Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

YANGA YAIPASUA MBAO 3-0

$
0
0
 Golikipa wa Mbao FC, Emanuel Mseja akiruka kudaka mpira bila mafanikio uliokwenda moja kwa moja wavuni baada ya kurushwa na Mchezaji wa Yanga, Mbuyi Twite na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 3-0.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mbao Fc ya mkoani Mwanza na kufikisha alama 27 nyuma ya alama tano kwa mahasimu wao wa jadi Simba.

Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu sana kwa Yanga hasa baada ya Mbao kuonekana wako makini katika kuhakikisha hawaruhusu goli la mapema na mpaka zinafikia dakika 45 za kipindi cha kwanza timu hizo zilienda mapumziko 0-0.

Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kwa Yanga kutafuta goli la dakika ya 53, mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima na kumfanya golikipa wa Mbao kushindwa kuudaka na baada ya beki wa kimataifa wa Yanga toka nchini Togo, Vicent Bossou kuumalizia kwa kichwa na kuiandikia Yanga goli la kwanza.
 
Dakika ya 55, Mkongo Mbuyi Twite anarusha mpira unaomponyoka golikipa wa Mbao, Emanuel Mseja na kuingia nyavuni na kuiandikia Yanga goli la pili na Amisi Tambwe akitumia madhaifu ya mabeki hao na kuiandikia Yanga goli la tatu na la ushindi.

Mabadiliko ya Yanga yaliifanya safu ya ulinzi ya Mbao kuanza kucheza kwa umakini zaidi hasa baada ya kuingia Donald Ngoma na kutoka Obrey Chirwa, Deus Kaseke kutoka na kuingia Juma Mahadhi pamoja na Hassan Kessy na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo Thaban Kamosoku.

Baada ya ushindi huo, Yanga wanakwea pipa hadi Jijini Mbeya kwenda kuvaana na Mbeya City Novemba 02, na kumaliza na Prison Novemba 06  kabla ya kurejea tena Dar es salaam kuvaana na Ruvu Shooting Novemba 11.

































TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA UPOTOSHAJI WA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII JUU YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016

$
0
0
  Hivi karibuni kumeibuka upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira nzima ya Mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016,aliyevishwa taji hilo jana usiku ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zikieleza upotoshaji wa taarifa mbalimbali za mlimbwende huyo zikiwemo na elimu yake.

SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;

MISS TANZANIA 2016
🙊🙊🙊🙊🙊🙊
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
😂😂😂😂😂😂
Ingawa sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili


HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016,DIANA EDWARD LOY.

Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.

Ahsanteni.

Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
(wilflow101@gmail.com).

MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ARUSHA WAMSHANGAZA KAMANDA MPINGA

$
0
0
Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL
Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akikagua "Birthday Surprise Cake " aliyopewa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akipokea Chupa ya Shampeni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bw. Bakari Msangi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akigonga Cheers na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga wakishiriki shampeni na Mabaozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Daniel Urioh akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga huku kulia akishuhudiwa na Mwenyekiti. Bi. Stella na Kushoto ni Balozi Wilbard Ngambeki katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Mustafa Panju akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Wilbard Ngambeki akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Seria Tumainiel akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga huku mwenye kiti akishuhudia katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akikata "Birthday Surprise Cake " huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Mustafa Panju akimlisha keki Kamanda Mpinga kwa niaba ya wazee waliopo katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Balozi Vero Ignatus akimlisha keki Kamanda Mpinga kwa niaba ya wadada waliopo katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mpinga akimlisha Keki Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akimlisha keki Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani wakipongezana na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akifurahia mlo wa usiku na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akipata mlo wa usiku na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.


Mabalozi wakizungumza na kufurahi ujio wa Kamanda Mpinga Jijini Arusha na kututafuta Mabalozi katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. Picha Zote na Gadiola Emanuel.

Na Vero Ignatus, RSA Arusha. 

Mabalozi wa usalama wa barabarani (Road Safety Ambassadors - Arusha) wamesherehekea sikukuu ya kuzaliwa ya Kamanda Mohammed Mpinga jijini Arusha.  Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Milestone Park -Sakina , imeandaliwa na kamati ya (RSA -Arusha) chini ya mwenyekiti wa mkoa Bi. Stella Rutaguza na kuhudhuriwa na wajumbe wa( RSA - Arusha)  "Kwakweli mmenistua jamani sikutegemea kama mmeniandalia jambo kubwa kama hili ,nilijua nakuja kukutana tu na mabalozi ili kufahamiana na kuongelea maswala yetu ya usalama barabarani "alisema Mpinga. 

DCP Mpinga mbaye yupo kikazi jijini Arusha alikutana na mabalozi wa usalama barabarani,kwa lengo la kuongelea na kujadili maswala ya usalama barabarani na mabalozi hao,ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha jamii,kukemea na kuripoti matukio yanayoathiri usalama barabarani,na kushawishi mabadiliko ya tabia ,sheria na sera. 

Amezungumzia changamoto iliyopo kwa sasa kwa utoaji wa risiti pale dereva anapotakiwa kulipa faini kutokana na makosa yanayofanyika barabarani,amesema kuwa mfumo huo wa kieletroniki tayari umeshaanza kutumika jijini Dar-es-salaam na hivi karibuni mfumo huo utaanza kutumika katika mikoa sita iliyopewa kipaumbela kabla ya mwaka huu kumalizika.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha,Pwani,Morogoro,Mbeya,Dodoma,na Mwanza,na amewataka askari wa usalama barabarani kutumia lugha njema kuwaelewesha madereva pale wanapohitaji kupewa risiti za( EFD)ili waweze kutambua changamoto hiyo kwa sasa ambayo serikali inalishughulikia. Kwa upande wake mkurugenzi wa Bushbuck safaris Bw. Mustafa Panju amemuomba mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha SSP. Eng.Nurum Suleimani ampe ruhusa ya kutoa mafunzo kwa askari wa usalama barabarani Arusha kuhusu huduma kwa mteja.

"Nipo tayari kutoa ofa ya mafunzo kwa askari wetu wa kikosi cha usalama barabarani ukinipatia nafasi ,na hii itasidia sana " Alisema Panju.  Naye mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bi. Stella Rutaguza amempongeza Kamanda Mpinga katika siku yake ya kuzaliwa na
kumtakia maisha marefu, yenye afya tele.

Bi. Stella ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha kutakuwa na oparasheni Abiria paza sauti itakayofanyika kwa miezi mitatu lengo kuu likiwa ni kumjengea uwezo na kumuhamasisha dereva na abiria kuchukua tahadhari kuepuka ajali.

Amesema kampeni hii inalenga kumfanya abiria atambue haki na wajibu wake ,akiwa kwenye basi APAZE SAUTI pale panapotokea uendeshaji hatarishi barabarani,na pia kumfanya dereva abadili mtazamo wake na kujenga utamaduni wa usalama barabarani,hii inamfanya dereva na abiria
kuwa sehemu ya suluhisho la ajali za barabarani.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 31

Kitabu kinachoelezea mbinu zinazotumiwa na watu matajiri kufanikiwa kimaisha chazinduliwa Dar

$
0
0

Imeelezwa kwamba watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa na mipango ya kimaisha ambayo wanaweza kuifanyia kazi ili waweze kufanikiwa kama jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wanaonekana kuwa na mafanikio.

Hayo yamesemwa na Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka wakati wa uzinduzi wa kitabu hcho ambacho kinnaelezea mbinu 60 ambazo zinatumiwa na watu waliofanikiwa kimaisha kuweza kufikia alengo ambayo wamejiwekeakatika maisha yao.

Nanauka alisema watu wengi wamekuwa wakitamani kufanikiwa lakini wamekuwa hawajui ni hatua gani za kupitia na kufanikiwa na baada ya yeye kufanya utafiti wa muda mrefu kwa watu mbalimbali duniani waliofanikiwa na wasiofanikiwa, ameweza kupata mbinu 60 ambazo ndiyo zinatofautisha watu wa matabaka hayo mawili

Alisema kupitia kitabu hicho msmaji ataweza kufahamu ni mambo gani anatakiwa kufanya na yapi hatakiwi kufanya ili kufanikiwa kama wengine kwa kuzingatia mbinu ambazo pia zimekuwa zikitumiwa na watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kama biashara, michezo, sanaa na hata uongozi.

"Watu wengi wanapenda kufanikiwa lakini kama huna malengo huwezi kufanikiwa, watu wengi hawajui wanatumia njia gani ili kufanikiwa na hadi wanaondoka duniani wanaondoka na ndoto walizokuwa nazo, ndoto ambazo zilitakiwa kubaki zikifanya kazi duniani,

"Sababu ya kuandika kitabu hiki ilianza nipotaka kujua utofauti wa waliofanikiwa na wasiofanikiwa, aliyefanikiwa kwa aliye Marekani na Tanzania na asiefanikiwa aliye Tanzania a Mareani, nilianza kusoa kwanini wengine wanaweza kufanikiwa katikati ya mamilioni ya watu na baada ya kupata mawazo ya jumla ndiyo nikapata mbinu 60 ambazo zipo katika kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO," alisema Nanauka.

Nanauka alisema kitabu hicho kitakuwa kikuzwa kwa Tsh. 10,000 na anaamini kila ambaye ataweza kusoma kitabu hicho ataweza kupata kitu kipya ambacho kitaweza kumsadiakufanikiwa na kufika ndoto abazo anatamani kuzifikia.

"Matumaini yangu kila atakaesoma kitabu hiki maisha yake yabadilike kutokana na mambo ambayo atayasoma na kila mtu hatajutia kusoma kitabu hiki, nimekiandaa kwa muda mrefu kwa kufanya tafiti nyingi na kuweka mifano ambayo naamini itabadili maisha ya watu wengi wataokisoma," alisema Nanauka.

Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka akizungumza kuhusu kitabu cha TIMIZA ALENGO YAKO na jinsi ambavyo kinaweza kubadili maisha ya watu ambao watakisoma.
Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka akizunguza kuhusu kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho ambacho kitauzwa kwa Tsh. 10,000.
Mshauri wa Saikolojia na Mahusiano, ambaye pia ni Mhadhiri wa somo la Saikolojia katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dr. Chris Mauki akizungumza mambo ya kuzingatiwa ili mtu afanikiwa kimaisha.
Mshauri wa Saikolojia na Mahusiano, ambaye pia ni Mhadhiri wa somo la Saikolojia katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dr. Chris Mauki akifanya uzinduzi wa kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO.
Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka akipiga makofi mara baada ya Mshauri wa Saikolojia na Mahusiano, ambaye pia ni Mhadhiri wa somo la Saikolojia katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dr. Chris Mauki kukamilisha zoezi la uzinduzi wa kitabu hicho.
Makamu wa Rais wa TCCIA, Octavian Mshiu akilezea jinsi kitabu TIMIZA MALENGO YAKO kilivyoandaliwa na faida kwa msomaji.
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO.

Wakati kampuni mpya ya Bima ya Clarckson ikizinduliwa jijini Dar es salaam TPSF yakaribisha ubunifu zaidi sekta hiyo nchini.

$
0
0
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers Justin Lambert mara baada ya uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima Bw. Godfrey Simbeye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF akizungumza wakati alipozindua Kampuni ya bima ya Clarkson Insurance Brokers kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo akizungumza kwenye uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima, katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Othman Chande akisalimiana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of Companies Limited ambayo ni Mwanahisa Mzawa Bw. Anic Kashasha wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Clarckson Insurance Brokers jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Clarkson Insurance Brokers Justin Lambert akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Tanzania Bw.Patrick Marimo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari .
Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akizungumza na Balozi Mstaafu Peter Kalaghe wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo wakati walipokuwa wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers inayojishughulisha na masuala ya bima, katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo wa tano kutoka kulia na Justin Lambert Mwenyekiti wa Kampuni ya Clarkson wakikata keki kuashiria uzinduzi wa kampuni hiyo katika ofisi yao iliyopoghorofa ya nane jengo la IPS Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam kabla ya uzinduzi rasmi.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Parkal Randall ambayo ni Kampuni Tanzu ya Clarkson Insurance Brokers Bw. Coutts Otolo akiwatambulisha watendaji wa mbalimbali wa kampuni hiyo.
wageni waalikwa mbalimbali pamoja na wafanya kazi wa kampuni hiyo wakiwa katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki John Muhina kulia akiimba pamoja na wanamuziki wenzake wa bendi ya Tanzanite Band katika uzinduzi huo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.

..................................................................

Na Mwandishi wetu,

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imekaribisha uwekezaji zaidi kwenye sekta ya Bima nchini ili kuibua ushindani utakaochochea ubunifu wenye tija zaidi kwa wadau wa sekta hiyo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni mpya ya Bima ijulikanayo kama Clarkson Insurance Brokers Tanzania Limited,Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF , Bw. Godfrey Simbeye alisema ustawi wa uchumi wa nchi kwa sasa unahitaji uimara na ubunifu zaidi kwenye sekta ya bima hivyo wingi wa kampuni hizo unaweza kuwa na tija zaidi katika kufanikisha hilo.

“Tanzania kwa sasa ipo kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa kama ile ya bomba la mafuta, ujenzi wa reli ya kati, ujenzi wa barabara na majengo makubwa ya kisasa, vyote hivi vinahitaji kulindwa na bima hivyo ujio wa kampuni kama hii ya Clarkson Insurance Brokers Tanzania Limited tunauona kama ni heri na wenye tija kwa taifa,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Bw Simbeye kwa sasa mchango wa sekta ya Bima kwenye Ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) ni chini ya asilimia 1 huku akiitaja sekta binafsi kuwa ni miongoni mwa sekta ambazo bado hazijafaidi ipasavyo matunda ya uwepo wa huduma za Bima ambapo alitaja suala la ukosefu wa ubunifu miongoni mwa makampuni ya Bima kuwa ni moja ya sababu ya uwepo wa changamoto hiyo.

“Matumaini yangu kwa kampuni ya Clarkson Insurance Brokers Tanzania Limited kwa kiasi kikubwa yanachochewa na ukongwe wao wa miaka 58 wakitoa huduma hii nchini Kenya ikiwa ni pamija na Uganda hivyo natarajia kwamba uzoefu wao katika kipindi hicho kirefu unaweza kuwa na tija zaidi hapa nchini,’’ aliongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa makampuni ya Bima ya Clarkson Insurance Brokers Tanzania Group Bw Justin Lambert alisema pamoja na kutoa huduma kwa weledi, kampuni yake itajikita zaidi katika kutoa elimu ya bima kwa jamii ili kuwavutia zaidi wengi ambao kwasasa bado hawajaingia kwenye huduma hiyo.

“Clarkson Insurance Brokers hatujaingia hapa nchini ili kuongeza idadi ya makampuni ya bima yaliyopo nchini bali lengo letu hasa kuongeza ushindani na kuleta mapinduzi makubwa na yenye tija kwa wadau wa sekta hii muhimu,’’ alibainisha.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo hapa nchini Bw, Patrick Marimo alisema mafanikio ya kampuni hiyo katika soko lake jipya hapa nchini kwa kiasi kikubwa yatachochewa na ubunifu mkubwa wa kampuni hiyo katika utoaji wa huduma zake.

“Tunalenga kuleta mabadiliko makubwa kwenye huduma hii muhimu na ndio maana pamoja na mambo mengine tutajikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii ili kuijengea uelewa zaidi kwenye masuala ya bima ili tutoe huduma kwa watu wenye uelewa zaidi …lakini pia uwekazaji wetu kwenye teknolojia ya kisasa unaweza kuwa chachu zaidi katika kufikia malengo,’’ alisema.

WAZIRI MAKAMBA AKIPONGEZA KIWANDA KINACHOZALISHA NISHATI MMBADALA KWA KUTUMIA TAKA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Leonard Kushoka wa pili kulia katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa nishati mbadala.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia mkaa uliokamilika baada ya uzalishaji, mkaa ambao ni rafiki kwa mazingira.

………………

Na Lulu Mussa TABORA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Jauary Makamba amempongeza Bw. Leordard Kushoka kwa kubuni kiwanda kinachotengeza nishati mbadala rafiki kwa mazingira.

Akiwa Mkoani Tabora, Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kusema kuwa Serikali inathamini sana ubunifu na uvumbuzi hasa unao okoa mazingira. “Bwana Kushoka mimi nakupongeza sana, niliona jitihada zako kupitia kipindi cha televisheni na kuamua kukuita na kukusaidia” alisisitiza Waziri Makamba.

Katika kuthamini mchango wa Kiwanda hicho cha “Kuja na Kushoka” Ofisi ya Makamu wa Rais imemsaidia Bw. Kushoka kupata haki miliki ya Kiwanda hicho.

Awali Bw. Leonard Kushoka, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka Tools Manufacture Group amesema kuwa kiwanda chake kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 13 na kufanikiwa kubuni teknolojia mbalimbali rafiki kwa mazingira ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuwafikia vijana zaidi ya 50 katika Wilaya za Tabora Manispaa, Urambo, Kaliua, Mlele pia Katavi na kufanikiwa kuwafundisha utengenezaji wa Majiko banifu yanayopunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa asilimia 50.

Pia Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mashine ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha kilo 160 kwa saa kwa kutumia dizeli lita 5 na kuzalisha wastani wa Kilo 1000 za mkaa mbadala na pia Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mtambo kwa kukaushia tumbaku kwa kutumia taka kavu au mabaki yote ya mazao kama maganda ya karanga, randa za mbao, magunzi ya mahindi na masuke ya mpunga.

Bw. Kushoka amesema kuwa “Mtambo huu umetoa matokeo mazuri katika ukaushaji wa tumbaku kwani wastani wa matumizi ya taka kilo 3 hukausha kilo moja ya tumbaku kwa kutumia mabani ya kisasa” Bw. Kushoka amemuomba Waziri kuisaidia Kampuni hiyo kupata mafunzo mbalimbali ya namna bora zaidi ya kubuni na kuendeleza uzalishaji wa nishati mbadala hasa katika nchi zinazofanya vizuri zaidi.

‘Kuja na Kushoka” ilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2013 na kupewa hati (TMC/CO/CBO/48).

Waziri Makamba akiwa katika Mkoa wa Tabora pia amepata fursa ya kutembelea Wilaya ya Nzega na Igunga, akihitimisha ziara yake ya Mikoa 10 hapa nchini yenye changamoto za kimazingira.

DC MUHEZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Haja Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2

Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti

Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiingia kwenye vyumba vya zahanati mpya ya Zeneti kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Lwiza
Mlelwa

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi


Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiangalia baadhi ya vyoo vya Zahanati hiyo wakati alipoitembelea kuikagua na kuona namna ujenzi wake
unavyoendelea.

Diwaniwa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akielezea mipango ya Halmashauri kuhusiana na kuhakikisha huduma za Afya zinawakuwa karibu na wananchi


NEWZ ALERT;BONDIA THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA

$
0
0

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii, inaeleza kuwa Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na mwili wake kukutwa maeneo ya Tabata, Jijini Dar es salaam. akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamasumbwi huyo, Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) amesema Mashali amefikwa na umauti huo usiku wa kumkia leo kwa kudaiwa kupigwa mpaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi. tutaendelea kujuzana taarifa zaidi za msiba huu wa Mwanamasumbwi huyu nguli hapa nchini, endelea kutembelea Libeneke la Globu ya Jamii.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WATEMBELEA MIRADI YA UWEKEZAJI YA LAPF

$
0
0
    Kaimu Mkurugenzi  Huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF ramadhani Mkeyenge akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusu miradi iliyotekelezwa  na LAPF katika maeneo mbali mbali nchini. 
 Maabara ya Kompyuta katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo 
 Baadhi ya Maofisa wa LAPF pamoja na waandishi wa Habari wakitembelea mradi wa mabweni katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo nje kidogo ya manisapaa ya Dododma. LAPF imetumia bilioni 39 kujenga baadhi ya majengo na miundimbinu katika chuo hicho. 
  Mradi wa Mabweni katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). LAPF imetumia bilioni 22 kujenga majengo na miundimbinu katika Chuo cha Elimu ya Tiba na Afya chuoni hapo kwa awamu ya kwanza ya mradi huo. 
Moja ya Vyumba vya madarasa katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo (Sehemu ya mradi wa LAPF). Darasa hili lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 520 kwa wakati mmoja.

Wakazi wa Ileje waiomba Serikali kuongeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Ileje.

Wakazi wa Kata ya Bupigu Wilayani Ileje wameiomba Serikali kuongeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji kwa wakazi wa eneo hilo ili kupunguza tatizo la njaa wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa kikundi Nguvu kazi, Isaka Kamwela, kinachojihusisha na kilimo cha umwagiliaji katika kata hiyo kwenye Mto Mtumbisi.

“tumekuwa tukilima kwa kumwagilia kwa kipindi cha misimu minne kwa mwaka hali inayowafanya wakulima kuwa na fedha za kujikimu lakini uzalishaji umekuwa mdogo kutoka na kukosa elimu ya kutosha juu ya kilimo hicho” amesema Kamwela.

Amasema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi sana hasa za masoko pindi wanapolima bidhaa za mbogamboga na kuishia kuoza mashambani bila kupata wateja.

Amaeongeza kuwa ni vyema serikali ikawatuma wataalam wa masuala ya usindikaji mazao kwenda kutoa elimu ya kutosha kupunguza hasara wanayopata wa kulima .
 Mmoja wa wakulima wa kikundi cha Nguvu Kazi akipalilia Mahindi yae 
  Katibu wa kikundi Nguvu kazi, Isaka Kamwela alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Blobu hii namna wanavyoshiriki kwenye kilimo cha umwagiliaji
sehemu  ya wana kikundi cha umwagiliaji cha nguvu kazi wakiendelea na shughuli yao ya kilimo.

WENYEVITI ZAIDI YA 44 WA SERIKALI ZA MITAA KUTOKA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILALA WAJIFUA BAGAMOYO

$
0
0
WENYEVITI wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam wamekutana Wilayani Bagamoyo katika Semina maalum ya kujengeana uwezo na uwelewa ikiwamo kutambua majukumu yao kwa lengo la kuepusha migongano kati ya Wenyeviti,Watedaji ,pamoja na Madiwani.

Akizungumza wilayani humo mara baada ya kufungua semina hiyo Mwenyekiti wa Wenyeviti mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti Wilaya ya Kinondoni Juma Zubery alipongeza hatua ya wenyeviti wa wilaya ya Ilala kuona kuna umuhimu wa kufanya semina ya kukumbusha na kuelekezana majukumu ya weyeviti katika mitaa mbalimbali ili kuepusha migongano kati yao na watendaji wengine wa Serikali.

Zubery alisema uendeshaji wa Serikali za mitaa unachangakubwa ,ikiwamo viongozi wengi kushindwa kujuwa mjukumu yao hali inayosababisha kutoautiana mara kwa mara miongoni mwao nakudai kwamba mtendaji wa mtaa na mwenyekiti wanafikia hatua ya kugombea hata mihuli jambo ambalo kimsingi linatokana na uelewa mdogo wa kutojuwa mipaka ya kazi zao.

Kwaupande wake Menyekiti wa Wenyeviti katika Manispaa ya Ilala Ubaya Chuma aliwataka wenyeviti hao kuogoopa kutumia mihuli ya watendaji wa mtaa huku akidai kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sharia na kwamba kufanya hivyo nikukaribisha migongano miongoni mwao. 

Katika Semina hiyo wenyeviti zaidi ya 44 kutoka Halmashuri hiyo wamekutana huku wakimomba Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo kama hayo kwa wenyeviti wote wa Serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za mitaa mkoa wa Dar es Salaam Juma Zubery Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Semina elekezi kwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wilaya ya Ilala ambapo lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwajengea uwezo na uwelewa juu ya majukumu yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mogo, Geoge Mtambalike akitoa mada ya ulinzi na usalama katika semina hiyo ya wenyeviti wa serikali ili kujuwa namna ya kuweza kukabiliana na vitendo vya kiarifu katika mitaa yao.
Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma akiwasilisha mada mbele ya wajumbe ambao ni wenyeviti wa Serikali za mitaa mbalimbali wilayani humo ambapo alijikita katika kutoa elimu ya kutambua majukumu yao nakuacha kumbea mihuri huku akidai ni makossa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kuchukua mhuhuri wa mtendaji wa mtaa au kata.
Wenyeviti wa Serikali za mitaa mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya ilala wakisikiliza kwa makini mada ambayo ilikuwa ina tolewa na mtoa mada,Ubaya Chuma kuhusu wenyeviti hao kuona kwamba wanajukumu kubwa la kulinda usalama wa maeneo yao ikiwa pamoja na kuimarisha vikundi vya ulinzi na usalama. 
Katibu Tawala wilaya Bagamoyo Mjini Doris Mwakitobe akizungumza jambo wakati wakufunga semina ya wenyeviti wa serikali za mitaa mbalimbali wilaya ya Ilala,ambapo katika kufunga semina hiyo aliwataka kwenda kutumia mafunzo hayo kufanya kazi kwa bidi na kwa kuzingatia kauli mbiuya rais ya Hapa kazi tu kulia ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mogo Geoge mtambalike.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

HAYATOU AMTEUA MALINZI KAMATI YA MAGEUZI CAF

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, Issa Hayatou ameteua Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa miongoni mwa wajumbe 11 wa Kamati maalumu ya mageuzi ya muundo wa CAF itakayokuwa na jukumu la kufanya mabadiliko mapya ya shirikisho, imefahamika.

 Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, katika Kamati hiyo ikayoongozwa na Rais Issa Hayatou mwenyewe, Malinzi ameteuliwa katika Kamati hiyo iliyotangazwa leo Oktoba 30, 2016 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.

HAYA NDIO ALIYOZUNGUMZA RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS KENYATTA JIJINI NAIROBI LEO

$
0
0
Hotubu ya Rais Dkt Magufuli Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta

UWEPO WA BARAZA HURU LA HABARI UTASAIDIA KUKUZA MAADILI KWA WANAHABARI.

$
0
0

Na Daudi Manongi.

UWEPO wa kifungu kinachopendekeza uanzishwaji wa Baraza Huru la Habari katika Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016 utasaidia kukuza maadili na viwango vya taaluma baina ya wanahabari na Kampuni za habari nchini.

Maoni hayo yametolewa na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim James Yonazi leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi

Ameongeza kuwa chombo hicho ni umuhimu kusimamia maadili ya Taalum ya habari na kufanya waandishi wa habari hapa nchini wawajibike kwa kazi zao za kila siku za kuhabarisha umma. Mhariri huyo Mtendaji amewahasa wanahabari kuukubali muswada unaopendekezwa kwani ni kwa maslahi yao wenyewe na utaipa heshima taaluma hii.

“Sheria hii ni muhimu sana kwa kuwa ukiangalia katika sekta zingine kama za Uhasibu, Uhandisi ,wakandarasi na wanasheria wanatambuana kupitia vyombo ambavyo wamejiwekea wakati sekta ya Habari hakuna kitu kama hicho kinachoweza kuonyesha huyu ni mwanahabari na hata kufahamu idadi yao nchini ni ngumu hata kuiendeleza katika viwango vya juu uwezekano huo haupo”alisema Dk Yonazi.

Aidha amewataka wamiliki na wadau wa tasnia ya Habari kuangalia mapungufu yake na kuona ni wapi panatakiwa kuboreshwa na kusisitiza ni vema kuwa na sheria hii kwanza halafu mapungufu yatafanyiwa kazi baadaye.

Kwa upande mwingine amewataka wandishi kutokuwa waoga wa muswada huu na kutoa maoni yao kama wafanyavyo katika mambo mengine na kuwataka kwa sasa kuruhusu utekelezaji wa muswada huu na kuendelea kuusimamia na kuufatilia ili kujua wapi kuna tatizo na kuliweka wazi ili liweze kurekebishwa.

Aidha ameongeza kuwa muswada huo unakusudia kuanzisha Bodi ya Ithibati ya wanahabari ambayo itasaidia katika kuwatambua waandishi wasio wanahabari ambao wanachafua taaalum ya habari.

WAZIRI NAPE AMLILIA BONDIA MACHALI

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na Chama cha Wanandondi nchini kufuatia kifo cha Bondia wa ngumi za kulipwa Bw. Christopher Fabian Mashale maarufu kama ‘Thomas Mashali’ kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 31/10/2016.

Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha bondia huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya michezo nchini.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha bondia Thomas Mashali, sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni niliyonayo, kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya masumbwi nchini” alisema Mhe.Nnauye.

Aidha, Waziri Nape Nnauye ameitaka jamii na wanamichezo kote nchini kuwa wavumilivu na watulivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.

Thomas Mashali alizaliwa Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Septemba, 1989 na kuweza kushiriki katika baadhi ya michezo mbalimbali ya masumbwi ya kulipwa ambapo kati ya michezo 26 aliyowahi kucheza alishinda michezo 19, ambayo tisa ni ya Knock Out (KO), lakini pia alipoteza michezo mitano yaani KO minne na kutoka sare mchezo mmoja.

Bondia Thomas Mashali aliwahi kupigana na baadhi ya mabondia maarufu wa ndani na nje ya nchi wakiwemo Francis Cheka, Abdallah Paziwapazi, Ibrahim Tamba na wengineo.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

31 Oktoba, 2016 .

KIGWANGALA:WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANA UWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

$
0
0

Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha.,aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.
Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala,Aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital

Waandishi wa habari wanawake wakifuatilia kwa karibu baadhi ya majibu ya yaliyokuwa yakijibiwa na madaktari walioendesha mafunzo,mafunzo hayo yalikwenda sambaba na upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi.

Na Woinde Shizza Arusha.

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha Saratani ya mlango wa kizazi

Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa kwa kujaamiana .

Kigwangala amesema kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima,amewataka kutokufanya ngono mapema.

Amesema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili zikiwa zinakwenda taratibu sana.

Kwa upande wake Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio,kutokwa na majimaji yenye harufu kali,amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Aidha Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema,kupunguza idadi ya kuzaa watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi,ukifanya ngono watumie kinga.

Sambamba na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa( DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.

Kwa upande wake Sr.Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.

Lyinga amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi. .

ULEGA AZINDUA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI MITAWA WILAYA YA MKURANGA,PWANI.

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amezindua ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi ya Mitawa,mwishoni mwa wiki,wilayani Mkuranga,Pwani,Ujenzi wa madara hayo unafuatiwa kutokana na shule ya hiyo kuwa na upungufu wa madarasa na kupelekea wanafunzi kusomea katika jengo la kupanga.

Akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mitawa, Ulega amesema karne hii wanafunzi kusoma katika jengo la kupanga imepitwa na wakati, hivyo ni lazima wazazi wajitoe kujenga shule na serikali itatia mkono wake baada ya kuona njia ya kufanikisha jambo hilo.

Amesema suala linaloweza kufanya Taifa kuwa na maendeleo ni pamoja na kuwa wataalam ambapo lazima watoto waandaliwe katika mazingira ya shule na bila kufanya hivyo hakuna maendeleo hayo.Ulega amesema kama mbunge anawajibu wa kusimamia suala la elimu, kwa wananchi wa Mkuranga wanapata maendeleo ya elimu kwa kuwa na shule pamoja na walimu wa kutosha.

Katika ujenzi wa shule hiyo Mbunge amechangia zaidi ya milioni mbili na kuahidi kuendelea kutoa mchango mpaka pale shule itakapokamilika.Aidha amesema kufikia Januari shule hiyo imekamilika na wanafunzi waweze kuanza kusoma katika madarasa hayo na kuachana na kupanga jengo ambalo linatumika kwa sasa. 
  Mbunge wa mkuranga akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya  ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mitawa pamoja na shughuli ya ufyatuaji matofali Mbunge huyo pia alishiriki upandaji miti na kuzungumza na wananchi,leo mkoani Pwani.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mitawa, Mkuranga juu ya maendeleo yaliyofikia katika Shule ya Msingi  Mitawa, leo. 
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega wapili (kutoka kushoto)  akishiriki mazoezi na vijana wa Mkuranga leo ikiwa ni sehemu ya kuwajenga vijana kuwa imara katika michezo. 
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizindua vyumba viwili vya madarasa viliyojengwa na wananchi kwa kushirikiana na ofisi ya  mbunge leo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
 Mbunge wa mkuranga ashiriki ujenzi wa darasa la shule ya msingi Mitawa pamoja na shughuli ya ufyatuaji matofali Mbunge huyo pia alishiriki upandaji miti na kuzungumza na wananchi,leo mkoani Pwani.

DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS,TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakati wa kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud akisoma kazi za Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ ACP Sida Muhamed Himid na (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika kikao cha robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Mhe,Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,akiuliza suala wakati wa kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 cha Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Balozi Seif Ali Iddi,na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd, Radhiya Rashid [Picha na Ikulu] 31/10/2016.
Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika mkutano wa siku moja unaozungumzia Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Mhe,Mwinyiussi Abdalla Hassan (kushoto) akisisitiza jambo wakati akiwa na Wakuu wa Wilaya nyengine katika mkutano wa siku moja unaozungumzia Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA UKUMBI WA NKURUMAH HALL CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
..........................................................................
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images