Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1012 | 1013 | (Page 1014) | 1015 | 1016 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi, Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu, wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Robi Bwiru. 
  Kaimu Mkurugenzi, Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Bernard Haule akiongea na waandishi

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

  Simu: 255-22-2114615, 211906-12
  Barua pepe: nje@nje.go.tz
  Barua pepe: gcu@nje.go.tz

  Nukushi: 255-22-2116600

                

   

                  20 KIVUKONI FRONT,
                             P.O. BOX 9000,
                    11466 DAR ES SALAAM, 
                                      Tanzania.
   
  Mchakato wa kuanzisha Viza ya Pamoja ya Utalii katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Ndugu wanahabari:
  Wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii ya hapa nchini na nje ya nchi iliandika taarifa kuhusu Tanzania kujitoa au kugomea utaratibu wa visa ya pamoja ya utalii (Single Tourist Visa) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

  Kufuatia taarifa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekuwa ikipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kutaka kufahamu ukweli wa jambo hilo. Hivyo, Wizara imeona leo itoe taarifa rasmi kufafanua namna ya mchakato wa uanzishwaji wa viza ya pamoja ya utalii ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unavyoendelea.

  Suala la Uanzishwaji wa Viza ya Pamoja ya Utalii kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki bado liko katika majadiliano ya Nchi Wanachama kupitia Vikao vya Sekta ya Utalii na Wanyamapori. Katika kufanikisha azma hii,  Baraza la Kisekta la Mawaziri wa  Maliasili na Usimamizi wa Wanyamapori uliofanyika  tarehe 1 Novemba 2008 liliunda Kikosi Kazi kwa ajili ya kufanya  utafiti kwa lengo la kubainisha mahitaji na utayari wa Nchi wanachama juu ya kuanzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii.  Utafiti uliofanyika mwaka 2010, ulibainisha masuala muhimu yafuatayo ya kuzingatiwa kabla ya kuanzishwa kwa Viza ya Pamoja ya Utalii:

  a)    Kurazinisha  (harmonization) sheria za Viza za Nchi Wanachama;
  b)     Idara ya Uhamiaji  kuanzisha Mfumo  wa  kudhibiti Usalama;
  c)     Utoaji wa Viza kuwa wa kielektroniki;
  d)   Kuwepo kwa mfumo wa ukusanyaji na ugawanyaji wa mapato pamoja na namna ya kulipa;
  e)     Kuwepo kwa maafisa uhamiaji katika kila ofisi za ubalozi;
  f)      Kujenga uwezo wa watumishi kwenye suala la  mfumo wa kieletroniki  wa utoaji wa viza ya pamoja ya Utalii.

  Kufuatia matokeo ya utafiti huo, Mkutano wa 5 wa Baraza  la Kisekta la Mawaziri wa Utalii na Usimamizi wa Wanyamapori  uliofanyika  mwezi Julai 2013  jijini Bujumbura, Burundi pamoja na mambo mengine uliagiza kuundwa kwa kikosi kazi ambacho kitajumuisha wataalamu kutoka Taasisi za Uhamiaji, Utalii, Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Tehama, Usalama, na Sheria katika nchi wanachama ili  kuandaa mpango kazi  na  kushughulikia masuala yote ambayo  yatajitokeza kuhusiana  na uanzishwaji wa  Viza ya Pamoja ya Utalii. Hata hivyo, kabla ya utekelezaji wa maagizo hayo, Nchi za Uganda, Kenya na Rwanda zilianzisha  Viza ya Pamoja ya Utalii baina yao nje ya vikao vya Jumuiya.

  Ni vema ikaeleweka kwa umma wa Watanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla kuwa kwa kuzingatia Mfumo wa Maamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao ni wa kukubaliana kwa pamoja (consensus) hakuna Mfumo wowote wa uanzishwaji wa Visa ya Pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanzishwa. Hii inamaanisha kuwa hakuna Visa ya Pamoja ya Utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokubalika. Kwa mantiki hiyo, taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazina ukweli wowote na zilikuwa na lengo la kuichafua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

   Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawawahakikishia umma wa Tanzania kuwa itaendelea kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya Jumuiya na kushiriki katika majadiliano ya kuanzisha visa ya pamoja ya utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 18 Oktoba  2016.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi kufuatia vifo vya watu 11 vilivyosababishwa na ajali ya basi la kampuni ya Barcelona iliyotokea jana tarehe 17 Oktoba, 2016 katika eneo la Miteja Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

  Basi hilo lenye namba T 101 CUU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kijiji cha Mahuta katika Wilaya ya Newala Mkoani Lindi, lilipinduka baada ya gurudumu lake la kushoto kupasuka na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na mwingine 1 kufariki dunia baadaye akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Lindi, huku watu wengine 43 wakiwa wamejeruhiwa.

  Katika salamu zake, Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za vifo vya watu hao kwa mshituko na huzuni kwa kuwa kwa mara nyingine Taifa limepoteza watu wake na familia zimepoteza wapendwa wao na watu ambao ziliwapenda na kuwategemea.

  "Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa wote waliopoteza jamaa na ndugu zao katika ajali hii, kwa hakika nimeguswa sana na vifo hivi na naungana na familia za marehemu wote katika maombolezo na sala"amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli amewasihi wote walioguswa na vifo hivyo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

  Pia Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa,
   
  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  18 Oktoba, 2016


  0 0

  Sehemu ya kingo za Mto Mkondoo zilizoharibiwa na uharibifu wa mazingira Wilayani Kilosa
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba katika mkutano na wananchi katika Kijiji cha Katarukila akiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katurukila na kuwapongeza kwa kuwa Kijiji cha mfano kwa kuonyesha jitihada za dhati za kuhifadhi mazingira.
  Bwana Candidius Songela akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akingalia ramani inayo onyesha eneo lenye mgogoro baina ya wanakijiji wa Katarukila na mwekezaji. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo.

  ………………………………………………………………..

  Na Lulu Mussa-Kilombero

  Wananchi wa Kijiji cha Katurulika, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameahidiwa Mifuko mia moja ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati katika tarafa yao inayohudumia wakazi wa vijiji sita.

  Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameahidi kutoa mifuko hiyo ndani ya wiki moja ikiwa ni pongezi kwa Kijiji hicho kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na msitu wa Magombera.

  Awali, Bwana Dandidius Songela alimfamisha Waziri Makamba changamoto wanazokutana nazo katika Kijiji chao kuwa, ni pamoja na mgogoro baina ya Kijiji cha Katarukila na mwekezaji anayehodhi sehemu ya eneo la Kijiji na kusababisha uharibifu wa mazingira. Waziri Makamba aliwasihi wanachi wa Kijiji cha Katarulika kuwa ni jukumu lao msingi kulinda msitu huo kwa nguvu zao zote na kubainisha kuwa Hifadhi endelevu ya mazingira ndio mustakabali wa maisha yao.

  Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kumpa mwekezaji huyo “Restoration Order” kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa kumtaka arejesha mazingira katika hali yake ya asili, kwakuwa ni eneo tengefu.

  kwa upande mwingine Waziri Makamba amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilombero Bw. Dennis Londo kuhakikisha wanasheria wa Manispaa wanahudhuria kesi baina yao na mwekezaji huyo bila kukosa kila inapotajwa na baada ya kuhumu kutolewa Waziri Makamba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza kwa kina endapo kulikua na mianya yoyote ya rushwa katika mchakato wa kumilikisha ardhi ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.

  Waziri Makamba yuko ziarani Kilombero kuangalia changamoto za mazingira na awali alitembelea Mto Mkondoa Wilayani Kilosa.

  0 0

  WAFANYABISHARA Mkoani Shinyanga, wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kusajili majina ya biashara zao katika zoezi linaloratibiwa na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kutambulika kisheria na kuchangia mapato ya Serikali.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Bi. Zainabu Telack, amewahamasisha wafanyabiashara mkoani humo kutumia fursa ya kuwepo maofisa wa BRELA kutoka makao makuu ya BRELA kurasimisha biashara zao na kujifunza umuhimu wa kusajili majina ya biashara.

  “Tumepata bahati kubwa kutembelewa na maofisa wa BRELA ambao wanaendesha semina kwa wafanyabiashara na wakati huo huo kusajili majina ya biashara,” Bi.Telack alisema hayo mkoani hapa jana wakati wa semina ya wiki moja ya uhamasishaji wa usajili majina ya biashara inayoratibiwa na BRELA.

  Alisema azima ya serikali ya Awamu ya Tano ni kuwekeza katika biashara na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa lengo kubwa kukuza uchumi wa taifa, kuongeza ajira na kukuza kipato cha watanzania.

  “Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwashukuru na kuwapongeza BRELA kwa zoezi ili la uhamasishaji kwani ni matumaini yangu mwitikio utakuwa mkubwa sana,” alisema na kuongeza kuwa Shinyanga itakuwa mfano wa kuigwa katika urasimishaji biashara.

  Afisa mtendaji mkuu wa BRELA, Frank Kanyus, akiainisha faida za usajili wa biashara, amesema pamoja na mambo mengine kutasaidia serikali kupata mapato ili iweze kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi, alisema Wakala umejipanga na zoezi la kuzunguka nchi nzima kutoa elimu na faida za kusajili majina ya biashara nchi nzima.

  “Mikoa ambayo tumeshafanya semina tulipata mwitikio mkubwa na pia watu wengi walijitokeza kusajili majina ya biashara zao,” alisema na kuongeza kuwa wakala ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kurasimisha shughuli zao.Alisema tayari BRELA imeshatoa semina katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Geita ambapo wiki ijayo semina za uhamasishaji zitafanyika mkoani Tabora.

  Naye, Afisa Mtendaji wa Chama cha wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), Mkoani Shinyanga, Bi.Malicelina Saulo,alisema jumuiya ya wafanyabiashara imefuruhishwa na semina yenye lengo la kuwajengea uelewa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kusajili majina ya biashara zao.

  “Hii ni fursa pekee kwa wafanyabishara mkoani Shinyanga kujisajili majina ya biashara zao na kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali mrefu hadi Dar es salaam,” alisisitiza.

  0 0

  Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) imejipanga kuwekeza katika sekta ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ili kuchangia kukuza uchumi wa taifa na ajira.

  Akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa kampuni hiyo jijiji Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Aloys Mwamanga, imejipanga kuanzaisha viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo, lakini hakutaja idadi ya viwanda na kiasi kitakachotumika. 

  Alipoulizwa nje ya mkutano sababu za kuwekeza katika viwanda hivyo, alisema kampuni inaunga mkono kwa dhati dhamira ya serikali ya kuwekeza katika sekta ya viwanda na hasa viwanda vya kusindika mazao. Kampuni imepata faida ya shilingi 564.18 milioni kabla ya kodi.

  Bw. Mwamanga amefafanua kuwa kampuni yao ni Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja ambayo imejitokeza kuwa mfano wa kuigwa nchini, na kuongeza kwamba pamoja na ongezeko la gharama za uendeshaji kwa sababu ya kupanuka kwa shughuli za kampuni bado ina uwezo wa kuwekeza. Mwaka 2014 kampuni ilipata faida ya shilingi 784.23 milioni.


  Mwenyekiti huyo amesema kwa uwezo iliyonao, kampuni imepanga kuwekeza pia katika dhamana za serekali na makampuni, amana katika mabenki, uanzishaji wa microfinance, ujenzi wa jingo la ofisi na maghala ya kuhifadhi bidhaa.

  Alisema uwekezaji huu utakapo kamilika utawezesha wanahisa kupata fedha nyingi zitakazo tokana na gawio la kila mwaka.Amefafanua kuwa kutokana na kushuka kwa thamani ya hisa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam, mtaji wa kampuni uliathirika kidogo na kupungua kutoka. bilioni 34.56 Desemba 31 mwaka 2014 kufikia bilioni 31.95 Desemba 31, mwaka 2015. 

  Kampuni ilipoanza shughuli za biashara Octoba,Mosi, 2005 mtaji wake ulikuwa sawa na bilioni 1.97, alieza Bw. Mwamanga.Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori alisema kampuni inakusudia kujiorodhesha katika Soko la Hisa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata mtaji na kufanya uwekezaji zaidi kwa manufaa ya wanahisa na nchi.

  “Lengo letu ni kuuza jumla ya hisa 112,500,000 kwa bei ya shilingi 400 kwa kila hisa moja,” na aliongeza kusema kuwa kama hisa zote zitauzwa, watapata bilioni 45.Mmoja wa Wanahisa, Dkt. Tom Maeda, kutoka Hanang, Mkoa wa Manyara ameunga mkono dhamira ya kampuni ya kupanua uwekezaji ili kuongeza mtaji utakao fungua fursa zaidi.

  Aliwataka wanahisa wenzake na Watanzania kununua hisa zitakapotangazwa sababu hisa ni uwekezaji ni ukombozi wa mtu anayenunua hisa.Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA ina wanahisa wake 2,443 na ina rekodi ya kufanya mkutano mkuu kila mwaka.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment Plc),Mhandisi Aloys Mwamanga (katikati) akifungua Mkutano Mkuu wa Kumi na Moja (11) wa wanahisa wa kapuni hiyo. (Kulia) ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori na kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Bi. Hanim Babiker. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam).

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori (kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji kwa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo, ambapo wanahisa walikutana kujadili maendeleo ya kampuni yao, (katikati)ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo,Mhandisi Aloys Mwamanga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti,Bi. Hanim Babiker.

  Wanahisa wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji yaTCCIA (TCCIA Investment PLC), Bw. Donald Kamori hayupo pichani wakati wa mkutano mkuu wa kumi na moja (11) wa kampuni hiyo. (Picha na mpiga picha wetu, Dr es Salaam

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa wa Lindi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaoharibu mazingira kwa kufyeka na kuchoma moto misitu kwa sababu wanaharibu mazingira na kusababisha ukame.

  Amesema mkoa huo upo hatarini kugeuka jangwa na tayari vyanzo vingi vya maji vimeanza kukauka kwa sababu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na watu kufanya shughuli za kijamii kwenye vyanzo vya maji.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 18, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Nanjaru, Nachinyimba, Nambiranje, Mkaranga, Nandenje, Nachinyimba na Mandarawe.

  Amesema wakulima wa ufuta wanatakiwa kuendelea kutumia mashamba yao ya zamani na kuacha tabia ya kufyeka misitu kila mwaka na badala yake waanzishe mpango wa upandaji miti ili kuepusha taifa kugeuka kuwa jangwa.

  “Vyanzo vya maji vimekauka kwa sababu tumekata miti mingi. Mito yote iliyokuwa inatiririsha maji imekauka. Viongozi wa mkoa hakikisheni misitu inalindwa na atakayekutwa analima kwenye vyanzo vya maji akamatwe,” amesema.

  Waziri mkuu aliongeza kuwa “Ukataji miti huu unaoendelea katika maeneo yetu  hakutosababisha kukosekana kwa maji tu, bali  hata mazao yatapungua. Jambo hili  itasababisha njaa katika vijiji vyetu, hivyo tuache kukata miti.

  Waziri Mkuu amesema kwa sasa Serikari inatumia gharama kubwa kuchimba visima virefu kutafuta maji. Amesema zamani walikuwa wanachimba mita 20 au 30 wanakuta maji na gharama yake ilikuwa sh. milioni 35, ambako kwa sasa wanalazimika kuchimba mita zaidi ya 150 kwa gharama y ash milioni 75 kwa kisima kimoja.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi,amewataka watendaji wa kata na vijiji kuimalisha ulinzi wa maeneo ya misitu na maji, na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  “Hatuko tayari kutengeneza jangwa hivyo tutapamba na wale wote wenye tabia za kuchoma moto misitu au kulima kwenye vyanzo vya maji,” amesema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMNNE, OKTOBA 18, 2016

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi akizungumza na wakazi wa Magomeni Suna, Jijini Dar es Salaam leo, baada ya kusikiliza kero zao.

  Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii.

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi, amemwagiza Mkuu wa Polisi Kanda ya Magomeni Salum Morcase, kufanya uchunguzi wa kina katika nyumba zinazo sadikiwa kuwa zinahifadhi katika kata ya Magomeni Makuti.

  Hapi alitoa agizo hilo, baada ya kusikiliza kero ya wanachi wa kata ya Magomeni Suna, waliolalamika kuna nyumba inayotunza wahalifu imekuwa tishio katika mtaa wa Makuti.Hapi alimwagiza Mkuu wa Polisi kufanya doria katika eneo hilo, kwani nyumba hiyo imekuwa kero kwa wananchi.

  Mbali na kuwakamata wahalifu hao, Hapi aliagiza mmiliki wa nyumba hiyo kukamatwa ili aweze kuisaidia Polisi kukamatwan kwa wahalifu hao.Naye Mkazi wa eneo hilo Sabrina Ibrahimu alisema kuwa, nyumba hiyo inatunza vibaka, wavuta bangi, ambao wamekuwa kero kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwaibia fedha na mali zao.

  Ibrahim alisema kuwa, vijana wanaoishi katika nyumba hiyo wamekuwa wakivuta bangi nje ya adhara, huku wakiwahalaso hata watoto wa shule wanaopita nje yanyumba hiyo wakielekea shule.Aidha mkazi huyo alidai kuwa, nyumba hiyo imekuwa tishio katika maeneo hayo, huku Polis wakionekana kutochukua hatua yoyote licha ya kuwa jershi hilo linataarifa za uhalifu huo.

  0 0

  Na Editha Karlo, wa blog ya jamii,Missenyi

  SHULE ya msingi Byamutemba iliyopo katika kata ya Nsunga Wilayani Misenyi imefungwa kwa muda wa wiki tatu baada ya shule hiyo mapaa ya shule hiyo kuezuliwa na upepo mkali.

  Tuki hilo limetokea leo majira ya mchana wakati wanafunzi wakiendekea na masomo darasani na kusababisha baadhi ya wanafunzi kujeruhi.Upepo huo umeezua mapaa ya shule hiyo nyumba moja ya mwalimu pamoja na nyimba tatu za wakazi wa kijiji cha Byamutemba.

  Mganga msaidizi wa Wilaya ya Missenyi Godon amekiri kupokea wanafunzi hao waliojeruhiwa 14 na wanafunzi 7 wakirudishwa nyumbani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Zahanati ya Igayaza.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denis Mwila alisema kuwa wameifunga shule hiyo kwa miezi mitatu wakati wanafanya utaratibu wa kuijenga shule hiyo kwa haraka.

  Alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 903.
  Shule ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi imeezuliwa na upepo mkali na kupelekea Wanafunzi saba kujeruhiwa,kufuatia tukio hilo, shule hiyo kwa sasa imefungwa kwa muda.
  Baadhi ya Wanafunzi wakiwa wamelazwa katika Zahanati ya Igayaza,baada ya kujeruhiwa na tukio hilo
  Baadhi ya wananchi wakijadiliana jambo kufutia shule hiyo kuezuliwa na upepo mkali .
   

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)  akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto) na Nirina Kiplagat, walipofika kwa ajili ya  kujadiliana juu  ya masuala ya amani na maendeleo.Kulia ni Katibu wa naibu waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  unb2
  Meneja Mradi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat akizungumza na  Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Katikati ni Mshauri wa Mradi kutoka UNDP, Lawrence Lachmansingh. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  unb3
  Mshauri wa Mradi kutoka  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Lawrence Lachmansingh (wapili kushoto), akizungumza na Naibu Waziri waWizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo.Watatu kushoto ni Meneja Mradi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  unb4
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiagana na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat (aliyeshikana naye mkono) na ) Lawrence Lachmansingh, baada ya kumaliza majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  unb5
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiwasindikiza wageni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Nirina Kiplagat na Lawrence Lachmansingh(kushoto), baada ya kumaliza majadiliano juu ya masuala ya amani na maendeleo. Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0


       Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akifungua Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. Mkutano huo umeandaliwa na Africa Group for Justice and Accountability.  
  1.       Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye Majadiliano leo jijini Arusha. Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wamewakilisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini, Sierra Leone, Uganda, Tanzania, Kenya, na Botswana.      
  1   Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akishiriki kwenye Mjadala kuhusu masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha.

   Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki Kimataifa wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Hayupo Pichani) wakati akifungua mkutano huo leo jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability Mheshimiwa Catherine Samba-Panza.
     Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman (Katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Africa Group for Justice and Accountability na aliyekuwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Mheshimiwa Hassan Bubacar Jallow kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa unaojadili masuala ya Haki kimataifa leo jijini Arusha. 
  PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya katiba na Sheria Bw Amon Mpanyu akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau kutoka Nchini Ghana, Marekani na mashirika ya Kimataifa ya maendeleo waliokutana hii leo Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani kwa lengo la kujadili Mifumo mbalimbali ya kisheria inayosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na Ukusanyaji wa takwimu,kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson na kushoto kwake ni Msajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu kutoka Marekani state ya Hawaii Bw Alvin Onaka,pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi Erica Yegela.
  Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kwa umakini majadiliano kuhusu maboresho ya mifumo ya sheria zinazosimamia masuala ya usajili wa matukio muhimu ya maisha ya binadamu katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.
  Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw Amon Mpanju katika Hoteli ya Stella Maris Mjini Bagamoya Mkoani Pwani.


  0 0

  0 0

  NA VICTOR MASANGU, RUFIJI.

  MBUNGE wa jimbo la rufiji Mohamed Mchengerwa ameahidi kuvisadia vikundi mbali mbali vya wakinamama wajasiriamali kwa lengo la kuweza kuwainua kiuchumi na kuweza kuinua mitaji waliyonayo ili kuondokana na janga la umasikini na kuwa tegemezi.

  Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuwatembeea wananchi wa jimboni kwake kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbai zinazowakabili kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

  Alisema kuwa katika jimbo lake la rufiji kuna vikundi mbali mbali vya ujasiriamali hivyo atajitahidi kwa hali na mali kuvisaidia kuviwezesha fedha ambazo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kaatika shughuli zao za kila siku na kuleta mabadiliko chanaya ya kimaendeleo.

  “Mimi kama mbunge wa jimbo la rufiji wananchi mmenipa dhamana kubwa ya kuwatumikia hivyo kwa upande wangu nitahakikisha yale yote ambayo nimewea kuwaahidi wakati wa kampeni nitayafanyia kazi kwa vitendo, na ninahitaji wakinamama wote mjiunge katika vikundi ili iweze kuwa rahisi katika kuwasaidia kuliko mtu mmoja mmoja,”alisema Mchengrwa.

  Aidha aliongeza kuwa ana imani endapo vikundi hivyo vya wakinamama vikiwezeshwa vitaweza kupiga hatua kubwa ya kuweza kujiajiri wao wenyewe na kuendesha biashara zao ambao zitaweza kuwapataia kipato amabcho kitaweza kusaidaia katika kuendesha familia zao kuliko ya kuwa na tabia ya kuwa tegemezi kwa watu wengine.

  Alisema kuwa japo anatambua wananchi wa jimbo lake wanakabiliwa na changamoto mbali mbali lakini kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano atashirikiana nayo bega kwa bega kwa lengo la kuweza kuleta maendeleo makubwa katika Wilaya ya Rufuji.

  Aidha katika hatua nyingine Mchengerwa katika ziara yake hiyo aliweza kukitembelea kikundi cha wakinamama wajasiriamali katika kijiji cha mloka na kukikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuweza kukuza mtaji wao pamoja ana kujiendeleza zaidi katika kukuza biashara zao wanazozifanya kila siku.

  Pia mbunge huyo aliwahimiza wakinamama wa wilayani Rufiji kuhakikisha fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya kikundi zinatumika vizuri bila ya kuwa na ubaguzi wa aina yoyote na badala yake zitumike kwa manufaa ya wanachama wote ambao wanatarajia kujikwamua kiuchumi na kuweza kuondokana na tatizo la umasikini.
  Mbunge wa jimbo Rufiji Mohamed Mchengerwa kulia akimkabidhi mmoja wa viongozi wa kikundi cha wakinamama wajasiriamali katika kijiji cha Mloka cheki ya kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kukuza mtaji wao
  Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na badhi ya wakinamama baada ya kufanya ziara yake ya kuwatembelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanagamoto zao zinazowakabili.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa mabati 100 yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni mbili kutoka kwa Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Lindi Mhe. Hamida Abdallah.

  Msaada huo umetolewa leo (Jumatano, Oktoba 19, 2016) katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu hospitalini hapo.Mbunge huyo amesema amekabidhi msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu wakati Waziri Mkuu alipofanya ziara katika Hospitali hiyo.

  “Ulipofanya ziara ya mwezi wanne hospitalini hapa nilikuahidi kukupa mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake. Nilitoa ahadi hii baada ya kuona jitihada kubwa unazozifanya katika kuimarisha hospitali hii,” amesema.

  Akipokea msaada huo Waziri Mkuu amemshukuru Mhe. Hamida kwa kutekeleza ahadi yake na kumuomba aendelee kuisaidia hospitali hiyo pindi anapopata nafasi.” Nashukuru sana kwa msaada wako tunajua kutoa ni moyo na si utajiri,”.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema mkakati wake kwa sasa ni kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kuwawezesha wananchi kupata matibabu karibu na makazi yao.

  “Nataka sekta ya afya inapata mafanikio makubwa. Nitashirikiana na wananchi kuhakikisha kunakuwa na zahanati katika kila kijiji na vituo vya afya kwenye kata zote,” amesema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue alimshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada zake za kuboresha huduma hospitalini hapo.

  Amesema hivi karibuni walipokea sh. milioni 100 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi kwa ajili ya ukarabati wa wodi mbili ambazo tayari ukarabati huo umekamilika na zitaanza kutumika kuanzia Novemba 15 mwaka huu.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, OKTOBA 19, 2016.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea mchango wa mabati 100 kutoka kwa Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Lindi,Bi Amida Abdalah kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya  ya Ruangwa,kulia ni Mganga MKuu wa Wilaya ya Ruangwa Dkt Japhet Simeo,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Majaliwa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh.Godfrey Zambi wakishuhudia tukio hilo  ambali makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali Ruangwa 
   Mama Majaliwa akiwasalimia wauguzi na wananchi walio jitokeza katika makabidhiano ya mabati 100 yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Lindi. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi na Mganga mkuu wa Hospitali ya Ruangwa Dr Japhet Simeo wakati waziri mkuu alipotembelea Hospitali ya Wilaya Ruangwa Mkoa wa Lindi.Picha na Chris Mfinanga.

  0 0

  Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi (Nec) inaendelea kutekeleza mkakati Wa Kutoa Elimu Ya Mpiga Kura Kwa Wananchi Ili Kuimarisha Demokrasia Nchini.

  Mwenyekiti Wa Tume Hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva Anatoa Wito Kwa Wananchi Kuendelean Kutoa Ushirikiano Wao Kwa Nec Ili Kufanikisha Mkakati Huo.

  Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Uchaguzi Wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Anatoa Wito Kwa Wananchi Ili Kuhakikisha Elimu Ya Mpiga Kura Inamfikia Mlengwa.

  Mkakati Wa Kutoa Elimu Ya Mpiga Kura Ni Utekelezaji Wa Kifungu Cha 4 (C) Cha Sheria Ya Uchaguzi Ya Mwaka 1985 Inayoitaka Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi Kutoa Elimu Hiyo, Kusimamia Na Kuratibu Asasi Na Taasisi Zinazotaka Kutoa Elimu Ya Mpiga Kura.

  0 0

  Kuna taarifa inasambazwa katika mitandano mbalimbali ya kijamii  leo hii ikidaiwa imetolewa na kitengo cha Mawasiliano,IKULU, kama inavyoeleza hapo juu,si ya ukweli,mnaombwa muipuuze,ni taarifa iliotengenezwa na baadhi ya watu wenye nia ovu ya kupotosha ukweli,hivyo mnaombwa kuipuunza.

  0 0

  Kuna taarifa inasambazwa katika mitandano mbalimbali ya kijamii  leo hii ikidaiwa imetolewa na kitengo cha Mawasiliano,IKULU, kama inavyoeleza hapo juu,si ya ukweli,mnaombwa muipuuze,ni taarifa iliotengenezwa na baadhi ya watu wenye nia ovu ya kupotosha ukweli,hivyo mnaombwa kuipuunza.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari kusiana na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce na kushoto ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP bw, Charles Matondane
  Toka kulia ni meneja wa Airtel Money bw, Moses Alphonce akiwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakionyesha jinsi huduma yao ya kulipia simu za smartphone Bima ijulikanayo kama “Linda simu na Airtel Simu Bima” Inavyofanya kazi. Kupitia huduma hiyo sasa wateja wote wanaotumia Smarphone nchni wataweza kuziwekea Bima zao simu kulipia kupitia huduma ya Airtel Money na endapo simu hiyo itaibwa au kupotea mteja atalipwa ndani ya siku tano. kushoto anaefuatilia uzinduzi huo ni muwakilishi wa kampuni ya bima ya UAP Tanzaninia bw Charles Matondane ambao wao watakuwa wakiwalipa wateja.
  Meneja Masoko wa kampuni ya Bima ya UAP bw, Raymond Komanga akielezea jinsi mfumo wa malipo wa Airtel SimuBima unavyofanya kazi kwa kushirikiana kampuni yake mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya kulinda simu za smartphone kupitia bima ijulikanayo kama Airtel SimuBima, katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money bw, Moses Alphonce (kulia) huduma ya AirtelSimuBima itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.

  …………………………………………………………….

  · Wateja wa mitandao mingine pia wataweza kusajili simu zao na bima hiyo na kulipia kwa Airtel money

  · Airtel Simu Bima kufidia simu za wateja wake zilizopotea au kuibwa

  Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP leo wamezindua huduma kabambe itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money.

  Huduma hiyo mpya nchini kwa watumiaji wa smartphone itajulikana kama “Airtel SimuBima” ambapo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbandoalisema “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya ‘Airtel SimuBima’ ambapo mteja mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili katika mfumo huu. Ikitokea mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia mteja huyo pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena”.

  “Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima” mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu yake na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila mwezi” aliongeza Mmbando

  “Airtel Tanzania tunaamini kuwa ushirika wetu na shirika la bima la UAP kupitia ‘Airtel SimuBima’ utasaidia kuhamasisha watumiaji wa simu za mkononi kununua simu orijino ili waweze kufurahia huduma hii pamoja na huduma zingine za Airtel za kimtandao kama vile Airtel TV, Kujisomea masomo ya VETA –VSOMO kupitia mtandao pamoja na kufaidi aplikesheni mbalimbali za airtel zenye kusaidia wateja katika mambo ya kiuchumi na kijamii” alieleza Mmbando

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema “tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na kutujulisha sisi, tutalipa simu za hadi shilingi milioni moja na laki tano, lakini wateja waelewe kuwa bima yetu haitakuwa ikilipa simu kuvunjika au

  Komanga aliendelea kuelezea kuwa “Ikitokea simu ya mteja iliyosajiliwa na “Airtel SimuBima” imepotea au kuibiwa mteja atatakiwa kutoa taarifa mapema sana na kupata taarifa ya polisi kuhusiana na upotevu huo au wizi ili kuweza kukamilisha malipo yake. Swala hili linatakiwa kufanywa na wateja wote waliojisali na kulipia bima ya mwezi au ya mwaka mzima kupitia Airtel SimuBima”

  Wateja wa “Airtel SimuBima” wataweza kudai malipo yao kwa kutumia simu nyingine ya smartphone na kuingia katika Aplikesheni ya Airtel SimuBima kisha kufuata maelekezo ya malipo. Vilevile mteja anaweza kutumia kompyuta na kuingia katika ukurasa wa ‘Airtel SimuBima’ na kukamilisha taarifa za madai.

  “Ukitaka kulipia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ piga *150*60# kisha chagua malipo, na uchague SimuBima, papohapo malipo yatatufikia sisi moja kwa moja”. Bw, Komanga alisema.

  0 0

  Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer akitoa hotuba yake katika Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Katikati ni Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-meza kuu), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu. Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Wapili kushoto meza kuu ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (katikati), akiteta jambo na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer, mara baada ya Katibu huyo kufungua Warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Fella alisema baada ya warsha hiyo, washiriki hao wataanza kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-waliokaa), Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer (wapili kushoto-waliokaa), Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi (kushoto-waliokaa), Meneja wa Mradi Umoja wa Ulaya (EU), Anna Costantini, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Taasisi za Serikali pamoja na Mashirika yasiyokuwa ya Serikali, mara baada ya kufunguliwa warsha ya siku mbili ya kujadili namna ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  ………………………………………………………….

  Na Felix Mwagara, MOHA

  SERIKALI kwa kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa wameanza kujadili nyenzo mbalimbali ambazo zitasaidia kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu nchini.

  Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu, inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella alisema warsha hiyo ni muhimu ikiwa na lengo la kusaidia idadi kubwa ya watoto walioathirika nchini.

  Alisema Tanzania ambayo ni kati ya mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto kwa lengo la kwenda kuwatumikisha kazi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na duniani kwa ujumla, kupitia nyenzo hizo zitakazo jadiliwa zitasaidia kutoa elimu kwa umma juu ya matatizo hayo nchini.

  “Nyenzo hizi za kuwasaidia na kuwalinda wale watoto walioathirika baada ya kutoka katika maeneo mbalimbali zitasaidia kutoa elimu ya kuwandaa kisaikolojia ili wasikate tamaa na maisha, pia watoto watalindwa na baadaye watarudishwa kwa wazazi wao ili waweze kuendelea majukumu mengine ya kujenga taifa,” alisema Fella na kuongeza;

  “Kumekuwepo na wimbi kubwa la kuwasafirisha wasichana wa Kitanzania kwenda nchi za uarabuni kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani, ila wanapofika huko mambo yanawaharibikia wanaanza kudhalilishwa, kunyanyaswa kiasi kwamba wanashindwa kupata misaada, kutokana na manyanyaso hayo urudi nchini wakiwa wameathirika kwa kiasi kikubwa.”

  Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma kuhusu kukomeshwa kwa biashara hiyo haramu na wazazi kutokuwaruhusu watoto wao kwenda kufanyiwa unyanyasaji huo kwa kuwa ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, kutokana na wimbi hilo kuzidi kushika kasi nchini, pia wadau hao watatoa elimu ya watoto walioathirika mara baada ya kurudi nchini ili wajitambue kutokana na mateso mbalimbali waliokumbana nayo ili wasiweze kukata tama kutokana na vitendo vya ukatili walivyofanyiwa katika maeneo wanayotoka.

  Aidha, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer alisema Tanzania ni kati ya nchi zilizoathirika na biashara haramu ya kusafirisha watoto, hivyo elimu inahitajika ili kukomesha biashara hii hatari.

  “Watoto wa leo ni mabibi na mabwana wa kesho, hivyo wapaswa kulindwa pamoja na kuelimishwa, Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwasaidia watoto waweze kuepuka mateso wanayoyapata,” alisema Roeland.

  Warsha hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na inatarajiwa kumalizika Oktoba 20 mwezi huu ambapo wadau hao wataanza kufanyia kazi nyenzo hizo zilizojadiliwa.

  0 0


older | 1 | .... | 1012 | 1013 | (Page 1014) | 1015 | 1016 | .... | 1898 | newer