Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1025 | 1026 | (Page 1027) | 1028 | 1029 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global (Global Publisher Ltd) Bw. Erick James Shigongo(kushoto) akimsikiliza mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) Bi. Eva Klerruu leo Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akifanya usajili katika Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Uendeshaji wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) Bw. Peter Mayunga.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akielezea historia ya maisha yake alipokuwa akiwasilisha maada kuhusu namna ya kurejea katika ndoto ya maisha baada ya kuanguka wakati wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.Aliyesimama ni Bw. Severin Faustine (55) Aaliyekuwa amefungwa kwa sasa anasaidiwa na Shigongo kwa dhana ya kuwa na upendo kwa wakosaji na si kuwachukia.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali. Kongamano hilo limefanyika na kuwakutanisha viongozi wa Dini, wafanyabiashara na wanasiasa.

  Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi( Global Leadership Summit) wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali. Kongamano hilo limefanyika na kuwakutanisha viongozi wa Dini, wafanyabiashara na wanasiasa.
  Mwakilishi Mkazi wa Global Leadership Summit nchini Tanzania Bw. Mbutho Chibwaye(kushoto) akimpongeza mshiriki kutoka Kigoma Bi. Gloria Dominicus Kasilo ambaye aliamu kuacha kazi yake ili aweze kushiriki Kongamano la Kimataifa la Uongozi.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo akibadilishana mawasiliano na mshiriki wa Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) Bi. Gloria Dominicus Kasilo leo Jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyo alikuwa anafanya kazi katika Shirika la Plan International kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Nduta lakini aliamua kujiuzulu kazi yake ili aweze kuhudhuria kongamano hilo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kuchapisha Magazeti ya Global Bw. Erick James Shigongo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya Kongamano la Kimataifa la Uongozi(GLS) leo Jijini Dar es Salaam.

  Na: Mpiga picha wetu.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akifafanua jambo kuhusu wananchi waliovamia msitu wa hifadhi ya Kijiji. Kushoto ni Bi. Veronica Nyasa mkazi wa eneo hilo ambae amesema yuko tayari kuondoka endapo atapatiwa sehemu mbadala.
  Uongozi wa Wilaya ya Kaliua wakimwonyesha Waziri Makamba magogo ya miti ya asili yanayotumiwa na wanachi katika kukaushia tumbaku kwa kutumia majiko ya kienyeji
  Pichani ni moja ya majiko ya kienyeji yanayotumia kuni/miti mingi katika kukaushia tumbaku. Waziri Makamba amewaagiza wakazi wa Kitongoji cha Mtakuja Magharibi kutumia majiko banifu ili kunusuru ukataji miti kwa wingi husnan ile ya asili

  …………………………………………………………………

  Na Lulu Mussa-Tabora

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira hii leo ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoani Kigoma.

  Akiwa Mkoani Tabora Waziri Makamba ametembelea Wilaya ya Kaliua na kukutana na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Mazingira na Uvamizi wa Misitu unaofanywa na wananchi. Katika Kijiji cha Ufugala Wilaya ya Kaliua Waziri Makamba amefanya Mkutano wa hadhara kijijini hapo na kubaini kuwa Kitongoji hicho hakikufuata taratibu za kisheria katika kuanzishwa kwake na kimeanzishwa ndani ya Hifadhi.

  Akitoa maelezo ya Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abel Yeji Busalama amemueleza Waziri kuwa Kitongoji hicho kiko ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Kijiji ambapo jumla ya Vijiji 11 viamua kutenga eneo hilo kwa ajili ya Hifadhi.

  Bw. Busalama amesema kuwa wakazi hao wamekwisha amriwa kuondoka katika hifadhi hiyo na utekelezaji wake unaendelea.

  Akijibu hoja zilizowasilishwa na wakazi wa eneo hilo Waziri Makamba amesema kuwa wajibu wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Sheria, tararibu na kanuni zinafuatwa bila kukiukwa. Waziri Makamba pia amesisitiza kuwa maamuzi ya matumizi bora ya ardhi yapo mikononi mwao. “Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mliamua kutenga eneo hili maalumu kwa hifadhi ya msitu wa kijiji na kufuata taratibu zote za kisheri katika kuusajili, maamuzi yenu ya awali yatabaki palepale mpaka mtakapofuata taratibu nyinginezo.” Makamba alisisitiza.

  Aidha, Waziri Makamba ameahidi kuwasilisha suala hilo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupata ufumbuzi wa kudumu. “Nitaongea na Mawaziri wenzangu na kuleta timu ya wataalumu kupitia upya mipaka ya kijiji na kuifanyia kazi” Makamba alisisitiza.

  Kuhusu hifadhi ya Mazingira Waziri Makamba amewataka wakazi wa Ufulaga kuacha tabia ya kukata miti ya asili na kusisitiza kuwa uharibifu wa mazingira unabadilisha tabia za watu. “Wana Ufulaga, binadamu wakiharibu mazingira kwa kiasi kikubwa wanaanza wizi na udokozi na wanyama wataanza kuwinda watu kwa kukosa malisho” alisema Waziri Makamba.

  Waziri Makamba pia amefanya ziara katika Wilaya ya Urambo na kubaini changamoto kubwa ya uvamizi wa misitu na ukataji wa miti ya asili kwa ajili ya kuni za kukaushia tumbaku.

  Waziri ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutumia Sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kifungu namba 196 (1) (a na b) kupiga marufuku ya matumizi ya majiko banifu ya kienyeji pia ukataji mkubwa wa miti ya asili kwa ajili ya biashara ya tumbaku. Katazo hilo litawahusu Wakulima na Vyama vya Msingi vyote vinavyojishughulisha na biashara ya tumbaku.

  Waziri Makamba anaendelea na ziara yake kwa kutembelea Wilaya za Nzega na Igunga.

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini wakati anatoa elimu juu ya Ukatili dhidi ya Watoto kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Evelyn Simalenga. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini Arusha wakishangilia mara baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya Watoto iliyotolewa na kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto la mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

  Askari Polisi kutoka kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Arusha Happy Mshana akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini iliyopo jijini hapa aina za Ukatili dhidi ya Watoto huku wanafunzi hao wakionekana kumsikiliza kwa umakini. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

  Mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Sombetini Jackson Mutalemwa akiuliza swali baada ya kupata elimu ya Ukatili dhidi ya watoto kutoka Ofisi ya Dawati la Jinsia na watoto mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) 
  …………………………………………………………..
  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia kitengo chake cha Dawati la Jinsia na Watoto limeanza kutembelea shule za Msingi kwa nia ya kutoa elimu ya Ukatili dhidi ya watoto. Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo hicho Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu wakati alipokuwa anatoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Sombetini iliyopo halmashauri ya jiji la Arusha.

  Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipokea malalamiko mbalimbali ya wanawake, wanaume na watoto wakiwa ofisini lakini wamegundua kwamba wanafunzi wengi wa shule za Msingi hawana uelewa juu ya vitendo vya Ukatili unaotokea miongoni mwao.

  Akitoa elimu hiyo kwa wanafunzi hao Mkuu huyo wa Dawati alisema kwamba baadhi ya watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili kwa kubakwa na kulawitiwa lakini ukaa kimya na wasijue nani wa kumwambia, hivyo kuwataka pindi wanapoona dalili za watu kutaka kuwafanyia vitendo vya aina hii watoe taarifa haraka kwa wazazi wao, majirani au walimu.

  Alisema kumekuwa na mbinu tofauti tofauti zinazotumiwa na walaghai kama vile kumnunulia Mwanafunzi pipi, kumpa msaada wa kumpeleka shule na kumrudisha nyumbani “lift”, kumpa pesa hali ambayo aliwaambia wanafunzi waikatae kwani sio watu wote wana nia nzuri na wao.

  “Mara unapohisi kuna mtu ambaye anasogea karibu yako na kukudanganya kwa kukupa msaada wa lift au kukunulia pipi unatakiwa kutoa taarifa mapema kwa wazazi wako, walezi wako, majirani au walimu wako hali ambayo itasaidia kukuepusha kuingia kwenye matatizo”. Alisisitiza Mkuu huyo wa Dawati.

  Alisema watoto wanaweza wakafanyiwa vitendo hivyo si kwa watu wa nje na nyumba zao tu bali hata watu wao wa karibu kwa maana ya wazazi au walezi wao wanaweza kuwafanyia vitendo hivyo, na kuwaeleza kwamba wana nafasi ya kuwaeleza majirani na walimu wao ambapo taarifa hizo baadae zitawafikia katika ofisi yao ya Dawati na wao kuchukua hatua mara moja.

  Akizungumzia aina mbalimbali za ukatili askari wa kitengo hicho, Happy Mshana alisema kwamba ukatili upo wa aina tofauti tofauti kama vile ukatili wa kingono, ukatili wa kijinsia, ukatili wa Kisaikolojia, ukatili wa kielimu na kadhalika. 

  Alisema mara nyingi wanafunzi wanaathirika na ukatili wa kielimu ambapo hali hii inatokana na wazazi au walezi kuwazuia watoto wao kwenda shule huku wakiwa wanastahili kusoma, hivyo kuwataka pindi wanapoona wao au wenzao wanakumbwa na hali hii watoe taarifa kwa majirani na ikishindikana wawaeleze walimu wao.

  Kutokana na elimu iliyotolewa na Dawati hilo iliweza kuibua hisia za wanafunzi mbalimbali ambao wengi waliuliza maswali ambayo yalijibiwa na askari wa kitengo hicho walioongozwa vyema na Mkuu wa kitengo hicho Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu, huku wengi wao wakionekana kushangilia baada ya mmoja wao kutaka adhabu ya kunyongwa itumike kwa watuhumiwa wanaokutwa na hatia kwa makosa ya ubakaji na ulawiti badala ya kifungo.

  Mwanafunzi wa darasa la sita aitwaye Jackson Mutalemwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Haki za Watoto (Children Right Club) alisema kwamba kitendo cha Dawati kutoa elimu shuleni hapo kimekuja muda muafaka kutokana na vitendo hivyo kuripotiwa kwenye Klabu yao mara kwa mara hasa wanavyofanyiwa watoto wa mitaani hivyo kuwataka wasiishie kwenye shule tu bali wawaelimishe pia watoto wa mitaani

  Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Evelyn Simalenga alisema kwamba Dawati la Jinsia na watoto limewafanya wanafunzi wake wawe na uelewa mpana zaidi hivyo utawafanya wawe makini na kushauri kwamba elimu hiyo iendelee kutolewa kwa wazazi ili wawe karibu na watoto wao.

  0 0

   Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwapungia Mkono wananchi wa Jiji la Mwanza mara baada ya kutangazwa Mshiindi wa Miss Tanzania 2016 Jijini Mwanza Leo wakati wa Kuhitishimisha hindano la Miss Tanzania 2016. 
  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward  katikati akiwa na mshindi wa pili na watatu Grace Malikita na Maria Peter mara baada ya Msindi wa shindano la Miss Tanzania 2016 kutangazwa Mshindi jijini Mwanza leo.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa na washindi watano wa kwanza katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2016 jiji Mwanza leo.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward kushoto akiwa na wenzake wakati wa Kunesha Vazi la ubunifu wakati wa kusaka mshindi wa Miss Tanzania 2016 jijini Mwanza leo.  Mamiss Tanzania 2016 wakionesha Mavazi yao ya ubunifu wakti wakati wa Kusaka Mshindi wa Miss Tanzania 2016 katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza Leo.


  Washindani wa Mamiss Tanzania 2016 wakiburudisha Jamii waliohudhulia wakati wa kumsaka Miss Tanzania 2016 jijini Mwanza leo.

  Mamiss Tanzania wakionesha Mavazi ya Ufukweni wakati wa kushindania nani ni nani katika shindano la Miss Tanzania 2016 yaliyohitimishwa katika viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.
  Burudani ikiendelea  ikitumbuizwa na msaaniioka kutoka jijini Mwanza.
  Msheereshaji akifanya yake.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura ambaye ndiye Mgeni Rasmi wa siku ya Kuhitimisha Mashindano ya Miss Tanzania kwa 2016 akiangalia mashindanohayo jinsi yanavyoendelea kufanyika katika Viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza Leo.

  Madam Wema Sepetu hakusita kufika katika Mashindano ya Miss Tanzania 2016 jijini Mwanza.

  Baahi ya u waliojitokeza katika Hitmisho la Miss Tanzania 2016 jijini Mwanza.
  Gari la zawadi ya Mshindi wa Miss Tanzania 2016.


  Mamiss Tanzania wakionesha mavaji ya jioni.
  Tano Bora.
  Kumi na Tano bora ya Miss Tanzania 2016.

  Top 5 wakiwa katika pozi.

  Meza ya Majaji.
  Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akizungumza wakati wa hitimisho la Mashindano ya Miss Tanzania 2016 mara baada ya kuombwa na wananchi wa jijini Mwanza apande jukwaani.


  Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima akizungumza machache kabla ya kukabidhi Taji la Miss Tanzania kwa mshindi wa 2016, Diana Edward.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima akiwa katika picha ya Pamoja na washindi watano wa kwanza kabla ya kutangazwa washindi watatu wa kwanza.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Lilian Kamanzima akimvisha Taji la Miss Tanzania  mshindi wa 2016, Diana Edward mara baada ya kuibuka mshindi wa Kinyang'anyiro hicho.
  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwapungia Mkono wanachi mara baada ya kuvishwa taji la Miss Tanzania 2016.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura  akimkabidhi ufunguo Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward mara baada ya kuibuka Mshindi wa Miss Tanzania 2016.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia James Wambura  akimpongeza Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward.

  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa amepozi katika gari lake.


  Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward akipongezwa.  Red Carpet ndivyo ilivyokuwa.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii, Mwanza.  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Benoit Janin  (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto ni Meneja Uendeshaji Mtandao, Ahmed Hassan Abdallah na Meneja Mauzo, Herbet Louis.

   Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Hebert  Louis (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto ni Meneja Uendeshaji Mtandao, Ahmed Hassan Abdallah na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin.
   Meneja Uendeshaji Mtandao wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Ahmed Hassan Abdallah (wa pili kushoto),  akiwaonyesha waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, jinsi ya kurekebisha simu na kuwa katika mpangilio wa automatiki  wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mtandao wa  4G ambapo sasa miji yote nchini itafikiwa na huduma hiyo.  Kushoto kwake ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Meneja Mauzo, Herbet Louis.
  Baadhi ya waandishi  kutoka vyombo mbalimbali vya habari walihudhuria uzinduzi huo. 

  0 0

  Kocha wa JKT Mlale Edga Msabila akihojiwa na Ruvuma TV on Line baada ya mpira kumalizika na kutoka sale ya moja moja  na Coast Union ya Tanga katika mchezo uliochezwa uwanja wa MAJI MAJI uliopo miji Songea Mkoani Ruvuma

  0 0

  WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage leo amezindua rasmi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Maisha Plus. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo Mhe. Mwijage alisema kitendo cha washiriki hao 16 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kuweza kubuni mashine ni sawa na kufaulu mitihani mikubwa ya kimaisha. Alisema mashine hiyo ni mkombozi kwa watu wote wa Afrika Mashariki kwa sababu inaweza kusaga bila kutumia umeme lakini pia inamuwezesha mtu kufanya mazoezi.  “Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage.  Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki. 
   Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho." 

  Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter. Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications. 

  #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu

  0 0

   Meneja wa TEMESA Iringa Mhandisi Ian Makule (Kulia) akimuonesha Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) stoo ya vifaa kwa ajili ya ukarabati mdogo wa magari.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Iringa. 
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Iringa kutoka kwa Meneja wa kituo hicho Mhandisi Ian Makule.


  Na Theresia Mwami TEMESA iringa

  Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) imeanzisha program ya kubaini vipuri bandia kwa ajili ya kuboresha huduma za matengenezo ya magari na mashine mbalimbali.

  Agizo hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.Mussa Mgwatu alipotembelea karakana ya TEMESA mkoani Iringa kujionea jinsi karakana hiyo inayotumia kutumia mfumo huo wa kubaini vipuri bandia.

  Dkt Mgwatu ameongeza kuwa mfumo huu umekuja wakati sahihi kwani kwa sasa kumekuwa na uingizwaji wa vipuri bandia ambao umesababisha hasara kwa wamiliki wa vifaa vinavyotumia vipuri kutoka nje ya Tanzania.

  “Ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia inabidi tuwe na mfumo ambao utatusaidia kutambua vipuri bandia kwani vinakwamisha sana utendaji kazi wetu” alisema Dkt Mgwatu.

  Akieleza jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Meneja wa TEMESA Iringa Mhandisi Ian Makule alisema kuwa kwa kuingiza taarifa za namba ya gari husika kwenye program ya kompyuta, unaweza kubaini kama kipuri kinachokusudiwa ni halisi kabla ya kukiagiza.

  Mhandisi Makule aliongeza kuwa kama namba na jina la kipuri zitakuwa sahihi kwenye kasha lake lakini kipuri chenyewe sio halisi, kitaweza kutambuliwa kwa kutumia programu ya ‘barcode scanner’.

  Dkt. Mussa Mgwatu ameziagiza karakana zote za TEMESA nchini kuanza kutumia programu ya kompyuta katika kuagizia vipuri toka kwa wazabuni ili kuondokana na lawama zinaotokea wakati wa kutengeneza na kukarabati magari ya Serikali na mitambo mbalimbali.

  Soko la vipuri vya magari, kama yalivyo masoko ya vifaa vingine, limeingiliwa kwa kasi na uwepo wa vipuri bandia (Non genuine parts) katika kukabiliana na tatizo hili TEMESA imeamua kuanzisha mfumo wa kubaini vipuri bandia.

  0 0

  Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Taasisi ya Twaweza wamesema kuwa Muswaada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ni bora kuliko Miswada iliyowahi kuwasilishwa nchini.

  Haya yamebainishwa katika maoni yao waliyowasilisha kwenye Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Mjini Dodoma katika juhudi za kuufanya Muswada huo kuwa bora zaidi na kupelekea kuapa sheria yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  TLS na Twaweza wamebainisha kuwa Muswada huu ni bora zaidi  na utasaidia kuwajengea wadau wa habari nchini heshima kwa kutoa huduma bora kupitia  vyombo vya habari kwa kuzingatia taaluma ya Habari waliyonayo hatua ambayo inautofautisha na muswada uliowasilishwa Bungeni mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa maoni yalitolewa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) yamesema Muswada huo mzuri zaidi na unaifuta Sheria ya  Magazeti ya Mwaka 1976 hatua ambayo wameipongeza Serikali kwani Sheria hiyo  iliwahi kuainishwa kuwa miongoni mwa Sheria 40 na kusadikiwa na Tume ya Jaji Francis Nyalali kama Sheria kandamizi.

  Kwa upande wa Taasisi ya Twaweza wao wamesema kuwa Muswada huo utaanzisha utaratibu ambao utawatambua waandishi wa habari kwa kuanzisha Baraza Huru la Habari pamoja na Bodi ya Ithibati ya wanahabari amabazo zitasimamia kanuni na maadili ya wanahabari, kusimamia viwango na mienendo ya kitaaluma na kuendeleza vigezo bora vya maadili na nidhamu miongoni mwa wanahabari.

  Kwa mantiki hiyo, maoni yaliyowasilishwa kwa Kamati hiyo yanaendana na Muswada ambao unasisitiza  kuanzisha mahusiano na taasisi nyingine za taaluma ya habari ndani na nje ya nchi ili wadau wa habari waweze kubadilishana mawazo na kuwa na namna bora ya kuhabarisha umma katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

  Aidha, Baraza huru la habari kutakuwa suluhisho katika kusimamia na kusikiliza malalamiko ambayo yatawasilishwa kwenye baraza hilo kulingana na kanuni za maadili ya taaluma ya habari hatimaye kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.

  Uboreshwaji wa Muswada huo unalenga kuleta Sheria itakayosimamia Tasnia ya Habari ili iweze kuendana na wakati pamoja na Sheria za kimataifa na namna bora ya kuwahudumia wananchi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari. Mkutano huo unafanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha zote na WMNN.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisikiliza mada zilizokuwa zinatolewa katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha na WMNN.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha na WMNN.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mratibu wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi wa Kudhibiti Biashara na Usafirishaji wa Dawa za Kulenya kwa njia ya bahari unaofanyika mjini Colombo nchini Sri Lanka. Picha zote na WMNN.

  0 0


  Mmoja wa wananchi waliosaidiwa kupata mradi wa kuku kupitia Mradi wa Uondoaji wa Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita, Shabani Masanja akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi huo ulivyomsaidia.

  Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT), Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa Mkoa wa Geita ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.
  ……………………………………………………………….
  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Geita

  Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT) limejipanga kuwasaidia jumla ya wananchi 7000 wanaoishi katika mazingira magumu Mkoani Geita ili waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini linalowakabili.


  Shirika hilo ni moja ya mashirika yanayoshirikiana na Shirika la Plan International katika kutekeleza Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kuratibiwa na shirika la plan International kwa kuwapatia wananchi hao vifaa pamoja na elimu ya ujasiriamali.


  Hayo yamesemwa leo Mkoani Geita na Msimamizi wa Miradi wa shirika hilo, Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa mkoa huo ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.

  Saramba amesema kuwa mradi huo unaoratibiwa na shirika la Plan International umewasaidia wananchi wa mkoani Geita kuinua maisha yao kwa kuwasaidia kuunda vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na kuwapatia vifaa mbalimbali vinavyowawezesha kujipatia vipato ambavyo vinawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.

  “Awamu ya kwanza ya mradi huu iliisha Novemba 2015 na tulifanikiwa kuwafikia wananchi wenye mazingira magumu zaidi ya 4000 waishio katika Wilaya za Nyan’ghwale na Geita, kwa awamu hii tumeongeza wilaya ya Chato hivyo tumejipanga kuwafikia wananchi 7000 tukiamini kuwa kuwasaidia wananchi hao kutapunguza ajira hatarishi kwa watoto”, alisema Saramba.

  Amevitaja baadhi ya vifaa walivyovitoa kwa wananchi wanaoishi kwenye mazingira magumu kuwa ni mashine za kujazia upepo magari na pikipiki (compressor), vyerehani, mabomba ya maji, mizinga ya nyuki, viti na meza kwa mama lishe, kuwapatia wafugaji kuku pamoja na mbegu za mahindi na mpunga kwa wakulima, zaidi ya hayo waliweza kufadhili mafunzo ya kutengeneza baiskeli, pikipiki na cherehani.

  Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliosaidiwa kupitia Mradi huo, Shabani Masanja ameyashukuru mashirika hayo kwa sababu kabla ya mradi huo kumfikia alikua na maisha magumu lakini baada ya kuanza ufugaji wa kuku aliopewa kutoka katika shirika hilo ameona tofauti kubwa ya maisha.

  “Nashukuru sana mashirika yaliyoniwezesha kwa sababu yameninufaisha, kwa sasa ninaweza nikauza kuku na mayai vinavyoniwezesha kusomesha watoto wangu, kununua chakula, nimeweka umeme kwenye nyumba yangu ambao unanisaidia kufanya ufugaji wa kisasa kwa sababu mwanzoni nilikua nikikuza vifaranga kwa kuwawekea moto lakini sasa hivi natumia umeme kuwakuza”, alisema Masanja.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

  Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.

  Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.

  WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
  Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.

  Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya TALIRI.

  Jaffar Haniu
  Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  30 Oktoba, 2016

  0 0

   
  Waziri wa Elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako  sambamba na viongozi wengie wa wilaya ya Mkuranfa wakishiriki kufyatulia tofali,wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga. 
   Pichani kushoto ni Waziri wa Elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako  pamoja na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakishriki kwa pamoja kuchanganya mchanga wa kufyatulia tofali,wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga. 
   Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa Mkuranga wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega 
  akizungumza na wananchi wake wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.


  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

  Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wananchi wa Mkuranga wamejitoa katika kupata Mandeleo.

    Profesa Ndalichako wakati kufunga kambi ya kufyatua tofali 45000 kwa ajili ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya msonga wilaya Mkuranga.

  Amesema kuwa wananchi wamejitoa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na mazingira. Amesema kuwa nia yake nikuona mkuranga kunapatikana mapinduzi ya Elimu.

  Amesema vijana 53 wameamua kumuunga mkono kutokana na kuona njia inaonekana ya kujitoa na kwao katika kusaidia maendeleo ya Taifa.

  Amesema ujenzi wa mabweni hayo itakuwa suluhu kwa wasichana  kufanya vizuri.Amesena jitihada zinaendelea kutatua baadhi ya changamoto za Elimu kwa kushirikiana na wananchi.Katika ufungaji wa kambi hiyo Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana yenye tija.

  Waliohudhuria ufungaji ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya, Filberto Sanga na viongozi mbalimbali.

  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO.

  MUSWADA wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 umeonekana kuwa mlinzi kwa wanahabari nchini kwa kuwa na kipengele kinachowataka waajiri kuwapa bima na mifuko ya hifadhi ya jamii waajiriwa wake mara baada ya kuwaajiri kama wafanyakazi halali wa chombo husika.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti na Mratibu wa kampeni ya Media Car Wash for Cancer Bw. Benjamin Thomson Kasenyenda wakati wa kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya huduma za Habari ya 2016 hivi karibuni.

  “Hakika Muswada huu umekuja muda muafaka kwani tumepitia changamoto nyingi sana kama wanahabari ikiwa ni kupata ajali na kuugua mara kwa mara bila ya kuhudumiwa chochote na wamiliki wa vyombo husika vya habari hapa nchini” alisema Bw. Kasenyenda.

  Aidha Bw. Kasenyenda ambaye pia ni Mwanahabari mkongwe anayetumikia hii tasnia kwa muda mrefu amesema kuwa wanahabari wanatakiwa kuishukuru Serikali kwa kuleta huu muswada kwani una manufaa na ulinzi kwa wanahabari pindi wanapokuwa maeneo yao ya kazi .

  Mbali na hayo Mwanahabri huyo mkongwe nchini amesema kuwa wanahabari wanatakiwa kuusoma vizuri huo muswada na kutumia fursa hii kwa kutoa maoni yao ili upite na kuwa sheria nchini na wasicheze ngoma za wanasiasa ambao wanajinufaisha wao wenyewe bila kujali maslahi ya mwanahabari nchini.

  Kwa upande wa Mmiliki wa Blogu ya jamii inayojulikana kwa jina la Fullshangwe Bw. John Bukuku amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuleta muswada huu kwani kwa upande wa kipengele cha kuwapa bima waandishi wa habari itawafanya wawe salama Katika kazi zao wakati wowote na sehemu yoyote.

  “Naishukuru Serikali kwa kuleta muswada wa sheria ya habari hasa kwenye kipengele cha bima na mfuko wa hifadhi ya jamii kwani utakua ulinzi tosha kwa mwanahabari pindi atakapoumwa au kufariki itakuwa msaada mkubwa kwetu sisi wenyewe” alisema Bw. Bukuku.

  Naye Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira anayeripotia Tanga Bw. Mashaka amesema kuwa wanahabari wasibweteke katika kutoa maoni kuhusu huu muswada kwani ndio kimbilio la haki zao kutoka kwa waajiri wao ili kufanya kazi zao kwa usalama na amani wawapo sehemu zao za kazi.

  “Kwakweli wanahabari umefika muda wetu wa kufanya kazi kwa usalama na haki kama muswada huu utapita kwani utatufanya tupate haki yetu ya msingi Katika kazi zetu hivyo tusibweteke kutoa maoni yetu ili tuupitishe huu muswada kwa maendeleo yetu wenye”alisema Bw. Mashaka.

  Muswada wa sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 kifungu cha 58(1) kinasema mwajiri ni lazima amwekee bima na mfuko wa hifadhi ya jamii mwajiriwa wake hivyo wanahabari wanatakiwa kutoa maoni yao kupitia cna@bunge.co.tz.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
   Hapo ni mkurugenzi mtendaji akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
   Mmoja wa Wenyeviti wa Vijiji akizungumza katika kikao kazi hicho.
   Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Abel Noel akitoa ufafanuzi wa misingi ya Utawala bora.
   Viongozi watendaji, Maafisa Tarafa waliofika katika kikao kazi cha DC.


  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amewataka Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji kusimamia misingi ya utawala bora katika kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Aliyazungumza hayo katika kikao kazi alichokiitisha siku ijumaa tarehe 28/10/2016.

  Mh. Gondwe amewataka viongozi kusimamia rasilimali za umma ikiwemo misitu, ardhi na usimamizi wa suala zima la usafi na mazingira katika maeneo yao. Pia aliwakumbusha kusikiliza kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini ikiwa na kushughulikia malalamiko yao kabla ya kufika ngazi ya Wilaya. Wananchi wanatakiwa kusikilizwa matatizo yao, pale ambapo ngazi za chini zimeshindwa basi ngazi ya Wilaya itashughulika kikamilifu.

  Mh. Gondwe amewaeleza Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kwamba kutokana na hali mbaya ya chakula suala la kulima ekari moja ya muhogo kwa kila kaya ni lazima sio jambo la hiari tena. Aidha amepiga marufuku kutumia mazao ya chakula katika kutengenezea pombe kwa sababu hali ya chakula kwa sasa katika Wilaya ya Handeni sio nzuri.” Ni marufuku mazao ya chakula kutumika katika kupikia pombe kwa sababu hatuna chakula cha kutosha” alisema.

  Ametoa tahadhari kwa viongozi na Watendaji kuwa makini na taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s)zinapokuja kufanya huduma katika maeneo yetu, kwani taasisi nyingine zinakuwa hazina dhamira njema kwa wananchi kwani zimeonekana kufanya mambo ya kitapeli mfano baadhi yao zimekuwa zikichangisha fedha kwa wananchi bila kufuata utaratibu., ,”Viongozi wote na Maafisa Tarafa pale mnapoona kwenye maeneo yenu kuna taasisi zisizo za kiserikali zimekuja na hamuelewi mienendo yao tafadhali naomba mtoe taarifa mapema ili Uongozi wa Wilaya uweze kushughulikia mapema ” alisema.

  Aidha Mkuu wa Wilaya ya Handeni aliwataka Kitengo cha misitu kusaidia kuainisha hifadhi za misitu kwa ngazi ya Serikali kuu, Halmashauri na Vijiji ili wananchi waweze kuyatambua na kwamba watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi waondoke wenyewe kwa hiari yao kabla ya Serikali kuu na Halmashauri ya Wilaya haijawaondoa kwa nguvu. 
   
  Alisisitiza kwamba suala la kulinda maeneo ya hifadhi kama vile misitu, vyanzo vya maji na maeneo yaliyohifadhiwa sio la hiari Aliwataka halmashauri kuripoti pindi uharibifu wa maeneo hayo unapofanyika . Aidha Alipiga marufuku pia watoto chini ya umri wa miaka 18 kuchunga ng’ombe hasa siku za shule na kuwaripoti watu wanaoharibu miundombinu ya maji.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kutakua na ratiba ya kupanda miti laki 6 kwa msimu unaokuja wa mvua ambapo kila kaya itatakiwa kupanda miche ya miti kumi (10) ambayo watalazimika kuitunza ili iweze kukua.

  Mkurugenzi mtendendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kwamba atasimamia utekelezaji wa maelekezo yote aliyoyatoa ikiwemo utawala bora utakao husisha usomwaji wa mapato na matumizi katika vijiji vyote , utunzaji miti, hifadhi ya misitu na ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji.

  Alda Sadango

  Afisa Habari

  Halmashauri ya Wilaya Handeni

  29/10/2016


  0 0  Rais Dkt John Pombe Magufuli             
   


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

  Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.

  Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi

  Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldovillekilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

  Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.
  Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Nairobi
  30 Oktoba, 2016


  0 0  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
  Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
  Ofisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Okoa Njaa Wilayani Kongwa
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Richard Mwite
  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi akisisitiza vijana Kulima na kuacha kucheza mchezo wa Pool Table wakati wa kazi

  Na Peter Daffi, Dodoma

  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

  Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

  Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.

  Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

  Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

  Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029, Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.

  Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

  DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

  Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.

  Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.

  0 0
  Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.
   Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto . 
   Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa
   Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
   Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza
   Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto

older | 1 | .... | 1025 | 1026 | (Page 1027) | 1028 | 1029 | .... | 1897 | newer