Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

RAIS wa zanzibar dkt SHEIN AZINDUA MRADI WA ONE WORLD FOOTBAL

$
0
0


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",mradi ambao utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali mbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


 Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti unaosisitiza kulindwa haki zao,wakipita kwa maandamano mbele ya Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za  uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studiuam,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar





 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh Mohamed,wa Skuli ya Mwembeshauri Mjini Unguja,kitabu  chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii kushirikiana katika kuwapatia haki zao za Msingi bila unyanyasaji. katika uzinduzi wa Mradi wa  "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",katika uwanja wa Amaan Studium ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA" ,katika   Uwanja wa Amaan Studium, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[

======  ======  ======  =======
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohammed Shein ameuagiza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Amali kuhakikisha michezo yote inayoruhusiwa kisheria Zanzibar kuchezwa mashuleni isipokuwa mchezo wa Ngumi (Boxing).

Amesema michezo yote inafaa kuchezwa wala haipunguzi kasi ya mwanafunzi kusoma na kwamba Wizara inapaswa kulisimamia agizo hilo ili Zanzibar iweze kupata vipaji vitakavoiletea nchi Medali za mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Rais Shein ameyasema hayo alipokuwa akizindua Mradi wa “Mpira Mmoja” “One World Football ball Project for Africa”  Wenye lengo la kupambana na Ukatili dhidi ya Watoto kupitia mchezo wa Mpira katika Uwanja wa Aman mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema Mradi huo ambao umewalenga zaidi Wanafunzi wa Shule umefufua matumaini mapya ya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali Zanzibar na kwamba kinachohitajika kwa sasa ni mipangilio mizuri kutoka kwa Walimu na wasimamizi wa michezo mashuleni.

Aidha amesisitiza kuwa michezo haimzuii mwanafunzi kufanya vizuri darasani hivyo Wazazi na walezi waendelee kutoa mashirikiano kwa watoto wao kuhusu michezo stahiki wanayoipenda.

“Jukumu lenu Wizara ya Elimu ni kuhakikisha kuwa Michezo yote ile iliyoruhusiwa kisheria chini ya Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo kuwa inachezwa Mashuleni..Wala michezo haimzuii mwanafunzi kufanya vyema Darasani ” Alisema Rais Shein.

Rais Shein alifahamisha kuwa mradi huo pia utasaidia sana kujenga kikosi imara cha Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa vile vipaji vya Soka vitaibuka vingi mashuleni vitakavyosaidia Timu hiyo kuwa tishio Afrika Mashariki na Kati.

Akigusia suala la Zanzibar Heroes na ushindi wa nafasi ya tatu uliyoipata katika Mashindano ya SECAFA Rais Shein amesema timu hiyo ilicheza vizuri kiasi cha kumvutia sana na kuongeza kuwa Zawadi yao ipo kinachohitajika ni kumalizwa tofauti baina ya Wachezaji na Viongozi wa Timu hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari na Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Mradi huo umelenga kuleta vuguvugu la michezo na kuondoa tatizo la vifaa vya michezo Zanzibar ili kuibua vipaji vitakavyoifanya Zanzibar iwe tishio katika michezo mbalimbali.

Aidha ameongeza kuwa Mipira hiyo itagaiwa katika maeneo yote ya Unguja na Pemba bila ya upendeleo na kwamba Timu zote zilizosajiliwa na Makundi maalum watanufaika na mipira hiyo.

Mradi huo ambao umefadhiliwa na One World Futbal,Shirika la Kusaidia Watoto Duniani kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar unajumuisha Mipira-Elfu 20, itakayogaiwa kwa Wanafunzi wa shule na Timu za Soka za Unguja na Pemba.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

NAFASI ZA KAZI ZA HOTEL (APPRAISER HOTELS & RESORTS).

$
0
0

Ni hotel mpya na ya kisasa iliyopo Bagamoyo ufukweni mwa Bahari ya Hindi. 
Tunapenda kuwatangazia watanzania wote nafasi za kazi mbali mbali katika hotel yetu.

1.Wapishi 10.
-Amemaliza Form Four au Form Six
-Awe na Mafunzo(Certificate) ya Upishi

2.Wahudumu(Waiter and Waitres) 15
-Amemaliza Form Four au Form Six pia awe na Uzoefu wa Kuhudumia.

3.Supervisor 5
-Amemaliza Form Four au Form Six na pia awe na uzoefu wa kusimamia.

4.Internet Cafe Attendant 5
-Amemaliza Form Four au Form Six.
-Awe na Mafunzo(Certificate) ya Mafunzo ya Computer

5.Cashiers 3
-Amemaliza Form Four au Form Six
-Awe na mafunzo(Certificate) ya  Uhasibu/Commerce


Tafadhali tuma maombi yako kwa,

UNIQUE MODEL OF THE YEAR 2012/2013 CATHERINE MASUMBIGANA KUWASHA MOTO LADY IN RED

$
0
0


Mwanamitindo aliebuka na taji la Unique model of the year 2012/2013kutoka katika shindano la Unique model 2012 Catherine masumbigana anatarajiwa kuonekana kwa mara kwanza karika runway ya lady in Lady baada ya kunyakua taji hilo mwishoni mwa mwaka jana.


 Catherine Masumbigana ndiye atakaekuwa yule mwanamitindo atakaetoka na vazi la LADY IN RED usiku wa tarehe 9 february.


 Mipango na mikakati ya mwanamitindo huyu ni kusonga mbele katika tasnia ya mitindo na kuhamasisha tasnia ya mitindo kwa wanamitindo wachanga kukua siku hadi siku katika sanaa.

NAIBU WAZIRI ASISITIZA RESI ZA NGARAWA KUENDELEZWA

$
0
0

 Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 


Na  Zahira Bilali –Maelezo Zanzibar 
11/01/2012

Naibu Waziri wa Ardhi Makazi, Maji na Nishati Haji Mwadini Makame amewataka Manahodha wa Ngarawa waendelee kudumisha utamaduni wao wa kufanya mashindano ya Resi za Ngalawa kila ifikapo nuda wa maadhimisho ya shererhe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Wito huo aliutoa jioni ya jana wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Manahodha walioshiriki mashindano hayo huko Forodha Mchanga Mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema kuwa Resi za Ngarawa ni moja ya utamaduni wa Zanzibar hivyo ipo haja ya kuenziwa mchezo huo ili kukuza utamaduni na kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar yaliyo wakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka kwa Wakoloni.

“Udumisheni utamaduni huu kwani unaleta mshikamano na furaha miongoni mwenu na ni njia nzuri ya kudhihirisha utamaduni wetu kwani Zanzibar watu wake ni wavuvui kihistoria” alisema Mwadini.

Alifahamisha kuwa kuudumisha mchezo huo ni kuwapa umuhimu Wavuvi ilikuona na wao wanathaminiwa na taifa lao kwavile viongozi wa Serikali ndio wanaokuwa Wageni rasmi na Wadhamini wa mchezo huo.

Waziri Mwadini aliwaomba Washriki wa mchezo huo kuwahamasisha wenzao kutoka Vitongoji mbalimbali vya Zanzibar kushiriki mchezo huo ili kuunogesha zaidi.

Aidha aliwataka pia Washirikia kujiandaa vyema zaidi katika mashindano yanayokuja na kuuthamini mchezo wao huo ambao amedai kuwa hauna tofauti na michezo mingine inayochezwa Zanzibar

Mchezo huo ulishirikisha ngalawa 10 kutoka vitongoji mbali mbali vya unguja kama vile Dimani ,chukwani ,Nyamazi Bumbwni ambapo Mshindi wa mchezo huo Fundi Abubakari kutoka Bubwini alizawadiwa Shilingi Laki 2.

 IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR  11/01/2012

MAKAMU WA RAiS DKT. BILAL AZINDUA HOTELI YA KITALII YA GOLD ZANZIBAR BEACH HOUSE & SPA, MKOA WA KASKAZINI A UNGUJA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Januari 11, 2013, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Alexandro Azola. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, Alexandro Azola (ushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya hiyo, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Januari 11, 2013, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mhudumu wa mapokezi wa chumba cha mazoezi na masaji, Zuhura Saleh (kushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo, uliofanyika leo Januari 11, 2013, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, Alexandro Azola (ushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya hiyo, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa  hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Januari 11, 2013, mjini Unguja. 

=====  ======  ====  =====


Ali Issa na Zariha Makame, Maelezo

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal, amewataka maofisa wa Kamisheni ya  Utalii Zanzibar kuwashirikisha kikamilifu wananchi ili waweze kuendeleza sekta ya utalii nchini na kufaidika nayo.

Hayo ameyasema leo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa ufunguzi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano, iitwayo Gold Hotel.  Amesema njia ya kuwashirikisha wananchi    itawafanya waweze kufaidika na matunda ya utalii hasa kupata ajira na kuongeza kipato.

“Mjiulize mnafaidika kwa kiasi gani katika utalii, vipi unachangia uchumi wa Serikali ya Zanzibar na  Tanzania kwa jumla,  lakini  pia ni lazima utalii huu uchangie moja kwa moja kwa wananchi”, alisema. Alisema njia za kuwafaidisha wananchi ni kuwaajiri na kuwasomesha vijana elimu ya utalii itakayowawezesha kuifanyia kazi katika mchanganyiko wa watalii na wageni kiujumla.

Aidha Dkt. Bilal alifahamisha njia za kulikuza soko la utalii nchini, akisema kuna umuhimu mkubwa kuwasomesha watu wanaowatembeza wageni ili waijue vyema historia ya Zanzibar na mazingira, na kwa hivyo waweze kuwashawishi wageni kubakia nchini kwa muda mrefu. Njia nyengine, alisema ni pamoja na kuwafundisha namna ya kuwapokea wageni, kuwashawishi kutumia pesa zao na kutoa miongozo ya kuleta sifa katika mazingira ya visiwa vya  Zanzibar na fukwe zake.

Dkt Bilal alisema miongozo hiyo na mengine mingi, ni muhimu sana na endapo itafuatwa, ni wazi kuwa soko la utalii litakua kwa kasi kubwa.  Aidha aliwaeleza viongozi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), wazingatie na kufikiria kwa makini  kuwavutia wengi wakiwemo wawekezaji wa ndani ili kuijengea sura nzuri Zanzibar kwa kuchangia miji na vijji, na kuwataka katika uwekezaji huo waangalie njia za kutunza  silka na  utamaduni wa Mzanzibari.

Makamu wa Rais alifahamisha kuwa sekta ya utalii inakua kwa kasi kubwa duniani na zaidi ya dola trilioni mbili za Kimarekani zinazopatikana katika nchi nyingi hutokana na mchango wa utalii, ambao pia umeajiri watu milioni 98 duniani kote.   Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Salum Nassor, alisema mpaka sasa jumla ya miradi 511 imeidhinishwa na mamlaka yake katika sekta mbalimbali, ambapo wawekezaji wageni ni 340 na wenyeji 171.

Amesema sekta ya utalii peke yake ina miradi 328 sawa na asilimia 64.19 ambapo kati ya hiyo, wenyeji wanamiliki miradi 214 na wageni 114.  Mkurugenzi huyo alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo ni ishara ya mafanikio, kwani itaweza kuhamasisha sekta nyengine kama vile biashara, kilimo na uvuvi ambavyo vitapelekea kukua kwa uchumi wa nchi. Hoteli hiyo mpya yenye vyumba 66 inatarajia kuajiri wafanyakazi 200.

Mbali na idadi hiyo ya vyumba vya wageni vya daraja mbalimbali, hoteli hiyo ina kumbi kadhaa za mikutano, nyumba tatu zinazojitegemea (villa) ambapo kila moja ina nyumba mbili.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR LEO 11/1/2013

Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania na Benard Mcociech wa Kenya wapima uzito

$
0
0


Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania (kushoto) na Benard Mcociech wa Kenya wakitunishiana Misuli baada ya kupima 
Uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao wa 
Ubingwa wa Afrika Mashariki utakaofanyika leo katika 
ukumbi wa Frends Corner Manzese.


Mabondia Thomas Mashali wa Tanzania (kushoto) na Benard Mcociech wa Kenya wakitunishiana Misuli baada ya kupima 
Uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao wa 
Ubingwa wa Afrika Mashariki utakaofanyika leo katika 
ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxing coach.blogspot.com.

IGP SAID MWEMA AKABIDHI PIKIPIKI 564 KWA POLISI NCHI NZIMA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza. Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova akijaribu kuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nchi nzima mara baada ya makabidhiano, anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba
Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa leo kwa maafisa wa jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjaakizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKAGUA MRADI WA BARABARA YA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR LEO.

$
0
0


Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto) akiongozana na Wakandarasi wa TANROADS pamoja na viongozi wa Kata ya Gongo la Mboto kukagua mradi wa barabara hiyo.
 InjiniaEliseus Mtenga (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Mstahiki 
Meya.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ukaguzi wa barabara ya kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi njia panda ya Kiltex yenye urefu wa Kilometa 1.6.

Pichani Juu na Chini ni Muonekano wa Barabara ya Kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi Njia Panda ya Kiltex ikiwa kwenye matengenezo ya kuweka mifereji ya kupitisha maji ambayo yamekuwa yakiathiri barabara kipindi cha Mvua.
    
Injinia Eliseus Mtenga akiendelea kutoa maelezo ya mradi huo kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto.

Shughuli za ujenzi zikiendelea katika barabara hiyo kama inavyoonekana pichani.

Pichani Juu na Chini ni Msongamano wa magari na wapita kwa miguu kutokana na ufinyu wa barabara unaosababishwa na usafiri wa daladala pamoja na wafanyabiashara waliopanga bidhaa zao kando kando mwa barabara hiyo ambao wanatakiwa kuondoka mara moja ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.





 
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa (katikati) akizungumza na wakandarasi wanaoshughulikia upanuzi wa barabara ya Nyerere kuanzia makutano ya uwanja wa ndege kuelekea Gongo la Mboto ambapo amesema kwa ujumla barabara inatanuliwa kutoka barabara mbili kuwa barabara tatu na kuchimbwa mitaro ya mvua ili maji yaliyokuwa yakiharibu barabara yaweze kupata njia.

Amesema ukubwa wa kazi nzima ni kilomita 1.6 utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwa mradi huo unasimamiwa na wakala wa barabara yaani TANROADS. Aidha Mstahiki Meya ameitaka serikali ya kata kumsaidia mkandarasi kuondoa wafanyabiashara ambao wapo maeneo ya barabara ili kazi iweze kufanyika kwa wakati kwa kuwa kazi hii inatakiwa kuisha mwezi Mei mwaka huu. Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki.

Pichani juu na chini ni Injinia Eliseus Mtenga (katikati) kutoka TANROADS Dar akitoa maelezo mafupi kwa Mh. Mstahiki Meya wa Ilala juu ya mradi wa upanuzi wa barabara ya kuelekea Gongo la Mboto kuanzia Ukonga Mombasa hadi njia panda ya Kiltex na marekebisho ya eneo korofi karibu na Sekondari ya Pugu ambapo amesema lengo ni kupanua barabara kwa Mita 3.0 kila upande ili kuwezesha njia tatu za magari kupatikana.

Hii ni awamu ya tatu katika upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi tatu ambapo awamu ya kwanza ilihusisha Kilometa 1.8 na Awamu ya pili Kilometa 2.5 zilishakamilika. Kushoto ni Injinia Eliamin Tenga wa TANROADS na kulia ni Site Engeneer wa mradi huo Godson Tenga.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA TROIKA CHA SADC JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Mwenyekti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha asasi hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Katibu mkuu wa SADC, Dk.Tomaz Salomao, Rais Armando Guebuza wa Msumbiji, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na kulia ni Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini. (PICHA NA FREDDY MARO -IKULU.

anayetuhumiwa kuwa ni kibaka mzoefu eneo la samora anaswa na askari kanzu leo jijini dar,akutwa na vifaa vya kufungulia milango ya magari

$
0
0
Mtu Mmoja anaetuhumiwa kuwa ni kibaka mzoezi maeneo ya mtaa wa Samora akiwa amenaswa na kuwekwa chini ya ulinzi na Askari kanzu,ambao inaelezwa walikuwa wakimsaka muda mrefu mhalifu huyo,na leo siku zake zikawa zimetimia,mtu huyo ambaye jina lake halikujulikana mara moja alikuwa na vifaa mbalimbali kama vile spana,dispisi na vitu vingine ambavyo ilielezwa kuwa amekuwa akivitumia kuiba vifaa mbalimbali vya magari kati kati ya jiji.
 Mtuhumiwa huyo akiwa ameweka chini ya ulinzi ili asikimbie
 Mtuhumiwa huyo akifungwa pingu mara baada ya kuletwa na Askari kanzu wengine waliokuwa jirani wakifanya doria kati kati ya jiji la dar,ambapo sasa hivi inaelezwa kumeibuka wimbi kubwa la ukwapuaji/ama wizi wa vifaa mbalimbali vya magari.
Pichani ni Askari Kanzu wikiwa wamemuweka chini ya Ulinzi mtu mmoja anaetuhumiwa kuwa ni kibaka mzoefu katikati ya jiji la Dar,Mtaa wa Samora Avenue mapema leo mchana,Mtuhumiwa huyo inadaiwa ni mahiri wa kukwapua vifaa mbalimbali vya magari,kama vile Radio,Power window,Site Mirror,na vitu mbalimbali,aidha katika hali ya kushangaza mtuhumiwa huyo alianza kuropoka kwa kudai kuwa leo wameamua kumkamata kwa sababu hajawapa kitu (Visent) wala kuwatumia vocha ndio maana wamemtia nguvuvuni.

VIDEO YA HOTUBA YA RAIS KIKWETE NA UZINDUZI WA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU, IGUNGA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa darala la Mbutu wilayani Igunga katika mkoa wa Tabora Januari 7, 2013. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili mnamo Novemba mwaka huu kutakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo na mikoa ya jirani

Question: J.Kassam Ft Ivan

$
0
0

Bloggers

Nawaletea Link ya mwimbo mwingine wa mwanamuziki chipukizi Juma Kassam akisindikizwa na Ivan ,anakuja kivingine
akiuliza swali"Question",ni
zaidi ya ubunifu.

Muelekeo mpya zaidi ya vile tulivyozoea ya nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi.




Wasalaam.
E.N.M.Manase
Mdau -Image Profession

mtazamo wa msanii mkongwe afande sele katika hili

$
0
0

NIONAVYO MSINDI.


Wanalalamika kila siku Chinga kukimbilia Dar-es-Salaam na ongezeko la watu dsm, foleni halafu bado kila kitu wanataka walundike Dsm. Sasa nani atabaki Mikoani? Afanye nini Lindi, Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Iringa, Singida, Mara n.k kama kila kitu kipo Dsm?

Ukistaabu ya Musa .... Kila siku viongozi wa Serikali wanalalamika kwamba wamachinga/vijana mikoani kukimbilia DSM ni tatizo la kitaifa au ni bomu hatari kwa amani ya Taifa, ila kila siku wanajenga na kubomoa miundo mbinu ya Jiji la Dsm ili kukabiliana na foleni,

 misongamano ya watu na makazi kwa kuwa ongezeko la watu Dsm linakua maradufu kila mwaka na yote ni kwa sababu nyanja kuu za ajira/uchumi kwa kiasi kikubwa zipo Dsm. Watu wengi huja Dsm sasa kitu cha ajabu;



Bado viongozi wa Serikali tena Wasomi wakubwa (Maprofesa/madokta) hawalioni hilo tatizo kama ni tatizo ambalo hata asiejua kusoma/kuandika analiona lakini wao hawaoni wanazidi kulazimisha kila kitu kiwe DSM, nani atabaki Kigoma, Lindi, Mtwara, Singida n.k afanye nini?



Cha ajabu wanawabeza wananchi wa Lindi na Mtwara ni wapuuzi/wahaini wa kupuuzwa wajinga wasiojielewa kwa kukosa shukrani, eti wamepewa umeme wa megawati 18, hawawezi kuutumia kwa lolote, Watautumia ikiwa mumeua viwanda vya Korosho Lindi na Mtwara, Mumeua Mashamba ya Mkonge Lindi, Karanga Nachingwea, mnawakopa Korosho na Ufuta hamuwalipi kwa wakati, hawapati pembejeo za kilimo kama inavyostahili, ni dhambi kubwa kuwaita wapuuzi hawakatai Umeme unaotokana na Gesi ya kusini kutumika Tanzania nzima!


 Ndani ya Miaka 50 ya Uhuru mumeshindwa kuwawekea road mpaka leo inasuasua haijaisha ni kama km 500 tu, Munajua kuzorota kwa uchumi wa mikoa ya Kusini ni kutokana na kutumika kwake kwenye Ukombozi wa Nchi za kusini mwa Afrika! Msumbiji, South Afrika, Angole n.k.. Katika mwaka wa uchumi unaoishia Novemba Korosho imeingizi US DOLA 151 MILIONI, pamba dola 53 milioni.. licha ya zao la korosho kuliingizia taifa kiasi cha shilingi trilioni 7.2, ndio mikoa iliyo nyuma kimaendeleo katika mika 51 ya uhuru


MUNGU IBARIKI TANZANIA

mambo moto moto ndani ya Mjengwablog

$
0
0

Nini Kipya?

Blog yako kipenzi ya Mjengwablog imefanya maboresho ya kina katika kuhakikisha tunaboresha muonekano, usalama na muundo wa uendeshaji.
 Pata mhabari kwa urahisia   
 Tuma makala moja kwa moja
 Ujumbe juu ya maoni
 Majadiliano kwenye forums h
 Matangazo bila gharamakkkk
 Muonekano wenye mvuto fffff
 Habari za papo kwa hapofff
 Maoni moja kwa moja ggfg
 Mawasiliano yaliyoboreshwa

Mlisho wa habari

Pokea mukhtasari wa habari moja kwa moja kwenye email yako.

Chambuzi za Wiki

Ujasiriamali ni ajira kamili -  Na. Albett Nyaluke Sanga
Kama ningekuwa Waziri wa Elimu  -  Na. M Nyoni.

Zenye   Hisia Zaidi

Habari zilizovuta hisia za watu kwa kuwa na maoni mengi zaidi.

Tarime  kuchafuka tena

sisi ni wakulima halali wa nchi kama sasa hata tutashindwa kujiajiri kwa mavuno tutafanya kazi gani?TARIME IMEKUWA KISIWA HUWEZI KUFANYA KAZI KWA UHURU MAMLAKA ZINATUMIKA VIBAYAsasa tunaamuliwa kuchoma moto shehena ama tusage mahindi tule!! zaidi ya tani mia 5 tutakula mpaka lini? na t ukisaga sumu inaisha?

 
hh 
Bibi naye analea                     Utamu wa wali uule kwa mkono             Umwene Maggid huyu

Mlisho wa habari

Pokea mukhtasari wa habari moja kwa moja kwenye email yako.

Kanisa ladaiwa kutishwa na njaa Handeni.

$
0
0

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

MWENYEKITI wa Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini, ambaye pia Mchungaji wa Kanisa la Pentekost, mkoani Mbeya, William Mwamalanga, amesema hali ni mbaya wilayani Handeni mkoani Tanga, kufuatia njaa na ukosefu maji safi na salama.

Akizungumza na Handeni Kwetu jana jijini Dar es Salaam, Mwamalanga, alisema kwamba njaa ni kali kiasi kwamba watu wengine wanakula maembe na mboga mboga.

Alisema baada ya kusikia hali hiyo kwenye vyombo vya habari, akiwa kama kiongozi wa dini, alilazimika kufunga safari hadi katika wilaya hiyo ili kuangalia balaa hilo.

“Hali ni mbaya, hivyo naomba wadau sasa waingilie kati kwa kunusuru watu ambao watapoteza utu na uhai wao kwasababu ya njaa, ambayo ndio tishio kubwa kwa wakazi wa Handeni.

“Nimetoka Mbeya kwa ajili ya kwenda Handeni na kukaa kwa wiki mbili nikitembelea sehemu kubwa ya wilaya, hivyo nimejionea mwenyewe na watu wajuwe hali si nzuri,” alisema Mwamalanga.

Hata hivyo serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, walitangaza kupelekewa chakula cha bei rahisi, ambapo wananchi wao watalazimika kununua kwa bei isiyozi 750 hadi 900.

Habari hii kwa hisani ya  http://www.handenikwetu.blogspot.com/

dala dala yamgonga mwendesha piki piki na kufa papo hapo jijini mwanza.

$
0
0

Askari wa usalama barabarani wakipima ajali iliyotokea leo jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW ambapo dereva wake (ambaye ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa) alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea, inasemekana kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.

Kijana aliyefariki  alitambulika kwa jina la Mayunga Clement Lufuta.

Pikipiki hiyo yenye namba za usajili T988 BDW eneo lake la mbele limezama kabisa uvunguni mwa daladala kiasi cha kuharibika vibaya.
Mwili wa marehemu Mayunga Clement Lufuta ukitolewa barabarani kusubiri gari maalum kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando kuhifadhiwa.
Hiki ndicho kitambulisho kilichosaidia kumtambua marehemu.
HABARI KWA HISANI YA GSENGO BLOG.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Picha na OMR. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo.

dr shein aongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya zanzibar leo.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikagua gwaride la Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza kukagua gwaride la  Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zabzibar.{Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.

sikiliza pini jipya la Belle 9-listen.

Wasipoangalia, UVCCM utakuwa ni umoja wa porojo

$
0
0

 Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

JUMUIYA za vyama vya siasa ni muhimu sana. Jumuiya ndio muhimili wa chama chochote cha siasa. Kwa Tanzania, jumuiya za chama, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimekuwa na ukakasi sana.
 
Licha ya kuwa na purukushani nyingi katika utafutwaji wa viongozi wake, lakini baada ya kupatikana, umuhimu wake hauonekani. Wote huwa kimya, wakishindwa kukitetea chama. Nasema haya huku nikiangalia namna jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), wanaposhindwa kutangaza vipaumbele vyao katika kuhakikisha kuwa chama kinakuwa salama.
 
Katika Uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma mwaka jana, tulishuhudia vijana wakitunishiana misuri wakishinikiza au kutetea baadhi ya watu wao ambao kwa kiasi fulani walishindwa. Ingawa mwenyekiti Taifa alibahatika kuchaguliwa Sadifa Khamis Juma, kuna uwezekano mkubwa kuwa atashindwa kuimudu kasi ya kisiasa inavyozidi kuwa juu siku hadi siku.
 
Huku Sadifa akishinda nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi huo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa Mboni Mhita, mtu ambaye kwa pamoja baadhi ya vijana walipinga na kusema ushindi wao ulitawaliwa na hira. Sitaki kusema zaidi juu ya ushindi wa wanachama hao wa CCM, ila kikubwa ni kujadili namna gani jumuiya hiyo inaweza kujiendesha kwa kushindana na kasi ya mabadiliko ya kisiasa.
 
Watu wengi wamekuwa na mawazo kuwa CCM imezeeka na inastahili kuwekwa kando ili kupatikana chama mbadala wa kuliongoza Taifa.  Ni mawazo yanayoweza kuaminiwa na wengi, maana kupanuka kwa sekta ya mawasiliano, habari mbaya za CCM zimekuwa zikisambazwa kwa njia mbalimbali.
 
Kwa mfano, unaweza kufungua email na kukutana na ujumbe unaoeneza sumu mbaya ya kushindwa kwa CCM kuwaongoza Watanzania. Mbali na hilo, kwenye mitandao ya kijamii habari hizo sasa ni kawaida.   Kwa bahati mbaya, sumu hiyo inasambazwa zaidi kwa vijana, wakiamini ndio wenye uwezo wa kufanya mabadiliko. Wanajua kama vijana wakiamua, basi malengo yatatimia.
 
Kwa wanaofuatilia siasa za Tanzania, watakubaliana na mimi kuwa, siasa zinazofanywa na vyama vya upinzani zisipoangaliwa, hali inaweza kuwa mbaya kwa chama tawala.  Vyama hivyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa ya kueneza elimu ya uraia ambayo ndio tatizo kubwa. Kama hivyo ndivyo, basi kuna sababu sasa jumuiya za CCM, hasa ya vijana kubuni namna gani ya kuwatembelea wanachama wao kueneza sera na ilani za chama chao.
 
Wao kama jumuiya inayojipambua ya vijana wana kila sababu ya kuwaweka sawa vijana wanaoyumbishwa na sakata la urais 2015. Baadhi yao wanatumiwa ovyo ovyo na wanasiasa bila huruma. Wengine wamemwagwa katika mitandao ya kijamii wakihubiri hili na lile kwa ajili ya watu wao. Kwa bahati mbaya, watu hao wanapofanya kazi hiyo hawaangalii athari ya chama chao.
 
Kwa mfano, mtu yupo tayari kumtukana au kumsema kiongozi fulani kwa ajili ya kumbeba yule amtakae. Hii sio njia nzuri.  Sote tunaamini kuwa kampeni bado na kinachofanywa sasa ni hisia na maandalizi ya kiundani, maana hakuna mwanasiasa hata mmoja ndani ya CCM aliyetangaza hadharani kuwa anagombea urais 2015 akipitishwa na chama chake.
 
Kwa sababu hiyo basi, huyu Juma na Mboni na viongozi wengine wa jumuiya hiyo ya UVCCM wanafanya nini kunusuru msururu huu wa vijana wanaoweweseka na siasa za maji taka?  Wao kama viongozi wa vijana wote wa Tanzania waliokuwapo ndani ya chama hicho kikongwe, wamefanya ziara ngapi kwa ajili ya kutafuta wanachama wapya na kuwaweka sawa wale wanaotaka kukihama, au wale wanaolia na maisha duni kutoka kwenye serikali ya CCM?
 
Wao kama jumuiya ya vijana, inafanya kazi zake kwa mtindo gani kuhakikisha kuwa wote wanakuwa kitu kimoja? Je, yale makundi yaliyoundwa katika kipindi cha uchaguzi yamevunjwa? Kama hayajavunjwa, hawaoni athari kwa CCM itazidi kuwa kubwa na kuyumbishwa katika Uchaguzi ujao, ukiwamo wa Serikali za Mitaa? Maswali kama haya majibu yake ni njia nzuri kwa uhai wa CCM.
 
Tuachane na wale wanaosema chama kinapendwa. Ndio kinapendwa, lakini si wote wanaokipenda na kukiheshimu. Chama kitapendwa zaidi kwa kuhakikisha waliokuwa kwenye uongozi wanafanya kazi nzuri na kuondoa kero za Watanzania wao.  Kama jumuiya zitafanya kazi kwenye uchaguzi wa ndani tu, chama kitaanguka. Huo ndio ukweli wa mambo. Wanachama wa CCM wanastahili kulijua hilo kwa ajili ya uhai wa chama chao.
 
Mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akirithi mikoba ya Willson Mukama, alifanya ziara katika baadhi ya mikoa kufanya mikutano ya hadhara.  Pamoja na mambo mengine, Kinana alitumia nafasi hiyo kuwazindua watendaji wa serikali ambao wapo chini ya CCM, wakiwamo mawaziri ambao baadhi yao walikuwapo na kujibu maswali ya wananchi wao.
 
Ni hatua nzuri sana kwa ajili ya kutangaza sera, kutafuta wanachama wapya, maana bila hivyo hali itakuwa mbaya. Ni kweli, hivyo nilitegemea kuwa hata hizi jumuiya za CCM, ikiwapo ya UVCCM, wanaweza kutumia njia hiyo, ukizingatia kuwa ni wenye nguvu zao.  Badala ya kumsubiri Kinana aende huku na kule kuelezea sera za chama chake, Juma na viongozi wenzake wanatakiwa waifanye wao kazi hiyo kwa kutembelea sehemu hizo kuzungumza na wapiga kura wao.
 
Naamini katika ziara hiyo, faida yake kubwa ni kuona inawavutia vijana ili waingie kwa waliokuwa nje au kuwazuia waliokuwa ndani wasitoke na kuhamia kwenye vyama vya upinzani.  Sitaki kuamini kuwa ni kweli viongozi waliochaguliwa katika jumuiya ya UVCCM hautakuwa na jipya na kutekwa kabisa na jumuiya nyingine.
 
Ukiangalia kwa haraka, utagundua jumuiya ya vijana CCM ina nguvu kwenye uchaguzi maana joto hilo hukolezwa na wenye mlengo wao wa kisiasa, huku wengineo wakimwaga ‘noti’ kama ilivyodaiwa na wahusika.
 
Lakini kiutendaji na kuvitetea vyama vyao, nashawishika kusema kuwa, viongozi wa hao wa upinzani wamekuwa juu mno. Hii ni picha mbaya. Picha isiyovutia kwa Tanzania yenye kelele za mabadiliko.  Kupoa huku kwa jumuiya za CCM, hasa UVCCM ni dalili njema? Wao kama wamelala kiasi hiki, je, ni kijana gani anayetaka kuwa mwanachama atakuwa kwenye kundi lao?
 
Kuna haja ya kuinuka kwa viongozi hao wa UVCCM. Kuna hatari kubwa kwa kukaa kwao kimya, hasa kwa waliokuwa wakipayuka kulia na ushindi wao kupata la kusema kuwaaminisha Watanzania kuwa waliochaguliwa hawakuwa na jipya, hata la kuwaunganisha vijana ili wazungumze kitu kimoja kinachohusu Tanzania na chama chao.
 
Kulisema hili kunahitaji moyo wa chuma, hasa kwa wale ambao daima wamekuwa makini kusubiri kusifiwa na sio kukosolewa, jambo ambalo katika Dunia ya leo halipo.  Natuamini baada ya kusema haya, Juma na Mboni wao kama viongozi wa umoja huo wa vijana wa CCM watakaa na kutafuta namna ya kusaidiana na viongozi wengine wa CCM, akiwamo mwenyekiti wao, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Vijana wakifanya kazi imara za chama, hata wakubwa wao hawatakuwa na kazi ngumu ya kufanya, hasa kitakapofika kipindi cha uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao kwa hakika utakuwa na ugumu wa aina yake.
 
Ni pale wapinzani, wakiwamo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), TLP, NCCR-Mageuzi na vinginevyo vinavyopigania kulikomboa Taifa, wakisema kuwa CCM kimeshindwa kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maisha bora.
 
Tukutane wiki ijayo.
0712 053949
0753 806087
 
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images