Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live

Heri ya X-mass kutoka Ngoma Africa Band aka FFU

0
0


Bendi ya Muziki wa dansi Ngoma Africa Band yenye makao yake nchini
Ujerumani inawatakia wadau wote Heri ya Siku kuu  ya X-Mass,
Amani na Upendo ndio msingi pekee wa furaha ya maisha.
Merry X-Mass wadau wote ! Popote mlipo
Furahia Merry Christmass na midundo 

TONITE/USIKU WA LEO-XMAS EVE WASHINGTON DC,NEW VENUE,VIP STYLE

0
0

MEYA JERRY SILAA ASHIRIKI KATIKA KAMPENI YA USAFI KATIKA KATA YA GONGO LA MBOTO

0
0

Pichani Juu na Chini ni Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto, Jerry Silaa akiwa na baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakifanya kazi ya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu.

Mstahiki Meya wa Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la mboto,Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakati wa kufanya usafi katika eneo la Stendi ya Mabasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhimiza usafi na kuhifadhi mazingira katika jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa na makamu wa Rais mwanzoni mwa mwezi huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim akimpongeza mshindi wa Miss East Africa 2012

0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Exim ya Tanzania Bw. Anthony Grant (kushoto) akimpongeza mishindi wa mashindano ya ulimbwende ya Miss East Africa 2012 Jocelyne Maro, ambaye ni mshiriki kutoka Tanzania, mara tu baada ya kuvishwa taji la ushindi baada ya kuwabwaga warembo 15 waliofika fainali kutoka nchi mbali mbali. Fainali hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mkutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni mmoja wa majaji wa mashindano hayo, Bi Ayan Ahmed.

USIKOSE MKESHA WA X-MASS NDANI YA KIOTA CHA THAI VILLAGE LEO USIKU NA SKYLIGHT BAND.

0
0

Kikosi kazi cha SKYLIGHT Bendi kikiongozwa na Joniko Flower kuporomosha burudani mwishoni mwa juma katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. USIKOSE Mkesha wa X-MASS na SKYLIGHT BAND leo Usiku kuanzia saa tatu pale pale Thai Village.
Diva's wa SKYLIGHT Band Aneth Kushaba AK 47 sambamba na Mary Lucos wakishambulia jukwaa.
SONY MASAMBA sambamba na Aneth Kushaba AK47 wakipiga shoo ya nguvu.
Muziki umenoga mpaka wengine waliamua kuvua mashati.
Pichani juu na chini ni Binti wa Kiafrika mrembo aliyeumbika kisawa sawa.... akimwaga radhi mbele ya kadamnasi kuonyesha umahiri wake wa kuzungusha nyonga wakati nyimbo ya Carolina ikiimbwa na kuwaacha hoi wengine wote waliokuwa kwenye dancing floor.
Sebene limekolea....asiyekuwa na mwana aeleke jiwe.


It's Reggae and Ragga time....Aneth Kushana AK 47 akionyesha ufundi wake.
Uzao wa BSS Mary Lucos akielekea kwenye viti kunyanyua mashabiki wake.
Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakijimwaga kwa dancing floor.
Pichani Juu na Chini Umati wa Mashabiki wa SKYLIGHT Band wakizungusha mduara wa mbele aende mbele na wa nyuma arudi nyuma.
Pichani Juu na Chini ni Papa Justin Ndege na mdau wakiwatunza wapiga vyombo na waimbaji wa SKYLIGHT Bendi baada ya kuguswa na uimbaji pamoja na upigaji wa vyombo.
Mario Mpingirwa akionyesha jinsi gani anavyopenda kinywaji chake.
Papa Justine Ndege ( wa pili kulia) akiwa na marafiki wa karibu na mashabiki wa SKYLIGHT Bendi.
Wadau wa Makumbusho Kijitonyama, Yusuph (kushoto) huku Eric Ndalu akiwa na mai waifu.
Mdau Lussa ( wa pili kulia) alitia timu SKYLIGHT Band kula bata na marafiki zake.
One and Only Mekydiva Mash Macha (katikati) akishow love na Blogger King Kif, huku Jacqueline Mzindakaya akiipa mgongo Camera yetu.
Mdau Mwika (wa kwanza kulia) bila kukosa akishow love na marafiki zake.
Mashabiki nambari One wa Skylight Band wakishow love.
Models wakitega pozi kwa Kodak. Looking Fly Girls.
Hata shida na mtu kwa raha zake...Kuna msemo unasema 'raha jipe mwenyewe'.
King Kif na Mdau Godwin Gondwe a.k.a Double G alipita pande hizi kuchungulia burudani ya Sky Light Bendi ikoje.
Diva's wa SKYLIGHT Band Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos baada ya kupiga show ya nguvu walipata Ukodak.

kampuni ya Msama promotions yatoa MISAADA kwa VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMASI na mwaka mpya

0
0

 Baadhi ya vitu vilivyokabidhiwa kwa vituo vya Msimbazi Center na Chamzi Group kwa ajili ya shereje za sikukuu ya krismasi na mwaka mpya  .

Mkurugenzi wa Msama Promosheni, Alex Msama (kushoto) akikabidhi vitu mbalimbali kwa mwakilishi wa kituo cha watoto yatima cha Chamazi Group, Haruna Mtandika ikiwa ni sehemu ya mapato ya fedha zilizopatikana na tamasha la Pasaka, kwa ajili ya sherehe za sikukuu ya krisimasi na mwaka mpya. Katikati ni mratibu wa tamasha la Pasaka kutoka Baraza la Sanaa la Taifa,Malimi Mashiri.

Mkurugenzi wa Msama Promotions,  Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam. 

 Mratibu wa tamasha la Pasaka kutoka Baraza la Sanaa la Taifa, Malimi Mashiri akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kushuhudia zoezi la kukabidhi vyakula mbalimbali kwa katika vituo vya kulelea watoto yatima.

  Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Center, Consolata Pius akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa  Mkurugenzi wa Msama Promosheni, Alex Msama (kulia) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za sikukuu ya krismasi, vitu hivyo vimetokana na mapato yaliyotokana na tamasha la Pasaka.

 Alex Msama akiwa na watoto wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi Center








=========  ========  =======  ========

 MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ametoa msaada wa vyakula katika vituo viwili wenye thamani ya sh.milioni 2.8.


 Akizungumza katika hafla maalum ya ugawaji misaada hiyo, alisema ametoa misaada hiyo  ikiwa ni sehemu ya ahadi yake katika tamasha la pasaka. Alisema kuwa kwa sasa amekabidhi vyakula kama, mchele, maharage, unga wa ngano, unga wa sembe na mafuta. 


Misaada hiyo imekabidhiwa kwa vituo vya msimbazi Center na Yatima Group ya Mbagala Chalambe.  Msama alisema kwa sasa amekabidhi katika vituo hivyo ambavyo vipo Dar es Salaam na atafanya hivyo katika mikoa tofauti. Kwa upande wa mlezi wa kituo cha Yatima Group Haruna Mtandika, alimshukuru Msama kwa msada huo ambao umesaidia kituo chake. " 


Namshukuru sana Msama kwa kuweza kusaidia kituo chetu haswa katika kipindi hiki cha siku kuu"alisema Mtandika.  Kwa upande wa Afisa Sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Malima Mashili, alimpongeza Msama kwa kutimiza ahadi zake kwa walengwa.


 Alisema Basata inawataka wengine waige anavyofanya Msama kwa kuweza kutimiza ahadi zake katika tamasha. 
Kwa upande wa kituo Mlezi wa kituo cha Msimbazi Center Imakulata Pius, alisema anamshukuru sana Msama na kuwataka wengine waige mfano huo. "Naomba na wengine waige mfano huu wa kampuni hii kuandaa tamasha na kutoa kile walichoaidi katika matasha wanayofanya"alisema Pius.

MWAKYEMBE APIGA MARUFUKU VIZUIZI VILIVYOWEKWA NA HALMASHAURI KWENYE STENDI ZA BARABARA KUBWA NCHINI

0
0

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amepiga marufuku na kuagiza kuondolewa vizuizi vyote vilivyoanzishwa na Halmashauri kwenye stendi za barabara kubwa kwa ajili ya kukusanya ushuru kwani vinaleta usumbufu kwa abiria.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo jijini Dar es Salaam, wakati alipofanya ya ziara ya kushtukiza kwenye Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi majira ya saa 11:30 alfajiri, ili kujionea utendaji kazi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), na Kikosi cha Usalama Barabarni (Trafic), haswa katika udhibiti wa nauli holela katika kipindi hiki cha sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya.

Alisema uwamuzi wake huo unatokana na kubaini kuwa Halmashauri hizo, zimekuwa zikiwalazimisha madereva kuingiza magari (Mabasi), kwenye vituo hivyo ambavyo siyo rasmi kwa lengo la kujikusanyia ushuru. Amevitaja vituo hivyo vilivyolalamikiwa kwa usumbufu huo, kuwa ni pamoja na Mafinga, Kibaigwa, Nzega, Kibaha na vingine.

“Madereva wamekuwa wakilazimishwa kuingia katika stendi hizi hata kama hawana abiria wakushuka amakupakia, kitendo ambacho kinawapotezea abiria muda wao wakufika kule wanakokwenda bila sababu za msingi”alisema Dk Mwakyembe. Alisema utaratibu huo haukubaliki, endapo ukiachwa uendelee hivyo iko siku watazuka watu watafikia hatua ya kuanzisha vizuizi kama hivyo majumbani mwao lengo likiwa ni kuibia wananchi. Dk Mwakyembe amezitaka Halmashauri hizo kuacha utaratibu huo na baadala yake watafute vyanzo vingine vya ukusanyaji mapato.

Katika hatua nyingine Dk Mwakyembe amewaonya baadhi polisi wa kikosi cha usalama barabarani kutokana na mtindo wao wakusimamisha magari kwa kushtukiza wakitokea vichakani. Alisema malalamiko hayo ameyesikia siku nyingi hivyo ameahidi kuwa atayafanyia kazi, ambapo aliwatahadharisha askari wenye tabia kama hizo, watambuwe muda wao sasa unahesabika.

Akizungumzia hali ya usafiri katika kipindi hiki cha sikukuu hizo mbili, Alisema hali aliyoikuta Kituoni hapo inaridhisha kwakuwa abiria wote kwenye mabasi walikuwa wamepata tiketi kwa bei elekezi ya Sumatra. Dk. Mwakyembe alitoa wito kwa abiria wote kuwa wahakikishe wanatoa ushirikiano kwenye vyombo vinavyohusika pindi watakapotozwa nauli kinyume na ile ya kawaida. “Msikubali kulipishwa zaidi toeni taarifa haraka, hata katika nauli za mizigo msikubali kulipia mzigo wa kilo 20 atakaekubali yote hayo mtambue amejitakia mwenyewe na asilaumiwe mtu”alisema.

Naye Kaimu Mkurugezi Udhibiti Usafiri wa Barabarani (Sumatra), Leo Ngowi, alisema katika operesheni inayoendelea ya kuyakamata magari yanapandisha nauli holela jana, walifanikiwa kulikamata basi la Kampuni ya KVC lenye usajili namba T709AAT. Alisema gari hilo lilikwenda kinyume kwa kuwatoza nauli ya sh 35,000 baadala ya sh 25,000 abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Arusha.

Aidha, Sumatra imetoa leseni za muda kwa wamiliki magagri ambayo yamekidhi viwango vilivyohitajika na mamlaka hiyo, yenye uwezo wa kuchukua abiria 30 kwa lengo la kusaidia kusafirisha abiria wanaofika kwa wingi kituoni hapo ambapo mikoa inayoongoza kwa abiria ni Kilimanjoro, Arusha na Mwanza.

Nafasi za Kazi ya Ualimu

0
0

Little Wonders Nursery & Primary School                                        (Bagamoyo,Kiwangwa/Msata Road)

Ni shule mpya ya kisasa ya bweni,ipo Kiwangwa/msata road nje kidogo ya Bagamoyo umbali wa km 1.5, tunatangaza nafasi za kazi ya Ualimu wa Chekechea(Nursery) na Primary

Chekechea(Nursery)nafasi 5,Sifa za muombaji;
-Cheti cha kufundisha elimu ya Awali
-Cheti cha Kumaliza Form Four au Leaving Certificate 

Mwalimu Primary nafasi 4, Sifa za Mwombaji     
-Cheti cha Kufundisha Primary kama Grade A au Diploma.
-Cheti cha kumaliza Form Four au Leaving Certificate

*Mshahara ni maelewano ambayo yatafanyika wakati wa interview.

Tafadhali tuma maombi yako ukiambatanisha na namba yako ya simu kwenye 
email; j-humba@live.com  au piga simu  +255712619767

gazeti lako makini la dira liko sokoni kwa sh 500/= tu.

0
0



JUST IN; basi la New Force toka Mbeya kwenda DAR lapata ajali ASUBUHI HII

0
0
Breaking newss basi la New Force toka Mbeya kwenda Dsm lapata ajali asubuhi hii zaidi ya majeruhi 20 wakimbizwa hospitali.  CHANZO CHA HABARI Tone Multmedia Group tumeshuhudia tukio zima . zaidi fuatilia www.blogszamikoa.blogspot.com.

Club 327 lands American DJ for New Year’s Eve Celebrations

0
0

Club 327 lands American DJ for New Year’s Eve Celebrations


DJ Topspin returns to Dar after one year.


Club 327 today announced that the American DJ, DJ Topspin, would be the headliner for the club’s New Year’s Eve celebrations.  DJ Topspin has become a favorite in Bongo, as he was here just over a year ago to celebrate the two-year anniversary of Groove Theory, a once amonth soulful house music event.


According to Club 327 owner, Mr. Lawrence Kadri, the confirmation of DJ Topspin positions Club 327 as the place for music lovers to be on New Year’s Eve. “At Club 327 we are firm believers in originality in the market. That is why we have positioned Club 327 as the place to be for anyone who loves music” said Kadri “Other locations are doing different things, some are having dinners, while others are having balls, all of this is great as it creates options in the market, Club 327 is the option for people who want to bring in the New Year on the dance floor” added Kadri


DJ Topspin is widely recognized for his eclectic ear as well as his mastery of a wide range of musical genres including Top 40, Hip-Hop, Rap, Old School, Soulful House, Reggae, and more giving listeners amazing options on the dace floor.  His style has been described as “Cognac-Smooth” and perhaps this is why he was also selected for the evening, as Hennessy Cognac has partnered with Club 327 for the New Year’s Eve Celebration.  When not on the turntables that night, DJ Topspin is expected to meet & greet lucky guests in the Hennessy VIP Suite within Club 327.


Tanzania is a destination that ranks high on DJ Topspin’s list of global party spots as he even passed on a New Year’s Eve party in the Central American country of Panama this year to return to Dar es Salaam. “Tanzania has a special place in my heart” said Topspin “It is the very first country I ever visited in Africa and changed my whole perception of the mother land, I am very excited to return,” added Topspin.


New Year’s Eve festivities kick off at 9pm on the 31st and DJ Topspin is expected to start spinning a little before midnight and continue deep into the morning.  Admission is 30,000/= and admission is restricted to those aged 21 and above. 

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMTEMBELEA MZEE SAID NOOR ABDULKADIR NA KUTEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA, MKOA KUSINI UNGUJA LEO

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba 23, 2012. Mzee huyo anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 13.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal.
 Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea ramani ya ujenzi mpya wa shule ya Chwaka, kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fadhili Hamada Mshamba, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kituo hicho leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mzee Silima Jendele, wakati Makamu alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Wazee leo, katika Mkoa wa Kusini Unguja.PICHA ZOTE NA OMR

SCHOOLMATES WA ZANAKI GIRLS.

0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angella Kairuki akishow love na my schoolmate wake Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu katika viwanja vya Mnazi hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani.

MABONDIA WA ‘NDONGA ZA MWAKA’ WAPIMA UZITO KWA MPAMBANO WA KESHO

0
0
Mabondia wote wakiwa katika picha ya pamoja.
Mada Maugo akiwa na mpinzani wake toka Uganda, Iga Jumaa.
Mada Maugo akipimwa uzito.
Mbwana Matumla naye akifanya zoezi hilohilo.
Esther Kimbe akipima uzito.
Irene naye akiwa kwenye mashine ya kupimia uzito.
David Charanga akiwa juu ya mashine ya kupimia uzito.
Iga Juma akipima uzito.
--
MABONDIA watakaotwangana kesho ndani ya ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala wamepima uzito leo asubuhi katika ukumbi wa Hoteli ya Atriums, iliyoko Afrika Sana, Sinza, Dar es Salaam.
Mabondia hao ni Mada Maugo wa Tanzania, Iga Juma wa Uganda, Mbwana Matumla wa Tanzania na David Charanga kutoka Kenya, Wengine ni Chupaki Chipinda, atakayezipiga dhidi ya Bahati Mwafyele na mabondia wa kike Esther Kimbe na mpinzani wake Irene Kimaro.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)

Mshindi wa Shindano la Facebook ya Airtel Atangazwa

0
0
 Mshindi wa jezi ya Manchester united kupitia shindano la Facebook ya Airtel bi.Seba Aggrey akionyesha jezi yake iliyosainiwa na wanachama wa timu hiyo aliyokabidhiwa katika ofisi za makao makuu ya Airtel  jijini Dar Es Salaam baada ya kutangazwa mshindi.
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel kushoto Dangio Kaniki akimkabidhi  jezi  ya Manchester United mshindi wa Facebook ya Airtel bi. Seba Aggrey  alipotembelea makao makuu ya Airtel jijini Dar Es Salaam baada ya kuibuka mshindi 

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel kushoto Dangio Kaniki pamoja na mshindi wa shindano la Facebook ya Airtel bi. Seba Aggrey wakiangalia kwa pamoja jezi  ya Manchester United iliyosainiwa na wanachama ya timu hiyo baada ya kushinda katika shindano la Facebook ya Airtel.

CLUB Bilicanas yaja na Toto Shoo Krismas ya Kesho

0
0

KATIKA kusherehekea sikukuu ya Krismas, Club yenye hadhi ya kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Bilicanas, kesho inatarajiwa kuwapa burudani kabambe mashabiki wa muziki wa disko wakiwemo watoto.

Mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary alisema amesema leo kwamba  kwamba, kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ndiyo maana wameandaa burudani kabambe ili kutoa fursa kwa watu wa rika lote kusherehekea kwa furaha.

Alisema shamrashamra hizo zitaanza usiku wa leo ambapo kutakuwa na usiku wa Kwaito ‘Kwaito Special’ uliongozwa na kundi la Wakli Dancers.

Omary alisema, kesho (jumanne) mchana kutakuwa na Watoto Shoo ambapo pamoja na muziki wa disko watoto watakaojitokeza ukumbini hapo wataburudika na Father Krismas ambaye atamwaga zawadi ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa kila motto huku wakubwa watakaoambatana nao watalipa sh 3,000.

“Usiku wa Krismasi utakuwa na shamrashamra nyingi ambapo watakaongia kila mmoja atapata mvinyo mwekundu au mweupe, hii kiingilio kitakuwa sh 10,000 kwa kila mmmoja,”alisema. Aidha, Omary aliongeza kwamba siku ya boxing Day ukumbi huo utaendelea kupambwa na burudani mbalimbali ambapo kiingilio kitakuwa sh 5,000 kwa kila mmoja.

Fichuka Development Agency yatambulisha mfumo mpya wa usambazaji wa kazi za wasanii

0
0

Kampuni ya Fichuka Development Agency Ltd, leo tarehe 21/12/2012 inatambulisha mfumo mpya kabisa  wa usambazaji wa  kazi za wasanii ambao umepewa jina la MFUMO RAFIKI (Code number) na utaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 23/12/2012 siku ya uzinduzi wa BUM KUBAM DVD utakaofanyika katika ukumbi wa New maisha Club ikiwa ni sehemu pia ya kuutambulisha mfumo huu mpya, tunaanza na msanii wa muziki  wa kizazi kipya aina ya Hip hop Tanzania Nikki wa Pili katika Makala (Documentary) ya wimbo wake iliyopewa jina la BUM KUBAM DVD.

Bum Kubam inafungua njia ya mpya na ya kimaslahi kwa wasanii wa Muziki pamoja na Filamu nchini Tanzania, ikiwa ndio sekta pekee ambayo inakisiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa ajira kwa Vijana na rika lolote lakini ajira hizi hazikuonyesha kuzaa matunda lakini ujio wa MFUMO RAFIKI (Code Number) uliofanyiwa utafiti kwa  kina kwa lengo la kuokoa kizazi hicho katika kupambana na Maharamia.


Teknolojia hii mpya imegharimu kampuni fedha nyingi ikiwa katika utafiti pia kuutengeneza mfumo wa mauzo kwa kutumia mfumo wa Digitali ambao ni wa kwanza kabisa kufanyika Afrika pengine hata Ulimwenguni, hadi leo unatambulishwa kwenu wanahabari na umma kwa ujumla, kama tulivyosema awali kuwa makala ya Bum Kubam ni kazi ya kwanza lakini baada ya mwezi pia tutangaza kazi inayofuata kwa mfumo kama huu wa mauzo.


Kwa utafiti uliofanywa  kwa zaidi ya miaka mitatu na muasisi/mkurugenzi  wa kampuni ya Fichuka Develoment Agency  Frank John akishirikiana na wataalam kutoka sehemu mbalimbali waligundua kwamba sababu za wasanii kutonufaika na kazi zao ni, kuwepo kwa bidhaa Bandia (Fake) sokoni, kukosekana njia rahisi ya msanii kujua mauzo halisi  ya kazi zake, kutopatikana kwa kazi ya msanii kwa 

Rais kikwete aTOA MILIONI 30 KWA MRADI WA KULEA NA KUHIFADHI MBWA MWITU HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI MKOANI MARA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wasimamizi na wafadhili wa mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na wawakilishi wa Kampuni  ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo imechangia  dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu ili kufanikisha mradi huo, ambao ulizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka 2011. kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012 wakiwa nje ya  boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu akishuhudia kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
 Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Joseph Kaboya, mhifadhi wa  boma maalumu la mradi huo  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara, kwa kufanikisha zoezi hilo kwa mara ya pili. Kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dkt. Simon Mduma (kushoto kwake) na meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga baada ya sherehe hizo eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 

Wahifadhi wakifungua wigo wa senyenge  ili kuachia huru kundi la pili la mbwa mwitu  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma hilo maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Mbwa mwitu hao 15 wakitoka katika hifadhin waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma hilo maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Salaam maalumu kutoka kwa mdau mwenzetu henry Mdimu.

0
0
Pichani kulia nikiwa na rafiki yangu Henry Mdimu a.k.a Zee la Nyeti  aliyetutumia salamu zake za xmass na mwaka mpya hapa jamvini,ama kwa hakika abarikiwe sana na Mungu azidi kuzibariki kazi za mikono yetu daima,upendo mioyoni mwetu uwe ndio ngao ya kutuongoza katika maisha yetu ya kila siku hapa Duniani.Pichani tukiwa tumepozi eneo la Wami darajani,tukiwa kwenye moja ya safari zetu za kikazi.Picha hii ilipigwa tarehe 28 mwezi wa 7,2007.Ama kwa hakika Mungu ni Mwema sana.
======= ======= ========
Napenda kuchukua wasaa huu binafsi kuwashukuru wadau wa Blog hii kwa kuiunga mkono japo kwa uchache wao, huku nikiamini kwamba huu ni mwanzo mzuri na huko tuendako tutakuwa wazuri zaidi.
Heri ya Krismas na shukrani sana kwa kuichagua Blog ya Mdimu kila kunapokucha.

lakini shukrani za dhati kwa Kaka Muhidin Issa Michuzi, hajajua tu lakini kaleta ajira na kipato kwa vijana, amechangia vijana wengi sana kujiajiri na kuwa na maisha bora, nikipata nafasi nitamwambia mwenyewe lakini nyie mnaosoma mkimuona mwambie akiweza hata hizi salamu aweke kwenye blogu ya jamii, tunatambua mchango wake na tunamshukuru sana.

Binafsi nina shukrani za dhati kwa Bloggers Cathbert Angello, Mroki Mroki, Ahmad Michuzi na Othman Michuzi.

Hawa jamaa kila kukicha wananichukulia kama tumezaliwa tumbo moja, sijajua sababu maana hakuna la maana nililowahi kuwafanyia, lakini kila ninapokutana nao hunipa ushirikiano hata wa kutembea, kwa kunishika mkono na kuniambia pa kupita, na wakati mwingine hata kuniuliza kama nimekula au ninataka nini.
Huu ni upendo wa ajabu sana, msinione nimenyamaza nawafikiria sana na cha kuwalipa sina, ila yote kwa yot6e, nawatakia heri ya sikukuu ya krismas.
nawapenda sana!

ASIA IDAROUS,GYMKHANA HILALL NA MARTIN KADINDA WATEULIWA NA KUTOA UAMUZI UNIQUE MODEL 2012

0
0


Baraza la sanaa la taifa limeteua majina matatu ya wabuni wa mavazi nchini Tanzania kuwa waamuzi wa shindano la wanamitindo bora wa mwaka wenye sifa za kipekee nchini Tanzania.

Uteuzi  wa majaji hawa umezingatia sifa za cv za majaji sita zilizowakilishwa baraza la sanaa la taifa na hatima yake yakarudi majina matatu ambayo ni Asia Idarous,Gymkhana Hilall(paka wear) na Martin Kadinda.

Fainali za unique model  2012 zinafanyika ijumaa ya wiki hii tarehe 28 Desemba katika kumbi la maraha lililoko kule Oysterbay yaani naongelea  New Maisha club ambapo wanamitindo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.

Burudani ya bendi mahili katika muziki Mashujaa band ikiongozwa na Chalz Baba watatoa burudani kali kwa mashabiki watakaohudhulia fainali hizo siku ya Ijumaa hii.pia msanii B-shop kwa mara ya kwanza  ataonekana jukwaani. Ikiambatana  na mashamushamu ya Costa siboka na  burudani ya wanamuziki mbalimbali kwa kiingilio cha Tsh 15,000 tu.

Viewing all 46129 articles
Browse latest View live




Latest Images