Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA NCHINI INDIA.

$
0
0

Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habar juu ya Mashindano hayo yatakayo fanyika nchini India mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na Michuano hiyo leo jijini
Timu ya Wachezaji wa Mchezo wa Kabaddi wakiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Bw Sandeep Arya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Mkenyenge Leo jijini


Timu ya taifa ya michezo ya kabbadi nchini tanzania inatarajiwa kushiriki kombe la dunia la michezo ya kabaddi yatakayoanza rasmi novemba mwaka huu katika jimbo la punjab.

Hayo yamebainishwa na balozi wa india nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kueleza kuwa mchezo huo utashirikisha jumla ya watu 34 kati yao ikiwa ni timu ya wanawake na timu ya wanaume pamoja na makocha wa nne.

"Tunafuraha kwa nchi ya tanzania kupata washiriki watakaoenda nchini india kushiriki kombe hilo la dunia la kabadi wanaume wakiwa kumi na tano na wanawake kumi na tatu wakiongozwa na makapteni wao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi idara ya maendeleo ya michezo,Alex NKenyenge ameongeza kuwa serikali ya Tanzania itazidi kutoa ushirikiano na nchi hiyo hususani katika michezo ya jadi huku akizitaka timu hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kuipeperusha bendera ya Tanzania."Michezo isiishie hapa hasa hii ya jadi bali ipewe kipaumbele zaidi iweze kufika mbali na hvyo viongozi wasing'ang'anie michezo iliyozoeleka"aliongeza kaimu mkurugenzi .

Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la punjab na mikoa mingine ya india ambapo hii ni mara ya sita kufanyika kwa kombe la dunia la mchezo huo ambapo kwa mwaka huu timu 13 kutoka sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki ambazo ni Tanzania,USA,England,Kenya,India,Mexico n.k.

TAARIFA YA SPIKA WA BUNGE OKTOBA 31,2016

IDARA YA ANGA YA ETIHAD KUTOA FURSA ZA AJIRA 425,000 AFRIKA.

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Idara ya anga ya Etihad, James Hogan

IDARA ya anga ya Shirika la ndege la Etihad kwa kushirikiana na wadau wake, wanatarajia kutoa takriban fursa 425,000 za ajira ikiwa ni pamoja na kutoa Dola za Marekani 3.6 milioni kwa lengo la kuinua uchumi wa Afrika mwaka 2016, fursa hiyo inatolewa kufuatia kukua kwa mji wa Abu Dhabi katika sekta ya biashara ya usafirishaji nje na ndani ya mji huo.

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Uchumi ya Oxford, inabainisha kwamba Idara hiyo ya anga pamoja na wadau wake wana mchango mkubwa katika kukuza uchumi barani Afrika na duniani kote ikiwa ni pamoja na kuunganisha vituo vya biashara na masoko yaliyopo.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba,Idara hiyo ya anga (EAG) na wadau wake wanatarajia kuchangia dola za Marekani1.1 bilioni katika uchumi na Sekta ya Utalii dola 2.5 bilioni. Licha ya hiyo, zitatolewa ajira 117,000 na zingine 308,000 katika sekta ya utalii.

Kwa Mwaka huu wa 2016, Shirika la ndege la Etihad linahudumia jumla ya vituo 117 vya abiria na pamoja na mizigo duniani kote. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kufikia abiria 19 milioni watakao hudumiwa kwa zaidi ya ndege 100,000 ambazo kati ya hizo, ndege 8,300 zitafanya safari za Amerika kwa abiria 1.1 milioni kutoka duniani kote.

Tangu kuzinduliwa kwa safari yake ya kwanza kwenda Misri mwaka 2004, Etihad imepanua wigo wa huduma zake barani Afrika, sambamba na ufunguzi wa vituo vingine zaidi katika nchi nane zingine zikiwamo Afrika Kusini, Morocco, Libya, Sudan, Kenya, Nigeria, Uganda na Tanzania.

Kiasi cha dola 1.1bilioni kilichotolewa, kinatokana na shughuli zinazofanywa na idara hiyo ya anga duniani kote,pamoja na  mchango wa wadau wake. Katika mchango huo, Idara ya anga pekee inatarajiwa kuchangia dola 400 milioni na fursa za ajira 3,900 mwaka huu. Kiasi hicho cha fedha kwa sehemu kubwa kitategemea   bidhaa zitakazo uzwa barani Afrika.

Afisa mtendaji mkuu wa idara ya anga ya Etihad, James Hogan amesema “ fursa za ajira zilizotolewa  katika  utalii, sekta ya usafirishaji, na huduma za vyakula zinatokana na uwepo wa idara ya anga ambayo imetoa fursa mbalimbali za ajira katika soko letu la Afrika, pia ni ishara ya kukua kwa sekta ya usafirishaji kupitia kitovu chetu cha biashara cha Abu Dhabi.”


Jumla ya wageni 1.1 milioni wanatarajiwa kuitembelea Afrika kupitia Shirika la Etihad na wadau wake mwaka huu. Wageni hao wanatarajiwa kukuza pato la Afrika kupitia sekta mbalimbali, ambapo pato la Afrika litaongezeka kufikia dola 2.5 bilioni sambamba na ajira 308,000 ifikapo mwaka 2024. 

Idadi ya wageni watakao wasili Afrika inatarajiwa kuongezeka na kuwa zaidi ya watu 3.2 milioni, ambapo idadi hiyo itakuza uchumi kufikia dola 5.6 bilioni na ajira 596,000.

Aidha, ripoti imeonesha namna faida iliyopatikana kutokana na kuimarika kwa huduma za anga zinazotolewa na Etihad zilivyoingizwa katika bajeti ya barani Afrika, juhudi hizi zinalenga kukuza uzalishaji ambao ni sawa na dola 1.1 bilioni kwa mwaka huu, ikiwa ni sawa na ajira 72,200. Hata hivyo, uzalishaji unatarajiwa kuongezeka kufikia dola 2.2 bilioni ifikapo 2024 ambapo ni sawa na ajira 145,000.

Idara ya anga alianzishwa mwaka 2014, ikiwa na vitengo vinne vya Shirika la Etihad, Uhandisi, kikundi cha Hala na wanahisa. Idara pia imewekeza katika mashirika saba ya ndege ambayo ni Air Berlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia, na Darwin Airline ya Uswisi, ambayo inafanya kazi kama sehemu ya Etihad.  

Hogan aliongeza kuwa, “wadau wetu ni sehemu muhimu ya kuendeleza shughuli zetu Afrika, tunawashukuru kwa ushirikiano wanao uonesha na tuko tayari kuitumikia Afrika kifanisi zaidi. Wadau wetu pia  ni sehemu muhimu ya kuimarisha shughuli zetu”

Kampuni ya Bayport yasherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwake pamoja na watoto wa KCVC

$
0
0


Mgeni rasmi, Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa, akiongea na wafanyakazi wa Bayport, waandishi wa habari na walimu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo hicho juzi, Kibaha mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport, John Mbaga, akiongea na wafanyakaziwa Bayport, waandishi wa habari na walimuwakituo cha kuleleawatotoyatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wakati wakusherehekeamiaka 10 ya Bayport ambayoilifanyikakatikakituohichojuzi, KibahamkoaniPwani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Bayport Tanzania wakiwa valisha fulana watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Kibaha Children Village Center, wakati wafanyakazi hao walipokwenda kusherehekea miaka 10 ya kampuni hiyo

Wafanyakazi wa Bayport wakipiga picha ya pamoja kwenye bango lao

Watoto wakibembea wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania

Watoto wakiwa wanakula pamoja kusherehekea miaka 10 ya Bayport Tanzania








Wafanyakazi wa bayport wakiwa katika picha ya pamoja naviongozi, watoto yatimanawatotowawafanyakaziwa Bayport Tanzania, wakati wa kusherehekea miaka 10 ya Bayport ambayo ilifanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kibaha Children Village Center (KCVC), wengine pichani (Kuliakwa Mama Mkapa) ni MkurugenziMtendajiwa Bayport John Mbaga na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano NgulaCheyo.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AKUTANA NA WASAMBAZAJI WA GESI MAJUMBANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha kampuni zinazohusika na usambazaji wa gesi majumbani pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini (PBPA).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kushoto) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini (PBPA), wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)
Watendaji kutoka kampuni zinazohusika na usambazaji wa gesi majumbani wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tanzania Association of Oil Marketing, Salum Busarara akieleza jambo katika kikao hicho.

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA USHINDI WA OLIVE KIARIE KATKA SHINDANO LA MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016

$
0
0
Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30. “Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.” Alisema Olive huku akitoka machozi baada ya kutangazwa mshindi. Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.



Hivi ndivyo ilivyokua pale OLIVE KIARIE alipotangazwa mshindi wa Maisha Plus East Africa 2016. #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu


A video posted by Maisha Plus (@maishaplus) on Oct 30, 2016 at 10:19pm PDT
Add caption

Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio waliofanikiwa kuingia fainali. Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa jana usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two. [caption id="attachment_148" align="alignnone" width="742"] Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce Sambuta, Alex Essau, Olive Kiarie, Irene Ishengoma na Ngenda Pilly.[/caption] Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya mshiriki mdogo wa kike. [caption id="attachment_150" align="alignnone" width="742"] Top 3 ya Maisha Plus Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishongoma, Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo. 880A9978880A0043880A0055  880A0125880A0127880A0129880A0130880A0132880A0134880A0166880A0169880A0172880A0184880A0210

Rais Magufuli asema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Tanzania katika Afrika

$
0
0

Rais Dkt John Pombe Magufuli, akilakiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya leo. Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakipokea salamu za kijeshi, katika viwanja vya Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya, alipowasili Ikulu jijini Nairobi leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza  mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika.


Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 31 Oktoba, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambako ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.


Rais Magufuli ambaye kabla ya Mkutano huo na waandishi wa habari amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, amesema takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.


Pia, Rais Magufuli amebainisha kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044.

"Naomba niwahakikishie kuwa uhusiano na ushirikiano wetu ni mzuri na utaendelea kuwa mzuri zaidi, na kwetu sisi Tanzania, Kenya ndio nchi ya kwanza kwa uwekezaji kuliko nchi zote za Afrika.


"Tunashirikiana vizuri katika uchumi, watu wetu wanafanya kazi pamoja, yapo makabila yetu ambayo yanaingiliana kwa shughuli zao za kila siku na hata wanyamapori wetu wanazunguka katika nchi zote mbili bila kujali mipaka"amesema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa Serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na Kenya ulioasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na amewakaribisha wafanyabiashara wengi zaidi wa Kenya kuwekeza nchini Tanzania.


"Kabla ya kuja hapa nimekwenda kutoa heshima katika kaburi la Mzee Jomo Kenyatta, kwa kweli nimeguswa sana na kazi kubwa iliyofanywa na wazee wetu, naomba niwahakikishie kuwa tunawathamini sana ndugu zetu Wakenya na tutaendelea kufanya hivyo" amesisitiza Dkt. Magufuli.


Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake na amemhakikishia kuwa Kenya itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Tanzania."Kwetu sisi Tanzania ni ndugu zetu, ni kaka na dada zetu tunao ushirikiano wa siku nyingi na wa kidugu na tutahakikisha tunauendeleza ushirikiano na uhusiano huu mzuri ulioasisiwa na wazee wetu" amesema Mhe. Kenyatta.


Rais Kenyatta amesema Tanzania na Kenya ni nchi zinazofanana kwa mambo mengi muhimu ikiwemo kubadilishana uongozi wa Serikali kwa njia ya amani na ameongeza kuwa katika mazungumzo yao wamekubaliana kuwa nchi hizi zitaendelea kuzisaidia nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazokabiliwa na matatizo mbalimbali.


Aidha, Rais Kenyatta amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara ya Bagamoyo (Tanzania) hadi Malindi (Kenya) pamoja na mambo mengine ambayo Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili (Joint Commission Cooperation) itayaainisha.


Baadaye leo, Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa katika Ikulu ya Nairobi aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta na Kesho anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldovillekilichopo Karen Jijini Nairobi, na  kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi

31 Oktoba, 2016


Rais Dk. Shein akutana na ujumbe wa JICA kutoka Japan

$
0
0







Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki (wa pili kulia) alipofika na ujumbe aliofuatana nao leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.

RAIS DKT. MAGUFULI AANDALIWA DHIFA YA KITAIFA NCHINI KENYA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Nairobi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glass na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo huku akiwa amewashika mikono kwa pamoja Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Kenya William Ruto na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margaret Kenyatta katika dhifa hiyo ya kitaifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mabalozi mbalimbali wa Kenya waliohudhuria katika dhifa hiyo ya Kitaifa. PICHA NA IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOV 1,2016

ZIFF ANNOUNCES NEW FESTIVAL DIRECTOR

$
0
0
 As the Zanzibar International Film Festival prepares for its 20thannual edition, The Board of Directors is proud to officially announce the appointment of a new Festival Director. Fabrizoi Colombo will follow in the footsteps of Dr. Martin Mhando who stepped down in 2016 after nearly 10 years at the helm.  The ZIFF Board of Directors has officially confirmed that Fabrizio Colombo will take over as ZIFF Festival Director from November 2016 and will be responsible for overseeing the festival as it enters into its 3rd decade.

Fabrizio is no stranger to ZIFF or Zanzibar, having played a critical role in ZIFF for the past 5 years as Assistant Festival Director. Fabrizio’s passion for cinema, and particularly African cinema, has developed over many decade’s worth of development and media work across Europe and Africa.

Fabrizio has worked across various media platforms since the 1980’s with a particular focus on training and development within the sector. In addition to his work at ZIFF, Fabrizio was the Acting Director of the African Film Festival of Verona from 2006-2012, and also held the position of Programmer and Artistic Director at the KIKAKA African Film Festival in Florence Italy for a number of years. Fabrizio Colombo is director of the of office of the world association for media SIGNIS in Rome.
 
Fabrizio has an extensive knowledge of, and an unmatched passion for, African cinema and over the past few years at ZIFF he has become an invaluable resource in terms of his organizational skills, programming ability, as well as for his communication and management skills.

Former ZIFF Festival Director, Dr. Martin Mhando has this to say of his replacement, “ZIFF could not have found a better replacement for the position of Festival Director. Fabrizio's knowledge of world cinema, his flare for the arts, his experience in festival management and in the ZIFF festival ethos, makes him the natural successor. ZIFF is in very capable and safe hands.”

Fabrizio has committed to putting film at the centre of next year’s festival that will celebrate the theme, Finding Joy, Kusikaa Furaha.  With Fabrizio officially leading the way to 2017, supported by a full team of dedicated staff, major announcements will be coming soon in regards to film submissions and programming.

The ZIFF Board of Directors would like to take this opportunity to thank Dr. Martin Mhando for his many years of devoted and committed service, and to welcome Fabrizio into his role going forward.

For continued  festival updates,  please visit www.ziff.or.tzwww.facebook.com/zanzibarinternationalfilmfestival , twitter @ZIFF_2016 and Instagram Zanzibarinternationalfilmfest


JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU 200 KWA MAKOSA MBALMBALI

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha panga ambazo wamezikamata katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha gari la Polisi likiwa linabeba mzigo wa bangi uliokatwa na Polisi katika msako ulifanyika jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni walizozifanya hivi karibuni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha bunduki ambayo iliangushwa na wtu wanaodhaniwa kuwa majambazi leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro akionyesha kwa waandishi habari begi la bangi ambalo lilikuwa likiinga Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu zaidi ya 200 kwa tuhuma mbalimbali likiwemo kwa watu Raia wa China kutapeliwa dola za kimarekani 800 kwa kutumia jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema kukamatwa kwa watu hao imetokana na operesheni zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wananchi na mali zao wanaishi kwa amani.

Amesema katika waliokamatwa ni pamoja ni panya road saba waliomvamia Nyumbani kwa Askari wa Jeshi la Wananchi , Ladislaus Kaitaba.

Katika tukio waliweza kukamata mtandao wa panya road kwa kutumia Ramadhani Ndabi (35)ambaye alichukua simu ya askari hiyo baada ya kupiga akapatikana na kuanza kutaja wenzie wanaofanya matukio.

Aidha amesema kuwa wizi wa magari unaendelea lakini polisi waliweza kukamata gari lilokuwa likiuzwa kwa kujifanya wateja na ilipogundulika walioiba wakatoweka.

Kamanda Sirro amesema kuwa bangi imekuwa ikiingzwa kwa njia nyingi na sasa watu wanatumia mabegi wakiwa wasafiri kumbe wanakuwa wameweka bangi.

Waziri Jafo aonya udanganyifu kwenye mtihani kidato cha nne inayoanza leo.

$
0
0

wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo. 

Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi selemani jafo akiagana na wanafunzi wa  shule ya sekondari msalato mara baada ya kuzungumza nao.

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake.

Ameeleza hatarajii mitihani hiyo ifanyike kinyume na kuwataka walimu wasisubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.Jafo ame sema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi wa mitihani na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.

Akizungumza na wanafunzi, Jafo amewataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.

Hata hivyo amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka kuwajibika ipasavyo.

RAIS PAUL KAGAME AENDESHA GARI KUMSINDIKIZA MFALME WA MOROCCO KWENDA UWANJA WA NDEGE.

$
0
0
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameendesha gari kumpeleka mfalme wa Morroco Mohammed VI katika uwanja wa ndege baada ya kukamilisha ziara yake nchini humo.

TAZAMA BUNGE LA 11 HAPA


MWAKA MMOJA WA JPM, TRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA MAPATO.

$
0
0
 YAKUSANYA WASTANI WA TRILIONI 1.1 KILA MWEZI
Na JOVINA BUJULU- MAELEZO.


Novemba Tano mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, Watanzania wameshuhudia mafanikio makubwa katika katika sekta ya ukusanyaji kodi kupitia vyanzo mbali mbali vya mapato. Hatua hii inatokana na kuwa Rais Magufuli alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayekwepa ulipaji kodi na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanadai risiti kwa kila bidhaa au huduma wanayolipia.

Hivyo Serikali hii tangu ianze kazi rasmi imekuwa ikitilia mkazo ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza makusanyo ya Serikali.Juhudi hizi za Rais Magufuli za kuongeza mapato na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali zimejionyesha katika mikutano yake mingi ambapo mara nyingi amekuwa akisema “Ukinunua bidhaa dai risiti na ukiuza bidhaa toa risiti”.

Jitihada hizo za wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa zitatekelezwa na uongozi wa Rais Magufuli zinaunga mkono wosia aliwahi kuutoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo alisema kuwa “Serikali yeyote isiyokusanya kodi ni “corrupt”.

Hatua hiyo ya kutoa na kudai risiti ina mchango mkubwa kwa serikali katika kukusanya kodi ambazo zitasaidia katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji, umeme, usafirishaji, ujenzi na uendeshaji wa serikali kwa ujumla kutokana na mapato yanayopatikana.

Hapa nchini, Mamlaka ya Mapato (TRA) ndicho chombo chenye jukumu la kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Taifa na imekuwa ikitimiza lengo hilo kwa kutekeleza mikakati mbalimbali kama ilivyoainishwa katika mpango mkuu wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo, katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli kumekuwepo na ongezeko la makusanyo ya mapato ya serikali yatokanayo na kodi.

Anasema kuwa katika kipindi hiki, TRA inakusanya wastani wa trillion 1.1 kila mwezi kuanzia mwezi Novemba, 2015 hadi Septemba 2016.
“Hili ni ongezeko la asilimia 28.1 kutoka kwenye kukusanya wastani wa shilingi bilioni 867 kwa mwezi katika kipindi cha mwezi Novemba, 2014 hadi Septemba 2015” anasema Bw. Kayombo.

Makusanyo ya mapato katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli kuanzia mwezi Novemba 2015 yamekuwa yakiongezeka ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kwa mfano mwaka wa fedha 2015/2016 mapato yaliyokusanywa yalikuwa shillingi trilioni 12.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.4 ya makusanyo ya mwaka 2014/2015. Aidha TRA imekwisha kusanya kodi kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwezi Septemba 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.4 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha robo mwaka 2015/16.

Bw. Kayombo anaongeza kuwa kwa sasa TRA inatekeleza mpango mkakati wa nne wa ukusanyaji kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani kwa kuongeza ulipaji kodi wa hiari.

“Jitihada mojawapo zinazofanywa na TRA ni pamoja na kuboresha mifumo ya makusanyo inayoendana na mazingira ya sasa ya ukuaji wa teknolojia ili kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa urahisi kama ilivyo dhamira yake ya kurahisisha ulipaji kodi na kufanya mazingira yawe bora” anasema Bw. Kayombo. Katika kipindi cha mwaka mmoja ambao Rais Magufuli amekuwa madarakani, juhudi mbalimbali zimefanyika ili kuhakikisha matarajio ya Rais ya kuimarisha makusanyo ya kodi na kudhibiti mianya ya rushwa yanafanikiwa.

Mafanikio hayo yatamuwezesha Rais Magufuli kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zikiwemo kuboresha afya, upatikanaji wa maji, umeme, kutoa elimu bure, ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, reli na barabara. Aidha makusanyo hayo yatawezesha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa wananchi na serikali kuweza kujitegemea na hivyo kupunguza utegemezi wa misaada kutoka kwa wafadhili.

Bw.Kayombo anataja kiini cha ongezeko la kukusanya kodi kuwa ni matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD) ambazo zinatumika zaidi badala ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono. “Matumizi ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono hayakuwa na ubora mzuri wa kukusanya na kuongeza mapato na kutunza kumbukumbu sahihi ambayo yaliifanya serikali ipoteze mapato mengi” anaongeza.

Katika hatua nyingine TRA ilitoa mashine za EFDs 130 bure kwa makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali kwa ajili ya taasisi za serikali ambazo zinakusanya maduhuli ya serikali kwa nia ya kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.

Katika kuhakikisha makusanyo ya kodi yanaongezeka TRA imeendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kufichua wakwepa kodi, kupambana na rushwa na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa sambamba na kuendesha zoezi la kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) linaloendelea jijini Dar es Salaam kwa sasa ili kuboresha daftari la walipa kodi.

Pamoja na mafanikio hayo Kayombo alizitaja changamoto wanazokutana nazo katika ukusanyaji kodi kuwa ni pamoja na taarifa za kodi kutowafikia wananchi wote ili kujenga uhiari wa kulipa kodi na uwepo wa ukanda mrefu wa Pwani unaosababisha kuwepo mianya mingi ya ukwepaji kodi ambapo bidhaa huingizwa nchini kwa njia za panya.

Pamoja na changamoto hizo, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeendelea kubuni mikakati mbali mbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “HAPA KAZI TU” ili kutimiza na kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.

Utaratibu wa ajira kwa watanzania wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati kuangaliwa upya

$
0
0


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Watanzania 5600 wanakadiriwa kufanya kazi katika kada za madaktari, walimu, wauguzi, wahadhiri, wapishi, wahudumu wa mashambani na bustani na watumishi wa nyumbani, na kati ya hao karibu watanzania 200 ndio wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.

Kada inayofanya kazi za ndani ndio inayopata changamoto nyingi huko ugenini ikiwemo ujira mdogo na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji. Jambo hili halipaswi kufumbiwa macho. Hata hivyo zipo jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimefanyika kupunguza ama kuondoa hali hii.

Kufanya kazi nje ya nchi bila mateso au manyanyaso ni haki ya binadamu kama inavyoainishwa katika mikataba ya kimataifa. Katika makala hii utaweza kuona baadhi ya vipengele vya mikataba hiyo.

Mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia na kisiasa wa mwaka 1966, unataja haki mbalimbali za kiraia zinazolindwa na mkataba huo ikiwa ni pamoja na haki ya kutopewa mateso au kufanyiwa ukatili au vitendo vya kikatili na udhalilishaji ikiwemo hukumu za kikatili katika ibara ya 7. Uhuru wa mtu na usalama wake katika ibara ya 9 na uhuru wa mtu kwenda atakako na kuchagua mahala pa kuishi katika ibara 12.

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 17 Kifungu cha (1) kinampa haki raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kwenda kokote ndani na nje ya nchi bila kuvunja sheria za nchi. Kwa misingi hiyo watanzania wanapata fursa za kwenda nje ya nchi, hususani nchi za kiarabu kwa lengo la kufanya kazi za ndani ili kujiongezea kipato na kuweza kuinua uchumi wa familia zao na pamoja na taifa kwa ujumla.

Lakini jambo linalovutia idadi kubwa ya watanzania kwenda kufanya kazi katika nchi za Mashariki ya Kati ambazo ni Omani, Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, Kuwait, Lebanon, Syria, Iran, Iraq na Yemen pamoja na nchi zinazounda Falme za kiarabu ambazo ni Abu dhabi, Dubai, Ajman, Al Ain, Fujuirah, Ras al Khaimah na Sharjah ni uhusiano wa karibu sana ambao ni wa kihistoria na kidamu, ambapo nusu ya familia za Oman asili yake ni Tanzania na hivyo kufanya kuwa na mwingiliano wa karibu.

Lakini pia, nchi hizi kwa kiasi kikubwa ni tegemezi ya nguvu kazi kutoka nje ya eneo hilo na hivyo kusababisha soko kubwa la ajira katika maeneo mbalimbali kama vile madaktari, wauguzi, madereva, wapishi, wahudumu wa saluni, watumishi wa shambani na hasa watumishi wa nyumbani(house maids).

Asha Abdallah (si jina halisi) mwenye umri wa miaka 25, aliacha familia yake ya mume na mtoto mmoja, na kwenda kufanyakazi za ndani nchini Omani akiamini kuwa atapata kipato kitakachosaidia kuitunza familia yake nchini Tanzania.Hata hivyo, maisha yake ya nchini Omani yameififisha ndoto yake, kwa vile imemlazimu kurudi nchini Tanzania kwa visa vilivyomkumba nchini humo.

“Nilinyanyasika mno, kazi zilikua nyingi sana, sikuwa napata muda wa kupumzika, hata chakula nilikula kwa uoga, nilipoona siwezi kuvumilia zaidi baada ya kukaa mwaka mmoja ilinilazimu kusema nimefiwa na muwe wangu ili mradi nirudi nchini Tanzania”, anasema Asha. Hadi kufikia Januari mwaka huu karibu watanzania 200 wameajiriwa katika kazi za utumishi wa nyumbani nchini Omani.

Naye, mwanamke mmoja mwenye asili ya Tanzania (jina limehifadhiwa) aliyekuwa akifanya kazi ya uwakala wa kusafirisha wasichana kutoka Tanzania kwenda kufanya kazi za ndani nchini Omani, anasema ni kweli kumekuwepo na changamoto nyingi katika kazi hiyo, na wakati mwingine changamoto hizo si za kweli ama zinakuzwa.

“Nilifanyakazi hii kwa miaka 10, nimeacha hivi karibuni baada ya kuona inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ya wasichana wanasafirishwa hadi Omani na wanapofika huku wanakua hawako tayari kufanya kazi kulingana na makubaliano ya kazi yenyewe”.

Anaongeza kuwa,“Wengine wanajisahau kama huku si Tanzania na hivyo lazima waendane na maisha ya huku, hata hivyo naishauri Serikali ya Tanzania na Omani kupatia ufumbuzi changamoto zenye ukweli kwa vile hivi karibuni kumekuwepo na visa vingi kuhusu wasichana wa kazi hapa Omani”, anasema wakala huyo.

Licha ya kuwa ni kazi inayowapatia kipato watanzania hao, kumekuwepo na malalamiko kadhaa ikiwemo mazingira magumu ya kufanyia kazi, kufanyakazi masaa mengi, kukosa mapumziko, mshahara mdogo, kufanyishwa kazi za ziada ya makubaliano pamoja na kunyanyaswa kijinsia.

Katika kupambana na hali hii Serikali imeandelea na utaratibu wake wa kawaida pamoja na kuanzisha utaratibu mpya ambao utasaidia kudhibiti changamoto mbalimbali zinazowakumba watanzania wanaokwenda kufanyakazi za utumishi wa ndani nchini Omani pamoja na nchi nyingine za Mashariki ya Kati.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima anasema Ubalozi kwa kushirikiana na wadau wengine kama Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Wakala wa huduma za ajira Tanzania (TAESA), Kamisheni ya kazi Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa wamekua wakifanya kazi kwa karibu ya kufuatilia watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi na hasa nchini Omani.

“Watanzania wanatakiwa kufahamu na kufuata utaratibu ambao unamtaka raia wa Omani mwenye nia ya kumwajiri mtanzania kuwa anatakiwa kwenda katika Ubalozi wa Tanzania na kujaza fomu ya maombi ya kumwajiri mtanzania na baada ya fomu yake kuridhiwa na Ubalozi, basi atapewa mkataba ambao atajaza na kuurudisha Ubalozi”, anasema Balozi Kilima.

Balozi Kilima anaongeza kuwa, “Mhusika anaporudisha fomu hiyo anatakiwa kuambatisha nakala ya kitambulisho cha utaifa, uthibitisho wa makazi, nakala ya pasi ya kusafiria ya mfanyakazi, hati ya kiapo na dhamana ya fedha za Omani kiasi cha rial 100”.

Baada ya Ubalozi kuridhika na vielelezo vyake, ubalozi utapitisha mkataba wa kumtaka mwajiri husika kuuwasilisha nchini Tanzania kwa mtumishi husika ambae atauwasilisha TAESA au Kamisheni ya kazi ambao nao watamhoji mhusika pamoja na kujidhihirisha kama ameuelewa mkataba na kazi atakayofanya na baada ya hapo mwajiri huyo wa kitanzania ataruhusiwa kwa kupewa kibali ambacho ni barua ya kumuomba Kamishna wa Uhamiaji kutoa ruhusa ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi baada ya kufuata utaratibu uliowekwa.

Aidha, Serikali imeweka mkazo katika hatua kadhaa katika kutatua tatizo hili, ambapo imeanza kutumia wakala rasmi wa ajira ambao wameandikishwa na mamlaka husika.Kutumia mkataba wa ajira na kuhakikisha kila Ubalozi wa Tanzania katika nchi za Mashariki ya Kati unandaa mikataba ya kazi kutokana na muongozo uliokubaliwa na wadau wote.

Vilevile, Serikali inaandaa mtaala wa kuongeza ustadi na ujuzi kwa watanzania wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.Aidha, Balozi huyo amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuanzisha mtaala huo ni katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba nazo watanzania wanaofanyakazi za ndani nchini Omani.

“Serikali imeazimia kutumia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ili kuwa na mtaala utakaosaidia kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo utaratibu na utamaduni wa nchi mbalimbali wanazokwenda kufanya kazi, ili kusaidia watanzania kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kazi husika na changamoto zake kabla ya kukubali kufanya kazi hizo,” anasema Balozi Kilima

Sambamba na hilo, Serikali imeendelea kuwataka watanzania kufuata utaratibu kabla ya kwenda kufanya kazi katika nchi hizo kwa kutumia wakala rasmi wa ajira walioandikishwa na mamlaka husika pamoja na kuwepo mkataba wa ajira unaotambuliwa na Mamlaka za nchi wanazookwenda ili kuepuka usumbufu na changamoto wanazoweza kuzipata ikiwemo kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.




Balozi Kilima ameongoza kuwa katika kupata suluhisho la kudumu katika kuwasaidia watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi,Wizara kwa kushirikiana na wadau imeendelea kufanya jitihada za kusaini Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya ajira na kazi baina ya Serikali ya Tanzania na nchi mbalimbali.

WADAU WA HABARI WALIVYOSHIRIKI KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA ZA HABARI.

$
0
0

Jovina Bujulu.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari. Muswada huu utatoa mwelekeo na dira ya tasnia ya Habari katika utendaji kazi wake.

Kabla ya kuwasilisha muswada huu Bungeni Serikali ilipokea maoni kutoka kwa wadau wa habari, vyama visivyokuwa vya Kiserikali (NGO’s) na taasisi mbali mbali kuhusu namna na jinsi wanavyotaka muswada wa habari uwe mwongozo wa tasnia ya habari.Miongoni mwa wadau ambao walifikisha maoni Serikalini ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania ( MCT), Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB), Tanganyika Law Society, Sikika pamoja na Nation Organization for Legal Assistance (NOLA).

Wadau wengine ni Jukwaa la Wahariri (TEF), Kituo cha Haki za Binadamu (LHCR), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Tanzania Human Rights Defenders (THRDs), Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Nchi za Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Baadhi ya mambo yaliyowasilishwa Serikalini na wadau hao mnamo Machi, 31, 2016 ni pamoja na kuimarisha utendaji wa vyombo vya habari nchini, kuendeleza weledi katika taaluma ya habari na kulinda usalama wa wanahabari.

Mapendekezo yao kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyopo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambao umewasilishwa ili ujadiliwe katika kamati ya Bunge na Huduma za Jamii. Kamati hii na wadau inakutana mjini Dodoma kwa sasa.Baadhi ya mambo yaliyomo katika muswada huu ni pamoja na kuunda Bodi ya Ithibati, ambayo itatoa ithibati na vitambulisho kwa wanahabari,kusimamia kanunu za maadili ya wanahabari na kuishauri Serikali katika suala la elimu na mafunzo kwa wanahabari.

Kwa kuangalia baadhi ya maoni yaliyopendekezwa na wadau, na masuala yaliyomo katika muswada huu wa sheria inayopendekezwa, yote yameegemea katika kuipa tasnia hadhi kwa kuzingatia vigezo vya weledi, maadili na elimu kwa wanahabari.Aidha, wadau waliwasilisha kuwa uwepo uhuru wa vyombo vya habari na kwamba wanahabari wawe huru kutafuta, kuchunguza na kuchapisha habari bila kuingiliwa.

Suala hili lipo katika muswada wa sheria inayopendekezwa na kwamba hakuna mwandishi ayekatazwa kutafuta na kuchapisha habari ila muswada lakini uhuru huo sio kigezo cha kuingilia sheria nyingine.Wadau hao pia walipendekeza sheria ijayo itoe fursa kwa Serikali kuendelea kusajili vyombo vya habari bila kuweka masharti , jambo ambalo lipo pia katika sheria inayopendekezwa kwamba Serikali itaendelea kusajili kwa kuzingatia kanunu, sheria na taratibu zilizopo.

Kuhusu suala la ulinzi na usalama wa waandishi , wadau walipendekeza kuwa wamiliki wa vyombo vya habari wawe na wajibu wa kuzingatia usalama wa wanahabari wanapokuwa kazini ,suala ambalo limo katika muswada wa sheria inayopendekezwa ambapo inamtaka kila mwajiri kuweka Bima na hifadhi ya jamii kwa kila mtu aliyeajiriwa katika chombo cha habari husika.

Kutokana na tasnia ya habari kukosa taasisi inayosimamia wanahabari na vyombo vya habari, muswada wa sheria hii umekuja wakati muafaka kwani endapo itapitishwa itakuwa mkombozi wa wanahabari na tasnia yenyewe. Aidha sheria hii itawapa wanahabari mwelekeo wa kazi na kujua ni mahali gani wanakosea na jinsi ya kujisahihisha. Hii ni kutokana na kuwepo kwa Baraza Huru la Habari ambalo litaandaa na kuidhinisha kanuni za maadili ya wanahabari.

Kwa wadau wa habari, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kiu ya kupata chombo ambacho kitaelekeza na kuongoza tasnia hii, huu ni wakati muafaka kwao kuiunga mkono muswada wa sheria hii ili upitishwe kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.Tumeona manufaa mengi ya elimu na weledi kwa wanahabari,kwa kuwepo kwa mfuko wa mafunzo ya habari, usalama wao kwa kuwataka waajiri wao kuwawekea bima. Kwa kupitisha sheria hii wanahabari watatekeleza wajibu wao kwa weledi na ufanisi zaidi.

SEMTAWA NJE WIKI MBILI ZAIDI

$
0
0
KIUNGO mahili wa Mbeya City Fc , Ayoub Semtawa atalazimika kusubiri kwa majuma mawili zaidi kuweza kurejea uwanjani, kufutia majeraha ya kuchanika nyama za paja mguu wake wa kulia kwenye mchezo dhidi ya African Lyon uliochezwa jijini Dar,wiki moja iliyopita.

Kwa mujibu wa daktari wa kikosi, Dr Selaphini Mushi, Semtawa alichanika vibaya nyama za paja baada ya kugongwa na mlinzi wa Lyon wakati alipokuwa akijaribu kukontroo mpira wa juu na kulazimika kutolewa nje kwa msaada baada kushindwa kabisa kutembea kufuatia tukio hilo lililotokea kwenye dakika ya 60 ya mchezo huo.

“Baada ya kutolewa ilitulazimu kumpa magongo ili aweze kutembea kwa sababu alikuwa hawezi, juma moja limepita sasa ameacha kutumia magongo na anaweza kutembea mwenyewe, taratibu za matibabu zinaendelea lakini atalazimika kusubiri wiki mbili zaidi ili kuweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida na hatimaye kuingia tena uwanjani, hatuna shaka sana na hali yake kwa sasa na imani yangu kubwa baada ya muda huo atakuwa tayari kwa kuitumikia timu” alisema.

Katika hatua nyingine Dr Mushi alithibitisha kupona na kuanza mazoezi kwa golikipa Owen Chaima ambaye alitolewa nje kwenye mchezo uliopita dhidi ya Majimaji kufutia maumivu makali ya mgongo aliyopata wakati akiwa kwenye mchezo.

“Chaima alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Fikirini Bakari, alipata maumivu makali wakati akiwa kwenye mchezo, jambo jema ni kuwa baada ya matibabu sasa yuko fiti kabisa na amefanya mazoezi siku ya jana na leo atafanya pia kwa ajili ya kujiweka sawa tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga hapo kesho kama ilivyo kwa mshambuliaji Geofrey Mlawa ambaye naye aliumia lakini sasa yuko kwenye hali nzuri kabisa” alimaliza.
 

MAKAMU WA RAIS APOKEA UJUMBE MAALUM KWA NIABA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKA KWA RAIS WA CONGO BRAZZAVILLE

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ujumbe maalum kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa Rais wa Congo Brazavile Mhe. Denis Sassou Nguesso uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo Mhe. Jean Claude Gakosso (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya Congo Brazzaville Mhe. Jean Claude Gakosso (kushoto) ambaye alimkabidhi Makamu wa Rais wa Ujumbe Maalum wa Rais John Pombe Magufuli kutoka kwa Rais wa Congo Brazzaville Mhe. Denis Sassou Nguesso, Ikulu jijini Dar es salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images