Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Semina ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa wanahabari yatolewa na TAMWA.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.  Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.Mmoja wa watoa mada kutoka TAWLA akiwasilisha mada yake katika mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam. Mmoja wa watoa mada kutoka TAWLA akiwasilisha mada yake katika mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. 

Alisema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia. 

 Alisema wanawake wanaoachwa peke yao na familia wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa familia jambo ambalo limeendelea kuwaingiza katika hali ngumu. Aidha aliongeza kuwa pamoja na hayo ajali nyingi za waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zimekuwa zikiwaathiri akina dada na akina mama ambao ndio watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kiasi kikubwa. 

 Tamwa katika mradi huo imejikita katika kutoa elimu ya madereva kuepuka ulevi, ufungaji mikanda ya usalama katika magari, mwendo kasi na matumizi ya kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao. Kwa upande wake Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema suala la usalama barabarani si jukumu la taasisi moja hivyo kila mtu anapaswa kushiriki katika kupambana na hatimaye kutokomeza ajali hizo ambazo zimekuwa zikipoteza roho za watu, mali pamoja na kusababisha ulemavu kwa baadhi ya waathirika wa ajali hizo.

NHIF MANYARA YAZINDUZI iCHF ILIYOBORESHWA KWA WANANCHI WA HANANG'

$
0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Bryceson Kibasa akizungumza na wananchi wa Tafara ya Simbay kwenye uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) ambapo alisema wameboresha hospitali ya wilaya hiyo Tumaini ikiwemo dawa kupatikana kwa wingi.


 Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, Henry Shekifu akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Simbay Wilayani Hanang’ juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) ambapo huduma hizo zitatolewa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za Serikali ndani ya wilaya pia katika zahanati, vituo vya afya na hospitali binafsi na taasisi za dini zilizo ndani ya wilaya na kusajiliwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Sarah Msafiri Ally akizungumza kwenye uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (iCHF) wilayani hupo ulioratibiwa na ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara na kufanyika katika Kata ya Simbay ambapo wananchi wanapaswa kuchangia shilingi 30,000 na kutibiwa kaya moja yenye watu sita kwa mwaka mmoja.
Mkazi wa Tarafa ya Simbay Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Stephan Songay akizungumza kwa kuwasisitizia wananchi wa eneo hilo kujiunga na mfuko wa afya iliyoboreshwa iCHF kwa kuchangia shilingi 30,000 na kutibiwa bure kwa mwaka mmoja, kaya moja yenye watu sita, baba, mama na watoto wanne ambao hawajatimiza umri wa miaka 18.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WILSON MASILINGI NA PHILIP MARMO PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERALI GEORGE WAITARA IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa  Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kitabu  kutoka kwa Mkuu wa Majesho Mstaafu Jenerali George Waitara aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
akiagana na  Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara baada ya kukutana   naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe: Philip Marmo alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016

Rais Magufuli afuta safari za Viongozi wa Mikoa na Wilaya kwenda Bariadi Kuzima Mwenge wa Uhuru

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akitangaza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na sherehe za kuzima mwenge mkoani Simiyu.PICHA NA IKULU






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.

Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.

Kwa kuwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka Viongozi wote wa Mikoa na Wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza Wilaya zote ambazo zimefanya vizuri katika shughuli za maendeleo wakati Mwenge ulipokuwa katika maeneo yao, zitambuliwe kwa kutangazwa rasmi katika siku ya kilele cha Mbio za Mwenge na kwamba zawadi zilizoandaliwa zitapelekwa kwa wahusika kwa utaratibu utakaoelekezwa na Mamlaka inayohusika kutoa zawadi hizo.

Hata hivyo Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa kutokana na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa Taifa, Viongozi wote wa Serikali ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake pamoja na wananchi wote wa mkoa huo wajitokeze kwa wingi na kushiriki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru siku hiyo ya tarehe 14 Oktoba, 2016.

Mgeni Rasmi katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam          
12 Oktoba, 2016

TAARIFA KUTOKA MAKAO MAKUU YA JWTZ

$
0
0
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis  Mwamunyange (watatu kushoto), akiwa na Mkuu wa Jeshi la Anga la Zimbabwe luteni Jenerali (Air Martial) Penance Shiri (wapili kushoto), alipotembelea Makao Makuu  ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Octoba 2016.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis  Mwamunyange (kulia) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Anga la Zimbabwe luteni Jenerali (Air Martial) Penance Shiri, alipotembelea Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Octoba 2016, wakati wa ziara ya kikazi nchini.

TAARIFA YA KUANZA KWA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE MJINI DODOMA

$
0
0

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza tarehe 17 Oktoba hadi tarehe 30 Oktoba 2016, Mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa
Tano wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 1 Novemba 2016. 

Kufuatia
Ratiba hiyo ya shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote
wanapaswa kuwa wamewasili Mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 16
Oktoba, 2016 kwa ajili ya kushiriki vikao hivyo.

2.0       SHUGHULI ZILIZOPANGWA KATIKA RATIBA
katika Vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama
ifuatavyo:
  1. a)KUPOKEAMAONI YA WADAU WA MISWADA MBALIMBALI
Kamati mbili (2) za Kisekta zitajadili Miswada miwili ya Sheria
ambapo Kamati ya Katiba na Sheria itajadili Muswada wa Sheria
ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na. 3 wa Mwaka 2016 [The
Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2016] na itakuwa na
vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya
tarehe 21 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Serengeti, Ofisi ya Hazina
Mjini Dodoma kuanzia saa tano (5:00) Asubuhi ambapo Sheria hiyo
ina jumla ya Sheria 9 zitakazofanyiwa marekebisho na Muswada
huu.

Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
ambayo itajadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa
Mwaka 2016 [The Media Services Bill, 2016] na itakuwa na vikao vya
kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 19
Oktoba, 2016 Katika ukumbi ulipo katika Jengo la Mdhibiti na
Mkaguzi     Mkuu wa Hesabu za Serikali Mjini Dodoma kuanzia saa
tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa(9:000) Alasiri.

Pamoja na kamati hizo mbili za kisekta, pia Kamati ya Sekta
Mtambuka ambayo ni Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo nayo
imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public
Hearing) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali
katika Mkutano wa Nne wa Bunge. Mikutano hiyo inatarajiwa
kufanyika kati ya Jumanne tarehe 18 Oktoba, 2016 na Alhamisi
tarehe 27 Oktoba, 2016 katika Jengo la Hazina (Treasury Square)
Mjini Dodoma.

Wadau wote katika Miswada tajwa hapo juu wanakaribishwa
kufika mbele ya Kamati kutoa maoni yao katika tarehe na muda
uliotajwa.
  1. b)KUPOKEATAARIFA ZA KIUTENDAJI WA WIZARA
Kamati tisa (9) za kisekta zitapokea Taarifa za utendaji wa Wizara
zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1)
(c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo Januari, 2016.
  1. i) Kamatiya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama itapokea na
kujadili Taarifa za wawakilishi wa Bunge katika SADC – PF,
ACP – EU na CPA kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (2) (iii) na (iv)
cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016.

MJI WA DODOMA LAZIMA UPANGWE – WAZIRI MKUU.

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Molad Bwana Abeid Abdallah akimuonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baadhi ya picha na michoro ya nyumba za kisasa na zabei nafuu zinazo weza kujengwa Dodoma Picha na ofisi ya Waziri Mkuu.

 Waziri Mkuu Kassim Majiliwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molad Tanzania Bwana Abeid Abdallah ambaye kampuni yake inajishughulisha na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa gharama nafuu Waziri mkuu ameikaribibisha kampuni hiyo kujenga nyumba za watumishi Mkoani Dodoma mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mji wa Dodoma ni lazima upangwe ili uwe tofauti na miji mingine hapa nchini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kuelezea nia yake ya kutaka kuwekeza mjini Dodoma.

Amesema Serikali haitaki kurudia makosa yaliyofanyika kwenye miji mingine. “Katika kuupanga ule mji, ni lazima mji upangwe kama ambavyo miji mingine mikuu inapangwa. Kila eneo kutakuwa na nyumba za aina fulani. Hatuwezi kuachia watu wajenge popote na wanavyotaka, mji unakuwa haupangiki. Na hilo ndilo kosa lililofanyika kwenye miji mingine mikubwa ambayo tunayo kwa sasa.”

Amesema Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya kuhamia Dodoma imepewa jukumu la kupitia upya Master Plan ya mji wa Dodoma na kuainisha maeneo ambako nyumba za aina mbalimbali zitajengwa.

“Kimsingi tunataka tuanze kujenga miji iliyopangiliwa na Dodoma tunataka uwe wa mji kwanza kuujenga vizuri kwa standard ya sasa. Kutakuwa na nyumba za ghorofa katika maeneo fulani, na nyumba za kawaida katika maeneo fulani. Mkurugenzi wa CDA amekwishaandaa ramani rasmi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu ujenzi kwenye maeneo ambayo tayari wananchi wanaishi, Waziri Mkuu amesema Serikali itaweka utaratibu ili kuwe na mikataba baina ya mwekezaji na mwananchi anayemiliki eneo husika ili asinyimwe haki ya kumiliki eneo lake.

“Kama tutahitaji eneo ambalo tayari lina makazi, taratibu zetu ni zilezile kwamba tutaweka mikataba kati ya mwekezaji na mwananchi. Kama anataka kujenga kwenye eneo lile, basi lazima amhusishe mwenye eneo na kama anataka kujenga ghorofa ni lazima ahakikishe mwenye eneo anapata umiliki kama tulivyofanya kule Magomeni,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali katika zoezi la Serikali kuhamia Dodoma kwa lengo wa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata makazi bora na ya kudumu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.
JUMATANO, OKTOBA 12, 2016. 

KAMPUNI YA MOLADI KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI DODOMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameikaribisha kampuni ya ujenzi ya Moladi Tanzania ielekeze nguvu zake Dodoma ambako kuna mahitaji makubwa ya nyumba za watumishi.

“Natambua kuwa mnatumia teknolojia ya kisasa na ujenzi wa nyumba zenu unachukua siku chache sana. Ninawaencourage mje Dodoma ambako kuanzia Machi mwakani, watumishi wengi wataanza kuhamia huko,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kumuonyesha ramani ya nyumba za watumishi ambazo wanazitumia.

Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina maeneo ambayo imeyatenga rasmi kwa ajili ya viwanja vya makazi na anaamini katika muda wa miezi miwili wanaweza kujenga nyumba za kutosha watumishi wanaotarajiwa kuhamia katika awamu ya pili.

“Nimeangalia michoro yenu, nyumba za vyumba vitatu vya kulala zina hadhi ya kukaa hata wakurugenzi; na watumishi wa kawaida wanaweza kumudu zile za vyumba viwili vya kulala… ninawatia moyo mwende haraka Dodoma na wale ambao wako serious wataleta maombi yao mara moja,” amesema.

Waziri Mkuu amesema amefarijika kuona kuwa size ya ramani zao inatosha kwenye kiwanja cha ukubwa wa mita za mraba 550 ambacho ni high density na watumishi wengi wanaweza kumudu kuvinunua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba nyumba ya ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala, yenye sebule, jiko, stoo na choo inatosha eneo la mita za mraba 94 tu.

“Kati ya vyumba hivyo vitatu, kimoja ni master, pia kuna sebule, chumba cha kulia na kibaraza. Hii inaanzia shilingi milioni 35 hadi milioni 41 kutegemea na aina ya vifaa unavyoweka kwenye umaliziaji. Lakini tukiongeza na servant quarter utalazimika kulipia shilingi milioni 7 ambapo unapata vyumba viwili na choo na bafu ndani,” amesema.

“Kimsingi, ni lazima tutaweka madirisha, milango, vyoo, masinki ya bafuni na jikoni, tiles (na mtu anaruhusiwa kuchagua za China, Italy au Spain),” ameongeza.

Akifafanua kuhusu nyumba yenye vyumba viwili vya kulala, Bw. Abdalla amesema nayo pia ina sebule, jiko, stoo na choo kimoja na inatosha eneo la mita za mraba 54. Amesema nyumba hizo zinaanzia sh. milioni 20 hadi 25 kutegemeana na aina ya vifaa vinavyowekwa kwenye umaliziaji.

Amesema ujenzi wa nyumba moja unachukua wiki sita na kama viwanja viko eneo moja au jirani, wanaokoa muda wa siku tatu hadi tano kwa kila nyumba. “Tunajenga ukuta kwa kumwaga theluji isiyochanganywa na kokoto ambayo ni mchanganyiko wa saruji, mchanga na kemikali. Inakauka baada ya saa saba na ukuta wetu ni imara mara nne zaidi ya ukuta uliojengwa na tofali la zege.”

Teknolojia yetu inawezesha ukuta wa nyumba nzima kukamilika ndani ya siku sita, nyumba zetu zinastahimili matetemeko, vimbunga na ujenzi wake unapunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nyumba hizo, Bw. Abdalla amesema wana mikataba na mabenki kwa hiyo wanaweza kujenga nyumba na kuziuza mara moja lakini pia wananchi wanaweza kuingia mikataba na mabenki na kulipia kidogo kidogo katika muda maalum (mortgage).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.
JUMATANO, OKTOBA 12, 2016  

MTENDAJI MKUU TEMESA AWAFUKUZA KAZI WAFANYAKAZI SITA NA KUWAPA ONYO WAWILI WA KIVUKO CHA MV KOME MWANZA.

$
0
0
Abiria wakiteremka katika Kivuko cha Mv Kome II kinachotoa huduma kati ya Nyakarilo na Kome wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Mwanza.Picha Zote na Theresia Mwami TEMESA Mwanza.
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Mussa Mgwatu (kushoto) akisikiliza taarifa ya kituo cha TEMESA Mkoa wa Mwanza kutoka kwa Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.

Na Theresia Mwami TEMESA Mwanza

Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo kuwafuta kazi mara moja watumishi sita wa kivuko cha Mv Kome kuanzia 11/10/2016 pamoja na kuwapa onyo kali watumishi wengine wawili wa kivuko hicho kwa kuondoka katika eneo la kazi bila ruhusa ya mkuu wao wa kazi.

Ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha TEMESA mkoani Mwanza na kutembelea kivuko cha Mv Kome kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Kome na Nyakarilo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Dkt Mussa Mgwatu pia amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo kuhakikisha wafanyakazi wa karakana na kivuko wanawajibika ipasavyo ili kuondoka na uzembe kama uliojitokeza.

“Hatuwezi kuvumilia uzembe namna hii watumishi wanaamua tu kuondoka eneo la kazi bila kupata ruhusa kutoka kwa wakuu wao hii sio sawa kabisa na nakuagiza Meneja hawa watumishi waache kazi mara moja” alisisitiza Dkt Mgwatu.

Aidha Dkt Mussa Mgwatu amemwagiza Meneja wa TEMESA Mwanza kuajiri watumishi wengine ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji wawatumishi watakao waajiri.

Kwa upande Meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo alikiri kuwa hakukuwa na ruhusa yoyote ya maandishi iliyotolewa kwa watumishi kutokuwepo kazini siku hiyo.

“Mtendaji sina barua yoyote kutoka kwa watumishi hawa iliyofika kwangu kuomba ruhusa ya kutokuwepo katika kituo cha kazi.” alisisitiza Mhandisi Mishamo.

Mhandisi Ferdinand Mishamo amewaja watumishi waliachishwa kazi kuwa ni walinzi wanne Bw. Apolinary Kapulula, Bw. Marwa Nchagwa , Bw. Msomi Stanley na Joseph Mtokambali, wengine ni Bw. Baharia Geofrey Biseko na Mkusanya Mapato wa kivuko hicho Bw. Elisha Mbondo.

Amewataja Watumishi wanaopewa onyo kali ni Mkuu wa Kivuko cha Mv Kome Bw.Elias Mabushi na dereva wa kivuko hicho Bw.Juma Bugingo.

Dr. Musa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.

MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA NA UONGOZI WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS NA KUFANYA MAZUNGUMZO NAE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Ujumbe wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi  uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana nae masuala mbali mbali yanayohusu changamoto za mtoto wa kike na mwanamke.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi Profesa Ruth Meena ambaye pamoja na ujumbe wake uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi  uliomtembelea Makamu wa Rais na kuzungumza nae Ikulu jijini Dar es Salaam na kujadiliana nae masuala mbali mbali yanayohusu changamoto zinazomkabili mtoto wa kike na mwanamke.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI ATOA TAARIFA YA MATEMBEZI YA HIYARI NA UCHANGIAJI DAMU

$
0
0
ku2
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed akitoa tarifa kwa wandishi wa habari kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi yatayofanyika tarehe 16/10/2016. 
ku3
Sehemu ya wandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alipokuwa akitoa tarifa kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar

SERIKALI YABARIKI MBIO ZA KILI MARATHON.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano ya mbio za  Kili Marathon  Oktoba 12  Jijini Dar  es Salaam.
jr1
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge  (katikati ) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuashiria uzinduzi wa mashindano ya mbio za Kili Marathon  Oktoba 12 Jijini Dar  es Salaam.
jr2
Afisa Masoko kutoka kampuni ya Gapco Tanzania  Bibi.Cariline Kakwezi akitoa maelezo kuhusu udhamini wao katika mashindano ya Kili Marathon wakati wa  uzinduzi wa mbio hizo  Oktoba 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
jr3
Kikundi cha ngoma kutoka Dar es Salaam  kikitoa burudani kwa wageni waalikwa na waandishi wa Habari ( hawapo pichani) katika uzinduzi wa mashindano ya mbio za  Kilimarathon  Oktoba 12, 2016 Jijini Dar  es Salaam.
PICHA zote na  Shamimu Nyaki WHUSM

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea soko kuu Mkoani Dodoma.

RAIS AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Suzan Alphonce Kolimba wakati alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
nz2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Suzan Alphonce Kolimba wakati alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]

TABATA KIMANGA JIJINI DAR ES SALAAM WAOMBA KUONDOLEWA TAKATAKA BARABARANI

$
0
0

 Mchuuzi wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
 Takataka zikiwa kando ya barabara.
Mwendesha bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.

"Takataka nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema Mfaume.

Aliongeza kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.

Aliongeza kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua zinaponyesha.

WANAZUONI KUCHAMBUA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Na May Simba-MAELEZO

Wanazuoni nchini wanatarajia kukutana na kuchambua miiko na maadili ya viongozi wa Umma tarehe 14, Octoba mwaka huu kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 8: 00 mchana, katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA), ili kuenzi siku ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam kuhusu kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Profesa Mwakalila amesema kuwa Chuo hicho kimeandaa Kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliamini kuwa kila nchi Duniani ina miiko yake na maadili inayowaongoza viongozi wa Umma.

“Chuo kimewaalika wanazuoni watano ambao ni Dkt Harun Kondo atakaye chambua Azimio la Arusha, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama na Mzee Joseph Butiku watachambua Miiko ya uongozi pamoja na Ibrahim Kaduma na Mhe Philip Mangula watakaojadili maadili ya viongozi,” alisema Prof. Mwakalila.

Mbali na hayo Prof. Mwakalila amesema kuwa Miiko ya uongozi na maadili ya viongozi wa Umma ilisisitizwa na Mwalimu mara baada ya Uhuru na baadaye kusisitizwa zaidi katika Azimio la Arusha la mwaka 1967.

Vile vile Mwalimu Nyerere katika hotuba zake alikuwa akiwaasa viongozi wa Umma kuwa na maadili na kufuata miiko ya Uongozi ili kuwa mfano bora kwa jamii inayowazunguka.

Kongamano hilo linafanyika ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Miiko ya uongozi na Azimio la Arusha”.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI

$
0
0
Muuguzi Mkuu wa Hospital ya wagonjwa wa akili Ruzuna Abdulrahim Mohammed akisoma risala ya wafanyakazi katika madhimisho ya siku ya Afya ya akili Duniani yaliyofanyika Hospitali ya Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.
Kaimu Daktari dhamana wa Hospital ya ugonjwa wa akili Dkt. Zena Kassim Moh’d akitoa taarifa fupi kwa Mgeni rasmi kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo na kumkaribisha mgeni rasmi DKT. Mohd Dahoma kwa niaba ya Katibu Mkuu katika madhimisho ya siku ya Afya ya akili Duniani.
Mgeni rasmin Mkurugenzi wa huduma za Hospitali Dkt. Muhammed Dahoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya akihutubia katika madhimisho ya siku ya Afya ya akili Duniani yaliyofanyika Hospitali ya Kidongo Chekundu Mjini Zanzibar.
Baadhi ya waalikwa na wagonjwa wa akili waliohudhuria madhimisho ya siku ya Afya ya akili Duniani wakimsikiliza mgeni rasmin Dkt. Muhammed Dahoma (hayupo pichani) kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Kaimu mratibu Afya ya akili Zanzibar Mohamed Joel Mihambo aitoa neno la shukari baada ya hotuba iliyotolewa na Dkt. Dahoma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

……………

Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili amesema janga la madawa ya kulevya linalowakabili vijana wengi nchini linapoteza nguvu kazi katika kujenga na kusukuma mbele maendeleo.

Dkt. Juma ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani yalyofanyika kitaifa Hospitali ya wagonjwa wa maradhi hayo Kidongo chekundu katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa huduma za Hospitali Dkt. Mohd Dahoma.

Amesema pamoja na kuwepo sababu nyengine za kupata matatizo ya akili kama vile urithi, matatizo ya kijamii, majanga ya kimaumbile mafuriko na maradhi bado madawa ya kulevya yanaongoza kwa kuathiri vijana wengi.

Katibu Mkuu amesema takwimu za wagonjwa wa akili waliosajiliwa na kupewa huduma za afya ya akili katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2006 Zanzibar ni 139,547 ambapo wagonjwa 9239 walilazwa.

Ameongeza kuwa pamoja na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na waingizaji na watumiaji wa dawa za kulevya bado dawa hizo zinaendelea kuingizwa nchini na kutumiwa na vijana wengi.

Amesema katika kukabiliana na dawa za kulevya, Serikali imeanzisha huduma za masafa ambapo madaktari wanakwenda maskulini kutoa taaluma ya athari ya madawa hayo na kuanzisha utaratibu wa wagonjwa kuishi na jamii.

Katibu Mkuu amewashukuru wananchi wanaojitokeza kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia wagonjwa wa akili kwa kuwapatia msaada wa chakula na dawa.

Hata hivyo ameeleza kuwa bado kunachangamoto katika kukabiliana na madawa ya kulevya nchini ikiwemo kutokuwa na chombo kimoja kinachohudumia afya ya akili kama ilivyopendekezwa kwenye sheria ya afya ya akili ya mwaka 2001.

“Bado kuna Idara tatu za Wizara ya Afya zinazoongoza huduma za afya ya akili, Hospitali ya Mnazimmoja inaongoza Hospitali ya Kidongo chekundu, Programa ya afya ya akili inaongozwa na Idara ya Kinga na madawa ya kulevya na Mental Health Pemba inaongozwa na Idara ya Kinga,”alisema Katibu Mkuu.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo ya mwaka 2001 Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu inatakiwa ijitegemee na kuwajibika kwa matibabu ya afya ya akili yenyewe.

Aidha ameeleza tatizo jengine ni kutoshirikishwa watu wa afya ya akili katika kutunga sheria na kwamba kunamgongano wa sheria ya afya ya akili ya mwaka 2001 na sheria ya Hospitali ya Mnazimmoja ya mwaka 2004 na ile ya 2016.

Katika risala ya wafanyakazi wa Hospitali ya wagonjwa wa akili iliyosomwa na Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Ruzuna Abdulrahim Muhammed wamesema wanakabiliwa na upungufu wa dawa wafanyakazi kwa baadhi ya sehemu.

IMETOLEWA NA MAELEZO/ZANZIBAR

DC Mjema atoa wiki tatu wananchi kupewa hati zao.

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na wakazi wa kata ya Msongola katika ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika wilaya hiyo.
 Mtendaji mkuu wa Kampunia ya upimaji na uuzaji Viwanja ya Tanzania Remex, Ali Hamadi, akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa kata ya Msongola ramaninya mipango miji katika eneo hilo .
Katibu tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola wakati wa ziara ya kutatua kero za wananchi katika maeneo yao . 

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesikiliza kero 126 za wananchi wakati wa ziara yake katika kata tatu za Vingunguti, Pugu, Gongolamboto na Msongola na kuipa wiki tatu kampuni ya Tanzania Remix kuwapatia wananchi hati zao za viwanja.

Mjema amesema kuwa wananchi hao wamesubiri kwa miaka mitatu sasa juu ya mpango huo bila kuona matumaini, hivyo hakuna haja ya kuendelea kusubiri.

"Sasa natoa wiki tatu kuhakikisha fidia za wenye viwanja zinapatikana na baada ya wiki mbili kila mmoja awe amepatiwa hati yake ambayo itamuwezesha kuuza au kukopa katika mabenki mbalimbali"amesema Dc Mjema.

Dc Mjema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ulinzi katika kata ya Msongola kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uporaji na mauaji.

TIMU YA GOLF YA JESHI YATAMBA KUREJEA NA USHINDI ARUSHA OPEN.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa klabu ya gofu  ya  Lugalo ya Jijini  Dar es Salaam Kanali Rajabu Mwenyumbu  akiangalia Mazoezi  ya mwisho ya timu ya  klabu hiyo  ambayo inatarajia  kushiriki  katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika   Mwishoni mwa Wiki Hii Jijini Arusha. 
 Naibu katibu mkuu wa Klabu ya gofu ya jeshi ya Lugalo  Kanali Rajabu Mwenyumbu  akizungumza na  wachezaji wa gofu wa  klabu hiyo ya jijini Dar es salaam wanao tarajiwa  kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika mwisho wa  Wiki hii Jijini Arusha.
Naibu katibu Mkuu wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu  akisalimiana na wachezaji wa gofu wa timu hiyo wanao tarajiwa  kushiriki katika mashindano ya wazi Jijini Arusha  mwisho wa  Wiki hii. 

PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)

WANANCHI WAPEWE ELIMU JUU YA MADHARA YA UCHAFU KIUCHUMI NA KIAFYA.

$
0
0
Mwakilishi Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Boniface Temba (katikati) akiwa katika kikao cha wadau wa maji kuhusu kuhusu kuhuisha mipango ya maji Mkoa, Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Abdalah Dihenda na kushoto kwake ni Mhandisi wa Maji kutoka Sekretariet ya Mkoa Emaeli Nkopi.
Kikao cha wadau wa maji Mkoa wa Singida kikiendelea mweye tai nyekundu ni Afisa Afya Mkoa wa Singida Habib akiwa na kushoto kwake ni mkurugenzi wa mpango wa Water Aid Tanzania Abel Dugange.
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao.
Wadau wa Maji Mkoa wa Singida wakiendelea na kikao.

………………………………………………………………………

Na Grace Singida.

Serikali na wadau mbalimbali wanatakiwa kuunganisha nguvu na kuzielekeza katika kuelimisha jamii juu ya athari za uchafu ili wahamasike na kuupinga kwa kujenga vyoo bora, kutumia maji safi na salama na kutumia huduma za usafi wa mazingira.

Ari hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mpango wa ‘Water Aid’ Tanzania Bw. Abel Dugange wakati wa kikao cha wadau wa maji wakati wa kuhuisha mipango ya sekta ya maji ya Mkoa wa Singida. Dugange amesema nguvu kubwa inatakiwa ielekezwe katika kutoa elimu kwa jamii ili wajenge vyoo bora na kuvitumia, watumie maji safi na salama ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafu.

Ameongeza kuwa serikali inapoteza fedha nyingi katika kuwatibu wananchi wanaogua magonjwa kama kipindupindu, kuhara pamoja na ukusanyaji na utekezaji wa uchafu huku wananchi pia hupoteza pesa kwa kujitibu huku wakipoteza muda wa kuzalisha mali kwenye matibabu.

Dugange amesema mpango wa ‘Water Aid’ kwa mwaka 2016 mpaka 2020 utalenga kuunganisha nguvu na kusaidiana na halmashauri katika kutekeleza mipango yao ya sekta ya maji na usafi wa mazingira ili kufikia malengo ya kitaifa katika sekta hiyo.

Amesema kwa tafiti za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa asilimia 58 ya watanzania hupata na kutumia maji safi na salama huku asilimia 18 tu hutumia huduma za usafi wa mazingira. Dugange amesema kwa upande wa upatikanaji na matumizi ya vyoo bora vya kwa Mkoa wa Singida mijini ni asilimia 31 wakati vijijini ni asilimia nane.

Katika majadiliano hayo wahandisi wa maji na maafisa mazingira wa halmashauri walitoa changamoto za sekta hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa hasa vya usafiri wa kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali.

Changamoto nyingine ni pamoja na visima vingi vya vijijini kuchimbwa maeneo ya mashamba ya wanakijiji ambapo hawalipwi fidia na kusababisha uharibifu wa vyanzo na visima vya maji hasa ukataji wa miti.

Kumekuwepo na wizi wa vifaa katika miradi ya maji hasa solar huku wanakijiji wakiomba kuwekewa umeme wakati utunzaji wa miradi hiyo wakishindwa kuchangia huduma hizo. Kwa pamoja wadau wamekubaliana kuunganisha nguvu katika kutatua kero za upatikanaji wa maji pamoja na kuboresha usafi wa mazingira.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images