Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1003 | 1004 | (Page 1005) | 1006 | 1007 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Maendeleo  ya  Afrika (AfDB), Ubalozi wa  Sweden na Shirika la Maendeleo  la  Umoja wa Mataifa (UNDP).
   

  Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano litakalokutanisha nchi mbalimbali za Afrika kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu katika masuala ya Nishati linalotarajiwa kufanyika Aprili mwaka 2017. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipofanya kikao na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichokutanisha wawakilishi kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Madini,  Benki ya Maendeleo  ya  Afrika (AfDB), Ubalozi wa  Sweden na Shirika la Maendeleo  la  Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa  Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
   Wawakilishi kutoka Benki ya Maendeleo  ya  Afrika (AfDB), Ubalozi wa  Sweden na Shirika la Maendeleo  la  Umoja wa Mataifa (UNDP), wakifuatilia maelezo  yaliyokuwa yanatolewa na  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
   Wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mkazi wa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (hayupo pichani) katika kikao hicho.

  Mkurugenzi Mkazi wa na Shirika la Maendeleo  la  Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akisisitiza  jambo katika kikao hicho.
   Mkurugenzi Mkazi wa  Shirika la Maendeleo  la  Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa makampuni ya Azam Bwana Said Salim Bakhresa ambapo alimueleza waziri mkuu nia yake yakuendelea kujenga viwanda zaidi vya kusindika matunda na chakula mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa waziri mkuu magogoni Dar es salaam leo Picha na Chris Mfinanga.

   
  KAMPUNI ya Bakhresa Foods imedhamiria kuongeza viwanda vingine vya usindikaji matunda hapa nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.

  Ahadi hiyo imetolewa leo (Jumanne, Oktoba 11, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Said S. Bakhersa wakati alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam. Bw. Bakhresa amesema wana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam ndipo wayauze.

  “Kuanzia tarehe 15 Oktoba, tutaanza kupokea matunda kutoka Kahama na maeneo ya jirani, na kwa siku tunapata semi trela zaidi ya 30. Yakimalizika ya kule tunaanza kupokea mengine kutoka mikoa ya Pwani na Kusini.” “Tukijenga kiwanda Kanda ya Ziwa, tutapunguza adha ya wadau kusafirisha matunda kutoka kule hadi hapa kiwandani na badala yake sisi tutakuwa tunasafirisha concentrated juice na kuileta hapa kwa hatua zaidi za usindikaji,” amesema.

  Amesema wana mpango wa kuendeleza usindikaji wa vyakula vya nafaka kwenye mikoa ya Kusini na kwamba hadi sasa wameajiri wafanyakazi zaidi ya 8,000 wakiwemo Watanzania 180 ambao wameajiriwa kwenye matawi yake nje ya nchi. “Hawa tunawalipa kama expatriates,” amesisitiza.

  Amesema hivi sasa Kampuni hiyo imekwishafungua matawi mengine kwenye nchi za Rwanda, Burundi, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini. Kampuni ya Bakhresa Foods inatengeneza vyakula mbalimbali zikiwemo juisi, soda, maji, biskuti, ice-cream, vyakula vya nafaka kama ngano, mahindi, mchele na bidhaa za kuokwa.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu amemhakikishia Bw. Bakhresa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano kushirikiana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kwani imedhamiria kukuza uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji wa viwandani.

  “Serikali inathamini mchango wa wenye viwanda katika nchi yetu. Tunawashukuru ninyi ambao ni wakongwe kwenye sekta hii, na kwa hiyo tunawaomba msikate tamaa, muendelee kufungua viwanda zaidi ili wananchi wetu wapate mahali pa kuuzia mazao au bidhaa zao,” amesema.

  Amemuomba Bw. Bakhresa aangalie maeneo mengine zaidi ya kuwekeza kama vile sekta za hoteli na utalii ili kusaidiana na Serikali kukuza uchumi wa Tanzania.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,

  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMANNE, OKTOBA 11, 2016

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  MAENDELEO ya Viwanda yanahitaji mali ghafi za kilimo hivyo Benki ya Maendeleo ya  Kilimo nchini (TADB) inawajibu ya kuwafikia wakulima ili matokeo ya viwanda yaweze kuonekana ikiwemo na kuwa na masharti ya riba nafuu au kuondolewa kabisa.

  Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Fedha , Uchumi na Mipango, Dk. Ashantu Kijjaji wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), amesema kuwa sekta ya kilimo inaajiri watanzania asilimia 70 huku ikichangia pato la Taifa kwa asilimia 28 ambayo ni kidogo kutokana na ukuaji wa sekta ambayo inatakiwa kwenda na viwanda ambapo TADB ndio yenye kuweza kuleta mapinduzi hayo viwanda kwa kuwafikia watanzania waliowengi.

  Amesema bodi ya wakurugenzi ya TADB inajukumu la kutekeleza na kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwafikia watanzania wengi katika maeneo ya kijijini kutokana ni kuwa wazalishaji wa mazao mbalilmbali ambayo ndio yanaweza kuzalisha viwanda na nchi ikaweza kukua kiuchumi pamoja na kuongeza pato la taifa.

  Dk. Ashantu amesema benki ya kilimo ihakikishe wanatafuta vyanzo vya fedha ili waweze kukuza mtaji na kutoa mikopo kwa wakulima kwa masharti nafuu katika kumfanya mkulima kuweza kunufaika kilimo chake.

  "TADB ina deni kubwa kwa wakulima sasa ni wakati umefika wa bodi kufanya kazi kwa uadilifu katika kuinua sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo na sio kwa bodi kufanya mikutano nje ya nchi na kuacha kutatua changamoto ya mikopo katika sekta hiyo" amesema Dk. Ashantu.

  Nae Mweenyekiti wa Bodi hiyo, Rosebudy Kurwijla ameiomba serikali kuiwezesha benki ili kuweza kufikia wananchi waliowengi na wanahitaji ya kukopeshwa na TADB katika kuendeleza kilimo.
  Amesema kilio cha TADB ni mtaji na bila kufanya hivyo itakuwa ni vigumu kuwafikia wananchi waliowengi.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas Samkyi amesema mpango wao ni kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika  katika kuweza kupata mtaji wa kuweza kuwakopesha wakulima ili kuweza kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.
   Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Ashantu Kijaji akizungumza wakati uzinduzi wa Bodi ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi wa TADB, Rosebudy Kurwijila akizungumza katika uzinduzi juu ya majukumu ya bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Ashantu Kijjaji akipokea mfano wa hundi ya Sh.milioni tano kwa ajili ya tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Fedha, Uchumi na Mpango, Dk.Ashantu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi wa TADB leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Zao aina ya Mirungi likiteketezwa kwa moto
   Wakazi wa Kijiji cha Kisesa Kata ya Vudee wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa shambala Mirungi
  Mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara akiwa ameshika mafuta ya taa tayari kwa ajili ya kuteketeza shamba lake la Mirungi.
   Shamba la Mirungi likiteketea baada ya agizo la Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki
   Dc Staki akiwasisitiza wananchi kutojihusisha na kilimo cha zao la Mirungi

  Na Mathias Canal, Kilimanjaro

  Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu Uongozi wa Wilaya ya Same ulitangaza vita dhidi ya wakulima wa Bangi, na Mirungi huku akitangaza kuwa kifungo cha miaka 30 kitawahusu wakulima wote wanaojishughulisha na kilimo hicho haramu kwani Bangi na Mirungi ni hatari kwa afya za watumiaji na kuisababishia serikali hasara kwa kutopokea Kodi.

  Kiama hicho kilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule wakati akikabidhiwa mradi wa Ruvu muungano uliojumuisha zahanati sita, Nyumba mbili za waganga, matanki saba ya kuvuna maji na madarasa 54, ofisi 16 za walimu, vyumba na vyoo vya chuo cha ufundi makanya uliofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.

  Dc Staki alisema kuwa kwa asilimia kubwa serikali imekuwa ikiwadhibu wanaoingiza Mirungi na Bangi sokoni huku ikiwasahau kuwachukulia hatua wale wote wanalima zao hilo.

  Hivi karibu katika kijiji cha kisesa kata ya Vudee Wilayani humo ilibainika kuwa kuna wakulima wa Mirungi ambao wanajihusisha na zao hilo kwa muda mrefu pasina serikali kuwabaini na kuwa sugu kwa kilimo hicho hatimaye kukiona kama kilimo cha halali.

  Dc Staki alipotangaza kiama cha kukabiliana na wale wote wanaojihusisha na kilimo hicho aliahidi kuwatafuta wakulima hao na hatimaye kuwachukulia hatua za kisheria na kuhakikisha kuwa Wilaya ya same inakuwa safi pasina kuwa na Mirungi.

  Hata hivyo katika ziara yake ya kazi Mhe Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alipozuru kijiji cha kisesa kata ya Vudee alifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mkulima wa zao la Mirungi Johnson Charles Kangara na hatimaye kumuelekeza kuwasha kiberiti yeye mwenyewe katika shamba zima na kuchoma zao hilo.

  Dc Staki ameahidi kuhakikisha Wilaya ya Same inasifika kwa kilimo cha mazao mengine rafiki katika jamii ya Biashara na chakula na kuteketeza mazao yote haramu.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Saccos Duniani, Stellah Mtayabarwa (kushoto), akimwelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), alipotembelea banda la Saccos la Mamlaka ya Bandari (PTA), katika ufunguzi wa maadhimisho hayo uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
   Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard Kalinga (katikati), akihutubia wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo, Stellah Mtayabarwa.
   Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Habibu Mhezi (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mrakibu wa Polisi (SP), Scholastica Luhamba.


   Mjasiriamali Zamda Sasillo (kushoto), akiwa na wateja walitembelea banda lake katika maadhimisho hayo. Kutoka kulia ni  Magdalena Samkumbi, Lubanzo Kalufya na Ashura Shoka.
   Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na Ofisa Uendeshaji Mkuu, Mfuko wa Pembejeo, Pili Mogasa.
   Ofisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akitoa maelezo kwa  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka (kulia), kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
   Ofisa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania, Ezekiel Fumbo (kushoto), akimuelekeza Dk. Turuka kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
   Viongozi Meza kuu wakipiga makofi wakati wakipokea maandamano ya maadhimisho hayo.
   Wadau wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
   Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikitoa burudani kwenye hafla hiyo.
   Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Sanaa cha Magereza kikionesha umahiri wa kucheza ngoma aina ya chaso inayochezwa na wenyeji kutoka Pemba.
  Hapa ni mserebuko wa ngoma ya chaso ya wenyeji wa Pemba.

  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na vyama vya akiba na mikopo ili kujenga mazingira bora ya kuinua uchumi nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka wakati wa ufunguzi wa Siku ya Saccos duniani uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

  "Vyama vya akiba na mikopo ni wadau wakubwa wa serikali kwani vinasaidia sana katika kiinua uchumi wa nchi hivyo hatuna budi kuendelea kushirikiana" alisema Dk.Turuka.Dk. Turuka aliwataka viongozi wa vyama hivyo kumaliza changamoto zao wao wenyewe na wanachama wao pale zinapotokea badala ya kukimbilia serikalini.

  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Benard Kalinga alisema vyama hivyo vimepata mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kuanzisha Saccos 4,000 ambazo zipo hadi vijijini na kuwa na wanachama milioni 1.5 nchini.

  "Sheria namba sita ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 imeanza kutumika baada ya kupata idhini ya Rais mwezi Oktoba 2013 lakini ni dhahiri kuwa kumekuwa na malalamiko mengi juu ya baadhi ya maeneo yaliyoko kwenye sheria hiyo" alisema Kalinga.


  Alisema licha ya kupata mafanikio hayo changamoto kubwa waliyonayo ni ushirikishwaji wa kuandaa sheria inayoongoza vyama vya ushirika nchini.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea michango yenye thamani ya sh. milioni 660.25 zikiwa ni fedha taslimu, hundi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, mwezi uliopita.

  Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Oktoba 11, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wa kampuni ya ACACIA, Bw. Deodatus Mwanyika amesema wao wametoa sh. milioni 325 ambazo tayari wameshaziingiza kwenye akaunti ya maafa.

  Amewaomba wadau wengine na taasisi nyingine hapa nchini wajitokeze kuisaidia Serikali kukabiliana na janga hili kwani mahitaji halisi ni makubwa kuliko kiasi ambacho kimekusanywa hadi sasa.

  Wadau wengine waliochangia ni Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaharu Yoshinda pamoja na Shirika la Misaada la Maendeleo la Japan (JICA) ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 220. Vifaa hivyo ni mahema 220, mablanketi 1,100; vigodoro vyepesi (sleeping pads) 1,110; madumu ya maji 250 na plastic sheets 22. 

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC1, Dk. Ayoub Rioba ambaye alikabidhi hundi za sh. milioni 41.55, amesema kama taasisi waliguswa na tatizo la maafa ya Kagera kwa hiyo wakatafuta njia ya kuchangisha ili wapate fedha za kuisaidia Serikali kukabiliana na tatizo hilo.

  “Tuliamua kufanya harambee na kuwahamasisha wananchi wachangie ambapo wengine walileta kwetu na wengine wakapeleka moja kwa moja Kagera. Na leo tunakabidhi kiasi ambacho tulikikusanya kupitia harambee hiyo,” amesema.

  Wengine waliokabidhi michango yao, ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenye Magereji Tegeta, Bw. Leonard Mwanjela ambaye ametoa fedha taslimu sh. milioni mbili kwa niaba ya mafundi gereji wilaya ya Kinondoni. Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Bw. Abdalla Mwinyi amesema walifanya harambee na kupata sh. milioni 60.8 ambazo wameamua kununua nguo na magodoro, unga wa mahindi tani 10.

  Wengine ni Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani (Internal Audit) ambao wamekabidhi sh. milioni 6.7. Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo, Bw. Richard Magongo amesema baada ya kuona hilo, waliamua kuchangishana na kupata kiasi hicho cha fedha.

  Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sura Technologies, Bw. Ramadhar Reddy amekabidhi hundi ya sh. milioni 5 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

  Akitoa shukrani kwa waliotoa michango hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru wote kwa misaada yao na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

  “Tunawashukuru sana kwa michango yote. Kutoa ni moyo na siyo utajiri. Nawaomba Watanzania wengine muendelee kujitokeza ili tuweze kuwasaidia wenzetu waliokumbwa na maafa haya,” amesema.

  Pia amewashukuru waandishi wa habari kwa kuwapa wananchi taarifa za matukio hayo na kuwahamasisha wachangie ndugu zao waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi.  Tetemeko hilo lilitokea, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa.

  Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMANNE, OKTOBA 11, 2016  

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa sita kushoto) akiongoza kikao cha pamoja cha Mawaziri kilichofanyika katika Hoteli ya Pullman, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wengine katika picha upande wa kulia ni Mabalozi wa Nchi wanachama wa SADC wanaowakilisha nchi zao DRC. 
  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiongoza ujumbe wa SADC katika kikao alichokifanya na Mhe. Raymond Tshibanda (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC ambaye aliongozana na viongozi wa juu wanaoratibu uchaguzi nchini DRC. 

  ========   =======   =========
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe Augustine Mahiga yupo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 13 Oktoba, 2016.

  Mhe. Mahiga ambaye anaongoza ujumbe wa Mawaziri wa Asasi hiyo yupo nchini humo kwa maagizo ya Mwenyekiti wa Asasi, Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kutathmini hali ya siasa ilivyo nchini humo ili kushauri ipasavyo.

  Aidha, tathmini hiyo inafanyika kufuatia hali tete ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama nchini DRC iliyochangiwa na maandamano yaliyofanyika tarehe 19 Septemba, 2016 ambayo yaliandaliwa na vyama vya upinzani kwa lengo la kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya DRC (CENI) kutangaza tarehe ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. 

  Awali misheni hii ilikuwa ifanye ziara kati ya tarehe 4 na 5 Oktoba, 2016, lakini kutokana na ziara ya Kitaifa ya Mhe Joseph Kabila, Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo hapa nchini ililazimu kuahirishwa. Aidha, kufuatia mazungumzo kati ya Mhe Rais John Pombe Joseph Magufuli, na Mhe Rais Jospeh Kabila wakati wa ziara hiyo walikubaliana Misheni hiyo ifanye ziara kwa tarehe hizo.

  Hadi sasa Misheni hiyo imeweza kukutana na wadau mbalimbali ambapo imewasisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye mjadala ikiwa ni njia pekee ya kuweza kuwakwamua hapo walipo pamoja na umuhimu wa uvumilivu wa kisiasa na hatimaye kufanyika kwa uchaguzi kwa kipindi watakachokuwa wamekubaliana pamoja.

  Wadau hao ni pamoja na Mabalozi wa Nchi SADC walioko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; Mhe. Eden Kodjo, Msuluhishi Mkuu wa Umoja wa Afrika; Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo; Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Wadau wengine ni Muungano wa vyama vilivyosusia kushiriki katika mjadala shirikishi wa kitaifa ( Rassamblement); Muungano wa vyama vinavyounda Serikali (Presidential Majority); Asasi zisizo za kiserikali zinazoshiriki katika mjadala shirikishi wa kiitaifa; Asasi zisizoshiriki katika mjadala shirikishi wa kitaifa na Taaisi za kidini.

  Itakumbukwa kuwa, Mkutano wa 36 wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika uliofanyika Mbabane, Swaziland mwezi Agosti 2016 ulimteua Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama. Nchi zingine zinazounda Asasi hii ni Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti anayeondoka).


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 11 Oktoba, 2016.

  0 0

  Serikali haitavumilia watu au taasisi yoyote watakaobainika kuhusika na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja nchini kwa kuwa vitendo hivyo ni kosa la jinai  na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, kikundi au taasisi itakayobainika kufanya uhamasishaji, kuficha na kuendesha vitendo hivyo nchini
  .
  Waziri wa Mambo  ya Katiba na Sheria amesema hayo mjini Dar es salaam leo alipokutana na waandishi wa habari kuelezea kauli iliyotolewa na Serikali ya Marekani kuwa Tanzania inakiuka haki za binadamu kwa kutowatambua na kuwabagua katika kuwapatia huduma za afya wale walioathirika na ukimwi, kifua kikuu na vvu watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja nchini. 

  Amesema Tanzania haina na haijawahi kuwa na Sheria, Sera, kanuni au muongozo ambao unalenga kuwabagua waathirika wa ukimwi, vvu na kifua kikuu na kuongeza kuwa waathirika wote wanapata huduma zote stahili  bila ya kuulizwa au kujali kuwa wamepatajepataje maambukizi ya maradhi hayo kama ambavyo sera ya Afya inavyosema .Amesema Serikali ya Awamu ya Tano haiko tayari kuendeshwa huku ikiangalia sheria za nchi zikivunjwa kupitia vitendo visivyo vya kimaadili na hatimaye kuiletea nchi madhara makubwa kwa wakati huu na kwa baadae.

  "Serikali hii haiko tayari kuendeshwa endeshwa bila ya kuwa na principles na mambo ya kihovyo kama hayo hayawezi kuachwa yakiendelea , hayatavumiliwa au kufumbiwa macho kwa migongo ya kupata misaada ya kifedha kutoka kwa nchi zilizoendelea au mashirikia makubwa ya Kimataifa namna hiyo "

  Amesema Serikali haitalala na itaionyesha dunia kuwa nchi hii kuna utawala wa sheria na hakuna mambo ya hovyo yatakayoachwa yafanyike kila wanavyotaka kupitia miamvuli ya kutoa misaada kwa nchi hii hasa kisingizio cha kupambana na virusi vya ukimwi, na  Ukimwi.

  Amesema Serikali inayo uishahidi kuwa kuna Asasi 15 nchini yenye uhusiano na nchi zilizoendelea  ambayo yanajihusisha na uhamasishaji wa vitendo vya ndoa za jinsia moja kwa mwamvuli wa kusaidia harakati dhidi ya magonjwa ya kifua kikuu, ukimwi na vvu.

  Amesema serikali imefuatilia kwa undani suala hilo na kugundua kuwa asasi hizo zimejikita na kuendesha uhamasihaji katika mikoa 11 nchini ambayo ameitaja kuwa ni Dar es salaam, Arusha, Shinyanga, Mbeya, Iringa, Tabora, Dodoma, Kilimanjaro, Njombe, Lindi na Morogoro.Amesema ushahidi uliopo unaonyesha kuwa asasi hizo zimekuwa zikifanya mikutano  ya siri na sherehe  usiku, kuandaaa na kuchapisha machapisho yanayohamasisha vitendo hivyo , kusambaza vilainishi na kondom na kupeleka elimu ya ushoga katika shule za msingi na sekondari nchini.

  Amesema hayo yote yamekuwa yakifanyika kupitia mwamvuli wa kutoa misaada ya kusaida waathirika wa Ukimwi na VVU wkati wakijua kuwa hayo wanayoyafanya yana ajenda nyingine ambayo haitoa afua kwa magonjwa hayo kama wanavyosema.Amesema kuwa serikali imegundua kuwa Tanzania imepangwa kuwa kitovu cha vitendo hivyo katika ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

  Amesema kutokana na mpango huo Serikali iko tayari kukosa hiyo misaada ili kuifanya Tanzania kuwa nchi salama kwa sasa na kwa kizazi kijacho huku ikizingatia mila, tamaduni, desturi na imani za kidini kama ilivyokuwa tangu zama na zama.Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe amemtaka Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome kukutana na Makatibu wakuu wenzake kutoka Wizara za Afya, Mambo ya Ndani na Viwanda na Biashara ili kutafakari ni wapi kama nchini ilikosea hadi kujikuta katika hali na kuangalia cha kufaanya ili kujikwamua katika hali hii na kuchukua hatua kali za ksiheria kwa taasisi ambazo zinajihusisha na uhamsishaji wa vitendo hivyo nchini.


  0 0

  NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Dar es Salaam.

  Serikali imeunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka wizara sita zinazoshukulika na masuala ya ardhi ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika kutatua changamoto mbali mbali za ardhi ikiwemo maeneo ya Hifadhi.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaamu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani alisema kuwa lengo la kuhusisha Wizara hizo ni kufanya uchunguzi wa kina na wa kisheria kuhusu namna bora na endelevu ya kumaliza changamoto katika sekta ya ardhi.

  “Serikali imeamua kuunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka Wizara ya Ardhi ikiwa ni wadau wakuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo kwa madhumuni mapana ya kufanya uchunguzi wa kina na kupitia sheria zote endelevu za kumaliza changamoto za ardhi inayohusisha maeneo ya hifadhi” alifafanua Mhandisi Kamani

  Mhandisi Makani alisema kuwa kikosi hicho kimeanza kufanya kazi ya kusoma taarifa mbalimbali za baadhi ya maeneo yenye changamoto za ardhi na hivi karibuni kinatarajia kutembelea maeneo hayo ili kujua chanzo cha matatizo na jinsi ya kushughulikia changamoto hizo.

  Aidha, katika hatua hiyo ya Serikali ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu na endelevu wa changamoto za ardhi, Mhandisi Makani amewataka viongozi na watumishi wanaohusika na zoezi hilo kuzingatia taratibu katika kutekeleza sheria kwa wananchi walioko katika vitongoji na vijiji vilivyosajiliwa.

  Vilevile Mhandisi Makani amewataka wananchi walioko katika maeneo hayo kutoanzisha shughuli mpya za kibinadamu na kutoendelea na shughuli za kibinadamu zinazosababisha uharibifu wa mazingira na kuathiri tabia nchi.

  Wakati huohuo Mhandisi Kamani amewataka wafugaji kuondoa haraka mifugo iliyoko ndani ya maeneo yaliyoifadhiwa kisheria kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

  Mbali na hayo Serikali imewataka wananchi kutii sheria na kuepuka vitendo viovu vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili kwa kasi inayoendelea nchini na kutishia uhifadhi endelevu.

  0 0

  Katika kusheherekea siku ya mtoto wa kike kimataifa, ninawaletea kisa kifupi chenye mafunzo muhimu kwa wasichana wote duniani, kisa hichi ni cha MAYA.
  Maya ni binti wa miaka 12 aishie na wadogo zake wawili wa kiume katika familia maskini. “Ndoto” yake ni kuwa mwalimu ili kuisaidia jamii yake. Umasikini wa familia yake wamfanya Maya kukaa nyumbani na wadogo zake kwenda shule. Ndoto yake imevunjika. Maya hana elimu wala ajira (takwimu zaonyesha 1/3 ya wanawake Tanzania hawajasoma).
  Maya anajihatarisha kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI (huku asilimia 40 tu ya wasichana umri kati ya 15-19 wakiwa na elimu juu ya ugonjwa huu) au mimba ya utotoni kwa kujiuza ilia apate chakula, hifadhi na ulinzi. Anapata uja uzito akiwa na miaka 16 (huku ¼ ya wasichana kuaniza umri wa miaka 15 ni wazazi watoto). Anajifungua kwa matatizo mtoto Maryam ambapo anaamua kubadili msimamo wa maisha yake.
  Maya anajihusisha na kazi za kuajiriwa na biashara ndogo, anafanikiwa kufungua mgahawa. Sasa anaweza kumpeleka Maryam shule. 
  Maryam anasoma kwa bidii na kupata udhamini wa kwenda chuo ambapo anafanikiwa kuhitimu kama Mwalimu. Mustakabali wake sasa uko mikononi mwake tofauti na ule wa Maya, na sasa Maryam anaweza kusaidia jamii yake, ndoto ambayo alikuwa nayo mama yake.
  Kumbuka: Ukimuelimisha mwanaume unamueleimisha mtu mmoja, ukimuelimisha mwanamke basi unalielimisha Taifa!
  Tazama video hii fupi hapa chini upate kuelimika.

  0 0


   Mkuu wa Wilayaya Same, mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemare Staki Senyamule, (kulia), akimkaribisha ofisini kwake, Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele Oktoba 10, 2016


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SAME
  MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Staki Semanyule, (pichani), amesema wilaya yake inazo fursa za kutosha hususan kilimo cha Tangawizi na kuukaribisha Mfuko wa Pensheni wa PPF kujenga kiwanda cha kuchakata Tangawizi, ili kuongeza thamani ya zao hilo.Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo katika mazungumzo mafupi na MenejaUhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Lulu Mengele, aliyemtembelea ofisini kwake Oktoba 10, 2016.
  “Same tunalima Tangawizi kwa wingi, wakulima hawapati faida ya kutosha kwa vile wanauza mara tu wanapovuna, tunahitaji viwanda vya kuchakata Tangawizi ili iwe katika mfumo wa unga (powder) na itakuwa rahisi kusafirisha nje na kuuza kwa bei ya juu zaidi na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima wetu.” Alisema Bi Staki.Bi. Staki pia alisema, ukiacha wananchikujishughulisha na zao hilo, pia Same wanalima mazao ya chakula kwa wingi.
  Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, alisema, PPF inaendelea na kampeni yake ya kuongeza wanachama hususan kupitia mpango wa “Wote Scheme” unamuwezesha Mfanyakazi wa sekta rasmi na isiyo rasmi, (wajasiruimali) kujiunga nao.
  “ Wote Scheme, ni mpango utakaowafaa sana wajasiriamali, ambao ni wakulima, waendesha bodaboda, mama lishe na baba lishe.” Alisema Bi Mengele.Akifafanua zaidi, Bi.Mengele alisema, Mwanachamaaliyejiunga na mpango huo, atafaidika na Mafao mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata Bima ya Afya.
   Bi. Staki akimsikiliza Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele
  Meneja Uhusiano wa PPF, Bu.Lulu Mengele, (kushoto), akimueleza Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Bi. Rosemary Staki Semanyule, shughuli mbalimbali zifanywazo na PPF hususanMpango wa Wote Scheme.

  0 0


  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea msaada wa mablanketi kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa Shirika la JICA nchini Toshio Nagase.

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 6.7m kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Taasisi ya wakaguzi wa ndani wa Serikali na kampuni Binafsi Bw.Richard Magongo leo Jijini Dar es Salaam ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea pesa taslimu shilingi milioni 2 kutoka kwa Mwenyekiti wa Magereji Tegeta Bw.Lenard Mwanjela ukiwa ni msaada kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 325 kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 41.5 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bw.Ayoub Ryoba ikiwa ni kutokana na harambee iliyofanywa na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

  Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea moja ya misaada kutoka kwa Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa kariakoo Bw.Abdallah Mwinyi ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya milioni 60 ikiwa ni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

  Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

  …………………………………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea michango yenye thamani ya sh. milioni 660.25 zikiwa ni fedha taslimu, hundi na vifaa mbalimbali kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, mwezi uliopita.

  Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Oktoba 11, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wa kampuni ya ACACIA, Bw. Deodatus Mwanyika amesema wao wametoa sh. milioni 325 ambazo tayari wameshaziingiza kwenye akaunti ya maafa.

  Amewaomba wadau wengine na taasisi nyingine hapa nchini wajitokeze kuisaidia Serikali kukabiliana na janga hili kwani mahitaji halisi ni makubwa kuliko kiasi ambacho kimekusanywa hadi sasa.

  Wadau wengine waliochangia ni Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaharu Yoshinda pamoja na Shirika la Misaada la Maendeleo la Japan (JICA) ambao wametoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 220. Vifaa hivyo ni mahema 220, mablanketi 1,100; vigodoro vyepesi (sleeping pads) 1,110; madumu ya maji 250 na plastic sheets 22.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBC1, Dk. Ayoub Rioba ambaye alikabidhi hundi za sh. milioni 41.55, amesema kama taasisi waliguswa na tatizo la maafa ya Kagera kwa hiyo wakatafuta njia ya kuchangisha ili wapate fedha za kuisaidia Serikali kukabiliana na tatizo hilo.

  “Tuliamua kufanya harambee na kuwahamasisha wananchi wachangie ambapo wengine walileta kwetu na wengine wakapeleka moja kwa moja Kagera. Na leo tunakabidhi kiasi ambacho tulikikusanya kupitia harambee hiyo,” amesema.

  Wengine waliokabidhi michango yao, ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenye Magereji Tegeta, Bw. Leonard Mwanjela ambaye ametoa fedha taslimu sh. milioni mbili kwa niaba ya mafundi gereji wilaya ya Kinondoni. Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Bw. Abdalla Mwinyi amesema walifanya harambee na kupata sh. milioni 60.8 ambazo wameamua kununua nguo na magodoro, unga wa mahindi tani 10.

  Wengine ni Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani (Internal Audit) ambao wamekabidhi sh. milioni 6.7. Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo, Bw. Richard Magongo amesema baada ya kuona hilo, waliamua kuchangishana na kupata kiasi hicho cha fedha.

  Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sura Technologies, Bw. Ramadhar Reddy amekabidhi hundi ya sh. milioni 5 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

  Akitoa shukrani kwa waliotoa michango hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru wote kwa misaada yao na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

  “Tunawashukuru sana kwa michango yote. Kutoa ni moyo na siyo utajiri. Nawaomba Watanzania wengine muendelee kujitokeza ili tuweze kuwasaidia wenzetu waliokumbwa na maafa haya,” amesema.

  Pia amewashukuru waandishi wa habari kwa kuwapa wananchi taarifa za matukio hayo na kuwahamasisha wachangie ndugu zao waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Tetemeko hilo lilitokea, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa.

  Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

  Benny Mwaipaja, MoFP, Washington DC, Marekani
  SERIKALI ya Japan, kupitia Shirika lake la Maendeleo-JICA, imeahidi kuongeza kiwango cha ruzuku kwa serikali ya Tanzania ili kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo kilimo, Maji, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za jamii ili kuisaidia kufikia maendeleo yaliyokusudiwa kwa wananchi wake.

  Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Jijini Washington DC, nchini Marekani.

  “Kabla ya mwaka 2013 tulikuwa tunatoa ruzuku ya dola milioni 1 kwa Tanzania kila mwaka, lakini kuanzia mwaka 2013 tumeongeza kiwango hadi kufikia dola milioni mia 3 kila mwaka na tunatarajia kuongeza kiwango hicho siku za hivi karibuni” aliongeza Makamu huyo wa Rais wa JICA
  Kato amesema kuwa Tanzania na Japan ni marafiki wa muda mrefu na kwamba nchi hiyo itaendelea kuisaidia kwa kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta tija kwa uchumi wa nchi na maisha ya watanzania kwa ujumla.

  “Hivi sasa tunataka kuanza kutekeleza awamu nyingine ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha zao la mpunga ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ni muhimu sana” Aliongeza Kato.

  Amesema kuwa Japan pia imeamua kuongeza kiwango cha ufadhili kwa Bara la Afrila kutoka Dola Milioni 13 ambazo nchi hiyo ilikuwa ikitoa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2013 hadi kufikia dola elfu 30 kwa mwaka kuanzia mwezi Agosti, 2016 kwa kipindi cha miaka 3 ijayo.

  Amesema pia kuwa ili kuwajengea uwezo na ujuzi vijana wa kiafrika, Japan imeanzisha program ya kutoa elimu ambapo hivi sasa vijana 60 kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wamepelekwa nchini humo kujifunza kwenye vyuo vilivyoko huko na watapelekwa kwenye kampuni na mashamba makubwa yanayojihusisha na kilimo ili waweze kupata uzoefu na kuwa chachu ya mabadiliko watakaporejea katika nchi zao.

  Akiongea na Makamu huyo wa Rais wa Shirila la Maendleo la Japan-JICA, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Japan kwa kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  Ametaja baadhi ya miradi ambayo nchi hiyo inafadhili nchini Tanzania kuwa ni ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Holili hadi Taveta nchini Kenya, Ujenzi wa barabara ya Juu (Flyover) ulioanza eneo la Tazara ili kupunguza msongamano Jijini Dar es salaam, miradi ya maji na kilimo cha umwagiliaji.

  “Asilimia 75 ya wananchi wetu wanategemea kilimo kwahiyo uamuzi wa Japan wa kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya kilimo cha umwagiliaji ni jambo tunalolipongeza kwasababu kilimo kitakuwa na tija na kitaendeshwa kibiashara” Alisema Dkt. Mpango.

  Ameishukuru pia serikali ya Japan kwa kufanya utafiti na upembuzi yakinifu wa mradi wa kudhibiti mafuriko ya mto Kondoa, eneo la mkoa wa Morogoro ili kudhibiti mto huo usiharibu miundombinu ya reli ya kati.

  “Mradi huu ni muhimu sana kwasababu serikali imekuwa ikiingia hasara karibu kila mwaka kukarabati njia hiyo ya reli baada ya kusombwa na maji, hivyo tunaishukuru Japan kwa kutusaidia kufanya utafiti huo ambao utasaidia kukabiliana na hali hiyo” aliongeza Dkt. Mpango
  Ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kukusanya kodi na kuziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali ikiwemo kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulika na mafisadi ili kuleta nidhamu katika utumishi wa umma.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibari  (ZMA) Abdallah Hussein Kombo akizungumza na  waandishi wa Habari  kukanusha tuhuma za kusajili Meli za Korea ya Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza  la Usalama la Umoja wa Mataifa.
   Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini  Abdallah Hussein Kombo wakati alipokutana nao Ofisini kwake Malindi .
   Mwandishi wa Idara ya  Habari  Maelezo  Zanzibar Ramadhan Ali akimuliza suala Mkurugenzi Mkuu  (ZMA) hayupo pichani.
  Katibu Mkuu wa  Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe  akitowa ufafanuzi  wa masuala yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari katika Mkutano huo. (Picha na Miza Othman Habari Maelezo Zanzibar).


  Na Ramadhan Ali/Maelezo Zanzibar          11.10.2016

  Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA) imekanusha tuhuma zinazotolewa kuwa imesajili meli za Korea Kaskazini kinyume na Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Machi mwaka huu za kuzikatalia usajili Kampuni za meli za nchi hiyo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurgenzi Mkuu wa ZMA Abdalla Hussein Kombo amesema tuhuma hizo zilizotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uchambuzi wa Taasisi ya NK News kupitia Jarida la NK Pro la Mjini Seoul, Korea Kusini sio za kweli.

  Amesema ZMA baada ya kupata taarifa ya Azimio hilo iliunda Kamati ya wataalamu kulifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo kwa Mamlaka juu ya hatua za kuchukuliwa."Azimio hilo limetaja majina ya meli 31 za Korea Kaskazini ambazo nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, ikiwemo Tanzania, inazitaka kuzifutia usajili au kutozisajili," alisema Mkurugenzi Mkuu ZMA.

  Aliongeza kuwa ZMA ilifanya uhakiki wa meli zote zilizosajiliwa na Mamlaka hiyo na orodha ya meli zilizoainishwa kupitia Azimio hilo na kubaini kuwa meli moja yenye jina la First Cleam ilikuwa imesajiliwa kabla ya vikwazo vya usajili wa meli za Korea Kaskazini lakini ikaamua kuifutia usajili.

  Amesema kuanzia wakati huo, Mamlaka haijawahi kusajili meli yeyote ambayo ilikuwemo katika orodha iliyotolewa na Umoja wa Mataifa na imekuwa ikichukua tahadhari kubwa katika usajili wa meli.

  Mkurugenzi Mkuu wa ZMA alisisitiza kuwa ili kuhakikisha hawatoi usajili kwa meli zenye uhusiano na Korea Kaskazini imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Taasisi za Kimataifa ikiwemo IMO.

  Hata hivyo amekiri kuwa Kampuni ya Filtex ambayo ilikuwa wakala wa ZMA nchini Dubai na kuvunja naye mkataba bado inaendelea kusajili meli kwa jina la Zanzibar  kinyume na sheria.

  Amesema  tayari wameshawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali  kuifuatilia Kampuni hiyo na kuifungulia mashtaka kwenye mahakama za Kimataifa.Amesema katika kukabiliana na uharamia unaofanywa na Kampuni ya Filtex, miezi michache ijayo, ZMA itafungua Ofisi yake nchi Dubai kwa ajili ya usajili wake wa meli wa Kimataifa.

  Kufuatia majaribio ya Korea Kaskazini kutengeneza silaha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha 7638 kilichofanyika tarehe 2 Machi, 2016 ilipitisha Azimio la kuiongezea vikwazo Korea Kaskazini ikiwemo kuzinyima usajili meli zote za nchi hiyo ama zenye uhusiano nazo.

  0 0

  Mwashungi Tahir na Fatma Makame/Maelezo Zanzibar

  Waziri wan chi ofisi ya makamo wa pili ya rais Mohammed Aboud Mohammed amesema uchumi wa Zanzibar     unazidi kuimarika kwa karibu ya asilimia saba na mfumuko wa bei bado upo kwenye tarakimu  moja na  pato la Taifa linazidi kukua.

  Ametoa maelezo hayo  ofisini kwake Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi Serikali ya awamu ya saba kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein.

  Amesema katika awamu hii kwa ujumla harakati za uchumi zinaendelea vizuri na ishara zote za kuimarisha uchumi katika mwaka huu wa fedha zinatoa sura nzuri za mafanikio.

  Akizungumzia  suala la Muungano amesema unaendelea kuimarika na  vikao mbali mbali vya watendaji wakuu wa pande mbili wakiwemo  mawaziri vimeshafanyika na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ameshafanya vikao viwili vya kisekta kwa nia ya kutatua changamoto zilizopo.

  Waziri Aboud ameelezea kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekamilisha kazi ya kuipandisha hadhi iliyokuwa Idara ya upigaji chapa na mpigaji chapa mkuu wa serikali na kuwa wakala wa serikali wa uchapaji.

  Aidha amesema kazi ya kufunga mitambo mipya ya uchapaji imekamilika na mafundi wa kiwanda hicho wanaendelea kupatiwa mafunzo ili kuimudu teknolojia mpya ya mitambo hiyo ili kuongeza ufanisi  na kuongeza upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati.

  Sambamba na hayo Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kupitia Tume ya kitaifa ya kuratibu na udhibiti madawa ya kulevya imepania kutoa athari za madawa ya kulevya kwa jamii.

  Hivyo Tume hiyo imefanya kikao maalum na maofisa na wapelelezi wa Jeshi la Polisi wa Mikoa na Wilaya  za Unguja kilichoongozwa na mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi kuweka mikakati dhidi ya uingizaji na usambazaji wa madawa ya kulevya .

  Mh Aboud amesema ofisi yake inashirikiana na Ofisi ya ukaguzi na mdhibiti mkuu wa Serikali kuendesha zoezi la uhakiki wa wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo ya Pili ya Rais na Taasisi zake ili kubaini wafanyakazi hewa.

  “Katika zoezi hili imebainika kwamba Ofisi yetu hakuna wafanyakazi hewa  kama inavyobainika sehemu nyengine" alisema wazirihuyo.

  Aidha amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais bado itaendelea kufanya kazi kwa bidii , ufanisi na tija ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Amesisitiza kuwa mambo muhimu ya kuzingatiwa hivi sa kwa nchi yetu ni kuimarisha uzalendo na kusimamia matumizi bora ya ardhi kwani watukishirikiano katika masulala hayo tutaweza kudumisha amani na upendo na kupiga hatua zaidi ya maendeleo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa tarifa ya mafanikio ya Ofisi yake kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
   Wandishi wa habari wakifuatilia tarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa na mazungumzo nao  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akijibu maswali ya wandishi wa habari katika Mkutano wake Ofisini kwake Vuga.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutbia kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa wodi tatu za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es salaam leo Octoba 11,2016.

  Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Wananyamala, Amana-Ilala na Temeke, wodi za kisasa zitakuwa vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akisoma maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na kulia ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya Amsons Group Bw. Suleiman K.Amour.

  Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Wananyamala, Amana-Ilala na Temeke, wodi za kisasa zitakuwa vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye hafla ya Uwekaji mawe ya msingi ujenzi wa wodi za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam leo Oktoba 11, 2016. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye hafla ya Uwekaji mawe ya msingi ujenzi wa wodi za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya Uwekaji mawe ya msingi ujenzi wa wodi za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam. Pembeni wanaoshuhudia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Makonda.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelekezo na wadhamini watakaojenga jengo hilo, Amsons Group.
  Moja ya Bango la ujenzi wa wodi ya wazazi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi.
  Wageni waalikwa.
  Mganga mkuu wa hospitali ya Temeke akisoma Risala.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza machache.
  Meya wa Jiji, Isaya Mwita akitoa shukrani. Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Andrea Kigwangalla akitoa neno.
  Mama Samia Suluhu akikata utepe, hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Amsons Group, Bw. Abdallah Nahad.
  Picha ya Pamoja.

  0 0

  SEHEMU ya tatu ya Wanafunzi 220 waliochaguliwa kusoma kwa Scholarship nje ya Nchi chini ya udhamini wa Universities Abroad wameondoka kwenda Nchini China na Uingereza.

  Wanafunzi hao 35 wengi wao wakiwa kwenye fani ya Udaktari, Uhandisi na Biashara za Kimataifa watalipa ada ya mwaka mmoja tu wa kozi na wengine wakigharamia asilimia 50 ya gharama zote.

  Taasisi ya UAL inaendelea na udahili kwa wanafunzi watakaokwenda Novemba na Februari 2017 katika ofisi zao zilizopo Posta Mpya jengo la Benjamini Mkapa Tower na Ofisi ya Kanda- Mwanza, Kenyatta Road na Exim Bank Ghorofa ya pili.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaaga wanafunzi 220 waliopata udhamini wa masomo kutoka Universities Abroad Link. (Picha na Francis Dande).
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), akizungumza na Esnath Mwaka (kushoto), ambaye ni mmoja wa wanafunzi 220 waliopata udhamini wa Universities Abroad Link kwenda kusomea masomo ya Uchumi na Biashara za Kimataifa nchini China. Hafla ya kuwaaga ilifanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni David Mwaka.
  Baadhi ya wanafunzi wanaokwenda katika masomo nchini UK na China wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Universities Abroad Link muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kuelekea China na Uingereza katika masomo yao.
  Wanafunzi waliopata ufadhili wa Universities Abroad Link wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, walezi wao wakati wa kuwaaga Uwanja wa Ndege.
  Picha ya pamoja.
  Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mwakilishi wa wanafunzi wanaokwenda China na Uingereza akitoa neno la shukrani muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kuelekea China na UK.

  0 0


  0 0

  Meneja masoko wa Benki ya CRDB Fredrick Siwale akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja mjini Babati Mkoani Manyara, katikati ni Mkurugenzi wa mji huo Fortunatus Fwema na Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul.
  Meneja wa utawala wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Domitila Bugomola, akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.

  ………………………………………………

  Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, imefanikiwa kutoa mikopo ya sh16.1 bilioni kwa wajasiriamali, watumishi wa Serikali, watumishi wa sekta binafsi, vyama vya kuweka na kukopa na asasi za fedha.

  Watumishi wa serikali na wasekta binafsi 1,604 walikopeshwa sh12.8 bilioni na wajasiriamali 84 walikopa sh3.3 bilioni ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara na wakulima.Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Babati, Ronald Paul akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, alisema wamedhamiria kuwapa wateja wao huduma bora na kuwanyanyua kiuchumi.

  Paul alisema kwa muda wa miaka miwili tangu waanzishe huduma ya benki hiyo mkoani Manyara, wamefanikiwa kufungua matawi mengine madogo wilaya za Mbulu, Hanang, Simanjiro na Kiteto.Alisema pia wamefanikiwa kufungua huduma za matawi madogo yaliyopo Magugu, Haydom na Mirerani ambayo kupitia hayo wameweza kupata akaunti za halmashauri za wilaya.

  Alisema kwenye matawi yao madogo wamefanikiwa kuwa na huduma za ATM ambazo wamefungua 10 kwenye mkoa huo na zinafanya kazi kwa muda wa saa 24.“Kwa kipindi hiki tumefanikiwa kuongeza ajira kwa watanzania hususani kwa wana Manyara kutoka wafanyakazi 12 hadi 37 kutokana na matawi mengine madogo yaliyofunguliwa katika wilaya mbalimbali,” alisema.

  Alisema wamefanikiwa kupata amana za sh11 bilioni zilizotokana na wateja 12,000 waliofungua akaunti za akiba, watoto jumbo, akaunti za malkia, akaunti maalum, bidhaa nyingi za kibenki za Simbanking, ATM na fahari huduma.Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alitoa wito kwa benki hiyo kuwatafutia wateja wa mbaazi wa nje ya nchi kwani hivi sasa wakulima wengi wanapata changamoto ya soko la zao hilo.

  Fwema alisema kutokana na benki hiyo kutoa huduma za fedha hadi nje ya nchi hasa nchini India, wangetumia fursa hiyo kwa kuwaunganisha wakulima hao moja kwa moja na soko la mbaazi ambalo wanunuzi wengi hutoka nchini India.

older | 1 | .... | 1003 | 1004 | (Page 1005) | 1006 | 1007 | .... | 1897 | newer