maudhui ya kuelimisha, kukosoa, kuonya na kuboresha bila ya kuudhi, kukiuka haki za wengine au kuharibu amani na usalama wa taifa letu.

WAJUMBE WA KAMATI LA BARAZA LA WAWAKILISHI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Konde Mh. Omar Seif Abeid wa Pili kutoka Kushoto akizungumza katika Kikao ilichowakutanisha Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.

Wa kwanza kutoka kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed, wa kwanza kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza, Naibu Katibu Mkuu Ahmad Kassim Haji na Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti - OMPR - Nd. Ameir Ussi.Picha na – OPMR – ZNZ.

TAMKO LA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU KUHUSU MIKOPO YA ELIMU YA JUU

MGODI WA ACACIA BUZWAGI WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYA MILIONI 22.4 KWA HOSPITALI YA MJI WA KAHAMA

$
0
0
Jumanne, Novemba 1, 2016-Kulia ni meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga Asa Mwaipopo akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa kwa ajili hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama.

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia mgodi wake wa Buzwagi imekabidhi vifaa tiba vya kisasa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 22,410,000/= kwa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kwa ajili ya kuisaidia katika kuboresha huduma zake za fya kwa jamii. 
 
Vifaa vilivyokabidhiwa ni mashine tatu maalumu za oksijeni,viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa,machela mbili za kisasa zenye magurudumu,mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa na mashine mbili maalum za umeme za kusafishia vifaa vya upasuaji. Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa hospitali hiyo, meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo alisema wametoa msaada huo baada ya uongozi wa Acacia kutembelea hospitali hiyo na kujionea mapungufu ya vifaa tiba. 
 
“Kutokana na kwamba kuwajibika kwa watu wetu na jamii inayozunguka imekuwa utamaduni wetu,tulifanya kikao na baadhi ya viongozi wa hospitali hii,walionesha nia ya kuhitaji msaada ili kukabiliana na changamoto za tiba”,alieleza Mwaipopo. “Kama sehemu ya mpango wa sera yetu ya mahusiano ya jamii,leo tunakabidhi vifaa hivi ambavyo tunaamini vitasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za tiba kwa wagonjwa na kuleta ahueni kwa wagonjwa na pia vitawasaidia madaktari waweze kutoa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi ili kuokoa maisha ya watu wengi zaidi”,aliongeza Mwaipopo.
 
 Akipokea msaada huo,mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu mbali na kuupongeza mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo,pia aliwataka viongozi wa hospitali hiyo kutunza vifaa hivyo vya kisasa na kutumia kwa matumizi yanayotakiwa kwani wananchi wengi wanahitaji huduma. Naye mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt. Bruno Minja aliushukuru uongozi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao umelenga moja kwa moja kuboresha huduma kwa wagonjwa na kurahisisha utoaji huduma kwa watoa huduma. Minja alisema watavitumia vyema vifaa hivyo hususani katika huduma ya mama na mtoto,huduma za upasuaji na huduma za dharura ikiwemo ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikijitokeza.


Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametuletea picha 22 za matukio,angalia hapa chini . Kushoto ni meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama Novemba 1,2016 wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama lengo ni kusaidia hospitali hiyo kuboresha huduma zake za fya kwa jamii.



Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Nyuma ni mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama Kazini katika mgodi wa Acacia Buzwagi, Dkt. Antoinette George. Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kahama Dkt. Bruno Minja akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi ambapo alisema hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama inahudumia wagonjwa kutoka halmashauri zote za wilaya ya Kahama ambazo ni mji Kahama ,Ushetu na Msalala pia wagonjwa kutoka maeneo ya wilaya ya Shinyanga,mkoa wa Tabora (Urambo,Kaliua,Nzega) na Geita. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama,Anderson Msumba akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliupongeza mgodi wa Acacia Buzwagi kwa msaada huo na kuongeza kuwa Buzwagi wamekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Kahama kutokana na kujitokeza mara kwa mara kusaidia jamii katika masuala mbalimbali. Meneja mkuu wa mgodi wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo alisema kampuni ya Acacia imetoa msaada wa vifaa tiba hivyo kufuatia ziara ya kawaida aliyoifanya akiwa ameambatana na Mkuu wa kitengo cha Afya na Usalama kazini katika mgodi wa Acacia Buzwagi,Dkt. Antoinette George katika hospitali hiyo na kujionea mapungufu ya vifaa tiba katika hospitali hiyo. Mwaipopo alivitaja vifaa tiba hivyo kuwa ni mashine tatu maalumu za oksijeni,viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa,machela mbili za kisasa zenye magurudumu,mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa na mashine mbili maalum za umeme za kusafishia vifaa vya upasuaji(Autoclave Mashines).Wa kwanza kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya. Watoa huduma katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama.Kulia ni mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama, Dkt. Joseph Ngowi. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimsikiliza meneja mkuu wa mgodi wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo. Wafanyakazi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama wakifuatilia zoezi la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi Kulia ni meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, Asa Mwaipopo akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa. Mashine maalumu ya ufuatiliaji wa mapigo ya moyo ya mgonjwa iliyotolewa na mgodi wa Buzwagi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama. Kulia ni meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, Asa Mwaipopo akikabidhi moja ya mashine maalumu ya kutengenezea oksijeni kati ya mashine tatu zilizotolewa na mgodi huo. Mashine ya kutengenezea Oksijeni iliyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi. Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Acacia Buzwagi, George Mkanza akiwa amekaa katika kiti cha wagonjwa wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba huku furaha ikitawala eneo hilo .Mgodi huo umetoa viti vitano vya magurudumu kwa ajili ya wagonjwa. Kiti cha magurudumu kwa ajili ya wagonjwa. Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi Asa Mwaipopo akikabidhi mashine maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuaji (Autoclave mashine).Acacia Buzwagi wametoa mashine mbili maalumu za umeme kwa ajili ya kusafishia vifaa vya upasuaji.  
Mashine maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuajiKushoto ni Mashine ya Oksijeni,kulia ni machela za kisasa zenye magurudumu. Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na mgodi wa Acacia Buzwagi ambapo aliushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii na kuwaomba kutochoka kuwasaidia wananchi. Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyakazi katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kutunza vifaa hivyo na kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.Kulia ni waandishi wa habari wakichukua matukio Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu alitoa wito kwa wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia hospitali na vituo vya afya kwani bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali. Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliuomba mgodi wa Buzwagi kuendelea kushirikiana na halmashauri hiyo kusaidia jamii. Mwishoni mwa mwaka 2015 mgodi wa Buzwagi pia ulikabidhi vifaa tiba mbalimbali katika kituo cha afya cha Mwendakulima kilichojengwa na mgodi huo ambapo ujenzi wa kituo hicho chenye kitengo cha afya ya mzazi na mtoto (RCH) na kitengo cha kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) pia ulihusisha ujenzi wa nyumba za wafanya kazi.

Mgodi wa Buzwagi umeweka huduma ya umeme wa solar katika kituo hicho na nyumba za wafanyakazi,huduma ya kukinga maji ya mvua na kuyahifadhi.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Serikali kukipandisha kituo cha afya cha Laela kuwa hospitali ya Wilaya

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla akiongea kuhusu upatikanaji wa dawa na vifaa tiba leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleimani Jafo akijibu swali la Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Malocha (hayupo pichani) aliyehitaji kujua ni lini kituo hicho cha afya kitapewa hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya,

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kukarabati kituo cha afya cha Laela kilichopo mkoani Rukwa ili kikidhi vigezo vya kuwa Hospitali ya Wilaya ikiwa ni moja ya jitihada za kupunguza adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya zilipo.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Suleimani Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Malocha aliyehitaji kujua ni lini kituo hicho cha afya kitapewa hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

Mhe. Jafo amesema kuwa ni uamuzi wa muda mrefu wa Serikali kuiweka Hospitali hiyo kuwa ya Wilaya na ndiyo sababu ya kufanya jitihada za kukiongezea uwezo kituo hicho kwa kujenga wodi nyingi pamoja na kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya kwani kwa sasa kituo hicho kina upungufu wa watumishi .

Amefafanua kuwa hadi sasa kuna baadhi ya majengo ambayo tayari yameshakamilika ambayo ni jengo la upasuaji wa dharura, wodi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji pamoja na wodi ya mama wajawazito.

“Kwa sasa kituo cha afya cha Laela hakina miundombinu inayokidhi sifa za kuwa Hospitali ya Wilaya ila kutokana na kupanuka kwa Mji huo na kuongezeka kwa watu wanaohitaji huduma katika kituo hicho tumeamua kukiboresha ili kifikie hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya”, amesema Jafo.

Ameongeza kuwa kwa sasa huduma za rufaa kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hicho zinatolewa kupitia magari ya kawaida ya Halmashauri kutokana na ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa lakini Wizara ina matarajio ya kutenga fedha ya kununulia gari hilo katika Bajeti ya mwaka 2017/2018.

Aidha, Mhe. Jafo amethibitisha kuwa kituo hicho kimetengewa jumla ya shilingi 9,358,100 katika Bajeti ya fedha ya mwaka huu ambayo itagharamia kununua dawa na vifaa tiba vitakavyorahisisha upatikanaji wa matibabu kwa wananchi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Wizara hiyo inaendelea kuipitia mikataba ya makampuni binafsi ili kuangalia namna ya kushirikiana nao katika kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali na vituo vya afya nchini.

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI LEO BAADA YA ZIARA YA KISERIKALI YA SIKU MBILI KENYA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kwenye ndege baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea  na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya,  alikokuwa katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili leo Jumanne Novemba 1, 2016 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO,NOV 02


WADAU WA UJENZI WAKAGUA UWANJA WA KIMATAIFA WA MWL. JULIUS NYERERE (TB III)

$
0
0
Muonekano wa juu wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Mwenyekiti wa Ujumbe maalum wa wadau wa Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora (wa kwanza kulia), akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa kwanza kushoto), wakati ujumbe huo ulipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la tatu la Abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). 
Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi Milanga akifafanua jambo kwa ujumbe maalum wa wadau wa ujenzi walipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo. 
Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi Milanga akionesha wajumbe maalum wa wadau wa ujenzi eneo la kupumzikia abiria katika Jengo la Tatu la Abiria (TB III) waliokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo. 
Muendelezo wa jengo la tatu la abiria sehemu ya pili katika hatua za ujenzi. Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800 kwa wakati mmoja. 
Muonekano wa eneo zitakapokuwepo huduma za kibenki na Idara ya Uhamiaji katika Jengo la tatu la Abiria (TB III). 
Muonekano wa sehemu ya mbele ya wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). Jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao. 

Dc Momba abaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma katika kituo cha Afya Tunduma

$
0
0
Na Saimeni Mgalula,Songwe

MKUU wa wilaya ya momba Mkoani hapa,Juma Irando ametoa onyo kali kwa mganga mtawala wa kituo cha afya cha Tunduma Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo aliyasema baada ya kwenda kutembelea kituo hicho cha afya jana na kubaini utaratibu mbovu wa utoaji huduma zakiafya baada ya kukaa katika kituo hicho kwa muda wa nusu saa bila ya kumuona hata muudumu mmoja akiwa mapokezi

''Viongozi niliongozana nao walilazimika kuwatafuta watoa huduma kwa dakika zaidi ya 45 baada ya kuwasuburi mapokezi kwa kipindi cha dakika 30 bila kupewa huduma pamoja na kuwepo kwa wagonjwa waliokuwa wakisuburi kusikilizwa eneo la mapokezi kwa kipindi kirefu''alisema.

Hali iliyomlazimu Dc Irando kuwasiliana na Mganga mkuu wa Wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina moja Dr Felister na kumtaka ampe jina la mganga mtawala wa kituo na mganga wa zamu, ambao walipatikana baada ya dakika 30 kinyume na utaratibu.alisema

Dc Irando pia aligundua kutokujazwa kwa taarifa za wagonjwa katika vitabu vya kuchukulia taarifa za wagonjwa kituoni hapo wakati akimuhoji mganga mtawala wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Dr Kaogo ofisini kwake, ambapo vitabu vya wagonjwa vilivyokutwa kituoni hapo vilionyesha kuhudumiwa wagonjwa 15 kwa siku na vingine kuonyeshwa kutokujazwa tangu tarehe 11 mwezi huu.

''Nikiwa kama mkuu wa wilaya siwezi kukubaliana nasuala la uzembe kazini ambaye alisema uhalali wa kituo hicho kuhudumia wagonjwa 15 tu kwa siku licha ya kuwa ndio kituo pekee kinachotoa huduma chenye hadhi ya wilaya'',alisema baada ya kubaini kinaudumia wagonjwa kumi na tano.
Dc Irando alipowahoji wagonjwa hao walikiri kutokusikilizwa kwa muda huo hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya kuwafata wahudumu wodini, kuonesha kuwa hawakuwa wakijuwa uwepo wa Mkuu wa wilaya kituoni hapo, wauguzi waliokutwa wodini hawakuonesha kushtuka wala kuuliza shida waliyonayo hadi pale Dc Irando alipojitambulisha, huu ni ushahidi wa utaratibu mbovu walionao watumishi wa kituo hicho kwa wagonjwa wanaofika kuhudumiwa katika kituo chao.

Dc alimtaka Mganga mkuu wa wilaya kumpa maelezo juu ya utaratibu mbovu wa utoaji huduma kwa wananchi unaofanywa na watumishi wa kituo hicho pamoja na kukaa na watumishi wa kituo hicho na kuwataka kubadilika mara moja akiahidi kurejea hapo kesho yake.

Aliagiza kuwepo kwa watoa huduma muda wote wa kazi na kutoa ovyo kali kwa mganga mtawala wa kituo hicho Dr Kaogo na kumtaka kujirekebisha na kurekebisha mapungufu aliyobaini na kuwa tayari kuendana na kasi ya Sereikali ya awamu ya tano na kuamtaka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

.Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tunduma Ally Mwafongo (chadema) alimwambia mkuu wa wilaya kuwa kituo hicho kina utaratibu mbovu na watumishi wa kituo hicho wanafanya kazi kwa mazoea hivyo kumtaka mkuu wa wilaya kuingilia kati ili wananchi wasiendelee kunyanyasika.

Akiongozea juu ya huduma mbovu za watumishi wa kituo hicho Mwafongo alisema kuwa alifika kituoni hapo siku kadhaa zilizopita mida ya saa mbili usiku hakukuta wahudumu wala waganga wanaotakiwa kuwepo licha kukuta uwepo wa wagonjwa waliokuwa wanasubiri kusikilizwa kwa muda mrefu na kumshukuru mkuu wa wilaya kujionea yeye mwenyewe isijekuonekana kuwa wanawachongea

VUAI AFUNGUA MAFUNZO YA WATUMISHI WA CCM Z'BAR.

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi kimewataka Watumishi wake kuelekeza nguvu zaidi katika kutekeleza ipasavyo majukumu yao kwa weledi na juhudi kubwa ili kukiletea ufanisi ndani ya Chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, ametoa kauli hiyo, alipokuwa akifungua mafunzo maalum ya watumishi wa Chama na Jumuiya zake wa kada ya Udereva, Walinzi, Waangalizi wa Ofisi, Makarani wa Masjala na Wahudumu wa Chama hicho, kutoka Mikoa na Wilaya zote za Zanzibar. Mafunzo hayo ya takriban wiki moja yanafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Mjini Unguja.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kinaridhishwa na utendaji wa watumishi wa kada hizo, isipokuwa CCM kimeona kuna umuhimu wa kuandaa mafunzo maalum kwa watumishi hao, kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa mpana zaidi katika kufanikisha majukumu yao na hivyo waendane na kasi ya Chama kwa sasa.

Mhe. Vuai amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwapatia mafunzo watumishi wake wa kada mbali mbali kwa lengo sio tu la kuwaleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ndani ya Chama bali pia kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mbadala za kiutumishi.

“Chama Cha Mapinduzi kitafanya kila linalowezeka kuhakikisha watumishi wake wa ngazi zote wanapatiwa mafunzo pamoja na kuwaendeleza kielimu, kwa madhumuni ya kunyanyua viwango vyao vya uelewa, na hivyo kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi”. Alidai Mhe. Vuai.

Amesisitiza haja kwa wanafunzo hao juu ya umuhimu wa kuimarisha Chama  na kudumisha suala zima la nidhamu pamoja na kuwepo kwa mawasiliano mazuri baina yao na Viongozi wao, ni dhahiri kutakijengea heshima kubwa chama hicho mbele ya jamii.

Nao wanafunzo hao, wametumia mkutano huo kumpongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa jinsi anavyotekeleza kwa kasi kubwa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 - 2020 pamoja na kupambana vilivyo na suala zima la rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Wamempongeza pia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kusimamia vyema Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020, kusimamia suala zima la amani na utulivu wa nchi, kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu ya kiuchumi kwa maslahi ya Wananchi wa Zanzibar. 

Waziri wa Fedha na Mpango Dkt. Philip Mpango awasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma

Serikali imeainisha maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2017/2018 kulingana na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka ujao wa fedha.
 
Waziri wa Fedha na Mpiango Dkt. Philip Mpango amesema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018.

Dkt. Mpango amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na miradi ya kielelezo ya maendeleo ambayo inayolenga kufanikisha utekelezaji wa Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ni pamoja na miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma, Mchuchuma Liganga, ujenzi wa reli ya kati kutoka Dar es salaam, Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa km 1,251 kwa “Standard Gauge” pamoja na matawi yake ya Tabora kupitia Isaka hadi Mwanza yenye urefu wa km 379, Isaka hadi Rusumo km 371, Kaliua kupitia Mapanda hadi Karema km 321, Keza hadi Ruvubu km 36 na Uvinza hadi Kelelema kuelekea Musongati yenye urefu wa km 203.

Miradi mingine ya kielelezo ni uboreshaji wa Shirika la Ndege TAanzania (ATC), ujenzi wa mitambo ya kusindika gesi mkoani Lindi, uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumimkoani Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Ruvuma, uanzishwaji wa kituo cha biashara cha Kurasini, kusomesha vijana katika stadi za mafuta na gesi, uhandisi na huduma za afya.

Waziri Dkt. Mpango ameyataja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa kukuza uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo y uchumi na maendeleo ya watu, mazingira ya wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji, ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na maeneo mengine muhimu kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa.

Dkt. Mpango amesema kuwa shabaha ya uandaaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2017/18 unaongozwa Serikali kusimamia mambo ya uchumi kwa ujumla ikiwemo kuongeza kasi ya ukuaji wa pato halisi la taifa kufikia asilimia 7.5 kwa mwaka 2017, asilimia 7.9 mwaka 2018 na asilimia 8.2 mwaka 2019, kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja kufikia asilimia 5.0 katika kipindi cha muda wakati, kuwa na pato ghafi la taifa la sh. trilioni 123.9 kwa mwaka 2017/18, sh. trilioni 139.7 kwa mwaka 2018/19 na sh. trilioni 165.4 mwaka 2019/20 pamoja na mapato ya kodi kufikia asilimia 14.6 ya pato la taifa mwaka 2017/18, asilimia 15.5 mwaka 2018/19 na asilimia 15.8 mwaka 2019/20.

Aidha, ametaja misingi ya mpango na bajeti kuwa ni amani, usalama, utulivu na utangamano wa ndani ya nchi na nchi jirani ambavyo vitaendelea kudumishwa nchini. Kuhusu mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018, Dkt. Mpango amesema amewaagiza Maafisa Masuuli kuzingatia masuala muhimu wakati wa uandaaji wa mipango na bajeti za mafungu yao ili kutekeleza Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015.

Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango amesisitiza uwepo usimamizi na udhibiti wa matumizi, ulipaji na ongezeko la madeni ya Serikali, ukusanyaji wa mapato pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za utekelezaji.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Hawa Ghasia alipokuwa akitoa taarifa ya kamati yake amesema kuwa Kamati yake inardhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia Sheria ya Bajeti na kanuni zake ambayo inahakikisha usimamizi na uwajibikaji katika hatua zote za mchakato wa bajeti unazingatiwa.

Naye Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Halima Mdee alipokuwa akiwasilisha hotuba yake amesema kuwa Kambi Rasmi inaunga mkono hatua za kisheria zinazochukuliwa na Serikali kwa wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuhujumu uchumi wa nchi.

Mkutano wa Tano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uanatarajiwa kuhitimishwa Novemba 11 mwaka huu huku shughuli mbalimbali za kuishauri Serikali zikiwasilishwa kupitia mijadala ya Wabunge.

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY WAJIPANGA KUADHIMISHA JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) KWA KUWASAIDIA WATOTO NDANI YA SHULE YA WALEMAVU YA UHURU MCHANGANYIKO

$
0
0


Foundation for civil society ambao ni asasi huru imetangaza kutumia utaratibu wa JUMANNE YA KUTOA (GIVINGTUESDAY) utaratibu ambao unatumika duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha watu na jamii kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wahitaji ambapo asasi hiyo imetangaza kuadhimisha siku hiyo hapa nchini kwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko ikiwa ni mara ya kwanza kwa Asasi hiyo kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Akizungumza na mtandao huu katika mahojiano maalum leo Martha Olotu ambaye ni Busness,Development and Partinaship Manager wa Asasi hiyo amesema kuwa FCS inalenga kutumia Utaratibu wa Jumanne ya Kutoa kwa namna ya kuhamasisha Moyo wa kujitolewa kwa wenye Uhitaji,ikiwa ni Jitihada za ulimwengu ambazo zilizinduliwa Rasmi Tangu mwaka 2012 na shirika la New York’s 92nd streat Y kwa ushirikiano na UN Foundation,Lengo likiwa ni kuweka siku maalum kwa ajili kuheshimu na kuadhimisha ukarimu katika kutoa,ambapo kwa sasa siku hii imekuwa ikiadhimishwa na nchi nyingi Duniani ikihusisha makampuni Binafsi,watu binafsi,familia na asasi za kiraia.



Akizungumzia maadhimisho hayo ambayo yatafanyika Tarehe 29 mwezi wa November Karin Rupia Ambaye Ni Resource Mobilization Executive Kutoka katika asasi hiyo amesema kuwa shirika hilo litakabidhi michango iliyotolewa, na kujiunga kufurahi na watoto kwenye shughuli kama kupima afya za watoto hao,kuchora na watoto,kucheza na watoto kusafisha watoto pamoja na kuwasomea watoto hao wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.

Kwa maelezo zaidi Juu ya siku hiyo unaweza kutizama HABARI24 TV kwenye Youtube account yetu hapo.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images